MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila pengo umepewa majibu manne. Chagua jawabu lifaalo zaidi.
Matumizi mabaya ya mihadarati..................1..................maisha ya watu wengi...................2.................Yakini, yaani...................3.................kuna watu ..................4................kiafya huku wengine..................5................hoi, hawamjui aingiaye..................6................atokaye. Vijana wanastahili ..................7................ dhidi ya uraibu huo lau sivyo jamii..................8................warithi.
-
- yamewasababisha
- imeyasababisha
- yameyasababisha
- imewasababisha
-
- kutumbukia nyongo
- kuenda joshi
- kula mwata
- kufa moyo
-
- huenda
- labda
- yamkini
- kwa hakika
-
- waliodhoofisha
- waliodhoofika
- waliodhoofia
- waliodhoofiwa
-
- wamebaki
- wanabaki
- wangebaki
- wakibaki
-
- ila
- kama
- wala
- ilhali
-
- kuusiwa
- kuhusishwa
- kuhasiwa
- kudhulumiwa
-
- watakosa
- itakosa
- litakosa
- mtakosa
Juhudi alijitahidi kadri...................9..................ili afanikiwe masomoni...................10..................Moyoni, alijawa na shukrani kwa, ...................11.................. aliyejitolea ...................12.................. licha ya kuwa ...................13.................. Kama walivyosema wahenga...................14.................. Juhudi zake zilizaa matunda kwani alifuzu ...................15..................na shule ya kitaifa.
-
- alioweza
- alipoweza
- alivyoweza
- aliyoweza
-
- yake
- yao
- mwao
- mwake
-
- mhisani
- mwadhini
- mlanguzi
- msaliti
-
- kumdhamini masomo yake
- kuyadhamini masomo yake
- kumthamini masomo yake
- kuithamini masomo yake
-
- hawakuhusiana kwa damu wala usaha
- walibaidika kama ardhi na mbingu
- alijitia kati kama mchuzi
- alikula huu na hasara juu
-
- juhudi si pato
- upweke ni uvundo
- bahati ni chudi
- mpanda ngazi hushuka
-
- akaungana
- akaungia
- akajiunga
- akaungwa
Kutoka swali 16-30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo.
- Tambua maneno yaliyoangaziwa katika sentensi ifuatayo.
Aghalabu watu warefu hutembea haraka kuliko wafupi.- Kiunganishi, kivumishi, kivumishi.
- Kielezi, kiwakilishi, kivumishi.
- Kiunganishi, kiwakilishi, kiwakilishi.
- Kielezi, kivumishi, kiwakilishi.
- Andika sentensi ifuatayo katika umoja. Nyua hizo ndizo zilizopaliliwa na vibarua wale.
- Ua hilo ndilo lililopaliliwa na kibarua huyu.
- Ua huo ndio uliopaliliwa na kibarua yule.
- Nyua hiyo ndiyo iliyopaliliwa na kibarua huyu.
- Nyua hiyo ndiyo iliyopaliliwa na vibarua wale.
- Fuawe ni kwa mhunzi kama ilivyo timazi kwa
- mwashi
- sonara
- seremala
- mjumu.
- Chagua sentensi iliyo katika wakati uliopo hali isiyodhihirika.
- Mama anawalisha ng'ombe majani.
- Mwelu amefanya vizuri katika mtihani huu.
- Nawapa wenzangu nasaha kuhusu maisha.
- Balozi wetu atakuwa akitutetea huko. ugenini.
- Kati ya wadudu wafuatao yupi si kimelea?
- Pange
- Nondo
- Mbu
- Utitiri
- Chagua sentensi yenye kivumishi kisichochukua kiambishi ngeli.
- Mwembe mrefu ulikuwa shambani. mwao.
- Kiatu kile ndicho alichokushonea.
- Muziki ninaoupenda unazingatia maadili.
- Mchezaji stadi amefunga bao jingine.
- Tegua kitendawili kifuatacho. Kondoo wangu mnene huchafua njia nzima.
- Konokono
- Mvua
- Kobe
- Ndovu
- Kiambishi 'ka' kimetumiwa kuonyesha nini katika sentensi ifuatayo?
Ametumwa nyumbani akamlete mzazi wake.- Kuonyesha amri.
- Kuonyesha kusudi.
- Mfululizo wa matukio.
- Kukamilika kwa jambo.
- Chagua methali yenye maana sawa na hii.
Afadhali dooteni kama ambari kutanda.- Bura yangu sibadili na rehani.
- Usiache mbachao kwa msala upitao.
- Moja shika si kenda nenda urudi.
- Heri kujikwaa dole kuliko kujikwaa ulimi.
- Chagua maelezo yasiyoonyesha maana ya neno 'kinga'.
- Kumlinda mtu kutokana na madhara.
- Kipande cha ukuni chenye moto.
- Ubao wa chini ya mlango.
- Tayarisha mikono ili kupokea kitu.
- Kanusha sentensi ifuatayo,
Shamba lililolimwa limepandwa mahindi.- Shamba lisilolimwa halikupandwa mahindi.
- Shamba lililolimwa halijapandwa mahindi.
- Shamba ambalo halikulimwa halipandwi mahindi.
- Shamba lililolimwa halipandwi mahindi.
- Ikiwa leo ni Jumanne, mtondogoo itakuwa hini?
- Ijumaa
- Jumapili
- Jumatatu
- Jumamosi
- Kauli 'mkono wangu ulikufa ganzi' imetumia tamathali gani ya usemi?
- Nahau
- Chuku
- Tashhisi
- Kinaya
- Bainisha nomino iliyoundwa kutokana na kitenzi.
- Mcheshi-Cheka
- Kataa-Kataza
- Aminika Uaminifu
- Kicheko Mcheshi
- Badilisha sentensi ifuatayo katika hali ya udogo.
Nyumba hiyo imejengwa papa hapa mjini.- Jumba hilo limejengwa papa hapa mjini.
- Kijumba hicho kimejengwa papa hapa. jijini.
- Jumba hilo limejengwa papa hapa kijijini.
- Kijumba hicho kimejengwa papa hapa kijijini.
Soma ufahamu kwa makini kisha ujibu maswali 31-40.
Fanaka alikuwa ghulamu mcheshi aliyependwa sana na wanafunzi wengine darasani mwetu. Katika shughuli za vikundi, tulipendelea kujiunga naye kutokana na weledi wake wa masuala mbalimbali. Jingine lililotuvutia kwake ni jinsi alivyoonekana nadhifu siku yoyote, wakati wowote. Ama kweli, alikuwa kipenzi na kielelezo kwa wengi.
Siku moja, mwalimu alitupangia somo kuhusu usafi wa kibinafsi. Alituonyesha vitu vinavyohitajika kudumisha usafi wa kibinafsi mathalani sabuni, mswaki, dawa ya meno na kitana. Baadhi ya vitu vilikuwa vifaa halisi na picha za vingine. Isitoshe, alitumia projekta kuonyesha video za vijana mbalimbali wakitekeleza shughuli za usafi wa kibinafsi. Baadaye, alitupa nafasi ya kuwaelezea wenzetu jinsi tunavyoshughulikia usafi wetu wa kibinafsi. Hapo Fanaka alijitolea kulishughulikia darasa.
Alianza kwa kutujulisha jinsi wavyele wake walivyomhimiza kudumisha usafi tangu utotoni. Walielewa umuhimu wa kumkunja kambare angali mbichi. Mazoea haya yalimwepushia matatizo ya kiafya na kumwezesha kuhudhuria masomo yake bila shida.
Fanaka alisema kuwa ilikuwa ada yake kuoga kila asubuhi na jioni. Mtu anapoendelea na shughuli zake za kila siku, huenda akadondokwa na jasho, akatifuliwa vumbi au uchafu mwingine ambao huenda hata hauonekani. Joto la usiku nalo humfanya aliyelala kulowa jasho rovurovu hususan ikiwa anatumia mablanketi mazito. Uchafu huu hauna budi kuondolewa kwa kuoga lau sivyo mtu atanuka gugumo asubuhi na jioni.
Tuliendelea kumtegea Fanaka masikio yetu ndi. Alitueleza kwamba alikuwa na mazoea ya kupiga mswaki kuondoa mabaki ya vyakula ambayo yanaweza kufanya meno kuoza. Hapo tulielewa kiini cha meno ya Fanaka kuwa meupe mithili ya tui la kasimile.
Jingine alilotukumbusha Fanaka ni kujiepusha na uraibu wa pombe na uvutaji sigara. Hata mtu akioga namna gani, uvundo wa dawa hizi za kulevya huwaghasi wale walio karibu naye. Ni vyema mja ajitanibu kabisa na dawa hizi. Nilipoyasikia hayo nilijikumbusha kimoyomoyo kuwa uraibu wa mihadarati huathiri utendakazi wa mwanafunzi kiasi cha kukosa makini katika shughuli za kielimu miongoni mwa nyingine.
Kabla ya kuketi, Fanaka alitukumbusha tusipuuze mambo yanayoonekana madogomadogo kama vile kuzifua lebasi zetu, kunyolewa au kusukwa ikiwa ni wasichana, kunawa mikono na kuangua kucha. Mtu akizingatia hayo na mengine kisha aishi katika mazingira safi, ataonekana mwenye bashasha wakati wote.
Tulimpigia Fanaka makofi kwa ushauri wake. Yamkini, kila mmoja wetu alikuwa akijiahidi kimoyomoyo kumwiga Fanaka katika yale aliyotueleza. Alipojiunga nami pale nilipoketi, nilijua kuwa yote aliyoyasema yalikuwa ukweli mtupu. Nilijivunia uhusiano wetu wa karibu kwani nilikuwa nimeathiriwa vyema.
- Kulingana na aya ya kwanza
- Fanaka alipendelea ucheshi wa vikundi darasani
- Fanaka alivutiwa zaidi na kikundi cha mwandishi
- Fanaka alikuwa kijana mwenye kichwa chepesi
- Fanaka alipendwa na mwalimu kuliko wenzake.
- Kulingana na ufahamu, mwalimu
- aliwaonyesha wanafunzi jinsi ya kutekeleza usafi wa kibinafsi
- alitumia mbinu mbalimbali kufanikisha masomo darasani
- ndiye aliyefunza kila kitu kuhusu usafi wa kibinafsi
- alimpa msimulizi nafasi ya kuwaeleza wenzake kuhusu usafi wa kibinafsi.
- Nimethali gani inayofaa zaidi kueleza ujumbe katika aya ya tatu?
- Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina.
- Mwana mui ni dawa ya mlango.
- Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
- Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
- Eleza manufaa ya usafi kulingana na kifungu
- Kudumisha afya na kufanikisha utendakazi nyumbani.
- Kuepuka vimelea na uchafu wa mavazi.
- Kuvuta urafiki na kuondoa mabaki ya vyakula.
- Kutunza siha na kuondoa uvundo.
- Mtu anapaswa kuoga kila usubuhi. Ni uchafu upi unaoondolewa kwa kufanya hivyo?
- Jasho, matongo
- Vumbi, jasho
- Matongo, vumbi
- Nta, vumbi.
- Kauli meupe mithili ya tui la kasimile' imetumia tamathali gani ya usemi?
- Sitiari
- Chuku
- Kinaya
- Tashbihi.
- Fanaka hakuwaambia wenzake kuwa
- mtu anapaswa kuoga angaa mara mbili kwa siku
- wanaotumia dawa za kulevya hutoa uvundo unaokirihi
- mtu asipopiga mswaki meno yake huoza
- matumizi ya mihadarati huvuruga utendaji wa wanafunzi.
- Usafi wa kibinafsi si pamoja na
- kunyoa nywele
- kukata kucha
- kupiga deki
- kufua nguo.
- Kulingana na aya ya mwisho
- Fanaka aliwaathiri vyema wenzake darasani
- wanafunzi walimwahidi Fanaka kufuata ushauri wake
- ilikuwa mara ya kwanza kwa mwandishi na Fanaka kukaa pamoja
- wengine waliyatilia shaka maneno ya Fanaka.
- Neno lebasi lina maana sawa na
- malazi
- mavazi
- mapambo
- mazingira.
Soma kifungukifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 41 hadi 50.
Matumizi ya mitandao ya kijamii yamefikia upeo wa juu katika miaka ya hivi karibuni. Si ajabu kuwaona waja wanaotumia simu zao, tabuleti au vipakatalishi katika magari ya uchukuzi wa umma, ofisini, nyumbani na katika bustani mbalimbali. Utawapata watu wenyewe wakionyesha hisia mbalimbali kwa kutegemea picha, jumbe au video wanazotazama kwenye mitandao hiyo.
Watu wengi hutumia mitandao hii kujiburudisha. Wao hutazama video zinazohusiana na nyimbo, michezo, mitindo ya mavazi na ya nywelle. Aghalabu utawaona wakibadilisha mitindo yao kuambatana na vigezo wanavyovipata mitandaoni. Video hizi zinapopata idadi kubwa ya watazamaji, wanaozipakia huanza kujipatia kipato. Kuna watu walioimarika sana kiuchumi
kutokana na video kama hizi.
Mumo humo mitandaoni huwa soko la huduma na bidhaa mbalimbali. Wawekezaji hutumia njia hii kunadi biashara zao hivyo basi kujiongezea idadi ya wateja. Gharama ya utangazaji huu ni nafuu ikilinganishwa na matangazo mbadala kama vile ya redio, runinga, magezeti na maonyesho. Mteja naye hurahisishiwa kazi ya kusaka bidhaa kwani analinganisha maelezo na bei za bidhaa mbalimbali pasipo kusumbuka sana. Akifikia uamuzi wa kununua bidhaa au huduma fulani, atawasiliana naye kwa simu au mitandao iyo hiyo, kisha hupelekewa bidhaa popote alipo kwa ada nafuu.
Watu wengi hasa vijana huwa na marafiki wengi katika mitandao ya kijamii. Urafiki huu unaweza kumfaa mtu kiuchumi, kisaikolojia na kisosholojia. Wengine wamewahi hata kupata wachumba na wenzi wao katika ndoa kupitia mitandao hii.
Elimu ni bahari. Kupitia mitandao ya kijamii, tunaweza kupata maarifa ya kielimu, kidini, uwekezaji, utamaduni na mengine mengi. Wanaotumia maarifa haya kwa njia ifaayo huongeza thamani katika maisha yao. Wao hufanya hivi kwa kuanzisha biashara zao, kazi za kiufundi, vilabu vya mazoezi, upishi na uokaji wa keki. Almradi, kila mmoja hufaidika kivyake na maarifa ya mtandaoni.
Chambilecho wahenga, hakuna bamvua lisilokuwa na usubi. Kuna watu waliowahi kuhasirika kutokana na mitandao hii. Uhalifu wa mitandaoni umekuwa tatizo sugu hivi kwamba serikali imeapa kulivalia njuga. Wapo waja wanaotumia mitandao hii kuwatishia wengine wawape kiwango kikubwa cha fedha lau sivyo wafichue siri zao au kuweka picha zao za kuaibisha. Ajabu ni kuwa wanaofanya hivyo aghalabu waliwahi kuwa marafiki wa wahasiriwa. Matukio ya aina hii yamewahi kuwaletea wengi mzongo wa mawazo huku baadhi yao wakijitia kitanzi.
Utapeli ni uhalifu mwingine unaotekelezwa mitandaoni. Wapo wanaojifanya kuuza huduma au bidhaa ambazo hazipo. Nyingine nazo hupambwa kwa picha nzuri nzuri wateja wakaziagiza kwa wingi pasipo kujua kwamba hazifikii viwango. Waliofikia viwango vya juu vya uhalifu huu hudukua akaunti za wengine na kuzitumia kuwalaghai marafiki zao ili wawatumie pesa.
Mitandao hii ikitumika vizuri, italeta manufaa kochokocho. Wanajamii hawana budi kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuwafichua wanaotumia mitandao ya kijamii kueneza porojo, kufaidi jasho la wengine au kuvuruga mahusiano ya kijamii. Serikali pekee haiwezi kufanikiwa kukomesha uhalifu huu maadamu kofi hazilii ila kwa viganja viwili.
- Chagua maelezo yaliyo sahihi.
- Mitandao ya kijamii huwaathiri watumiaji kwa njia zinazohitilafiana.
- Uchukuzi wa magari ya umma umeifanya mitandao ya kijamii kupata umaarufu.
- Mitandao ya kijamii hutumiwa na vijana peke yao.
- Hisia mbalimbali huwatambulisha wanaotumia mitandao ya kijamii.
- Aya ya pili inaonyesha kuwa
- watu hubadilishiwa mitindo yao ya mavazi mitandaoni
- watu wengi walianza kujipamba walipojiunga na mitandao
- mazoea ya mtu huathiriwa na yale anayoshuhudia mitandaoni
- mitindo bora zaidi ya nywele ni ile ishuhudiwayo mtandaoni.
- Ni kweli kusema kuwa
- wanaotazama video nyingi mitandaoni hupokea malipo
- mitandao ya kijamii inaweza kumwimarisha mtu kiuchumi
- bidhaa hununuliwa na kusafirishwa mumo humo mitandaoni
- wafanyabiashara wengi wana maduka yao mitandaoni.
- Jambo lipi ni sahihi kuhusu matangazo mitandaoni?
- Bei yake ni rafi.
- Bei yake ni ya kuruka.
- Bidhaa huwa bora zaidi.
- Mengine yametiwa chumvi.
- Manufaa ya urafiki kulingana na kifungu hiki ni
- kumpunguzia mtu matatizo ya kiakili
- kumwezesha kuepuka hila za matapeli
- kupata umaarufu kitaifa na kimataifa
- kupata video mbalimbali mitandaoni.
- Wanaoanzisha miradi ya kujifaidi kutokana na mitandao ni wale
- wanaotumia mitandao kujiburudisha
- wanaotumia mitandao kwa wingi zaidi
- wanaotumia mitandao kutafuta maarifa
- wanaopitisha maarifa kwa wenzao mitandaoni.
- Kauli 'kulivalia njuga' ina maana gani?
- Kulivalia viatu.
- Kulishughulikia sawasawa.
- Kulipuuza kwa vyovyote.
- Kuliwazia kwa kina.
- Ili kukomesha uhalifu wa mitandaoni, mwandishi anahimiza kuwa na
- uaminifu
- uvumilivu
- utangamano
- ushirikiano.
- "Wanaofanya hivyo aghalabu waliwahi kuwa marafiki wa wahasiriwa." Kauli hii inaonyesha kuwa
- mtu hughulumiwa zaidi na mahasimu wake
- wale tuliowaamini wanaweza kusaliti uhusiano wetu
- hatufai kumwamini mtu yeyote maishani
- mtu akikufanyia mabaya mlipe kwa ubaya uo huo.
- Maana ya neno 'kunadi' ni
- kusifu
- kuuza
- kutangaza
- kuonyesha.
MAJIBU
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 8.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students