MASWALI
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umpewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi.
Visa vya uhalifu vinaweza kugeuka na kuwa .............1................ la kitaifa iwapo .............2............... na serikali. Wananchi wengi ...............3............. nchini mwetu .............4............... na ..............5.............. mali ..............6.............. hususan katika miji yetu. Mikakati madhubuti inapaswa kuwekwa ili ............7................ wahalifu ..............8.............. maendeleo. Ikumbukwe kuwa idadi kubwa ya vijana .............9............... watu huishi pamoja na raia wa kawaida kwani .............10.................
-
- tabu
- shida
- mkasa
- janga
-
- havitathibitiwa
- havitadhibitiwa
- havitadibithiwa
- havitathaminiwa
-
- huku
- humo
- humu
- mle
-
- huvamiwa
- huvamia
- hukabiliana
- hukumbana
-
- kuibwa
- kunyang'anywa
- kukabidhiwa
- kukabwa
-
- wao
- lao
- zao
- yao
-
- kuwatia mbaroni
- kuwatia kiwi
- kuwatia hamasa
- kuwatia kiwewe
-
- wanaoduwaza
- wanaoshurutisha
- wanaodidimiza
- wanaoandamana
-
- inayohangaisha
- wanaohangaisha
- wanahangaisha
- inahangaisha
-
- kinga na kinga ndipo moto uwakapo
- kikulacho ki nguoni mwako
- usipoziba ufa utajenga ukuta
- pwagu hupata pwaguzi
Likizo ..............11............... tulimzuru nyanya mashambani. Wakati ...............12.............. alitupokea kwa furaha tele. Babu alikuwa ...............13.............. kivuli chini ya mbuyu. Tulimkabidhi nyanya mzigo uliojaa. .............14................ matunda, sukari, unga na kilo tano za mchele. ...............15.............. kuingia chumbani, nyanya aliomba na kumshukuru Mungu. Tukajiunga na babu chini ya mbuyu.
-
- iliopita
- ilipopita
- iliyopita
- ilikopoita
-
- tulipofika
- tutakapofika
- tunafika
- tulifika
-
- katikati
- kati ya
- chini ya
- kwenye
-
- !
- :
- ;
- ,
-
- Kabla ya
- Baada ya
- Sembuse
- Mradi
Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi
- Kukanusha kwa: "Mti ambao ulikatwa umeanza kukauka, 'ni:
- Mti ambao ulikatwa haukuanza kukauka
- Mti ambao haukukatwa haujaanza kukauka
- Mti ambao ulikatwa haujaanza kukauka
- Mti ambao haukukatwa haujaanza kukauka
- Ni sentensi ipi ambayo ina matumizi ya kiambishi "ki' cha wakati pekee?
- Chakula kikipikwa nitafurahi sana
- Dereva alipoingia garini alimpata akilala
- Kitabu hiki kina picha za kupendeza
- Shangazi anatembea kijeshi
- Ikiwa keshokutwa itakuwa Alhamisi, juzi ilikuwa:
- Jumatatu
- Jumamosi
- Ijumaa
- Jumapili
- Somi ameolewa na Hamisi. Dada yake Somi ameolewa na Charo. Hamisi na Charo wataitana:
- Mwanyumba
- Mavyaa
- Kivyele
- Mkwe
- Sentensi inayounganisha sentensi: "Kirui ni mzee. Kirui anatembea bila mkongojo." ni
- Kirui anatembea bila mkongojo minghairi ya yeye kuwa mzee.
- Kirui ni mzee madhali anatembea bila mkongojo
- Kirui anatembea bila mkongojo licha ya kuwa yeye ni mzee.
- Kirui ni mzee maadamu anatembea bila mkongojo.
- Chagua nomino isiyoafikiana na nyingine.
- Werevu
- Ushindi
- Amani
- Unga
- Johari hapendi kufanya kazi. Anazembea kwa kila jambo. Ni nahau gani iliyoafikiana na tabia yake?
- Kupiga zohali
- Kufanya inda
- Kujifunga kibwebwe
- Kupiga chuku
- Kauli, 'Sinyorita ni ninga' imetumia tamathali gani ya usemi?
- Nahau
- Tashbihi
- Istiara
- Kinaya
- Onyesha sentensi yenye kivumishi.
- Omondi alilima shamba juzi
- Pale pana madawati machache
- Ndege imeondoka mapema
- Watatu waliumia uwanjani
- Chagua jibu ambalo lina vihusishi pekee.
- Mno, tena, baadaye
- Kati ya, labda, ama
- Kama, kwa haraka, vizuri
- Katika, kando ya, tangu
- Chagua wingi wa: Hukujua kuwa seremala angemnunulia bata mkubwa.
- Hawakujua kuwa seremala angewanunulia mabata wakubwa.
- Hamkujua kuwa maseremala wangewanunulia mabata wakubwa
- Hamkujua kuwa maseremala wangemnunulia mabata wakubwa
- Hawakujua kuwa maseremala wangemnunulia mabata wakubwa
- Neno, Mkalimani lina silabi ngapi?
- Nne
- Sita
- Tano
- Tisa
- Maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo ni:
Babu yangu amerudi nyumbani lakini wake ataondoka kesho.- Kivumishi, kiwakilishi, kielezi
- Kimilikishi, kielezi, nomino
- Kivumishi, kielezi, kiwakilishi
- Kielezi, kivumishi, kiwakilishi
- Tegua kitendawili:
Kikigongwagongwa wanawe hutoka nje- hindi
- ngoma
- mgomba
- kichuguu
- Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
- Je? Ulifika shuleni saa ngapi?
- Kaka alinunua; kitabu, rula na kalamu.
- Mwalimu wetu(Bi. Mona) anapenda michezo.
- lahaula unamfahamu mama yangu!
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Wengi wetu tumewahi kusikia kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu. Hata hivyo, sio wote wanaoelewa hatari ya ugonjwa huu. Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria. Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kuwadhuru watu hata kusababisha vifo katika nchi maskini. Kenya ni mojawapo ya nchi zilizo na mzigo mkubwa wa kifua kikuu kote ulimwenguni huku zaidi ya Wakenya laki moja wakiambukizwa ugonjwa huu kila mwaka.
Kifua kikuu ni ugonjwa ambukizi ambao huchukua miezi kadhaa kuutibu, usipogunduliwa na kutibiwa mapema, unaweza kusababisha madhara kadhaa mwilini kama vile kupoteza mapafu na uwezo wa kusikia. Aidha unaweza kusababisha kiharusi. Hata hivyo, ugonjwa huu una tiba. Wagonjwa wengi hupata nafuu na kupona na miili yao kuanza kufanya kazi vizuri tena baada ya mgonjwa kukamilisha matibabu.
Ugonjwa huu husambaa mgonjwa anapokohoa, kupiga chafya au anapozungumza na mtu anapopumua hewa iliyo na viini vya ugonjwa huu. Ingawa hivyo sio kila mmoja anayepumua hewa yenye viini anayepata kifua kikuu. Watu wengi walio na kinga imara ya mwili hupambana na viini vya ugonjwa huu na kuvishinda.
Watoto wachanga na watu waliozeeka ndio walio na hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu kutokana na kinga yao dhaifu ya mwili. Matibabu ya saratani na ukimwi hupunguza kinga ya mwili na kuhatarisha maisha ya wagonjwa hao ambao hunyemelewa kwa urahisi na kifua kikuu. walio tena kwenye hatari ya maambukizi ya kifua kikuu ni watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda iliyo na msongamano mkubwa wa watu. walio kwenye magereza, wanaofanya kazi maeneo yaliyo na maambukizi mengi ya kifua kikuu hasa wafanyakazi katika hospitali zetu na wanaoishi kwenye chumba kimoja na mgonjwa wa kifua kikuu.
Baadhi ya dalili za kifua kikuu ni pamoja na joto jingi mwilini, kupunguka kwa uzani, kutoka jasho usiku na kikohozi. Ugonjwa wa kifua kikuu una tiba. Tiba bila malipo inapatikana katika hospitali zote za umma na zahanati Tiba ya dezo pia inapatikana katika kliniki kadhaa za umma nchini. Dawa hutumiwa kwa takribani miezi sita na baadaye mgonjwa hukaguliwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa karibu.
Kwa kweli mti hauendi ila kwa nyenzo. Hatuwezi kujipakatia mikono na afya nzuri ije kwetu. Ili kupunguza maambukizi, epuka sehemu zilizo na misongamano mikubwa ya watu, hakikisha makazi yana mzunguko mzuri wa hewa hasa palipo na msongamano; hakikisha kuwa walio na kifua kikuu wamepata matibabu.
- Kulingana na aya ya kwanza:
- Watu wote wana habari kuhusu kifua kikuu
- Baadhi ya watu wanaelewa hatari ya kifua kikuu
- Kifua kikuu ni ugonjwa unaoua watu wengi zaidi ulimwenguni.
- Kifua kikuu ni ugonjwa unaosambazwa na bakteria
- Kifua kikuu;
- hupatikana nchini Kenya pekee
- husababisha vifo vya watu laki moja kila mwaka katika nchi maskini
- ni ugonjwa usiokuwa na tiba
- ni chanzo cha kifo katika nchi nyingi maskini
- "Kifua kikuu ni ugonjwa ambukizi" inamaanisha:
- Mtu huchukua muda mrefu kupona ugonjwa huu
- Husababisha kiharusi
- Unaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine
- Ugonjwa huu unatibika
- Chagua kundi lisilokuwa kwenye hatari ya kuambukizwa kifua kikuu kwa mujibu wa kifungu.
- Wakazi wa mitaa ya mabanda
- Wafungwa gerezani
- Madaktari wanaotibu wagonjwa wa kifua kikuu
- Wagonjwa wote wanaougua kansa
- Kifua kikuu ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia zifuatazo isipokuwa:
- Wakati mtu mwenye afya hupumua
- Kupitia kikohozi cha anayeugua kifua kikuu
- Mgonjwa wa kifua kikuu anapopiga chafya
- Mtu anapopumua hewa viini vinavyosababisha kifua kikuu
- Kulingana na kifungu, ni nani asiyeweza kuugua kifua kikuu hata baada ya kupumua hewa yenye viini vya ugonjwa huo?
- Watu wenye afya bora
- Wenye kinga ya mwili iliyo madhubuti
- Watu waliozeeka sana
- Wagonjwa wa ukimwi
- Maana ya methali, 'Mri hauendi ila kwa nyenzi imedhihirika namna gani katika kifungu?
- Wanaopata matibabu ya kifua kikuu hupona
- Watoto wachanga na wazee hukumbwana maambukizi.
- Wanaochukua tahadhari huepuka ugonjwa wa kifua kikuu.
- Wahudumu wa afya hospitalini huweza kuambukizwa kifua kikuu.
- Tiba ya dezo ni tiba gani?
- Isiyokuwa na malipo
- Ya malipo yaliyopunguzwa
- Ya lazima
- Isiyoepukika kabisa
- Kulingana na kifungu, tiba ya kifua kikuu huchukua muda gani?
- Zaidi ya miezi sita
- Miezi sita
- Mwaka mmoja
- Karibu miezi sita
- Yafuatayo ni madhara ya kifua kikuu ila:
- Keathiriwa mapafu
- Kupoteza uwezo wa kusikia
- Kupungua kwa uzani wa mwili
- Kusababisha kiharusi
Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 41-50.
Punda na nguruwe waliumbwa kuwa marafiki wa dhati daima. Hata hivyo, urafiki wao uliosambaratika siku moja Nguruwe alipozuru kwa rafikiye. Wasemao husema kuwa mambo ni kangaja huenda yakaja.
Ndugu hawa wawili walikuwa wazawa wa kijiji kimoja. Wazazi wao walikuwa marafiki wa kufa kuzikana jambo lililosababisha wawili hao kuishi na kukua pamoja kama ndugu wa mzazi mmoja. Kifo kilinyemelea familia hizi na kuacha wafaruku wakiyahangaikia maisha. Wote wakiwa na moto wa kiume wa kulea. Walijifunga kibwebwe kazini ili kuwakidhia wana wao mahitaji ya kimsingi.
Punda na nguruwe walikua na kuwa mabarobaro na hata kujijengea makazi yao. Hata hivyo, waliwategemea wazazi waliobaki kujipatia riziki ya kila siku. Ndugu hao wawili kila walipokutana ugani, wangemenyana miereka ili kubainisha mwenye nguvu japo walifanya hivyo kupitisha wakati. Mara nyingi nguruwe angeibuka mshindi kwa hisani ya mamaye. Jambo hili lilimkera punda ambaye alikuwa dhaifu kutokana na ukosefu wa lishe bora.
"Rafiki yangu," Punda alimwambia Nguruwe, "Nasadiki kuwa sasa tunaweza kujikidhia mahitaji yetu. yafan tuwasafirishe abera wazazi wetu maadamu wamekula chumvi nyingi. Sisi tu wapishi hodari."
Kutokana na madai kwamba walikuwa wapishi stadi, nguruwe aliyavalia maneno na ushauri wa nduguye njuga. Bila kuwazia zaidi, wawili hao walisuka mpango wa kuyatatiza maisha ya wazazi wao.
"Hili ni jambo rahisi," punda alisema, "Wanahitaji kichapo na kuwasafirisha kaburini," alishauri huku akitabasama kichinichini.
Baada ya maandalizi ya mada, wawili hao walikuwa tayari kutimiza mpango wao walivyokubaliana. Punda alitoa amri. 'Gonga' na wote wakaanza kuwachapa wazazi wao.
Nguruwe alimpondaponda mama yake hadi akamsafirisha jongomeo. Kwa upande mwingine punda aligongagonga ngoma huku akipiga mayowe na kuiga kilio cha mwanamke. Alijitoma kwenye nyumba ya nguruwe machozi yakimdondoka njia mbilimbili. "Nimemaliza" Punda alisema. Nguruwe naye akamwambia, "Wangu anapumzika kaburini.
Baada ya miezi kadhaa walikutana mahali paopa kawaida na kupiga gumzo kuhusu maisha bila wazazi. Punda alikuwa amenenepa lakini nguruwe alikuwa mkondefu kama mwiko wa pilau. Wakaelewana kupunguza ziara za kutembeleana kutokana na kazi iliyowabana. Nguruwe alikuwa amepigwa mafamba vilivyo.
Siku moja nguruwe alipokuwa kwenye pitapita zake karibu na nyumba ya punda akitafuta chakula, alishtuka kumwona mamaye punda akinywa uji huku akiota jua. Nguruwe alitaka kulia, akakata shauri kuachana na usuhuba wa punda.
- Kulingana na aya ya kwanza, urafiki kati ya punda na nguruwe unaweza kuelezwa kuwani wa:
- Kudumu
- Kujitolea
- Kusambaratika
- Unafiki
- Aya ya pili imebainisha kuwa:
- Punda na nguruwe walizaliwa na mzazi mmoja
- Punda na nguruwe walikuwa na tabia zilizofanana
- Wazazi wa kike wa punda na nguruwe walifariki kwanza
- Urafiki wa wazazi ulisababisha malezi ya pamoja ya punda na nguruwe
- Sentensi, kifo kilinyemelea familia hizi na kuacha wafaruku wakiyahangaikia maisha" imetumia tamathali gani ya usemi?
- Tashhisi
- Nahau
- Istiara
- Kinaya
- Ni jambo gani linaloonyesha kuwa wazazi wa punda na nguruwe waliwajibikia majukumu yao?
- Kuwazaa wana wao katika kijiji kimoja
- Kutimizia haja familia zao
- Kuwalea wana wao katika mazingira sawa
- Kuishi pamoja na kuwa marafiki wa kufa kuzikana
- Miereka ni
- mchezo wa kushindana na kuvuta kamba
- michezo ya kujificha na kutafutana
- michezo ya kushikana na kuvamiana kwa lengo la kuangushana
- michezo ya mazoezi ya viungo vya mwili
- Baada ya punda kushindwa na nguruwe;
- punda alilalamikia mamaye
- aligundua kuwa alikosa lishe bora
- alifurahishwa na ushindi wa nduguye
- alikasirishwa na kushindwa kwake.
- Punda alimshauri nguruwe kuwaua wazazi kutokana na sababu zifuatazo isipokuwa:
- Walikuwa na uwezo wa kujikidhia mahitaji yao
- Walishakuwa mabarobaro na hata kujijengea makazi
- Walikuwa na uzoefu wa kujipikia
- Wazazi wao walikuwa wamezecka
- Wazazi wa punda na nguruwe walipoanza kupata kichapo
- walikuwa wamefahamu mpango wa wanao
- nguruwe alimchapa mama yake hadi akafa
- hakuna mwana aliyekusudia kuua mzazi wake
- punda hakupoteza muda, aliua mama yake
- Chagua jawabu lisilokuwa sahihi; Baada ya vifo vya wazazi:
- Nguruwe alijipata na shughuli nyingi za kujitafutia riziki
- Marafiki hao wawili walisimuliana kuhusu maisha yao.
- Hatimaye siri ya punda ilifichuka
- Nguruwe alianza kumtembelea punda mara kwa mara.
- Funzo linalotokana na kisa hiki hasa ni: Yafaa
- tujiamini
- kuwasiliana kwa njia nzuri
- tufikiri kabla ya kutenda
- tuwe wabunifu
Insha
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako
Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa: Andika insha itakayomalizika kwa maneno yafuatayo:
.............................................................................................Hapo ndipo nilipogundua kuwa hatupaswi kukata tamaa maishani.
MAJIBU
Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 9.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students