Friday, 14 April 2023 13:25

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 5

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Wahenga na wahenguzi hawakukanyaga chechele walipolonga kuwa Mungu ...................1.................. Ama kwa ....................2.................. Mungu si mtovu. Yeyote anayemwamini atajibiwa ...................3.................. yake. Mara nyingi tumewasikia watu akitoa ...................4.................. kuhusu nasaha waliyokwisha kupokea kutoka kwa wajuzi wa nyanja mbalimbali. Ukweli ni kwamba, wenye ...................5.................. ,wote huishia kubarikiwa. Yote tuyafanyayo bila kumtegemea Rabuka huwa ni kazi  ...................6..................  hata ingawa tutatia bidii ya mchwa.

  1.                          
    1. hamwachi mja wake
    2. huwabariki waja wake
    3. hawaachi waja wao
    4. humwacha mja wake
  2.                          
    1. yamkini
    2. lakini
    3. yakini
    4. makini
  3.                
    1. ombi
    2. dau
    3. doa
    4. dua
  4.                
    1. ushahidi
    2. shahidi
    3. ushuhuda
    4. shahada
  5.                  
    1. amani
    2. amana
    3. dhamana.
    4. imani
  6.                  
    1. bure bilashi
    2. kuntu kabisa
    3. nzuri zaidi
    4. nyingi mno

Siku ..............7..................., sote tulibakia uwanjani huku tukicheza mchezo wa ..............8.................. yaani kibe. Mara tulimwona akiwa amesimama mlangoni. Mmoja wetu alitudokezea tukakimbia, tukaingia darasani na ..............9.................. Tulijua kuwa mambo yalikuwa ..............10.................. Tulingojea huku tukiwa na huzuni ..............11.................. sisemi wasiwasi. ..............12.................. kuhusu makosa yetu na ..............13.................. kuwa tulikuwa tumemkosea mwalimu wetu. Mdarisi alipoingia tulisimama tisti na kumwomba msamaha. Mwalimu alifurahi na kutufunza ..............14.................. badala ya kipindi cha Kiswahili alichokiandaa. Alitukumbusha kuwa heshima ..............15..................

  1.                            
    1. hilo
    2. hio
    3. hizo
    4. hiyo
  2.                
    1. kukimbizana na kuangushana
    2. kuiga na kuigiza majukumu ya wazazi nyumbani
    3. watoto wa kujificha na kutafutana
    4. kuvuta kamba kwa kushindania
  3.                      
    1. kukimya
    2. kunyamazana
    3. kunyamaza
    4. kuropokwa
  4.                  
    1. yamezidi unga
    2. yametumbukia nyongo
    3. yametengenea sana
    4. yameimarika zaidi
  5.                      
    1. mwingi
    2. mingi
    3. wingi
    4. nyingi
  6.                        
    1. Tulichunguzwa
    2. Tulikumbuka
    3. Tulitafakari
    4. Tulisahau
  7.                
    1. kukiri
    2. kukana
    3. kukanusha
    4. kukataa
  8.                  
    1. maadili
    2. madili
    3. adhabu
    4. utundu
  9.                      
    1. utumwa
    2. haidumu kamwe
    3. si utumwa
    4. inadumu daima.

Kuanzia swali la 16 hadi la 30. jibu kulingana na maagizo.

  1. Maneno yafuatayo yatapangwaje katika kamusi?
    1. Pasa
    2. Paka
    3. Pakua
    4. Paku
      1. ii, iv, iii, i
      2. i, iii, iv, ii
      3. iii, i, ii, iv.
      4. iv, ii, iii, i
  2. Kamilisha sentensi ifuatayo kwa maneno yafaayo.
    ___wake amemnunulia___ ____ nguvu _____
    1. Mzazi, fahali, enye, malindandi
    2. Msasi, fahari, mwenye, malidandi
    3. Mzazi, fahali, mwenye, maridadi
    4. Mzazi, fahari, enye, maridadi
  3. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.
    Hakuelewa kuwa ningechelewa.
    1. Hawakuelewa kuwa tungechelewa
    2. Hamkuelewa kuwa tungechelewa.
    3. Hamkuelewa kuwa ningechelewa.
    4. Hawakuelewa kuwa ningechelewa.
  4. Tambua sentensi sanifu inayolinganisha hizi.
    Utubora alifaulu.
    Utubora hakufurahi.
    1. Lau Utubora alifaulu hakufurahi.
    2. Utubora hakufurahi aghalabu alifaulu.
    3. Utubora hakufurahi licha ya kufaulu.
    4. Maadamu Utubora hakufurahi alifaulu.
  5. 3051660 kwa maneno ni
    1. Milioni tatu, laki hamsini na moja mia sita sitini
    2. Milioni tatu elfu hamsini na moja mia sita na sita
    3. Milioni tatu hamsini na moja elfu, mia sita na sitini
    4. Milioni tatu hamsini elfu na moja mia sita na tisini
  6. Ni nini maana ya 'kutia masikio nta"?
    1. Kutojali yasemwayo.
    2. Kujali yasemwayo.
    3. Kuweka masikio vipuli.
    4. Kutia masikio pamba.
  7. Mwasaru alinipigia simu, nami nikampigia simu. Kwa hivyo sote wawili ...............................
    1. tulipigiana pigiana simu
    2. tulipigiwa simu
    3. tulipigana simu
    4. tulipigiana simu
  8. Ni methali gani iliyo na maana sawa na
    "polepole ndio mwendo"?
    1. Chelewa chelewa utapata mwana si wako.
    2. Haraka haraka haina baraka.
    3. Chovya chovya humaliza buyu la asali.
    4. Heri kenda kuliko kumi nenda rudi.
  9. Ni sentensi gani iliyo na kivumishi cha pekee?
    1. Kusafiri kwa gari moshi ni kuzuri
    2. Chakula hiki ni kitamu sana.
    3. Ukucha wangu umekatika.
    4. Nyumba yote iliteketea moto.
  10. Chagua ukubwa wa sentensi hii
    Gari hili zuri, lina dirisha kubwa na mlango wa kupendeza.
    1. Kigari hiki ni kizuri, kina kijidirisha kikubwa na kijilango cha kupendeza.
    2. Jigari hili ni zuri, lina jidirisha kubwa na lango la kupendeza.
    3. Jigari hili ni mzuri, lina dirisha kubwa na lango la kupendeza.
    4. Ligari hili ni zuri, lina dirisha kubwa na lango la kupendeza.
  11. Fuma ni kusuka nyusi. Vile vile fuma ni
    1. kudunga kwa kifaa chenye makali.
    2. kudunga kwa mtutu wa bunduki. 
    3. kushona nguo paliporaruka.
    4. kupachika nguo kiraka kipya.
  12. Umbo lifuatalo ni
    27 asdadada
    1. Mstari sulubu
    2. Pembe butu
    3. Pembe kali
    4. Pembe nyoofu
  13. Chagua sentensi inayoonyesha 'jl' ya nafsi.
    1. Uimbaji wake uliwatumbuiza wageni. 
    2. Jibwa limefungiwa chumbani. 
    3. Msomaji wa taarifa alisikika vizuri.
    4. Nilijisomea Riwaya ya Siku Njema.
  14. Ikiwa mtondogoo itakuwa Jumamosi Machi tarehe mbili 2023, jana ilikuwa lini?
    1. Jumatatu Februari tarehe ishirini na tatu
    2. Jumatatu Februari tarehe ishirini na saba.
    3. Jumatatu Februari tarehe ishirini na sita.
    4. Jumatatu Februari tarehe ishirini na tano.
  15. Mzee Weru ameishi miaka mingi sana. Yaani
    1. amekula siku zake
    2. ameona mambo mengi
    3. amekula tarehe
    4. amekula chumvi nyingi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40

Waswahili husema kuwa safari ya kesho hupangwa leo. Waaidha, msafiri ni aliye bandarini. Mwanadamu anatakiwa awe na mpango madhubuti wakati anapohitaji kufanya jambo lolote; liwe jambo dogo au kubwa. Kimsingi ni kwamba, mtu hawezi akafyeka kichaka akalima, akapanda, akapalilia na kufaidi matunda kwa siku moja. Ni sharti mtu kujua kwamba mambo hutayarishwa hatua kwa hatua na kupatiwa muda ili yatengence.

Mtahiniwa yeyote anafaa kujiandaa barabara wakati ambapo anaungojea mtihani

wowote. Mtu hupata kufahamu wakati wa mtihani mapema zaidi. Kwa hivyo si vyema hata kidogo mtu kungojea hadi siku ya siku kuwa pua karibu na mdomo illi aweze kuanza kujiandaa. Mwanzo kabisa, ni sharti awe na ratiba yake binafsi. Ratiba huwa kama dira na rubani. Rubani anapokosa dira bila shaka atasalia pale hewani na wala hataweza kutua hata kidogo. Hivyo ndivyo ilivyo kwa mwanafunzi pia. Hakuna vile unaweza kuketi tu na kuchomoa kitabu na kuanza kusoma. Mwanafunzi anapofanya hivyo atajipata kuwa amesoma masomo anayoyapenda huku akiyasahau yale ambayo yanampa changamoto.

Mtahiniwa anapodurusu, afanye udadisi wa kutosha. Asichukue vitabu tu bila kufahamu kinachohitajika ili kujiandaa vyema ni lazima asome mwanzo akili ya mtahini. Atafanya hivi kwa kutazama karatasi zilizofanywa awali. Hili litamsaidia kusoma tu yale muhimu kwa mujibu wa kuupasi mtihani huo. Mtu anaposomasoma kila kitu hata kisichomhusu atamalizia kuyajua mambo mengi zaidi ambayo hayamhusu ndewe wala sikio. Huu ndio unaoitwa ukasuku katika kusoma. Hebu nikuulize, je, mwanafunzi anaweza kufaulu kwa kusoma magazeti tokea asubuhi hadi jioni? Hapo nafikiri hatafua dafu mtihanini.

Aidha, mwanafunzi anashauriwa kuwa pahali pake pa kusomea pasiwe karakana. Yaani pasiwe na kelele wala vitu vinavyoweza kumchachawiza msomaji akaacha kusoma. Ijapokuwa wengine hupenda kudurusu huku wakisikiliza muziki, ni bora kuwe kutulivu na shwari kwa uelewa aula. Vile vile, sehemu hiyo iwe na hewa safi; madirisha yafunguliwe, pasiwe baridi sana au joto kupita kiasi. Licha ya hayo, aandae vifaa vyake mapema, mathalan meza, kiti, vitabu, kallamu, karatasi na vingine vingi vinavyohitajika. Fauka ya hayo, awe na saa ili aweze kuyapatia masomo yake wakati maalum.

Kusoma pia kuna mipaka. Mwanafunzi asijilazimishe na kujipagaza bure hasa anapoona kwamba anasinzia. Inafaa ajipumzishe kidogo au atembee kidogo ili kupata hewa safi, halafu arudie kusoma. Ikiwa ni usiku, anaweza hata akaenda kulala ili aamke alfajiri kuendelea na masomo wakati hana chelewa ya usingizi. Ifahamike kwamba binadamu anapaswa angalau kulala muda wa saa sita na saa nane ili akili na mwili viweze kufanya kazi vyema. Pia, anaposoma, ahakikishe kwamba hana njaa wala kushiba sana kupita kiasi.

Wakati wa mtihani, mtahiniwa anafaa kuamka mapema kama kawaida. Afike darasani kabla ya muda rasmi wa kuanza mtihani. Apatiwapo karatasi ya maswali, asome maagizo kwa makini na ayaclewe vizuri kabla ya kuanza kujibu maswali. Kufuata maagizo aliyopewa pia ni sehemu ya mtihani. Asilimia kubwa ya watahiniwa hufeli mtihani kwa kuyapuuza maagizo yaliyotolewa. Kumbuka kuwa mtu hutungiwa mtihani, hajitungii mwenyewe.

  1. Mwandishi anazingatia nini katika aya ya kwanza?
    1. Mtu akifanya maandalizi vyema anaweza kuvuna siku hiyo hiyo
    2. Hakuna haja ya kuyafanya mambo hatua kwa hatua ila kwa mkupuo
    3. Ili jambo lolote kufanikiwa linahitaji kupewa subira
    4. Wakulima ndio watu wanaotakikana kuwa na subira
  2. "...akafyeka kichaka, akalima, akapanda, akapalilia..." 'ka' imetumikaje katika muktadha huu?
    1. Mfululizo wa matukio
    2. Kuradidi kwa matukio
    3. Usisitizo wa matukio
    4. Mkururo wa matukio
  3. Ratiba kwa mwanafunzi imemithilishwa na
    1. ndege kwa rubani
    2. mwanafunzi na bidii
    3. mtahiniwa na mtihani
    4. dira kwa rubani
  4. Mwanafunzi anayesomasoma tu bila kuwa na ratiba hutokewa na nini?
    1. Kufeli katika mitihani yake kila mara
    2. Kuyasoma masomo anayoyahenzi pekee
    3. Kuyadurusu hata yale masomo asiyoyapenda
    4. Hujiandaa barabara dhidi ya mitihani ijayo
  5. 'Ukasuku katika kusoma unamaanisha nini kulingana na mwandishi?
    1. Kusomasoma mambo mengi ambayo hayakuhusu
    2. Kusomasoma kwa kukariri tu bila kuelewa
    3. Kusoma jinsi kasuku anavyosoma
    4. Kusoma na kuropokwa kwa kuiga kasuku
  6. Ni kwa nini mwanafunzi anafaa kusomea mahali patulivu?
    1. Ili aweze kuwa na vitu vinavyohitajika
    2. Kuna wengine wanaopenda kusoma huku muziki ukidunda
    3. Ili yanayosomwa yaweze kueleweka bila shida yoyote
    4. Kwa kuwa muziki hautahiniwi katika mtihani wowote
  7. Mwanafunzi anayesoma tu somo moja kila wakati hatimaye
    1. hupita vizuri mitihani yake
    2. hujiburudisha
    3. huchoka akili
    4. hafaulu mtihani wake
  8. Ni mambo gani mwanafunzi hafai kufanya anapodurusu ili kujiandaa kufanya mtihani? 
    1. Asome mchana na usiku bila kupumzika 
    2. Ale lakini asishibe kupita kiasi
    3. Asisome huku akiwa na chelewa ya usingizi
    4. Asiendelee kusoma iwapo anahisi uchovu
  9. Mwanafunzi anapofanya mtihani bila kusoma na kufuata maagizo ni sawa na
    1. anayefanya mtihani akipanga kufeli
    2. anayejitahini na kuyajibu maswali yake mwenyewe
    3. wanafunzi wale werevu wanaoanguka mtihani
    4. anayechelewa kufika kwenye chumba cha mtihani
  10. Baadhi ya wanafunzi waliojiandaa vyema hufeli mtihani kwa
    1. kufanya mtihani pasi kusoma maagizo
    2. kufanya mtihani palipo na kelele nyingi
    3. kuanza kujibu maswali pasi kusoma na kuelewa maagizo
    4. kufanya asilimia kubwa ya maswali kwa papara 

Soma habari inayofuata kisha ujibu maswali 41-50

Nilikuwa nimeungojea wakati huo kwa hamu na ghamu. Japo niliona kuwa siku hiyo ilikuwa mbali, hauchi hauchi unakucha, hatimaye iliwadia. Mwalimu wetu alikuwa anasisitiza kuwa achanikaye kwenye mpini hafi njaa; waaidha, mchumia juani hulia kivulini. Wahaka usio na kifani ulinivaa kwani nilifahamu kuwa ni vyema kujiandaa mapema ili niende kupokea Hidaya yangu. Furaha mpwitompwito ilinivaa kwelikweli.

Niliondoka kitandani huku nikiimba nyimbo za furaha. Nilijua kuwa safari yangu ingechukua takriban saa tatu unusu. Tayari ilikuwa saa thenashara na sherehe ingeanza mida ya saa nane. Kwa pupa nilivalia sare zangu za shule yangu ya awali. Mwalimu mkuu ambaye angeandamana nami alikuwa amenishauri niweze kuvalia sare hizo. Hafla hiyo yote ingeonekana kwenye televisheni zote nchini. Alikuwa akitaka sare hiyo ipate kunadi shule yake ambayo ilikuwa haijatia fora kwa mwongo mmoja mtawalia. "Shule ya upili ya Busara itatambuliwa leo na dunia nzima," nilijisemea kimoyomoyo. Niliwaza na kuwazua kuhusu maisha ya chuo.

Baada ya kujiandaa, niliharakisha kufika katika kituo cha mabasi. Inshallah, nipate basi bado halijaondoka. Mwalimu mkuu alikuwa tayari amekata nauli ya watu wawili. Basi lenyewe lilikuwa jipya. Mlikuwa na abiria wengi ambao walikuwa wameabiri. Basini mlikuwa na viti vinne ambavyo havikuwa na abiria. Mwalimu aliniambia kuwa twende kutafuta staftahi. Tuliandamana naye kuelekea kwenye mkahawa tukanywa chai kwa mahamri. Japo mwalimu alitaka tunywe kwa haraka, chai ile ilikuwa moto ajabu. Hata hivyo, tulijikaza tukaimaliza. Tulirudi kituoni huku tukihema na kutweta. Tulifahamishwa kuwa basi lilikuwa limeondoka. Kwa hivyo ilitulazimu kusubiri saa moja kabla ya basi jingine kufika. Nilitekwa na hisia za huzuni lakini nikajizuia kulia. Hapo ndipo nilianza kusinzia na kukumbuka maisha yangu yalivyokuwa.

Nilikuwa nimezaliwa katika familia ya ukata. Mazingira niliyokulia yalikuwa yenye matatizo chungu nzima. Haya ndiyo yaliyonifanya kusoma kwa bidii ili niinusuru familia yetu kutokana na uchochole. Nilipopelekwa katika shule ya msingi nilitia fora masomoni nikaweza kujiunga na shule ya sekondari ya kutwa pale karibu na kwetu. Kupitia wadhamini wenye ukarimu si haba niliweza kukamilisha masomo yangu na kupata alama ya A iliyonipa hadhi niliyokuwa nayo.

Mawazo yangu yalikatizwa na milio ya hofu. Mwalimu wangu aliniashiria kitu. Nilipotazama upande wangu wa kulia niliona basi ambalo nilikuwa nikilisubiri likigongana na lori la takataka. Niliharakisha kwenda kuwasaidia watu waliokuwa wamejeruhiwa. Kwa nyota ya jaha, wote walikuwa salama salimini. Lakini tatizo la usafiri likatokea tena. Basi hilo lilihitajika kukarabatiwa tena kabla ya kuendelea na safari. Pasipo budi hubidi.

Punde si punde, simu ya mwalimu ilitoa mlio. Alitazama kidogo kisha akaanza kutetemeka kama aliyetoka kwenye friji. "Wamepiga simu" alisema. Aliichukua, akazungumza nayo kisha nikaona akitabasamu. Baada ya kumaliza, alinifahamisha kuwa sherehe ile ilihairishwa hadi wiki ambayo ingefuata. Nilifurahia sana kwa kuwa nilikuwa nimekata tamaa-muda wetu ulikuwa umekwisha. Tuliamua kurudi nyumbani japo tulikuwa tumechoka hoi bin tiki.

  1.  Ni kwa nini mwandishi wa makala haya alikuwa na furaha?
    1. Siku yenyewe ilikuwa imengojewa kwa hamu na ghamu
    2. Jitihada zake masomoni zingetambuliwa siku hiyo
    3. Alikuwa ametuzwa kwa bidii zake
    4. Maisha yake yangebadilika siku hiyo
  2. Kulingana na aya ya pili ni kweli kusema kuwa
    1. mwandishi alikuwa amefaulu katika mtihani wa shule ya msingi
    2. shule ya Busara ilikuwa na utamaduni wa kung'aa mtihanini
    3. mwandishi hakutarajiwa kuvalia sare ya shule ya awali
    4. hafla hiyo ilitarajiwa kuonyeshwa kwenye televisheni za kitaifa
  3. Msimulizi alivalia sare
    1. kwa kuwa alinuia kuitumia kunadi umaarufu mpya wa shule hiyo
    2. alikuwa amefanya vizuri katika mtihani uliotangulia
    3. kwa kuwa alikuwa na furaha mpwitompwito
    4. kwa kuwa walikuwa waandamane na mwalimu mkuu
  4. Mwandishi wa makala haya alitarajiwa kufika shereheni saa ngapi?
    1. Saa thenashara
    2. Saa nane mchana
    3. Saa saba za asubuhi
    4. Saa kumi na mbili
  5. Lengo la kujitahidi masomoni ilikuwa 
    1. kuinua hali ya jamii aliyoishi
    2. kujipatia shahada na kazi bora 
    3. kuimarisha hali ya jamaa yake
    4. kupata tunu maridhawa
  6. Kuachwa na basi kwa mwandishi
    1. kulimkumbusha shida alizokulia kijijini
    2. kulimfanya akate tamaa kuhusu zawadi yake
    3. kulimfanya aende kutafuta staftahi
    4. kulimfanya afanye bidii masomoni
  7. Taarifa hii inatoa sifa gani kwa mwandishi wa makala haya?
    1. Mkakamavu, mwenye moyo mwepesi
    2. Mkakamavu, mwenye moyo thabiti
    3. Mchochole, mwenye moyo thabiti
    4. Mlegevu, mwenye mori kubwa
  8. Tunajifunza nini kuhusiana na maisha ya mwandishi?
    1. Mafanikio hupatikana tu wadhamini wakijitolea
    2. Wanaojiunga na shule za kutwa hujiunga na vyuo vikuu
    3. Wenye elimu ya juu hupata tunu masomoni
    4. Mafanikio huweza kupatikana hata na walio na uwezo duni wa kifedha
  9. Mwandishi alitabasamu katika aya ya mwisho kwa kuwa
    1. alikuwa na nafasi nyingine ya kuhudhuria sherehe
    2. alimwona mwalimu wake akitabasamu
    3. aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kuchoka
    4. hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali iliyotendeka
  10. "... kutetemeka kama aliyetoka kwenye friji." Ni tamathali gani ya lugha iliyotumiwa kwenye kifungu hiki?
    1. Methali
    2. Istiari
    3. Tashbihi
    4. Msemo

INSHA

Andika insha ya kusisimua isiyopungua ukurasa mmoja na nusu huku ukimalizia kwa kifungu kifuatacho:-

....................................................................................... nilifurahishwa na tabia ya utu wema wa rafiki yangu.

MWONGOZO

swa ms 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 5.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students