Friday, 14 April 2023 13:39

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 2 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua ibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Klabu ..............1.................. Kipaumbele yaendelea kujipinda  ..............2.................. kuhakikisha kuwa tuzo  ..............3.................. msimu  ..............4.................. wa  ..............5.................. la mwadhamu Changuchetu imetwaliwa. Vijana  ..............6.................. wameapa kwa  ..............7.................. vipana kuwa wataendeleza vipaji  ..............8.................. kwa kusakata gozi kuanzia mashinani hadi kwenye ngazi za kimataifa. Kutokana na uchechefu wa ajira, ni muhimu vijana kujisakia  ..............9.................. vya kujipatia  ..............10.................. wa kila siku badala ya kungojea kuajiriwa.

  1.                      
    1. cha
    2. ya
    3. za
    4. la
  2.                  
    1. mkono
    2. kichwa
    3. mgongo
    4. mguu
  3.                
    1. iliyotengewa
    2. lilitengewa
    3. zilizotengewa
    4. yaliyotengewa
  4.                  
    1. hii
    2. hizi
    3. hiyo
    4. huu
  5.                  
    1. kikombe
    2. kombe
    3. nishani
    4. medali
  6.                  
    1. vingi
    2. wengi
    3. kwingi
    4. pengi
  7.                
    1. vinywa
    2. vidomo
    3. ndimi
    4. matamshi
  8.                
    1. chao
    2. vyao
    3. yao
    4. zao
  9.                  
    1. vitegauchumi
    2. sera
    3. nyenzo
    4. mawanda
  10.                        
    1. pato
    2. riziki
    3. mkate
    4. bahati

Tangu utotoni,  ..............11.................. nikijitenga ..............12.................. matumizi ya dawa za kulevya kwa vyovyote vile. Dawa ..............13.................. za kulevya zimedhoofisha maisha ya wengi  ..............14.................. chipukizi na larwatia kichaa, kisha kuwasafirisha  ..............15.................. Dawa zenyewe zina madhara chungu furiko kwa watumizi na wasio watumizi wa moja kwa moja.

  1.                      
    1. nilikuwa
    2. nimekuwa
    3. ningekuwa
    4. nishakuwa
  2.                    
    1. katika
    2. kwa
    3. na
    4. dhidi
  3.                  
    1. hii
    2. hiyo
    3. hizi
    4. haya
  4.                
    1. halisi
    2. hususan
    3. mahsusi
    4. hasi
  5.                    
    1. mbinguni
    2. peponi
    3. jongomeo
    4. mawinguni

Kutoka swali la 16-30, jibu swali kulingana na maagizo?

  1. Je, ni sentensi gani iliyotumia o-rejeshi tamati kwa usahihi?
    1. Mifugo -inyweshayo ndio wetu.
    2. Malango yafunguliwayo ndiyo yaliyopambwa.
    3. Watoto wanaoimba wana sauti nyororo ajabu.
    4. Sisi tusiyo na vitabu vya hadithi tusome nini?

Tumia kiunganishi bora zaidi kujazia kihasho

  1. Walijizatiti vilivyo ...................................... hawakufua dafu mbioni.
    1. lau
    2. seuze
    3. na
    4. ingawaje
  2. Ni pambo gani lililo tofauti na mengine kimatumizi?
    1. Kipini
    2. Shemere
    3. Kishaufu
    4. Kifumanzi
  3. Chagua sentensi iliyotumia "kwa" ya kimilikishi.
    1. Kushinda kwa mbunge wetu uchaguzini kulitiliwa shaka.
    2. Walisamehewa kwa kuwa walikuwa na mtetezi hodari.
    3. Tukifika kwake tutampokeza zawadi kochokocho.
    4. Mgonjwa akizidiwa mumpeleke kwa mganga.
  4. Kinyume cha: Ajuza alianika nguo asubuhi ni.
    1. Shaibu alianua nguo jioni.
    2. Ajuza alianika nguo jioni.
    3. Shaibu hakuanika nguo asubuhi.
    4. Ajuza alianua nguo asubuhi.
  5. Teua sentensi iliyoakifishwa vilivyo. 
    1. Ala! kwani unanikumbuka? 
    2. Mama we! kumbe leo ni sikukuu? 
    3. Acheni uzembe. Mkiendelea hivyo... 
    4. Njooni twende kwa kina Rosa
  6. Ni sentensi ipi iliyo sahihi kisarufi? 
    1. Mtainunua mitamba ipi?
    2. Minana waliotegwa walikuwa wangapi?
    3. Garini mlikuwa na abiria kumi na nane na dereva.
    4. Ikiwa hautanisaidia, nami pia sitakusaidia.
      Kamilisha methall ifuatayo kwa ustadi,
  7. Nguo ya kuazima
    1. matako hulia mbwata.
    2. ni kuondoka na mavi.
    3. hakistahimili kilemba. 
    4. haisitiri matako.
      Ni upi ukanusho sahihi wa sentensi ifuatayo?
  8. Mtungi ulionumuliwa umepotea. 
    1. Mtungi ulionunuliwa haujapotea.
    2. Mtungi usionunuliwa haujapotea. 
    3. Mtungi usionunuliwa hujapotea. 
    4. Mtungi usionunuliwa hujapotea.
  9. Kitenzi kutokana na nomino mfinyanzi ni
    1. ufinyanzi. 
    2. finyanzi.
    3. finyanga.
    4. finya.
  10. Ukitaka kukaza au kulegeza parafujo, unashauriwa kutumia
    1. keekee.
    2. bisibisi.
    3. nati.
    4. fuawe.
  11. "Miti hii ina matunda" kwa ukubwa ni
    1. Majiti haya yana matunda.
    2. Majiti haya yana majitunda. 
    3. Miti hii ina majitunda.
    4. Majimiti haya yana majitunda.
  12. Tegua kitendawili kifuatacho. Tandika mkeka tule kunazi.
    1. Jahazi na tanga 
    2. Ugali
    3. Mbingu na nyota
    4. Maji ya mto
  13. Chagua sentensi yenye matumizi sahihi ya "-nge".
    1. Tungelisukuma lingeenda
    2. Wangesoma wasingelianguka mtihani. 
    3. Tusingalionana tusingalisaidiana. 
    4. Ningelijua ningelijitahidi.
  14. Bingwa wa kufua vyuma huitwa
    1. dobi.
    2. sonara.
    3. mjumu.
    4. mhunzi.

Soma kifungu kisha ujibu maswall 31-40.

Waja huwa na akili razini na tambuzi ya kukabiliana mkabala na matatizo yao lakini utekelezaji ndio huwa changamoto. Hebu tuangalie kuhusu ajali barabarani. Baada ya kugundua chanzo cha ajali, hatua muhimu zilichukuliwa. Vidhibitimwendo viliwekwa ili kuzuia magari yasiende kasi zaidi. Alikanda ya usalama ilikuwa na jukumu ili pakitokea ajali, abiria wasirushwe nje kupitia viooni na madereva kupewa vibali vinavyoonyesha kuwa wao ni raia wema ili mshikausukani asiwe ni jambazi anayetafutwa na polisi. Hayo yote ni mema. Lakini ajali zimeisha au bado watu wanaangamia barabarani? Tatizo lipo wapi?

Nilifanya utafiti na kugundua penye tatizo. Nimegundua kuwa matatizo yangalipo, nayoni nyeti. Kubwa mno likiwa jangamizi la uzungukaji wa mbuyu. Kupokea rushwa kwa maafisa wa usalama kunachangia sana. Wahudumu wengi hubeba abiria wengi kupita kiasi na kuwahonga maafisa ili wasitiwe nguvuni. Kwa sababu hiyo abiria wengi hawawezi kufunga mikanda ya usalama. Ajali inapotokea watu wengi huangukiana kwa sababu ya kusongamana.

Kuna wale waliovitoa vidhibitimwendo na magari yao huenda kwa kasi sana. Wakati mwingine wenye magari huwafanyisha kazi kwa muda mrefu madereva na wasaidizi wao. Hilo niligundua siku moja ambapo nilikarwa nikisafiri kwa basi. Niliketi karibu na dereva na kujionea vituko ambavyo siwezi kusahau. Gari lilikuwa likienda kwa kasi ungedhani lingepaa. Niliingiwa na wasiwasi mpaka nikaamua kumsaili dereva.

"Mbona unaendesha gari hivyo?" Hakunijibu.

"Huoni kuwa unayahatarisha maisha yetu?"

"Unataka nikupishe uendeshe gari? Sitaki kufunzwa kazi. Unadhani maisha yako pekee ndiyo yaliyo humu garini? Mimi nina haki ya kuenda kwa kasi. Nilitoka Mombasa usiku. Sikulala. Nilifika Nairobi alfajiri na ba do ninarudi Mombasa mapema angaa nilale."

Sikuwa na la kujibu. Mshale wa kasi ulikuwa umelalia mia moja na arubaini. Sikuongea neno. Tulipofika Mtito Andei, nilishuka. Sikuliabiri gari hilo tena. Niliamua heri kupoteza pesa kuliko kupoteza maisha, uhi niuthaminio. Nilijipa moyo kwa kusema "kwa mwoga huenda kicheko". Nililiacha likaenda na kuliahiri jingine. Tulipofika Manyani, tuliwakuta watu wakilia kando ya barabara na kuomba msaada. Basi lilikuwa msituni. Tulisimama na kuwasaidia majeruhi. Wengi walikuwa wamekufa. Nilipashwa habari kuwa dereva alisinzia na kupoteza mwelekeo.

Tunapaswa kushirikiana sote kama tunataka kukabiliana na matatizo kama vile ajali barabarani. Hata kama tunajua kuwa ajali haina kinga, ajali haitokei yenyewe bali husababishwa na binadamu.

  1. Tatizo kubwa la binadamu ni lipi? 
    1. Kutekeleza mawazo mazuri waliyo nayo.
    2. Kuwa na mawazo mazuri ambayo yanaweza kutatua matatizo waliyo nayo. 
    3. Kujua chanzo cha matatizo ambayo yanawakabili katika nyanja mbalimbali. 
    4. Kutotekeleza mawazo mema waliyo nayo.
  2. Kazi ya vidhibitimwendo ni
    1. kufanya magari yasiende.
    2. kuhakikisha kuwa magari yanaenda kwa mwendo uliokubalika.
    3. kufanya magari yaende polepole ili ajali isitokee.
    4. kuzuia ajali isitokee wakati wowote..
  3. Kwa nini madereva hupewa vibali vya uraia mwema?
    1. Ili waendeshe magari kwa ustadi mkubwa 
    2. Kuhakikisha kuwa si wahalifu wanaojificha katika udereva.
    3. Kuhakikisha kuwa gari lina vidhibitimwendo na mikanda ya usalama.
    4. Ili kumzuia dereva asiendeshe gari bila kuzingatia sheria.
  4. Kutoa au kupokea rushwa kunachangia vipi kwa kuongezeka kwa ajali?
    1. Askari wanawaruhusu madereva kuendesha magari kwa kasi maana hawawaangalii.
    2. Idadi ya wanaonusurika ajalini huongezeka maradufu.
    3. Maafisa na madereva wengi hupoteza ajira zao.
    4. Sheria za barabarani huvunjwa ovyoovyo
  5. Kulingana na taarifa hii, ni nini kinachoshababisha ajali nyingi za barabarani?
    1. Ubebaji wa abiria kupita kiasi. 
    2. Magari kuendeshwa kwa kasi mno.
    3. Madereva walevi na barabara mbovu. 
    4. Magari kupasuka magurudumu.
  6. Wenye magari wanaweza kufanya nini ili kupunguza ajali barabarani?
    1. Kuwaamuru madereva na wasaidizi wao kuzunguka mbuyu.
    2. Kuwaajiri madereva wakongwe wenye ujuzi kuliko vijana.
    3. Kuwawekea mipaka nafuu ya nyakati za utendakazi wafanyakazi wao.
    4. Kununua magari mengi ili abiria wasihangaike.
  7. Kulingana na jinsi dereva alivyomjibu mwandishi, ni wazi kuwa
    1. alikuwa na hasira kwa sababu ya kufanya kazi kwa muda mrefu.
    2. aligundua kuwa mwandishi hakujua kuendesha gari.
    3. alikuwa na tabia ya ujeuri na ufidhuli. 
    4. mwandishi hakuwa na haki ya kuuliza lolote.
  8. Ni kweli kusema gari la kwanza alilosafiria mwandishi
    1. liliwabeba abiria wengi waliobanana kama ndizi.
    2. halikuwa na kidhibitimwendo.
    3. liliendeshwa na dereva mlevi.
    4. liliwafikisha abiria salama.
  9. Aya ya mwisho yaenda sambamba na methali ipi hapa?
    1. Mkono mmoja hauchinji ng'ombe.
    2. Ajali haina kinga wala kafara.
    3. Zinguo la mtukutu ni ufito.
    4. Heri kufa kuliko kufariki.
  10. Kichwa bora zaidi cha habari hii ni
    1. Kwa mwoga huenda kicheko, kwa shujaa kilio.
    2. Ajali barabarani.
    3. Jinsi ya kuzuia ajali barabarani 
    4. Siku njema huonekana asubuhi.

Soma kifungu kisha ujibu maswali41-50.

Msonge ni nyumba ya mviringo yenye paa lenye umbo la pia. Zamani wenyeji walikuwa wakijenga nyumba za namna hii. Kitu kikubwa cha kushangaza juu ya nyumba hizi ni kuwa zina sehemu tumbi nzima.

Ukianzia chini ya nyumba hizo utakuta msingi. Hapa wenyeji walikuwa wakichimba chini na kupatandaza vizuri kwa kupapigilia kwa kutumia vijiti maalumu. Baadhi ya makabila yalivihifadhi vijiti hivyo ili kutumiwa kwa ujenzi mwingine. Sehemu hizo zimalizikapo, huwa sakafu za nyumba hizo.

Ukienda juu kidogo kuna ukuta. Ukuta huu ulijengwa kwa kusimamishwa nguzo katika mviringo kufuatana na sakafu na kukingamana na boriti zilizosimamishwa. Baada ya hapo udongo ulikandikwa katikati ili kukamilisha ukuta. Ukuta wa nyumba ya msonge ulikuwa na sehemu mbili. Sehemu ya chini iliitwa kiuno cha nyumba nayo sehemu ya juu haikuwa na jina lakini haikuwekewa mawe kama kiuno cha nyumba.

Ulipojengwa ukuta, uliwekwa mti wa juu kabisa ambao kazi yake ni kushikilia paa. Mti huu huitwa kombamoyo au mtambaapanya. Mbali na kuwa na mtambaapanya, pia ukuta huo uliwekewa vizingiti vya milango na madirisha na hatimaye milango yenyewe na madirisha.

Hatua ya mwisho katika ukuta ilikuwa ni kuusiriba. Ukuta huo ulitupiwa udongo uliokuwa umekanyagwakanyagwa na kulainishwa kwa mikono au mwiko maalumu ili kuufanya upendeze.

Katikati ya ukuta na paa, lilijengwa dari. Zilichukuliwa boriti upande hadi upande. Boriti hizo zilifungwa fito pia. Baada ya kufungiwa fito nyingi sana dari hilo lilikandikwa na haikuachwa nafasi ya kupanda juu kama madari ya kizungu. Hii ni kwa sababu hakuna kitu chochote kilichowekwa juu. Sehemu iliyowekewa kitu chochote ilikuwa uchaga. Uchaga ulikuwa sehemu ya mekoni ambako kuliwekwa kuni. Sehemu hiyo ilijengwa juu ya meko ili kupika kufanyiwe chini na kuni ziwekwe juu. Hii ilikuwa kwa sababu wakati wa masika, ilikuwa shida kwenda kuchanja kuni kwa sababu ya kuloa maji ya mvua.

Sehemu ya juu kabisa ya msonge kulikuwa na paa. Ujenzi wa paa ulihitaji fundi kuliunda na kuliczeka. Paa lililojengwa kivoloya halikudumu kwa muda mrefu maana liliharibiwa na mvua na upepo baada ya siku chache.

Katika ujenzi wa paa, yalihitajika mapau ambayo yaliwekewa fito pia. Fito hizo zilifungwa kwa kamba maalumu. Baada ya kufungwa fito, paa liliezekwa na fundi. Uczekaji ulianzia chini kuelekea juu hadi kilele cha mlingoti. Hapa kumbuka kuwa ule mlingoti ulisimamishwa kutoka katikati ya sakafu hadi katikati ya paa. Fundi wa kuezeka alitakiwa kuwa na ujuzi wa kukanyaga sehemu alizoezeka bila kuzitia dosari. Pili, paa lilitakiwa lisivuje kabisa na mwisho kabisa, lilihitajika likae hivyo hivyo miaka nenda miaka rudi bila kuezekwaezekwa mara nyingi.

Kuna nyasi za aina nyingi zilizotumiwa kuezeka. Sehemu za pwani, makuti yalitumika zaidi na bara zilitumika nyasi tofautitofauti. Kilichofanya nyasi hizo kuwa sawa sawa ni kuwa wenyewe walizichagua kwa makini. Zilihitajika kuwa nyasi ambazo hazikuchakaa haraka na zilizopatikana kwa urahisi.

Baada ya paa kuisha, fundi aliweka namna ya kofia kileleni. Lilichukuliwa bonge la udongo na kukatwa katika mviringo mzuri. Kwisha yote hayo, kijiti chenye ncha ndefu kiliwekwa kileleni na kupitishiwa lile bonge ili likae pale pale sawa sawa. Ujenzi huo ulikuwa wa kuzuia mvua isiingie ndani kupitia kileleni.

Ndani ya nyumba hamkuwa na vyumba lakini ilipobidi nyumba hizo ziligawanyika sehemu mbili tu. Yaani sebule na sehemu ya kulala.

  1. Nyumba ya msonge iligawanywa katika sehemu mbili, nazo ni
    1. sebule na jikoni.
    2. jikoni na sehemu ya kulala. 
    3. sehemu ya kulala na sebule. 
    4. uchaga na sakafu.
  2. Ni kitu gani kilichostaajibisha kuhusu msonge?
    1. Ustadi uliotumika katika kuujenga.
    2. Umbo la pia katika paa na sakafu ya mviringo.
    3. Vyumba mbalimbali vilivyopatikana katika msonge.
    4. Sehemu nyingi zilizokuwa katika nyumba hii.
  3. Ni kweli kusema kuwa:-
    1. sakafu ya nyumba ilichimbwa, kutandazwa kisha ikapigiliwa
    2. vijiti vilivyotumiwa kupigilia sakafu vilihifadhiwa na makabila yote
    3. vijiti maalumu vilichimbiwa chini vikawa sakafu
    4. ujenzi wa sakafu ulikuwa na hatua mbili zilizofuatwa.
  4. Hatua ya mwisho katika ujenzi wa kiambaza ilikuwa gani?
    1. Kusimamisha nguzo katika mviringo kulingana na sakafu.
    2. Kufungwa kwa fito nje na ndani.
    3. Kukandikwa kwa udongo katikati ya fito. 
    4. Kukisiriba kwa udongo laini.
  5. Ni nini kilichotumika kuufanya ukuta wa msonge kuwa imara na kushikilia paa? 
    1. Kuwekwa kwa mtambaapanya katika kombamoyo
    2. Kwa kuweka bonge la udongo katika mviringo
    3. Kwa kuweka kijiti chenye ncha ndefu 
    4. Kuwekwa kwa mtambaapanya
  6. Ni gani ni tofauti kuu ya dari la msonge na lile la kisasa?
    1. Dari la msonge ilikandikwa kwa udongo. 
    2. Dari la msonge huwa na uchaga. 
    3. Dari la kisasa huachiwa nafasi ya kupandia juu.
    4. Dari la kisasa huhifadhiwa kuni.
  7. Fundi wa ujenzi wa paa alionyesha ujuzi wake katika yafuatayo isipokuwa
    1. kujenga paa lililodumu kwa muda mrefu.
    2. kukanyaga sehemu zilizoezekwa bila kuzitia dosari.
    3. kuczeka paa lisilovuja.
    4. kuezeka paa lililoonekana maridadi.
  8. Ni wazo lipi ambalo ni sahihi kuhusu paa?
    1. Mapaa yote ya msonge yaliezekwa kwa makuti.
    2. Mapaa yote ya msonge yaliezekwa kwa nyasi pekee.
    3. Nyasi zilizopatikana kwa urahisi katika eneo fulani ndizo zilizotumika kuezekea mapaa.
    4. Nyasi zozote zingetumika kuezekea mapaa. 
  9. Mvua ilizuiliwaje isiingie ndani kupitia kileleni?
    1. Kwa kutumia bonge la udongo lililokatwa katika mviringo mzuri.
    2. Kwa kuezekwa nyasi ambazo hazikuchakaa kwa urahisi.
    3. Kwa kupitishia kijiti kirefu chenye ncha ndefu kilichopitishwa katika bonge la udongo kuliweka sawa sawa.
    4. Kwa kukanyaga kwa makini sehemu hiyo yenye bonge na kijiti kirefu.
  10. Ni kichwa kipi kifaacho zaidi taarifa hii?
    1. Msonge.
    2. Fundi wa kujenga msonge.
    3. Ujenzi wa nyumba za kale.
    4. Ujenzi wa msonge.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Andika insha ya kusisimua ukiamalizia kwa maneno haya:

....................................................................................................Tangu siku hiyo, wanafunzi wote wa darasa letu waliamini kuwa hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana bila bidii.

MWONGOZO

swa adad

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 2 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students