Displaying items by tag: Shughuli za Kiswahili

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5

Mwanafunzi:   Shikamoo mwalimu?
Mwalimu:        Marahaba Juma. Karibu ukae kitini
Mwanafunzi:   Asante mwalimu
Mwalimu:        Nikusaidiaje Juma?
Mwanafunzi:   Nimekuja kulalamikia uchafuzi wa mazingira shuleni. Wanafunzi wengi wamekataa kufuata maagizo ya kutupa taka kwenye                                 majalala na kumwaga maji chooni baada ya haja zao humo.
Mwalimu:        Asante Juma kwa kuwa mwanafunzi mtiifu na anayewajali wengine.
Mwanafunzi:   Nimehongera mwalimu. Wamesahau jinsi ulivyotufunza kuwa mazingira machafu yanaweza kusababisha magonjwa mengi Mwalimu:         Unakumbuka baadhi ya magonjwa hayo?
Mwanafunzi:    Naam mwalimu! Kuna ugonjwa wa kipindupindu, kuna kichocho na hata kuumwa na tumbo na maleria.
Mwalimu:         Vizuri sana. Haya twende darasani pako niwazungumzie tena wanafunzi hao kuhusu umuhimu wa kuyatunza mazingira yao
Mwanafunzi:   Asante mwalimu

  1. Jibu la shikamoo ni
    1. shikamooo
    2. marahaba
    3. sabalkheri
    4. asante
  2. Juma alienda kufanya nini ofisini?
    1. Kumsalimia mwalimu
    2. Kumshukuru mwalimu
    3. Kumkaribisha mwalimu
    4. Kulalamikia uchafuzi wa mazingira
  3. Tatataka zinafaa kutupwa wapi?
    1. Chooni
    2. Majalalani
    3. Darasani
    4. Uwanjani
  4. Mazingira machafu husababisha nini?
    1. Magonjwa
    2. Kiangazi
    3. Homa
    4. Nidhamu
  5. Ni ugonjwa gani ambao hausababishwi na mazingira machafu?
    1. Maleria
    2. Kichocho
    3. Kifua kikuu
    4. Kipindupindu

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 6-10

Kila muhula tunapokaribia kufunga shule kwa likizo, walimu wa shule yetu huandaa siku spesheli ya michezo. Shule yetu ya Malezi Bora huwa na wanafunzi mia nane. Siku ya michezo, wanafunzi wote pamoja na walimu hukusanyika uwanjani.

Wiki iliyopita ndiyo wiki tuliyoandaliwa michezo. Mchezo uliochezwa kwanza ulikuwa ni mbio fupi za mita mia moja. Moha, Talia, Amen and Mercy ndio waliochaguliwa kuanza. Wote walipanga mstari. "Ni nani atashinda leo?" Sara, mwanafunzi wa darasa la nane alishangaaa. Aliwaangalia marafiki zake. Prrr.... Firimbi ikalia. Moha na Amen wana mbio sana. Amen akawa anaongoza mbio hizo. Sara na wanafunzi wengine walishangiliwa kwa vifijo. Moha alitoka nyuma mbio sana akampita Amen kwenye mstari wa kumalizia na akawa wa kwanza. Talia naye alimaliza wa tatu huku Mercy akiridhika na nafasi ya nne. Yalikuwa mashindano na kufana sana.

  1. Kila mwisho wa muhula, walimu wa shule huandaa nini?
    1. Siku ya michezo
    2. Siku ya kufunga shule
    3. Wakati wa mtihani 
    4. Siku ya kuenda sokoni  
  2. Wanafunzi wa shule hii ni wangapi?
    1. 1000
    2. 80
    3. 800
    4. 500
  3. Ni mchezo gani ulioandaliwa siku hiyo?
    1. Mpira
    2. Mbio fupi
    3. Ndondi
    4. Mpira wa vikapu
  4. Ni wanafunzi gani walio na mbio sana? 
    1. Talia na Moha
    2. Moha na Amen
    3. Mercy na Talia
    4. Amen na Mercy 
  5. Ni mwanafunzi gani aliyeibuka mshindi?
    1. Talia
    2. Mercy
    3. Amen
    4. Moha

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 11-15

Zipo nyakati nyingine ambapo tunapatwa na matatizo ya kiafya yanayohitaji huduma za dharura. Matatizo haya hutokea mahali popote kama vile shuleni, njiani ama nyumbani. Haya yanapotokea huduma ya kwanza huhitajika ili kupunguza au kuzuia hali kuwa mbaya zaidi. Ni vizuri kujua kuwa tatizo dogo kama vile kusakamwa na chakula kooni linaweza kuwa na athari kubwa endapo halitashughulikiwa kwa haraka. Pia, jereha lisiposhughulikiwa upesi na kwa njia ifaayo, linaweza kuingiwa na wadudu na kufanya hali ya mwathiriwa kuwa mbaya zaidi.

Katika jamii, ni vyema kuwa na watu waliohitimu kutoa huduma ya kwanza. Watu hao wanapaswa kuwa na ujuzi wa kukabiliana na hali mbalimbali ambazo zinahitaji maarifa ya hali ya juu. Aidha, ni jambo zuri kuwa na chama cha huduma ya kwanza shuleni. Wanafunzi katika chama hiki hupewa mafunzo ya kukabiliana na ajali ndogondongo na matatizo ya kiafya.

  1. Matatizo ya kiafya huhitaji nini?
    1. huduma za dharura
    2. kutibiwa haraka
    3. kupuuzwa vizuri
    4. kuwatibu wagonjwa
  2. Tatizo la kiafya laweza kutokea wapi?
    1. Shuleni na nyumbani
    2. Tumboni na chumbani
    3. Kichwani na kinywani
    4.  Masomoni na pembeni
  3. Ni tatizo gani linaweza kuwa baya zaidi kulingana na ufahamu?
    1. Kunywa maji
    2. Kuoga bafuni
    3. Kusakamwa na chakula
    4. Kuenda haja
  4. Watu wanaostahili kufanya huduma ya kwanza lazima wawe na nini?
    1. Pesa
    2. Magari
    3. Dawa
    4. Ujuzi
  5. Ni jambo gani zuri linalostahili kuwa shuleni?
    1. Kuwa na hospitali shuleni
    2. Kuwa na chama cha huduma ya kwanza 
    3. Kuanzisha chama cha kuwafunza wanafunzi 
    4. Kuendeleza matibabu ya majeruhi

Some mtungo ufuatao kisha ujaze nafasi zilizoachwa wazi kwa jibu sahihi.

Zuri alikuwa mchoraji mahiri. Alipenda kuchora majora ___16___ leso yaliyopendeza sana. Watengenezaji leso walipenda ___17___ hiyo. Waliichukua na kuonyeshana kwenye majukuwaa ya biashara, Michoro hiyo ya Zuri ilipata umaarufu ___18___. Zuri alikuwa akipata cheki za pesa ___19___  sana kutokana na michoro ___20___.

   A  B  C  D
 16.  za  ya   la   wa 
 17.  michongo  mapambo   picha   michoro 
 18.  mkubwa  kidogo  kubwa  kikubwa
 19.  mingi  wengi  nyingi  mengi
 20.  yake  zao  yangu  zertu 


Kutoka swali la 21 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Chagua nomino katika sentensi hizi
    Darasa hili ni kubwa sana
    1. hili
    2. kubwa
    3. darasa
    4. sana
  2. Tulipikiwa chakula kizuri tukala
    1. Tulipikiwa
    2. Chakula
    3. Kizuri
    4. Tukala
  3. Mtoto wa kuku anaitwaje?
    1. Kinda
    2. Ndege
    3. Mwana
    4. Kifaranga
  4. Chagua sentensi yenye kiwakilishi cha nafsi ya kwanza
    1. Wewe ni mtoto mzuri
    2. Wao ni walimu wetu
    3. Sisi tutakutembelea kesho
    4. Nyinyi hamjui kupika chai
  5. Chagua kielezi cha namna katika sentensi hii Wanariadha waliokimbia vizuri walituzwa jana
    1. Jana
    2. Walituzwa
    3. Vizuri
    4. Waliokimbia
  6. Tegua kitendawili hiki. Ninatembea na paa mgongoni
    1. Kobe
    2. Nyumba
    3. Upepo
    4. Jua
  7. Chagua jibu ambalo si kiunganishi
    1. Lakini
    2. Nyeupe
    3. Pia
    4. Kwa hivyo
  8. Kamilisha sentensi hii kwa njia sahihi.
    Panya ameingia _____________________ shimo.
    1. ndani ya
    2. juu ya
    3. chini ya
    4. karibu na
  9. Jaza pengo kwa neno ambalo ni kinyume cha lililopigiwa mstari
    Nyanya ni mgonjwa lakini ______________ ni mzima
    1. mjomba
    2. baba
    3. kaka
    4. babu
  10. Kamilisha tashbihi ifuatayo.
    Karani ni mrefu kama
    1. barabara
    2. nyundo
    3. twiga
    4. ndovu

SEHEMU YA B: INSHA

Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo:-

MWIZI KIJIJINI

MARKING SCHEME

  1. B
  2. D
  3. B
  4. A
  5. C
  6. A
  7. C
  8. B
  9. B
  10. D
  11. A
  12. A
  13. C
  14. D
  15. B
  16. B
  17. D
  18. A
  19. C
  20. A
  21. C
  22. B
  23. D
  24. C
  25. C
  26. A
  27. B
  28. A
  29. D
  30. C

 

Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali 1-5

Rafiki:  Njoki, hebu njoo kidogo. Unafaa kuamshwa kidogo.
Njoki:   Kwa nini rafiki yangu? Kwani nimekosea? Haya niambie
Rafiki:  Usinielewe vibaya. Ninataka kukufahamisha kuwa wewe unafikiria vibaya kuhusu utamaduni wetu
Njoki:   Bado sikuelewi
Rafiki:  Ulisema kuwa hukutaka kusoma tena. Eti wanaosoma tu ni watoto wavulana.
Njoki:   Lakini si ni ukweli. Sisi tukiwa wakubwa tutaolewa tu.
Rafiki:  Hapana. Hayo ndiyo mabaya ya tamaduni zetu. Yameachwa hayo. Lazima mtoto wa kiume asome sambamba na wakike. Wote wana nafasi sawa. Ukisoma huenda mkawa
mwalimu, daktari ama mhandisi utuundie vitu mpya. Hebu soma kwa bidii.
Njoki:   Kama ni hivyo basi nitafanya bidii zaidi. Asante rafiki yangu.

  1. Kwa nini rafiki alimwita Njoki? Ili
    1. amwamshe kidogo
    2. waende kucheza
    3. wasome kidogo
    4. wafanye kazi za nyumbani
  2. Rafiki alitaka kumweleza nini Njoki?
    1. Kuhusu kazi ya walimu
    2. Kuhusu mazoezi ya mhandisi
    3. Kuhusu Njoki kuelewa vibaya utamaduni wao
    4. Kuhusu maisha yao magumu
  3. Kwa nini Njoki hakutaka kusoma?
    1. Hawakuwa na pesa za kumlipia karo
    2. Alijua angeolewa baadaye
    3. Masomo yalikuwa magumu
    4. Aliambiwa na wazazi wake aache masomo
  4. Siku hizi ni akina nani wanasoma sambamba?
    1. Wavulana na wasichana
    2. Wasichana pekee
    3. Wavulana pekee
    4. Wavulana na vijana
  5. Njoki angesoma angekuwa nini maishani?
    1. Mkulima, dereva, mtembezi
    2. Mchukuzi, mganga, mkulima
    3. Msomi, mtanashati, dereva 
    4. Daktari, mwalimu, mhandisi

Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 6-10.

Mimea ikipandwa mahali penye rutuba huota na kustawi. Pia huitwa kunawiri. Hii ni ile hali ya mimea kuonekana mizuri kwa kuwa inapata mahitaji yote muhimu kama maji, hewa, mbolea, madini na kadhalika. Mimea mingi kwa kawaida ikistawi huwa rangi ya kijani kibichi. Mimea huhitaji kupaliliwa. Huku ni kung'oa mimea isiyohitajika shambani. Mimea hiyo isiyohitajika huitwa nagugu. Mimea ikikua huvunwa. Mahindi na maharagwe hukaushwa na kuwekwa kwenye magunia ili kuihifadhi ili kutumiwa wakati wa usoni.

  1. Mimea hunawiri wakati gani?
    1. Ikipanda mahali penye rutuba
    2. Mvua ikiwa kidogo
    3. Ikipandwa mahali penye joto jingi
    4. Ikipandwa mahali hakuna rotuba
  2. Mimea kuonekana kuwa mizuri tunasema mimea
    1. imeharibika
    2. imekauka
    3. imefufuka
    4. imenawiri
  3. Mimea huhitaji nini ili kuwa katika hali nzuri?
    1. Maji kidogo, joto na hewa
    2. Maji, hewa, mbolea na madini
    3. Mbolea na maji pekee
    4. Madini na mbolea pekee 
  4. Rangi ya mimea huwa ni gani?
    1. Manjano
    2. Zambarau
    3. Kijani kibichi
    4. Samawati hafifu
  5. Ni nini maana ya kupalilia?
    1. kung'oa magugu au mimea isiyohitajika shambani
    2. kung'oa mimea iliyokwisha kumea
    3. kutoa mazao yaliyokwisha kukomaa 
    4. kukata mimea ili kutengeza mbolea

Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 11-15

Hapo zamani za kale, paliondokea mzee mmoja aliyeitwa Mkonobirika. Mzee huyu alikuwa mgumu kama jiwe upande wa pesa. Ilikuwa ni vigumu kwake kutoa hata shillingi moja kwa sababu yoyote ile. Alizitafuta Desa kwa bidii sana na alipozipata, aliziweka katika shimo alilochimba nyumbani kwake.

Siku moja rafiki yake alimshauri aziweke pesa kwenye benki. Akakataa akasema zikiwa huko hatakuwa akipata nafasi ya kuziona na kuzishikashika. Rafiki huyo akamwambia, "Unajua pesa zako siku moja zitaliwa na watu usiowajua. Ni afadhali basi uoe, upate watoto kisha watakuja kuzitumia pesa zako." Alikataa wazo la rafikiye. Siku moja aliwakisha moto na akasahau kuuzima baada ya kupika chakula cha jioni. Moto ule ukatatarika akawa amelala na likashika karatasi zilizokuwa karibu. Kilichomwamsha ni moshi mingi na joto jingi. Alishtuka na kuona nyumba yote imeshika moto. Akatorokea nje kunusuru maisha yake. Kila kitu kilichokuwa mle kilichomeka zikiwemo pesa zile.

  1. Mzee alikuwa mgumu kwa nini?
    1. Hakutaka kutumia pesa zake
    2. Alitumia pesa zake vibaya
    3. Aliwapa watu pesa zake.
    4. Watu hawakumpa pesa zake
  2. Mkonobirika alizificha wapi pesa zake?
    1. Katika benki
    2. Katika mifuko
    3. Chini ya kitanda
    4. Katika shimo alilolichimba nyumbani kwake
  3. Rafikiye Mkonobirika alimshauri afanye nini?
    1. Atumie pesa zake
    2. Azihifadhi pesa zake benkini-
    3. Awagawie maskini pesa zake
    4. Awekeze katika miradi mbalimbali
  4. Mkonobirika alikataa wazo la rafiki yake kwa sababu gani?
    1. Pesa zilikuwa nyingi mno
    2. Pesa zake zingepotea
    3. Pesa za benkini hazikuwa nzuri
    4. Asingeweza kuziona na kuzishikashika pesa zake
  5. Nyumba yake Mkonobirika ilichomeka kwa sababu gani?
    1. Aliwasha moto akasahau kuuzima
    2. Kulikuwa na tatizo la stima
    3. Watu waliirushia mafuta nyumba yake
    4. Mkewe aliichoma wakiwa usingizini

Jaza nafasi 16-20, kwa jibu sahihi.

Safari ___16___ iliwachukua muda wa siku ___17___ Walipofika Diani, walishangaa kuona mazingira tofauti ___18___ yale ya huko kwao. Kwanza, walifikishwa kwenye ufuo wa bahari. Hapo walikutana na ___19___  waliokuwa wamebeba samaki. Samaki ___20___ walikuwa wakiokwa na kukaangwa.

   A  B  C  D
 16.  hiyo  hicho   hilo   hayo 
 17.  mmoja  kimoja  moja  limoja
 18.  kwa  wa  pa  na
 19.  walikuwa  wavuvi  madereva  madaktari
 20.  nyingine  mingine  wengine  kwingine
  1. Andika udogo wa maneno haya;
    Mto, mji
    1. jito, jiji
    2. majito, majiji
    3. vijito, vijiji
    4. kijito, kijiji
  2. Kanusha sentensi hii
    Amekuja kututembelea
    1. Hakuja kututembelea
    2. Hajaja kututembelea
    3. Hatakuja kututembelea
    4. Asingekuja kutembelea  
  3. Sentensi hii imeandikwa katika wakati gani?
    Askari watakuwa wakilinda usalama wa kila mtu
    1. wakati ujao hali ya kuendelea
    2. wakati uliopita hali ya kuendelea
    3. wakati uliopo hali ya kuendelea
    4. wakati wa hali tegemezi
  4. Mtoto wa ngombe huitwaje?
    1. Kinyau
    2. Kifaranga
    3. Ndama
    4. Kinda 
  5. Tunasema mfupi kama nyundo na mnene kama
    1. makaa
    2. mlingoti
    3. pamba
    4. nguruwe
  6. Jaza pengo kwa kutumia kinyume cha nomino iliyopigiwa mstari katika sentensi hii.
    Baada ya kicheko chake kulikuwa na
    1. furaha
    2. huzuni
    3. kilio
    4. mshangao
  7. Andika neno jenga katika kauli ya kutendwa ili ujaze nafasi katika sentensi hii.
    Nyumba yake ime __________________________ (jenga) nyuma ya soko.
    1. jengwa
    2. jengewa
    3. jengeka
    4. jengesha
  8. Ni neno lipi ambalo ni kisawe cha runinga?
    1. Redio
    2. Rununu
    3. Tarakilishi
    4. Televisheni.
  9. Jaza silabi inayokosekana katika sentensi hiii
    Joto ____________ kizidi watu hutoa mashati
    1. ya
    2. li
    3. zi
    4. ki
  10. Andika wingi wa sentensi hii
    Kikapu kimefumwa
    1. Makapu yamefumwa
    2. Vikapu zimefumwa
    3. Likapu limefumwa
    4. Vikapu vimefumwa

SEHEMU YA B: INSHA

Andika insha ya kusisimua kuhusu

SHEREHE NYUMBANI

MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. B
  4. A
  5. D
  6. A
  7. D
  8. B
  9. C
  10. A
  11. A
  12. D
  13. B
  14. D
  15. A
  16. A
  17. C
  18. D
  19. B
  20. C
  21. D
  22. B
  23. A
  24. C
  25. D
  26. C
  27. A
  28. D
  29. B
  30. D

Soma makala yafuatayo halafu ujibu maswali yanayofuata.

G5SwaT3OS12023Q1

Katika msitu wa Eshikalame, Njiwa alijulikana sana kwa sauti yake ya kupendeza. Karibu kila mnyama na kiumbe katika msitu huo alimfahamu kwa ushauri wake aliowatolea. Kila wakati wa jua kuaga miti, ungewapata ndege wakiwa wamejaa kwenye mti ili kufurahia utamu wa nyimbo na ushauri wa njiwa. Wanyama mbalimbali pia walisimama chini ya mti huo. Siku moja, palitokea vita katika msitu huo. Wanyama na ndege walipigana bila kujali. Walipokuwa katika hali hiyo ya vita, Njiwa aliwakariria shairi lililofanya kuacha kupigana. Alianza hivi:

Na wenzangu sikiliza, vita ni kitu kibaya,
Wengi wetu angamiza, kuua bila ya haya,

Kwa makini kichunguza, hapakuwa na ubaya,
Sote tuweni pamoja, tuwe na amani tena.

Makosa yakitokea, usamehe tafadhali,
Vyema wewe kutulia, hasira naziwe mbali,
Jamani nakuambia, yote haya ni ukweli,
Sote tuweni pamoja, tuwe na amani tena.

  1. Kulingana na makala haya, Njiwa;
    1. alijua karibu kila mnyama na kiumbe.
    2. alijulikana na kila mnyama na kiumbe.
    3. alijulikana na wanyama na viumbe wengi.
    4. alikuwa akitolewa ushauri.
  2. Maneno 'wakati wa jua kuaga miti' yana maana gani jinsi yalivyotumika katika kifungu? 
    1. wakati wa jioni
    2. wakati wa mchana
    3. wakati wa adhuhuri
    4. wakati wa asubuhi
  3. Kibwagizo cha shairi lililokaririwa na Njiwa kina mizani mingapi?
    1. 15
    2. 4
    3. 2
    4. 16
  4. Tambua vina vya kati vya ubeti wa kwanza.
    1. ya
    2. za
    3. ja
    4. ya
  5. Ushauri wa Njiwa katika shairi unaweza ukarejelewa kwa methali gani?
    1. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. 
    2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    3. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
    4. Siku za mwizi ni arubaini.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.

G5SwaT3OS12023Q2

Hezekia Omulama, kijana aliyekuwa katika gredi ya tatu, alipewa shilingi mia mbili na shangazi yake mwezi wa Disemba. Wakati huo, Hezekia alikuwa mfupi kama nyundo. Baada ya kumshukuru shangazi yake, alitumia pesa hizo kununua sungura mmoja mdogo. Baada ya miezi sita, sungura huyo alizaa vitungule waliopendeza sana. Watoto hao wa sungura waliendelea kulishwa majani mbalimbali ambayo Hezekia na dada yake walichuma shambani. Alifuata ushauri wa wazazi wake kuhusu ufugaji wa sungura hadi alipokuwa na sungura wengi. Alianza kuuza sungura wachache ili apate pesa alizojiwekea katika benki. Baba yake alikuwa amemfungulia akaunti ya watoto.

Hezekia alizungumza na mama yake ili ampe nafasi ya shamba dogo hapo nyumbani pao. Alianza kupanda mboga na matunda. Wakati ambao hakuenda shuleni, yeye na marafiki zake walipalilia mboga na matundo ili kuondoa magugu. Walipomaliza kazi hiyo, Hezekia aliwapa marafiki zake matunda kadhaa kama shukrani. Pia, aliwapa mboga kidogo ili wapeleke nyumbani kwao. Hezekia ana mpango wa kuwa mwanabiashara mkubwa baada ya kumaliza masomo yake. 6.

  1. Hezekia alipewa pesa na nani?
    1. dada wa mama yake
    2. dada wa baba yake
    3. mfanyakazi wa nyumbani
    4. dada yake
  2. Kauli 'mfupi kama nyundo' ni mfano wa;
    1. nahau
    2. tashbihi ya tabia
    3. tashbihi ya umbo
    4. kitanzandimi
  3. Ni kweli kuwa sungura wa Hezekia alizaa Hezekia akiwa katika;
    1. Gredi ya tatu
    2. Gredi ya nne
    3. Gredi ya tano
    4. Gredi ya sita
  4. Kifungu kinaeleza kuwa Hezekia alikuwa na tabia gani;
    A. mtiifu, mwenye bidii
    B. mjanja, mwaminifu
    C. mwenye bidii, mwongo
    D. mpole, anayependa kucheza
  5. Hezekia ana mpango wa kuwa mfanyabiashara katika;
    1. gredi ya saba.
    2. maisha yake yaliyopita.
    3. maisha ya sasa
    4. maisha yake yajaayo.

Soma ufahamu unaofuata kisha ujibu maswali.

G5SwaT3OS12023Q3

Kuna aina nyingi za simu. Simu ambayo hutumika sana ni simu ya mkononi. Simu ya mkononi huitwa rununu, rukono, simutamba au selula. Watu wengi sana hutumia simu siku hizi. Hii ni tofauti na kitambo ambapo watu waliotumia simu walikuwa wachache. Kazi kubwa ya simu ya mkononi ni mawasiliano. Mawasiliano ni kupitisha ujumbe kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine. Faida ya mawasiliano ya kuzungumza kwa simu ni kuwa hata watu wasiojua kusoma na kuandika huweza kuwasiliana.

Kunao watu ambao husikiliza redio kupitia simu. Watu hao husikiliza taarifa za habari na mambo mengine kupitia redio iliyo kwenye simu. Simu pia hutumika kupiga hesabu kwa kutumia kikokotoo, kupiga picha na kucheza video. Hakika, simu ina umuhimu mkubwa katika maisha. Hata hivyo, simu pia ina madhara yake. Kutumia simu kila wakati kunaleta shida mbalimbali. Kwa mwanafunzi, kutumia simu kila wakati humpotezea mwanafunzi huyo nafasi ya kufanya mambo muhimu. Mambo muhimu kwa mwanafunzi ni kusoma na kufanya kazi za ziada.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, ni kweli kuwa;
    1. kuna aina za simu zisizojulikana.
    2. watu wote hutumia simu siku hizi. 
    3. watu wachache huwa hawatumii simu. 
    4. kuna aina chache za simu.
  2. Kifungu kinaeleza kuwa kitambo;
    1. hakuna aliyetumia simu.
    2. watu wengi hawakujua simu.
    3. watu wengi hawakuwa na simu.
    4. hakuna aliyejua simu.
  3. Kulingana na aya ya pili, simu huweza kufanya yafuatayo isipokuwa;
    1. kusikiliza taarifa za habari.
    2. kupiga picha.
    3. kupiga hesabu
    4. kufanya mawasiliano
  4. Ufahamu unaeleza kuwa mambo gani ambayo ni muhimu kwa mwanafunzi?
    1. kusoma na kufanya kazi za ziada
    2. kusoma na kucheza na wenzake
    3. chakula bora na kucheza
    4. kucheza na kufanya kazi za ziada
  5. Ufahamu unaeleza kuwa simu;
    1. haina umuhimu wowote. 
    2. ina faida na madhara. 
    3. ina madhara mengi.
    4. haina madhara yoyote.

Chagua jibu linalofaa kati ya majibu uliyopewa ili kujazia nafasi zilizoachwa.

Fisi alipohisi kuwa chakula ___16___ kilikuwa kikiandaliwa mahali, ___17___ na mate ndo ndo ndo! Alianza kutembea
___18___ ili mtu asimsikie. Alielewa kuwa haraka haraka haina baraka. ___19___ karibu na nyumba hiyo, aliingia na kuchukua chakula kilichokuwa ndani ya chungu. Baada ya kumeza, ndipo alipogundua kuwa alikuwa amemeza jiwe. Alichomeka sana tumboni ___20___. Akaelewa kuwa tamaa ina madhara mengi.

   A   B   C   D 
 16.   vitamu   tamu   kitamu   mtamu 
 17.  alitiririkwa  alidondokwa   aliteremkwa   alimwagikwa 
 18.  kwa upole   polepole   haraka   kwa mbio 
 19.  Alipofika  Alivyofika  Aliyefika  Aliofika
 20.  wake  yake   lake   mwake 


Jibu maswali yafuatayo kulingana na maagizo.

  1. Tambua nomino ya pekee kwenye sentensi ifuatayo.
    Amina alicheza kwa furaha baada ya kusoma na kunywa chai.
    1. chai
    2. Amina
    3. furaha
    4. kusoma
  2. 'Cheza' ni kwa chezewa kama vile pika ni kwa;
    1. pikwa
    2. pikia
    3. pikiwa
    4. pikika
  3. Chagua neno litakalokuwa la pili kwenye kamusi.
    1. chupa
    2. chungu
    3. chumba
    4. chuma
      1. iii
      2. iv
      3. i
      4. ii
  4. Orodha gani iliyo na nomino za dhahania pekee?
    1. huzuni, uchoyo, uchafu
    2. maji, maziwa, sukari
    3. amani, upendo, chuki
    4. umati, kicha, thureya
  5. Sentensi gani iliyoakifishwa kwa njia inayofaa?
    1. Miji ninayoijua ni Nairobi na Mombasa.
    2. Tutaenda sokoni siku ya alhamisi.
    3. Nimenunua unga, sukari, na sabuni.
    4. Darasa letu limeoshwa na wanafunzi
  6. Nomino gani isiyopatikana katika ngeli ya LI-YA?
    1. gari 
    2. darasa
    3. giza
    4. jitu
  7. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari. Amerudi kwa sababu alisahau pesa juu ya meza.
    1. kiunganishi, kihisishi
    2. kiunganishi, kihusishi
    3. kivumishi, kihisishi
    4. kivumishi, kihusishi
  8. Chagua wingi wa;
    Mwashi huyu amechukua saa yangu.
    1. Waashi hawa wamechukua saa zangu.
    2. Waashi hawa wamechukua masaa yetu. 
    3. Waashi hawa wamechukua masaa yangu
    4. Waashi hawa wamechukua saa zetu. 
  9. Sentensi gani iliyo katika wakati uliopita hali ya kuendelea?
    1. Musa alienda sokoni.
    2. Sote tunapangusa viatu vyetu.
    3. Yohana angali anakata kucha zake.
    4. Walikuwa wakisugua meno yao.
  10. Tegua kitendawili.
    Nifunue nikufunike.
    1. kofia
    2. mwavuli
    3. nyumba
    4. kifuniko

INSHA

Andika insha ya masimulizi kuhusu mada inayofuata.

AJALI BARABARANI

MARKING SCHEME

  1. C
  2. A
  3. D
  4. B
  5. A
  6. B
  7. C
  8. C
  9. A
  10. D
  11. C
  12. C
  13. D
  14. A
  15. B
  16. C
  17. B
  18. B
  19. A
  20. D
  21. B
  22. C
  23. A
  24. C
  25. A
  26. C
  27. B
  28. D
  29. D
  30. B

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 1 hadi la 5

(Ni asubuhi baada ya gwaride. Kasim anabisha mlango wa ofisi ya Mwalimu Mkuu. Mwalimu anamkaribisha ndani.)

                                         GRADE5KISWAHILISET22023Q1

Kasim                        : (Akiinama kwa heshima.) Shikamoo mwalimu?

Mwalimu mkuu          : Marahaba Kasim. Umeamkaje? Natumai kila kitu ni salama. Si kawaida yako kunitembelea ofisini asubuhi.

Kasim                        : Nimeamka vyema mwalimu. Nashukuru. Hakika niliamka alfajiri. Mzazi wangu aliniamsha ili anikabidhi barua hii.                                                      (Anamkabidhi mwalimu bahasha.)

Mwalimu mkuu          : Aha! Nilijua lazima una sababu ya kuja ofisini mwangu asubuhi. Barua ina ujumbe gani?

Kasim                        : Sina habari. Nimepewa tu. Labda ni mwaliko au jambo fulani. Mwalimu, ulitufunza kuwa si vyema kusoma barua za watu                                          wengine.

Mwalimu mkuu          : (Akimpongeza.) Hongera Kasim. Wewe ni mtoto mwema. Ni vizuri kutosoma barua ambazo si zako.

Kasim                        : (Akinyenyekea.) Shukran mwalimu. Mzazi wangu pia hunihimiza niwe na uaminifu kwa kuwa, heshima si utumwa.

Mwalimu mkuu          : Nashukuru kwa maneno yako. Sasa unaweza kujiunga na wengine darasani. Endelea kutia bidii za mchwa masomoni.                                            Nitakupatia majibu ya barua alasiri.

Kasim                        : Asante mwalimu. Kwaheri. Tutaonana wakati huo wa alasiri.

Mwalimu mkuu          : Kwaheri ya kuonana.

  1. Je, Kasim alienda katika ofisi ya mwalimu wakati gani?
    1. Jioni
    2. Alasiri
    3. Adhuhuri
    4. Asubuhi
  2. Kitendo cha Kasim kutoisoma barua aliyopewa na mama yake kinaonyesha maadili gani?
    1. Utiifu
    2. Uaminifu
    3. Upendo
    4. Ushirikiano
  3. Kasim na Mwalimu Mkuu walikamilisha mazungumzo yao kwa
    1. Kusalimiana
    2. Kuamkuana
    3. Kuagana
    4. Kufarijiana
  4. Nini maana ya neno hunihimiza?
    1. Hunishauri
    2. Hunionya
    3. Huniambia
    4. Hunitia moyo
  5. Ni Methali gani imetumiwa katika mazungumzo haya?
    1. Heshima si utumwa
    2. Bidii za mchwa
    3. Kwaheri ya kuonana
    4. Hongera

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

                                     GRADE5KISWAHILISET22023Q6

Jamii inaweza kukabiliana na tatizo la umaskini ikiwa itajitahidi. Kila raia anafaa kutia bidii katika shughuli anazofanya ili kujipatia riziki. Kazi hizo zinaweza kuwa za kiufundi au za ofisini. Tukumbuke kuwa kazi ni kazi.

Mazingira bora ya kufanyia kazi ni muhimu kwa kila mwananchi. Kuwepo kwa amani na utulivu kutawawezesha raia kubuni nafasi za kazi. Wataweza kujiajiri na kuwaajiri wengine.

Hatua ya kuwaelimisha raia kuhusu kazi za kiufundi ni muhimu kwani itapunguza umaskini. Kazi hizo za kiufundi ni kama vile, usonara, ususi, useremala, na upishi. Wananchi wakipata maarifa haya wataweza kujitegemea na kutegemewa na jamii.

Ni muhimu kutambua kuwa afya bora ina manufaa kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Ukiwa na afya njema utafanya kazi kikamilifu. Hivyo basi umaskini utapunguzwa.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, jamii inaweza kukabiliana na tatizo la umaskini ikiwa _____
    1. itafanya bidii
    2. itakuwa na heshima
    3. itakuwa na utiifu
    4.  itakuwa na uzembe
  2. Kati ya kazi hizi za kiufundi ni gani inahusu utengenezaji wa fanicha
    1. Usonara
    2. Ususi
    3. Useremala.
    4. Upishi
  3. Kulingana na kifungu ni gani kati ya hizi si njia ya kukabiliana na umaskini?
    1. Kujitahidi
    2. Kuondoa amani na utulivu
    3. Mazingira bora ya kufanyia kazi
    4. Kuelimisha raia kuhusu kazi za kiufundi
  4. Ujumbe wa kifungu hiki ni gani?
    1. Kukabiliana na umaskini
    2. Kujitahidi
    3. Afya njema
    4. Kujiajiri na kuajiriwa

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Sungura aliwaalika wanyama wengi kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake. Alimtafuta Kobe ili ampikie. Aliagiza keki kubwa ya karoti. Siku ilipowadia Kobe alirauka kwa Sungura.

"Naomba uwatayarishie wageni wangu nyama, pilau na supu." Alisema Sungura. "Sawa. Je, viungo vyote unavyo?" Aliuliza Kobe. "Ninavyo. Nina mdalasini, iliki, kitunguu maji na kitunguu saumu.' Akajibu Sungura. "Hivyo havitoshi. Bado tutahitaji chumvi, pilipili hoho na nyanya." Alisema Kobe. "Kwa nini viungo hivyo vyote?" Aliuliza Sungura."Nataka kutayarisha supu nzito. Wageni wanywe supu na kula shibe yao." Alisema Kobe. Sungura alimpa Kobe viungo vyote alivyohitaji. Kobe alitayarisha mlo ulionukia. Wanyama walipowasili waliona nyungu kubwa iliyokuwa ikitokota nje ya jiko. Fisi alikuwa miongoni mwa wanyama hawa.

Fisi alinyemelea nyungu wakati wanyama walikuwa wakimwimbia Sungura. " Leo ni siku yangu. Nitakula na kunywa kuliko siku zote." Fisi alijisemea.

Aliepua nyungu na kuanza kunywa supu tamu. Supu yenyewe ilikuwa moto. Hata hivyo, Fisi aliinywa yote huku jasho likimtoka. Hakuwajali wengine. Fisi alipomaliza kunywa supu alijaribu kutembea akashindwa. Alipumua kwa shida. Mara akamwona Kobe akiwa amebeba sinia kubwa la pilau na bakuli la nyama.Fisi alijuta kwanini hangeweza kula chakula hicho.

"Naomba msamaha kwa kunywa supu yote." Fisi alilia. Wanyama walimsamehe na kumpa onyo kali. Fisi aliahidi kuwa hangerudia kosa hilo.

  1. Kwa nini Sungura alimtafuta Kobe?
    1. Awakaribishe wageni
    2. Amwonyeshe kupika
    3. Atafute chakula
    4. Ili afanye shughuli ya upishi
  2. Tabia ya fisi kunywa supu yote bila kuwajali wengine inadhihirisha kuwa fisi ana
    1. ukarimu
    2. ulafi
    3. upendo
    4. njaa
  3. Jina lingine la chakula ni mlo. Je, jina lingine la sherehe ni :
    1. Sikukuu
    2. Karamu
    3. Furaha
    4. Siku ya kuzaliwa

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

                                GRADE5KISWAHILISET22023Q13

Baraka ni mvulana anayependa kula lishe bora. Ana menyu ambayo humhakikishia amepata virutubisho muhimu katika mwili wake. Akimaliza kula huwa anakunywa maji bilauri moja. Anajua umuhimu wa lishe bora ni kumfanya awe na afya bora. Yeye huwa haugui ovyoovyo. Ifuatayo ndiyo ratiba yake.

          Asubuhi        Adhuhuri         Jioni
 Glasi moja ya maziwa  Pilau  Ugali wa wimbi 
 Viazi vikuu  Mchuzi wa kuku   Maharagwe
 Mboga za kiasili  Sukumawiki  Mboga za kiasili
 Tunda  Tunda  Tunda

 

  1. Chakula ambacho Baraka hula siku inapoanza ni gani?
    1. Chamcha
    2.  Virutubisho
    3. Kiamshakinywa
    4. Chajio
  2. Baraka hula _____ katika kila mlo?
    1. Mboga
    2. Matunda
    3. Wali
    4. Ugali
  3. Kwa nini Baraka hula lishe bora?
    1. Ili aepuke magonjwa
    2. Kwa sababu ana ratiba
    3. Ili apewe zawadi
    4. Ili asiwe na afya bora

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Nilienda shambani nikaona__16_ya siafu. Walikuwa wametengeneza mstari __17__. Wakati huo nilikuwa nimebeba redio __18__ mkononi. Niliwaondokea wadudu ___19__ nikaenda kukaa __20___ mchungwa kwenye kivuli kuisikiliza redio

 
 16  halailki  safu   mlolongo   kikosi 
 17  ndefu  refu   kirefu   mrefu 
 18  yangu  wangu   changu   langu 
 19  huyo  hayo   hao   hizo 
 20  ndani ya   chini ya   juu ya   katikati ya

 

Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu sahihi.

  1. Chagua nomino ambayo si dhahania:
    1. Furaha
    2. Uzi
    3. Hekima
    4. Ukarimu
  2. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wingi:
    Unyoya wa kuku yule ni mweupe.
    1. Manyoya ya kuku wale ni meupe
    2. Nyoya za kuku wale ni nyeupe
    3. Unyoya wa kuku wale ni mweupe
    4. Manyoya ya kuku yule ni meupe
  3. Chagua sentensi yenye nomino iliyo katika ngeli ya I-ZI:
    1. Ng'ombe wetu alipelekwa malishoni.
    2. Wimbo ulioimbwa uliwavutia wengi.
    3. Nguo iliyofuliwa ilikauka haraka.
    4. Wino ulimwagika sakafuni jana.
  4. Jaza pengo kwa jibu sahihi. Kusoma _____ kunapendeza.
    1. yake
    2. chake
    3. kwake
    4. lake
  5. Jaza pengo katika sentensi hii.
    Mangi alimwita Otieno naye Otieno akamwita Mangi.
    Hivyo wote _____
    1. waliitika
    2. waliitana
    3. waliitiana
    4. waliitwa
  6. Kinyume cha kitenzi anika ni
    1. osha
    2. fu
    3. vua
    4. anua
  7. Sentensi hii iko katika wakati au hali gani?
    Wanafunzi huenda uwanjani kucheza soka.
    1. Hali timilifu
    2. Hali ya mazoea
    3. Wakati ujao
    4. Wakati uliopita
  8. Kanusha sentensi hii: Yeye ataandika ubaoni.
    1. Wao hawataandika ubaoni
    2. Yeye hakuandika ubaoni
    3. Yeye haandiki ubaoni
    4. Yeye hataandika ubaoni
  9. Kati ya Maneno haya ni lipi litakuwa la mwisho katika kamusi?
    1. Pona
    2. Dawa
    3. Kodi
    4. Tibu
  10. Chagua kiambishi kinachofaa kujaza pengo katika sentensi hii.
    Nyinyi _____ tafanikiwa maishani
    1. wa
    2. m
    3. a
    4. ni

INSHA

Andika insha kuhusu mada ifuatayo:

MWALIMU WANGU WA KISWAHILI

MARKING SCHEME

  1. D
  2. B
  3. C
  4. D
  5. A
  6. A
  7. C
  8. B
  9. A
  10. D
  11. B
  12. B
  13. C
  14. B
  15. A
  16. B
  17. D
  18. A
  19. C
  20. B
  21. B
  22. A
  23. C
  24. C
  25. B
  26. D
  27. B
  28. D
  29. D
  30. B

 

 

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.    

                     GRADE4KISWAHILISET22023Q1

Neema         : Salaam aleikum sahibu yangu.   

Juhudi          : (Kwa furaha) Aleikum salaam msena wangu. Wambaje ?

Neema         : Sina la kuamba.

Juhudi          : Mimi pia sina neno. Ninakuomba twende nyumbani kwetu kwa matembezi..

Neema         : Nashukuru kwa makaribisho. Ningetaka kwanza niwapigie wazazi wangu simu niombe ruhusa. (Anapiga simu)

Juhudi          : (Akimtazama kwa makini) Je, wamekupatia idhini?

Neema         : (Kwa tabasamu) Naam! Lakini baba ameniambia ikifika saa kumi na moja jioni niwe nimerudi nyumbani. 

                       (Wote wanatembea pamoja)

Juhudi          : (Akifungua mlango) Karibu nyumbani kwetu.

Neema         : Starehe! Sebule yenu inavutia sana.

Juhudi          : Namshukuru Mungu kwa kutubariki na fanicha kama vile: Makochi, meza, viti na kabati.

Neema         : Matendegu ya samani zenu ni ya kipekee.

 Juhudi         : Seremala aliyeyatengeneza ni hodari. Pia alitengeneza fremu ya mlango wetu.

Neema         : (Akiangalia huku na kule) Pia ninaona televisheni, mazulia, mapazia na vitu vingine vingi.

 Juhudi         : Kila siku mimi hupendezwa na vitu hivi vyote.

Neema         : Kusema kweli nyumba yenu inapendeza.Pia ninaona balbu zenu na picha zilizo ukutani ni za kupendeza.

 Juhudi         : Ninaomba Mungu awawezeshe kupata vitu kama hivi.

Neema         : Inshallah!
                      (mazungumzo yanakatika wazazi wa Juhudi wanapoingia)

  1. Mazungumzo kati ya Juhudi na Neema yalianza kwa
    1. kuagana
    2. kujuliana hali
    3. kuomba ruhusa
    4. matembezi
  2. Kulingana na mazungumzo haya neno sahibu ni sawa na:
    1. Laazizi
    2. Msena
    3. Ndugu
    4. Jirani
  3. Kulingana na mazungumzo uliyoyasoma ni fanicha gani haipatikani katika sebule ya akina Juhudi?
    1. Makochi
    2. Meza
    3. Rafu
    4. Kabati.
  4. Neema anawaheshimu wazazi wake kwa sababu?
    1. Ana rafiki mzuri.
    2. Alimtembelea Juhudi.
    3. Aliomba ruhusa kabla hajaenda kumtembelea Juhudi.
    4. Anamsalimia rafiki yake kwa heshima.
  5. Ni nini kilichofanya mazungumzo hayo kuisha?
    1. Wakati wa kurudi nyumbani ulipofika.
    2. Wazazi wa Juhudi kufika nyumbani.
    3. Giza kuingia.
    4. Walichoka kuongea.

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
                  GRADE4KISWAHILISET22023Q6

Tedi na Njeru walisomea shule ya Baraka. Waliishi katika kijiji cha Mamboleo. Ilikuwa kawaida yao kukutana mara kwa mara ili kusoma pamoja. Jumamosi iliyopita walikutana nyumbani kwa kina Tedi. Walikuwa wamepewa kazi ya kuchora bendera ya Kenya kwenye chati. Pia walifaa kupaka bendera hiyo rangi zake.

Tedi alikuwa amefundishwa kuhusu bendera ya Kenya na kaka yake. Kaka yake anaitwa Rashid. Tedi alichukua chati nyeupe na penseli za kuchorea. Alimwelekeza Njeru jinsi ya kuchora bendera ya Kenya. Walichora bendera vizuri na kuipaka rangi. Rashid alifika akaiona bendera waliyochora. Alifurahi na kuwapongeza. 'Je, rangi za bendera yetu zinaonyesha nini ?" Njeru alimwuliza Rashid.

Rashid aliwaeleza maana ya kila rangi. Alisema kuwa rangi nyeusi inaonyesha rangi ya ngozi yetu. Nyeupe nayo inaonyesha amani na uaminifu. Tedi na Njeru waliendelea kusikiliza kwa makini. Rashid aliendelea kuwaeleza kuwa rangi nyekundu inasimamia damu iliyomwagika wakati wa vita vya kutafuta uhuru. Nayo rangi ya kijani inaonyesha ardhi. Tedi na Njeru walifurahi. Walimshukuru Rashid kwa kuwaelimisha.

  1. Tedi na Njeru waliishi wapi?
    1. Kijiji cha Mamboleo
    2. Shule ya Baraka
    3. Nyumbani kwao
    4. Shuleni
  2. Tedi anamjali Njeru. Toa sababu.
    1. Alimtembelea
    2. Walisoma pamoja
    3. Alikuwa rafiki yake
    4. Alimsaidia kuchora bendera ya Kenya
  3. Ni watu wangapi waliotajwa katika kifungu hiki?
    1. Wawili
    2. Watatu
    3. Wannne
    4. Mmoja
  4. Kukutana mara kwa mara inamaanisha nini
    1. Kukutana mara nyingi
    2. Kukutana baada ya muda mrefu
    3. Kukutana mara moja
    4. Kukutana bila kutarajia

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Karibu wangu mwandani, twende sote ziarani,
Tutazunguka shambani, kuna matunda mitini,
Nina mimea bondeni, na miche kando mtoni,
Karibu kwangu shambani, twende sote ziarani.

Michungwa ni tele kwangu, tena yote imezaa,
Miembe ninayo kwangu, maembe yaning'inia,
Minanasi mingi kwangu, nanasi zimezagaa,
Karibu kwangu shambani, twende sote ziarani.

Minazi ni ile kule, ina nazi na madafu,
Mipera ni ile pale, inazaa maradufu,
Mianzi nayo ni ile, kimo chake ni kirefu,
Karibu kwangu shambani, twende sote ziarani.

Ziara tumemaliza, miche ninakupa shika,
Naomba kama waweza, panda kwako ukifika,
Maswali nayo uliza, upate kufaidika,
Karibu kwangu shambani, twende sote ziarani.

  1. Msimulizi anamwalika mwandani wake waende wapi?
    1. Safari ya shambani
    2. Sherehe ya shambani
    3. Kazi ya shambani
    4. likizo shambani
  2. Kwa nini miche ilipandwa kando ya mto?
    1. Ili isipate magugu
    2. Ili isiharibiwe na wadudu  
    3. Ili ipate maji
    4. Ili ipate kivuli
  3. Jina lingine la shambani ni gani?
    1. Mtoni
    2. Ziarani
    3. Kondeni
    4. Safarini

Swali la 13 hadi la 15.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Shangazi Naomi hututembelea kwetu kila likizo. Likizo iliyopita, nasi tuliruhusiwa kwenda kumtembelea. Tulimpelekea sukari, unga na matunda. Shangazi alifurahi sana. Mimi na kakangu pia tulifurahi kumwona.

Shangazi alituandalia chakula kilichonukia kama ruhani. Alitukaribisha mezani. Kila mmoja aliketi umbali wa mita moja na nusu kutoka kwa mwenzake.Tulizingatia maagizo ya Wizara ya Afya. Kaka aliombea chakula kisha tukanawa mikono. Kila mmoja alijipakulia chakula kiasi cha kumtosha.

Shangazi alitupongeza kwa kuzingatia adabu mezani. Alitupongeza tulivyokula kwa heshima. Aidha, alisema tumelelewa vizuri. Hakuna aliyebakisha chakula kwenye sahani. Shangazi alitushukuru nasi tukamuahidi kumtembelea tena.

  1. Shangazi Naomi alipelekewa bidhaa zifuatazo isipokuwa
    1. Ugali
    2. Unga
    3. Sukari
    4. Matunda
  2. Katika kifungu hiki ni nini kinachoonyesha kuwa wahusika wanajali afya zao?
    1. Kuombea chakula
    2. Kuketi umbali wa mita moja na nusu kutoka kwa mwingine
    3. Kujipakulia chakula cha kutosha
    4. Kula chakula cha kutosha
  3. Shangazi aliwapongeza wapwa wake kwa sababu ya
    1. Kula chakula na kumaliza
    2. Kulelewa vizuri
    3. Kumtembelea
    4. Kuzingatia adabu mezani

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

            Je, ___16___unajua mavazi mbalimbali? Kuna mavazi ya wanaume na ya___17__. Nguo___18___ jinsia ya kike pekee ni kama vile__19__na shimizi. Mavazi__20___ faida nyingi kwa watu.

   A
 16  sisi  wewe   nyinyi   mimi 
 17  wanawake  wasichana  wavulana  wazee
 18  wa  la   za   ya 
 19  kaptura  mashati   suruali   marinda 
 20  zina  ina   yana   una 

 

Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu sahihi.

  1. Ni neno gani limeambatanishwa vizuri na aina yake?
    1. Mrefu- Nomino
    2. Gilasi -Kitenzi
    3. Kimbia- Kielezi
    4. Vizuri- Kivumishi
  2. Jaza nafasi kwa jibu sahihi. Yai ____ meliwa na mtoto.
    1. li
    2. i
    3. u
    4. a
  3. Andika sentensi hii katika hali ya umoja. Wapishi wamepika vyakula.
    1. Mpishi amepika chakula
    2. Wapishi wamepika vyakula
    3. Wapishi wamepika chakula
    4. Wapishi amepika vyakula
  4. Ni kundi gani lina mpangilio mzuri wa maneno kama yatakavyofuatana katika kamusi?
    1. Kula, pakua, pika, nawa
    2. Salamu, salama, salimu, sala
    3. Kinu, kisu, mwiko, mchi
    4. Zulia,tumbuu, pazia, fremu
  5. Pita aliukata mti huo. Katika kukanusha tunasema, Pita_____
    1. hataukata mti huo
    2. hakuukata mti huo
    3. hajaukata mti huo
    4. hakati mti huo
  6. Jaza nafasi kwa jibu sahihi. Wachezaji watapewa zawadi
    1. sasa
    2. jana
    3. kila siku
    4. kesho
  7. Chagua kiunganishi katika sentensi ifuatayo: Nitaosha matunda ili nimpe mama;
    1. matunda
    2. ili
    3. mama
    4. nitaosha 
  8. Jaza pengo kwa jibu sahihi. Mimi nina mpira wangu. Yeye ana mpira
    1. yake
    2. wake
    3. lake
    4. chake
  9. Kisan ana mazoea ya kufanya mambo upesi. Mara nyingi anakosea. Je, Kisao anaweza kuambiwa methali gani ili awe makini?
    1. Haraka haraka haina baraka.
    2. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
    3. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
    4. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. kipindi cha mwisho.
  10. Chagua jibu sahihi. Wanafunzi walifagia darasa ______ kipoindi cha mwisho. 
    1. kati ya
    2. baada ya
    3. ndani ya
    4. juu ya

INSHA

Andika insha kuhusu mada ifuatayo:

SHULE YETU

 

 

Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswali 1-5.

Zara:   Kakai ulielewa somo la leo la kufunga na kufungua faili?
Kakai: Ndio, sasa ninafanya mazoezi ya kusakura matini kwenye tovuti. Natafuta vifungu vya kusoma vyenye mada ya dira.
Zara:   Kumbuka mwalimu alivyotueleza. Tunapaswa kuzingatia hatua za kiusalama katika matumizi ya vifaa vya kidijitali, pia
            tutambue mitandao salama kwa sababu kuna watu hatari mtandaoni
Kakai: Ni kweli kuna hatari nyingi mtandaoni mtu anaweza kutekwa nyara kwa kutoa maelezo yake mtandaoni.
Zora:   Pia kuna mitandao iliyo na habari zisizo nzuri. Kuna hata watu wanaosambaza video zisizo nzuri : Mimi nitakuwa makini                        ninapokuzwa mtandaoni. Nikuona mtu au jambo ambalo nadhani ni hatari nitamwambia mwalimu
Zora:   Mimi pia nitakuwa mwangalifu sana. Napenda sana kutumia kompyuta. Ninapata maarifa mengi sana mtandaoni
Kakai: Tumalize kazi ili twende nyumbani

  1. Ni kweli kusema kuwa
    1. mtandaoni hamna hatia yoyote
    2. mtu anaweza kutekwa nyara kwa kutumia mitandao
    3. ni watu wazuri tu hutumia mitandao
    4. kompyuta ni mbaya
  2. Neno lenye maana sawa na kompyuta ni
    1. rununu
    2. simu tamba
    3. tarakilishi
    4. faksi
  3. Kakai alikuwa anatafuta nini mtandaoni?
    1. Hatari zilizomo mtandaoni
    2. Jinsi ya kutekwa nyara
    3. Mada kuhusu dira
    4. Video zilizo mtandaoni
  4. Neno kompyuta lina silabi ngapi
    1. tatu
    2. nane
    3. saba
    4. tano
  5. Kichwa mwafaka cha mazungumzo haya ni\
    1. video mtandaoni
    2. umuhimu wa kompyuta
    3. mtandao
    4. hatari za kompyuta

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu swali 6-10.

Siku moja mimi na sahibu yangu Baraka tulikuwa tukipalilia mimea kwenye mradi wetu shuleni. Tulipiga soga huku tukiipinda migongo yetu. Ghafla kama mauti sahibu yangu alipiga mayowe. Alikuwa amejikata muundi kwa jembe baada ya kugonga jiwe. Bila kupoteza wakati nilienda shoti hadi kwenye ofisi ya mwalimu wa zamu na kumuarifu kilichokuwa kimetokea.

Bi. Sara, aliyekuwa mwalimu wa zamu alichukua hatua mara moja. Aliwaita maskauti wapatao wanne tukaandamana nao. Tulipofika alipokuwa ameketi baraka, Bi Sara aliwaelekeza maskauti jinsi ya kumpatia majeruhi huduma ya kwanza. Walichukua kitambaa safi na kufuga jeraha. Damu iliposita kutoka waliosha lile eneo kwa maji safi yaliyotiwa chumvi. Kisha walifunga kidonda bendeji na kumpeleka kwenye zahanati iliyokuwa karibu. Tangu siku hiyo niliamua kujiunga na maskauti.

  1. Maana ya kupiga soga ni
    1. kufanya mazungumzo
    2. kucheza soka
    3. kufanya uzembe
    4. kulima shambani
  2. Ni nini hakuonyeshi kuwa B.Sara anawajibika?
    1. Alikuwa zamu
    2. Alichukua hatua mara moja
    3. Aliwaelekeza maskauti kumpa baraka huduma ya kwanza
    4. Alikuwa ameketi ofisini
  3. Kupiga soga, kupinda migongo, kuenda shoti yote ni mifano ya tamathali gani ya lugha?
    1. Methali
    2. Misemo
    3. Nahau
    4. Tashbihi
  4. Je majeruhi ni nani?
    1. Jeraha
    2. Mitu au watu waliojeruhiwa
    3. Maumivu
    4. Maiti
  5. Kisawe cha neno sahibu ni
    1. ndugu
    2. rafiki
    3. adui
    4. baba mzee

Soma kifungu kifuatacho kwa kujaza nafasi wazi 11-15.

__11__ ya mjomba kuwasili nyumbani tulimkaribisha __12__. Mama alimpa maji baridi ili akate kiu __13__. Aliketi kwenye kochi huku
__14__ na baba. Alikuwa amekawia __15__.

   A   B   C   D 
 11.   Kabla   Kando   Sababu   Baada 
 12.  chumbani   sebuleni   jikoni   hamamuni 
 13.  yake  chake   yao   zake 
 14.  wakipiga kamsa   wakipiga miayo   wakipiga gumzo   wakapiga hoihoi 
 15.  kutembea  kutembezwa   kutembelewa   kututembelea 

 

Kuanzia swali la 16-30. Jibu kulingana na maagizo.

  1. Chagua kundi la nomino pekee
    1. kuimba, hasira, maji
    2. Shuleni, polepole, jana
    3. Safi, yoyote, wale
    4. Ilhali, maandamo, bora
  2. Maneno yapi yaliyo katika ngeli ya U-ZI pekee?
    1. Mkate, ukuta, unga
    2. Uzi, ufagio, wino
    3. Ubinda, wenzo, ulimi
    4. Ukucha, uwanja, ugali
  3. Chagua sentensi sahihi kisarufi 
    1. Kiprop ni mrefu kumliko kirui
    2. Asingeimba vyema asingalituzwa 
    3. Vazi zuri hupendeza
    4. Panya ameingia shimoni pale
  4. Kinyume cha kutabasamu ni
    1. kucheka
    2. kununa
    3. kulia
    4. kukasirika 
  5. Kati ya viungo hivi vya mwili ni kipi si cha  ndani?
    1. Wengu
    2. Utosi
    3. Nyongo
    4. Maju 
  6. Kanusha: Aliamka na kuenda sokoni
    1. Aliamka na kuelekea kwa soko
    2. Hakuamka wala hakuenda sokoni
    3. Haamki kuenda sokoni
    4. Hataamka na kuenda sokoni
  7. Chagua jibu lenye tashbihi
    1. yeye ni wembe masomoni
    2. alikata kiu baada ya mbio zake
    3. wana bidii kama mchwa
    4. mwizi alilewa chakari
  8. Chagua sentensi iliyo katika hali ya ukubwa
    1. Jiko hilo litawashwa baadaye
    2. Kabati lake limefungwa vizuri
    3. Jina lake lina herufi chache
    4. Kono hilo lina nguvu nyingi
  9. Tegua kitendawili
    Huku ng'o huko ng'o
    1. Kaburi
    2. shamba
    3. giza
    4. kamasi
  10. Mchoro huu unaonyesha saa ngapi?
    G6SwaT2OS22023Q25
    1. saa nane kamili
    2. saa mbili kamili
    3. saa sita na dakika kumi
    4. saa sita kamili
  11. Nahau gani yenye maana ya kukamatwa na askari
    1. Shika sikio
    2. Tia mbaroni
    3. Kula kalenda
    4. Mkono mrefu
  12. Bunda ni kwa punda kama vile zaa ni kwa
    1. saa
    2. zao
    3. zana
    4. sana
  13. Maneno yaliyopigiwa kistari ni mfano kwa
    Gari safi lilioshwa vizuri
    1. nomino, kivumishi
    2. kielezi, kivumishi
    3. kivumishi, kitenzi
    4. kivumishi, kielezi
  14. Mavazi rasmi ya wachezaji huitwa
    1. jozi
    2. sare
    3. daluga
    4. fulana
  15. Jibu la makiwa ni
    1. sijambo 
    2. tunayo
    3. pole
    4. nishapoa

INSHA

Andika insha kuhusu

MCHEZO NIUPENDAO

MARKING SCHEME

  1. B
  2. C
  3. C
  4. A
  5. B
  6. A
  7. D
  8. C
  9. B
  10. B
  11. D
  12. B
  13. B
  14. C
  15. D
  16. A
  17. C
  18. C
  19. B
  20. B
  21. B
  22. C
  23. D
  24. C
  25. A
  26. B
  27. A
  28. D
  29. B
  30. B

Kusikiliza na kuzungumza

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.

G6SwaT2OS32023Q1

Juma :         Shikamoo mwalimu?
Bw. Bakari: Marahaba Juma. (Akimwashiria akae) Karibu uketi.
Juma :         (Akiketi) Asante sana mwalimu.
Bw. Bakari: Darasani unaendeleaje na masomo?
Juma :         Mwalimu, ninaendelea vizuri. Ninajikaza kwani mvumilivu hula mbivu.
Bw. Bakari: (Akitikisa kichwa) vizuri sana Juma. Nina furaha sana kusikia kuwa unafanya bidii za mchwa. Je, kuna somo                                          linalokutatiza?
Juma :        Naam mwalimu! Somo la Kiswahili linanipatia changamoto nyingi. Ninajaribu juu chini kujikaza ili nilielewe vizuri.
Bw. Bakari: Bidii ni muhimu sana kama ulivyosema. Vilevile unafaa kufanya mazoezi ya kusikiliza na kuzungumza Kiswahili. Ukifanya                      hivi utazidi kukipenda Kiswahili.
Juma :        (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Siku hizi huwa nasikiliza vipindi vya Kiswahili kwenye redio na kutazama habari katika                       Kiswahili. Baadaye huwaelezea wenzangu niliyosikia.
Bw. Bakari: Vizuri sana. Hiyo ni hatua ya kutia moyo. Zaidi ya hayo hakikisha unauliza maswali darasani mahali ambapo hujaelewa.
Juma :         Huwa naogopa kuchekwa na wenzangu kwani wanakielewa Kiswahili kuniliko mimi.
Bw. Bakari: (Akimkata kauli) Kuogopa? Kumbuka kuuliza si ujinga.
Juma :         (Akiwazia maneno hayo) Nimekuelewa mwalimu. Kutoka leo nitaanza kuuliza maswali.
Bw. Bakari: Vilevile uwe ukisoma vitabu vya Kiswahili ili ukuze ubunifu wako hasa katika kuandika.
Juma :         Nitafanya hivyo kwa sababu nataka kuwa mwandishi bora darasani.
Bw. Bakari: Aidha kumbuka kushirikiana na wenzako masomoni kwani mkono mmoja haulei mwana.
Juma :         Ndio mwalimu. Nitaufuata ushauri huo. Ninaelewa kuwa umoja ni nguvu...
Bw. Bakari:(Akimchachawiza) Nao utengano ni udhaifu. Ninaona sasa umepata mwamko mpya. Hakikisha umefanya yale                                        tuliyozungumzia. Sasa enda darasani ukaendelee na masomo yako.
Juma :        (Akiondoka) Asante mwalimu. Mungu akujalie mema.

  1. Mwanafunzi alimwamkua mwalimu wake Shikamoo kuonyesha maadili gani?
    1. Bidii
    2. Heshima
    3. Huruma
    4. Uoga
  2. Juma anapata changamoto katika somo gani?
    1. Hesabu
    2. Kiswahili
    3. Kiingereza
    4. Sayansi
  3. Ili kukuza stadi ya kusikiliza na kuzungumza Juma anafanya nini?
    1. Kusikiliza na kutazana vipindi kisha kuwaelezea wenzake.
    2. Kusoma vitabu vya Kiswahili.
    3. Kuandika insha nyingi.
    4. Kushirikiana na wenzake.
  4. Je, ungeyasikiliza mazungumzo ya mwalimu na mwanafunzi, ungejifunza nini?
    1. Kuongea na mwalimu humfanya mwanafunzi asifiwe.
    2. Si vizuri kuuliza maswali sana darasani.
    3. Ni vizuri kutafuta ushauri-nasaha kutoka kwa wakubwa wako.
    4. Somo la Kiswahili ni gumu sana.
  5. Methali 'mkono mmoja haulei mwana' inatufunza kuwa na:
    1. Bidii
    2. Ushirikiano
    3. Upole
    4. Utengano

Swali la 6 hadi la 8

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Songambele

G6SwaT2OS32023Q2

Kijiji cha Songambele kina wakazi wengi sana. Wakazi hawa walifurahia utulivu kwa muda mrefu. Hata hivyo, likizo iliyopita wanakijiji walilalamikia mienendo mibaya ya baadhi ya vijana. Kuna vijana ambao walivalia mavazi yasiyofaa. Kuna wale ambao walianza kukataa kwenda shuleni. Wengine hawakutii watu wazima. Walisahau kuwa heshima si utumwa.

Bi.Mwema ni mmoja wa wanakijiji hiki. Alikuwa na shirika lake kwa jina, Boresha Vijana. Kupitia kwa shirika hili, alitumia redio kuwaelimisha vijana kuhusu mienendo mizuri. Aliandaa siku ya michezo kijijini. Vikundi mbalimbali vilishiriki. Baada ya michezo hii, washindi walituzwa. Bi.Mwema alitumia nafasi hii kuwashauri.

Bidii ya Bi.Mwema ilifaulu. Vijana waliokuwa wamepotoka walibadilika. Wanakijiji walifurahi. Walitambua juhudi za Bi.Mwema. Waliandaa sherehe kubwa. Walimtuza Bi.Mwema kwa juhudi zake. Hakika, mcheza kwao hutuzwa.

  1. Wakazi wa kijiji cha Songambele walifurahia _______________________________ kwa muda mrefu.
    1. maandamano
    2. amani
    3. vijana
    4. shida
  2. Kulingana na aya ya kwanza baadhi ya vijana walikosa maadili gani?
    1. Utiifu
    2. Umoja
    3. Bidii
    4. Ukarimu
  3. Maana ya neno andaa kama ilivyotumika katika kifungu hiki ni:
    1. Tayarisha
    2. Safari
    3. Zuru
    4. Maliza

Swali la 9 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

SHULE YA TAMARA, S.L.P 130,
BUSARA.
05-05-2023

Kwa muhibu Pendo,
Pokea salamu nyingi kutoka kwangu. Hujambo? Natumai huna neno. Mimi ni mzima. Ninaendelea vizuri na masomo yangu. Musimu huu wa masika huku kwetu kuna mvua nyingi sana. Wazazi na walimu wanahakikisha kuwa tumejikinga vilivyo na mvua na mbu ambao wameongezeka. Kwa kufanya hivi hatutapata magonjwa kama vile Mafua, Nimonia na Malaria. Nakushauri pia uwe mwangalifu.

Madhumuni ya kukuandikia barua hii ni kukupa mawaidha kuhusu faida za mahusiano mema na wenzako shuleni. Kuanzia ukiwa na uhusiano mzuri na wenzako, utaweza kushirikiana nao. Umoja huu utakufaa masomoni na maishani. Utaweza kujifunza mengi kutoka kwa wenzako. Vilevile ukiwa na matatizo watakusaidia. Kumbuka kuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

Kuongezea mahusiano mema huleta heshima. Wahenga walisema kuwa heshima si utumwa. Ukimheshimu mwenzako atakupenda na kukukubali jinsi ulivyo. Heshima kwa wengine huondoa uadui ambao huleta utengano shuleni. Wanafunzi hushirikiana na kufanya vyema masomoni. Kusema kweli mahusiano mema ni uti wa mgongo wa elimu.

Licha ya hayo amani huletwa na mahusiano mema. Mwanafunzi akitangamana na wengine huweza kuwaelewa nao kumwelewa. Shuleni kuna wanafunzi wenye hali mbalimbali. Utangamano mzuri wa wanafunzi hukuza amani. Amani huwawezesha kusoma vyema bila usumbufu wowote. Huweza kujifunza mengi na kuwa mwerevu zaidi.

Ninatumai nimekuongezea maarifa sahibu yangu. Hakikisha unahusiana vyema na wenzako ili uishi maisha mema. Kwaheri!

Wako wa moyoni,
Amara Mwara

  1. Kifungu ulichokisoma ni cha aina gani?
    1. Masimulizi
    2. Barua ya kirafiki
    3. Barua rasmi
    4. Wasifu
  2. Mwandishi aliandika barua hii katika msimu gani?
    A. Wa jua kali
    B. Wa baridi kali
    C. Wa mvua nyingi
    D. Wa mvua ndogo ndogo.
  3. Mwandishi wa barua hii ni nani?
    1. Tamara
    2. Amara
    3. Mwalimu
    4. Mzazi
  4. Gani si manufaa ya mahusiano mema kulingana na kifungu?
    1. Heshima
    2. Umoja
    3. Amani
    4. Fujo

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G6SwaT2OS32023Q3

Siku moja tulizuru hospitali na kumuuliza daktari kiungo kilicho muhimu kuliko vingine. Daktari alitueleza kuwa mwili wa binadamu una viungo mbalimbali vinavyotekeleza kazi tofautitofauti. Viungo vinavyomeng'enya au kusaga chakula ni tumbo kongosho, uchengelele, utumbo mpana, nyongo, kibofu cha nyongo, kibole na wengu. Ubongo na uti wa mgongo huwezesha mwili kujifahamu. Moyo nao huzungusha damu mwilini. Hatimaye zoloto na pafu hutumika katika mfumo wa hewa. Ni vigumu kusema ni kiungo kipi kilicho muhimu kuliko vingine. Tunafaa kutunza viungo hivi. Tunafaa kufanya kazi kwa kuchangizana kama viungo vya mwili.

  1. Neno tulizuru lina maana sawa na
    1. tuliuliza
    2. tulitoka
    3. tuliona
    4. tulitembea
  2. Kifungu hiki kinazungumzia nini?
    1. Utunzaji wa viungo vya mwili.
    2. Viungo vya ndani vya mwili.
    3. Viungo muhimu kuliko vingine
    4. Viungo vya ndani na vya nje vya mwili
  3. Kulingana na kifungu:
    1. Hakuna kiungo kilicho muhimu kuliko kingine.
    2. Moyo ni muhimu kuliko viungo vingine vyote.
    3. Kuna viungo muhimu kuliko vingine.
    4. Mapafu ni muhimu kuliko moyo.

Swali la 16 hadi la 20

Soma kifungu kifuatacho. Kwa kila swali umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Muhula ___16__ tulifunzwa mambo __17__ katika somo __18__ ninalipenda sana Kiswahili. Tulifundishwa vivumishi vya sifa kama vile  __19__ na viwakilishi vya nafsi kama vile __20__.

   A   B   C   D 
 16.   uliopita   iliyopita   zilizopita   kilichopita 
 17.  kingi  wengi   vingi   mengi 
 18.  ambayo   ambazo   ambalo  ambao
 19.  changu  kubwa  hili  watatu
 20.  mimi  huu  kumi  dogo

 

Swali la 21 hadi la 30

Chagua jibu sahihi.

  1. Hii ni picha ya mchezaji. Anacheza mchezo gani?
    G6SwaT2OS32023Q21
    1. Chesi
    2. Kandanda
    3. Tenisi
    4. Jugwe
  2. Hili ni jedwali la maneno. Chagua jibu linaloonyesha vitenzi?
     A   shamba   Mimi   Wangu 
     B  lakini  Lo!   Polepole 
     C  lala  Soma   palilia
     D  Nyuma ya   Igiza   Pendwa 
  3. Kati ya maneno haya ni gani litakuja mwisho kialfabeti?
    1. Kavu
    2. Kaa
    3. Kaza
    4. Hal
  4. Ni maneno yapi yaliyo katika ngeli moja?
    1. Ukuta, unywele, uzi
    2. Mkeka, sikio, jicho
    3. Nyusi, goti, tumbo 
    4. Pafu, moyo, ini
  5. Chagua jibu ambalo ni wingi wa sentensi:
    Mpera wa mkulima mrefu una ua.
    1. Mpera wa wakulima warefu una maua. 
    2. Mipera ya wakulima warefu ina maua.
    3. Mipera ya mkulima mrefu ina maua. 
    4. Mipera ya wakulima warefu ina nyua.
  6. Chagua maamkuzi au maagano ya wakati wowote
    1. Masalkheri
    2. Sabalkheri
    3. Alamsiki
    4. Salaam aleikum!
  7. Ni maelezo gani yasiyo sahihi kuhusu alama za uakifishi?
    1. Alama ya hisi hutumiwa kuonyesha mshangao.
    2. Alama ya ritifaa hutumiwa katika maneno yenye ving'ong'o
    3. Koloni hutumika kuonyesha hisia mbalimbali.
    4. Alama ya kiulizi hutumika katika sentensi ambayo ni swali.
  8. Chagua sentensi ambayo imetumia kirejeshi 'amba-' vizuri.
    1. Waimbaji ambaye hawakuimba walienda.
    2. Kalamu ambayo imevunjika ni yangu.
    3. Mkeka ambalo umeanguka ni huu.
    4. Meza ambacho imejengwa ni nzuri.
  9. Kamilisha tashbihi hii:
    Mlafi kama ________________________________
    1. Fisi
    2. Chiriku
    3. Kasuku
    4. Nzi
  10. Chagua jibu ambalo ni tofauti na mengine.
    1. Kiangazi
    2. Masika 
    3. Kipupwe 
    4. Mafuriko

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako

Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo:

MECHI YA KUFURAHISHA

MARKING SCHEME

  1. B
  2. B
  3. B
  4. C
  5. B
  6. B
  7. A
  8. A
  9. B
  10. C
  11. B
  12. D
  13. D
  14. B
  15. A
  16. A
  17. D
  18. C
  19. B
  20. A
  21. B
  22. C
  23. C
  24. A
  25. B
  26. D
  27. C
  28. B
  29. A
  30. D

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G5SwaMT2S32023Q1

Wanyama wa porini ni rasilimali tuliyopewa na Mwenyezi Mungu. Wanyama hao wana umuhimu mkubwa katika taifa lolote. Umewahi kuwaona nyumbu wakivuka kutoka Kenya na kuingia Tanzania au kutoka Tanzania kuingia Kenya? Hali hiyo hutoa utulivu mkubwa katika moyo. Kuwaona simba wakiwawinda na kuwala wanyama wengine husababisha furaha kubwa. Hili lina maana kuwa kule kuwatazama wanyama wa porini huleta utulivu. Faida nyingine ya wanyamapori ni kule kuwavutia watalii. Watalii wanaotoka nchini na katika mataifa ya nje humiminika nchini ili kujionea wanyama hao.

Manufaa makubwa ambayo sisi hupata kutokana na watalii ni pesa za kigeni. Watalii wanapotuletea pesa za kigeni, serikali yetu huweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Ni kutokana na pesa hizo ndipo tunapoweza kujenga barabara, shule, hospitali na kadhalika. Wakenya wengi wameajiriwa kufanya kazi zinazohusiana na wanyamapori. Hao ni kama vile madereva, walinzi, wanaowatembeza watalii na wanaofanya kazi katika hoteli za watalii hao.Wafanyakazi hao hufanya kazi kwa bidii ili kufaulu katika maisha yao.Wafanyakazi hao hupata pesa za kusaidia familia zao ili waishi maisha mazuri. Tatizo hutokea wakati tamaa inapofanya tuwinde na kuwaua wanyama hao. Majangili huwawinda wanyamapori wakiwa na lengo la kupata vipusa, pembe za ndovu na ngozi za wanyama hao. Uovu huo unafaa kukomeshwa haraka mno. Ni vyema kuelewa kuwa kuwaangamiza wanyamapori ni kuiletea nchi yetu hasara. Kila mkenya ajitolee kuwatunza wanyamapori.

  1. Pesa za kigeni ambazo huletwa na watalii hutumiwa na;
    1. watalii
    2. shule
    3. wakenya
    4. serikali
  2. Ni kweli kwamba tusipokuwa na wanyamapori;
    1. watalii wataongezeka nchini.
    2. majangili watatajirika.
    3. kiwango cha maendeleo kitarudi chini.
    4. watu wengi wataajiriwa.
  3. Ufuatao ni umuhimu wa wanyamapori isipokuwa;
    1. hutuliza moyo
    2. huwaletea majangili faida
    3. huvutia watalii
    4. huwapa watu ajira
  4. Kifungu kinaeleza kuwa wanaowinda wanyamapori huongozwa na nini?
    1. umaskini
    2. njaa
    3. tamaa
    4. kutojua
  5. Wafanyakazi hao hufanya kazi kwa bidii ili kufaulu katika maisha yao. Maneno haya yanaweza kuelezwa kwa methali gani?
    1. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.
    2. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
    3. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
    4. Mtaka yote hukosa yote.
  6. Tambua maana ya 'majangili' kulingana na kifungu.
    1. Wezi wa wanyamapori
    2. Wawindaji haramu
    3. Askari wa wanyamapori
    4. Watalii katika mbuga
  7. Chagua kichwa kinachofaa kwa makala haya.
    1. umuhimu wa watalii
    2. faida na hasara za wanyamapori
    3. umuhimu wa wanyamapori
    4. kuwinda, wanyamapori

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G5SwaMT2S32023Q2

Kutoka kwa: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Kwenda kwa: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


MADA: MWALIKO WA KUPATA MAFUNZO

Kwa Bwana/Bi,

Jina langu ni Mapato Mapesa. Mimi ndimi katibu wa chama cha Akiba Haiozi. Chama cha Akiba Haiozi ni chama cha wafanyabiashara wa biashara ndogondogo katika mji wa Mumias. Sisi hujihusisha na biashara za rejareja, uchuuzi na shughuli za juakali. Tumekuwa tukiweka akiba kidogo katika benki yenu ya Wekeza. Kwa sasa, tuna akiba ya kima cha shilingi milioni moja. Tuna hamu ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujipa faida zaidi. Hata hivyo, hatuna ujuzi wa kutosha kuhusu uwekezaji. Kwa kuwa kuuliza si ujinga, tumeamua kutoa ombi ili mtutumie afisa au maafisa ambao watatueleza mengi kuhusu uwekezaji. Vilevile, tugependa kujua iwapo tunaweza tukapewa mkopo. Tatizo jingine ni kwamba hatujui aina za mikopo mnayotoa na riba inayohusiana na kila aina ya mkopo.

Tuna matumaini makubwa kuwa mtalikubali ombi letu na kukifaa chama hiki. Tunatoa ahadi ya kuendelea kushirikiana na benki yenu pamoja na maafisa wenu. Isitoshe, tutazidi kuweka akiba katika banki iyo hiyo nyakati zote. Iwapo ombi letu litakubalika, tafadhali tupeni ujumbe na wakati mnaopatikana ili tujiendae. Tunawapa shukrani za awali kutoka katika vilindi vya mioyo yetu. Kwaherini.

Wenu mwaminifu,
G5SwaMT2S32023Q3
Mapato Mapesa (katibu)

  1. Kifungu hiki ni mfano wa;
    1. barua ya kirafiki.
    2. barua rasmi.
    3. baruapepe.
    4. barua ya kiofisi.
  2. Ni kweli kuwa anayeandikiwa barua hii ni wa jinsia gani?
    1. ya kike
    2. ya kiume
    3. haijulinani
    4. katibu
  3. kulingana na kifungu, kwa nini mwandishi na wenzake wana hamu ya kuwekeza katika miradi mbalimbali?
    1. ili wajue mengi kuhusu uwekezaji
    2. ili wapate faida
    3. ili watembelewe na maafisa wa benki
    4. ili waweke akiba
  4. Wanachama wa chama cha Akiba Haiozi wanafahamu kuwa;
    1. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. 
    2. Majuto ni mjukuu huja baadaye.
    3. Ngoja ngoja huumiza matumbo. 
    4. Haba na haba hujaza kibaba.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Familia kuteseka, sababu umasikini,
Chakula wanaposaka, ni ukweli hawaoni,
Mavazi yameraruka, kichwa hadi mguuni,
Bidii yahitajika, kuushinda uchochole.

Kuanza kule shuleni, kujikaza ni lazima,
Shambani pia kazini, tukilala tutazama,
Bidii iwe moyoni, kujitolea daima,
Bidii yahitajika, kuushinda uchochole.

  1. Chagua kina cha kati cha ubeti wa kwanza.
    1. na
    2. ma
    3. ni
    4. ka
  2. Mwandishi wa shairi hili angetumia neno gani jingine badala ya neno 'familia'?
    1. ayali
    2. jamii
    3. ndugu
    4. sahibu
  3. Umaskini husababisha nini kutokana na ubeti wa kwanza?
    1. ukosefu wa mavazi na chakula
    2. ukosefu wa elimu na amani
    3. ukosefu wa chakula na elimu
    4. ukosefu wa mavazi na amani
  4. Kibwagizo cha shairi hili kina mizani mingapi?
    1. 10
    2. 2
    3. 14
    4. 16

Chagua jibu lifaalo ili kujazia nafasi zilizoachwa.

Mtu __16__ anayetaka kufaulu __17__ lazima awe mwenye bidii. Bidii ni muhimu sana kwetu. Tunafaa kuwa wenye bidii masomoni, kazini __18__ michezoni. Mtu asiyependa bidii hawezi akafaulu katika __19__ lolote. Je __20__ wewe ni mwenye bidii au unapenda uzembe?

   A   B   C   D 
 16.   yoyote   yeyote   wowote   ambaye 
 17.  kwenye maisha   kwa maisha   katika maisha   katika maishani 
 18.  lakini  au  wala   na 
 19.  kitu  shughuli   mambo   jambo 
 20.  ,  ?  !  :

 

  1. Tambua aina za nomino zilizopigiwa mistari. Mtoto alijawa na furaha alipokunywa maziwa.
    1. pekee, wingi, dhahania
    2. kawaida, wingi, shahania
    3. pekee, dhahania, wingi
    4. kawaida, dhahania, wingi
  2. Chagua neno lenye silabi nne kati ya maneno yafuatayo.
    1. beba
    2. wekea
    3. tembelea
    4. hajaja
  3. Tambua sentensi iliyotumia koma.
    1. Amemaliza chakula.
    2. Wewe ni nani?
    3. Amenunua kitabu, kalamu na kichongeo.
    4. Ala! Wacha kuharibu mazingira.
  4. Ikiwa jana ilikuwa Jumatatu, keshokutwa itakuwa lini?
    1. Alhamisi
    2. Jumatano
    3. Jumanne
    4. Ijumaa
  5. Chagua wingi wa;
    Ubao wenyewe una ufa mkubwa.
    1. Mbao zenyewe zina maufa makubwa.
    2. Mabao yenyewe yana nyufa kubwa. 
    3. Mabao yenyewe yana maufa makubwa.
    4. Mbao zenyewe zina nyufa kubwa. 
  6. Tegua kitendawili.
    Dhahabu yangu ya thamani haisimami.
    1. shamba
    2. mkufu
    3. siafu
    4. maji
  7. Nomino gani isiyopatikana katika ngeli ya I-ZI?
    1. kabati
    2. kalamu
    3. karatasi
    4. kamba
  8. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari. Lo! Kumbe wote wamelala ndani ya chandarua.
    1. kiwakilishi, kihusishi
    2. kihisishi, kivumishi
    3. kihusishi, kihisishi
    4. kihisishi, kihusishi
  9. Bwana harusi alivaa ______________________________ shingoni.
    1. koja la maua
    2. shada la maua
    3. mkungu wa maua
    4. kishazi cha maua
  10. Chagua kitenzi kilichonyambuliwa katika kauli ya kutendeka.
    1. pika 
    2. weka
    3. fulika
    4. cheka

INSHA

Andika insha ya masimulizi kuhusu;

SAFARI YA KUFURAHISHA  

MARKING SCHEME

  1. D
  2. C
  3. B
  4. C
  5. B
  6. B
  7. C
  8. C
  9. C
  10. B
  11. D
  12. D
  13. A
  14. A
  15. D
  16. B
  17. C
  18. D
  19. D
  20. A
  21. D
  22. C
  23. C
  24. A
  25. D
  26. B
  27. A
  28. D
  29. A
  30. C

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 1-5.

G5SwaMT2S22023Q1
Sisi watoto wa nchi hii hatuna ubaguzi. Tunapendana. Tunasoma pamoja, tunacheza pamoja, tunaishi pamoja na tunakaa pamoja. Hatuna ubaguzi wa ukabila, dini, rangi wala cheo. Kwetu, kila mtu ni sawa, wasichana kwa wavulana,wake kwa waume na wazee kwa vijana. Tunaamini kwamba tukiishi pamoja kwa kupendana tutakuwa na amani, upendo na ushirikiano katika nchi yetu. Tukumbuke kwamba
nchi yetu ni moja. Na ndipo mahali petu pa kuishi hadi mwisho wa maisha yetu. Hivyo ni lazima sisi pia tuwe na umoja na ushirikiano.

Tunawaomba viongozi, wazazi, walimu wetu na kila mtu kwa jumla, huu ni wakati wa kuwajulisha vijana wote na watoto wa nchi hii kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Tuache ukabila ili tujiite kuwa sisi ni watu wa kabila moja linaloitwa 'Wakenya'.Tuanze leo hii kutumia lugha yetu moja ya taifa, ambayo ni Kiswahili. Wanaotubagua na kututenganisha, tuwakatae katakata na tuwaambie "Ng'o!"

  1. Sauti ya watoto wa nchi hii
    1. haina ubaguzi
    2. imejaa ukabila
    3. haitaki ukabila
    4. ina chuki.
  2. Vijana ni watu gani?
    1. Wavulana
    2. Wanaume wadogo
    3. Watoto kwa kiume
    4. Wasichana kwa wavulana.
  3. Tunahitaji umoja kwa sababu nchi yetu ni
    1. kubwa
    2. nzuri
    3. moja
    4. changa.
  4. Sisi sote wananchi tunafanana yaani tu
    1. pamoja
    2. umoja
    3. wamoja.
    4. kumoja
  5. Wanaotubagua tuwaambie ng'o kisha tuanze kutumia lugha ya
    1. kimombo
    2. mama
    3. Kiswahili
    4. ung'eng'e.

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 6 - 10.

Siku moja nilikuwa nimebaki nyumbani peke yangu. Wazazi wangu walikuwa wameenda kwenye matanga ya mjomba wangu. Nilikuwa mtoto wao wa kipekee. Wazazi wangu walinikanya na kunionya kuwa nisimkaribishe mtu yeyote nyumbani ikiwa wao hawakuwepo. Hakika sikutarajia kumruhusu mtu au kumkaribisha mtu yeyote aje akae nami kwetu. Lakini ilipofika jioni, akaja rafiki yangu wa chanda na pete Kichwachuma alijidai kuja kunisalimia. Nilishangaa kuhusu hizo salamu zake za jioni. Alipoketi tu hata kabla hatujaanza kuulizana za hujambo- sijambo, mvua ilianza kunyesha huku ngurumo kama za simba zikiandamana na radi. Hakika niliduwaa kushuhudia mvua ya miujiza isiyokuwa na dalili yoyote ya mawingu.

Sikuwa na jingine la kufanya. Nilimruhusu Kichwachuma kulala kwetu. Ajabu ni kwamba, kesho yake sikuamka mapema nilivyozoea. Nililala hadi saa tano asubuhi. Nilipoamka nilijikuta nimelala sakafuni.

Sikumpata rafiki yangu. Pia kila kitu nyumbani kwetu kilikuwa kimechukuliwa hadi kitanda tulichokuwa tumekilalia. Kila kitu! Vitu vyote havikuwepo. Nilibaki mimi tu nikishangaa jinsi ya kuwaambia wazazi wangu.

  1. Mwadishi anasema kuwa alibaki nyumbani peke yake. Hivyo alikuwa
    1. peke
    2. upweke
    3. pweke
    4. pekee 
  2. Aliyekuwa ameaga dunia ni
    1. dada wa mama
    2. kaka wa baba
    3. kaka wa mama
    4. dada wa baba.
  3. Wazazi wake walitoa onyo kwamba
    1. asikaribishe watu nyumbani milele
    2. amkaribishe mtu yeyote nyumbani
    3. mtu akaribishwe bila wao kuwapo
    4. asimkaribishe yeyote nyumbani wasipokuwepo.
  4. Mvua ilikuwa ya miujiza kwa sababu
    1.  ilikuwa na radi
    2. ilileta wezi
    3. haikuonyesha dalili kabla ya kunyesha
    4. ilikuwa na ngurumo za simba.
  5. Alipoamka aligundua kuwa vitu vyote nyumbani vilikuwa
    1. vimeuzwa
    2. vimeibiwa
    3. vimepotea
    4. vimetoroka

Soma kisa kifuatacho kisha ujibu swali la 11 - 15.

Siku hiyo ya Alhamisi, Kalume alikataa katakata kwenda shuleni. Siku hiyo ilikuwa ya kufanya mtihani wa Kiswahili. Alikataa kwenda shule kwa sababu mama yake alikataa kumnunuli vibanzi vya kula wakati wa mtihani. Mama alimwacha nyumbani asubuhi na mapema baada ya kumwamsha. Akamwambia kuwa akimaliza kufungua kinywa aende upesi shuleni asichelewe. Naye akaenda zake kazini.

Kalume alijua kimoyomoyo kuwa hangeenda shuleni. Alitaka vibanzi kwanza. Aliona kuwa vibanzi vilikuwa vitamu kuliko masomo au hata mtihani wa Kiswahili. Mama yake aliporudi saa saba adhuhuri alimkuta akiwa amejikunja akilia. Alipoulizwa alichokuwa akililia alisema: "Umekataa kuninunulia vibanzi"

Kesho yake mama alimpeleka shuleni. Akawaeleza walimu sababu za kukosa shule. Walimu walishangaa. Wanafunzi waliposikia habari hizo walimcheka Kalume sana, wakamwita Bwana Vibanzi. Wengine wakambatiza Kalume banzi! Hadi wa leo wanamwita hivyo. Je, wewe ni Kalume nani? Au Kalume nini?

  1. Kalume alikataa kwenda shuleni siku ya
    1. Alhamisi
    2. Jumatano
    3. Ijumaa
    4. Jumanne.
  2. Ni kwa nini Kalume alikataa kwenda shuleni?
    1. Alichukia shule.
    2. Alikuwa na njaa.
    3. Aliogopa mtihani.
    4. Alitaka vibanzi.
  3. Kufungua kinywa ni
    1. kulia
    2. kupanua mdomo.
    3. kusugua meno
    4. kula asubuhi.
  4. Neno jingine lenye maana sawa na vibanzi ni
    1. mahamri
    2. viazi
    3. chipsi
    4. viazi karai,
  5. Mama alipotoka nyumbani asubuhi alijua kuwa Kalume
    1. haendi shule
    2. atachelewa shule
    3. alikataa chipsi
    4. angeenda shule

Jaza mapengo kwa jibu mwafaka.

Kitabu __16__ kilianguka chini __17__ vipandevipande. Kipande __18__ kikachukuliwa na upepo lakini kipande __19__ kiliingia ndani __20__ maji.

   A   B   C   D 
 16.    yangu   changu    zangu   langu 
 17.  ikararuka   akararuka   kikararuka   kikararua 
 18.  kimoja  moja   mmoja   kamoja 
 19.  ingine  mwingine   nyingine   kingine 
 20.  ya  cha  mwa  wa


Kutoka swali la 21 hadi 30 jibu kulingana na maagizo.

  1. Ipi si jozi ya vitate vyenye sauti zinazokaribiana kimatamshi?
    1. Sima- Zima
    2. Fuka- Vuka
    3. Fora-Fola
    4. Cheka-Choka.
  2. Mwalimu akitusalimu masalkheri. Salamu hii inatumika wakati gani?
    1. Mchana
    2. Jioni
    3. Asubuhi
    4. Usiku
  3. Neno la mwisho kupatikana kwenye kamusi kati ya haya ni
    1. mbio
    2. mbuzi
    3. mbili
    4. mbuni. 
  4. Ni aina ipi ya nomino iliyo katika sentensi ifuatayo?
    Maji mengi yamemwagika chini.
    1. Idadi
    2. Mahali
    3. Wingi
    4. Pekee
  5. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo.
    Kula kwake huko kunaudhi. 
    1. Kula kwao huko kunaudhi.
    2. Kula kwake huko kunaudhi.
    3. Kukula kwake huko kunaudhi.
    4. Vyakula vyake hivyo vinaudhi.
  6. Tegua kitendawili kifuatacho.
    Ananitazama, hasemi, hasikii
    1. Kivuli
    2. Kioo
    3. Picha
    4. Mtoto
  7. Kamilisha. ___________________________ ya ndizi.
    1. Mkungu
    2. Tita
    3. Bunda
    4. Chane
  8. Chagua nomino zinazoweza kuunda nomino ambata sahihi.
    1. Mwana + maji
    2. mwana + muke.
    3. mwana + mbe.
    4. mwana + inchi
  9. Neno lipi lisilo la heshima kati ya haya?
    1. Endesha
    2. Choo
    3. Kinyesi
    4. Mjamzito
  10. Chagua sentensi sahihi kisarufi.
    1. Mbuzi zimeshiba.
    2. Ndege limeanguka chini.
    3. Daktari wamegoma.
    4. Choo kinaoshwa.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha ya kusisimua kuhusu;

JINSI YA KUKABILIANA NA UMASKINI

MARKING SCHEME

  1. A
  2. D
  3. B
  4. D
  5. C
  6. B
  7. C
  8. D
  9. C
  10. B
  11. A
  12. D
  13. D
  14. C
  15. D
  16. B
  17. C
  18. A
  19. D
  20. A
  21. D
  22. B
  23. B
  24. C
  25. A
  26. C
  27. D
  28. A
  29. B
  30. D

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali

G5SwaT2OS22023Q1
(Nyanya ameketi chini ya mti akifuma sweta. Anaiweka sweta kando anapomwona Wakesho)
Wakesho :  (akimkaribia nyanya) Shikamoo nyanya?
Nyanya :     (kwa tabasamu) Marahaba mjukuu wangu! Habari za shule?
Wakesho :  Njema nyanya! (kimya) Nyanya, nikwambie kitu?
Nyanya :     Naam, niambie mjukuu wangu.
Wakesho :  Wenzangu walinichagua kuwa kiranja wa darasa.
Nyanya :     Hongera! Jambo zuri sana.
Wakesho :  (akijikuna kichwa). Lakini Nyanya, sijui ninastahili kufanya nini ili niwe kiongozi bora.
Nyanya :     Aha! Wakesho, sikiliza. Ili kuwa kiongozi bora unastahili kuwa na maadili.
Wakesho :  Ooh! Maadili
Nyanya :     Naam mjukuu wangu. Unaweza kuonyesha maadili kwa namna mbalimbali. Kwanza usiwe na ubaguzi unapowahudumia wenzako.
Wakesho :  Kweli Nyanya, ninafikiria pia ninastahili kuwa na upendo.
Nyanya :     Ndiyo Wakesho. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwajali na kuwasaidia wenzako wanapokuwa na shida.
Wakesho :  Kweli Nyanya! Ninaona kwamba ushirikiano ni jambo muhimu.
Nyanya :     Haswa! Kidole kimoja hakivunji chawa. Je, unaweza kushirikiana na wengine kwa njia gani?
Wakesho :  (Kwa ujasiri) Kwa kuwahusisha katika mambo mbalimbali.
Nyanya :     Vyema! Unastahili pia kuwa na uaminifu. Tunaonyesha uaminifu kwa kusema ukweli na kufanya mambo inavyostahili.
Wakesho:   Asante Nyanya! Hakika umenifunza mengi.

  1. Wakesho alipoulizwa na Nyanya kuhusu habari za shule alimjibu vipi?
    1. Naam
    2. Njema
    3. Shikamoo
    4. Marahaba
  2. Ni neno gani ambalo nyanya alitumia kumpongeza Wakesho kwa kuchaguliwa kuwa kiranja?
    1. Hongera!
    2. Naam
    3. Ndiyo
    4. Haswa!
  3. Kulingana na kifungu, kiongozi mwema hafai kuwa na ____________________________
    1. ushirikiano
    2. heshima
    3. upendo
    4. ubaguzi
  4. Baada ya mazungumzo haya Wakesho anafaa kufanya nini?
    1. Kufurahia kuwa kiongozi shuleni.
    2. Kufuata mawaidha ya nyanya
    3. Kueleza wenzake kuhusu nyanya yake
    4. Kuwashukuru wenzake
  5. Maadili ni nini?
    1. Ushauri
    2. Kuwajali wengine
    3. Uongozi mzuri
    4. Mwenendo mzuri

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SwaT2OS22023Q3

Simba mwenye njaa, katika pitapita zake za kuwinda, alimkuta Sungura akiwa amelala fofofo. Alishusha pumzi, akatabasamu na kumshukuru sana Mungu kwa ukarimu wake wa kumpatia chakula bila kukifanyia kazi.

Taratibu alimsogelea Sungura ili asije akamwamsha, akalala yeye... Alipoinua miguu yake kutaka kumkamata, mara akatokea swara mnono ambaye alipita akikimbia karibu naye, akielekea upande wa kaskazini kwenye nyasi fupi.

Simba alimwacha Sungura na kumkimbiza yule Swara.Kelele za Simba akimkimbiza swara zilimgutusha na kumwamsha Sungura ambaye aliamka na kutimua mbio kuelekea upande wa kusini.

Baada ya kumkimbiza swara kwa muda mrefu Simba alishindwa na kuamua kurudi ili akamle yule Sungura.

Alipogundua kuwa Sungura naye alikuwa ameamka na kukimbia, Simba alisema kwa kujilaumu, "Ama kweli nimepata nilichostahili; kwa kuwa nilikiacha chakula nilichokitia mkononi tayari kwa tamaa ya kutaka kupata zaidi."

  1. Ni wanyama wangapi waliotajwa katika kifungu hiki?
    1. Watatu
    2. Wawili
    3. Wanne
    4. Mmoja
  2. Kati ya wanyama walio kwenye kifungu ni yupi hali nyasi?
    1. Swara
    2. Sungura
    3. Simba
    4. Wote
  3. Hadithi hii inatufunza nini?
    1. Tuwe na ukarimu
    2. Tusiwe na tamaa
    3. Tukifanya makosa tujilaumu
    4. Tuwe watu wenye shukrani
  4. Kinyume cha kitenzi tabasamu ni nini?
    1. Cheka
    2. Lia
    3. Nuna
    4. Waza

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Wanafunzi wa gredi ya tano katika Shule ya msingi ya Faulu walipewa mradi wa kutafuta aina mbalimbali za mapambo kwenye mtandao.Wanafunzi waligawanywa katika vikundi vinne kama ifuatavyo: Starehe, Amani, Upendo, Nuru. Kila kikundi kilitafuta mapambo yake. Tazama jedwali hili kisha ujibu maswali

 VIKUNDI   Mapambo   Mapambo   mapambo 
 Starehe  Herini   Pete   Mkufu 
 Amani  Mkufu   Bangili   Herini 
 Upendo  Pete   Mkufu   Bangili 
 Nuru  Bangili   Herini  Pete

 

  1. Ni kikundi kipi hakikupata mapambo ya masikioni?
    1. Starehe
    2. Upendo
    3. Amani
    4. Nuru
  2. Ni kikundi kipi hakikupata bangili?
    1. Nuru
    2. Amani
    3. Upendo
    4. Starehe
  3. Ni kikundi kipi hakikupata pambo la shingoni? 
    1. Starehe
    2. Upendo
    3. Nuru
    4. Amani

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G5SwaT2OS22023Q2

Huduma ya kwanza ni muhimu sana katika maisha yetu. Mtu hupewa huduma ya kwanza anapopata ajali au anapokuwa mgonjwa. Huduma ya kwanza humsaidia mwathiriwa aweze kufika kwa daktari ili kupata matibabu. Mtu akikosa kupewa huduma ya kwanza anaweza akaaga dunia.

Shuleni kuna ajali mbalimbali ambazo hutokea. Ajali hizi ni kama vile: Kuzirai, kuteguka mguu, kuvunjika viungo vya mwili, kuchomeka, muhina (kutokwa na damu puani) kukatwa na kifaa chenye makali na kuumwa na mdudu.

Mtu akizirai kagua kama ameumia kwanza. Kisha mbebe hadi mahali penye hewa safi kama vile kivulini, mlaze chali na uinue miguu yake juu kidogo. Legeza mavazi yaliyombana kwa kufungua mshipi wake, ukosi au mavazi mengine yaliyombana ili apate hewa safi.

Mtu akitokwa na damu puani, mketishe wima huku akiinama upande wa mbele, finya taratibu sehemu iliyo laini ya pua na umwagize apumue kupitia mdomoni kisha uendelee kufinya taratibu kwa muda wa dakika kumi hadi kumi na tano. Mpatie hanchifu ashikilie upande wa pua.

Njia hizi na nyingine ni muhimu kuzijua ili kuweza kuokoa maisha.

  1. Umuhimu wa huduma ya kwanza ni gani?
    1. Kumwezesha aliyeumia kufika kwa daktari.
    2. Kumsaidia mwathiriwa apone.
    3. Kuleta pesa kwa anayefanya huduma ya kwanza.
    4. Kumsaidia mwathiriwa kuaga dunia.
  2. Ni nini maana ya msemo kuaga dunia?
    1. Kuhamia nchi nyingine
    2. Kupona
    3. Kufa
    4. Kupata nafuu.
  3. Ni njia ngapi za kufanya huduma ya kwanza zilizoelezewa?
    1. Moja
    2. Tatu
    3. Nne
    4. Mbili

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Katika gredi ya tano tumefunzwa mambo __16__. Katika matamshi bora mtu anafaa kusema__17__anapomaanisha kuosha nguo. Vilevile sasa najua kuwa kwaheri ni aina ya __18__. Isitoshe ninaweza kutega na __19__ vitendawili. Zaidi ya hayo ninafahamu kuwa kikosi cha askari ni nomino ya __20__.

   A   B   C   D 
 16.   mengi   mingi   vingi   wengi 
 17.  fua  mvua   vua   vuka 
 18.  salamu   methali   tashbihi   maangano 
 19.  kutegua   kujibu   kufumbua   kutegewa 
 20.  wingi  makundi   kitenzi-jina   dhahania 


Swali la 21-30
SARUFI
Kutoka swali la 21 hadi 30, chagua jibu sahihi.

  1. Ni picha gani haijaambatanishwa sawasawa na nomino yake ya makundi?
    G5SwaT2OS22023Q21
  2. Watoto wenye nidhamu, huheshimu walimu ____________________A
    1. wao
    2. yao
    3. zao
    4. vyao
  3. Anwanipepe hutumika katika uandishi wa
    1. Barua rasmi
    2. Barua ya kirafiki
    3. Baruapepe
    4. Barua ya kiofisi
  4. Chagua wingi wa: Nyumba yangu inapendeza
    1. Nyumba yetu inapendeza.
    2. Majumba yetu yanapendeza.
    3. Vijumba vyetu vinapendeza.
    4. Nyumba zetu zinapendeza
  5. Zawadi alimsaidia Nuru kuchora picha. Kwa hivyo Zawadi
    1. alimchoresha Nuru picha.
    2. alimchorea Nuru picha.
    3. alichoreshwa picha na Nuru. 
    4. alichoreshea Nuru picha.
  6. Ni sentensi ipi sahihi?
    1. Chakula hizi imeiva.
    2. Mti huu umekatwa.
    3. Giza hili linatisha.
    4. Gazeti hii imesomwa.
  7. Ni sentensi ipi iliyoakifishwa vyema? 
    1. Nimefurahi sana!
    2. Ninajua kutumia dira?
    3. Tulicheza soka, chesi na jugwe. 
    4. Ngombe ni mnyama mzuri.
  8. Chagua ukubwa wa nomino mto:
    1. Kito
    2. Kijito
    3. Jito
    4. Mito
  9. Chagua jibu lisilo sahihi.
    1. Fupi kama nyundo
    2. Miguu mirefu kama korongo
    3. Mrefu kama mlingoti 
    4. Shingo ndefu kama mbilikimo
  10. Kamilisha Methali hii: Mtoto umleavyo ____________________________________
    1. huvunjika guu
    2. hutazama kisogo cha nina
    3. hufunzwa na ulimwengu
    4. ndivyo akuavyo

KISWAHILI: INSHA

Andika insha kuhusu mada ifuatayo:

SIKU NILIYOFURAHIA SANA  

Page 1 of 3