Wednesday, 04 May 2022 07:30

Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End of Term 1 SET 2 2022

Share via Whatsapp

MASWALI
SEHEMU A: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu amuulize mwanafunzi maswali yafuatavo.

  1. Wewe na wenzako mna zamu yakulisha mifugo wa nyumbani?
    (Mwanafunzi ajibu)
  2. Taja wanyama wawili wa nyumbani mtakaolisha.
    (Mwanafunzi ajibu)
  3. Taja viakula viwili ambavyo hawa mifugo watakula.
    (Mwanafunzi ajibu)
  4. Toa maelezo mafupi kuhusu jiinsi mtakavyo watunza hawa mifugo kado na kuwapa chakula.
    (Mwanafunzi ajibu)
  5. Eleza umuhimu wa kuwafuga wanyama wa nyumbani.
    (Mwanafunzi ajibu)
  6. Taja mahali ambapo wanyama hawa hulala.
    (Mwanafunzi ajibu)

Musa anafuga wanyama shambani mwake. Wanyama hawa ni ng'ombe, kondoo, mbuzi na samaki. Musa pia hufuga ndege. Kuna kuku, bata, bata mzinga na kasuku. Ng ' ombe wa Musa ni wa maziwa. Kuna ng'ombe watano ambao hutoa maziwa. Kila Ijumaa Juma huvua samaki watatu. Musa humpa mkewe samaki hawa. Mkewe anaitwa Mario hutengenezea familia yake mchuzi wa samaki. Mchuzi huo huwa mtamu sana.
Kuku wa Musa si wengi. Wanapotaga mayai yeye huchukua machache. Kisha anampa mkewe awakipie watoto.

Maswali

  1. Taja wanyama wawili wanaofugwa na musa.
  2. Musa ono ng'ombe wangapi?
  3. Musa huvua samaki siku gani?
  4. Mario ni nani katika hadithi?
  5. Musa hufuga na

SEHEMU 2: KUSOMA KWA SAUTI
Mwanafunzi asome kifun hiki kwa sauti. _
Kasuku wangu anaitwa Pendo. Nilipewa Pendo kama zawadi na mwalimu wangu baada ya kuupita mtihani. Mwalimu wangu alinifunza jinsi ya kumtunza Pendo ili awe mwenye afya na furaha. Koko yangu alimjengea Pendo tundu lenye nafasi ya kutosha iii Pendo aweze kucheza akiwa humo ndani. Mara kwa mara mimi humtoa Pendo tunduni na kucheza naye.
Pendo hupenda sana kula majani mabichi, viazi vitamu, karoti na matunda. Pendo hufurahi sana kila ninapomwosha. Yeye hurukaruku kwa furaha huku akicheza na maji. Baada ya kumwosha Pendo mimi huvisafisha vyombo anavyotumia kuoga kwa maji safe kisha kuvianika juani•
Daktari wa mifugo huja kumchunguza na kumtibu Pendo kila anapougua. Nampenda sana Pendo wangu.

SEHEMU 3: UFAMMU
Soma hadithi hii kisha ujibu maswali.
Kadoti alikuwa anasafiri pamoj a na familia yake. Walikuwa wanatembea mbuga ya wanyama ya Nakuru. Walikuwa wamebeba chakula na matunda. Kadoti alikuwa ameketi katika kiti cha nyuma ya gari lao. Mara alipohisi njaa, alichukua nyama ya kuku na kuila. Mifupa alitupa nje kupitia kwenye dirisha la gari. Alikuwa anateremsha kioo kisha anatupa uchafu nje. Mamake alimwonya dhidi ya kufanya hivyo. Alimwambia kuwa uchafuzi wa mazingira haukubaliwi na sheria za nchi. Walipokuwa wanapita mji wa Nakuru, Kadoti alitoa ndizi mbili. Akatoa maganda akala, kisha akatupa hayo maganda nje. Baada ya mita chache gari lao lilisimamishwa na askari wa baraza la mji. Mamake Kadoti alistakiwa kwa kuruhusu mtoto kutupa taka katika barabara za mji. Alijitetea lakini askari hakumsikiliza. Alitozwa faini. Hapo ndipo Kadoti alijifunza kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.

Maswali.

  1. Kadoti na familia yake walitembea wapi?
  2. Mama Kadoti alimwonya dhidi ya kufanya nini?
  3. Mamake Kadoti alistakiwa kwa kosa gani?
  4. Kadoti na familia yake walibeba nini?
  5. Kisa hiki kinatufunza nini?

SARUFI
Andika kinyume cha neno lililopigwa mstari.

  1. Mtoto alifunga mlango.
  2. Mzee alipanda mlima.
  3. Mama alianika nguo.
  4. Mwashi alijenga nyumba

Kamilisha sentensi.

  1. Tunatumia kulima. (jembe, shoka)
  2. ______hutumiwa kukata muwa. (shoka, panga)

Tumia -ake.

  1. Kichwa
  2. Kalamu

Andika kwa maneno.

  1. 56
  2. 71

Andika wingi wa sentensi hizi.

  1. Kijiko kilioshwa na kaka.
  2. Chakula kilikuwa juu ya meza.

Tegua vitendawili.

  1. Akitolewa nje ya maji hufa.
  2. Babu asemaye
  3. Mwaka huwa na miezi

SEHEMU 4: KUANDIKA
STADI ZA KUANDIKA BARUA YA KIRAFIKI
Mwaandikie rafiki yako barua ukimweleza jinsi unavyoendelea masomoni katika nafasi uliyopewa.



MWONGOZO WA KUSAHIHISHA 

Sehemu ya A

  1. Ng'ombe/Kondo/ Mbuzi
  2. Tano
  3. ijumaa
  4. mke wa Musa 
  5. Wanyama na ndege

Ufahamu

  1. Mbuga ya wanyama ya Nakuru
  2. Kutupa takataka nje ya gari. 
  3. Kuruhusu mtoto kutupa takataka barabarani
  4. Chakula na matunda 
  5. Umuhimu wa kutunza mazingira

Sarufi

  1. alifimgua 
  2. alichuka 
  3. alianua
  4. alibomoa
  5. jembe 
  6. Panga 
  7. chake 
  8. yake 
  9. Hamsini na sita
  10. Sabini na moja 
  11. Vijiko vilioshwa na kaka 
  12. Vyakula vilikuwa juu ya meza.
  13. samaki 
  14. kalamu 
  15. kumi na mbili
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End of Term 1 SET 2 2022.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students