MASWALI
SEHEMU YA A: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Jibu maswali kwa kutamka (Alama 5)
- Ni nini wingi wa neno daftari?
- Bendera yetu ina rangi ngapi?
- Eleza maana ya "kutiwa nguvani"
- Kamilisha methali ifuatayo, "Asiyesikia la mkuu....
- Taja vazi moja la kike unalolijua.
KUSOMA KWA SAUTI
Soma kifungu hiki kwa sauti (Alama 10)
Shule yetu inaitwa Bidii Jumanne ilikuwa ni siku ya sherehe ya kutia zawadi. Walimu wetu waliwasili mapema kwa matayarisho. Mgeni wetu wa heshima alipowasili, alipewa shada la maua. Shehe na kasisi walituombea kabla ya kuanza sherehe. Wanafunzi thelathini wa gredi ya nne walituzwa. Shangazi yangu alihudhuria kwa naiba ya mama yangu. Thuluthi mbili ya watu ambao walihudhuria walikuwa kina mama.
SEHEMU YA B: SARUFI
Andika visawe vya maneno yafuatayo
- Tembo
- Nyanya
- Jogoo
- Barua
- Motokaa
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendwa.
- Chora
- osha
- tuma
- panga
- lipa
Unganisha sentensi kuwa joja kwa kutumia kiunganishi sahihi
- Alitekwa nyara. Hakudhulumiwa
- Maria amevaa koti. Maria anahisi baridi
- Utavaa jaketi. Utavaa koti
- Nilienda katika kituo cha mabasi. Nilisafiri Lamu
- Juma hakuvaa mlapa. Juma hakuvaa daluga
Taja majina ya heshima unayotumia kuwaita wafuatao.
- Mzazi wa kiume
- Ndugu wa kiume wa baba yako
- Baba wa mama yako
- Ndugu wa kiume.
- Ndugu wa kike
Andika nomino zozote tano
Andika kwa wingi
- mpira
- kiatu
- ndizi
- ua
- chungwa
SEHEMU YA C: UFAHAMU
Soma ufahamu kisha ujibu maswali (Alama 5)
Auni anamiaka kumi. Wazazi wake waliaga dunia. Anaishi na nyanya yake. Kila siku Auni na nyanya yake hula mihogo. Siku moja, Auni aliugua utapiamlo kwa kula mihogo pekee. Auni hakupata aina zote za vyakula.
Kuna aina nyingiya vyakula. Kuna vyakula vya kujenga mwili kama vile maharagwe. Kuna vyakula vya kupatia mwili nguvu kama vile mihogo. Kuna vyakula vya kuongeza kinga ya mwili kama vile matunda.
Auni hakuwa anaenda shuleni. Hatari hii ilimfikia chifu Stela. Chifu Stela alienda kumwona nyanya yake Auni. Auni alipelekwa katika kambi ya watoto mayatima. Huko alipewa lishe bora.
- Auni alikuwa na umri wa miaka mingapi?
- Auni aliugua ugonjwa wa
- Taja aina ya vyakula vya kujenga mwili
- Auni alipelekwa wapi
- Habari za Auni kutoenda shuleni zilimfikia nani?
SEHEMU YA D: KUANDIKA
Mwandikie binamu yako barua ya kirafiki ukimwalika kwa sherehe ya kuzaliwa kwako.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
|
(21-25) Sahihisha jibu sahihi |
|
Download Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 4 End of Term 2 Exams 2022 SET 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students