Tuesday, 30 August 2022 13:31

Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 End of Term 2 Exams 2022 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.

(Ni wakati wa mapumziko shuleni. Mwalimu na mwanafunzi wanajadiliana.)

Mwanafunzi: Shikamoo mwalimu. Nimefurahi kukupata bila shughuli nyingi.

Mwalimu: Marahaba Zigwembe. Nimemaliza kuzikagua insha zenu punde tu. Eh! Naona mnaendelea vizuri katika uandishi.

Mwanafunzi: Siyaamini masikio yangu. Awali tulikuwa mbumbumbu mno katika uandishi. Sina budi kukushukuru kwa juhudi zako tumbi nzima.

Mwalimu: Hilo ndilo jukumu langu; kuwanoa muwe wembe. (Kimya kidogo) Haya kibibi, ungependa nikusaidieje leo?

Mwanafunzi: (Huku akiketi mkabala na mwalimu) Bi. Chui, suala la kutofautisha vihisishi na vihusishi linaniiemea pakubwa. Sijui ni...

Mwalimu: (Akichanua uso kwa tabasamu angavu) Zigwembe, ni kama kwamba ulijua. Hilo ndilo funzo linalofuata baada ya kipindi hiki cha mapumziko. Nitatoa ufafanuzi kemkem darasani.

Mwanafunzi: (Akiinuka kuondoka) Sawasawa mwalimu, tukutane darasani niupate uhondo huo.

  1. Kilichomfurahisha mwalimu mwanzoni mwa mazungumzo haya ni
    1. kutokuwa na shughuli nyingi. 
    2. hatua waliyoipiga wanafunzi wake katika uandishi. 
    3. kuwa hapo awali, wanafunzi wake walikuwa mbumbumbu.
    4. kwamba alikuwa amemaliza kuhakiki insha.
  2. Yawezekana kuwa mazungumzo haya yalitukia mnamo majira ya
    1. alfajiri.
    2. usiku.
    3. adhuhuri.
    4. asubuhi.
  3. Unadhani ni kwa nini mwanafunzi hakuyaamini masikio yake? 
    1. Hakuyaamini maneno ya mwalimu.
    2. Mwalimu aliyatilia chumvi maelezo yake.
    3. Hakuamini kuimarika kwao ghafla katika uandishi 
    4. Maneno ya mwalimu hayakuwa na ukweli wowote.
  4. Kulingana na mazungumzo haya, ni kweli kusema kuwa mwalimu huyu ni 
    1. hodari.
    2. hatari.
    3. mjanja.
    4. mwongo.
  5. Je, kwa nini Bi. Chui hakumfafanulia
    Zigwembe tofauti baina ya vihisishi na vihusishi? 
    1. Alikuwa na shughuli chungu nzima. 
    2. Alitaka awaeleze wote darasani katika kipindi kilichofuata. 
    3. Alihitaji wanafunzi wengi ili kutoa maelezo yake. 
    4. Wakati ulikuwa umeyoyoma.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Serikali inapaswa kuwaelimisha wakulima nchini. Hivi ni kwa sababu ya upungufu wa mazao ya kilimo. Wakulima wengi wamepungukiwa na ujuzi wa shughuli za ukulima. Hivyo basi, kuna haja ya kuwafunza njia za kunyunyizia mazao yao dawa. Pia inafaa wafunzwe njia bora za upanzi. Kwa wengine, kutumia mbolea huwa ni jambo wasilolijua wala kulithamini. Hii hupunguza mazao ikiwa mashamba hayana rutuba.
Kwa wanaofuga wanyama na ndege kama vile kuku, wanapaswa kufundishwa mbinu za kukabiliana na magonjwa kama ville sotoka kwa ng'ombe na kideri kwa kuku. Maafisa wa kilimo kukabiliana na magonjwa kama vile sotoka kwa ng'ombe na kideri kwa kuku. Maafisa wa kilimo hawana budi  kuwa katika mstari wa mbele katika kuwapa wakulima misaada ya kila aina maana kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu.

  1. Kulingana na taarifa, ni kwa nini mazao ya kilimo yamepungua?
    1. Wakulima hawafanyi bidii.
    2. Wakulima hawana ujuzi unaohitajika. 
    3. Kuna upungufu mkubwa wa mvua.
    4. Kwa sababu kuna ukame uliokithiri nchini.
  2. Taarifa hii inasema kuwa, kwa wakulima wengine, matumizi ya mbolea 
    1. ni kitu muhimu mno. 
    2. ni jambo geni wasilolielewa. 
    3. hustalili kufunzwa na maafisa wa kilimo.
    4. ni jambo walilo na mazoea makuu nalo.
  3. Kulingana na ufahamu, si kweli kusema kuwa
    1. serikali haina budi kuwapa wakulima mafunzo kemkem.
    2. mashamba yasiyo na rutuba huhitaji mbolea. 
    3. sotoka huwaathiri sana kuku huku ng'ombe wakiugua kideri. 
    4. si wakulima wote wanatambua mbinu bora za kilimo.
  4. Sehemu iliyopigiwa mstari mwishoni mwa taarifa hii ina maana gani?
    1. Taifa letu linategemea sana kilimo. 
    2. Wananchi wengi wa nchi hii ni wakulima.
    3. Wananchi wote wa nchi hii ni wakulima. 
    4. Wakulima wa humu nchini hawana budi kuongeza bidii kazini.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 9 hadi 12.
Juzi tulipokuwa sebuleni tukitazama runinga, mjomba alianza kutusimulia jinsi ambavyo mwalimu wao alikuwa akiwaeleza kuhusu umuhimu wa miti. Alianza kwa kusema kuwa mwalimu wao alisema kuwa miti huwa ni maskani ya wanyama mbalimbali, sanasana nyuni ambao hutengeneza viota vyao na kutagia mayai humo. Aliendelea kutuambia kuwa wanyama wengine wanaotegemea miti kama makazi ni wanyamapori kama vile simba, chui, pundamilia na wengine. Si hayo tu, aidha, alisema kuwa miti huweza kutumiwa kujengea, kuundia samani na pia kutumika kama dawa ambapo sehemu mbalimbali za miti hutumika kutibia magonjwa mbalimbali. Tulipokuwa tumechoka kumsikiliza, alituaga na kila mmoja wetu akaelekea kulala ili turauke siku iliyofuata.

  1. Msimulizi na wenzake walikuwa wakisimuliwa kuhusu nini?
    1. Madhara ya wanyama.
    2. Matumizi ya maji. 
    3. Umuhimu wa miti.
    4. Wanyama wa porini.
  2. Yawezekana kuwa masimulizi haya yalifanyika
    1. adhuhuri.
    2. asubuhi.
    3. alasiri.
    4. usiku.
  3. Kulingana na habari hii, miti hutusaidia katika haya yote ila kutupa 
    1. dawa 
    2. kuni.
    3. vifaa vya ujenzi. 
    4. vifaa vya kutengenezea samani. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Hapo zamani za kale, palikuwa na sungura na mbwa. Wanyama hawa walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Naam, walipendana kama uta na upote. Wanyama hawa walipokuwa makaoni mwao, mbwa alimwambia sungura kuwa yeye alihisi njaa sana. Aliendelea kumwambia kuwa angependa kumla yeye kwa kuwa sungura huwa na nyama nzuri na tamu. Kusikia vile, sungura alijifanya kutojali ingawa alishtuka sana moyoni. Punde kidogo wakati mbwa alikuwa ameangalia kando, sungura alitoweka na kuingia kichakani. Tangu siku hiyo, mbwa aliana kumwinda sungura mahali popote wakati wowote.

  1. Kulingana na taarifa hii, unadhani ni kwa nini sungura hujificha kichakani? 
    1. Asipatikane na mbwa. 
    2. Anaendelea kumtafuta mbwa. 
    3. Anaaibika anapomwona mbwa
    4.  Anatafuta mawindo humo. 
  2. Kwa maoni yako, mbwa alikuwa
    1. rafiki wa dhati.
    2. rafiki mnafiki.
    3. na nyama bora zaidi.
    4. rafiki mzuri.
  3. Sungura alipata mwanya wa kutoweka pale ambapo 
    1. mbwa alimwambia nyama yake ilikuwa tamu. 
    2. walikuwa wamekaa maskanini kwao.
    3. mbwa alikuwa ameangalia kando.
    4. mbwa alitoweka na kuingia kichakani. 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa
Visa vya watu kuwaua wake, waume au watoto wao vimekuwa _16__ sana siku hizi. Si jambo _17_ mtu kufikia hatua kama _18_ . Hakika, ni_19_ mkubwa. Si hayo tu, wengine hufikia hatua ya kujiangamiza wao wenyewe kwa kujitoa uhai. Binadamu wanafaa kujua njia_20_ za kusuluhisha matatizo yao kuliko kuchinjana na kuuana.

  1.                    
    1. mingi
    2. wengi 
    3. nyingi
    4. vingi 
  2.                    
    1. jema
    2. nzuri
    3. baya
    4. mbaya 
  3.                
    1. hili
    2. hiyo
    3. hizi
    4. huo 
  4.                    
    1. mnyama
    2. wanyama 
    3. unyama
    4. kinyama
  5.                    
    1. mzuri
    2. fupi
    3. ndefu
    4. bora 

Katika swali la 21-30. jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Chagua sentensi ambayo haina kivumishi cha sifa. 
    1. Tuliambiwa kuwa Mombasa kuna joto jingi. 
    2. Rama alilila tunda bichi. 
    3. Chakula tulichoandaliwa kilikuwa kitamu. 
    4. Mwalimu wetu wa lugha ni mnene.
  2. Hii, huyu na lile vyote ni
    1. vielezi vya mahali. 
    2. vivumishi viashiria. 
    3. viwakilishi vionyeshi. 
    4. vivumishi halisi.
  3. Sehemu inayosukuma damu ienee mwilini ni
    1. ini
    2. ubongo.
    3. figo.
    4. moyo.
  4. Tegua kitendawili hiki. Hawa wanaingia, hawa wanatoka. 
    1. Samaki.
    2. Maji.
    3. Nyuki.
    4. Nzi.
  5. Chagua orodha ya vivumishi vya aina moja.
    1. Nene, wako, vyetu.
    2. Hii, wao, chafu.
    3. Letu, yao, chake.
    4. Huyu, wangu, bovu.
  6. Jibu la alamsiki ni
    1. marahaba.
    2. nawe pia
    3. jaala.
    4. binuru.
  7. Ni neno lipi kati ya haya litakuwa la mwisho katika kamusi?
    1. Kibindo
    2. Kibanda
    3. Kibarua
    4. Kibanio
  8. Chagua sentensi yenye matumizi yasiyo sahihi ya amba.
    1. Ambao waliwasili mapema walipata nafasi.
    2. Wanyama ambao waliogongwa na lori wameondolewa.
    3. Mafunzo ambayo tulipewa yametufaa. 
    4. Ambao hawana vitabu wasome magazeti.
  9. Msimu wa mvua nyingi huitwa 
    1. masika.
    2. vuli. 
    3. mafuriko. 
    4. 'iangazi.
  10. Chagua sentensi iliyotumia lugha ya adabu.
    1. Mtoto amekojoa kitandani. 
    2. Shangazi yangu amejifungua salam 
    3. Wanawake wenye mimba wapewe viti.
    4. Mgonjwa alihara hadi akafa.

MWONGOZO WA KUSAHISHA

swa timer ms

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 End of Term 2 Exams 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students