Wednesday, 20 April 2022 11:38

Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 1 Exams 2022 SET 1

Share via Whatsapp

MASWALI

SEHEMU 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu amsomee mwanafunzi kifungu hiki kisha amwulize maswali yafuatayo.
Paka yuko jikoni. Amebeba panya mdomoni. Panya huyo ni mweusi. Paka anajificha mvunguni mwa meza. Mama anamwona paka.

  1. Paka yuko wapi?
    (Mwanafunzi ajibu)
  2. Paka amebeba nini mdomoni?
    (Mwanafunzi ajibu)
  3. Panya huyo ni wa rangi gani?
    (Mwanafunzi ajibu)
  4. Paka anajificha wapi?
    (Mwanafunzi ajibu)
  5. Nani anamwona paka?
    (Mwanafunzi ajibu)

Vigezo vya Kutathminia Kusikiliza na kuzungumza

Kiwango cha utendaji 
 Upeo/Alama  4  3  0 - 2

SEHEMU 2: KUSOMA KWA SAUTI (Alama 5)
Mwanafunzi asome kifungu hiki kwa sauti.
Ilikuwa siku ya Ijumaa tulipokuwa sebuleni tukitazama runinga. Sabu alianza kutusimulia jinsi ambavyo mwalimu wao alikuwa akiwaeleza kuhusu umuhimu wa miti. Hata ingawa alikuwa shuleni miaka sitini iliyopita, alikuwa akiyakumbuka vizuri.
Alianza kwa kusema kuwa mwalimu wao alisema kuwa miti huwa ni maskani ya wanyama mbalimbali sanasana nyuni ambao hutengeneza viota vyao na kutagia mayai humo. Aliendelea kutuambia kuwa wanyama wengine wanaotegemea miti kama makazi ni wanyamapori kama vile simba, chui, pundamilia na wengine.
Vigezo vya Kuathminia - Kusoma

Kiwango cha utendaji
Maneno yaliyosomwa katika dakika moja 60 na zaidi  41 - 60 21 - 40  0-20

SEHEMU 3: UFAHAMU (Alama 5).
Mwanafunzi asome kifungu hiki na kujibu maswali.

  1. NDOTO YA AMINA
    Babu alimnunulia Amina godoro na foronya. Usiku alipolala aliota ndoto. Aliota kuwa alikuwa msichana mkubwa. Alikuwa akifanya kazi ya ualimu. Baada ya miaka miwili aliacha ualimu akawa mkulima. Aliuza mazao akapata shilingi laki tatu. Alipokuwa akipeleka pesa zake benkini, aliamka kutoka usingizini.
    1. Nani alimnunulia Amina godoro?
    2. Aliota ndoto wakati gani?
    3. Mara ya kwanza alikuwa akifanya kazi gani?
    4. Baada ya miaka miwili alianza kufanya kazi gani?
    5. Alikuwa akipeleka pesa zake wapi? 
  2. MWALIMU BIDII
    Mwalimu Bidii ni mwalimu wa Kiswahili. Anafundisha katika shule ya msingi ya Hekima. Kila siku yeye hutukumbusha kuwa tuwe watoto safi. Kuna siku alituletea ndizi. Tulifurahia mno. Alituahidi kuwa atatupeleka jijini Mombasa.
    1. Mwalimu Bidii hufundisha somo gani?
    2. Mwalimu Bidii hufundisha katika shule gani?
    3. Mwalimu Bilii huwahimiza wanafunzi kuwa watoto
    4. Mwalimu aliwaletea nini?
    5. Mwalimu aliwaahidi kuwa atawapeleka wapi?

Vigezo vya Kutathminia - Ufahamu 

Kiwango cha utendaji 
 Upeo/Alama  4  3  0 - 2

SEHEMU 4: SARUFI
Tunga sentensi ukitumia maneno haya.

  1. jiwe
  2. embe 
  3. mwiko
  4. soko
  5. fimbo

Andika sentensi kwa wingi.

  1. Kiatu chake kimeraruka.
  2. Mtoto yule anakula tunda.
  3. Goti lake limeumia.
  4. Kioo hiki kilivunjika jana.
  5. Meza hii ni ya mwanafunzi.

Andika akisami kwa maneno.

  1. 1/6 -
  2. 1/4 -
  3. 1/2 -
  4. 1/3 -
  5. 1/5 -

Geuza maneno yafuatayo katika hali ya ukubwa.

  1. Mto - 
  2. Mtu - 
  3. Mke -
  4. Mti -
  5. Mji -

Vigezo vya kutathminia - Sarufi

Kiwango cha utendaji 
 Upeo/Alama 19-20  13-18 7-12 0 - 6

SEHEMU 4: KUANDIKA
INSHA Andika insha juu ya:
NYUMBANI KWETU

Vigezo vya kutathminia - Kuandika

Kiwango cha utendaji 
 Upeo/Alama 19-20  13-18 7-12 0 - 6

MAJIBU

SEHEMU 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu amsomee mwanafunzi kifungu hiki kisha amwulize maswali yafuatayo.
Paka yuko jikoni. Amebeba panya mdomoni. Panya huyo ni mweusi. Paka anajificha mvunguni mwa meza. Mama anamwona paka.

  1. Paka yuko wapi?
    Jikoni
  2. Paka amebeba nini mdomoni?
    Panya
  3. Panya huyo ni wa rangi gani?
    Mweusi
  4. Paka anajificha wapi?
    mvunguni mwa meza
  5. Nani anamwona paka?
    Mama

Vigezo vya Kutathminia Kusikiliza na kuzungumza

Kiwango cha utendaji 
 Upeo/Alama  4  3  0 - 2

SEHEMU 2: KUSOMA KWA SAUTI (Alama 5)
Mwanafunzi asome kifungu hiki kwa sauti.
Ilikuwa siku ya Ijumaa tulipokuwa sebuleni tukitazama runinga. Sabu alianza kutusimulia jinsi ambavyo mwalimu wao alikuwa akiwaeleza kuhusu umuhimu wa miti. Hata ingawa alikuwa shuleni miaka sitini iliyopita, alikuwa akiyakumbuka vizuri.
Alianza kwa kusema kuwa mwalimu wao alisema kuwa miti huwa ni maskani ya wanyama mbalimbali sanasana nyuni ambao hutengeneza viota vyao na kutagia mayai humo. Aliendelea kutuambia kuwa wanyama wengine wanaotegemea miti kama makazi ni wanyamapori kama vile simba, chui, pundamilia na wengine.
Vigezo vya Kuathminia - Kusoma

Kiwango cha utendaji
Maneno yaliyosomwa katika dakika moja 60 na zaidi  41 - 60 21 - 40  0-20

SEHEMU 3: UFAHAMU (Alama 5).
Mwanafunzi asome kifungu hiki na kujibu maswali.

  1. NDOTO YA AMINA
    Babu alimnunulia Amina godoro na foronya. Usiku alipolala aliota ndoto. Aliota kuwa alikuwa msichana mkubwa. Alikuwa akifanya kazi ya ualimu. Baada ya miaka miwili aliacha ualimu akawa mkulima. Aliuza mazao akapata shilingi laki tatu. Alipokuwa akipeleka pesa zake benkini, aliamka kutoka usingizini.
    1. Nani alimnunulia Amina godoro?Babu
    2. Aliota ndoto wakati gani? Usiku
    3. Mara ya kwanza alikuwa akifanya kazi gani? Ualimu
    4. Baada ya miaka miwili alianza kufanya kazi gani? Mkulima
    5. Alikuwa akipeleka pesa zake wapi?  benkini
  2. MWALIMU BIDII
    Mwalimu Bidii ni mwalimu wa Kiswahili. Anafundisha katika shule ya msingi ya Hekima. Kila siku yeye hutukumbusha kuwa tuwe watoto safi. Kuna siku alituletea ndizi. Tulifurahia mno. Alituahidi kuwa atatupeleka jijini Mombasa.
    1. Mwalimu Bidii hufundisha somo gani? Kiswahili
    2. Mwalimu Bidii hufundisha katika shule gani? shule ya msingi ya Hekima
    3. Mwalimu Bilii huwahimiza wanafunzi kuwa watoto safi
    4. Mwalimu aliwaletea nini? Ndizi
    5. Mwalimu aliwaahidi kuwa atawapeleka wapi? Mombasa

SEHEMU 4: SARUFI
Tunga sentensi ukitumia maneno haya.
( Mwanafunzi awe amejibu maswali yakiwa yamejibiwa yapasavyo apewe alama)

  1. embe - Embe ni tunda tamu na lenye vitamini nyingi
  2. mwiko - Mama aliutumia mwiko kupika ugali.
  3. soko - Tulienda soko na baba tukanunua maembe.
  4. fimbo - Mkulima alitumia fimbo kufukuza mbwa alikua akitaka kula kuku.

Andika sentensi kwa wingi.

  1. Kiatu chake kimeraruka.
    Viatu vyao vimeraruka.
  2. Mtoto yule anakula tunda.
    Watoto wale wanakula matunda.
  3. Goti lake limeumia.
    Magoti yao yameumia.
  4. Kioo hiki kilivunjika jana.
    Vioo hivi vilivunjika jana.
  5. Meza hii ni ya mwanafunzi.a sixth1/6
    Meza hizi ni za wanafunzi.

Andika akisami kwa maneno.

  1. 1/6 - sudusi / moja ya sita
  2. 1/4robo / moja ya nne
  3. 1/2nusu
  4. 1/3thuluthi
  5. 1/5 - hamusi / moja ya tano

Geuza maneno yafuatayo katika hali ya ukubwa.

  1. Mto -  jito
  2. Mtu - jitu
  3. Mke - janajike
  4. Mti - jiti
  5. Mji - Jiji
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 1 Exams 2022 SET 1.

Tap Here to Download for 30/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students