Swali la 1 hadi 5: Soma mazungumzo haya kisha ujibu maswall 1 hadi 5
Rehema: (Huku akiutoa mkoba wako mabegani) Mama umeshindaje leo?
Mama: Nimeshinda vyema sana, labda wewe mwanane.
Rehema: Nami pia.
Mama: Nenda basi ukafue sare. Nami naenda jikoni kuandaa chajio.
Rehema. Sawa mama. Nataka pia nifanye kazi ya ziada tuliyopewa na mwalimu.
- Mazungumzo haya yalifanyika wakati gani?
- Asubuhi
- Mchana
- Jioni
- Usiku
- Neno 'sare' kama lilivyotumika kwenye mazungumzo lina maana ya
- Nguo za sherehe
- Kaptura na shati
- Rinda na sweta
- Mavazi yanayovaliwa shuleni
- Mamake Rehema alikuwa na shughuli gani?
- Kuandaa chujio
- Kufanya kazi ya ziada
- Kuandaa chamcha
- Kuenda shambani
- Ni nani aliyempa Rehema kazi ya ziada?
- Mama yake
- Mwalimu wake
- Baba yake
- Rafiki yake
- Kitendo cha Rehema kukubali kufanya kazi ya ziada aliyopewa kinaonyesha kuwa yeye ni
- mtukutu
- mtundu
- mtiifu
- mvivu
Swali la 6 hadi 10, Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.
Ilikuwa likizo ya mwezi wa Aprili. Mimi na dada yangu Pendo tulihudhuria harusi ya shangazi yetu, Zainabu. Tulikuwa tumealikwa ili kubeba pete za bibi na bwana harusi, Watu wengi walihudhuria harusi hiyo ambayo ilikuwa ya kufana na kila mtu alitaka kuona shangazi yetu akifunga pingu za maisha na mpenzi wake Jabali.
Watu walifurahia kula keki na vyakula vya aina mbalimbali. Kulikuwa pia na vinywaji. Baada ya kufunga pingu za maisha shangazi yangu na mume wake Jabali walibebwa na ndege kuelekea Uarabuni.
- Ni nani na nani walifunga pingu za maisha?
- Mimi na dadangu
- Pendo na dadake
- Zainabu na jabali
- Shangazi na Pendo
- Kila mtu alitaka kuona nani akifunga pingu za maisha?
- Shangazi
- Mjomba
- Mama
- Dada
- Bwana harusi alikuwa anaitwa nani?
- Mpenzi
- Zainabu
- Mume
- Jabali
- Baada ya harusi, mume na mke walienda wapi?
- Uaribuni
- Kwa ndege .
- Nyumbani
- Pwani
- 'Kufunga pingu za maisha' ni aina gani ya tamathali?
- Nahau
- Tashbihi
- Methali
- Kitendawili
Swali la 11 hadi 15, Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Wanyama wanaofugwa huitwa mifugo. Wanyama hawa ni kama mbuzi, kondoo, ng'ombe, ngamia na punda. Wanyama hawa wana faida nyingi sana. Mfugaji huwakamua ng'ombe, ambao humpa maziwa ambayo humpa pesa nyingi akiyauza.
Maziwa pia hutumiwa kutengeneza siagi. Maziwa ni tamu sana, Kondoo hutupa sufi ambazo hutumiwa kutengeneza fulana. Maziwa ya mbuzi ni mazuri sana. Ngamia hutumiwa kutubebea mizigo. Maziwa yake pia hunywewa na watu wengine huamini kuwa ni dawa. Wanyama wote wanahitaji kutunzwa, Sharti waishi mahali safi na wapewe chakula cha kutosha ili wawe na afya nzuri.
- Wanyama wanaofugwa nyumbani huitwa
- mifugo
- Ng'ombe'
- Jibini
- Sufi
- Ni mnyama yupi kati ya hawa hafugwi nyumbani?
- Ng'ombe
- Mbuzi
- Kondoo
- Simba
- Ni ipi si faida ya maziwa
- Hutupa pesa
- Kutengeneza siagi
- Kunywewa
- Kutengeneza sufi
- Ni mnyama yupi hutumika kubebea mizigo
- Ng'ombe'.
- Kondoo
- Mbuzi
- Ngamia
- Anayewafuga wanyama huitwa _________________
- Mtu
- Mfugaji
- Mfungaji
- Wavulana
Soma kifungu hiki kisha ujaze nafasi 16 - 20 kwa jibu sahihi.
Elimu ni kitu chenye umuhimu ____16____ kwetu. Kwanza elimu hutufanya tujue kusoma na ___17___ . Bila elimu hatuwezi___18___ wa wenzetu kwa njia ya kuandika au kusoma. Watu ___19___ hawajasoma hukumbwa na changamoto ___20___. Sharti sote tuipende elimu.
-
- Kubwa
- mkumbwa
- kikubwa
- mkubwa
-
- kulia
- kuandika
- kuketi
- kucheka
-
- kuwasiliana
- kuwasilisha
- kuwasiliwa
- kuwasilika
-
- ambayo
- ambaye
- ambamo
- ambao
-
- mingi
- nyingi
- jingi
- wengi
Swali la 21 hadi 30. Chagua jibu sahihi.
- Kanusha sentensi hizi: Alisoma hadithi.
- Hangesoma hadithi
- Hakusoma hadithi
- Hajasoma hadithi
- Hatasoma hadithi
- Andika kwa wingi: Ndoo hii imejaa maji..
- Ndoo hizi zimejaa maji
- Ndoo haya yamejaa maji
- Mandoo hizi zimějaa maji
- Mandoo hizi zimejaa maji
- Kisawe cha barabara ni ___________
- chete
- lami
- njia
- soko
- Tegua vitendawili hivi: Nyama nje ngozi ndani
- Firigisi
- Muwa
- Mkate
- Ndizi
- Kamilisha methali hizi: Kidole kimoja hakivunji ______________________
- kidole
- chawa
- dawa
- mto
- Tumia kimilikishi '-ake' ipasavyo:Mtoto analilia kalamu
- yake
- lake
- chake
- vyao
- Jibu la 'Alamsiki" ni
- alamsiki
- vyema
- aheri
- binuru
- Kikundi cha matunda huitwa
- pakacha
- mtumba
- bumba
- numbi
- Andika kwa tarakimu
Elfu kumi na moja- 11000
- 10001
- 1001
- 1100
- Kitendo cha kupasha chakula moto
- kukanza
- kupika
- kuinjika
- kuoka
INSHA
Andika insha kuhusu;
LIKIZO YA KUPENDEZA
MARKING SCHEME
- C
- D
- A
- B
- C
- C
- A
- D
- A
- A
- A
- D
- D
- D
- B
- D
- B
- A
- D
- B
- B
- A
- C
- A
- B
- A
- D
- A
- A
- A
Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 2 CBC Exams 2022 Set 2.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students