Displaying items by tag: Insha

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya vale uliyopewa.

Sisi _ 1_ na mama_ 2__mkali sana. Mama_3_ hakuturuhusu_4_ sheria zozote kiamboni petu. Kila alipohisi kuwa 5_kuoga, alitulazimisha kuoga maji baridi lakini 6 kutumia sabuni mbayo 7__ vizuri sana. Au kila alipogundua ___8utovu kinidhamu, tulikaripiwa na kukumbushwa kuwa ulikuwa wajibu 9 _kuwalinda wavyele wetu kwa tabia.

  1.        
    1. tulilelewa
    2. tulielewa
    3. tulilelea
    4. tulilea
  2.        
    1. aliyokuwa
    2. aliyekuwa
    3. aliyekua
    4. aliokuwa
  3.        
    1. huo
    2. hio
    3. huyo
    4. hilo
  4.        
    1. kuvuja
    2. kufunja
    3. ufuja
    4. kuvunja
  5.        
    1. tuliogopa
    2. tumeogopa
    3. tutaogopa
    4. wanaogopa
  6.      
    1. ingawa
    2. na
    3. kwa
    4. kuwa
  7.          
    1. ilinukwa
    2. ilinukia
    3. inanukia
    4. ilinuka
  8.            
    1. tuna
    2. mna
    3. wana
    4. lima
  9.            
    1. wangu
    2. wetu
    3. wao
    4. yetu

Mawasiliano ni kitendo cha_10_ujumbe. Hii ni _ 11_. binadamu sanasana. Kuna njia 12 za mawasiliano. Kunazo zile za jadi kama vile kuwasha moto, kupiga uyoma au kutuma watu maalum_ 13 ujumbe mahali ulipohitajika, siku hizi, watu 14_ simu, magazeti, majarida na vifaa__15_ kuwasiliana.

  1.          
    1. kupishana
    2. kupashia
    3. kupashika
    4. kupashana
  2.          
    1. licha ya
    2. katikati ya
    3. baina ya
    4. mithili ya
  3.        
    1. ' mingi
    2. nyingi
    3. jingi
    4. mingi
  4.          
    1. kuupeleka
    2. kuzipeleka
    3. kulipeleka
    4. kukupeleka
  5.          
    1. walitumia
    2. hutumia
    3. wametumia
    4. wangetumia
  6.          
    1. nyinginezo
    2. zinginezo
    3. mengineyo
    4. vinginevyo

Kuanzia swali la 16-30. jibu kila swali kulingana na maagizo.

  1. Chagua orodha ambayo ni ya vielezi
    1. hivi, nyingi, yoyote, chake
    2. nyinyi, wewe, mimi, sisi
    3. sana, upesi, hakika, kabisa
    4. lini, gani, vipi mbona
  2. Chagua kiashiria takriri kilicho sahihi kujaza pengo:
    Vikombe              vilianguka hapa.
    1. Vivi hivyo 
    2. hivyo hivi 
    3. hivi vivi
    4. vivi hivi
  3. Jaza pengo kwa neno sahihi:
    Mama alienda shambani na alishinda kuko huko mchana -
    1. kutua 
    2. kutwa 
    3. kutwaa 
    4. kucha
  4. Ni yupi mpangilio uletao mfululizo ufaao wa wakati?
    1. Alfajiri, asubuhi, adhuhuri, alasiri magharibi
    2. Alasiri, asubuhi, alfajiri, magharibiadhuhuri
    3. Asubuhi, alfajiri, alasiri, adhuhuri,magharibi.
    4. Alfajiri, asubuhi, alasiri, adhuhuri,magharibi
  5. Umbo hili ni
    1
    1. duara
    2. mche
    3. mpira 
    4. duara dufu
  6. Mnyama ana manyoya mwilini, naye binadamu ana 
    1. nywele 
    2. malaika 
    3. ndewe 
    4. mashamba
  7. Tegua kitendawili hiki:
    Mava hapo mava pale
    1. kifo
    2. kioo
    3. kumetamcta
    4. kivuli
  8. Kutangaza kwa sauti kubwa ni
    1. kupiga maji
    2. kupiga mayowe
    3. kupiga mbiu
    4. kipiga domo
  9. Chagua kinyume cha sentensi ifuatayo:
    Kitindamimba alifurahi sana.
    1. Kifunguamimba alifurahi sana. 
    2. Kitindamimba alikasirika sana, 
    3. Mwanambee alifurahi sana. 
    4. Mwanambee alikasirika sana.
  10. Kanusha: Nimekula nikashiba
    1. Sijala nikashiba.
    2. Sijakula nikashiba.
    3. Sijala wala kushiba.
    4. Sikula wala kushiba.
  11. Jaza pengo kwa usahihi:
    Nyinyi               mli             tualika karamuni.
    1. ndinyi/o
    2. ndiwo/ wo
    3. ndio/o
    4. ndio/ ye
  12. Tunasema shungi la nywele                la kuni pia                 la mchanga.
    1. chane/ tita
    2. tita/ fungu
    3. shado/koja
    4. kicha/ bumba
  13. 3, 7, 17, 31 na 43 ni baadhi ya nambari
    1. tasa
    2. shufwa 
    3. chanya 
    4. witiri
  14. Kamilisha sentensi kwa usahihi:
    Mahali hapa palifyekwa
    1. pakafyekana
    2. pakafyekeshwa
    3. pakafyekela
    4. pakafyekewa
  15. Katika milioni sita kuna laki ngapi?
    1. Sita
    2. Sitini
    3. Elfu sita
    4. Mia sita

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.
Mlango ulibishwa. Bakari akachungulia kwenye tundu la mlangoni. Akaona mwanamke na mwanamume wamesimama wamebeba matunda. “Baba na mama wako?" waliuliza watu wale wawili. "La, hawapo, wameenda sokoni," Bakari alijibu,
“Basi watakapokuja wasalimie na uwape matunda haya na kuku huyu," wakamaliza. "Ngojeni niwapokee, insiende tafadhali." Bakari alisema huku akifungua mlango. Kufumba na kufumbua, Bakari alijikuta amewekewa bastola kichwani. “Funga mdono wako ukitaka usalama wako, ng'ombe wewe. Nyinyi mnashiba na watu wafa njaa!" Alisema mwanamume yule kwa ghadhabu. "Pesa, dhahabu na vyombo vya mama yako viko wapi?" Mwanamke aliuliza huku akizaba Bakari makofi mawili mazito. Bakari akamwonyesha kila kitu kwani roho yake ilikuwa mikononi, alikuwa hajijui hajitambui!
Wezi wale wawili wakaisafisha nyumba na kuifanya msikiti. Wakampulizia Bakari dawa ya usingizi. Papo hapo akaanguka na kulala fofofo!

  1. Bakari alikuwa na nani nyumbani?
    1. Pekee
    2. Bibiye
    3. Rafiki yake
    4. Mama  na baba
  2. Watu wale wawili waliuliza akina nani?
    1. Baba
    2. Wazee
    3. Baba na mama
    4. Mama
  3. Ni nini kilichomfanya Bakari afungue mlango?
    1. Alishurutishwa kufanya hivyo.
    2. Zawadi alizoambiwa ni za wazazi wake.
    3. Alitaka kuwaona wageni wale vizuri.
    4. Aliwaona mwanamume na mwanamke.
  4. Bakari alipigwa makofi na nani?
    1. Mamake
    2. Rafikiye 
    3. Mwanamume yule 
    4. Mwanamke yule
  5. "Kufumba na kufumbua' ina maana gani?
    1. Hapo hapo
    2. Mara kwa mara 
    3. Baadaye 
    4. Kwa haraka kabisa
  6. Kumpokea mtu ni kufanya nini?
    1. Kumchukia 
    2. Kumkaribisha 
    3. Kumwongelesha 
    4. Kumfungulia mlango
  7. Kuwa roho mkononi ni sawa na kusema
    1. kuwa karibu kufa. 
    2. kuwa na woga zaidi. 
    3. kwenda na roho kwenye mkono. 
    4. kubeba roho kwenye mkono.
  8. Wezi walilalamikia nini?
    1. Kutofunguliwa mlango. 
    2. Wao kushiba na watu kufa kwa njaa. 
    3. Kutokuweko na wazazi. 
    4. Kutopata dhahabu, vy'ombo na pesa.
  9. Wezi hawa wangeshikwa wakiiba tungewaambia methali gani? 
    1. Siku za mwizi ni arubaini.
    2. Mtaka yote hukosa yote.
    3. Bendera hufuata upepo.
    4. Mtegemea cha nduguye hufa masikini.
  10. Neno ghadhabu lina maana gani kuligana na ufahamu? 
    1. Elekeza 
    2. Haraka kabisa 
    3. Hofu kubwa 
    4. Kukasirika

Soma kifingu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Simu ni chombo cha watu cha kuwasiliana. Simu hutumia mawimbi ili kupokea sauti au picha. Kuna aina mbili za simu. Rununu na simu ya ofisi.
Stepford Press and Publishers, 2021
Simu ya ofisi au simu ya nyumbani mara nyingi hutumiwa ofisini ama nyumbani. Simu hii huwekwa mahali fulani maalum katika ofisi. Simu hii huwekwa katika mapokezi. Inapopigwa, huwezi kuona nambari ya anayepiga.
Rununu pia huitwa simu tamba, selula au rokono. Rununu ni simu ndogo ambayo unaweza kuibeba mahali popote unapoenda. Rumunu hutuinia simu kadi. Pia hutumia kadihela ili kupata muda wa maongezi. Manufaa ya rununu ni tumbi tumbi. Hata kama ni ndogo wahenga walisema usione wembamba wa reli, gari moshi hupita.
Manufaa ya rununu ni kuwa huweza kutuma arafa. Arafa ni ujumbe mfupi unaotumwa kwa njia ya kuandika. Pia, hutumika katika biashara kwa kutuma pesa za kununua bidhaa.
Simu pia hutumika kuwapa watu ajira kwa kuajiriwa katika duka la M-pesa, kuuza rununu na vifaa vyake. Watu wengine huzitengeneza simu zilizoharibika kwa malipo na wao hupata ajira.
Hakuna kizuri kisichokuwa na hila. Rununu ina hasara pia. Inaweza kutumiwa na waovu kuwaibia watu pesa. Aidha kutuma ujumbe wa chuki, matusi na picha chafu zisizofaa.
Daima, tutumie rununu kwa uangalifu mkubwa tusije tukajuta majuto ya mjukuu ambayo huja baadaye.

  1. Simu ndogo ambayo mtu anaweza akatembea nayo mahali popote inaitwa 
    1. simu tamba 
    2. simu ya nyumbani 
    3. simu ya ofisi 
    4. arafa
  2. Rununu ni kifaa cha
    1. maliasili 
    2. ajira 
    3. teknolojia 
    4. madini
  3. Rununu pia haiitwi
    1. ofisi 
    2. selula 
    3. rukono 
    4. simu tamba
  4. Kadi ambayo hununuliwa yenye nambari fulani za rununu ambazo mtu hutumia kwa kitambulisho chake pekee huitwa
    1. ajira 
    2. kadi 
    3. simu kadi 
    4. simu hela
  5. Ipi si manufaa ya rununu?
    1. Kutuma arafa.
    2. Kuwapa watu ajira.
    3. Kuwaibia watu pesa. 
    4. Kupata pesa kwa kutengeneza rununu zilizoharibika.
  6. Manufaa ya rununu ni tumbi tumbi.
    Maana ya tumbi tumbi ni
    1. si tele 
    2. chache 
    3. nyingi 
    4. haba
  7. Maana ya neno ‘ajira' ni
    1. Kazi 
    2. pesa 
    3. malipo 
    4. hela
  8. Ni methali gani inalingana na maelezo haya: Rununu, hata kama ni kifaa kidogo, kina faida nyingi? 
    1. Enga kabla ya kujenga. 
    2. Hakuna kizuri kisichokuwa na ila. 
    3. Majuto ni mjukuu huja kinyume. 
    4. Usione wembamba wa reli gari moshi hupita.
  9. Mojawapo ya hasara za rununu ni
    1. kuuza rununu na vifaa vyake kwa malipo kwenye duka la simu kama mfanyi kazi.
    2. kuwasiliana na marafiki.
    3. kutuma ujumbe wa chuki na matusi. 
    4. kuajiriwa katika duka la M-pesa.
  10. Kichwa mwafaka cha kifungu hiki ni
    1. Kadihela 
    2. Rununu 
    3. Mawasiliano 
    4. Arafa

INSHA
Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.
HASARA ZA MMOMONYOKO WA UDONGO

MARKING SCHEME

  1. A
  2. B
  3. C
  4. D
  5. A
  6. C
  7. B
  8. A
  9. B
  10. D
  11. C
  12. B
  13. A
  14. B
  15. D
  16. C
  17. D
  18. B
  19. A
  20. B
  21. A
  22. D
  23. C
  24. D
  25. C
  26. C
  27. B
  28. A
  29. C
  30. B
  31. A
  32. C
  33. B
  34. D
  35. B
  36. B
  37. A
  38. B
  39. A
  40. D
  41. A
  42. C
  43. A
  44. C
  45. C
  46. C
  47. A
  48. D
  49. C
  50. B
Thursday, 16 September 2021 06:44

Insha - Class 7 Kiswahili Revision Notes

Insha ya Masimulizi

Insha hii huwa na hisi mbili: furaha na huzuni

Vinaweza visa vya kubuni au halisi

Mtahiniwa aweza kutahiniwa mara tatu

Mwanzo wa handithi – dokezo
Huhitajika aendeleze
Kimalizio/tamati

Mtahiniwa lazima aane insha na atamatishe kwa kutumia kimalizio hicho

Huzuni au Tanzia

Visawe vya huzuni ni masikitiko, majonzi, jitimai, buka, chonda na msiba

Hivi ni visa vinanyoleta majonzi, huzuni, simanzi, sikitiko au jitimai

  • Mikondo
  • Ujambazi/unyang’anyi/uporaji/wizi
  • Utekajinyara
  • Ujangili
  • Wizi wa mifugo
  • Ulaghai
  • Magendo
  • Ugomvi wa kijamii
  • Uvamizi na watu katili
  • Migomo

Misamiati na mapambo

  • Mayowe – ukemi, usiahi, mayowe
  • Wasiwasi- jekejeke, jakamoyo, kiherehere
  • Kufa – kata kamba, enda ahera, jongomeo
  • Hasira – pandwa na mori, kuwa na tumbo joto, kama zaibaki kwenye kipimajoto
  • Nilinyapianyapia/nilinyatianyatia nyatunyatu
  • Joho la kiwewe lilinivaa
  • Nilichana mbuga/nilitifua vumbi ili kuyaokoa maish -
  • Moyo ulinidwikadwika/ulinipapa kama ngoma za mahepe
  • Malaika yalinisimama wima
  • Tulisikia sauti zilizotweta kama
  • Sikuyaamini macho nilipoona
  • Nilipiga usiahi ambao ungewafufua wafu
  • Ulimi uliniganda kinywani
  • Nililia kwa kite na imani lakini kilio si dawa
  • Nilitoka shoti kama
  • Ngeu ilimtiririka kama
  • Milio ya risasi ilitamalaki kwenye anga
  • Parafujo za miguu ziliregea
  • Macho yalinitoka pima kama
  • Nilitetemeka kama unyasi nyikanu
  • Kijasho chembamba kikaanza kunitoka

Methali

  • Mbwa hafi maji akiona ukoko
  • Damu ni nzito kuliko maji
  • Tama mbele mauti nyuma
  • Unjanja wa nyani huishia jagwani
  • Siku za mwizi ni arubaini
  • Pwagu hupata pwaguzi

Ragba

  • Juhudi ziligonga mwaba
  • Maisha yalianza kuingia ufa
  • Jaribu kwa udi na uvumba
  • Sijui alipandwa na pepo gani
  • Mambo yalimwendea tege/upogo upogo
  • Alitoka na michirizi ya damu
  • Alipigwa kitutu/kipopo

Dekeza

  • Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
  • Huruma zake ziligeuka kama umande
  • Alilia kilio cha kite na shake bila kufahamu kilio si dawa
  • Alivamiwa vaa bin vu

Takriri

  • Haambiliki hasemezeki
  • Hana hanani
  • Hazindishi hapunguzi
  • Hapiki hapakui
  • Jando wala togo

Insha ya Mikasa

Mikasa ni matukio yaletayo maafa, masaibu na matatizo kwa watu
Visawe

  • Msiba
  • Balaa
  • Zani
  • Baa
  • Maafa
  • Janga
  • Belua

Mifano ya mikasa

  • Moto
  • Wizi
  • Ajali barabarani
  • Ugaidi
  • Ubakaji
  • Utekaji nyara
  • Zilizala
  • Kuza maji
  • Maporomoko ya ardhi
  • Mlipuko wa bomu
  • Ukame
  • Kabobo

Jinsi yakujadili

  • Eleza mahali pa mkasa
  • Jinsi tukio lilivyotukia
  • Wakati
  • Msaada uliotoa
  • Maafa/hasara
  • Utafiti
  • Changamoto
  • Mkasa wa moto

Mada

  • KIFO KICHUNGU
  • JEHANAMU DUNIANI
  • NDIMI ZA JEHANAMU
  • MOTO WA KUTISHA
  • NDIMI ZA MANAYA/MAUTI
  • NARI YA KUTISHA

Msamiati

  • Ndimi za moto
  • Jiko lililolipuka laweza kuwa gesi, umeme , mbomba la mafuta.tangi la mafuta
  • Mavundo ya moshi yalifuka
  • Mashungi ya moto
  • Cheche za moto
  • Moto ulitatarika an kurindima
  • Upepo ulivuma kwa ghamidha na ghadhabu
  • Matagaa na mapogoo mabichi
  • Kujitoma ndani ya nyumba kama mwehu
  • Nahodha hodari haogopi mawimbi
  • Moto ulifakamia majengo kama nzige wavamiavyo shamaba la mihogo
  • Wengine walichomeka kiwango cha kutotambulikavilio vilinywewa na kuwapwetea
  • Nilifadhaika kwa fadhaa na wahaka
  • Kichwa kilinizunguka kama tiara
  • Vilio vya ving’ora vya makarandinga na ambulensi vilitanda na kuhinikiza hewa
  • Uma uliuputa moto na kuwaokoa manusura
  • Tulitoa huduma za kwanza
  • Wengi walisali/kufanya dua zisizoeleweka

Msamiati mwingine

  • Nilibaki kinywa wazi
  • Machozi ya majonzi yalinilengalenga
  • Machozi yalinienda njia mbilimbili
  • Lia kwikwikwi
  • Nilifikiri macho yangu yalikuwa yakinchezea shere
  • Choka hoi bin tiki
  • Fafanua kinaga ubaga
  • Pigwa na butwaa
  • Nilibung’aa na kuduwaa waa
  • Ponea chupuchupu

Ragba

  • Alipovunja ungo alianza kuwa na mienendo benibeni
  • Mambo yalimwendea upogo/tenge/msobemsobe
  • Alitokwa ma michirizi ya damu ______________ baada ya kupigwa kipopo/kitutu
  • Kijasho chembamba kilianza kumtoka
  • Aliondoka kichwa kifuani kama kondoo /shikwa na zabaiki ya uso, tayarini/haya/soni
  • Uzuri wake ulimteka bakunja akawa haoni hasikii
  • Akasahau penye urembo ndipo penye ulimbo
  • Aliyatemea mawaidha/nasaha mate
  • Alikuwa hayawani kwenye ngozi ya binadamu
  • Ama kweli _____________
  • Dekeza/engaenga kama yai
  • Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
  • Huruma zake ziligeuka kama umande
  • Alilia kilio cha kite na shaka bila kufahamu kuwa kilio si dawa
  • Alikuwa ndumakuwili kikulacho ki nguono mwako
  • Husuda/wivu zilimzidi hadi akakosa utulivu
  • Alivamiwa ghafla bin vuu

Methali

  • Maji hufuata mkondo
  • Bendera ikipepea sana huraruka
  • Mpiga ngumi ukuta huumia mwenyewe
  • Mpiga mbizi kwenye nchi kavuhuchunue usoni
  • Pwagu hupata pwaguzi
  • Mchimba kisima huingia mwenyewe
  • Vyote ving’aavyo si dhahabu
  • Vyote viowevu si maji
  • Njia ya mhini na mhiniwa ni moja

Takriri

  • Haambiliki hasemezeki
  • Hana hanani
  • Hazidishi hapunguzi
  • Hapiki hapakui
  • Jando wala togo
  • Vihusishi
  • Lahaula!
  • Yarabi!
  • masalaale!
  • Lo!
  • Lakwata!
  • Usaindizi
  • Walitupiga njeki
  • Niliwatupia upondo
  • Niliwapa mkono
  • Tulisaidiana kama kiko na dagali, maiti na jeneza

Tamati

  • Hakika, hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
  • Daima dawamu sitalisahau tukio hilo
  • Matukio hayo hayatafutika kutoka tafakirini mwangu
  • Ninapokumbuka kisa hicho, machozi hunitiririka njia mbilimbili

Hisia za Furaha

Furaha hutokana na

  • Sherehe – harusi
  • Mwakampya
  • Kuzaliwa kwa motto
  • Sikukuu ya krismasi
  • Sikukuu ya pasaka
  • Mahafali – sherehe za kufuzu
  • Siku ya tuzo/harambee
  • Kutembelewa na wageni
  • Sherehe za kitaifa
  • Sherehe za asili

Msamiati na mapambo

  • Maua ya kila ainati – si asmini, mawaridi
  • Ukumbi ulijaa na kuwatapika adinasi
  • Vipaza sauti vilihinikiza sauti
  • Vyakula vya kila aina/jamii vilitishia kuangusha meza
  • Msichana /kidosho/kipusa alitembea kwa madaha
  • Mkalimani na mfawidhi walishirikiana kama
  • Tulilakiwa kwa kupigwa pambaja
  • Waja walijaa si si si si
  • Waja waliwasili makundimakundi/mmoja mmoja/pacha pacha
  • Nikitembea aste aste hadi jukwaani
  • Kula/kushtaki njaa/fanyia mlo haki
  • Nilikumbuka nilivyojifunga kibwebwe/masombo
  • Kaka angeasi ukapera
  • Waja walisakata ruma/dansi
  • Msafara/mlolongo wa magari
  • Mrembo/spoti/sawa na hurulaini kutoka peponi
  • Wapambe walivalia sare za kupendeza
  • Kusakata rumba/dansi/kunengua viungo
  • Msafara/mlolongo wa magari
  • Mtibwiriko wa kukata na shoka
  • Sheheneza pongezi sufufu
  • Mkono wa tahania
  • Pofushwa na vimulimuli vya wapiga picha
  • Walijaa sisisi/pomoni
  • Hojiwa na sailiwa na wanahabari

Vipokezi vya methali

  • Yakini, ___________
  • Waama, _____________
  • Ama kweli ________________
  • Wahenga hawakukosea walipokili _______________

Methali

  • Chanda chema huvishwa pete
  • Baada ya dhiki faraja
  • Hauchi hauchi unakucha
  • Siku njema huonekana asubuhi
  • Mvumilivu hula mbivu
  • Safari ys kesho hupangwa leo
  • Msafiri ni aliye bandarini

Insha za Ndoto/Njozi/Ruya/Ruiya

Ni maono anayoyapata mtu akiwa usingiziniBarua/Waraka

Huketa hisia za furaha au huzuni

Mtu anaweza kupiga mayowe au kuweweseka kulinga na ndoto

Ndoto za huzuni zinaweza kuhusu

  • Kifo
  • Wizi
  • Moto
  • Mafuriko
  • Kutishwa na viumbe hatari

Wakati mwingine mhusika hutokwa na jasho, kutabawali au kujikuta mvunguni mwa kitanda

Ndoto ya furaha humfanya mhusika kujilaumu kuwa ilikuwa ni ndoto tu. Inaweza kuhusu

  • Mahafali
  • Kuwa tajiri
  • Kapasi mtihani
  • Kuzaliwa mahali kama ikulu

Mwandishi asianze kwa kusema kuwa alianza kuota

Mapambo

  • Baada ya kula chajio _____________
  • Nilikuwa nimechoka hoi bin tiki _______________
  • Niliubwaga mgogole wangu kwenye kitanda ____________
  • Nilijifunika gubigubi na kulala fo fo fo
    Hisia za furaha
  • Nilifurahi ghaya ya kufurahi
  • Furaha upeo wa furaha
  • Nilidamka wanguwangu na kushika hamsini zangu
  • Niliamka alfajiri ya Mungu/ya musa
  • Ukumbi ulijaa shangwe, nderemo na hoi hoi
  • Nilipaa na kuelea angani
  • Vicheko vilishika hatamu jari moja
    Hisia za huzunu – jinamizi
  • Maji yalikuwa yamenifika shingoni
  • Ulimi uliniganda kinywani
  • Moyo ulinipapa kama kwamba ulitaka ufunguliwe utoke
  • Nilishindwa kuongea ni kawa kama mja aluyepokonywa ulimi
  • Malaika alinisimamia tisti/wima/kititi
  • Mambo yaliniendea mpera mpera
  • Nilipiga usiahi/mayowe ambayo yangewafufua wafu
  • Zogo na zahama lilizuga
  • Nililia kwa kite na imani lakini hakuna aliyenihurumia
  • Niliduwaa na kubung’aa kama mzungu wa reli
  • Kilio cha kikweukweu kilihitimu kikawa cha mayowe

Barua/Waraka

Kuna aina mbili

  1. Barua ya kirafiki
  2. Barua rasmi

Barua ya Kirafiki/Kidugu

Huandikwa ili kupeana mwaliko, kujuliana hali, kufahamisha au kuarifu kuhusu jambo

BIDII FAULU,
S.L.P 93,
NAIVASHA.
18-11-2015

Kwa sahibu yangu, fundi msanifu ,
Utangulizi _______________
Mwili

Hatima
Ni mimi wako,
Jina lamwandishi

Sehemu muhimu za barua hii ni anwani ya mwandishi

  • Huandikwa pembeni kabisa wa kulia sehemu ya juu
  • Hujumuisha jina la mwandishi au anakosomea au kufanya kazi
  • Huwa pia na mahali anakoishi na sanduku la posta

Kianzio

  • Hudhihirisha anayeandikiwa
  • Hubainisha uhusiano wake na mwandishi
  • Kwa mpendwa
  • Kwa laazizi
  • Rafiki yangu
  • Kwa mwanangu mpendwa

Utangulizi

Haya ni maamkizi na kujuliana hali
Mfano

  • Pokea salamu sufufu/furifuri
  • Mimi ni buheri w afya/mzima kama

Mwili

  • Hubeba ujumbe au kusudio la barua
  • Lengo/nia/azma ya kukuandikia barua hii ni __________
  • Jina la
  • Ninaomba unitendee hisani/fadhila
  • Kwa kuwa wema hauozi
  • Ninakuhakikishia kuwa nitatia bidii
  • Ningependa kukujuvya kuwa
  • Tumia viunganishi ili kuunganisha mawazo
    • Isitoshe, zaidi ya hayo, aidha

Tamati

  • Ningependa kutia nanga kwa kukueleza
  • Ningependa kukunja jamvi
  • Kwa kuwa muda umenip kisogo
  • Ni mimi wako mpenzi,
  • Ni wako mpendwa,
  • Jina la mwandishi

Barua Rasmi

  • Huandikwa ili kuwasilisha ujumbe maalum
  • Huandikwa ili kuomba msamaha
  • Kuomba nafasi kwa kazi
  • Kuwasilisha malalamishi
  • Kuagizia/kuthibitisha mapokezi ya kampuni, shirika , idara

Sehemu

Anwani ya mwandishi

  • Huandikwa pembeni kabisa upande wa kulia sehemu ya juu ya karatasi
  • Hujumuisha jina la mwandishi, sanduku la posta, mahali anakoishi na tarehe baada ya anwani vuka mstari mmoja

Anwani ya mwandikiwa

  • Hutaja cheo cha anayeandikiwa
  • Taja jina la kampuni/shirika/dara
  • Taja S.L.P

Kianzio

  • Huanzia chini ya anwani ya mwandikiwa
    • Bwana/BW
    • Bibi/BI
    • Mabibi
    • Mabwana

Mtajo

  • Huelezea lengo la barua
  • Hutangulizwa kwa MINT: (mintirafu), KUH: (kuhusu), OMBI: , kumb: (kumbuka)
  • Pigia mstari ujumbe wenyewe

Mwili

Hubeba ujumbe wa barua

Maudhui hutegemea nia au lengo la barua

Lugha iwe rasmi

Msamiati

  • Nina furaha riboribo/kuu/firifuri
  • Nina bashasha belele
  • Ninasikitika ninapokuandika waraka huu ____________________
  • Ningependa kuchukua fursa/wasaa/nafasi
  • Kurejelea habari Fulani
  • Kwa mujibu w habari niliyoisoma/kutokana na taarifa/ kulingana na ______________
  • Shule.kampuni/shirika _____________ imesifika
  • Imetajwa na kutajika
  • Sifa zake zimeenea kote _______________ kamamoto nyikani kama wakati wa hari/kiangazi
  • Katika Nyanja za michezo ____________________ idara/shirika/shule yako
  • Wasifu/tawasifu _____________ mimi ni mwananchi kindakindaki/halisi
  • Nina nidhamu na taadhima ya hali ya ___________________
  • Nina talanta katika fani ya riadha uimbaji
  • Nina sauti ya ninga
  • Nitakuwa kielelzo dhabiti kwa
  • Nitatia bidii za mchwa ajengaye kichunguu
  • Nitavumilia/nitajikaza kisabuni ili kuafikia ndoto yangu
  • Vyeti vyangu vimeambatanishwa pamoja na waraka huu

Tamati

Ni mwisho wa barua
Huandikwa pembeni upande wa kulia sehemu ya chini
Herufi ya kwanza iwe kubwa

Insha ya Methali

Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiliwa na jamii na hutumiwa kufumbia jambo fulani

Methali hutahiniwa kwa namna tatu

Ikiwa kama mada

Mwanafunzi anafaa aeleze maana ya juu na ya ndani yake na matumizi yake iwapo anaifahamu vyema

Methali za Majuto, Maonyo na Tahadhari

  • Hutumiwa kuonyesha athari au madhara yanayotokea baada ya mtu kugaidi maagizo, nasaha au maonyo
  • Methali hutahiniwa kwa njia tatu
    Ikiwa mada
    Mwanzo – mwanafunzi huhitajika kuendeleza bila kufafanua maana ya methali
    Kimalizio – lazima kisa kishahibiane na methali ile.

    Tanbihi
    Ikiwa methali itakuwa mada, mtahiniwa atahitajika kueleza maana ya nje, ya ndani na matumizi endapo anafahamu

  • Hutumiwa kutoa funzo kwa wenginekutokana na dhiki na majuto yaliyomfika mhusika
    • Asiyefunzwa na mamaya hufunzwa na ulimwengu
    • Asiyeskia la mkuu huvunjika guu
    • Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe
    • Mbio za sakafuni huishia ukingoni
    • Mchuma janga hula na wa kwao
    • Ujanja wa nyani huishia jangwani
    • Majuto ni mjukuu huja kinyume
    • Mchimba kisima huingia mwenyewe
    • Msiba wa kujitakia hauna kilio
    • Kilio si dawa
    • Asiyeangalia huishi laiti ningalijua
    • Mkata pema pabaya panamwita
    • Sikio la kufa halisikii dawa
    • Haraka haraka haina baraka
  • Vipokezi vya methali
    Yawe yasiwe ____________
    Aisee! __________
    Labeka! _________________
    Lahaula! Lakwata ____________
    Chambilecho wenye ndimi walihenga ______________
    Hapo ndipo nilipoamini na kusadiki kuwa ______________
    Waledi wa lugha waligonga ndipo walipoganga kuwa _______________
    Wakale hawakupanda upepo wakavuna tufani _____________
  • Visa husika
    • Wizi
    • Utumizi wa dawa za kulevya
    • Kujiingiza katika anasa

Mapambo na msamiati

  • Kutofuata ushauri
    • Alikuwa hakanywi hakanyiki
    • Hasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini
    • Alikuwa haliki hatafunuki
    • Haambiliki hasenezeki
    • Alikuwa hajijui hajitambui
  • Kujuta
    • Aliishia na laiti kinywani
    • Alijiuma kidole/alilia chanda kili kinywani
    • Nilikabiliana ana kwa ana na ulimwengu usiokuwa na huruma
    • Niliyaona ya firauni
    • Nilikiona kilichomtoa kanga manyoya
  • Kupuuza
    • Alivalia miwani mashauri
    • Niliyatemea mate mawaidha
    • Alijitia hamnazo
    • Aliyatia kapuni yota aliyoambiwa
  • Mambo kuharibika
    • Mambo yalimwendea pete/tenge/mrisi/shoto/shambiro
    • Kutowezekana kwa
    • Ilikuwa sawa na kukama tetere
    • Kufunuka jua kwa ungo au chekeche
    • Kuchota maji kwa pakacha
  • Tashbihi
    • Pukutikwa na machozi kama ngamia
    • Tiririkwa na machozi kama maji mlimani
    • Mchafu kama kilihafu/fungo
    • Nuka kama mzoga/beberu/kindonda
  • Unafiki na kujitakia shida
    • Chui aliyevalia ngozi ya kondoo
    • Panya aliyeumia na kuvuvia
    • Kujipali makaa kama chachandu
    • Kuogelea katika bahari ya moto
    • Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiliwa na jamii kuwa wa kweli na unaotumia kufumbia
  • Ragba
    • Aliona cha mtema kuni
    • Kilichompata peku na lungo kilimpata
    • Mambo yalimwendea visivyo
    • Alitamani mauti yaje yamwokoe
    • Maji yalizidi ynga
    • Alitamani dunia ipasuke immeze mzima mzima
    • Kumwashia kipofu taa
    • Alitia masikio pamba
    • Machozi ya majonzi
    • Lia kilio cha kite na shaka
    • Machozi yalimtoka kapakapa
    • Pyorea mdomo
    • Huzunika ghaya ya kuhuzunika
    • Machozi yalinienda mbilimbili
    • Kuwa na kamusi ya matusi
  • Tashbihi
    • Pukutikwa na machozi ka,a ngamia
    • Tiririkwa na machozi kama maji mlimani
    • Bubunjikwa na machozi kama mfereji
    • Nuka kama mzoga
    • Mchafu kama fugo
  • Takriri
    • Hakiri hakubali
    • Hajali jando wala togo
    • Si wa uji si wa maji
    • Kutomjulia heri wala shari
    • Akiulizwa haungani

Methali za Kutohadaika na Uzuri wa Nje wa Kitu na Tamaa

Hutumiwa kuwaonya adinasi dhidi ya kudanganyika au kuhadaika na uzuri wa kitu bila kudadisi matokeo na athari zake.

Methali ikiwa kama kichwa huhitajika kuelezea maana ya nje, ya ndani na matumizi
Mfano wa visa

  • Kumkaribisha mtu nyumbani
  • Kupatiwa lifti
  • Biashara gushi
  • Urembo
  • Fisadi

Methali

  • Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
  • Hakuna kizuri kisichokuwa na dosari
  • Penye urembo ndipo penye ulimbo
  • Uzuri wa mkakasi, ukipata maji basi
  • Vyote ving’aavyo sio dhahabu
  • Tama ilimwua fisi
  • Uzuri si hoja hoja ni tabia
  • Mpanda farasi wawili hupasuka msamba
  • Mtaka yote hukosa yote
  • Mbio za sakafuni huishia ukingoni
  • Mla kwa wawili hana mwisho mwema
  • Penye uhondo pana uvundo
  • Uzuri wa biyu ndani mabuu
  • Usiache mbachao kwa msala upitao

Vipokezi vya methali

  • Kwa yakini ______________
  • Taib ___________
  • Ama kweli ______________
  • Kuntu _____________
  • Ni jahara kama pengo kuwa _____________
  • Ni wazi kama ju ala mtikati kuwa _____________
  • Chambilecho wahenga au wazee wenye tabasuri tepetepe _______________

Nahau

  • Maji kuzidi unga
  • Kitumbua kiliingia mchanga
  • Valia miwani
  • Meza mrututu
  • Meza mate machungu
  • Tulia huku ukitolea kule
  • Vimba kichwa
  • Kuwa na mkono mrefu
  • Bwaga zani

Takriri

  • Dhahiri shahiri
  • Haambiliki hasemezeki
  • Hakanywi hakanyiki
  • Kuwa kiguu na njia
  • Hana harusi hana matanga

Ragba

  • Walimdekeza mwana wao
  • Alikuwa ndumakuwili aliyeuma ndani yakini kikulacho ki nguoni
  • Alijaribu bahati kwani asiyekuwa na bahati habahatishi
  • Pigwa kipopo
  • Temea mate
  • Kumwonea gere
  • Mambo yalimwendea sambejambe
  • Alilia kilio cha kite

Tashbihi

  • Huzunika kama mfiwa
  • Kuwa na wasiwasi kama mwasi
  • Aminika kama njiwa
  • Jambo wazi kama mchana
  • Kuwa mzembe kama kupe

Insha ya Maelezo

Huitwa wasifu

Hutoa ufafanuzi kuhusu jambo, mtu, mahali au kitu fulani

Maelezo haya huwa ni sifa au hoja maalum

Insha hizi hutahadharisha, huelezea, huarifu na huburudisha

Mtahiniwa atangulize kwa ufafanuzi wa mada yake

Ahitimishe kwa kutoa changamotokwa waliohusika

Mtahiniwa asijadili chini ya hoja sita. Atoe hoja za ukweli

Mfano

  • Athari za ukimwi
  • Athari za dawa za kulevya
  • Faida na Athari za teknolojia
  • Mchezo niupendao
  • Haki za watoto
  • Faida ya elimu, miti na wanyamapori
  • Ukosefu wa usalama
  • Dawa za Kulevya

Haki na Ajira za Watoto

  • Haki ni mstahiki au ni jambo ambalo ni halali ya mtu
  • Mstahiki pia ni mtu mwenye haki ya kupata kitu
  • Ajira ni kazi zinazofanywa katika mashamba, viwanda, nyumbani na migodini
  • Watoto wanapopewa ajira ni kinyume cha sheria
  • Baadhi ya haki hizi ni
    • Lishe bora
      • Watoto wanafaa wapewe mlo ulio na viinilishe muhimu kwa protini, kabohaidrati, madini na maji safi.
      • Wasipolishwa huenda wakaathiriwa na magonjwa kama kwashakoo, utapiamlo.
    • Mavazi
      • Humkinga dhidi ya mabadiliko ya hali ya anga
      • Huzuia maradhi kama mafua, nimonia na pumu
        Methali
        Kinga ni bora kuliko tiba
    • Makao salama
      • Humsitiri dhidi ya wanyama hatari, maadui na mabadiliko katika hali ya anga
    • Kupata elimu
      • Asibaguliwe kwa misingi ya jinsia, kidini, kikabila au rangi ya ngozi
      • Wasichana wasiozwe mapema
      • Wasijiingize katika vitendo vya ukosefu na maadili kama ukahaba
      • Wafundishwe maadili na nidhamu
        Methali
        Elimu haitekeki
        Elimu ni bahari
        Elimu haina mwisho
    • Afya njema
      • Watoto wanafaa kukulia katika mazingira safi
      • Wapewe matibabu wanapougua
      • Wapewe lishe bora
        Methali
        Afya ni bora kuliko mali
        Kinga ni bora kuliko tiba
    • Wakingwe dhidi ya dhuluma
      • Hii ni kama kuchomwa na kukatakatwa mwilini
      • Waadhibiwe kwa kadiri na wastani
      • Wakuzwe vyema kwa maadili na mapenzi
        Methali
        Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
        Masukuzi ya leo ndio msitu wa kesho
    • Wasiajiriwe
      • Hii ni kinyume na sheria katika katiba ya nchi
      • Waajiri huwatesa na kuwanyanyasa watoto
      • Wengine huwarapua kwa mijeledi
      • Wengine huajiri kama vijakazi, watwana

Michezo

Ni jambo lifanywalo kwa ajili ya kujifurahisha kujichangamsha au kupoteza wakati

Baadhi ya michezo

  • Jugwe
  • Gugwi
  • Bembea
  • Kibe
  • Msabaka
  • Kandanda
  • Riadha
  • Sarakasi
  • Netiboli
  • Naga
  • Voliboli
  • Gololi
  • Hoki
  • Langalanga
  • Kriketi
  • Mpira wa wavu

Kandanda

Pia huitwa kambumbu, soka , gozi au mpira wa miguu

Hushirikisha timu mbili pinzani
Wachezaji huvalia

  • jezi
  • Daluga
  • Soksi
  • Bukta

Katikati  ya uwanja huitwa kitovu/senta
Otea – kujificha kwa makusudi ya kushambulia kwa ghafla
Penalty – adhabu kwa mlindalango
Mlindalango, mdakaji, golikipa
Kimia
Refa/refarii
Mshika bendera/kibendera
Mhimili/goli
Ngware – cheza visivyo
Kipindi cha lala salama ni kipindi cha nwishi
Kadi nyekundu huonyesha kutimuliwa kwa mchezaji
Kadi ya jano – onyo

Huwa na wachezaji kumi na mmoja katika kila upande

  • Walinzi au difensi
  • Wachezaji wa kati
  • Safu ya mashambulizi
  • Wachezaji wa akiba
  • Piga mkwanju
  • Kocha/mkufunzi

Mapambo

  • Uwanja ulijaa hadi pomoni
  • Wachezaji walishonona
  • Mdakaji aliudaka mpira ungedhani ni tumbili aliyedadia tawi la mti
  • Pasi fupifupi na za uhakika ungedhani walikuwa na mashine miguuni
  • Mpira haukulenga goli _______ kweli kulenga si kufuma
  • Kuutia mpira vifuani kana kwamba una spaki za kuunasa
  • Walinda ngome walikuwa imara kama chuma cha pua
  • Kwenda kubwaga moyo baada ya kipindi cha kwanza
  • Safu ya ilinzi ulikuwa imara kama ukuta uliotengenezwa kwa zege
  • Enda nyatunyatu na kufyatua zinga la kombora
  • Visha kanzu
  • Nyota ya jaha
  • Bao la kuta machozi
  • Piga kombora kimo cha mbuzi , kuku au ngamia
  • Mashabikiwalijawa na bashasha
  • Kipindi cha pili tukihisi kuwa na nishati mpya
  • Bao la bua liliweza kuzitubua nyoyo za wapinzani wetu
  • Mrisi bin kappa

Dawa za Kulevya

Hatua

Kufafanua maana

Ni kitu chochote kinachoathiri fahamu au mwili wa binadamu
Dawa hizi ni kama vile

  • Bangi
  • Sigara
  • Heroini
  • Miraa/mirungi
  • Pombe haramu

Anayeuza dawa hizi huitwa mlaguzi
Njia ya kutumia dawa hizi ni

  • Hunuswa
  • Hunywewa
  • Hudungwa
  • Hulambwa
  • Hutafunwa

Madhara ya dawa za kulevya

  • Kuvurugika kwa akili
  • Mja hugeuka kuwa zuzu, mkia wa mbuzi
  • Hupata ujasiri bandia
  • Hujiingiza katika visanga
  • Hudhuru afya
  • Hukonda na kukondeana kama ng’onda
  • Sura huambuliwa na kusawijika kama sokwe
  • Utovu wa nidhamu
  • Husheheni cheche za matusi
  • Kutabawali kadamnasi
  • Vaa mavazi vichungi na vioo
  • Kuzorota kwa uchumi
  • Kukosa elimu
  • Jamaa hukosa mavazi, makao na mlo
  • Humtilisha mtumiaja
  • Husababisha uraibu
  • Hushinda kutwa kucha wakitumia dawa hizo
  • Huwa kupe
  • Huwa maajenti wa mawakala
  • Chanzo cha maafa
  • Madereva hukosa kuwa waangalifu
  • Huleta shinikizo la damu mwilini
  • Ajali barasteni
  • Wizi wa mabavu
  • Kufanya mapenzi bila kinga

Tamati

  • Changamoto/nasaha
  • Wasiwe pweza kujipalia makaa
  • Kizazi cha baadaye kitaangamia
  • Kushirikiana kama kiko na digali kuangamiza janga hili
  • Wito kwa serikali – kuwasaka
  • Kufungua mashtaka

Mada

  • KIDIMBWI CHA MANAYA
  • NAULI YA AHERA
  • BARABARA YA KUZIMU
  • TARIKI YA MAUKO

Misemo

  • Kujipalia makaa
  • Bwaga zani
  • Meza mrututu
  • Tumbulia macho
  • Gofu la mtu

Takriri

  • Kufa kupona
  • Kwa hali na mali
  • Liwalo liwe
  • Balaa belua
  • Methali
  • Tahadhari kabla ya hatari
  • Mwiba wa kujidunga hauambiwi pole
  • Ajali haina kinga
  • Mchezea mavi humnukia
  • Nzi kufia juu ya kindonda si haramu
  • Masukuzi ya leo ndiyo msitu wa kesho
  • Wazee hukumbuka vijana hukumbushwa

Tashbihi

  • Konda kama ng’onda
  • Nyong’onyea kama muwele wa malaria
  • Dhaifu kama mkufu
  • Epuka ambao kama mgonjwa wa ukoma/ebola

Umuhimu wa Maji

Mwongozo ambao ni mwanzo wa insha kisha aendeleze
Mfano
“maji yana manufaa anuwai ___________ ”

  • Atoe hoja zisizopungua sita
  • Iwe na mtiririko mmoja
  • Sehemu ya hitimisho;atoe change moto kwa jamii au serikali

Mfano

UMUHIMU WA MAJi

Utangulizi

Maana ya maji
Maji ni kiowevu kisicho na rangi kinapatikana mtoni, ziwani, baharini na hata kutokana
na mvua
Maji ni uhai

Umuhimu wa maji

  • Kukonga roho au kukata kiu
    Adinasi hukonga roho
    Huweza kuishi bila shabuka au shida yoyote
    Husaidia usagaji wa chakula
    Mapishi ya vyakula
    Chakula hulainika na kuwa na ladha
    Huimarisha siha/udole wa binadamu
    Humweupusha mlimwengu na magonjwa
  • Usafi na unadhifu
    Kutakata mili ili kuepukana na magonjwa
    Kupiga deki
    Kusafisha mashine viwandani
    Kuwa mchafu kama fungo
    Kusafiri jongomeo baada ya kugua maradhi
  • Usafiri baharini, maziwani na mitoni
    Kusafirisha shehena za mizigo
    Mizigo mizito kama nanga
    Vyombo hivi vya usafiri ni meli, motaboti, ngalawa, merikebu, mashua, manahodha na maserahangi
  • Kuzungusha mitambo au mashine
    Hupata nguvu za umeme au nishati
    Nishati hizi huweza kutengeneza bidhaa za madini, vyakula na mavazi
  • Makao ya wanyama
    Kama samaki, kiboko, mamba, kamba na kasa
    Samaki ni chakula murua kwa mja na humzuia mja kuoata ndwele
  • Burudani na michezo
    Hamamu na mandibwi ya maji hutumika na wanamichezo kwa mashindano ya kuogelea
  • Huwa sehemu ya ajira
  • Huletea nchi pesa za kigeni
  • Kuondoa uchafu baada ya kazi
  • Maji ni asili ya uhai
  • Kuuzima moto
  • Kivutio cha watalii
  • Kunyunyizia mimea maji

Viunganishi

  • Mbali na _____________
  • Fauka ya ______________
  • Isitoshe _______________
  • Zaidi ya ______________
  • Hali kadhalika _______________

Hitimisho

  • Nikilikunja jamvi ninawashauri ________________
  • Hatuna la msalie mtume wala nabii ili kuyatumia maji ipasavyo __________________
  • Ama kweli maji ni kito cha dhamani ambacho kinafaa kulindwa kwa hali na mali

Methali

  • Maji yakimwagika hayazoleki
  • Maji ya kifuu ni bahari ya uchungu
  • Maji mapwa hayaogwi
  • Maji ni uhai
  • Maji hufuata mkondo
  • Maji ukiyavulie nguo yaoge

Hotuba

Hotuba ni maneno au malezo maalum yanayotokana na mtu mmoja mbele ya hadhira

Anayetoa hotuba huitwa hatibu

Hadhira ni watu wanaohutubiwa

Hotuba inaweza kuwa ya

  • Mwalimu mkuu juu ya wazazi
  • Mwanasiasa nyakati za kampeni
  • Maafisa wa serikali katika sherehe tofauti
  • Rais akihutubia taifa

Mambo ya kuzingatia

  • Kufuata itifaki
  • Kutambua waliohidhuria kufuata cheo/mamlaka na umri
    Mfano “mwalimu mkuu, naibu wa mwalimu mkuu, viranja na wanafunzi wenzangu hamjambo? ______
  • Wakati uliopo hutumika yaani usemi halisi
  • Nafsi ya kwanza na ya pili hutumika
    Mfano
    Nimesimama kadamnasi nikiwa mzima kama kigongo ________
  • Hutumia alama za kunukuuu ikiwa unahutubia kwa niaba ya mtu mwengine
    Mfano
    rais, naibu wa rais ______
  • Kila hoja husimuliwa katika aya yake
  • Hitimisho huhusu kuwashukuru wasikilizaji na pia kuwapa funzo au changa moto au nasaha

Umuhimu wa Elimu

Elimu ni mafunzo yanayopatikana shuleni na maishani
Hupevusha fikira
Mja hujielewa, huelewa wengine na ulimwengu
Huheshimiana
Huweza kutumia raslimali vilivyo
Elimu huondoa ujinga/ujuha
Mwanafunzi humakinika katika maisha ya baadaye
Msamiati

  • Leo si jana, jana si leo
  • Enda na ucheo, siende na uchwao

Elimu ya vitabu humsaidia mtu kuhifadhi siri ujumbe na kumbukumbu za kutumia na kizazi cha baadaye

Msamiati

  • Elimu huboresha maisha
  • Kujenga makao mazuri
  • Kuwasaidia jamaa na jamii
  • Elimu ni daraja la kuvusha mtu kwenye gange/kazi yenyefulusi nono
  • Mtu hupata hela za kujimudu pasi kuwategemea wengine
    Methali
  • Mtegemea cha nduguye hufa maskini
  • Mtegemea nundu haachi kunona
  • Mja hupewa heshima
    Ragba
  • Nimesimama imara kama chuma cha pua
  • Tisti kama ngarange za mvule
  • Kidete kama kitawi cha mkarakala
    Pongezi za dhati
  • Ninawapa mkono wa tahania kwa kufanya bidii za mchwa na duduvule
  • Nawamiminia shukrani sufufu
  • Ninawashukuru kwa kujitolea mhanga na kujifunga kibwebwe/masombo/kujikaza kisabuni

Methali

  • Elimu ni bahari
  • Elimu maisha si vitabu
  • Elimu ni taa gizani hung’aa
  • Elimu ni mali ambayo adui hawezi kuteka
  • Elimu bila mali ni kama nta bila asali

Tashbihi

  • Bidii za mchwa /duduvule
  • Ng’aa kama mbalamwezi
  • Pesa kama njugu
  • Julikana kama pesa

Misemo

  • Kujitolea mhanga
  • Shika usukani
  • Kuna kichwa
  • Ambua kitu
  • Tia pamba/nta

Mjadala

Insha sampuli hii huwa na sehemu mbili: Kuunga na kupinga
Mwanafunzi ana uhuru wa kuunga ama kupinga

Katika sehemu ya hitimisho mtahiniwa anatarajiwa kutoa mawazo yake

Tamati
Ningependa kuwajuza kuwa ______________
Ningeomba sote tupinge kwa jino na ukucha _____________
tusiwe kama chachandu wa kujipalia makaa kwa ______________

Teknolojia

Ni maarifa ya sayansi na matumizi yake katika mitambo, vyombo na zana katika viwanda, kilimo, ufundi na njia za mawasiliano
Mifano

  • Kilimo 
    Trekta   
    Beleshi   
    Pilau   
    Mbolea   
    Toroli   
  • Zana za vita   
    Manowari   
    Bazooka   
    Vifaru
    Darubini   
    Grunedi   
    Bunduki   
    Bastola
    Gomborora
    Nyambizi
    Mzinga
    Kombati
    Dirizi/dereya
  • Mawasiliano
    Simu – tamba/rununu/mkono
    Tarakilishi
    Tovuti
    Kitenzambali
    Barua meme
    Kikotoo
    Kimemeshi
  • Mitambo
    Kiyoyozi/feni/pauka/pangaboi
    Lifti/eleveta
    Kreni/winchi/kambarau
    Meli
    Ndege
    Mashua

Faida za Teknolojia

  • Mawasiliano – kupasha habari
  • Elimisha na kutumbuiza
    Methali
    Kipya kinyemi ngawa kindonda
  • Utafiti
    Kuvumbua dawa za ndwele/mitambo kurahihisha kazi
    Mitambo ya kuchunguza hali ya anga
  • Elimu
    Matumizi ya mitambo
    Kanda za video
    Methali
    Elimu ni bahari
    Elimu haitekeki
    Mali bila daftari hupotea bila habari
    Elimu bila mali ni kama sega bila asali
  • Usalama
    Zana za vita
    Donge nono hupatikana baada yakuuza vifaa
    Methali
    Tahadhari kabla ya hatari
    Kilimo na ufugaji
    Pembenjeo – mbegu, mbolea, dawa
    Ghala la kuhifadhi mazao
    Mashine za kukama ng’ombe
    Methali
    Tembe na tembe huwa mkate
  • Usafiri
    Vyombo vya majini, nchi kavu au barabara
    Kuokoa wakati na maisha
    Methali
    Ngoja ngoja huumiza matumbo
  • Mavazi
    Rahisisha kazi
    Kuimarisha uchumi wa nchi

Madhara

  • Mmomonyoko wa maadili
  • Huleta maradhi kama saratani
  • Huleta maafa
  • Punguza nafasi za kazi
  • Kuiga tabia za kigeni
  • Vita
  • Kuwafanya waja kulaza damu
  • Mambo mengine muhimu

Viunganishi vya insha ya maelezo

  • Licha ya
  • Fauka ya
  • Aidha
  • Zaidi ya
  • Pia isitishe
  • Mbali na
  • Hali kadhalika

Insha ya Mazungumzo

Mazungumzo ni maongezi, mahojiano ama malimbano baina ya mtu na mwengine au kundi moja na jengine
Yanaweza kuwa Porojo/soga/domo
Ni mazungumzo ya kupitisha wakati
Kutafuta ujumbe maalum
Hufanywa kwa njia ya mahojiano
Kudadisi au kumwelekeza mtu
Baina ya mtu na tajriba na Yule anayetakamsaada

  • Mhusika mmoja asichukue nafasi kubwa
  • Tumia alama za uakifishaji kama vile koloni, kitone na kipumuo
  • Sharti pawe na mahali pa kumchachawiza
  • Vitendo viweze kuandikwa katika alama za mabano
  • Fani za lugha zitumike ili kuleta uhondo
  • Pawe na maagano

Hatua

  • Mada/kichwa
    Huandikwa kwa herufi kubwa kupigiwa mstari
  • Maudhui
    Ni lengo au kusudi la mazungumzo
    Msamiati kutegemea lengo la mazungumzo
  • Vitendo na ishara
    Haya yataandikwa katika mabano (akitari, akilia, akicheka)
  • Alama za uakifishaji
    • Koloni( : ) Huandikwa baada ya jina au cheo cha watu
    • Alama za dukuduku ( _ _ _ ) Mazungumzo yanaendelea
    • Parandesi au mabano ( ) Kubana maneno ambayo hayatasemwa
    • Alama ya hisi ( ! ) Hutumiwa pamoja na viigizi kuonyesha hisia

Insha za Hadithi

Hadithi hutambiwa kwa njia ya kusimuliwa
Hurejelea matukio au visa vyenye nasaha kwa jamii
Visa hivi hutumiwa

  • Kuelimisha
  • Kushauri
  • Kuonya
  • Bidii
  • Kuonyesha umoja

Enzi za kale watoto walisimuliwa visa hivi na babu au nyanya wakati wa jiono
Mifano

  • Abunuwasi
  • Shamba la wanyama
  • Sungura mwenye pembe
  • Shujaa fumo liyongo

Ikiwa kisa kilisimuliwa na mwingine mwanafunzi atahitajika kunukuu kazi yake
Mfano
“ babu alizoea kutuambia ngano.alianza hivi ____________”

Baada ya kuhitimisha kisa mtahiniwa anahitajika kufunga
Ahitimishe kwa ushauri au nasaha

Insha hii yaweza kuchukua mikondo tofauti

  • Furaha
  • Majuto
  • Huzuni
  • Bidii

Tanbihi
Sanasana wahusika huwa wanyama ambao huwa na hisia za binadamu

Jinsi ya kuanzisha

  • Paukwa?pakawa!
  • Aliondokea chanjagaa kujenga nyumba kaka mwanangu mwana siti kijino kama chikichi cha kujengea vikuta na vilango vya kupitia
  • Hapo zama za zama _____________
  • Hapo kale ___________
  • Hapo jado aliondokea _____________
  • Enzi za konga mawe ______________
  • Miaka na dahari iliyopita ___________________
  • Katika karne za mababu na bibi zetu _____________________
  • Miaka na mikaka iliyopita _____________
  • Hadithi!hadithi! hapo zama za kale katika kaya/kijiji ______________

Fani za lugha

Takriri

  • Miaka na mikaka
  • Dhahiri shahiri
  • Hana hanani
  • Maskini hohehahe
  • Daima dawamu
  • Afriti kijiti

Misemo

  • Salimu amri
  • Shika sikio
  • Temea nasaha mate
  • Valia miwani
  • Tia kapuni
  • Mambo kuenda shoro
  • Kutojulia heri wala shari
  • Kuwa fremu ya mtu

Tashbihi

  • Roho ngumu kama paka
  • Zurura kama mbwa msokwao/mbwakoko
  • Tabia kunuka kama kindonda/beberu
  • Macho mekundu kama ngeu/damu
  • Kuchukua wekundu wa moto

Methali

  • Bendera hufuata upepo
  • Sikio la kufa halisikii dawa
  • Kutosikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini
  • Nzi kufia juu ya kindonda si haramu
  • Maji hufuata mkondo
  • Aambiwaye akakataa hujionea

Ragba

  • Kabla ya mwadhini kuadhana adhna zake
  • Maji kwa pakacha
  • Julikana kwa ufedhuli
  • Kuwa sawa na kutumbutia maji
  • Andamana na makundi yenye mienendo benibeni
  • Heshima likawa neno geni kwake
  • Lala kitandani hoi akiwangoja pumzi yake ya mwisho
  • Lia kilio cha mbwa

Hitimisho

  • Nyanya/babu alitueleza bayana umuhumu wa
  • Hapo ndipo niliposandiki kuwa
  • Ulumbi wa ulidhihirika waziwazi kuwa
Monday, 13 September 2021 08:46

Insha - Class 8 Kiswahili Revision Notes

Insha za Methali

Hutahiniwa kwa namna tatu
Mwanzo, mada na tamati au kijalizio
Iwapo ni mada,jadili au fafanua ikiwa una uwezo
Iwapo ni tamati, jalizia kwa maneno uliyopewa
Iwapo ni mwanzo, endeleza kisa moja kwa moja
Simulia kisa kinachooana na maudhui

Methali za wema, Usaidizi wa Rafiki na Udugu

  • Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
  • Heri jirani wa karibu kuliko ndugu wa mbali
  • Kwendako mema hurudi mema
  • Wema hauozi
  • Jaza ya ihsani ni ihsani
  • Kumpoa mwenzio sio kutupa
  • Wawili si mmoja
  • Damu ni mzito kuliko maji
  • Damu ni damu si kitarasa
  • Zimwi likujualo halikuli likakwisha

MsamiatI na Mapambo

  • Saidia na kama
  • Maiti na jeneza
  • Kiko na digali
  • Sahani na kawa
  • Kinu na mchi
  • Alinitilia upendo/alinipiga jeki
  • Hali mbaya ya mtu
  • Mchafu kama kilihafu/fungo/kisafu
  • Dovuo mdomoni/mashavuni
  • Ngecha menoni/matongo machoni
  • Hali ya umaskini/unyonge/ugonjwa
  • Si lolote si chochote
  • Masikini hohehahe
  • Si wa koleo si wa mani
  • Kwake hakufuki moshi
  • Si hayati si mamati/si hai si mahututi
  • Hawana be wala te
  • Nikawa gofu la mtu/kifefe/fremu ya mtu
  • Anachungulia kaburi

Miundo ya maumbo

  • Ilikuwa dhahiri shahiri kuwa angeenda jongomeo
  • Nilipiga moyo konde nikampiga jeki Kwa hali na mali
  • Alinitilia upendo kwani akufaaye Kwa dhiki ndiye rafiki
  • Nilikumbuka alivyonipakatana kuniasa
  • Nilikuwa sina be wala te baada ya wazazi kwenda jongomeo
  • Matumaini yangu yalifufuka pindi nilipokutana na _______________
  • Machozi yalimlengalenga na kumbubujika kama maji mferejini

Kupokea methali

  • Waambao waliamba _____________
  • Wahenga hawakutupa ulimi wa kulazia walipoanga ______________
  • Chambilecho wahenga ______________
  • Wahenga hawakutoa ngebe walipokuli ________________
  • Yakini, wema ____________________

Tamati

  • Ndipo iliponiwia bayana kuwa ______________
  • Ndipo walipofutika mtimani kwangu ukweli wa methali _______________
  • Sitalifuta tukio hilo katika kumbukumbu zangu
  • Tanbihi-mwalimu ana uhuru wa kuongeza mengine

Methali za Kutohadaika

Chanzo cha matatizo
Alipovunja ungo/baleghe
Alipovuka kizingiti cha lango la shule, chuo kikuu ___________ maisha yake yaliingia ufa
Alopowachagua marafiki vichwa maji/nyamafu _______________
Alianza kujipalia makaa kama chachandu pweza
Mambo yalianza kumwendea tenge/shote/shoro/mvange/msobe msobe/upogoupogo
Kufilisika – hana be wala te , hana kazi wala bazi/hana hanani, fukara fukarike
Kushikwa – kuhaha na kugwaya, kutweta na kuhema, pumzi juu juu
Alitamani dunia ipasuke na kummeza mzima mzima
Kamasi ilimtonatona puani kama matone ya mvua
Alinaswa/tiwa vituku/pingu/lishwa kalenda
Aibu – shikwa na haya/soni
Iva uso
Vunja uso
Kichwa kifuani kama kondoo
Teseka – alikula mumbi/mavi/kwata
Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
Kitumbua kiliingia mchanga
Alitekwa bakunja/pubazwa na
Urembo/fedha/sura/jamali

Vipokezi vya methali
Yakini ________________
Taibu __________________
Ama kweli __________________
Chambilecho wahenga ________________________
Wahenga na wahenguzi ______________________
Nakubaliana na wazee wa kale _______________________

Utekaji nyara

Mapambo
Uzuri wa siku/mtu – siku ilikucha vizuri/upepo mwanana
Umande ulimeremeta metumetu kama nyota angani
Ndege walikorokocha na kughani lahani nzuri
Nwele zake za nyufa., kiuno cha nyigu, meno ya mchele, pangika kama lulu
Sauti nyororo kama ya ninga/mwewe/kinanda/hurulaini wa peponi
Mwendo wa dalji/twiga wa savanna
Kutosikia nasaha
Juhudi zangu za kumwonya/kumnasihi ______________________
Ziligonga mwaba/paramia mwamba/ambulia pang’anda/tupwa kapuni
Udekezaji – alimwengaenga/alimlea kwa tunu na tamasha
Kumwasa motto kulikuwa jambo tukizi/nadra/dimu
Akawa haskii la mwadhini wala la mteka maji msikitini
Akatia maskio komango/nta/pamba
Kuwa sikio la kufa lisilosikia dawa/cha kuvunja ambacho hakina rubani

Methali Zinazoonya Kuhusu Tamaa na Uzuri wa Nje

Tamaa
Hamu kubwa ya kupata kitu, jambo, au hali Fulani
Visawe – uchu, ashiki, shauku, hamu, ari, nia, hanjamu, nyege, ukware, ghaidhi,
raghba

Methali za tamaa
Tamaa mbele mauti nyuma
Mkamia maji hayanywi, akiyanywa humsakama koo
Mwenye pupa hadiriki kula tamu
Mpanda farasi wawili hupasuka msaba/mwaranda
njia mbili zilimshinda fisi
Mwangata mbili moja humponyoka
Mchovya asli hachovyi mara moja
Mtaka yote huksa yote
Usiache mbachao kwa msala upitiapo

Methali za uzuri wa nje
Uzuri wa mkakasi ndanikipande cha mti
Sihadaike na rangi tamu ya chai ni sukari
Nyumba nzuri si mlango, ingia ndani
Kikulacho ki nguoni mwako
Ibilisi wa mtu ni mtu
Uzuri wa kuya ndani mabuu
Vyote viowevu si maji


Maudhui
Marafiki hadaa – ndumakuwili/mzandiki
Kutoaminiana katika ndoa
Ahadi za uongo – mchezo wa karata
Urembo ambao ni handaa

Insha ya Mjadala

Mjadala ni mazungumzo baina ya watu kuhusu mada au hoja kuu upande mmoja hupinga huku mwingine ukiunga mkono
Huhusu mazungumzo juu ya mada Fulani
Mfano:

  • Maisha ya mashambani ni bora kuliko y mjini
  • Teknolojia ina madhara mengi kuliko faida

Huhitaji mtahiniwa kuunga mkono hoja moja na kasha kuipinga katika aya inayofuata au kuunga mkono na baadaye kuzipinga hoja zake.
Kuna sehemu nne kuu

  • mada
  • utangulizi
  • mwili
  • tamati-kutoa kauli na ushauri

Mada huandikwa kwa herufi kubwa kulingana na swali
Utangulizi huhusu kufafanua mada na kutolea mifano
Mwili huhitaji kufafanuliwa kwa hoja
Kila hoja iwe katika aya yake
Hitimisho mtahiniwa huhitajikakutoa changamoto au ushauri

Kuna namna tatu za kuandika insha hii

  • kuunga na kupinga katika aya moja
  • kuunga mada mkono na baadaye kuipinga
  • kuipinga mada na baadaye kuiunga mkono

Usiandike chini ya hoja sita
Toa msimamo wako kwa mwandishi
Insha hizi hutumia viunganishi vya kuongezea

  • Licha ya
  • Aidha
  • Fauka ya
  • Zaidi ya
  • Pia

TEKNOLOJIA
Ni maarifa ya kisayansi yaliyowekwa katika matumizi ya vifaa, vyombo, mitambo na zana mbalimbali.
Teknolojia inaweza kutumika kwa njia ainati

  • Mawasiliano
  • Utafiti wa kisayansi
  • Usafi na afya ya mwili
  • Usafiri
  • Kilimo na ufugaji
  • Michezo na mashindano
  • Elimu
  • Biashara
  • Kutalii anga za juu

Mawasiliano

Vyombo vya mawasiliano kama tarakilishi, magazeti, simu

  • Hutupasha habari
  • Hutuepusha na maafa
  • Kuelimisha na kutumbuiza Kiingiacho mjini si haramu Kipya kinyemi kingawa kidonda

Utafiti

Wataalamu wamevumbua/wamegundua dawa za dwele
Mashine/mitambona vyombo vya kurahisisha kazi
Mitambo ya kuchunguza hali ya anga
Dawa za kuzuia mimba
Ukiona vyaelea vimeundwa

Elimu

Vyombo na vifaa vingi hutumiwa shuleni
Mitambo na vifaa vya utafiti
Matumizi ya mitandao
Kanda za video
Elimu ni bahari
Elimu haitekeki

Usalama

Zana za vita hutumiwa hutulinda dhidi ya maadui
Donge nono hupatikana baada ya kuuza vifaa
Nyua za umeme na ving’ora
Tahadhari kabla ya hatari

Kilimo na ufugaji

Pembejeo-mbegu, mbolea, dawa
Mashine za kulimia, kunyunyuzia maji
Mashine za kukama ng’ombe
Ukiona vyaelea vimeundwa
Tembe na tembe huwa mkate

Usafiri

Vyombo vya usafiri vya majini, angani na nchi kavu
Huenda kwa kasi ya umeme
Huokoa wakati
Ngoja ngoja huumiza matumbo

Madhara ya teknolojia

  • Huwafanya watu kuwa wazembe Chanzo cha mmomonyoko wa maadili
  • Hufundisha ulevi, ulanguzi wa dawa za kulevya
  • Hulemaza akili na fikira
  • Huchangia kutupilia mbali kwa tamaduni na desturi

Tamati

  • Ningependa kuwajuza kuwa ______________________
  • Ningeomba sote tupinge kwa jino na ukucha _______________________
  • Tusiwe kama chachandu kwa kujipalia makaa kwa ___________________________

Insha ya Masimulizi

Michezo

Michezo ni jumla ya shughuli za kujifurahisha, kujichangamsha,kujiburudisha au kupoteza wakati
Kuna michezo ainati kama vile

  • Kandanda
  • Mpira wa vikapu
  • Voliboli
  • Naga
  • Magongo
  • Riadha
  • Sarakasi/viroja

Riadha

Ni jumla ya michezo ya viungo vya mwili kama kukimbia, kuruka
Kuna mbio za masafa

  • Mafupi-mita 100, 200, 400
  • Kadiri-mita 800, 1500, 3000
  • Marefu-5000, 10,000, na mbio za nyika
  • Kuruka viunzi na maji
  • Kutupa tufe/kijisahani
  • Kubururana kwa kamba

Msamiati

  • Tufe
  • Mzingo
  • Nusu mzingo
  • Vijiti
  • Safu za kukimbilia
  • Wapasua hewa

Kandanda/kambumbu/soka /gozi/mpira wa miguu

  • Hushirikisha timu mbili
  • Mavazi ya wachezaji-jezi, kaptura, soksi
  • Viatu vya wachezaji-ndaruga, njumu
  • Uwanja wa michezo unaitwa uga/uchanjaa
  • Golikipa-mlinda lango/ mdakaji/mnyakati
  • Wachezaji wa ngome-walinzi/defense
  • Wachezaji wa kiungo
  • Kipindi cha lala salama/cha pili
  • Kadi ya manjano/nyekundu
  • Mshindi/mshinde
  • Mchuano/kinyang’anyiro/kindumbwendumbwe

Mapambo na maumbo

  • Uwanja/uga/uchanjaa ulijaa/ulifurika
  • Jiwe lisingeanguka ardhini
  • Shangwe, vifijo, vigelegele na nderemo vilihinikiza hewani
  • Ngome yao ilikuwa dhabiti mithili ya ukuta uliojengwa kwa zege
  • Wapasua hewa walihema na kutweta
  • Mithili ya mbwa aliyenusurika kumezwa na chatu
  • Kikorombwe cha mwisho kilipopulizwa
  • Alipiga zinga kimo
  • Cha mbuzi hadi ______________
  • Nilimvisha kanzu/kupiga tobwe
  • Mpira ulianza kwa kasi ya umeme
  • Mpira uludanadana wavuni

Methali

  • Hayawi hayawi huwa
  • Hauchi hauchi unakucha
  • Kutangulia si kufika
  • Subira huvuta heri

Mada

  • KINYANG’ANYIRO CHA KUKATA NA SHOKA
  • MECHI YA KUSISIMUA
  • KIPUTA CHA KIPEKEE
  • MECHI YA KUKUMBUKWA

Mikasa

Mikasa ni matukio au mambo ya kutisha yanayotokea kwa ghafal pasi ya kutarajiwa
Matukio haya yanaweza kuleta maafa, masaibu na majonzi
Mikasa hii inaweza kuwa ya moto, milipuko ya bomu, zilizala, mafuriko, ajali barabarani, mlipuko wa volkano na maporomoko ya ardhi
Yanayopaswa kuzingatiwa kwa masimulizi ni

  • Wakati wa mkasa
  • Mahali pa tukio
  • Jinsi tukio lilivyotokea
  • Kushiriki kwa msimulizi
  • Shughuli za uokozi

Msamiati na mapambo

Kelele-mayowe, kamsa, usiahi
Mlipuko-mfyatuko, mwatuko, mshindo, ngurumo
Vilio-shake, kusinana, kikweukweu, kwikwikwi, mayowr
Mochari-makafani, ufuoni,
Ving’ora vya ambulensi na makarandinga
Vifusi na majivu katika majengo
Manusura na majeruhi
Huduma ya dharura
Vukuto la moto
Helikopta za kijeshi na shirika la msalaba mwekundu
Mabehewa(mabogi) yalitapakaa
Gari liliyumba yumba/lilipiga danadana
Taharuki na hekaheka
Kuuputa moto kwa matagaa
Cheche za moto zilitanda kama fataki
Paparazi walizuka/walitokea ghafla bin vu kama mizuka
Upepo ulivuma kwa ghamidha na ghadhabu
Waja walipiga mbizi ili kujinusuru
Gari liligeuzwa likawa ganda tu
Ngeu ilitapakaa na kuzagaa kote
Mizigo ilfyatuka na kuwalenga wapiti njia
Ving’ora vilihinikiza/vilitanda/vilishamiri kote
Mavundevunde ya moshi yalitanda kote
Joto lilisambaa na kuzagaa
Vilikuwa vilio si vilio, majonzi si majonzi, zogo si zogo

Methali

  • Chelewa chelewa utampata mwana si wako
  • Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
  • Ngoja ngoja huumiza matumbo
  • Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo
  • Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
  • Juhudi si pato

Vihisishi vya majuto na mshangao

La haula la kwata !
Yarabi maskini!
Ole wangu!
Masaalale!
Lo!

Uasidizi

Walitupiga jeki
Niliwatilia upendo
Niliwapa mkono
Tulisaidiana kama kiko na digali
Maiti na jeneza
Kinu na mchi

Tamati
Hakika, hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
Daima dawamu sitalisahautukio hilo
Matukio hayo hayatafutika kutoka tafakulini mwangu
Ninapokumbuka kisa hicho, machozi hunitiririka njia mbilimbili

Huzuni

Insha humhitaji kuelezea kisa kinachoonyesha huzuni na woga

Insha nyingi huhusu mikasa au masaibu kwa watu
Visawe vya mikasa ni balaa, janga , balaa, baa, visanga
Mikasa yote hutokea kama ajali

  • Zilizala
  • Ajali barabarani au angani
  • Mlipuko wa bomu
  • Ukame
  • Maporomoko ya ardhi
  • Moto Ugaidi

Yanayozingatiwa mahali pa mkasa

  • Jinsi tukio lilivyotukia
  • Kushiriki kwako
  • Uchunguzi na matokeo

Tanbihi : mahali pa tukio – hotelini , mwituni, ofisini, kituo cha mafuta, kiwandani,
shuleni, dukakuu, barabarani, ufuoni mwa bahari, chumba cha maabara

Mapambo
Mlipuko – mfyatuko, mwatuko, mngurumo,
Ulikuwa mlipuko wa kuatua moyo/mtima, kushtua, kuogofya, kutisha
Ulikuwa mlipuko wa jiko la gesi/umeme/gari/bomba la mafuta
Kelele: usiahi, unyonge, kamsa, ukwezi, mayowe, ukwenje
Vilio vya –kusinasina, cha shake, kikweukweu kwikwikwi
Iwapo ni bomu, moto, ajali ya ndege
Moto ulirindima na kutatarisha majengo
Mabiwi/mashungi ya moto
Mavunde/mawingu ya moshi yalitanda kote
Vukuto la moto liliongezeka badala ya upepo kuvuma kwa hasira/ghamidha/hamaki/ghadhabu
Nilijitoma ndani ya nyumba kuwanusuru
Nahodha hodari haogopi moto
Kwa muda wa bana banua sehemu ile ikawa kama tanuri/joko/jehanamu
Jingo hilo liligeuzwa na kuwa majivu
Moto/nari ilifakamia majengo kama nzige wavamiavyo shamba la mihigo
Muda si muda, muda kiduchu, kutia na kutoa, fumbo fumbua,bana banua, kuku
kumeza
Punje paka kunawia mate, punda kunawia mavumbi,
Wengine walichomeka kiasi cha kutotambulika
Vilio vilinywea na sauti kuwapwelea
Tulipirikana na kupitana katika juhudi/hekaheka/pilikapilika za kuuputa moto
kuwaokoa wahasiriwa
Huzuni

Mikasa kwa jumla
Milio ya ving’ora vya makaradinga ya polisi, ambulensi, magari ya zima moto _____ tanda/tamalaki/tawala anga
Manusura/mahututi/majeruhi walipelekwa hospitalini/zahanatini
Walipewa hudum ya kwanza/ya dharura
Wafu walipelekwa mochari/ufuoni/makafari
Paparazi walizuka kama mizuka na kupeperusha picha sawia na matukio
Wanahabari walitangaza matukio ya mkasa redioni/runingani/magazetini
Wengine walisali/walipiga dua zisizoeleweka
Kwa nyota ya jaha/bahati ya mtende/kwa sudi wasamaria wema msalaba mwekundu wanajeshi zimamoto wakasaidia kuokoa
Basi lilipiga danadana na kuanguka bondeni ziwani/baharini
Tulifanya wanguwangu/himahima/chapu chapu/yosa yosa/ hala hala/mwendo wa arubili
Bila shaka tukio hilo halitafutika moyoni/sitalisahau daima dawamu
Niltamani ardi inimeze mzima mzima
Nilitamani kulia nikacheka nikalia
Machozi yaligoma

Methali
Ngoja ngoja huumiza matumbo
Chelewa chelewa utampata mwana si wako
Fimbo ya mbali haiui nyoka
Heri jirani wa karibu kuliko ndugu wa mbali
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo
Mja hakatai wito hukataa aitiwalo
Ajali haina kinga wala kafara
Tahadhari kabla ya hatari
Nahodha hodari haogopi moto

Furaha

Furaha inaweza kutokana na matukio mbalimbali kama vile

  • Sherehe –harusi
  • Siku ya kuzaliwa
  • Mahafali
  • Siku kuu ya krismasi
  • Kwenda ughaibuni
  • Matokeo mazuri ya mtihani

Mada
Siku ya siku
Akidi ya kufana
Sherehe ya kukata na shoka
Siku ya ndovu kumla mwanawe
Shamrashamra za
Msamiati na mapambo
Maua ya kila nui/ainati – asmini ,mawaridi afu, nangisi
Ukumbi wa mahema , jumba kubwa ,uwanja
Vipasa sauti/mikrofoni –vilihinikiza /sheheni
Muziki wa kuongoa ongoa ulitamalaki katika anga
Vyakula – mapochopocho/maakuli yaliyotishia kuangusha meza
Vinywaji vya kila jamii yalipenyeza kisirisiri
Mkalimani/mtarijumani alitafsiri haya yote
Kiume – mtanashati
Kike – mlibwede, spoti , mrembo kama mbega
Binti alikuwa mrembo mithili ya hurulaini aliyeasi/toka peponi
Alitembea kwa mwendo wa dalji/mwendo wa twiga wa savanna
Mwanaume mrefu njorinjori /mrefu kama unju/weusi kama kaniki
Udohoudoho , chipsi, bisi, kripsi
Waja walisakata rumba/dansi/tibwirika kwa miondoko
Msafara /mlolongo wa mashangingi
Walikula kiapo/yamini/vishana pete huku shangwe
Walipigana pambaja
Pofushwa na vimulimuli vya wapiga picha
Waja walijaa furifuri
Ilikuwa dhahiri shahiri kuwa ningefua dafu
Nilidamka wanguwangu kwa kuubwaga mgolole wangu na kuanza hamsini zangu
Kuche kusiche hatimaye kulikucha
Amka bukrata kichea
Niliamka asubuhi ya Mungu
Waja walisalimiana kwa furaha na farahani
Furaha sufufu ilinitinga si kidogo
Vyakula vya kunoga na kuhomolewa viliandaliwa na wapishi wajuzi
Vicheko vilipamba moto jari moja
Watu walichangamka na kukaramka kwa bashasha
Nilivalia meli zangu mpya zilizometameta kama mbalamwezi
Utamu wa malaji ungemfanya mtu kuramba viwiko vya mkono

Methali
Hauchi hauchi huwa
Hayawi hayawi huwa
Siku njema huonekana asubuhi
Baada ya dhiki, faraja
Mtu ni watu
Mgaagaa na upwa hali wali mkavu

Tashbihi
Shirikiana kama kinu na mchi, kiko na digali, soksi na kiatu
Lazima kama ibada
Kawaida kama sharia
Bidii kama mchwa ajengaye kichuguu/kishirazi/kidurusi
Bidii za msumeno ukerezao mbao
Bidii ni duduvule agatoye gogo la mti

Kumbukumbu

Kumbukumbu ni taarifa au rekodi zilizoandikwa na kuhifadhiwa
Anayeandika ni katibu au karani
Kiongozi wa mkutano huwa mwenyekiti au naibu wa mwenyekiti
Kumbukumbu ni maoni ya wote;hivyo basi katibu hafai kutoa hisia zake mwenyewe
Sehemu muhimu za kumbukumbu ni

  • Mada/kichwa
  • Mahudhurio
  • Ajenda za mikutano
  • Thibitisho

Mada/kichwa

  • Huwa na jina rasmi linalotambulisha shirika, kundi, kampuni
  • Huwa na tarehe, mahali na wakati(saa)
  • Kichwa kindikwe kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari
    Mfano
    KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA CHAMA CHA MAZINGIRA WA TAREHE 2 MEI 2010 KATIKA
    UKUMBI WA HOTELI YA MAJIMBO SAA MBILI ASUBUHI

Mahudhurio

  • Huonyesha majina ya waliohudhuria, waliokosa kuhudhuria na waliotuma udhuru(sababu) ya kutohudhuria
  • Huonyesha walioalikwa
  • Majina ya wanajopo/wanakamati/wanachama yafuate vyeo
  • Baadhi ya vyeo ni kama vile
    • Mwenyekiti au naibu mwenye kiti
    • Karani au naibu/katibu
    • Katibu mwandamizi/mratibu
    • Mhazini-anayetunza mali ya shirika au kampuni

Ajenda

  • Hizi ni hoja muhimu zinazojadiliwa k.v kufunguliwa kwa mkutano
  • Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia
  • Hoja nyinginezo zitategemea nia ya mkutano au shirika
  • Kufungwa kwa mkutano-taja anayeomba na wakati

Mapambo

  • Mkutano ulifahamishwa kwamba _______________
  • Ripoti ilitolewa kuwa ___________________
  • Mwenyekiti aliwaarifu/aliwajuza kuwa _____________________
  • Mkutano uliamua kwamba ___________________
  • Walipatana kwamba __________________
  • Kikao kilielezwa kuwa ____________________

Thibitisho
Sehemu hii huwa na sahihi na tarehe

Baada ya kumbukumbu kusomwa na kuthibitishwa katika mkutano unaofuata mwenyekiti na katibu hutia sahihi

Umbo la kumbukumbu

Mada:herufi kubwa
Waliohudhuria
_____________________
_____________________
_____________________

Waliotuma udhuru
_____________________
_____________________
_____________________

Wasiotuma udhuru
_____________________
_____________________

Waalikwa
_____________________
_____________________

Ajenda
_____________________
_____________________
_____________________

KUMB CCM1 1/02:

KUMB CCM 2 1/02:

Thibitisha
Mwenyekiti ________________________ (sahihi)
Tarehe ___________________________
Katibu ____________________________(sahihi)
Tarehe ___________________________

Insha ya Mazungumzo

Mazungumzo ni maongezi mahojiano au malumbano baina ya mtu na mwingine au kundi moja na jingine

Mazungumzo haya yanaweza kuwa
Poroja/soga/domo-ni mazungumzo ya kupitisha wakati
Kutafuta ujumbe maalum-hufanyika kwa njia ya mahojiano
Kumdadisi au kumwelekeza mtu-baina ya mtu aliye na tajriba na Yule anayetaka msaada

  • Kila mmoja hupewa nafasi ya kuzungumza
  • Mhusika mmoja asichukue nafasi kubwa
  • Tumia alama za uakifishaji ainati
  • Sharti pawe na hali ya kuchachawiza
  • Vitendo viweze kuandikwa katika alama za mabano
  • Fani za lugha zitumuke ili kuleta uhondo katika mazungumzo
  • Lazima pawe na maagano au maelewano
  • Tangaza msimamo iwapo ni mahojiano
  • Hatua

Mada/kichwa
Huandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa ,mstari
Mfano

MAZUNGUMZO BAINA YA DAKTARI NA MGONJWA
Maudhui-hili ni lengo au kusudi la mazungumzo
Msamiati utategemea lengo la mazungumzo
Vitendo na ishara-haya yataandikwa katika mabano mfano: (akiketi, akilia, wakibisha, akicheka)
Alama za uakifishaji
Koloni( : )huandikwa baada ya jina au cheo cha mtu
Alama za dukuduku ( -------------)kwamba mazungumzo yanaendelea
Parandesi au mabano ()
Kubana maneno ambayo hayatasemwa
Alama ya hisi ( ! ) hutumiwa pamoja na viingizi kuonyesha hisia
Mfano: yarabi maskini!

Insha ya Maelezo au Wasifu

Hii ni insha inayotoa maelezokuhusu jambo, mahali au kitu Fulani

  • Insha hii hueleza, huarifu, huburudisha au hutahadharisha
  • Mwandishi asiandike chini ya hoja sita
  • Tumia viunganishi unapounganisha mawazo katika aya au unapoaanza aya nyingine
  • Tiririsha mawazo ili pawena mtiririko na mshikamano
  • Katika tamati toa ushauri kwa makundi mbalimbali
  • Mwandishi anaweza kutoa msimamo wake kuhusu hoja Fulani

FAIDA ZA ELIMU

  • Elimu ni taaluma au mfuo wa mafunzo yanayofundishwa katika jamii zetu
  • Elimu inazo faida anuwai
  • Elimu huondoa ujinga akilini
  • Mja hupata maarifa, ujuzi na hekima
  • Mwanafunzi hutambua mambo tofauti
  • Humakinika katika mambo ayafanyayo
  • Elimu ni bahari na pia habari
  • Aliyeelimika huweza kuishi na wengine
  • Mtu hujiheshimu na kuheshimu wengine
  • Husaidia kudumisha amani, umoja na upendo baina ya watu
  • Kichango kuchangizana
  • Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
  • Ni daraja la kutuvusha katika umaskini
  • Waja hutia bidii za mchwa ili kufaulu maishani
  • Humwezesha mtu kuhitimu katika taaluma Fulani
  • Uhawinde hutokomea kama umande nyasini wakati wa jua la asubuhi
  • Hurahisisha mawasiliano Baina ya mtu mmoja na mwingine au baina ya mataifa
  • Hujifunza mengi kwani kuishi kwingi kuona mengi
  • Aliyesoma hutalii nchi nyingi
  • Kuhifadhi siri
    Elimu humwezesha mja kusoma uumbe kutoka katika barua au arafa akiwa pekee
  • Huchangia kuwepo kwa maendeleo
  • Serikali hujenga shule,vyuo na miundo msingi mingineyo ya elimu
  • Taasisi mbalimbali huboresha mitaala ya ufundishaji
  • Hufanikisha utafiti, utumiaji wa teknolpjia mpya na mitambo mbalimbali

Elimu ni irithi

Elimu ni mali ambayo haiteki
Ni almasi inayostahili kuchibwa na mtoto yeyote mwandilifu
Zamani watu waliridhi mashamba na mifugo
Elimu ni silaha na nguzo muhimu na madhubuti

Methali

Elimu ni bahari
Elimu ni taa, gizani huzagaa
Elimu ni ali ambayo adui hawezi kuiteka
Elimu maisha si vitabu

Viunganishi na mapambo

Isitoshe, elimu ni ,ali ambayo adui hawezi _____________________
Zaidi ya hayo, humwezesha mja kuhitimu _____________________
Hata hivyo, kuna wale wanaoitumia __________________________
Aidha, limu hurahisisha mawasilia ___________________________

Nahau

Tujifunge masombo/nira/kibwebwe ili ________________________
Tujikaze kisabuni _________________________
Tusiwe pweza wa kujipalia makaa kwa kutoelimika _________________________
Tujifunge masombo mithili ya _____________________ duduvule atoboaye gogo/mchwa ajengaye kichuguu

Tamati
Ningependa kukunja jamvi kwa ____________________________
Ninapofikia tamati
Jua linapoaga mikalatusi
Ninatia kitone nikitoa lulu kuwa

Barua Rasmi

Pia huitwa barua ya kiofisi
Huandikwa kuhusu jambo rasmi
Huandikwa ili

  • Kuomba nafasi ya kazi
  • Kuomba nafasi za masomo shuleni au chuoni
  • Maombi ya msaada kutoka kwa serikali
  • Kuomba msamaha au radhi
  • Malalamishi kuhusu jambo Fulani

Barua rasmi ina sehemu zufuatazo

  • Anwani
  • Anwani mbili – ya mwandishi na ya mwandikiwa
  • Anwani ya mwandishi huandikwa tarehe
  • Kianzio
    Sehemu hii huandikwa bwana (BW) au bibi (BI), Mkurugenzi mkuuu, mwalimu mkuu
    Mtajo
    Ni kichwa cha barua ambacho huashiria lengo au madhumuni kwa ufupi
    Kumbukumbu – KUMB
    Mintarafu – MINT
    Kusudi – KUS
    Kuhusu – KUH
    Yahusu – YAH
    Kichwa cha barua rasmi hupigiwa mstari
  • Mwili
    Huelezea zaidi kuhusu kusudi ya barua na lengo hasa kuandika barua
    Mtahiniwa huhitajika kuelezea kuhusu Elimu yake
    Wasifukwani haambatanishi stakabadhi zozote zile
    Tanbihi
    Insha yoyote ile lazima itimize ukurasa na nusu
  • Tamati/mwisho
    Humalizwa kwa
    Wako mwaminifu
    Sahihi
    Jina

Mtindo wa barua rasmi

SHULE YA MSINGI
YA LIZAR,
S.L.P 93,
NAIVASHA,
NOVEMBA 18, 2015.

MWALIMU MKUU,
SHULE YA UPILI YA ALLIANCE,
S.L.P 2003,
KIKUYU.
Kwa Bwana/Bi – kianzo

mtajo-MINT: NAFASI YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

mwili

hitimisho –
wako mwaminifu

Msamiati

Nina furaha kukuandikia __________________
Ninasikitika ninapokuandikia waraka _________________
Ningependa kuchukua fursa hii _____________
Kwa mujibu wa ilani ______________________ katika gazeti, runinga, mabango
Shule yako imetajwa na kutajika katika _________________ michezo, elimu, bidhaa bora
Shirika/kampuni imeipa kipaombela swala la _____________________
Nina nidhamu na taadhima ya hali ya juu
Vyeti vyangu pamoja na wasifu vimeambatanishwa na waraka
Nitakuwa kielelezo dhabiti kwa wenzangu
Nina talanta katika fani ya riadha _____________________
Ni matumaini yangu kuwa utaupokea waraka huu ________________________________

Barua Ya Kirafiki ama Kindugu

Huhusu kupatiana mwaliko, kujuliana hali, kufahamisha au kuarifu kuhusu jambo
Sehemu muhimu za barua hii ni

  • Anwani ya mwandishi
    Huandikwa pembeni kabisa upande wa kulia sehemu ya juu
    Huwa na jina la mwandishi , mahali anakoishi, sanduku laposta na tarehe
    Kianzio
    Hudhihirisha Yule anayeandikiwa
    Hubainisha uhusiano wake na mwandishi
    Mfano
    • Kwa mpendwa
    • Kwa mwanangu mpendwa
    • Kwa mpenzi wangu
    • Kwa sahibu/muhibu
  • Utangulizi
    Haya ni maamkizi kwa yule anayeandikiwa
    Mfano
    • Pokea salamu – sufufu, furifuri, tolatola nyingi kama nyota angani, mchanga
    • Mimi ni bugeri wa afya
    • Mzima kama chuma cha pua / ngarange za mvule
    • Nina buraha na furaha/furaha na bashasha
    • Nina imana kuwa Mola/Mkawini/Jalali
    • Nina matumaini kama tai kuwa u buheri wa afya/siha/zihi.rai
  • Methali
    • Ama kweli/yakini/waama
    • Waraka ni nusu ya kuonana
    • Afya ni bora kuliko mali
  • Mwili
    Sehemu – hii hubeba ujumbe wa mwandishi
    Wema – ninaomba unitendee fadhila/jamala
    Ninashukuru kwa wema ulionitendea
    Utiifu – ninakuhakikishia kwamba nitakuwa na utiifu, nidhamu na bidii
    Lengo au azma ya kukuandikia waraka huu ni
    Waraka huu ni kukujulisha kuwa
    Ningependa kukujuza kuwa
  • Tamati
    Ningependa kutia nanga kwa kukuelezea kuwa _______________
    Kwa kuwa wasaa umenitia kumbu/muda 
    Umenipa kisogo, ningependa kutia kitone
    Ninakunja jamvi kwa msemo usemao _______________________
    Kalamu yangu inalilia wino ____________________
    Ndimi mzazi wako ____________________
    Wako wa moyoni _____________________________
    ni wako mpendwa ______________________
    Ndimi mwana wako mpendwa

Sampuli
BIDII FAULU,
S.L.P 93,
NAIVASHA.

18-11-2015

Kwa sahibu yangu, fundi msanifu ,
Utangulizi ______________________________
Mwili
Hatima
Ni mimi wako,
Jina la mwandishi

Insha ya Hotuba

Hotuba ni maelezo yanayotolewa ili kupitisha ujumbe Fulani
Anayetoa hotuba huitwa katibu
Umati unaosikiliza huitwa hadhira
Huanza kwa mlahaka/salamu kwa kutambua vyeo kuanzia wa juu mpaka wa chini ,
sababu ya mkutano
Alama za kunukuu hutumiwa
Hotuba inaweza kuwa ya

  • Mwanafunzi akihutubia shuleni
  • Mwalimu
  • Mwalimu mkuu wa wazazi shuleni
  • Daktari au afisa wa afya
  • Rais wakati wa maadhimisho ya mashujaa
  • Waziri wa usala, afya na ugatuzi

Mfano wa utangulizi
“mgeni wa heshima, mkuu wa elimu gatuzini, mkaguzi wa elimu, mwenyekiti na
maafisa wa elimu na wanafunzi, hamjambo?
‘Mwalimu mkuu, naibu wa mwalimu mkuu, walimu wenzangu, viranja na wanafunzi,
sabalkheri?

Mapambo
ninazo bashasha/furaha/buraha
Nimesimama kidete/tisti/imara kama chuma
Cha pua/ngarange za mvule/kiini cha mpingo
Nitawandondolea hoja zangukuanzia utando hadi ukoko,shinani hadi kileleni
Rejelea hadhira mara kwa mara – nanyi, enyi wazazi, nasi wanafunzi

Tamati
Ningependa kutia kitone/nanga/kukunja jamvi kwa msemo usemao
Ninawamiminia shukrani tolatola/fokofoko
Kwa kutulia kama maji mtungini/maziwa kitomani
Kwa kuwa lililo na mwanzo halina budi kuwa na mwisho
Ninawatakia Baraka njema za Mualana/ninawatakia mbawazi za mkawini mbingu

Dawa za Kulevya

Ni kitu chochote kinachoathiri fahamu za mwili na afya ya mja
Mifano

  • Kokeini
  • Mandraksi
  • Bangi
  • Ganja
  • Miraa au mirungi
  • Tumbako

Athari za dawa za kulevya

  • Kuvuruga akili
  • Mtumiaji hugeuka na kuwa mkia wa mbuzi/juha/kalulu
  • Kupata ujasira bandia
  • Mja huwa katili
  • Hujiingiza katika visanga kama wizi
  • Hudhuru afya
  • Mhasiriwa kama ng’onda/kimbaumbau mwiko wa pilau
  • Sura huumbuka na kusawijika
  • Husababisha saratani
  • Kuenea kwa magonjwa ya zinaa

Methali
Kinga ni bora kuliko tiba
Tahadhari kabla ya hatari

utovu wa nidhamu
watumiaji husheheni matusi
hutabawali kadamnasi
kuvalia mavazi mafupi

Methali
mwacha mila ni mtumwa
usiache mbachao kwa msala upitao
kuzorota kwa uchumi
mtu binafsi hutumia njenje zote
watoto hawatimiziwi mahitaji
filisha mja- akabaki hana mbele wala nyuma
uchumi wa nchi huzorotabaada ya kutumia pesa kuwatibu wahasiriwa
husababisha uraibu
huleta wizi
husababisha uzembe
madereva kusababisha ajali
kupata magonjwa

Monday, 06 September 2021 08:14

Kiswahili - Class 6 End Term 1 Exam 2021 Set 1

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 1 hadi 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua lifaalo zaidi.

Ni _____1_____kadhaa _____2______ na mwalimu huyo. Alikuwa mwalimu _____3______ sana katika lugha ya Kiswahili. _____4______mwalimu huyo alikuwa na _____5_____moja. Alikuwa na hasira za _____6______. Jambo ______7______ tu ______8______ akasirike vilivyo. Sisi ______9______ tulimpenda na kumtamania lakini ______10______ alipopandwa na ______11______ tulikuwa ______12______ kwa woga. Katika hali kama hiyo, macho yake ya ______13______  yangebadilika rangi na kuwa ______14______. Daima dawamu sitamsahau mwalimu huyo aushini _______15______.

  1.  
    1. vitu
    2. mambo
    3. masaibu
    4. malalamiko
  2.  
    1. tulichofunzwa
    2. tulizofunzwa
    3. tuliofunzwa
    4. tuliyofunzwa
  3.  
    1. mstadi
    2. hatari
    3. mhodari
    4. stadi
  4.  
    1. Hata hivyo
    2. Na
    3. Kwa
    4. Ndiposa
  5.  
    1. jambo
    2. ila
    3. tatizo
    4. wahaka
  6.  
    1. fisi
    2. simba
    3. kihongwe
    4. mkizi
  7.  
    1. ndogo
    2. dogo
    3. lidogo
    4. mdogo
  8.  
    1. lingetume
    2. ingesababisha
    3. lingesababisha
    4. zingesababisha
  9.  
    1. sote
    2. zote
    3. wote
    4. nyote
  10.  
    1. nyakati
    2. wakati
    3. pindi
    4. saa
  11.  
    1. damu
    2. nyusi
    3. mori
    4. raha
  12.  
    1. tukifyata ulimi
    2. tukilia
    3. tukicheka
    4. tukicheza 
  13.  
    1. paa
    2. kikombe
    3. mamba
    4. ustadi
  14.  
    1. mekundu
    2. miekundu
    3. nyekundu
    4. kwekundu
  15.  
    1. kwangu
    2. zangu
    3. mwangu
    4. pangu

Kutoka swali la 16 hadi 30, jibu kulingana na maagizo

  1. Jibu maamkizi haya:
    Salaam aleikum ___________________________
    1. salaam aleikum
    2. binuru
    3. marahaba
    4. aleikum salaam
  2. Shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti huitwa:
    1. Tarbia
    2. Tathlitha
    3. Uwili
    4. Takhmisa
  3. Mtoto mdogo ameanguka vibaya. Kielezi katika sentensi hii ni:
    1. mtoto
    2. mdogo
    3. vibaya
    4. anguka
  4. Silabi za kati na za mwisho katika mishororo ya shairi huitwa,
    1. ubeti
    2. kibwagizo
    3. vina
    4. mizani
  5. Neno lipi haliko katika ngeli moja na mengine?
    1. Mwalimu
    2. Mlima
    3. Ndovu
    4. Daktari
  6. Mkoba wa kisu huitwa;
    1. podo
    2. upote
    3. ala
    4. ngao
  7. Kanusha sentensi ifuatayo:
    Muthungu amekuja shule leo.
    1. Muthungu hajaja shule leo
    2. Muthungu hajakuja shule leo
    3. Muthungu haji shule leo
    4. Muthungu hakuja shule leo
  8. Andika sudusi mbili kwa tarakimu:
    1. 3/5
    2. 3/6
    3. 2/5
    4. 2/6
  9. Malipo ya mtu aliyeshinda ni;
    1. faini
    2. karo
    3. mahari
    4. zawadi
  10. Tumia 'o-ote' katika sentensi hii;
    Maskani haya hayana manufaa ________________________
    1. zozote
    2. yoyote
    3. yeyote
    4. wowote
  11. Watu walipiga _____________ kumchagua mbunge wao.
    1. kura
    2. kula
    3. kalamu
    4. karo
  12. Anayetibu wagonjwa hospitalini huitwa:
    1. bawabu
    2. mhunzi
    3. tabibu 
    4. mwalimu
  13. Dada ya baba yako huitwa:
    1. shangazi
    2. halati
    3. mjomba
    4. shemeji
  14. Jaza jina la makundi.
    ________________ cha barua.
    1. Kikoa
    2. Doti
    3. Kipeto
    4. Kitosi
  15. Tegua Kitendawili
    "Nikitolewa majini hufa." Jibu ni:
    1. moyo
    2. yai 
    3. chura
    4. samaki

Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 31-40

Dawa ya kulevya ni chochote kinachoathiri hali ya kawaida ya mwili wa binadamu. Kuna aina mbalimbali za dawa za kulevya kama vile bangi, kokeini, heroini, madraksi na za nusu kaputi. Aidha, sigara pombe na gundi ni dawa za kulevya zinazouzwa na watu pasipo kufikiria madhara yake.

Pia kuna dawa zinazopendekezwa na daktari ili kupunguza maumivu au uchungu mwilini. Zinapotumiwa vibaya huleta uraibu unaoweza kuadhiri afya ya mtumiaji.

Watu tofauti hutumia dawa za kulevya kwa sababu zinazohitilafiana. Kuna wale wanaotaka kudadisi dawa hizi kwa kuiga mienendo ya marafiki zao na kukinaishwa na maisha. Wengine huzitumia kwa kuwa hawana shughuli za kufanya. Wameadhiriwa na vyombo vya mawasiliano hasa runinga na uozo wajamii.

Matumizi ya dawa hizi kwa muda mrefu husababisha uzoefu ambao ni vigumu kuukatiza. Hivyo basi huleta madhara mengi yasiyo na kifani. Miongoni mwa hayo ni kukosa makini kazini na masomoni. Aidha kichaa, saratani ya mapafu hasa kwa wavutao sigara, uhalifu ili kugharamia dawa hizi ghali na kudhoofisha uamuzi wa kiakili unaosababisha hasara kubwa.

Wakiwa katika hali hii ya kutojijua wala kujitambua, wengi huweza kujidunga kwa sindano chafu zinazoweza kusababisha maradhi mengi yakiwemo ukimwi. Hatima yao huwa ni kifo kwa wote wanaofuata njia hiyo.

Madhara haya yaweza kuepukika endapo sote tutawajibika kwa kukataa kuandamana na marafiki wabaya, wapotovu, kukataa kutumiwa na walanguzi wa dawa hizi na kutafuta uraibu unaofaa na kuheshimu miili yetu.

Mwito basi ni kushirikiana bega kwa bega ili kujaribu kuangamiza dawa za kulevya na biashara yake.

  1. Dawa za kulevya ni nini?
    1. Chochote kinachopendekezwa na daktari
    2. Chochote kinachoathiri hali ya binadamu
    3. Chochote kinachoathiri mwili wa binadamu
    4. Chochote kinachoathiri kawaida ya mwili.
  2. Mifano ya dawa za kulevya zinazouzwa na watu wengi ni:
    1. bangi, madraksi na chai
    2. kokeini, madraksi, na kahawa
    3. madraksi, chai ya mkandaa na bangi
    4. sigara, heroini, pombe na kokeini
  3. Ni kweli kusema, uzoefu wa mihadarati ni:
    1. vigumu kuukatiza
    2. vibaya kuukatiza
    3. rahisi kuukatiza
    4. vigumu kuupunguza
  4. Hatima ya wanaotumia dawa za kulevya ni ipi?
    1. Madhara
    2. Mauti
    3. Unusu kaputi
    4. Uhalisi
  5. Kisawe cha zinazohitilafiana ni:
    1. Zinazosikilizana
    2. Zinazolingana
    3. Zinazotofautiana
    4. Zinazoshahibiana
  6. Neno kukinaisha lina maana sawa na:
    1. kuwa na matumaini ya maisha
    2. kutosheka na maisha
    3. kufurahishwa na maisha
    4. kuchoshwa na maisha
  7. Matumizi ya mihadarati huleta uraibu unaoweza:
    1. kupunguza afya ya binadamu
    2. kudumisha afya ya binadamu
    3. kuboresha afya ya bianadamu
    4. kudunisha afya ya binadamu
  8. Ni maradhi yapi ambayo huwezi kupata kutokana na utumiaji wa mihadarati?
    1. Pumu
    2. Kichaa
    3. Saratani ya mapafiu
    4. Uraibu
  9. Ipi kati ya hizi si jinsi ya kuepukana na athari hizi?
    1. Kukataa kuandamana na marafiki wabaya
    2. Kukataa kutumwa na walanguzi wa dawa hizi
    3. Kutafuta uraibu unaofaa na kuheshimu miili yetu
    4. Kutumia na kulangua mihadarati
  10. Neno dawa liko katika ngeli gani?
    1. LI-YA
    2. U-ZI
    3. I-ZI
    4. KU-KU

Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 41-50.

Sote tulikuwa tumeketi chumbani ndugu alipojitoma ndani ghafla bin vuu, huku akihema kama aliyenusurika kumezwa na chatu. "Kulikoni? Mbona unahema kama mgonjwa wa pumu?" Nilisaili.

Alitueleza kuwa alipigwa kabari na wanyang'anyi wakamwibia kila kitu. Aliwaendea polisi kuwaambia yaliyojiri lakini badala ya kumsaidia walipora kichache kilichobaki. Tukashindwa kutofautisha wezi na polisi.

Yale maneno ya ndugu yangu yalinichochea kuwaza wajibu wa walinda usalama ni upi? Askari ndio wanaofaa kulinda raia na kuhifadhi haki za wananchi. Hata hivyo wao wamebadilika na kukiuka sheria zenyewe. Wanahujumu raia. Endapo yule aliyetunukiwa jukumu la kukulinda ndiye anayekuhasiri. je usalama wetu uko wapi?

Sio askari wote wanaodhulumu raia. Kuna kikosi cha askari kanzu au wapelelezi ambao wamejaribu kwa mapana na marefu kulinda jina la idara yao. Kuna visa vichache sana vya makachero wanaofanya uhalifu dhidi ya umma. Wapokee pongezi zetu kama wananchi.

Na wale askani wanaovaa mavazi rasmi tunawarai kuwa wasipokee rushwa barabarani, wasiwaibie raia, wasiwasaidie wezi wala wasitumie bunduki zao vibaya.

  1. Nani aliyeingia chumbani kwa kasi?
    1. Askari polisi
    2. Rafikiye mwandishi
    3. Kakake mwandishi
    4. Nduguye askari
  2. Alipigwa kabari na wezi ina maana:
    1. walimkimbiza mbio mbio
    2. walimsindikiza hadi nyumbani 
    3. walimkaba koo wakamwibia 
    4. waliomzomea mhusika
  3. Polisi walipopata habari za wizi huo:
    1. walimwibia mhusika 
    2. walianza kusaka wezi
    3. walimfukuza aliyeiba
    4. walifungua kesi kituoni
  4. Askari hawana jukumu la kulinda:
    1. wananchi
    2. waporaji
    3. umma
    4. raia
  5. Ina maana gani kuwa askari wamebadilika?
    1. wanachunga sheria
    2. hawakiuki sheria
    3. wanalinda sheria
    4. wanavunja sheria
  6. Ukihasiriwa na anayefaa kukulinda:
    1. huna matatizo
    2. huna usalama
    3. huna la kuogopa
    4. huna wasiwasi
  7. Kikosi gani kimetajwa kufanya kazi vizuri?
    1. Askari kanzu
    2. Askari polisi
    3. Askari jela
    4. Askari jeshi
  8. Hii ni fani gani ya lugha?
    Hema kama mgonjwa wa pumu?
    1. Takriri
    2. Methali
    3. Nahau
    4. Tashbihi
  9. Askari wanashauriwa:
    1. wapokee hongo barabarani
    2. wadhulumu raia
    3. wasitumie silaha zao ovyo ovyo
    4. wawasaidie wahalifu katika njama
  10. Kichwa kifaacho habari hii ni?
    1. Kudumisha usalama nchini
    2. Uhalifu wa askari wote
    3. Ndugu aliyevamiwa na kukabwa
    4. Usalama wa askari

INSHA

  • Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.
  • Andika insha ya kusisimua kuhusu;

                                                  ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

_____________________________________________________________________________________

Marking Scheme

  1. B
  2. D
  3. D
  4. A
  5. B
  6. D
  7. B
  8. C
  9. A
  10. C
  11. C
  12. A
  13. B
  14. A
  15. C
  16. D
  17. A
  18. C
  19. C
  20. B
  21. C
  22. A
  23. D
  24. D
  25. B
  26. A
  27. C
  28. A
  29. C
  30. D
  31. C
  32. D
  33. A
  34. A
  35. C
  36. B
  37. D
  38. D
  39. D
  40. C
  41. C
  42. C
  43. A
  44. B
  45. D
  46. B
  47. A
  48. D
  49. C
  50. A