- Insha ya Masimulizi
- Barua/Waraka
- Insha ya Methali
- Insha ya Maelezo
- Hotuba
- Mjadala
- Insha ya Mazungumzo
- Insha za Hadithi
Insha ya Masimulizi
Insha hii huwa na hisi mbili: furaha na huzuni
Vinaweza visa vya kubuni au halisi
Mtahiniwa aweza kutahiniwa mara tatu
Mwanzo wa handithi – dokezo
Huhitajika aendeleze
Kimalizio/tamati
Mtahiniwa lazima aane insha na atamatishe kwa kutumia kimalizio hicho
Huzuni au Tanzia
Visawe vya huzuni ni masikitiko, majonzi, jitimai, buka, chonda na msiba
Hivi ni visa vinanyoleta majonzi, huzuni, simanzi, sikitiko au jitimai
- Mikondo
- Ujambazi/unyang’anyi/uporaji/wizi
- Utekajinyara
- Ujangili
- Wizi wa mifugo
- Ulaghai
- Magendo
- Ugomvi wa kijamii
- Uvamizi na watu katili
- Migomo
Misamiati na mapambo
- Mayowe – ukemi, usiahi, mayowe
- Wasiwasi- jekejeke, jakamoyo, kiherehere
- Kufa – kata kamba, enda ahera, jongomeo
- Hasira – pandwa na mori, kuwa na tumbo joto, kama zaibaki kwenye kipimajoto
- Nilinyapianyapia/nilinyatianyatia nyatunyatu
- Joho la kiwewe lilinivaa
- Nilichana mbuga/nilitifua vumbi ili kuyaokoa maish -
- Moyo ulinidwikadwika/ulinipapa kama ngoma za mahepe
- Malaika yalinisimama wima
- Tulisikia sauti zilizotweta kama
- Sikuyaamini macho nilipoona
- Nilipiga usiahi ambao ungewafufua wafu
- Ulimi uliniganda kinywani
- Nililia kwa kite na imani lakini kilio si dawa
- Nilitoka shoti kama
- Ngeu ilimtiririka kama
- Milio ya risasi ilitamalaki kwenye anga
- Parafujo za miguu ziliregea
- Macho yalinitoka pima kama
- Nilitetemeka kama unyasi nyikanu
- Kijasho chembamba kikaanza kunitoka
Methali
- Mbwa hafi maji akiona ukoko
- Damu ni nzito kuliko maji
- Tama mbele mauti nyuma
- Unjanja wa nyani huishia jagwani
- Siku za mwizi ni arubaini
- Pwagu hupata pwaguzi
Ragba
- Juhudi ziligonga mwaba
- Maisha yalianza kuingia ufa
- Jaribu kwa udi na uvumba
- Sijui alipandwa na pepo gani
- Mambo yalimwendea tege/upogo upogo
- Alitoka na michirizi ya damu
- Alipigwa kitutu/kipopo
Dekeza
- Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
- Huruma zake ziligeuka kama umande
- Alilia kilio cha kite na shake bila kufahamu kilio si dawa
- Alivamiwa vaa bin vu
Takriri
- Haambiliki hasemezeki
- Hana hanani
- Hazindishi hapunguzi
- Hapiki hapakui
- Jando wala togo
Insha ya Mikasa
Mikasa ni matukio yaletayo maafa, masaibu na matatizo kwa watu
Visawe
- Msiba
- Balaa
- Zani
- Baa
- Maafa
- Janga
- Belua
Mifano ya mikasa
- Moto
- Wizi
- Ajali barabarani
- Ugaidi
- Ubakaji
- Utekaji nyara
- Zilizala
- Kuza maji
- Maporomoko ya ardhi
- Mlipuko wa bomu
- Ukame
- Kabobo
Jinsi yakujadili
- Eleza mahali pa mkasa
- Jinsi tukio lilivyotukia
- Wakati
- Msaada uliotoa
- Maafa/hasara
- Utafiti
- Changamoto
- Mkasa wa moto
Mada
- KIFO KICHUNGU
- JEHANAMU DUNIANI
- NDIMI ZA JEHANAMU
- MOTO WA KUTISHA
- NDIMI ZA MANAYA/MAUTI
- NARI YA KUTISHA
Msamiati
- Ndimi za moto
- Jiko lililolipuka laweza kuwa gesi, umeme , mbomba la mafuta.tangi la mafuta
- Mavundo ya moshi yalifuka
- Mashungi ya moto
- Cheche za moto
- Moto ulitatarika an kurindima
- Upepo ulivuma kwa ghamidha na ghadhabu
- Matagaa na mapogoo mabichi
- Kujitoma ndani ya nyumba kama mwehu
- Nahodha hodari haogopi mawimbi
- Moto ulifakamia majengo kama nzige wavamiavyo shamaba la mihogo
- Wengine walichomeka kiwango cha kutotambulikavilio vilinywewa na kuwapwetea
- Nilifadhaika kwa fadhaa na wahaka
- Kichwa kilinizunguka kama tiara
- Vilio vya ving’ora vya makarandinga na ambulensi vilitanda na kuhinikiza hewa
- Uma uliuputa moto na kuwaokoa manusura
- Tulitoa huduma za kwanza
- Wengi walisali/kufanya dua zisizoeleweka
Msamiati mwingine
- Nilibaki kinywa wazi
- Machozi ya majonzi yalinilengalenga
- Machozi yalinienda njia mbilimbili
- Lia kwikwikwi
- Nilifikiri macho yangu yalikuwa yakinchezea shere
- Choka hoi bin tiki
- Fafanua kinaga ubaga
- Pigwa na butwaa
- Nilibung’aa na kuduwaa waa
- Ponea chupuchupu
Ragba
- Alipovunja ungo alianza kuwa na mienendo benibeni
- Mambo yalimwendea upogo/tenge/msobemsobe
- Alitokwa ma michirizi ya damu ______________ baada ya kupigwa kipopo/kitutu
- Kijasho chembamba kilianza kumtoka
- Aliondoka kichwa kifuani kama kondoo /shikwa na zabaiki ya uso, tayarini/haya/soni
- Uzuri wake ulimteka bakunja akawa haoni hasikii
- Akasahau penye urembo ndipo penye ulimbo
- Aliyatemea mawaidha/nasaha mate
- Alikuwa hayawani kwenye ngozi ya binadamu
- Ama kweli _____________
- Dekeza/engaenga kama yai
- Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
- Huruma zake ziligeuka kama umande
- Alilia kilio cha kite na shaka bila kufahamu kuwa kilio si dawa
- Alikuwa ndumakuwili kikulacho ki nguono mwako
- Husuda/wivu zilimzidi hadi akakosa utulivu
- Alivamiwa ghafla bin vuu
Methali
- Maji hufuata mkondo
- Bendera ikipepea sana huraruka
- Mpiga ngumi ukuta huumia mwenyewe
- Mpiga mbizi kwenye nchi kavuhuchunue usoni
- Pwagu hupata pwaguzi
- Mchimba kisima huingia mwenyewe
- Vyote ving’aavyo si dhahabu
- Vyote viowevu si maji
- Njia ya mhini na mhiniwa ni moja
Takriri
- Haambiliki hasemezeki
- Hana hanani
- Hazidishi hapunguzi
- Hapiki hapakui
- Jando wala togo
- Vihusishi
- Lahaula!
- Yarabi!
- masalaale!
- Lo!
- Lakwata!
- Usaindizi
- Walitupiga njeki
- Niliwatupia upondo
- Niliwapa mkono
- Tulisaidiana kama kiko na dagali, maiti na jeneza
Tamati
- Hakika, hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
- Daima dawamu sitalisahau tukio hilo
- Matukio hayo hayatafutika kutoka tafakirini mwangu
- Ninapokumbuka kisa hicho, machozi hunitiririka njia mbilimbili
Hisia za Furaha
Furaha hutokana na
- Sherehe – harusi
- Mwakampya
- Kuzaliwa kwa motto
- Sikukuu ya krismasi
- Sikukuu ya pasaka
- Mahafali – sherehe za kufuzu
- Siku ya tuzo/harambee
- Kutembelewa na wageni
- Sherehe za kitaifa
- Sherehe za asili
Msamiati na mapambo
- Maua ya kila ainati – si asmini, mawaridi
- Ukumbi ulijaa na kuwatapika adinasi
- Vipaza sauti vilihinikiza sauti
- Vyakula vya kila aina/jamii vilitishia kuangusha meza
- Msichana /kidosho/kipusa alitembea kwa madaha
- Mkalimani na mfawidhi walishirikiana kama
- Tulilakiwa kwa kupigwa pambaja
- Waja walijaa si si si si
- Waja waliwasili makundimakundi/mmoja mmoja/pacha pacha
- Nikitembea aste aste hadi jukwaani
- Kula/kushtaki njaa/fanyia mlo haki
- Nilikumbuka nilivyojifunga kibwebwe/masombo
- Kaka angeasi ukapera
- Waja walisakata ruma/dansi
- Msafara/mlolongo wa magari
- Mrembo/spoti/sawa na hurulaini kutoka peponi
- Wapambe walivalia sare za kupendeza
- Kusakata rumba/dansi/kunengua viungo
- Msafara/mlolongo wa magari
- Mtibwiriko wa kukata na shoka
- Sheheneza pongezi sufufu
- Mkono wa tahania
- Pofushwa na vimulimuli vya wapiga picha
- Walijaa sisisi/pomoni
- Hojiwa na sailiwa na wanahabari
Vipokezi vya methali
- Yakini, ___________
- Waama, _____________
- Ama kweli ________________
- Wahenga hawakukosea walipokili _______________
Methali
- Chanda chema huvishwa pete
- Baada ya dhiki faraja
- Hauchi hauchi unakucha
- Siku njema huonekana asubuhi
- Mvumilivu hula mbivu
- Safari ys kesho hupangwa leo
- Msafiri ni aliye bandarini
Insha za Ndoto/Njozi/Ruya/Ruiya
Ni maono anayoyapata mtu akiwa usingiziniBarua/Waraka
Huketa hisia za furaha au huzuni
Mtu anaweza kupiga mayowe au kuweweseka kulinga na ndoto
Ndoto za huzuni zinaweza kuhusu
- Kifo
- Wizi
- Moto
- Mafuriko
- Kutishwa na viumbe hatari
Wakati mwingine mhusika hutokwa na jasho, kutabawali au kujikuta mvunguni mwa kitanda
Ndoto ya furaha humfanya mhusika kujilaumu kuwa ilikuwa ni ndoto tu. Inaweza kuhusu
- Mahafali
- Kuwa tajiri
- Kapasi mtihani
- Kuzaliwa mahali kama ikulu
Mwandishi asianze kwa kusema kuwa alianza kuota
Mapambo
- Baada ya kula chajio _____________
- Nilikuwa nimechoka hoi bin tiki _______________
- Niliubwaga mgogole wangu kwenye kitanda ____________
- Nilijifunika gubigubi na kulala fo fo fo
Hisia za furaha - Nilifurahi ghaya ya kufurahi
- Furaha upeo wa furaha
- Nilidamka wanguwangu na kushika hamsini zangu
- Niliamka alfajiri ya Mungu/ya musa
- Ukumbi ulijaa shangwe, nderemo na hoi hoi
- Nilipaa na kuelea angani
- Vicheko vilishika hatamu jari moja
Hisia za huzunu – jinamizi - Maji yalikuwa yamenifika shingoni
- Ulimi uliniganda kinywani
- Moyo ulinipapa kama kwamba ulitaka ufunguliwe utoke
- Nilishindwa kuongea ni kawa kama mja aluyepokonywa ulimi
- Malaika alinisimamia tisti/wima/kititi
- Mambo yaliniendea mpera mpera
- Nilipiga usiahi/mayowe ambayo yangewafufua wafu
- Zogo na zahama lilizuga
- Nililia kwa kite na imani lakini hakuna aliyenihurumia
- Niliduwaa na kubung’aa kama mzungu wa reli
- Kilio cha kikweukweu kilihitimu kikawa cha mayowe
Barua/Waraka
Kuna aina mbili
- Barua ya kirafiki
- Barua rasmi
Barua ya Kirafiki/Kidugu
Huandikwa ili kupeana mwaliko, kujuliana hali, kufahamisha au kuarifu kuhusu jambo
BIDII FAULU,
S.L.P 93,
NAIVASHA.
18-11-2015
Kwa sahibu yangu, fundi msanifu ,
Utangulizi _______________
Mwili
Hatima
Ni mimi wako,
Jina lamwandishi
Sehemu muhimu za barua hii ni anwani ya mwandishi
- Huandikwa pembeni kabisa wa kulia sehemu ya juu
- Hujumuisha jina la mwandishi au anakosomea au kufanya kazi
- Huwa pia na mahali anakoishi na sanduku la posta
Kianzio
- Hudhihirisha anayeandikiwa
- Hubainisha uhusiano wake na mwandishi
- Kwa mpendwa
- Kwa laazizi
- Rafiki yangu
- Kwa mwanangu mpendwa
Utangulizi
Haya ni maamkizi na kujuliana hali
Mfano
- Pokea salamu sufufu/furifuri
- Mimi ni buheri w afya/mzima kama
Mwili
- Hubeba ujumbe au kusudio la barua
- Lengo/nia/azma ya kukuandikia barua hii ni __________
- Jina la
- Ninaomba unitendee hisani/fadhila
- Kwa kuwa wema hauozi
- Ninakuhakikishia kuwa nitatia bidii
- Ningependa kukujuvya kuwa
- Tumia viunganishi ili kuunganisha mawazo
- Isitoshe, zaidi ya hayo, aidha
Tamati
- Ningependa kutia nanga kwa kukueleza
- Ningependa kukunja jamvi
- Kwa kuwa muda umenip kisogo
- Ni mimi wako mpenzi,
- Ni wako mpendwa,
- Jina la mwandishi
Barua Rasmi
- Huandikwa ili kuwasilisha ujumbe maalum
- Huandikwa ili kuomba msamaha
- Kuomba nafasi kwa kazi
- Kuwasilisha malalamishi
- Kuagizia/kuthibitisha mapokezi ya kampuni, shirika , idara
Sehemu
Anwani ya mwandishi
- Huandikwa pembeni kabisa upande wa kulia sehemu ya juu ya karatasi
- Hujumuisha jina la mwandishi, sanduku la posta, mahali anakoishi na tarehe baada ya anwani vuka mstari mmoja
Anwani ya mwandikiwa
- Hutaja cheo cha anayeandikiwa
- Taja jina la kampuni/shirika/dara
- Taja S.L.P
Kianzio
- Huanzia chini ya anwani ya mwandikiwa
- Bwana/BW
- Bibi/BI
- Mabibi
- Mabwana
Mtajo
- Huelezea lengo la barua
- Hutangulizwa kwa MINT: (mintirafu), KUH: (kuhusu), OMBI: , kumb: (kumbuka)
- Pigia mstari ujumbe wenyewe
Mwili
Hubeba ujumbe wa barua
Maudhui hutegemea nia au lengo la barua
Lugha iwe rasmi
Msamiati
- Nina furaha riboribo/kuu/firifuri
- Nina bashasha belele
- Ninasikitika ninapokuandika waraka huu ____________________
- Ningependa kuchukua fursa/wasaa/nafasi
- Kurejelea habari Fulani
- Kwa mujibu w habari niliyoisoma/kutokana na taarifa/ kulingana na ______________
- Shule.kampuni/shirika _____________ imesifika
- Imetajwa na kutajika
- Sifa zake zimeenea kote _______________ kamamoto nyikani kama wakati wa hari/kiangazi
- Katika Nyanja za michezo ____________________ idara/shirika/shule yako
- Wasifu/tawasifu _____________ mimi ni mwananchi kindakindaki/halisi
- Nina nidhamu na taadhima ya hali ya ___________________
- Nina talanta katika fani ya riadha uimbaji
- Nina sauti ya ninga
- Nitakuwa kielelzo dhabiti kwa
- Nitatia bidii za mchwa ajengaye kichunguu
- Nitavumilia/nitajikaza kisabuni ili kuafikia ndoto yangu
- Vyeti vyangu vimeambatanishwa pamoja na waraka huu
Tamati
Ni mwisho wa barua
Huandikwa pembeni upande wa kulia sehemu ya chini
Herufi ya kwanza iwe kubwa
Insha ya Methali
Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiliwa na jamii na hutumiwa kufumbia jambo fulani
Methali hutahiniwa kwa namna tatu
Ikiwa kama mada
Mwanafunzi anafaa aeleze maana ya juu na ya ndani yake na matumizi yake iwapo anaifahamu vyema
Methali za Majuto, Maonyo na Tahadhari
- Hutumiwa kuonyesha athari au madhara yanayotokea baada ya mtu kugaidi maagizo, nasaha au maonyo
-
Methali hutahiniwa kwa njia tatu
Ikiwa mada
Mwanzo – mwanafunzi huhitajika kuendeleza bila kufafanua maana ya methali
Kimalizio – lazima kisa kishahibiane na methali ile.Tanbihi
Ikiwa methali itakuwa mada, mtahiniwa atahitajika kueleza maana ya nje, ya ndani na matumizi endapo anafahamu - Hutumiwa kutoa funzo kwa wenginekutokana na dhiki na majuto yaliyomfika mhusika
- Asiyefunzwa na mamaya hufunzwa na ulimwengu
- Asiyeskia la mkuu huvunjika guu
- Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni
- Mchuma janga hula na wa kwao
- Ujanja wa nyani huishia jangwani
- Majuto ni mjukuu huja kinyume
- Mchimba kisima huingia mwenyewe
- Msiba wa kujitakia hauna kilio
- Kilio si dawa
- Asiyeangalia huishi laiti ningalijua
- Mkata pema pabaya panamwita
- Sikio la kufa halisikii dawa
- Haraka haraka haina baraka
- Vipokezi vya methali
Yawe yasiwe ____________
Aisee! __________
Labeka! _________________
Lahaula! Lakwata ____________
Chambilecho wenye ndimi walihenga ______________
Hapo ndipo nilipoamini na kusadiki kuwa ______________
Waledi wa lugha waligonga ndipo walipoganga kuwa _______________
Wakale hawakupanda upepo wakavuna tufani _____________ - Visa husika
- Wizi
- Utumizi wa dawa za kulevya
- Kujiingiza katika anasa
Mapambo na msamiati
- Kutofuata ushauri
- Alikuwa hakanywi hakanyiki
- Hasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini
- Alikuwa haliki hatafunuki
- Haambiliki hasenezeki
- Alikuwa hajijui hajitambui
- Kujuta
- Aliishia na laiti kinywani
- Alijiuma kidole/alilia chanda kili kinywani
- Nilikabiliana ana kwa ana na ulimwengu usiokuwa na huruma
- Niliyaona ya firauni
- Nilikiona kilichomtoa kanga manyoya
- Kupuuza
- Alivalia miwani mashauri
- Niliyatemea mate mawaidha
- Alijitia hamnazo
- Aliyatia kapuni yota aliyoambiwa
- Mambo kuharibika
- Mambo yalimwendea pete/tenge/mrisi/shoto/shambiro
- Kutowezekana kwa
- Ilikuwa sawa na kukama tetere
- Kufunuka jua kwa ungo au chekeche
- Kuchota maji kwa pakacha
- Tashbihi
- Pukutikwa na machozi kama ngamia
- Tiririkwa na machozi kama maji mlimani
- Mchafu kama kilihafu/fungo
- Nuka kama mzoga/beberu/kindonda
- Unafiki na kujitakia shida
- Chui aliyevalia ngozi ya kondoo
- Panya aliyeumia na kuvuvia
- Kujipali makaa kama chachandu
- Kuogelea katika bahari ya moto
- Methali ni usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiliwa na jamii kuwa wa kweli na unaotumia kufumbia
- Ragba
- Aliona cha mtema kuni
- Kilichompata peku na lungo kilimpata
- Mambo yalimwendea visivyo
- Alitamani mauti yaje yamwokoe
- Maji yalizidi ynga
- Alitamani dunia ipasuke immeze mzima mzima
- Kumwashia kipofu taa
- Alitia masikio pamba
- Machozi ya majonzi
- Lia kilio cha kite na shaka
- Machozi yalimtoka kapakapa
- Pyorea mdomo
- Huzunika ghaya ya kuhuzunika
- Machozi yalinienda mbilimbili
- Kuwa na kamusi ya matusi
- Tashbihi
- Pukutikwa na machozi ka,a ngamia
- Tiririkwa na machozi kama maji mlimani
- Bubunjikwa na machozi kama mfereji
- Nuka kama mzoga
- Mchafu kama fugo
- Takriri
- Hakiri hakubali
- Hajali jando wala togo
- Si wa uji si wa maji
- Kutomjulia heri wala shari
- Akiulizwa haungani
Methali za Kutohadaika na Uzuri wa Nje wa Kitu na Tamaa
Hutumiwa kuwaonya adinasi dhidi ya kudanganyika au kuhadaika na uzuri wa kitu bila kudadisi matokeo na athari zake.
Methali ikiwa kama kichwa huhitajika kuelezea maana ya nje, ya ndani na matumizi
Mfano wa visa
- Kumkaribisha mtu nyumbani
- Kupatiwa lifti
- Biashara gushi
- Urembo
- Fisadi
Methali
- Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
- Hakuna kizuri kisichokuwa na dosari
- Penye urembo ndipo penye ulimbo
- Uzuri wa mkakasi, ukipata maji basi
- Vyote ving’aavyo sio dhahabu
- Tama ilimwua fisi
- Uzuri si hoja hoja ni tabia
- Mpanda farasi wawili hupasuka msamba
- Mtaka yote hukosa yote
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni
- Mla kwa wawili hana mwisho mwema
- Penye uhondo pana uvundo
- Uzuri wa biyu ndani mabuu
- Usiache mbachao kwa msala upitao
Vipokezi vya methali
- Kwa yakini ______________
- Taib ___________
- Ama kweli ______________
- Kuntu _____________
- Ni jahara kama pengo kuwa _____________
- Ni wazi kama ju ala mtikati kuwa _____________
- Chambilecho wahenga au wazee wenye tabasuri tepetepe _______________
Nahau
- Maji kuzidi unga
- Kitumbua kiliingia mchanga
- Valia miwani
- Meza mrututu
- Meza mate machungu
- Tulia huku ukitolea kule
- Vimba kichwa
- Kuwa na mkono mrefu
- Bwaga zani
Takriri
- Dhahiri shahiri
- Haambiliki hasemezeki
- Hakanywi hakanyiki
- Kuwa kiguu na njia
- Hana harusi hana matanga
Ragba
- Walimdekeza mwana wao
- Alikuwa ndumakuwili aliyeuma ndani yakini kikulacho ki nguoni
- Alijaribu bahati kwani asiyekuwa na bahati habahatishi
- Pigwa kipopo
- Temea mate
- Kumwonea gere
- Mambo yalimwendea sambejambe
- Alilia kilio cha kite
Tashbihi
- Huzunika kama mfiwa
- Kuwa na wasiwasi kama mwasi
- Aminika kama njiwa
- Jambo wazi kama mchana
- Kuwa mzembe kama kupe
Insha ya Maelezo
Huitwa wasifu
Hutoa ufafanuzi kuhusu jambo, mtu, mahali au kitu fulani
Maelezo haya huwa ni sifa au hoja maalum
Insha hizi hutahadharisha, huelezea, huarifu na huburudisha
Mtahiniwa atangulize kwa ufafanuzi wa mada yake
Ahitimishe kwa kutoa changamotokwa waliohusika
Mtahiniwa asijadili chini ya hoja sita. Atoe hoja za ukweli
Mfano
- Athari za ukimwi
- Athari za dawa za kulevya
- Faida na Athari za teknolojia
- Mchezo niupendao
- Haki za watoto
- Faida ya elimu, miti na wanyamapori
- Ukosefu wa usalama
- Dawa za Kulevya
Haki na Ajira za Watoto
- Haki ni mstahiki au ni jambo ambalo ni halali ya mtu
- Mstahiki pia ni mtu mwenye haki ya kupata kitu
- Ajira ni kazi zinazofanywa katika mashamba, viwanda, nyumbani na migodini
- Watoto wanapopewa ajira ni kinyume cha sheria
- Baadhi ya haki hizi ni
- Lishe bora
- Watoto wanafaa wapewe mlo ulio na viinilishe muhimu kwa protini, kabohaidrati, madini na maji safi.
- Wasipolishwa huenda wakaathiriwa na magonjwa kama kwashakoo, utapiamlo.
- Mavazi
- Humkinga dhidi ya mabadiliko ya hali ya anga
- Huzuia maradhi kama mafua, nimonia na pumu
Methali
Kinga ni bora kuliko tiba
- Makao salama
- Humsitiri dhidi ya wanyama hatari, maadui na mabadiliko katika hali ya anga
- Kupata elimu
- Asibaguliwe kwa misingi ya jinsia, kidini, kikabila au rangi ya ngozi
- Wasichana wasiozwe mapema
- Wasijiingize katika vitendo vya ukosefu na maadili kama ukahaba
- Wafundishwe maadili na nidhamu
Methali
Elimu haitekeki
Elimu ni bahari
Elimu haina mwisho
- Afya njema
- Watoto wanafaa kukulia katika mazingira safi
- Wapewe matibabu wanapougua
- Wapewe lishe bora
Methali
Afya ni bora kuliko mali
Kinga ni bora kuliko tiba
- Wakingwe dhidi ya dhuluma
- Hii ni kama kuchomwa na kukatakatwa mwilini
- Waadhibiwe kwa kadiri na wastani
- Wakuzwe vyema kwa maadili na mapenzi
Methali
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
Masukuzi ya leo ndio msitu wa kesho
- Wasiajiriwe
- Hii ni kinyume na sheria katika katiba ya nchi
- Waajiri huwatesa na kuwanyanyasa watoto
- Wengine huwarapua kwa mijeledi
- Wengine huajiri kama vijakazi, watwana
- Lishe bora
Michezo
Ni jambo lifanywalo kwa ajili ya kujifurahisha kujichangamsha au kupoteza wakati
Baadhi ya michezo
- Jugwe
- Gugwi
- Bembea
- Kibe
- Msabaka
- Kandanda
- Riadha
- Sarakasi
- Netiboli
- Naga
- Voliboli
- Gololi
- Hoki
- Langalanga
- Kriketi
- Mpira wa wavu
Kandanda
Pia huitwa kambumbu, soka , gozi au mpira wa miguu
Hushirikisha timu mbili pinzani
Wachezaji huvalia
- jezi
- Daluga
- Soksi
- Bukta
Katikati ya uwanja huitwa kitovu/senta
Otea – kujificha kwa makusudi ya kushambulia kwa ghafla
Penalty – adhabu kwa mlindalango
Mlindalango, mdakaji, golikipa
Kimia
Refa/refarii
Mshika bendera/kibendera
Mhimili/goli
Ngware – cheza visivyo
Kipindi cha lala salama ni kipindi cha nwishi
Kadi nyekundu huonyesha kutimuliwa kwa mchezaji
Kadi ya jano – onyo
Huwa na wachezaji kumi na mmoja katika kila upande
- Walinzi au difensi
- Wachezaji wa kati
- Safu ya mashambulizi
- Wachezaji wa akiba
- Piga mkwanju
- Kocha/mkufunzi
Mapambo
- Uwanja ulijaa hadi pomoni
- Wachezaji walishonona
- Mdakaji aliudaka mpira ungedhani ni tumbili aliyedadia tawi la mti
- Pasi fupifupi na za uhakika ungedhani walikuwa na mashine miguuni
- Mpira haukulenga goli _______ kweli kulenga si kufuma
- Kuutia mpira vifuani kana kwamba una spaki za kuunasa
- Walinda ngome walikuwa imara kama chuma cha pua
- Kwenda kubwaga moyo baada ya kipindi cha kwanza
- Safu ya ilinzi ulikuwa imara kama ukuta uliotengenezwa kwa zege
- Enda nyatunyatu na kufyatua zinga la kombora
- Visha kanzu
- Nyota ya jaha
- Bao la kuta machozi
- Piga kombora kimo cha mbuzi , kuku au ngamia
- Mashabikiwalijawa na bashasha
- Kipindi cha pili tukihisi kuwa na nishati mpya
- Bao la bua liliweza kuzitubua nyoyo za wapinzani wetu
- Mrisi bin kappa
Dawa za Kulevya
Hatua
Kufafanua maana
Ni kitu chochote kinachoathiri fahamu au mwili wa binadamu
Dawa hizi ni kama vile
- Bangi
- Sigara
- Heroini
- Miraa/mirungi
- Pombe haramu
Anayeuza dawa hizi huitwa mlaguzi
Njia ya kutumia dawa hizi ni
- Hunuswa
- Hunywewa
- Hudungwa
- Hulambwa
- Hutafunwa
Madhara ya dawa za kulevya
- Kuvurugika kwa akili
- Mja hugeuka kuwa zuzu, mkia wa mbuzi
- Hupata ujasiri bandia
- Hujiingiza katika visanga
- Hudhuru afya
- Hukonda na kukondeana kama ng’onda
- Sura huambuliwa na kusawijika kama sokwe
- Utovu wa nidhamu
- Husheheni cheche za matusi
- Kutabawali kadamnasi
- Vaa mavazi vichungi na vioo
- Kuzorota kwa uchumi
- Kukosa elimu
- Jamaa hukosa mavazi, makao na mlo
- Humtilisha mtumiaja
- Husababisha uraibu
- Hushinda kutwa kucha wakitumia dawa hizo
- Huwa kupe
- Huwa maajenti wa mawakala
- Chanzo cha maafa
- Madereva hukosa kuwa waangalifu
- Huleta shinikizo la damu mwilini
- Ajali barasteni
- Wizi wa mabavu
- Kufanya mapenzi bila kinga
Tamati
- Changamoto/nasaha
- Wasiwe pweza kujipalia makaa
- Kizazi cha baadaye kitaangamia
- Kushirikiana kama kiko na digali kuangamiza janga hili
- Wito kwa serikali – kuwasaka
- Kufungua mashtaka
Mada
- KIDIMBWI CHA MANAYA
- NAULI YA AHERA
- BARABARA YA KUZIMU
- TARIKI YA MAUKO
Misemo
- Kujipalia makaa
- Bwaga zani
- Meza mrututu
- Tumbulia macho
- Gofu la mtu
Takriri
- Kufa kupona
- Kwa hali na mali
- Liwalo liwe
- Balaa belua
- Methali
- Tahadhari kabla ya hatari
- Mwiba wa kujidunga hauambiwi pole
- Ajali haina kinga
- Mchezea mavi humnukia
- Nzi kufia juu ya kindonda si haramu
- Masukuzi ya leo ndiyo msitu wa kesho
- Wazee hukumbuka vijana hukumbushwa
Tashbihi
- Konda kama ng’onda
- Nyong’onyea kama muwele wa malaria
- Dhaifu kama mkufu
- Epuka ambao kama mgonjwa wa ukoma/ebola
Umuhimu wa Maji
Mwongozo ambao ni mwanzo wa insha kisha aendeleze
Mfano
“maji yana manufaa anuwai ___________ ”
- Atoe hoja zisizopungua sita
- Iwe na mtiririko mmoja
- Sehemu ya hitimisho;atoe change moto kwa jamii au serikali
Mfano
UMUHIMU WA MAJi
Utangulizi
Maana ya maji
Maji ni kiowevu kisicho na rangi kinapatikana mtoni, ziwani, baharini na hata kutokana
na mvua
Maji ni uhai
Umuhimu wa maji
- Kukonga roho au kukata kiu
Adinasi hukonga roho
Huweza kuishi bila shabuka au shida yoyote
Husaidia usagaji wa chakula
Mapishi ya vyakula
Chakula hulainika na kuwa na ladha
Huimarisha siha/udole wa binadamu
Humweupusha mlimwengu na magonjwa - Usafi na unadhifu
Kutakata mili ili kuepukana na magonjwa
Kupiga deki
Kusafisha mashine viwandani
Kuwa mchafu kama fungo
Kusafiri jongomeo baada ya kugua maradhi - Usafiri baharini, maziwani na mitoni
Kusafirisha shehena za mizigo
Mizigo mizito kama nanga
Vyombo hivi vya usafiri ni meli, motaboti, ngalawa, merikebu, mashua, manahodha na maserahangi - Kuzungusha mitambo au mashine
Hupata nguvu za umeme au nishati
Nishati hizi huweza kutengeneza bidhaa za madini, vyakula na mavazi - Makao ya wanyama
Kama samaki, kiboko, mamba, kamba na kasa
Samaki ni chakula murua kwa mja na humzuia mja kuoata ndwele - Burudani na michezo
Hamamu na mandibwi ya maji hutumika na wanamichezo kwa mashindano ya kuogelea - Huwa sehemu ya ajira
- Huletea nchi pesa za kigeni
- Kuondoa uchafu baada ya kazi
- Maji ni asili ya uhai
- Kuuzima moto
- Kivutio cha watalii
- Kunyunyizia mimea maji
Viunganishi
- Mbali na _____________
- Fauka ya ______________
- Isitoshe _______________
- Zaidi ya ______________
- Hali kadhalika _______________
Hitimisho
- Nikilikunja jamvi ninawashauri ________________
- Hatuna la msalie mtume wala nabii ili kuyatumia maji ipasavyo __________________
- Ama kweli maji ni kito cha dhamani ambacho kinafaa kulindwa kwa hali na mali
Methali
- Maji yakimwagika hayazoleki
- Maji ya kifuu ni bahari ya uchungu
- Maji mapwa hayaogwi
- Maji ni uhai
- Maji hufuata mkondo
- Maji ukiyavulie nguo yaoge
Hotuba
Hotuba ni maneno au malezo maalum yanayotokana na mtu mmoja mbele ya hadhira
Anayetoa hotuba huitwa hatibu
Hadhira ni watu wanaohutubiwa
Hotuba inaweza kuwa ya
- Mwalimu mkuu juu ya wazazi
- Mwanasiasa nyakati za kampeni
- Maafisa wa serikali katika sherehe tofauti
- Rais akihutubia taifa
Mambo ya kuzingatia
- Kufuata itifaki
- Kutambua waliohidhuria kufuata cheo/mamlaka na umri
Mfano “mwalimu mkuu, naibu wa mwalimu mkuu, viranja na wanafunzi wenzangu hamjambo? ______ - Wakati uliopo hutumika yaani usemi halisi
- Nafsi ya kwanza na ya pili hutumika
Mfano
Nimesimama kadamnasi nikiwa mzima kama kigongo ________ - Hutumia alama za kunukuuu ikiwa unahutubia kwa niaba ya mtu mwengine
Mfano
rais, naibu wa rais ______ - Kila hoja husimuliwa katika aya yake
- Hitimisho huhusu kuwashukuru wasikilizaji na pia kuwapa funzo au changa moto au nasaha
Umuhimu wa Elimu
Elimu ni mafunzo yanayopatikana shuleni na maishani
Hupevusha fikira
Mja hujielewa, huelewa wengine na ulimwengu
Huheshimiana
Huweza kutumia raslimali vilivyo
Elimu huondoa ujinga/ujuha
Mwanafunzi humakinika katika maisha ya baadaye
Msamiati
- Leo si jana, jana si leo
- Enda na ucheo, siende na uchwao
Elimu ya vitabu humsaidia mtu kuhifadhi siri ujumbe na kumbukumbu za kutumia na kizazi cha baadaye
Msamiati
- Elimu huboresha maisha
- Kujenga makao mazuri
- Kuwasaidia jamaa na jamii
- Elimu ni daraja la kuvusha mtu kwenye gange/kazi yenyefulusi nono
- Mtu hupata hela za kujimudu pasi kuwategemea wengine
Methali - Mtegemea cha nduguye hufa maskini
- Mtegemea nundu haachi kunona
- Mja hupewa heshima
Ragba - Nimesimama imara kama chuma cha pua
- Tisti kama ngarange za mvule
- Kidete kama kitawi cha mkarakala
Pongezi za dhati - Ninawapa mkono wa tahania kwa kufanya bidii za mchwa na duduvule
- Nawamiminia shukrani sufufu
- Ninawashukuru kwa kujitolea mhanga na kujifunga kibwebwe/masombo/kujikaza kisabuni
Methali
- Elimu ni bahari
- Elimu maisha si vitabu
- Elimu ni taa gizani hung’aa
- Elimu ni mali ambayo adui hawezi kuteka
- Elimu bila mali ni kama nta bila asali
Tashbihi
- Bidii za mchwa /duduvule
- Ng’aa kama mbalamwezi
- Pesa kama njugu
- Julikana kama pesa
Misemo
- Kujitolea mhanga
- Shika usukani
- Kuna kichwa
- Ambua kitu
- Tia pamba/nta
Mjadala
Insha sampuli hii huwa na sehemu mbili: Kuunga na kupinga
Mwanafunzi ana uhuru wa kuunga ama kupinga
Katika sehemu ya hitimisho mtahiniwa anatarajiwa kutoa mawazo yake
Tamati
Ningependa kuwajuza kuwa ______________
Ningeomba sote tupinge kwa jino na ukucha _____________
tusiwe kama chachandu wa kujipalia makaa kwa ______________
Teknolojia
Ni maarifa ya sayansi na matumizi yake katika mitambo, vyombo na zana katika viwanda, kilimo, ufundi na njia za mawasiliano
Mifano
- Kilimo
Trekta
Beleshi
Pilau
Mbolea
Toroli - Zana za vita
Manowari
Bazooka
Vifaru
Darubini
Grunedi
Bunduki
Bastola
Gomborora
Nyambizi
Mzinga
Kombati
Dirizi/dereya - Mawasiliano
Simu – tamba/rununu/mkono
Tarakilishi
Tovuti
Kitenzambali
Barua meme
Kikotoo
Kimemeshi - Mitambo
Kiyoyozi/feni/pauka/pangaboi
Lifti/eleveta
Kreni/winchi/kambarau
Meli
Ndege
Mashua
Faida za Teknolojia
- Mawasiliano – kupasha habari
- Elimisha na kutumbuiza
Methali
Kipya kinyemi ngawa kindonda - Utafiti
Kuvumbua dawa za ndwele/mitambo kurahihisha kazi
Mitambo ya kuchunguza hali ya anga - Elimu
Matumizi ya mitambo
Kanda za video
Methali
Elimu ni bahari
Elimu haitekeki
Mali bila daftari hupotea bila habari
Elimu bila mali ni kama sega bila asali - Usalama
Zana za vita
Donge nono hupatikana baada yakuuza vifaa
Methali
Tahadhari kabla ya hatari
Kilimo na ufugaji
Pembenjeo – mbegu, mbolea, dawa
Ghala la kuhifadhi mazao
Mashine za kukama ng’ombe
Methali
Tembe na tembe huwa mkate - Usafiri
Vyombo vya majini, nchi kavu au barabara
Kuokoa wakati na maisha
Methali
Ngoja ngoja huumiza matumbo - Mavazi
Rahisisha kazi
Kuimarisha uchumi wa nchi
Madhara
- Mmomonyoko wa maadili
- Huleta maradhi kama saratani
- Huleta maafa
- Punguza nafasi za kazi
- Kuiga tabia za kigeni
- Vita
- Kuwafanya waja kulaza damu
- Mambo mengine muhimu
Viunganishi vya insha ya maelezo
- Licha ya
- Fauka ya
- Aidha
- Zaidi ya
- Pia isitishe
- Mbali na
- Hali kadhalika
Insha ya Mazungumzo
Mazungumzo ni maongezi, mahojiano ama malimbano baina ya mtu na mwengine au kundi moja na jengine
Yanaweza kuwa Porojo/soga/domo
Ni mazungumzo ya kupitisha wakati
Kutafuta ujumbe maalum
Hufanywa kwa njia ya mahojiano
Kudadisi au kumwelekeza mtu
Baina ya mtu na tajriba na Yule anayetakamsaada
- Mhusika mmoja asichukue nafasi kubwa
- Tumia alama za uakifishaji kama vile koloni, kitone na kipumuo
- Sharti pawe na mahali pa kumchachawiza
- Vitendo viweze kuandikwa katika alama za mabano
- Fani za lugha zitumike ili kuleta uhondo
- Pawe na maagano
Hatua
- Mada/kichwa
Huandikwa kwa herufi kubwa kupigiwa mstari - Maudhui
Ni lengo au kusudi la mazungumzo
Msamiati kutegemea lengo la mazungumzo - Vitendo na ishara
Haya yataandikwa katika mabano (akitari, akilia, akicheka) - Alama za uakifishaji
- Koloni( : ) Huandikwa baada ya jina au cheo cha watu
- Alama za dukuduku ( _ _ _ ) Mazungumzo yanaendelea
- Parandesi au mabano ( ) Kubana maneno ambayo hayatasemwa
- Alama ya hisi ( ! ) Hutumiwa pamoja na viigizi kuonyesha hisia
Insha za Hadithi
Hadithi hutambiwa kwa njia ya kusimuliwa
Hurejelea matukio au visa vyenye nasaha kwa jamii
Visa hivi hutumiwa
- Kuelimisha
- Kushauri
- Kuonya
- Bidii
- Kuonyesha umoja
Enzi za kale watoto walisimuliwa visa hivi na babu au nyanya wakati wa jiono
Mifano
- Abunuwasi
- Shamba la wanyama
- Sungura mwenye pembe
- Shujaa fumo liyongo
Ikiwa kisa kilisimuliwa na mwingine mwanafunzi atahitajika kunukuu kazi yake
Mfano
“ babu alizoea kutuambia ngano.alianza hivi ____________”
Baada ya kuhitimisha kisa mtahiniwa anahitajika kufunga
Ahitimishe kwa ushauri au nasaha
Insha hii yaweza kuchukua mikondo tofauti
- Furaha
- Majuto
- Huzuni
- Bidii
Tanbihi
Sanasana wahusika huwa wanyama ambao huwa na hisia za binadamu
Jinsi ya kuanzisha
- Paukwa?pakawa!
- Aliondokea chanjagaa kujenga nyumba kaka mwanangu mwana siti kijino kama chikichi cha kujengea vikuta na vilango vya kupitia
- Hapo zama za zama _____________
- Hapo kale ___________
- Hapo jado aliondokea _____________
- Enzi za konga mawe ______________
- Miaka na dahari iliyopita ___________________
- Katika karne za mababu na bibi zetu _____________________
- Miaka na mikaka iliyopita _____________
- Hadithi!hadithi! hapo zama za kale katika kaya/kijiji ______________
Fani za lugha
Takriri
- Miaka na mikaka
- Dhahiri shahiri
- Hana hanani
- Maskini hohehahe
- Daima dawamu
- Afriti kijiti
Misemo
- Salimu amri
- Shika sikio
- Temea nasaha mate
- Valia miwani
- Tia kapuni
- Mambo kuenda shoro
- Kutojulia heri wala shari
- Kuwa fremu ya mtu
Tashbihi
- Roho ngumu kama paka
- Zurura kama mbwa msokwao/mbwakoko
- Tabia kunuka kama kindonda/beberu
- Macho mekundu kama ngeu/damu
- Kuchukua wekundu wa moto
Methali
- Bendera hufuata upepo
- Sikio la kufa halisikii dawa
- Kutosikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini
- Nzi kufia juu ya kindonda si haramu
- Maji hufuata mkondo
- Aambiwaye akakataa hujionea
Ragba
- Kabla ya mwadhini kuadhana adhna zake
- Maji kwa pakacha
- Julikana kwa ufedhuli
- Kuwa sawa na kutumbutia maji
- Andamana na makundi yenye mienendo benibeni
- Heshima likawa neno geni kwake
- Lala kitandani hoi akiwangoja pumzi yake ya mwisho
- Lia kilio cha mbwa
Hitimisho
- Nyanya/babu alitueleza bayana umuhumu wa
- Hapo ndipo niliposandiki kuwa
- Ulumbi wa ulidhihirika waziwazi kuwa
Download Insha - Class 7 Kiswahili Revision Notes.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students