- Mnyambuliko wa Vitenzi
- Tanakali za Sauti
- Matumizi ya Vihusishi ‘katika’ na Viambishi Tamati –ni’
- Alama za Uakifishaji
- Ukubwa, Udogo na Wastani wa Nomino
- Kukanusha
- Vivumishi
- Vitawe
- Viwakilishi
- Ngeli na Viambishi Ngeli
Mnyambuliko wa Vitenzi
Huku ni kuvibadili vitenzi kwa kurefusha viambishi tamati ili kuleta kauli mbalimbali Kauli hizi ni.
- Tendana: uma - umana
- Tendesha: lala – laza
- Tendeka: Lima – limika
Huu ni upachikaji wa viambishi kwenye mzizi wa kitenzi ili kuunda vitenzi vipya
Kauli ya Kutendeshwa/Fanyisha
Huonyesha kuwa kitendo kimesababishwa na kitu Fulani
Vitenzi hivi hutambulishwa na vitenzi vya, za, sha, fya, na ,sa
Kauli ya Kutendata
Kauli hii huonyesha dhana ya kurudia rudia tendo
Mfano
Kata – katakata
Imba – imbaimba
Tia – tiatia
Ruka – rukaruka
Sifa Kutokana na Vitenzi
Ni kuunda maneno yenye kivumishi au kusifu nomino kutoka kwenye viarafa
Sifa hizi huwa ni herufi kama f, v, mw
Mfano
Amini – mwaminifu
Sikia- sikivu
Tii – tiifu
Dhulumu – dhalimu
Tanakali za Sauti
Ni maneno yanayoonyesha au kuiga milio ya sauti, hali Fulani, sura au vitendo mbalimbali. Hutumia kusisitiza namna vitendo vilivyo, vinavyotendeka au kitakavyotendeka
Mfano:
- Funika gubigubi!
- Papatika papatupapatu!
- Kula fyu!
- Kuregea regerege!
Matumizi ya Vihusishi ‘katika’ na Kiambishi Tamati –ni’
Katika na –ni ni vihusishi vinavyotumiwa kumaanisha ndani ya au kwenye
Vihusishi hivi havitumiwi pamoja katika sentensi
Mfano
- Ingia katika darasani ni kosa
- Ingia darasani au ingia katika darasa ni sahihi
-ni huambishwa kwenye nomino za kawaida kisha nomino hiyo huorodheshwa katika ngeli ya PAKUMU
Pia hutumika kuonyesha ndani ya au mahali ndani
Mfano
Vijiko vimo jikoni
Walimu wamo majilisini
Katika
- hutumiwa kuleta maana ya Miongoni mwa
mtu mmoja katika wale ni mgonjwa - Wakati
Tutakuwa na likizo katika mwezi wa Aprili - Ujumla wa vitu
Wote walishiriki katika michezo hiyo
Alama za Uakifishaji
Ni alama zinazotumiwa ili kuwasilisha nia halisi na maana kamili ya kwenye maandishi
Alama hizi pia hufanya kusomeka kwa sentensi kuwa rahisi
Mfano
Nusukoloni /Semikoloni/Nukta kipumuo(;)
Hutumiwa kuunganisha mawazo mawili
Mfano
Ninataka kuondoka mapema; sipendi kuchelewa
Koloni/Nuktambili/Nukta pacha (:)
Hutumiwa kuonyesha orodha ndefu
Mfano
Nenda ununue vutu vifuatavyo:maziwa, mkate, sukari, mafuta na chumvi
Ukubwa, Udogo na Wastani wa Nomino
Ukubwa ni hali ya kukuza nomino na udogo ni hali ya kudunisha nomino
Wastani ni hali ya kawaida ya nomino
Nomino katika ukubwa huwekwa katika ngeli ya LI – YA na nomino katika hali ya udogo huwekwa
katika ngeli ya KI – VI
Zipo kanuni ambazo hutumiwa
- Nomino zenye silabi mbili- dodosha moja
Mtu- jitu - Nomino zinazoanza kwa ki dondosha ki pachika ji
Kiatu-jiatu
Kukanusha
Kukanusha Amri
Wakati wa amri hukanushwa kwa kutumia si
Mifano
Aende – asiende
Nimpe – nisimpe
Ule – usile
Swali lije baadaye
Wewe kunywa dawa
Wewe usikunywe dawa
Wingi na Kukanusha
Wakati wa sasa hukanushwa kwa ha
Mifano
unasoma – mnasoma – hamsomi
unakula – mnakula – hamli
Vivumishi
Vivumishi vya Pekee Ingine na -O-ote
Vivumishi hivi ni ote, o-ote, enye, enyewe na ingine
Vitawe
Ni maneno yaliyo na maana zaidi ya moja
Mfano
- Vua-toa samaki majini
Toa nguo mwilini - Ala-aina ya mfuko ambamo kisu hufichwa
Tamko la kushangaa
Aina yoyote ya chombo cha kufanyia kazi
Viwakilishi
Ni neno linalosimama badala ya nomino kama yeye, sisi, wewe
Ngeli na Viambishi Ngeli
Mifano ya ngeli:
- A – WA
- U – YA
- I – ZI
- U – U
- YA – YA
- I – I
Ngeli ya A- WA
Ngeli hii inahusisha majina yenye sifa na hali ya wanyama, nyuni, malaika, samaki na wanadamu
Kutoa mifano katika umoja na wingi
Mfano
Mnyoo – minyoo
Kiwete – viwete
Nzi – nzi
Mkunga – mikunga
Ngeli ya U – I
Nomino za ngeli hii huchukua upatanisho wa U katika umoja na I katika wingi
Mifano
Mkono – mikono
Muundi – miundi
Mzigo – mizigo
Mtaa – mitaa
Muhula – mihula
Mwaka – miaka
Mlingoti – milingoti
Ngeli ya KI – VI
Nomino za ngeli hii ni vitu vya kawaida
Majina huanza kwa ‘ki’ katika umoja na ‘vi’ katika wingi
Mengine huanza kwa ‘ch’ kwa umoja na ‘vy kwa wingi
Mifano
Kiazi – viazi
Kiatu – viatu
Kioo – vioo
Kina – vina
Kikuba – vikuba
Cheti – vyeti
Chakula – vyakula
Chanda – vyanda
Chungu – vyungu
Wastani udogo
Mlango kilango
Mguu kiguu
Ngeli ya LI – YA
Maneno katika ngeli hii huanza na ma, me
Maneno yote katika hali ya ukubwa huingizwa katika ngeli hii
Mifano
Dirisha – madirisha
Embe – maembe
Zulia – mazulia
Ukubwa
Guu – maguu
Jibwa – majibwa
Ngeli ya U – YA
Maneno katika ngeli hii huanza kwa U katika umoja na Ya katika wingi
Mifano
Ugonjwa – magonjwa
Uuaji – mauaji
Ujazi - majazi
Upana - mapana
Ngeli ya YA – YA
Nomino zote huanzia kwa ma
Mifano
Masihara - masihara
Matatu- matatu
Makazi - makazi
Mahakama - mahakama
Maakuli - maakuli
Mawasiliano - mawasiliano
Ngeli ya I – ZI
Nomino hazibadiliki katika umoja na wingi
Mifano
Mashine - mashine
Sinia - sinia
Sahani - sahani
Ngozi - ngozi
Taa - taa
Pete - pete
Sakafu - sakafu
Shingo - shingo
Ngeli ya U – ZI
Maneno katika ngeli hii huwa na upatanisho wa U na ZI katka wingi
Mifano
Ubeti – beti
Uchane – chane
Uchega – chega
Ubavu – mbavu
Ubao – mbao
Ulimi – ndimi
Udevu – ndevu
Ujari – njari
Ujiti – njiti
Ugoe – ngoe
Uzi – nyuzi
Ufa – nyufa
Waadhi – nyaadhi
Walio – nyalio
Waraka – nyaraka
Ngeli ya U – U
Huchukua U katika umoja na U katika wingi
Kuelezea maneno hayabadiliki katika umoja na wingi
Mifano
Moto - moto
Ugali - ugali
Wema - wema
Ufisadi - ufisadi
Wizi - wizi
Ubaya - ubaya
Uzembe - uzembe
Ngeli ya KU
Maneno katika ngeli hii huchukua upatanisho wa kisarufi KU
Ngeli ya I – I
Majina ya nomino hii huchukua upatanisho wa sarufi kuwa I katika umoja na I katika wingi
Ngeli ya PA KU MU
Ni ngeli ya mahali
Huelezea hali tatu
- Hapa/hapo/pale- mahali dhahiri
- Huku/huko/kule – kusiko dhahiri
- Humo/humu/humo – mahali ndani
Kuelezea viambishi tofauti
Download Sarufi na Matumizi ya Lugha - Class 7 Kiswahili Revision Notes.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students