- Jumla ya hatua na kanuni ambazo hufuatwa na mtu anapopika au kuandaa kitu mlo/kinywaji.
Muundo
Sehemu muhimu za resipe ni:
- Kichwa- Jina la mlo unaoandaa, Idadi ya watu wanaopikiwa
- Orodha ya viungo unavyohitaji- majina ya viungo, Idadi au kiasi kinachohitajika
- Maagizo/namna ya kupika
- Eleza kwa utaratibu kila hatua
- Taja wakati utakaotumika katika kila hatua.
- Hakikisha kila aina ya viungo ulivyotaja, inajitokeza katika maelezo ya kupika.
- Tamati
- Baada ya chakula kuiva, eleza kinaweza kupakuliwa na chakula kipi kinginecho k.v ugali na kitoweo cha kuku
UPISHI WA PILAU
Walengwa/walaji
- Mipakuo mine (kwa watu wanne)
Viambata
- Vikombe viwili vya mchele
- Gramu 25 za mafuta ya majimaji
- Vijiko viwili vidogo vya pilau masala
- Nusu kilo ya nyama
- Vitunguu vinne vya ukubwa wa wastani
- Vikombe vinne vwa maji
Hatua za Upishi
- Kaanga vitunguu katika mafuta hadi rangi yake ikaribie rangi ya udhurungi
- Chemsha nyama pekee hadi ilainike
- Ongeza nyama kwenye sufuria yenye vitunguu na upike kwa dakika tano
- Ongeza mchele na uchanganye kwa mwiko
- Ongeza maji na uache mchanganyiko utokote kwa dakika kumi na tano
- Pakua pilau ikiwa tayari
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Insha ya Resipe - Kiswahili Insha Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students