Fani: Mbinu za Uandishi na Matumizi ya Lugha - Mwongozo wa Nguu za Jadi

Share via Whatsapp


 MBINU ZA UANDISHI

Katika riwaya hii, mwandishi amezingatia mbinu kadhaa wa kadha za Sanaa ili kuweza kuifanya hadithi yake iwe na ladha na ili msomaji aweze kufurahishwa na uandishi.

Mbinu hizi ni kama.

 1. Kinaya (irony) - Kinaya ni hali ya mambo katika riwaya/hadithi kuwa kinyume na matarajio.
 2. Taharuki (suspense) - ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kutumia maneno na kujenga hali inayozua hamu kwa hadhira; hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza.
 3. Sadfa (Coincidence) - Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa japo havikuwa vimepangiwa.
 4. Mbinu Rejeshi/Kisengere Nyuma (Flashback) - mwaandishi husimulia hubadilisha wakati wa masimulizi na kusimulia namna kisa kilivyokuwa wakti fulani uliopita.\
 5. Kisengere Mbele/Utabiri (Flash Forward) - Mwandishi anapobadilisha wakti na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni,kabla ya kuwa, huwa anatumia mbinu ya utabiri.
 6. Upeo wa Juu (Climax) na Upeo wa Chini (anticlimax)
 7. Wimbo
 8. Barua

Taharuki

 1. Barua ya Mrima – Katika sura ya kwanza, Mangawasha anapata barua iliyokuwa imeandikiwa Mrima. Inatutia taharuki maana tunaelezwa kwamba
 2. Mangwasha aishtuka kuisoma ila mwandishi hatuelezi yaliyomo wakati huo.
 3. Gari la Sihaba – Sagilu anapoona kwamba gari jekundu limechomwa, mwandishi hauelezi kule Sihaba alipo ila tunaelezwa kwamba Sagilu aliona kiatu kimoja jekundu. Taharuki inajitokeza pale ambapo hatujui kile kilichomfanyikia Sihaba kwa wakati huo.
 4. Barua ya chifu iliyoonekana kuwa na ramani - Barau hili linamtia Mangwasha ahofu anapoliona lakini mwandishi hatuelezi hapo hapo yale yaliyomo.
 5. Kupotea kwa Lonare wakati wa uchaguzi - Jamo hili liliwatia shaka kila mtu , wasijue kama atarudia ama amepotea kabisa
 6. Kumtafuta Mrima Majaani wasijue watakavyompata kwa sababu watu wote waliowaona walikuwa katika hali mbaya. Taharuki inajiokeza kwa dhana la hatujui hali ambayo Mrima angepatikana akiwa
 7. Wakaazi wa matango walikuwa na tarahuki wasijue jinsi kesi ya ardhi itakavoenda walipowaona Mafamba na Sagilu wakiingia kortini.
 8. Ndoto ya Mangwasha inatupa taharuki kwa sababu hatujui jinsi atakvyoweza kuondokea shida lile, jitu nyuma yake na moto mbele yake.
 9. Pia, Mashauri anapoenda kupeleleza kama aliyoambiwa na Ngoswe ni ya ukweli, hajui anachotarajia kupata. Alikaa akingoja asijue anachojarajia, sawa na msomaji.
 10. Nanzia anapomwambia Ngoswe kwamba alitaka kunena na yeye pekee yake, hata baba yake asiwe hapo ni jambo linaloleta taharauki kwa maana hatujui ni siri gani hiyo ambayo hata Lesulia hakupaswa kujua.

Sadfa (Coincidence)

 1. Ndoto ya Mangwasha ambapo anaota na jitu na moto na anapoamka anapata mtaa wa Matango kunachomeka.
 2. Lonare anatokea wakati ule ambapo watu walikuwa wameanza kujibizana na Mangwasha wakimuuliza kwanini alikuwa amejifungia.
 3. Lonare anaonekana mlangoni mwa nyumba ya Mangwasha siku ya asubuhi ya uchaguzi baada ya kupotea kwa muda.
 4. Ngoswe na Sagilu kuwa na usawa wa tabia na baadae Ngoswe kutambulishwa kwamba Sagilu ni babake halisi.
 5. Cheiya kuonekana na Lonare wanapoenda kuchukua cheti cha ugombeaji. Aidha, Cheiya anashikwa na Mashauri, mpenzi wake wa kitambo.
 6. Kwa kupoteza mali yao, Nanzia na Sagilu wanaugua magonjwa ya kiakili.
 7. Lombo kuwa daktari, anaporudi anajipata katikanafasi ambayo anaweza kuwasaidia wahusika wanaanza kuugua muda mdogo baada yake kufika. Mfano,
 8. Sagilu na Nanzia. Lombo anaonekana kuhusika vikubwa kwa matibabu ya wagonjwa hawa, walio wazazi wa rafiki zake.
 9. Lonare anatokea asubuhi nje ya nyumba ya Mangwasha asubuhi hiyo tu ya kuenda kupiga kura.

Kinaya (irony)

 1. Licha ya Waketwa kuwa na bidi, wengi wao wanaishi katika hali ya umaskini. Mwandishi anatueleza hii ni kwa sababu ya kufilisishwa na Wakule.
 2. Mrima anapotoshwa na Sagilu na kuingizwa katika ulevi na baada ya kutoka katika mtego huo na kuanza maisha mapya, anapokea pesa kutoka kwake kumfanyia kampeni
 3. Chifu mshabaha anafuta Mangwasha kazi na baadae anakuja kumtafuta ili amsaidie kupata mkopo.
 4. Mtemi Lesulia anasema kwamba hakutaka kuongoza tena baada ya kuona ameshindwa uchaguzi licha ya kuwa alikuwa amepanga njama na Sagilu kumteka nyara Lonare ili yeye aweze kushinda uchaguzi.
 5. Sagilu anamtishia Mashauri kwamba angemlaani ilhali ni yeye alienda kutolea laana na wazee wa ukoo yao baada ya kupatwa na kichaa.
 6. Ngoswe alikosana na Lesulia kwa kutaka kuwatumia vijana kuleta zogo. Ilhali yeye amewasbabisha kuingia mashakani kwa kuwauzia dawa za kulevya.

Kisengere Mbele/Utabiri (Flash Forward) 

 1. Ndoto ya Mangwasha – anaota kukiwa na moto na anaamka kukiwa kunachomeka
 2. Kupotea kwa Lonare mara ya kwanza kinaweza angaliwa kama utabiri wa kupote kwake wa mara ya pili kabla ya uchaguzi.

Mbinu Rejeshi/Kisengere Nyuma (Flashback)

 1. Sura ya pili ya riwaya hii imeandikwa kutumia singere nyuma, mabapo inatueleza maisha ya Mangwasha na Mrima ya awali , hadi walipofikia kuoana
 2. Kisa cha Lonare ya kupotea wakati wa uchaguzi uliopita kiemeelezwa kwa mbinu hii.
 3. Kisa cha Wakule walivyo ponda mali ya umma na kuwafilisisha Waketwa kimeandikwa kwa njia hii.
 4. Maisha ya Lonare- Kumpoteza bibiye na kulazimika kuwalea watoto wake kivyake.
 5. Kisa cha Sagilu na maziwa yaliyosababisha magnojwa kwa watoto wa shule kimeelzwa kwa mbinu hii
 6. Mbinu hii pia imetumika kumweleza Ngoswe historia ya familia yake, ikakuwaje Sagilu ndiye baba yake na kule ndugu yake alikoenda
 7. Mwandishi anatueleza kule chuki kati ya Waketwa na Wakule ilipotoka akitumia mbinu hii. Anatupa kisa cha kutoka kitambo ambapo Wakule na Waketwa walikuwa wanazozana kuhusu mifugo na kumiliki chemichemi za maji na mbuga za kulisha mifugo

Ndoto

 1. Ndoto ya Mangwasha aliyoota akikiimbizwa na jitu na alioweza kuushinda kwa kuurushia moto. Ndoto hiyo iliendanisha na hali yake aliyokuweko. Jitu hilo lilitoa manoti kila lilipofungua mdomo kushiria lile noti la elfu ambalo Sagilu alijaribu kumpa. Baada ya kuamka, alipata moto ukiwaka katika eneo lao. Aidha , kwa ukurasa wa 59 mwandishi anatueleza kwamba Mangwasha aimwona Sagilu kama jitu.

Barua

 1. Baura ya mrima aliyoanikiwa na pezni wake wa kando. Ulimjulisha Mangwasha kwamba Mrima alikuwa keshajiingiza katika usherati.
 2. Barua ya Chifu iliyo na ramani ya kujengwa kwa soko kuu. Barua hii inatumika katika ushahidi wa kuonyesha kwamba wakaazi wa Matango walikuwa wanyang’anywa ardhi kwa njia isiyo halali

Jazanda

 1. Gari nyekundu – kuashiria hatari
  Sihaba anaendesha gari nyekundu na pia kuvaa mavazi na hata viatu vyekundu kutahadharisha msomaji kwamba pale anapoonekana , kuna hatari.
 2. Taka zilizojaa majaani na hali ya watu wanaoishi huko – upweke
 3. Virago vidogo vya Mangwasha – upwekee
 4. Mashamba mengi yaliyomilikiwa na Wakule / Sagilu – utajiri
 5. Ndoto ya Mangwasha - Sagilu ndiye jitu aliyetema pesa. Sagilu alitaka kumvutia Mangwasha kwa kutumia pesa zake lakini Mangwasha aliweza kumfurusha.


MATUMIZI YA LUGHA

Katika riwaya hii, mwandishi amezingatia mbinu kadhaa wa kadha za lugha/fani na tamathali za usemi katika Fasihi ili kuiremebesha uandishi wake na kuweza kuieleza vyema zaidi. Aina za mbinu za lugha zilizo tumiwa ni kama

 1. Tashbihi (similies)-Ulinganishi kwa kutumia viunganishi kama, mithili, mfano na sawa.
 2. Sitiari/ Istiara(metaphor)-Ulinganishi usio wa moja kwa moja. Mfano;huyu ni fisi.
 3. Tashhisi/Uhaishaji(personification) -Kukipa kitu sifa ya uhai. Mfano;maji yalicheka
 4. Chuku/udamisi(hyperbole) -Kutia chumvi au kufanya kitu kionekane kikubwa sana au kidogo sana. Mfano;kijana alitoa sauti kama kipaza sauti.
 5. Tanakali za sauti (onamotopoeia/ ) - Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika.
 6. Takriri (repetition) - Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Isitoshe, takriri inaweza kujitokeza kwa kurudia rudio wazo fulani katika kazi ya sanaa.
 7. Tanakuzi (paradox)- Tanakuzi ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokanushana. Pia huitwa takriri tanakuzi
 8. Taswira (imagery)- Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.
 9. Majazi (figurative language/ symbolic meaning) - ni mbinu ya mhusika kuwa na jina lake rasmi (jina la kuzaliwa) linaloambatana na tabia/mienendo/sifa zake.
 10. Lakabu (nickname) - ni mbinu ya mhusika kupewa/kubadikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake.
 11. Misemo na nahau (idioms)- Nahau na misemo hutumika kupitisha ujumbe wa mwandishi kwa kutumia maneno ambayo hayamaanishi katika hali halisia. Misemo hutumika sana katika fasihi na katika mazungumzo ya kawaida ili kufanya lugha iwe ya kupendeza.
 12. Maswali ya balagha(rhetorical questions) - Mhusika au msimulizi huuliza maswali yasiyohitaji majibu.
 13. Uzungumzi nafsiya (self dialogue)- Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.
 14. Utohozi (loan word) - Ni kuswahilisha maneno ya lugha nyingine, yatamkike kama ya Kiswahili.
 15. Kuchanganya ndimi(mixing tongues) - Kuingiza maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili.
 16. kuhamisha ndimi - Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu
 17. Kejeli- Ni kutumia lugha inayoonyesha kudharau au kufanya kitu kiwe kidogo sana kuliko kilivyo Mwandishi ametumia mbinu kadha wa kadha za uandishi. Tutazingatia mifano kidogo kati ya yale mengi ambayo mwandishi ameweza kutumia.

Tashbihi

Ni mbinu ya ulinganishi kwa kutumia viunganishi kama, mithili, mfano na sawa/ sawa na.

 1. Akamsahau kama vile mtoto anavyosahau titi la mamaye.(uk 1)
 2. Alitetemeka kama aliyemwagika maji barafu (uk 1)
 3. …alimtupa kama tamabara bovu. ( uk2 )
 4. Hatua hii ni sawa na kuupanda mchongoma. Ni sawa na kobe kujaribu kuuma mkono wa chui. (uk 8)
 5. Sagilu alikuwa na tabia ya kubadilika kama lumbwi (uk 16)
 6. Mrima mwenyewe alikuwa keshamtema kama masuo ()
 7. Wakajiona bora kuliko malaika (uk 13)
 8. Walichezeshwa kama karata. ()
 9. Aliwafananishwa waketwaa wenzake na kundi la kondoo lisilokuwa na mchungaji. (uk 10)
 10. Nguo hizo zilicheua harufu mbaya mithili ya kicheche..(uk 100)

Tashhisi

Mbinu inayoipa kitu sifa ya uhai

 1. Starehe ya usingizi itoke wapi ikiwa vurumai na mahangaiko yalimwacha fukara? (uk 1)
 2. Upepo huouliandamana na chuki (uk 6)
 3. Chuki iliwavaa wakule, ikawavisha (uk 6)
 4. Dunia hupiga watu vikumbo (uk 12)
 5. Fikra zilienda mrama (uk 13)
 6. Kitete kikamvaa (uk 1)
 7. Mwanga wa alfajiri ukapambana na mbingu (uk 63)

Sitiari

Mbinu ya ulinganishi usio wa moja kwa moja bila kutumia viunganishi

 1. Watoto walikuwa uzi adhimu ya kuunganisha Dahari yao na kizazi kilichopita (uk 2)
 2. Ataanguka mwanguko wa mende (12)
 3. Uvivu na njaa ni mapacha. ( uk 16)
 4. Alihisi mkuki umemchoma kifuani (uk 10)
 5. Mrima amekumbatia chui (uk 77)
 6. Acha aendelee kuwabusu nyuki (uk 77)
 7. “Wale panya wamerudi kwa makao yao tena…”(uk 78)
 8. Sagilu ni chua ndani ya mchele (80)

Maswali Ya Balagha

Mhusika au msimulizi huuliza maswali yasiyohitaji majibu.

 1. Starehe ya usingizi itoke wapi ikiwa vurumai na mahangaiko yalimwacha fukara? (uk 1)
 2. Lakini..lakini hata akikitegua, salama itoke wapi? (uk 1)
 3. Angefanya nini iwapo navyo pia viliteketea? (uk 2)
 4. Barua lile lina maana gani hata akiisoma? (uk 3)
 5. Je, mwanamke angesikizwa katia jamii iliyokita ubabedume (uk 8)
 6. Je, ipo haja ya kuifurahisha ulimwengu. (uk 12)
 7. Je, hii ni njia moja ya kuwafumba macho? (uk 72)

Uzungumzi Nafsiya

Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.

 1. “Ama kweli moto ule umenitia tafsili….nitaishia kula mwande na wanangu. Huko ndiko kufa kingoto.” (uk 5)
 2. “ubao huu utakuwa msaidizi wangu…” (uk 5)
 3. “Mangwasha, siku zote hizi ulikuwa unachezeshwa kayamba tu. Ati walisema Osama alikuwa hatari…” (uk 4)
 4. “je, akipuuza nitakalimwambia…” (uk 11)

Taswira

Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.

 1. Tunajengewa taswira na jinsi Mrima alivyofanana walipomata huko Majaani (uk 100)-
  “Alikuwa hatazamiki. Uchafu wa siku nyingi ulifanya kunuka kama kisonzo. Nywele zilisokotana. Meno yalipiga manjano kutokana na ugaga uliokolea. Alivaa nguo bwaga mtwae tu. Nguo hizo zilicheua harufu mbaya mithili ya kicheche. ..”
 2. Mwandishi anatupa picha ya jinsi barua lile la Mrima lilivyoandikwa (uk 4)
  “Maandishi yalikuwa makubwa. Aliyeandika hakujali kufuata mistari ya ile karatasi aliyotumia. Yaliandikwa pengine na mtu asiyemakinika au aliyekuwa na haraka ya kuupitisha ujumbe. Maandishi yalitoka mashariki yakaelekea kaskazini badala ya magharibi, wala mwandishi hakuingatia viakifishi. Isitoshe, alichanganya herufi kubwa na ndogo kama mtoto wa chekechea anayeanza kujifunza kuandika. Ujumbe ulitirika bila kikomo wala kituo…”
 3. Taswira ya Bidii ya waketwa (uk 43)
  Mwandishi anatupa taswira ya bidi ya waketwa kwa zao.
 4. Tunajengewa taswira ya jinsi Wakule walivyoharibu rasili mali (uk 44- 47)
  Mwandishi anaupa maelezo ya kindani jinsi Wakule walivyoharibu rasili mali ya nchi yao.
 5. Tunapewa taswira ya jinsi eneo la Majaani kulivyoka kaa. (uk 97)
  “Palisheheni wahuni na wapochozi wa kila aina. Tokea wazururaj na wauwaji waliotoa roho z watu bila sababu maalumu. Mtaa huu pia uliitwa Majaani kwa sababu ya takataka zote za mji zilitupwa hapo. Marundo ya taka yalifanya vilima ambavyo wasakatonge wengi waliishi kuzumbua riziki hapo…”
 6. Sare za Kajewa na Sayore vinavyoelezwa kuwa mararu na duni (uk 58)
  “Watoto walihitaji sare mpya. Zile walizovaa zilikuwa zimechakaa sana. Suruali ya Sayore ilikuwa na viraka kadha kwenye sehemu ya makalio. Shati liliraruka mgongoni na vifungo kadha vilikuwa vimepotea. Rinda la Kajewa lilikuwa limeraruka raru raru. Alijisitiri kwa kuvaa sweta ambayo pia hailuwa na vifungo. Mikoba yao ya vitabu iling’ong’a na kudondosha vilivyokuwa ndani kila mara…”
 7. Urembo wa Mangwasha wa awali (uk 14)
  “Mangwasha alikuwa msichana mwenye umbo la wa kupendeza. Kila alipocheka, mwanya mwembamba kinywani uliitikia kicheko hicho. Alikuwa na uso duara uliopambwa kwa macho ya chawa. Midomo ya mviringo ilikaa vyema juu ya kidevu cha kupendeza. Kichwa chake kilitulia vyema juu ya shingo iliyonyooka. Nywele zake nyeusi na nyororo zilihudumiwa vyema. Hazikuwa na dalili ya ukoka kuu wala misokotano ya kuudhi. Alikuwa na mazoea ya kuzifunga tuta moja ambalo aliliremba kwa vibano vya rangi mbalimbali. Vibano hivyo pia vilitegemea ngu na herini alizovaa. Akivaa kibano chekundu, herini zitakuwa nyekundu pamoja na gauni alilovaa. Mangwasha alikuwa si mweusi si mweupe. Si mrefu su mfupi. Alikuwa mtaashati na mwenye umbo la kuvutia, sawa na tabia yake.
 8. Taswira ya Mangwasha alivyobadilika baada ya kuona dhiki juu ya mateso aliyopitia. (uk 60)
  “Macho yako madogo yaliyokuwa mangavu, ya kutamanisha kila mtu, sasa yamefifia ndani kweye vishimo vikavu. Uso uliokuwa na tabasamu ya kumfanya mtu akungwae, sasa unatangaza madhila matupu…”
 9. Taswira ya jitu lililokuwa kwenye ndoto ya Mangwasha.(uk 61)
  “Jinyama lilikuwa jeusi, limoeta nywele ndefu hadi usoni. Lilitoa sauti kama radi.Kila liliofunua kinywa kutoa sauti, machonge makubwa ya meno yalionekana…”

Chuku

Kutia chumvi au kufanya kitu kionekane kikubwa sana au kidogo sana.

 1. Matango ilikuwa kichaka kilichohamwa ata na panya (65) – Kuashiria kwamba hakuna kitu chochote cha maan ambacho kiliendelea Matango. Hakungekalika kwa hali ya kukauka kwake.

Tanakuzi

Tanakuzi ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokanushana. Pia huitwa takriri tanakuzi

 1. Mbivu na mbichi
 2. Mkata alisye na mbele wala nyuma (uk 1)
 3. Si mweusi si mweupe. Si mrefu si mfupi (uk 14)

Utohozi

Ni kuswahilisha maneno ya lugha nyingine, yatamkike kama ya Kiswahili.

 1. Chifu – chief
 2. Leseni-license
 3. Hoteli - hotel
 4. Kampeni – campaign
 5. Polisi – police
 6. Malori – lorry/lorries
 7. Bajeti – budget
 8. Manoti – notes
 9. Sweta - sweater

Majazi

ni mbinu ya mhusika kuwa na jina lake rasmi (jina la kuzaliwa) linaloambatana na tabia/mienendo/sifa zake

 1. Majuu - Kwa lugha ya sheng Majuu ni jina linalohusiana na Ulaya ama nchi ya Magharibi ambazo zinzjulikana kwa kuonekana kwa uzuri wao wa mazingira na kuonekana kuwa na maisha ya kiwango ya juu kuliko Kenya. Pia jina linaashiria kwamba wanaosihi huko ni wa tabaka la juu.
 2. Mpenda Bure - Mwenye hoteli hii, Sagilu, anaonekana kupenda ya bure kwa kujilimbikizia mali na kuwanyang’anya watu mali.
 3. Mwamba - Mwamba aliweza kuwasimamia wakaazo wa Matango. “Alikuwa mwamba”
 4. Mzee Shauri - Anapotokeakwa haidithi hii, anaonekana anapompa Mangwasha mawaidha ya jinsi ya kuishi n akujikimu.
 5. Majaani - Jina hili linahusiana na mazingira ya taka taka, yaani “jaa la taka”.
 6. Ponda Mali - Ni eneo ambalo lililojaa walijipoteza kwa anasa zao na kwa hivyo waliharibu lai waliyo nayo, mfano, Mrima.
 7. Waketwa - Jina hli linatolewa kwa kitenzi “kukatwa” ambapo tunawaona watu wa kabila hii waekatwa kutoka serikalini na uongozi, kutoka kazini na kutuiliwa mbali kwa hali ya nchi yao. Wamekatwa na kuwekwa kando pia kitabaka ambapo tunawaona ndio walijaza tabaka za chini.
 8. Wakule - Jina hili linatokana na kitenzi “kula”. Wakule wanaelezewa na mwandishi kujibugia mali ya umma. Wanaharibu rasilimali na kuleta upungufu wa vitu kwa jinsi wanavyo haribu ama kula mali.

Methali

 1. Chakani mwa simba halali nguruwe () – Methali hii inatumiwa kumaanisha pale palipo hatari mnyoge hajipeleki/ hakai huko.
 2. Heri nusu shari kuliko shari kamili. (uk 13) - Ni heri yale madogo ambayo Mangwasha alitaka kufanya na kupata nafasi hiyo kuliko kukosa nafasi kamili.
 3. Nguo ya kuomba haisitiri makalio (12) – Mtu anapasawa kujihadhari na vitu za kupewa. Kwa maana yake, yale ambayo mtu anapata kwa kutegemea mtu mwingine huja na aibu yake/ hayana busara wala hayaji na uzito way ale ambayo mtu amejitafutia.
 4. Kimya ni ua linalozunguka hekima (uk 23) – Hekima za mtu huwa zinafanya mtu awe kimya kwa kuweza kuelewa jambo zaidi. Mfano, Lonare anaonekana kuwa mwenye kimya kwa hekima zake.
 5. Penye penzi matusi hayaumi (uk 60) – Palipo na mapenzi matusi hayana uzito kwa sababu kuko n msamaha.
 6. Kifo cha panzi, furaha ya kunguru (uk 71) – Panzi wanapokufa, kungura anapata mlo. Kwa maana ya ndani, kuna wale wanaofaidika kwa hasara ya watu wengine. Kwa mfano hii, Mbwashu ameenda Matango kwa sababu ya kuchomeka kwa mtaa huo. Sio kwa huruma ila kwa masaibu ya wakaazi hawa, wamepata nafasi ya kujenga soko kuu.
 7. Afungaye kibwebwe si bure ana mchezo ( uk 75) – Anayeonekana kuwa tayari kwa jambo Fulani huwa amejitayarisha kwa jambo hilo hilo.
 8. Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha (80) – hakuna kitu kisichokuwa n a mwisho hata lionekane kuwa kirefu zaidi. Mambo yote yana mwisho.

Nahau

 1. Uliokita mizizi – ulioshika/ ulioenea sana/ uliojulikana kwa watu wengi/ uliokuwa maharufu
 2. Hapa mtaambulia patupu (uk 8) - hawangeweza kupata kile walichotaka.
 3. Alitaka kupiga mbizi (uk 13) - alitaka kuogelea/ alitaka kujiingiza kwa jambo kwa undani
 4. Kunyoshewa vidole vya lawama – aliwekelewa
 5. Kata tamaa - kuamua kuacha kufanya kitu
 6. Hamtafua dafu (uk 73) - ina maan asawa na kuambulia patupu.

Misemo

 1. Mtemi alitawala kwa mkono wa chuma (uk7) – Msemo huu unatumika kuonyesha ukali.
 2. Mtemi lesulia na Sagilu walikuwa tutu kwa ufu (uk 51) – Walikuwa wa karibu sana
 3. “…walivaa shaghalabaghala tu. Yaani bwaga mtwae tu…”(uk 55) - Walivaa kikawaida. Hawakuwa n ajambo la kuwafanya waonekane zaidi ya wengine.
 4. Maneno ya Chifu mShabaha yalipiga mwangwi akilini mwake (uk 62) – yalimshindia mawazoni
 5. Nguo za ‘kauka ‘n kuvae (uk 63) – nguo ambazo huvaliwa kuwa kufuatishwa siku baada ya nyingine.
 6. Bila shaka tutajua mbivu na mbichi (uk 73) – wangepata kujua ukweli
 7. Hakika shingo hubeba vyombo, moyo hubeba mambo (uk 77) -
 8. Asiye na be wala te (102) – Asiyejiweza/ asiye na mbele wa nyuma/ aliye bure

Kuchanganya Ndimi

Kuingiza maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili. Kwa riwaya hii ietumika haswa na wasomi au kuonyesha wahusika walio na kiwango Fulani ya masomo. Pia, mwanadishi ameitumia katika mazugumzo ya wahusika wawili walio na uhusiano wa karibu au wanaoshirikiana kwa karibu kwa jambo Fulani.

 1. Unaona nini my darling? (uk 21)
 2. Honey, Jifanye huui habari hizi (uk 21)
 3. Don’t worry my love hakuna lolote ngumu kwangu (uk 25)
 4. My love, una uhusiano upi na Sagilu?(uk 41)
 5. “Tell me the truth. Do you think babangu atashinda?”(uk132)
 6. ‘..Kisha manukato ya bei, kaka, talk of designer perfume….”(149)

Kuhamisha Ndimi

Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu

 1. “Don’t joke with some of these dot come girls, my friend. Their thirst for money is unquenchable.” (uk 123)

Kejeli

Ni kutumia lugha inayoonyesha kudharau au kufanya kitu kiwe kidogo sana kuliko kilivyo

 1. Mume ambaye ni mfano wa mume (uk 1) – Mume ambaye ni mume kwa jina tu ila haonekani kwa matendo yake.
 2. Zikaumbua utu wake akasalia suruale mtu tu (uk 77) – Akasalia mtu bure
 3. “Wale panya wamerudi kwa makao yao tena…”(uk 78) – Jina la dharau kwa Waketwa wanaolinganishwa na panya kwa hali yao ya upweke.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Fani: Mbinu za Uandishi na Matumizi ya Lugha - Mwongozo wa Nguu za Jadi.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?