Kiswahili - KCPE 2021 Prediction Set 1 (Questions and Answers)

Share via Whatsapp

Tumia misamiati mwafaka zaidi kukamilisha vihasho 1 hadi 15.

Tulipowasili ___1___ mahakama kuu jijini Nairobi, ambapo ___2___ kesi hiyo ilitarajiwa ___3___ , tulikuwa tumechoka kwelikweli. Safari hiyo ____4____ ilituchukua muda wa ___5___; tena tulisafiri usiku ili tuwahi ___6____ mjini majira ya asubuhi. "Saa mbili kamili ___7___ mjini," ndivyo tulivyoambiana baada ya safari yetu ____8___usiku uliotangulia. Kesi ilianza mwendo wa saa tatu unusu. ___9__alipoingia, sote tulisimama kama ishara ya kumpa_ 10_ zetu na alipoketi nasi tukaketi. Mshtakiwa alisimama kizimbani na kusomewa__11__ yake. Nilikuwa nimemshtaki kwa kosa la ___12___kazi msichana mdogo aliyepaswa kuwa shuleni. Mimi kama mtetezi wa haki za watoto ____13____jambo kama hilo litokee. Alijaribu kujitetea lakini wapi! Hatimaye, hukumu ___14___ aliyopatiwa, kufungwa miaka mitano jela, ikawa funzo kwa wengine wote ____15____ watoto.

kiswahli set1q1 15

Jibu maswali 16 hadi 30 kwa kufuata maagizo yaliyotolewa kwa kila swali.

  1. Jaza pengo ukitumia kivumishi-jina:
    Hapa pasiingie mtu ____
    A. mchafu
    B. yeyote
    C. mwingine                      
    D. mgeni
  2. Chagua orodha yenye vimilikishi pekee.
    A. kwake, langu, zenu
    B. huyo, hao, wale
    C. nyumbani, shuleni, kazini
    D. wao, hivyo, chako
  3. Chagua kauli iliyo sanifu:
    A. Makala lile ulilosoma linapendeza.
    B. Matatu haya hukimbia kasi.
    C. Mali yaliyoteketea ni mengi.
    D. Makaratasi yote yakusanywe panoja.
  4. Onyesha kiambishi kinachowakilisha o-rejeshi katika neno 'aliyeondolewa'.
    A. -ye-
    B. -0-
    C. -ndo-                             
    D. -le-
  5. Ni sentensi ipi imetumia kwa kuonyesha 'sehemu ya'?
    A. Watoto watatu kwa kumi walifaulu mtihanini.
    B. Amekula chakula chake kwa uma.
    C. Nimewasili hapa kwa kujitahidi tu.
    D. Waliopo ni mchanganyiko; waume kwa wake.
  6. Mjomba wangu huniita:-
    A. mjukuu
    B. umbu
    C. mpwa                            
    D. witara
  7. Tambua kauli iliyo katika hali ya wastani.
    A. Jino lake linamwuma sana.
    B. Majitu yalituvamia yakatukimbiza.
    C. Kitoto kichanga kimejichafua.
    D. Vijiatu vile vinahitaji kushonwa.
  8. Umbo liitwalo 'haram' pia huitwa:
    A. tiara
    B. piramidi
    C. tạo                                
    D. pia
  9. Ni usemi upi ulio katika wakati usiodhihirika waziwazi?
    A. Hajaondoka bado.
    B. Asiyekuwepo na lake halipo.
    C. Angealikwa angehudhuria.
    D. Hakuonekana tena.
  10. Jaza pengo kwa kiradidi:
    Pahali ____ ndipo utakapoketi.
    A. hapo
    B. papo hapo
    C. papo papo
    D. hapo hapo
  11. Onyesha neno lenye sauti changamano:
    A. Ndama
    B. Gogo
    C. Saa                               
    D. Matatizo
  12. "kijakazi' kwa 'mtwana' ni kama 'mtamba' kwa:
    A. fahali
    B. ndama
    C. beberu                          
    D. kikwara
  13. Maelezo yapi si sahihi kuhusu ushairi?.
    A. Shairi la tarbia lazima liwe na kibwagizo.
    B. Tathnia ni shairi la mishororo miwili katika kila ubeti.
    C. Ukwapi ni mshororo wa kwanza katika ubeti.
    D. Kipokeo ni mshororo unaorudiwa mwishoni mwa kila ubeti.
  14. Kipi ni kiulizi cha 'nafsi"?
    A. Wapi?
    B. Nini?
    C. Lini?                             
    D. Mgani?
  15. Tambua methali sawa na:
    Kawia Ufike.
    A. Haraka haraka haina baraka.
    B. Ngoja ngoja huumiza matumbo.
    C. Chelewa chelewa utapata mwana si wako.
    D. Chururu si ndo ndo ndo!

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 31 hadi 40.

Waliosema dunia ni tambara bovu hakika walilenga shabaha. Visanga na sarakasi zinazotokea kila siku bila shaka ni za kushangaza. Katika majarida, magazeti na taarifa za habari, kumejaa mambo ya kuatua mioyo ya wengi. Uwajibikaji umezikwa katika mava ya mghafala. Lakini kidole cha lawama kiashiriwe nani? Swali hili limebaki kuwa kitendawili ambacho hakina wa kukitegua. Ndoa za kudumu zimesalia mikononi mwa Jalali azinusuru. Wengi wamebaki kujiuliza iwapo siku ya kiama imekaribia au vipi

Zamani maisha ya ndoa yaliheshimiwa kwani kupitia nikaha, kizazi cha baadaye kilipatikana. Cha kushangaza zaidi ni jinsi wanaume wanavyodhulumiwa na wake zao. Ni jambo ambalo limegonga vichwa vya habari kila uchao. Wao huishia kupata majeraha mwilini. Mwanamke kumwashiria kidole mume wake kulikuwa mwiko katika jamii. Siku hizi mambo yameenda tenge kwani hawaashiriwi kidole tu bali pia hupokea kichapo. Huishia hata kulazwa hospitalini.

Utawasikia wanaume wakilalamikia kunyimwa chakula na kulala mvunguni mwa kitanda. Maisha yao yamekuwa hayana maana. Wengine hulazimika kutorokea kwa jirani kisa na maana kutafuta amani. Jambo hili linasababisha wanaume hawa kukosa uaminifu katika ndoa : kuwa na 'mpango wa kando kama wanavyouita. Husingizia kupata utulivu wa moyo na fikira.

Katika sehemu mbalimbali nchini, pombe haramu imekuwa chanzo cha masaibu yanayowapata wanaume. Wao hupiga mtindi mchana kutwa kiasi cha kutotimiza wajibu wao kama kichwa cha nyumba. Matokeo yake ni kuwa afya yao huzorota kwani hamu ya kula huyeyuka mithili ya barafu motoni. Kuutia msumari moto kwenye dondandugu, wengine hata hupofuka. Jamani! Tunaelekea wapi?

Ni siku kadhaa zilizopita wanawake walipopanga maandamano kulalamikia masaibu wanayopitia. Wanaume wameshindwa kutekeleza wajibu wao katika familia. Sioni ni kitu gani kitakachowazuia wanawake kupandwa na mori na kuwaadhibu wanaume hawa. Methali 'hasira hasara' haina maana yoyote kwao. Wengine hata huwachoma waume zao hata kwa maji moto wanapofika nyumbani wakiwa wamelewa chakari. Waume wamebaki magofu ya watu kiasi cha kutostahimili mapigo.

Shirika moja lisilo la kiserikali limejitokeza kuwatetea wanaume kutokana na dhuluma hizi. Wanadai kuwa wanaume wana haki ya kulindwa na kutetewa kisheria. Tusipotahadhari, nchi yetu huenda ikakosa viongozi wa kesho. Tutahadhari kabla ya hatari. Enyi wanaume, zindukeni kwani wakati ni sasa. Msipofanya hivyo, mtaishia kujuta.

  1. Kwa nini habari nyingi zinaatua moyo?
    A. Zinaangaziwa kwenye vyombo vya habari.
    B. Zinadhihirisha ukosefu wa uwajibikaji.
    C. Huwa si zenye kushangaza.
    D. Ni zenye kuashiria kidole cha lawama.
  2. Ni usemi upi uwezao kutumika badala ya
    'walilenga shabaha'?
    A. waligonga ndipo
    B. walipiga moyo konde
    C. walitoa ngebe
    D. walitia chumvi
  3. Kwa nini wengi wamebaki kujiuliza iwapo siku ya kiama imekaribia au vipi?
    A. Ndoa za kudumu zimenusuriwa na Jalali.
    B. Ili waweze kutegua kitendawili kilichokosa wa kukitegua.
    C. Ndoa nyingi hazidumu.
    D. Jalali ameshindwa kuzinusuru ndoa.
  4. Kulingana na aya ya pili, si kweli kwamba waume kupigwa na wake zao:
    A. kumesababisha majeraha
    B. ni kinyume cha haki
    C. ni kiini cha shida kwenye ndoa
    D. ni jambo la tangu jadi.
  5. Ni kipi haswa kiini cha waume wengine kukosa uaminifu katika ndoa?
    A. Kudhulumiwa na wake
    B. Kukaribishwa na majirani
    C. Utulivu wa moyo na fikira
    D. Kuwanyanyasa wake zao
  6. Lipi si tokeo la wanaume kutumia pombe haramu?
    A. Kuzorota kwa afya
    B. Kutotekeleza wajibu nyumbani
    C. Kukosa uwezo wa kuona
    D. Kutopungua kwa hamu ya chakula
  7. Kinachowachochea wake wengi kuwadhulumu waume zao ni waume:
    A. kubaki magofu kiasi cha kutostahimili mapigo
    B. kutekeleza wajibu wao katika familia
    C. kutelekeza wajibu wao katika familia
    D. kupanga maandamano kulalamikia masaibu wanayopitia.
  8. Neno 'mwiko' limetumiwa kwenye habari kumaanisha:
    A. haramu
    B. kawaida
    C. ajabu                            
    D. laana
  9. Mwandishi anamaanisha nini kwa kutumia usemi 'kuutia msumari moto kwenye dondandugu'?
    A. kumalizia orodha ya matatizo
    B. kuongeza shida juu ya shida nyingine
    C. kutoa suluhu kwa tatizo
    D. kujisababishia matatizo
  10. Habari hii imeangazia hasa:
    A. kutowajibika kwa wanawake katika ndoa
    B. kutowajibika kwa waume na dhuluma wanazokabili
    C. dhuluma wanazokabili wanawake
    D. jinsi ya kupigania haki za wanawake.

Soma kisa kifuatacho kwa makini kisha ujibu maswali 41 hadi 50,

Ajabu ya ajabu barua za walioachishwa kazi zilipotolewa, Ma'Ntilie alikuwa mmoja wao. Alishangaa! Wenzake waliposikia habari zile walishtuka hasa. "Hapana, haiwezekani! Iweje na alivyo na juhudi kubwa! Walilalamika. Lakini hamna aliyekisikia kilio hicho.

Waliosikika wakinung'unika waliulizwa, "mnataka muachishwe kazi nyie?" Wakafyata mikia na kumwachia Ma'Ntilie zigo lake pekee. Ma Ntilie akaondoka kwa huzuni nyingi na malipo ya shilingi elfu arubaini kuelekea kwao nyumbani. Alijua mzigo mkubwa umemwangukia. Alikuwa na watoto watano; baba yao naye keshaaga dunia.

Alipofika nyumbani hakujikalia kibwete tu, aliamua kutafuta la kufanya. Huu haukuwa wakati wa kukaa akishika tama na kujiuliza kwa nini aliachishwa kazi. Alishatambua ni akina nani waliohusika katika maamuzi hayo ya nani aachishwe kazi na nani abaki. Basi kwake haikuwa ajabu tangu hapo. Huko nyumbani alianzisha biashara ndogo ya kioski. Kwa bahati nzuri, nyumba yake haikuwa mbali na bwawa. Aliamua kuanza kupanda mboga za kila aina ambazo angeuza kwenye soko la karibu. Juhudi zake zilizaa matunda na baada ya muda akawa sasa anasambaza mboga kwa wingi sokoni. Kile kioski chake sasa kilipanuka; akaongeza mtaji na kuipanua kuwa duka dogo.

Kutokana na biashara yake hiyo, aliweza kumudu kuwalipia wanawe karo ya shule pamoja na kuyakidhi mahitaji yao mengine. Wakati wa likizo nao walikuwa tayari kumsaidia mama yao. Ma Ntilie aliendelea na juhudi zake. Siku mradi mkubwa wa ujenzi ulipoanzishwa kwenye soko la karibu, Ma Ntilie aliamua kujitosa kwenye uuzaji wa chakula au “kapile' kwa wale vibarua waliofanya kazi pale. Alioka chapati, kaimati na vyakula vingine huko nyumbani na kwenda kuwauzia vibarua hao. Wengi wao walikipenda chakula chake kwa sababu kadha: usali wake, upishi stadi na uchangamlu na ubinadamu wa muuzaji aliyekuwa radhi hata kuwakopesha.

Lakini biashara hii mpya ilimzulia matatizo mengine. Pale sokoni palikuwa na wenye hoteli mbili ambao walichukizwa na biashara yake hiyo. Walihisi kuwa aliwavuta wateja wao kama nyuki wanavyovutwa na mbelewele za maua. Biashara zao zilianza kukumbwa na matatizo. Mwanzoni waliamua kumtishia Ma'Ntilie au Mama Kapile kama alivyojulikana na watu wengi pale sokoni. Walimtishia kumshtaki kwa kufanya biashara bila ya kuwa na idhini. Lakini hapo walinoa. Mama Kapile alikuwa tayari keshanunua leseni ya kumruhusu kuifanya biashara hiyo.

Basi wafanyabiashara hao waliamua kumlia njama. Mwaka ulipokwisha, Mama Kapile alipokwenda kupata leseni, kama alivyofanya kila mwisho wa mwaka, alikumbwa na matatizo mapya. “Serikali imekataza uuzaji wa chakula kisichopimwa na wataalamu," jamaa aliyehusika alimwambia. Mama Kapile alimkumbusha kuwa alikuwa na leseni kila wakati na kwamba chakula chake kulikuwa kizuri daima lakini yule jamaa hakusikiliza lolote. Alilia kuwa alikuwa na jamaa ya kulisha lakini ikawa bure tu. Akaondoka kurudi zake kwa huzuni na kulazimika kuendelea na mauzo ya mboga. Hata hivyo, wale vibarua, baada ya kugundua njama iliyokuwako waliamua kususia hoteli zenyewe.

Watu waliungana na kuanza kumpigania Mama Kapile. Muda mfupi baadaye aliidhinishwa tena kuendelea na biashara yake.

  1. Kuachishwa kazi kwa Ma'Ntilie:
    A. kulifanya waliolalamika waachishwe kazi pia
    B. kuliwatia moyo wafanyakazi wenzake
    C. Kuliajabiwa na wafanyakazi wenzake
    D. kulionekana kuwa jambo halali kabisa.
  2. Alijua mzigo mkubwa umemwangukia.' Ulikuwa mzigo upi huo?
    A. Malipo ya shilingi elfu arubaini.
    B. Kuiendesha biashara ndogo ya kioski.
    C. Masimango na dhihaka za waliomsema.
    D. Kukidhi mahitaji ya familia yake kubwa.
  3. Msemo 'akishika tama' umetumiwa katika habari kumaanisha:
    A. akihuzunika
    B. akilalamika
    C. akizembea                    
    D. akishangaa
  4. Si kweli kwamba Ma Ntilie:
    A. alifanya kazi yake ya kuajiriwa kwa bidii
    B. aliona kufutwa kwake kazi kuwa jambo la haki
    C. alikuwa mjane
    D. alihangaishwa sana na kupoteza kwake kazi.
  5. Mara tu baada ya kufutwa kazi, Ma'Ntilie alianzisha:
    A. upanuzi wa duka dogo
    B. usambazaji wa mboga sokoni
    C. upanzi wa mboga bwawani
    D. biashara ndogo ya kioski.
  6. Neno 'mtaji limetumika katika habari kumaanisha:
    A. upanuaji wa kioski kuwa duka
    B. bidhaa zinazouzwa kwenye kioski au duka
    C. bidii anazotia mtu katika biashara
    D. hela zinazotumika kuanzisha biashara.
  7. Tumeelezwa kwamba mara tu mradi mkubwa wa ujenzi ulipoanzishwa sokoni, Ma'Ntilie:
    aliacha biashara yake ya duka
    B. aliona fursa ya kuanzisha biashara mpya
    C. alipanua biashara yake ya uuzaji wa chakula
    D. alianza kuzuliwa matatizo mengine na biashara yake.
  8. Vitisho alivyokabili Ma'Ntilie katika biashara yake ya kapile yalisababishwa na nini?
    A. Usafi, Listadi na uchangamfu wake
    B. Wivu wa wafanyabiashara waliopoteza wateja
    C. Wateja kuanza kususia chakula chake
    D. Kufanya kwake biashara bila idhini
  9. Kwa mujibu wa habari, yote haya ni kweli ila lipi?
    A. Biashara ya Ma'Ntilie ilifungwa kutokana na njama ya wenye hoteli.
    B. Ma'Ntilie alilipia leseni ya biashara yake kila mwaka.
    C. Watu walipendelea chakula cha Ma'Ntilie kuliko kile cha hotelini.
    D. Serikali ilikataza uuzaji wa chakula kisichopimwa na wataalamu.
  10. Kupiganiwa kwa Ma'Ntilie na watu kuliwafunza wafanyabiashara wa hoteli ukweli upi?
    A. Jitihada haiondoi kudura.
    B. Mnyonge hana haki.
    C. Mwenye nguvu mpishe.
    D. Dau la mnyonge haliendi joshi.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.

Andika insha yenye kuvutia yenye umalizio huu:

............. Kila mmoja akaondoka na kujiendea zake nyumbani kwa huzuni nyingi.



MAJIBU

kiswahili set 1 ms

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - KCPE 2021 Prediction Set 1 (Questions and Answers).


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest