Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - BSJE Mock Exams 2023

Share via Whatsapp
Maagizo
  • Andika jina na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  • Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani.
  • Jibu maswali yote.
  1. Soma dayolojia ifuatayyo kisha ujibu maswali yanayofuata. (Bw. Akot na Bi Khadija wamekaa katika sebule ya mkahawa wakiendesha dayolojia kuhusu uwajibikaji wa viongozi waliochaguliwa)
    Bw. Akot: Bibiye, yasikitisha sana kuona kuwa viongozi tunaowachagua hawaonyeshi hata chembe moja ya kuwajibika.
    Bi Khadija: Ah! Ndio sasa unayafahamu hayo? Wanapotuomba kura hudai kuwa ni watumishi wetu. Pindi wachaguliwapo, utumwa unawagura na wanajitwika joho la ubwana. Lakini usisahau kuwa hali hii si ya hapa nchini tu bali ni ya bara zima la Afrika.
    Bw. Akot: Ingawa ni tatizo la bara zima, hapa kwetu limekithiri mizizi. Hawa viongozi wetu wamezidi. Kila  baada ya miaka mitano sisi wananchi huenda kupiga kura. Huwa na matarajio makubwa kuwa tunaowachagua watayajali na kuyashughulikia maslahi yetu. Wanatufanya tuamini haya katika kipindi cha kampeni. Ukiwasikia katika majukwaa ya kuomba kura wanavyotongoa lugha na kutoa msururu wa ahadi, utafikiri maisha yetu, yahe, yataimarika mara tu tutakapowachagua. Ole wetu! Ukiamini haya, wajihadaa. Zote hizi ni ahadi za upepo zinazopeperushwa na hewa pindi wanapopata ushidi.
    Bi Khadija: Kumbuka kuwa lawama zote  haziwaendei viongozi hawa tu. Hata sisi raia twapaswa kulaumiwa. Baadhi yetu ni viongozi wazuri lakini tunaogopa kujitosa kwenye siasa.
    Bw. Akot: Kwa nini tulaumiwe ilhali si sisi tunaoupata uhondo wa uongozi?
    Bi. Khadija: Hapo  ndipo lawama  zinapojia. Sisi raia twapaswa kulaumiwa kwa sababu ya kuwaamini viongozi zaidi kupita mipaka. Sisi tunawaachia majukumu yote watuongoze mithili ya ng’ombe anayeongozwa na mchinjaji. Badala ya kutumia nafasi zilizoko za kuwaandama ili wawajibike, sisi raia hubaki tukilia tu. Hatujui kuwa tuna njia za kulazimisha viongozi wetu kuwajibika!
    Bw. Akot: Tutawezaje kutekeleza hayo ilhali tunapowachugua wanatuambaa kama wagonjwa wa ukoma? Muda wa kuwapata ni baada ya miaka mitano wanapokuja kutuomba tuwapigie kura tena.
    Bi. Khadija: Tusikate tama. Wakati huo ndio mwafaka kwetu kutumia kiboko tulichonacho kuwaadhibu wale ambao hawakutekeleza wajibu wao. Tunapaswa kutumia wakati huo kuwapiga kalamu walioshindwa kutekeleza majukumu yao. Kisha tusikomee hapo. Tunapaswa kuwachuja kwa makini viongozi tunaowachagua. Hatupaswi kukubali kuhadaiwa kwa porojo na ahadi zisizotimia. Ili kutekeleza haya ni muhimu kujua wajibu wa kila kiongozi anayechaguliwa.
    Hii ndiyo sababu wengi wetu raia huhadaika kwa urahisi wakati wanowania viti vya uwakilishi wanapotoa ahadi za kutujengea mbinu msingi kama shule, barabara na hospitali. Huu huwa uongo mtupu. Ujenzi wa mambo haya ni wetu raia kupitia kwa serikali. Ujenzi huu hutekelezwa kutoka kwa  pesa tunazozitoa kama kodi. Jukumu la wabunge ni kuhakikisha wanapigania ujenzi huu utekelezwe katika maeneo wanayoyawakilisha. Ahadi hizi za uongo hazipaswi kuwa kigezo chetu cha kuwateua.
    Bw. Akot: Lakini ukumbuke kuwa wanaotaka kuchaguliwa hutujia kwa hila nyingi.
    Bw. Khadija: Hayo sipingi. Umma unapong’amua kuwa wanaotaka kuchaguliwa hutumia hila, unapaswa kukaa ange na kuzitambua hila hizo na kuzipiga vita. Tatizo letu kubwa sisi tunaowachagua ni kutojua wajibu wetu.Pili, wengi wetu huwa wasakatonge na tunaporushiwa vihela kidogo kama chambo, tunakimbia kuziuza haki zetu na za watoto wetu.  Kwa njia hii,  tunawachagua viongozi wasiotujali na wanaotupotezea wakati pamoja na kuyahatarisha maisha yetu na ya watoto wetu.
    Bw. Akot: Wengi wao hubadilika na kuanza kutubeza kuwa sisi ni wahuni, wavivu na watu wasiostaarabika. Wengine hujilimbikizia mashangingi yanayomeza mafuta kama sijui nini. Juu ya haya hutembea na misururu ya magari na makundi ya wapambe na walinzi. Baadhi yao wamehamia kwenye makasri makubwa yenye vyumba sita vya kulala na vidimbwi vya kuogelea. Yote haya  kwa gharama ya yule mpigakura mlalahoi.
    Bw. Khadija: Mwenzangu, usisahau kuwa mimi na wewe tuna wajibu wa kuwaelimisha wenzetu kuhusu wajibu wao katika  uchaguzi wa viongozi.
    Bw. Akot: Ninakubaliana nawe kabisa. Naomba tushikane bega kwa bega ili tutoke katika giza hili.
    MASWALI
    1. Ni kwa namna gani viongozi waliochaguliwa hawaonyeshi chembe ya kuwajibika? (alama 1)
    2. Eleza mchango wa wapiga kura katika hali ya uongozi nchini mwao. (alama 4)
    3. Eleza maoni ya Bi. Khadija katika kufanikisha uongozi bora (alama 4)
    4. Bainisha mbinu wanazotumia viongozi ili kufanikisha ushindi wao kulingana na kifungu    (alama 3)
    5. Andika maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa kwenye kifungu. (alama 2)
      1. Limekithiri mizizi 
      2. Wasakatonge
  2. UFUPISHO (alama 15)
                                                                             CHIMBUKO LA KISWAHILI
    Kiswahili ni lugha ambayo huzungumzwa na takriban watu milioni mia moja kote ulimwenguni. Pia, ni lugha ya saba ulimwenguni na ya pili barani Afrika kwa kuwa na wazungumzaji  wengi. Asili ya lugha hii imetafitiwa na wanaisimu na wanahistoria. Kuna maoni aina tatu kuhusu asili na chimbuko  la Kiswahili. Baadhi ya watu kama F. Johnson, C. Meinhof, Akofu Steere, W.E. Taylor, G.W.Broomfield, W.H.Whitely na wengineo wameshikilia kuwa Kiswahili ni lugha mseto. Wasomi hawa wanadai kuwa Kiswahili kimetokana na maingiliano ya lugha za Kibantu na lugha za kigeni kama vile Kiajemi, Kiarabu na Kihindi. Wanaoshikilia wazo  hili  husema kuwa Kiswahili kilizuka ili kufanikisha mawasiliano katika shughuli za kibiashara. Wao wanasisitiza kuwa Kiswahili hakikuwepo kabla ya kuja kwa wageni.

    Kuna madai pia kuwa Kiswahili ni lahaja ya Kiarabu. Dhana hii inapotosha kwa sababu inaonyesha kuwa kabla ya kuja kwa wageni kwenye upwa wa Afrika Mashariki hapkuwa na Kiswahili. Wazo hili si sahihi kwa sababu hakuna lahaja ya aina hii huko Uarabuni. Pili Waarabu pia walienda Afrika Magharibi kupitia Afrika Kaskazini, mbona lahaja ya namna hii haikuzuka huko?

    Maoni ya mwisho ni kuwa, Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kiafrika yenye asili ya kibantu kama vile Kihaya, Kikuyu, Kiyao, Kimeru na Kigiriama. Lugha hii ya Kibantu iliweza kukopa maneno ya kigeni kutoka kwa lugha za Kiarabu, Kiingereza, Kijerumani, Kihindi, miongoni mwa zingine. Ukopaji huu ulitokana na maingiliano ya jamii hizi kupitia kwa  biashara na utawala.

    Maoni yanayoshikiliwa sasa ni kuwa Kiswahili ni lugha ya Kiafrika yenye asili ya Kibantu. Ithibati ya kutosha imetolewa kupitia kwa  utafiti wa Kiisimu, Fasihi  Simulizi  na Historia (mapisi).

    Uchunguzi wa isimu  historia na isimu linganishi uliofanywa na M Guthrie mwaka  wa 1948 unaonyesha kuwa Kiswahili kina uhusiano na lugha zingine za Kibantu hasa tunapotazama mashina ya maneno mengi kutoka lugha mbalimbali za Kibantu. Maneno ya asili kama vile kichwa, mkono, maji, njia na majina ya wanyama katika lugha hizi yanahusiana, na hivyo kubainisha kuwa yalitoka kitovu kimoja.

    Baada ya Wabantu kufanya makazi katika sehemu ya Mto Tana walishambuliwa na Wagalla. Baada ya mashambulizi haya Wabantu walitawanyika na kuanza makazi mapya kuanzia sehemu ya Modagishu upande wa kaskazini, hadi sehemu ya Mto Pangani, upande wa kusini. Baadhi yao walivuka Bahari ya Hindi na  kwenda kufanya maskani yao katika  visiwa vya Unguja. Pembe za Ngazija. Katika maeneo haya waliendelea kuzungumza lugha zao za Kibantu, lakini kutegemea wakati na umbali kati yao, tofauti za kimatamshi na msamiati zilizuka. Tofauti hizi zilisababisha kuwepo kwa lahaja  mbalimbali  za Kiswahili. Miongoni mwa lahaja hizi ni Kiamu, Kipate, Kingare, Kimvita,Kivumba, Kingazija, Kinzwani, Kipemba, Kiunguja, Kitumbatu, Kibajuni, Kisiu miomgoni mwa zingine.

    Jambo lingine ni kuwa Kiswahili kina irabu tano kama zilivyo lugha nyingi za Kibantu. Irabu hizi ni a, e,i,o, na u. Hali kadhalika muundo wa msamiati wa Kiswahili kimsingi  huchukua konsonanti –irabu - konsonanti –irabu. Kwa mfano; kigoda, maji, baba. Hata hivyo konsonanti mbili au tatu zinaweza kufuatana. Kwa mfano nywele, pwani, ngwena, afya na  mengine mengi.

    Mpangilio wa nomino za Kiswahili huleta uwiano wa kisarufi na huitwa ngeli za nomino. Hujitokeza katika lugha zingine za Kibantu. Mfano wa mpangilio wa nomino hizi ni ngeli ya KI-VI, U-I, A-WA, LI-YA. Nomino hizi zinapotumiwa katika lugha ya Kiswahili huwa na uwiano na vitenzi. Jambo hili  pia hujitokeza katika lugha zingine za Kibantu, na kudhihirisha kuwa Kiswahili ni mojawapo ya lugha za Kibantu.

    Katika maoni ya fasihi simulizi, asili ya Kiswahili ni Kingozi. Mashairi ya Hamziya yaliyoandikwa katika karne ya 18 yaliandikwa kwa Kiongozi. Kiongozi kilikuwa kikizungumzwa sehemu iliyoitwa Ushwahili upande wa visiwa vya Magunyoni(Pate, Lamu, Faza) hadi bara kupakana na Mto Tana

    Asili ya neno ‘Kiswahili’ inasemekana ilitoka na kijana wa Kingozi aliyeulizwa na wageni (wasafiri wa Kiarabu) kuwa wao ni kina nani? Akajibu kuwa “Sisi ni Wa-ziwa hili.” Yaani wenyeji wa ziwa hili. Kutegemea wakati na matamshi, jina hili lilibadilika na kuwa Waswahili
    1. Eleza ujumbe unajitokeza katika aya za kwanza tatu (Maneno 90, alama 9, 1 ya mtiririko)
      Nakala chafu
      Nakala safi
    2. Thibitisha kuwa Kiswahili ni lugha ya Kiafrika yenye asili ya kibantu. (Maneno 60. Alama 4,1 ya mtiririko)
      Nakala chafu
      Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Ni sauti gani haifai kuwa  miongoni mwa hizi. Toa sababu (alama 2)
      1. /ng’/ /g/ /t/ /k/
      2. /s/ /v/ /ch/ /sh/
    2. Andika neno lenye muundo ufuatao (alama 1)
      Nazali ya ufizi, kipasuo ghuna cha kaakaa laini, irabu ya juu nyuma, irabu ya nyuma wastani.
    3. Ainisha mofimu katika neno walionana (alama 3)
    4. Eleza maana ya mzizi wa neno  (alama 2)
    5. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. (alama 2)
      1. nywa (kutendwa) 
      2. fa(kutendwa)
    6. Eleza matumizi ya maneno yaliyopigiwa mstari katika  jozi ya sentensi hizi: (alama 2)
      Huyu ni mkufunzi msomi.
      Mkufunzi huyu ni msomi sana
    7. Ziandike upya sentensi zifuatazo kwa kufuata maagizo kwenye parandesi       (alama 6)
      1. Niliwaeleza wazazi wetu kwa dhati.Walikuwa wamepigwa mafamba hadi hawakuamini niliyosema. ( Anza: Wazazi…)
      2. Watoto wanaovaa nguo fupi fupi siku hizi wamethiriwa na tabia za kigeni. (Anza kwa: Nguo fupi…)
      3. Mtaalamu alituambia kwamba kusoma kwa mapana kungepalilia ubunifu wa wanafunzi wale wetu. (Andike kwa usemi halisi).
    8. Alama ya kiulizo hutumiwa katika sentensi ambayo ni swali. Eleza matumizi mengine ya alama hii. (alama 1)
    9. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi ‘O’ (alama 2)
    10. Ichanganue sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha visanduku (alama 3)
      Marekebisho ambayo yamefanywa yanavutia sana.
    11. Geuza sentensi ifuatayo iwe kwa wingi (alama 2)
      Mwanzi alioupanda karibu na mto umeshikana ukawa msitu mkubwa.
    12. Ashua ni mwanafunzi aliye na matatizo ya kibanafsi  katika masomo yake. Licha ya yeye ni mwanafunzi bora shuleni. Hakuna anayeelewa changamoto zake kwa kuwa ameziweka siri. Huenda akasitisha masomo ikiwa hatapata msaada. Ni methali gani inayoweza kumfaa Ashua?    (alama 1)
    13. Tunga sentensi moja itakayotofautisha maana ya baa na paa.   (alama 2)
    14. Tambua aina za virai katika sentensi hii (alama 2)
      Wanafunzi wote walizawidiwa na Rais.
    15. Kanusha sentensi ifuatayo (alama 2)
      Ukimwona Bakari umwambeia nitamtembelea kesho.
    16. Tunga sentensi  itakayodhihirisha shamirisho kitondo na chagizo (alama 2)
    17. Iandike sentensi ifuatayo katika kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari.  (alama 2)
      Onyango alihama Kilifi baada ya kuchimba makaburi.
    18. Yakinisha sentensi ifuatayo katika nafsi ya pili umoja (alama 1)
      Hataenda shuleni kesho
    19. Andika maana ya misemo ifuatayo (alama 2)
      fanya inda
      Changa bia
  4. ISIMUJAMII (ALAMA 10)
    Umealikwa kama mshauri nasaha katika shule moja ya upili inayokumbwa na tatizo la mihadarati miongoni mwa wanafunzi. Andika sifa kumi za lugha utakazozingatia ili kufaulisha uwasilishaji wako.

                                                      MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA

  1.  
    1.  
      • Wanapoomba kura hudai kuwa ni watumishi wetu. Pindi wachaguliwapo, utumwa unawagura na wanajitwika joho la ubwana.
      • Wengi wao hubadilika na kuanza kutubeza kuwa sisi ni wahuni na wavivu.
      • Wengine hujilimbikizia mashangingi yanayomeza mafuta               (yoyote 1x 1)
    2.  
      • Mchango wa wapiga kura
      • Walishiriki kupiga kura na kuwateua viongozi hafifu.
      • Wanawaamini viongozi kupita mpaka.
      • Baadhi yao huogopa kujitosa kwenye siasa.
      • Wao huuza kura zao. Wanaporushiwa vihela kidogo.           (zozote 4 x1)
    3.  
      • Kuwapiga kalamu walioshindwa kufanya kazi.
      • Kuwachuja viongozi wanaochguliwa.
      • Wasikubali kuhadaiwa kwa porojo na ahadi
      • Wananchi wafahamu wajibu wa kila kiongozi          (zozote 4 x1)
    4.  
      • Kutoa ahadi za uongo zisizotimizwa.
      • Kutoa vipesa vidogo
      • Porojo                 (zozote 3 x1)
      • limekithiri mizizi –limeenea sana/ limekuwa sugu
      • wasakatonge - watafutaji
  2. UFUPISHO
    1.  
      • Kiswahili ni lugha ambayo huzumzwa kote ulimwenguni.
      • Ni lugha ya saba ulimwenguni na ya pili varani Afrika.
      • Asili ya lugha hii imetafitiwa na wanaisimu na wanahistoria.
      • Baadhi hudai kuwa Kiswahili ni lugha mseto.
      • Hao wanadai Kiswahili kimetokana na maingiliano ya lugha  za kibantu na za kigeni.
      • Wengine wanadai Kiswahili ni lahaja ya Kiarabu
      • Hii si sahihi kwa kuwa hakuna lahaja kama hii kule Uarabuni.
      • Lahaja hii haiko Afrika kaskazini.
      • Kiswahili ni lugha ya Kiafrika yenye asili ya Kibantu.
      • Lugha hii ilikopa maneno ya kigeni kutoka lugha zingine.
    2.  
      • Kiswahili ni lugha ya Kiafrika yenye asili ya Kibantu.
      • Mashina ya maneno mengi hutoka lugha mbalimbali za kibantu.
      • Baada ya wabantu katika mto Tana kushambuliwa na kutawanyika waliendelea kuzungumza lugha zao za kibantu zilizosababisha kuwepo kwa lahaja za Kiswahili.
      • Kiswahili kina irabu tano kama zilivyo lugha nyingi za kibantu.
      • Miundo ya misamiati ya Kiswahili huchukua konsonanti irabu kama ilivyo katika lugha za Kibantu.
      • Maneno  mengi katika Kiswahili hujipanga katika ngeli.
      • Katika maoni ya fasihi simulizi, asili ya Kiswahili ni Kingozi.
  3. Matumiziyalugha (al. 40)
      1. Sauti  /ng’/ niking’ong’o
      2. Sauti  /ch/  ni kizuio kwamizwa               4 ×½=(al. 2)
    1. nguo (al. 1)
    2.      Wa – li – on – an – a
             Ι       Ι       Ι     Ι       Ι    
      Nafsi    wakati  mzizi    kauli  kiishio             Akikosa chochote, aondolewe ½
      Ngeli 
    3.  
      • Sehemu ya neno ambayo haibadiliki neno hilo likinyambuliwa katika – kauli mbalimbali
      • Umbo la msingi la neon  ambalo hutumika kuundia maumbo mengine yanayohusiana.   (2x1)
    4.  
      • nywa – nywewa /nywiwa (2x1)
      • fa      -   fiwa
    5. Huyu ni mkufunzi -Kivumishi
      Mkufunzi huyu ni msomi sana- Kivumishi
    6.  
      1. Wazazi wetu walikuwa wamepigwa mafamba hadi hawakuamini niliyowaeleza kwa dhati. (2/0)
      2. Nguo fupi fupi zinazovaliwa na watoto ni athari za tabia za kigeni. (2/0)
      3. “Kusoma kwa mapana kutapalilia ubunifu wa wanafunzi hawa wenu.” Mtaalamu  alituambia.    (4x½) = 2
    7. Kiulizo hutumiwa kuonyesha shaka katika sehemu fulani ya maandishi. mfano
      Hawa ndugu pacha (?)Walizaliwa Kenya?
    8. Kiambishi ‘O’ hutumiwa kama:
      • Kirejeshi cha ngeli ya U – ZI umoja mfano: uliozibwa
      • Kuonyesha kinyume cha vitenzi – chomoa
      • Ufupisho wa majina ya ukoo – mwanao
      • Viashiria vya mbali kidogo - huo
    9.  
                                                                         S   
                            KN                                    

                                          KT                       

       N    S      T         E 
       Marekebisho  ambayo yamefanywa  yanavutia  Sana
    10. Mianzi walioipanda karibu na mito imeshikana ikawa misitu mikubwa.    2/0
    11. Mficha uchi hazai.  1/0
    12. Sentensi idhihirishe maana:
      baa – jambo au tukio linaloleta hasara /shida / balaa
      paa – sehemu ya juu inayofunika nyumba /mnyama wa porini anayefanana na mbuzi / enda angani / ondoa magamba ya samaki kwa kuparuza.             2x1
    13. Wanafunzi wote - KN               zozote 2x1
       Walizawidiwa na Rais-   kirai Tenzi
      Na  Rais - RH
    14.  
      • Ukimwona  Bakari, usimwambie nitamtembelea kesho.
      • Ukimwona Bakari umwambie sitamtembelea  kesho.
    15. Kadiria
      Baba alimpikia mama ugali kwa sufuria kubwa
                              Kitondo               chagizo           2x1
    16. Onyango alihamia kilifi baada ya kufukia makaburi.     2x1
    17. Utaenda shuleni kesho al. 1/0
    18.  
      • fanya inda – kuwa na roho mbaya /kutomtakia mwenzako mafanikio
      • change bia - kushirikiana
  4. ISIMU JAMII
    • Lugha nyepesi inayoeleweka kwa urahisi.
    • Utohozi wa baadhi ya maneno
    • Kurudiarudia baadhi ya maneno
    • Msamiati maalum wa shuleni
    • Kuhamisha ndimi/lugha
    • Lugha yenye toni kali ya kuonya
    • Maswali balagha
    • Kutumia misimu ilikujinasibisha nao
    • Lugha rasmi.
    • Matumizi ya ucheshi. 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - BSJE Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?