Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  1. Rafiki yako anayesomea katika shule jirani amefukuzwa shule kwa sababu ya ukosefu wa nidhamu.Mwandikie barua ukimshauri kuhusu umuhimu wa kuwa na nidhamu shuleni.
  2. Teknolojia ya kisasa ina faida na madhara kwa vijana wetu.Jadili.
  3. Andika kisa kitakachoonyesha ukweli wa methali : Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  4. Andika insha itakayoishia kwa:
    …Ilinichukua muda mrefu kuyaamini niliyoyaona.

                                                              MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Swali la lazima
    • Hii ni barua ya kirafiki.
      Hoja ni kama vile:
      1. Elimu na nidhamu huwa zinaenda sambamba.
      2. Hudumisha uwezo wa kufikiria vizuri.
      3. Huboresha mawasiliano.
      4. Huleta uaminifu miongoni mwa wanafunzi.
      5. Huondoa migogoro shuleni.
      6. Husaidia katika kutia bidi masomoni.
      7. Husaidia kutunza muda vizuri.
      8. Humsaidia mwanafunzi kujifunza mambo mbalimbali ya Maisha.
  2. Faida za teknolojia
    1. Imeboresha Maisha yao.
    2. Ukuaji wa viwanda vinavyotoa ajira.
    3. Ulimwengu wa burudani umekuwa kwa kasi.
    4. Husaidia vijana kufanya kazi zao nyumbani.
    5. Kuwezesha utafiti.
    6. Kuboresha mawasiliano.
    7. Kuhifadhi habari.
    8. Kupata habari.
      Madhara ya teknolojia
    9. Imekuza uvivu.
    10. Ukosefu wa faragha.
    11. Ukosefu wa ajira
    12. Athari juu ya usingizi.
    13. Athari kwenye mahusiano ya kijamii.
    14. Uharibifu wa mazingira.
    15. Watu kutofikiria.
  3. METHALI
    1. Mwanafunzi athibitishe methali hii katika masimulizi.
    2. Aonyeshe maadili
    3. Aonyeshe mamna ya kutosikia la wakuu.
    4. Aonyeshe vile alivyovunjika guu.
  4. INSHA YA KUMALIZIA
    • Yaliyomo kwenye mwili yaoane na maneno yaliyomalizia insha.
    • Mada ikuzwe kikamilifu ili kuibua taharuki.
    • Mbinu za uandishi kama vile methali,tashbihi nk zitumiwe kwa njia inayofaa.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?