Maagizo
- Jibu maswali manne pekee.
- Swali la kwanza ni la lazima.
- Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki Riwaya, Ushairi, Tamthilia na Fasihi Simulizi.
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
- Maswali yote ni sharti yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
SEHEMU A: HADITHI FUPI (LAZIMA)
D.W. Lutomia na Phibbian Muthama : Mapambazuko Ya Machweo Na Hadithi Nyingine
- Lazima
Athari ya mawazo yake ilijiandika dhahiri shahiri usoni mwake. Aliazna kwa kuachia tabasamu pana mithili ya msafiri aliyefika salama. Baada ya dakika chache, machozi yalianza kumtoka njia mbilimbili huku kajishika tama. Alifikiria kuhusu mtihani uliodhamiriwa kuanza siku ya Jumanne. Mtihami ambao ungemwezesha kupata ufadhili katika shule ya upili ya bweni ikiwa angepita vyema. Hili ndilo wazo liliozua tabasamu. Lakini, angefeli aje? Hatima yake ingekua ipi? Maswali haya yalimliza yakwamwach akisinasina kama mgonjwa wa mafua. Akiwa katika hali hii, aliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu, '' Mizizi ya elimu ni michungu ial matunda yake ni matamu. Ikiwa mnataka kuyaonja matunda ya elimu, lazima mtie bidii kwani mtaka cha mvunguni sharti ainame.''
Akiwa amezama kwenye lind i la mawazo, aliziduliwa na sauti ya Yunuke ikimwita, ''Sabina! Sabina! Sabina!- Changanua mtindo kwenye kifungu. (alama 8)
- Suala la kazi na bidi limeangaziwa kwa kina kwenye diwani ya mapambazuko ya machweo. Tetea ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo:
- Fadhila za punda
- Mapambazuko ya machweo
- Sabina (alama 12)
SEHEMU B: RIWAYA
A.Matei: Chozi la Heri.
Jibu swali la 2 au la 3
- Naona wingu kubwa angani likitembea kwa kedi na madaha na kulifunika jua...Mawingu yaliyoshiba yakataka kutapika yanagooka, yanakaribiana, kupigana busu na kusababisha mwanguko wa matone mazito ya mvua; matone yanayoanguka kwenye ngozi laini zą wanangu wakembe... ubavuni mwangu amelala maskini mke wangu... Sijui kama inahalisi kumwita mke wangu.... Siye, siye, siye-e-e-e. Tazama uso wake ulivyovamiwa na majeraha kikwi... Amevimba na kuvimbiana kama dongo la unga ngano baada ya kutiwa hamira. Lakini yeye hana la hamira!
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Jadili aina nne za taswira katika dondoo hili (alama 4)
- Bainisha vipengele vingine vinne vya kimtindo katika dondoo hili (alama 4)
- Bainisha toni ya dondoo hili. (alama 2)
- Fafanua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili (alama 6)
- “Alijiona kama mfa maji ambaye anakabiliwa na mtutumo wa mawimbi ya misiba ,mmoja baada ya mwingine.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Ukimrejelea msemewa wa maneno haya na wahusika wengine kutoka kwenye riwaya,onyesha jinsi walivyokumbwa na mawimbi ya misiba. (alama 16)
SEHEMU C: TAMTHILIA
Timothy Arege: Bembea Ya Maisha
Jibu swali la 4 au la 5
- “Hata nikiitwa nitaondoka nikiwa nimeridhika.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili . (alama 4)
- Kwa hoja tano, eleza sifa za msemaji wa maneno haya . (alama 5)
- Tambua mbinu moja ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. (alama 1)
- Wahusika mbalimbali kwenye tamthilia wamekubwa na majonzi na furaha. Thibitisha. (alama 10)
- “...Tayari unakuwa umeonja seli.Hata wahudumu wenyewe hawana mlahaka mwema .amri na vitisho kama askari.Unashindwa kama uuguze moyo ama ugonjwa.Katika wodi hewa iliyojaaa harufu ya dawa imezagaa,vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zikagura.Yaani hali nzima haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora.matumaini yanadidimia .Tumaini lako unaliweka katika sala. ”
- Tambua toni mbili katika kifungu hiki (alama 2)
- Tambua aina mbili za taswira katika dondoo hili (alama 2)
- Kando na taswira chambua vipengele vingine vya kimtindo (alama 6)
- Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia kujenga tamthilia ya Bembea ya Maisha. (alama 10)
SEHEMU D: USHAIRI.
Jibu swali la 6 au la 7
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Taifa ni Ushuru
Lau kama ingakuwa, madhali tuna uhuru
Watu kodi kutotowa, na kuifanya kufuru
Vipi nchi ingakuwa, taifa bila ndururu
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Hivi taifa kumea , nakuendelea mbele
Kwamba lajitegemea, haliwategei wale
Yataka kujitolea, ushuru bila kelele
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Wafanyikazi wa umma, mfano mwema walimu
Wauguzi mahashuma, daktari wahadimu
Bila hizi darahima, vipi wangalihudumu?
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Si vyema kuombaomba, kwa wageni kila mara
Huwa twajifunga Kamba, na kujitia izara
Adha zinapotukumba, kujitegemea bora
Taifa halingakuwa,bilashi bila ushuru
Miradi ya maendeleo, yahitaji darahima
Ndo tufikie upeo, ulio dunia nzima
Wadogo na wenye vyeo, bila kodi tutakwama
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Ushuru si kwa wanyonge, wasokuwa na uwezo
Watozwe hata wabunge, na wengine wenye nazo
Yeyote asijitenge, kodi akalipa bezo
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Kwetu kutoa ushuru,ndiko kujitegemea
Pasiwepo na udhuru, usio wa kuelea
Huwa ni kama kiguru, asenao kutembea
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Maswali- Tambua hadhira inayolengwa katika shairi hili. (alama 1)
- Huku ukitoa mfano,onyesha mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kutosheleza uhuru wake. (alama 3)
- Bainisha aina tatu za urudiaji zinazojitokeza katika utungo huu. (alama 3)
- Eleza muundo wa ubeti wa sita. (alama 4)
- Andika ubeti wa nne katika lugha ya nathari/tutumbi (alama 4)
- Kwa kutolea mfano,taja mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika shairi hili. (alama 3)
- Weka shairi hili katika bahari yake ukirejelea : (alama 2)
- Vipande
- Vina
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Sikilizeni wimbo huu:
Niliokuwa mtoto nilitwa chacha Kwa matamshi yangu ya sasa
Nilipokuwa mtu mzima niliitwa Manywele Nilipokuwa mwalimu nikaitwa Bure.
Huu utakuwa wimbo wako Utakapostaafu urudipo nyumbani Umelewa kangara na nyayo zako
Zikishindwa kulenga njia nyembamba vijijini. Utakuwa kichekesho cha watoto Watakaoukuita, Ticha! Popote upitapo.
Kumbuka mwalimu utakapostaafu, Mijusi watataga mayai ndani ya viatu Vyako vilivyokwisha visiginino.
Na ndani ya sidiria chakavu Zilizoshikizwa Kamba kwa pini
Mende watazaliana ndani ya chupa tupu Za marashi na za bia.
Na manyigu yatajenga ndani ya kofia Zilizosahaulika kutani
Utakapokufa nge watazaliana Chini ya jiwe juu ya kaburi lako, Na mlevi fulani akipita atapenga
Na kupangusa vidole kwenye jiwe pweke
Mwanzo na mwisho wako ndio huo.
Lakini wakati ungali hai
Unaweza kubadilisha mkondo wa maji Lakini kwanza mzungumze. Wewe na mimi. Acha mioyo yote izungumzwe
Baada ya kunyanyaswa Na kisha nusu mshahara.
Utafundisha tena nyimbo kuwasifu viongozi? Utafundisha tena ngonjera?
Utapeleka tena wanafunzi asubuhi Wakajipange barabarani kusubiri Mgeni afikaye saa kumi na apitapo
Apunga tu mkono kuwatia kichaa cha shangwe
Na huku nyuma mwasambaa na njaa?
Tazama hilo runda madaftari mezani Utalimaliza kwa mshahara mkia wa mbuzi? Tuzungumze. Ninyi na mimi.
Acha mioyo yetu izungumze
Mkiwa waoga na kujikunja kama jongoo Mtawekwa kwenye vijiti na kutupwa Nje ya ua, ndani mtawaacha
Wacheza ngoma wakitunga nyimbo mpya
Sikilizeni walimu,
Anzeni kufundisha hesabu mpya
Mjinga mmoja kujumlisha na wezi ishirini Ni sawa na sifuri. Hapana utawala Fundisheni historia historia mpya
Hapo zamani za sasa Hapakuwa na serikali.
Sikilizeni kwa makini Umoja hatuna
Twasambaratika kama nyumba Tulicho nacho ni woga,
Na kinachotuangusha ni unafiki. Lakini tusikate tamaa kama mbuni. Tukiupata umoja bado tunayo silaha. Kura.
Maswali- Fafanua sifa za shairi huru zinazojitokeza katika shairi hili. (al. 5)
- Eleza jinsi maudhui ya utamaushi yanavyojitokeza ukimrejelea nafsi-nenewa. (al. 4)
- Nafsi-nenewa anapaswa kujilaumu kwa masaibu yake. Thibitisha. (al. 2)
- Bainisha nafsi-neni katika shairi hili. (al. 1)
- Taja toni ya shairi hili. Toa mfano. (al. 2)
- Eleza matumizi mawili mawili ya usambamba na jazanda katika shiri hili. (al. 4)
- Eleza maana ya kufungu kifuatacho:
Mjinga mmoja kujumlisha na wezi ishirini ni sawa na sufuri. (al. 2)
SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
- Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali
- Angole angole mwanangu
Mwanangu nakuchombeza
Nakuchombeza ulale
Ulale ukiamka
Nikupikie ubwabwa
Na mchuzi wa papa
Ukilia waniliza, wanikumbusha
Ukiwa wa baba na mama - Baba na mama watende
Ilimu kunikatizia
Ng’ombe, mbuzi kupokea
Kunioza dumu kongwe
Haliuki na halende
Kazi kupiga matonge - Likingia mvunguni
- Lavunjavunja vikombe
Likilala kitandani
Languruma kama gombe- Bainisha kipera cha utungo huu. Thibitisha. (alama 2)
- Eleza ujumbe unaofumbwa katika wimbo huu. (alama 5)
- Tambua mbinu za kifani ambazo zimetumiwa kuwasilisha utungo huu. (alama 3)
- Bainisha shughuli mojamoja ya kijamii na ya kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utungo huu. (alama 2)
- Unakusudia kukusanya data kuhusu kipera hiki. Eleza manufaa manne ya kutumia mahojiano. (alama 4)
- Kipera hiki kinazidi kufifia katika jamii yako. Fafanua njia nne ambazo jamii ya kisasa inaweza kutumia kukuza na kuendeleza kipera hiki. (alama 4)
- Angole angole mwanangu
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
SEHEMU A: HADITHI FUPI (LAZIMA)
D.W. Lutomia na Phibbian Muthama : Mapambazuko Ya Machweo Na Hadithi Nyingine
- Lazima
Athari ya mawazo yake ilijiandika dhahiri shahiri usoni mwake. Aliazna kwa kuachia tabasamu pana mithili ya msafiri aliyefika salama. Baada ya dakika chache, machozi yalianza kumtoka njia mbilimbili huku kajishika tama. Alifikiria kuhusu mtihani uliodhamiriwa kuanza siku ya Jumanne. Mtihami ambao ungemwezesha kupata ufadhili katika shule ya upili ya bweni ikiwa angepita vyema. Hili ndilo wazo liliozua tabasamu. Lakini, angefeli aje? Hatima yake ingekua ipi? Maswali haya yalimliza yakwamwach akisinasina kama mgonjwa wa mafua. Akiwa katika hali hii, aliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu, '' Mizizi ya elimu ni michungu ial matunda yake ni matamu. Ikiwa mnataka kuyaonja matunda ya elimu, lazima mtie bidii kwani mtaka cha mvunguni sharti ainame.''
Akiwa amezama kwenye lind i la mawazo, aliziduliwa na sauti ya Yunuke ikimwita, ''Sabina! Sabina! Sabina!- Changanua mtindo kwenye kifungu. (alama 8)
- Uhuishi – athari ya mawazo yake ilijiandika Dhahiri shahiri usoni mwake.
- Tashibihi – tabasamu pana mithili ya msafiri
- Taswira – tabasamu pana
- Takriri – njia mbilimbili
- Balagha – lakini, angefeli je?
- Mbinu rejeshi – maneno ya mwalimu mkuuS
- Jazanda – mizizi na matunda
- Methali – mtaka chv mvunguni sharti ainame
- Nidaa – Sabina!
- Suala la kazi na bidi limeangaziwa kwa kina kwenye diwani ya mapambazuko ya machweo. Tetea ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo:
- Fadhila za punda
- Mapambazuko ya machweo
- Sabina (alama 12)
SEHEMU B: RIWAYA
A.Matei: Chozi la Heri.
Jibu swali la 2 au la 3
- Changanua mtindo kwenye kifungu. (alama 8)
- Naona wingu kubwa angani likitembea kwa kedi na madaha na kulifunika jua...Mawingu yaliyoshiba yakataka kutapika yanagooka, yanakaribiana, kupigana busu na kusababisha mwanguko wa matone mazito ya mvua; matone yanayoanguka kwenye ngozi laini zą wanangu wakembe... ubavuni mwangu amelala maskini mke wangu... Sijui kama inahalisi kumwita mke wangu.... Siye, siye, siye-e-e-e. Tazama uso wake ulivyovamiwa na majeraha kikwi... Amevimba na kuvimbiana kama dongo la unga ngano baada ya kutiwa hamira. Lakini yeye hana la hamira!
-
- Ni usimulizi wa Kaizari
- Anawasimulia wakimbizi wenzake / Ridhaa.
- Yumo kambini / Misitu wa Mamba.
- Anarejelea hali ya ugeni kule kambini / anarejelea hali ya maumivu ambayo wanawe Lime na Mwanaheri wamo baada ya kubakwa / Hii ni baada ya uchanguzi kufurushwa kwao na kuishia kambini/anarejelea tandabelua ya baada ya uchaguzi. (4x1=4)
- Aina za taswira:
- Taswira oni/ya uoni/mwono - naona wingu kubwa angani likitembea
- Taswira mwendo - wingu kubwa likitembea
- Taswira sikivu - sauti ya mawingu yakigooka
- Taswira mguso - mawingu yanakaribiana, kupigana busu; wingu kulifunika jua; yanayoanguka kwenye ngozi laini za wanangu.
- Taswira hisi - yakataka kutapika (za kwanza 4x1=4)
- Vipengele vya kimtindo;
- Tashihisi/uhuishi - wingu kubwa angani likitembea kwa kedi na madaha / mawingu yakataka kutapika
- Urudiaji/Takriri/uradidi- matone; siye;mke wangu/hamira
- Mdokezo - ngozi Laini za wanangu wakembe.../maskini mke wangu...
- Tashbihi - amevimba na kuvimbiana kama dongo la unga ngano
- Nidaa - hana hamira!
- Nahau/msemo – majeraha kikwi
- kudumisha sauti – siye-e-e-e (za kwanza 4x1=4)
- Toni ya uchungu/masikitiko / huzuni (1x2=2)
- Umuhimu wa mandhari:
- Kuibua maudhui mbalimbali k.m maudhui ya ukatili - jinsi Lime na Mwanaheri walivyabakwa.
- Kuchimuza tabia za wahusika – k.m utu wa jiraniye Tulia; tabia za mwanzi kama katili kwani tunaambiwa Selume kuishi na wakimbizi kuliko kwenya kasri la dhuluma za mumewe.
- Kuonyesha wakati wa kutukia kwa matukio- tandabelua baada ya uchaguzi
- Huchangia kuibua toni na hali ya kijumla – mandhari haya yanaibua toni ya uchungu na masikitiko.
- Huibua dhamira ya mwandishi mandhari ya kambi ya wakimbizi yanaibua dhiki za wakimbizi baada ya ghasia za baada ya uchaguzi.
- Hutambulisha wahusika - tunabainishiwa wahusika kama Subira, Lime, Mwanaheri, Ridhaa, nk..
- Kudokeza migogoro - baina ya wafuasi wa Bi.Mwekevu na mpinzani wake mkuu.
- Husaidia kulinganua hali za matabaka - k.m. aliyekuwa waziri, familia ya Bw. Kute
- Kuonyesha mahali pa tukio – k.m Lime na Mwanaheri wanabakiwa nyumbani kwao
- Huibua taharuki - Kaizari akisimulia jinsi gari lao lilivyoishiwa na petroli taharuki inajengwa.
- Kuendeleza ploti – k.m Wakimbizi wanapofurushwa kutoka makwao na kuanza maisha upya katika kambi ya wakimbizi / Msitu wa Mamba. (zozote 6x1 = 6)
-
- “Alijiona kama mfa maji ambaye anakabiliwa na mtutumo wa mawimbi ya misiba ,mmoja baada ya mwingine.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Msemaji: maelezo ya mwandishi/msimulizi
- Msemewa:Anamrejelea Lunga
- Mahali:Msitu wa simba
- Sababu:Mwandishi anatueleza changamoto alizokumbana nazo Lunga baada ya kuhama kutoka msitu wa mamba.
- Ukimrejelea msemewa wa maneno haya na wahusika wengine kutoka kwenye riwaya,onyesha jinsi walivyokumbwa na mawimbi ya misiba. (alama 16)
- lunga anafutwa kazi baada ya kutetea raia dhidi ya kupewa mahindi yaliyokuwa hatari hata kwa panya
- lunga anapoteza mali yake yote baada ya kutimuliwa kutoka msitu wa mamba
- Naomi anamtoroka Lunga wakati alipomhitaji Zaidi.
- Ridhaa anaipoteza aila yake yote inayoangamizwa na mzee Kedi
- Umu anabaki mpweke baada ya ndugu zake kutoroshwa na kijakazi Sauna
- Lime na Mwanaheri kubakwa na vijana barobaro mbele ya baba yao
- Zohali anapata mimba akiwa kidato cha pili anaamua kutoroka nyumbani kwao baada ya kuachiwa kazi zote za nyumba
- Subira amejaa majeraha usoni mwake na pia mwili wake kuvimbiana kutokana na ubahaimu wa mwanadamu
- Ridhaa anabaguliwa na wanafunzi wenzake kitendo kinachomfanya kutoroka shule
- Majumba ya ridhaa yanabomolewa ikisemekana yalijengwa sehemu iliyotengewa ujenzi wa bypass.
- Sauna kubakwa na babake wa kambo na anapomfahamisha mamake anamnyamazisha kuwa asimpake tope babake
- Sauna anaamua kutoroka nyumbani kwao baada ya kulazimishwa kuavya mimba na mamake mzazi
- Riziki Immaculata kutupwa na mamake kwenye mapipa ili kijifie ila kinaokelewa na Neema na kupelekwa kwenye kituo kutunza watoto cha Benefactor.
- Jumba la Ridhaa alilokuwa amewapangisha wafanyabiashara kuchomeka kutokana hitilafu za umeme hadi kuwa unga tifutifu.watu wengi walifia humo ndani.
- kutokana na machafuzi ya uchaguzi Subira mkewe kaizari anakatwa kwa sime na vijana ambao pia wanawabaka lime na mwanaheri mabinti zake Kaizari mbele yake akishuhudia .
- Makaa amiye Mwangeka kuchomeka asibakie lolote alipoenda kuwaokoa watu walliokuwa wakifyonza mafuta kutoka kwa lori lililokuwa limeanguka.
- Baada ya machafuzi ya uchaguzi wakimbizi(Ridhaa ,Kaizari na wengine)wanaishia kwenye kambi ambako maisha ni magumu sana.Hawana chakula,maji safi ya kunywa,misala hakuna wanaishi kwenye vibanda wote wazee kwa watoto.
Kadiria majibu ya mwanafunzi 16x1
SEHEMU C: TAMTHILIA
Timothy Arege: Bembea Ya Maisha
Jibu swali la 4 au la 5
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- “Hata nikiitwa nitaondoka nikiwa nimeridhika.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili . (alama 4)
msemaji:Sara
Msemewa:Dina
Mahali:Nyumbani kwa Sara
Sababu:Anaonea fahari maisha ya watoto wake wanavyojiendeshea mambo yao licha ya kusemwa hapo awali. - Kwa hoja tano ,eleza sifa za msemaji wa maneno haya . (alama 5)
- mvumilivu-sara anavumilia mateso na kipigo cha mumewe
- mwenye Hekima –maneno anayoyazungumza yana wingi wa hekima na busara.
- Mwenye mapenzi-anampenda mumewe na watoto wake
- Mwenye msimamo thabiti –Hata baada ya kusutwa na kukejeliwa na wanajamii hayumbishwi na maneno yao.
- Mtamaduni-anasema fimbo hurithiwa na mtoto wa kiume
- Mwenye uhusiano mwema –Sara alikuwa na uhusiano mwema na Dina ndiposa anaenda kumsidia kupika.
- Mshauri-Anawashuri wanawe kuheshimu ndoa mila na baba yao.
- Mwenye shukrani- Anamshukuru Asna kwa kumpa uji.
- Mwenye heshima –Anamheshimu mumewe kwani ndiye moto wa kifuu. 5x1
- Tambua mbinu moja ya lugha iliyotumika katika dondoo hili.(alama 1)
Tafsida –nikiitwa nitaondoka - Wahusika mbalimbali kwenye tamthilia wamekubwa na majonzi na furaha vilevile.Thibitisha. (alama 10)
- Ndoa ya Sara na Yona imejaa furaha mwanzoni wanapooana.Maisha yao yaonekana yenye mafanikio na furaha.
- Ndoa hii inaingia dosari baada ya kukaa muda mrefu bila kupata watoto.
- Hatimaye wanabarikiwa na watoto watatu wa kike hali inayoleta furaha kwa muda.
- Wanajamii wanawacheka, kuwakejeli na kuwasuta kwa kutojaliwa mtoto wa kiume.
- Kutokana na kusutwa huku,Yona anaingilia ulevi hali inayomfanya kumchapa mkewe Sara na pia kuidharau familia yake.
- Ulevi wake Yona unamfanya kutelekeza majukumu yake kama mwalimu na kuishia kufutwa kazi
- Kichapo alichopewa Sara na Yona kinamsababishia ugonjwa wa moyo hali inayomfanya kukosa matumaini ya kuishi na kutamani kufa.
- Kabla kuingilia ulevi, Yona alikuwa mwalimu hodari ,watoto aliowafunza walipita sana naye akapata zawadi mzomzo kutoka kwa wazazi na serikali.
- Neema anasoma hadi chuo kikuu na kufuzu vyema ,anafanikiwa na kupata kazi.
- Neema anawajengea nyumba ,anawaajiria wazazi wake wafanyikazi wa kuwasaidia nyumbani na kuwanunulia jiko la gesi hali inayowapa furaha nyingi.
- kuna hali ya kutoelewana kati ya Bunju na Neema kutokana na masomo yake Lemi kwani kulingana na Bunju amerudi nyuma.
- Bunju na Neema wanakosa kuelewana kutokana na mila ambazo kulingana na Neema zimepitwa na wakati .-mama mkwe kutolala kwa Bunju.
- Neema kulazwa hospitalini kwa muda wa mwezi mzima bila fahamu kutokana na ajali mbaya.
- Bunju anakasirishwa na Neema kwa kutoshirikishwa kuhusu mpango wa kumpeleka Sara nyumbani baada ya kupata nafuu
- Eleza muktadha wa dondoo hili . (alama 4)
- “...Tayari unakuwa umeonja seli.Hata wahudumu wenyewe hawana mlahaka mwema .amri na vitisho kama askari.Unashindwa kama uuguze moyo ama ugonjwa.Katika wodi hewa iliyojaaa harufu ya dawa imezagaa,vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zikagura.Yaani hali nzima haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora.matumaini yanadidimia .Tumaini lako unaliweka katika sala. ”
- Tambua toni mbili katika kifungu hiki (alama2)
- Toni ya kutamauka ~ Yaani hali nzima haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora.
- Toni ya huzuni ~ Matumaini yanadidimia. Tumaini lako unaliweka katika sala.
- Tambua aina moja ya taswira katika dondoo hili (alama2)
- Taswira mnuso ~ hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa
- Kando na taswira chambua vipengele vingine vya mtindo: (alama6)
- Utohozi ~ seli, shiti, wodi
- Tashbihi ~ amri na vitisho kama askari
- Nahau ~ vitanda vimesalimu amri
- Tashihisi ~ vitanda vimesalimu amri, shiti zikagura.
- Fafanua namna mandhari ya dondoo hili yalivyochangia kujenga Tamthilia Bembea ya Maisha (alama10)
- Yanalinganisha huduma duni za afya kijijini na huduma bora za afya mjini.
- Yanatusaidia kuelewa maudhui ya kutowajibika kupitia wahudumu wa hospitalini za mjini.
- Yanachimuza maudhui ya uongozi mbaya hospitalini.
- Yanachangia katika kuonyesha sifa za wahudumu wa hospitalini.
- Yanachangia katika kuonyesha sifa za wahudumu wa hospitali za nyumbani (wazembe, dhalimu)
- Yanachimuza matatizo yanayokumba hospitali za mashambani(uchafu, uhaba wa vitanda vizuri, shiti) Yanajenga mtirirko wa vitushi Sara anapofika hospitalini kupata matibabu.
- Yanakuza sifa za Asna kama mdaku.
- Yanajenga sifa za Neema zinazjitokeza ~ mwadilifu.
- Yanakuza mtindo kupitia methali na dhihaka.
SEHEMU D: USHAIRI.
Jibu swali la 6 au la 7
- Tambua toni mbili katika kifungu hiki (alama2)
- SHAIRI LA KWANZA
- Tambua hadhira inayolengwa katika shairi hili. (alama 1)
- Wafanyikazi wa umma
- Maskini na matajiri
- Wadogo na wenye vyeo 1X1
- Huku ukitoa mfano,onyesha mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kutosheleza uhuru wake. (alama 3)
- tabdila – kutotowa/kutotoa
- inksari –ndo/ndio
- kuboronga sarufi/kufinyanga lugha-kujitegemea bora/bora kujitegemea 3X1
- Bainisha aina tatu za urudiaji zinazojitokeza katika utungo huu. (alama 3)
- Urudiaji wa neno/anafora-ushuru,taifa,bilashi,nk
- Urudiaji wa silabi-vina mf zo,ma
- Urudiaji wa sauti-o,a
- Urudiaji wa mshororo mf kibwagizo 3x1
- Eleza muundo wa ubeti wa sita. (alama 4)
- Una vipande viwili katika kila mshororo –ukwapi na utao
- Una mishororo minne
- Ubeti una kituo/kiishio
- Vina vya kati ni nge na vya mwisho ni zo isipokuwa kwenye kituo
- Mizani ni kumi na sita katika kila mshororo 4x1
- Andika ubeti wa nne katika lugha ya nathari/Tutumbi (alama 4)
- Si vizuri kuomba misaada ya kigeni kila wakati.
- Hivyo ni sawa na kuwa mateka
- Ni vyema kujitegemea kwa shida zetu
- Taifa haliwezi kuimarika bila ushuru
- Kwa kutolea mfano,taja mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika shairi hili. (alama 3)
- maswali ya balagha - vipi wangalihudumu
- jazanda/sitiari - twajifunga Kamba/kiguru
- tashbihi – ni kama kiguru
- takriri - bilashi,ushuru 3x1
- Weka shairi hili katika bahari yake ukirejelea : (alama 2)
- Vipande - Mathnawi
- Vina- ukaraguni 2X1
- Tambua hadhira inayolengwa katika shairi hili. (alama 1)
- SHAIRI LA PILI
- Haizingati idadi kwa mistari/mishororo katika kila ubeti.
- Idadi ya vipande hailingani katika mstari.
- Halizingatii mpangilio maalum wa vina.
- Halizingatii ulinganifu wa mizani katika kila mstari.
- Idadi ya vipande vya mishororo ni sawa.
- Halizingatii ukamilifu wa mishororo
- Utamaushi
- Mwalimu hathaminiwi – anaitwa bure/duni
- Mwalimu analewa na kupepesuka barabarani.
- Watoto kumcheka mwalimu wao apitapo.
- Viatu vya mwalimu kuisha visigino
- Sidiria ya mwalimu ni chakavu.
- Mwlaimu hawezi kumudu bei hya marashi baada ya kustaafu.
- Mwalimu atakufa na kuzikwa bila kusherekewa.
- Hata mlevi anamdharau mwalimu
- Mshahara duni. (Zozote 4 x 1 = 4)
- Jinsi mwalimu anapaswa kulaumiwa
- Yeye ndiye anatunga wimbo wa kuwasifu viongozi wasiotaka kubadilisha taaluma yake.
- Yeye ni mwoga – Anajikunja kama jongoo.
- Walimu hawana umoja.
-
- Nafsineni - Mwalimu
- Toni-utamaushi(kutaja al.1, mfano-al.1)
-
- Usambamba-Utafundisha tena
- Sikilizeni
- Jazanda –Bure, chacha,Mkia wa mbuzi
SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
-
- Bainisha kipera cha utungo huu. Thibitisha. (alama 2)
- Bembelezi / bembea / pembejezi
- Unawaliwaza na kuwabembeleza watoto walale auwanyamazewanapolia.
- Eleza ujumbe unaofumbwa katika wimbo huu. (alama 5)
- Kuhimiza uwajibikaji – nafsi neni kumpikia mwanawe ubwabwa
- Kueleza ugumu wa maisha / umaskini / ukilia wanikumbusha ukiwa wa baba na mama
- Nmafsi neni kukatiziwa elimu – ilimu kunikatizia
- Nafsineni kulazimishiwa ndoa – baba na mama kupokea ng’ombe na mbuzi
- Kuwepo kwa vurugu – lavunjavunja vikombe
- Ukosefu wa usingizi – languruma kama gombe.
- Tambua mbinu za kifani ambazo zimetumiwa kuwasilisha utungo huu. (alama 3)
- Tashbihi – languruma kama gombe
- Takriri/uradidi – ulale,ukiwa,nakuchombeza,
- Taswira - Languruma kama gombe
- Kinaya – wazazi kumwachisha shule nasfuineni na kumwoza.
- Bainisha shughuli mojamoja ya kijamii na ya kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utungo huu. (alama 2)
- Kijamii – ndoa – kunioza dume kongwe
- Kiuchumi–ufugaji ;languruma kama gombe
- Unakusudia kukusanya data kuhusu kipera hiki. Eleza manufaa manne ya kutumia mahojiano. (alama 4)
- Kwa vile mtafiti anakabiliana namhojiwa ana kwa ana ni rahisi kupata habari za ana kwa ana na za kutegemeka.
- Mbinu au sifa za uwasilishaji kama vile; Toni, utendaji, sauti, ishara za uso kubainika kwa mtafiti na hivyo kuimarisha kuelewa kwake.
- Mtafiti anaweza kumfafanulia mhojiwa habari na kuweza kupata data inayoaminika
- Mtafiti anaweza kubadilisha maswali au mtindo wa kuyauliza kulingana na kiwango cha elimu cha mhojiwa; lugha yake mhojiwa na mengine mengi
- Mtafiti anaweza kutambua iwapo mhojiwa anatoa habari zisizo za kweli.
- Kipera hiki kinazidi kufifia katika jamii yako. Fafanua njia nne ambazo jamii ya kisasa inaweza kutumia kukuza na kuendeleza kipera hiki. (alama 4)
- Jamii inafundisha kipera katika taasisi mbalimbali za elimu kama vile shule ya msingi, vya upili na vyuo vikuu.
- Kuhimiza wataalamu kujihusisha na usomaji na utafiti wa kipera hiki.
- Kuhakikisha kuwa kipera hiki kimepewa nafasi inayostahili katika mfumo wa elimu. kwa mfano kinahusishwa katika tamasha za muziki na drama zinazohusisha taasisi mbalimbali za elimu
- Wanasarakasi wa kisasa wanaendeleza usanii wa kipera hiki.
- Jamii ya kisasa inatumia teknolojia ya habari na mawasiliano k.v Runinga, tarakilishi na redio kuendeleza utendaji wa kipera maathalan kuna vipindi mbalimbali vya watoto nidhazautangazaji
- Watafiti wa fasihi simulizi wanaendelea kukifanyia kipera utafiti, kuandika na kurekodi viperavya fasihisimulizi
- Kipera hiki kinaendelezwa katika jamii za kisasa.
- Bainisha kipera cha utungo huu. Thibitisha. (alama 2)
Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Lanjet Joint Mock Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students