Kiswahili - KCPE 2021 Prediction Set 3 (Questions and Answers)

Share via Whatsapp

Chagua jibu lifaalo zaidi kujazia mapengo 1-15

Mila na __1__ zilizopitwa na __2__ zinafaa kutupiliwa __3__ na kuzikwa __4__kaburi la __5__, __6__wa mabinti ni dondo __7__ katika jamii kadha zinazoishi katika maeneo __8__ humu nchini. Kusema __9__ ni jambo la kukera na kukereketa kuona mambo haya yakifanyika katika karne hii

kisw set 3 q1 9

___10___ wanapopelekwa __11__ hukutana na kisu cha __12__ ilihali nao magashi hupelekwa __13__ ambako hushauriwa na masomo na __14__ ambao huwafunza kuhusu __15__ za nyumbani.

kisw set 3 q10 15

  1. Jibu kwa maamkuzi sahihi
    Profesa Wangari Mathai alipewa mkono wa ___ kwa kushinda tuzo ya Nobel
    A. Jahani
    B. Tanzia
    C. Tahania                         
    D. Faraja
  2. Bainisha matumizi ya 'ki'
    Kijoka kilikiuma kijiti cha kijumba cha kienyeji.
    A. udogo, kielelezi, ngeli
    B. ngeli, udogo, kielezi
    C. udogo, ngeli, kielezi
    D. ngeli, kielezi, udogo
  3. Wanawake walioolewa na mume mmoja huitana mkemwenza ilhali sisi huwaita
    A. mhavile
    B. mitara
    C. watawa                         
    D. vinyere
  4. Kikembe cha fisi ni kikuto nacho cha popo ni
    A. kipopo
    B. kidue
    C. kipura                           
    D. kipongea
  5. Semi iliyopigiwa mstari ina maana gani?
    Maswali tuliyofanya yalikuwa mswaki
    A. yalikuwa mazito
    B. yalikosa majibu
    C. yalikuwa magumu
    D. yalikuwa rahisi
  6. Chagua orodha yeneye vivumishi vya sifa ambishi
    A. Nadhifu, sita bora
    B. Jeme, hariri, kubwa
    C. imani, zuri, saba
    D. cheka, upendo, safi
  7. kanusha sentensi hii: Kusoma kwake kungefaa
    A. kusoma kwake kusingefaa
    B. kutosoma kwake kusingefaa
    C. kusoma kwake hakufai
    D. kutosoma kwake kusingefaa
  8. Mahali maalum ambapo vyungu na matafali huchomewa huitwaje?
    A. meko
    B. choto
    C. joko                              
    D. jirafu
  9. Maumbo haya ni
    maumbo kisw set 3q24.png
    A. haram, kistari, hori
    B. haram, tao, mche
    C. hilali, tao, kihori
    D. hilali, upinde, mche mraba
  10. Vidole vya mguu huitwaje?
    A. viganja
    B. vitanga
    C. viano                            
    D. vitengele
  11. Ukiona amabari na zinduna I papo
    Kiambishi kilichopigiwa mstari ni kiambishi cha aina gani?
    A. kimilikishi
    B. kivumishi
    C. kihusishi                       
    D. kiwakilishi
  12. Wanafunzi walisoma vitabu vichache maneno yaliyopigwa mistari ni
    A. Nomino, kiclezi
    B. Kitenzi kivumishi
    C. Kitenzi, sifa
    D. Kitenzi kivumishi idadi
  13. Mtoto ambaye angali tumboni na bado hajazaliwa huitwaje?
    A. kimwana
    B. mwanaserere
    C. kiduchu
    D. kijusi
  14. Chagua sentensi inayoonyesha 'ka' ya kusudi?
    A. Alienda msikitini na akasali
    B. Alisoma, akalaja kanywa na akalala
    C. walikaa, wakaenda zao wakasahaulika
    D. Aliadhibiwa na wa wazazi akatoroka
  15. Maradhi ya watoto ya kutokuwa na afya njema kutokana na kukosa lishe au chakula bora ni_
    A. Surua
    B. Unyafuzi
    C. ukosadisha                    
    D. Waba

Soma habari hii kisha ujibu maswali 31- 40

Mapinduzi yaliyotokea nchini Burundi ambapo jeshi lilitangaza kumpindua Rais Pierr Nkurunziza ni ya kushtua na hata kusikitisha. Lakini kutokana na nia ya kuendelea kukwamilia madaraka, rais huyo aliyetaka kuchaguliwa kwa awamu ya tatu kinyume na katiba ya nchi yake, wanajeshi hawakuwa na budi ila kumwondoa. Bw Nkurunziza alijaribu kujitetea kwamba ingawa katiba ya Burudi inakataza mtu kuwania uraisi zaidi ya vipindi viwili, kipindi cha kwanza alifanya kuteuliwa tu.

Madai yake yaliwakera watu wengi wanaoheshimu demokrasia. Msimamo wa Bw Nkurunziza umeonekana kujitokeza hata humu nchini, ambapo viongozi wamekuwa wakisisitiza kutaka kukwamia maklakani, hata baada ya kuhusishwa katika maovu ya aina mbalimbali. Kwa mfano Raisi Uhuru Kenyatta alipowalilisha orodha ya watu wanaoshukiwa kuhusika na ufisadi, magavana walijitokeza na kutangaza kwamba hawako tayari kujiuzulu.

Walionelea heri wachunguzwe wakiwa mamlakani, huku wakidai kwamba katiba haitoi nafasi ya wao kuchukua hatua kama hiyo. Inavyofahamika ni kuwa mshukiwa yeyote wa ufisadi ambaye alichaguliwa na wananchi anapaswa kukaa kando na kuruhusu uchunguzi usioegemea upande wowote ufanywe. Kuendelea kukaa uongozini na kujipiga kifua kwamba mtu haendi popote kunatoa picha mbaya. Hata kuna wakati baadhi ya wanasiasa humu nchini walisikika wakisema ni heri wafe kuliko kujiuzulu.

Tunapojifunza kutokana na ukaidi wa Bw Nkurunziza, tunamwomba Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine wa Afrika Mashariki wanaokutana nchini Tanzania, wamshauri ajivue mamlaka na kukubali uamuzi wa jeshi la nchi yake.

Burundi inafahamika kwa historia ya mwaka 1993 ambapo rais wake Melchior Ndadaye alikumbana na jaribio la kupinduliwa na alipokaidi hatua ya jeshi, akauawa.

  1. Rais Nkurunziza alipinduliwa, hivi ni kusema kuwa?
    A. alijiondoa uongozini
    B. alingatuliwa kutoka mamlakani
    C. alijingatua kutoka uongozini
    D. alikaidi mapinduzi
  2. Sababu za kupinduliwa kwa rais huyu ni?
    A. ukosefu wa utawala bora
    B. kutaka kuendelea kuongoza katika awamu ya pili
    C. kukosa kusitisha uongozi uongozi wake baada ya awamu zake kuisha
    D. kukosa kukithi haja za watu wake
  3. Kiongozi huyu Nkurunziza anajitetea kwa madai kuwa?
    A. hakupewa muda wa kutosha
    B. muda wake haukuwa umeisha
    C. alikuwa kiongozi wa kudumu
    D. katika awamu ya kwanza aliteuliwa
  4. Viongozi humu nchini wana mazoea gani?
    A. ya kwamia uongozini
    B. kukubali kushindwa
    C. kutokwania uongozini
    D. ya uongozi mzuri
  5. Kulingana na habari hii, Magarana walionelea ni heri?
    A. wajiondoe katika kazi
    B. wafungiliwe mashtaka
    C. wachunguzwe wakiwa mamlakani
    D. wasichunguzwe wala kushtakiwa
  6. Semi kujipiga kifure ina maana ya?
    A. kujipendelea zaidi
    B. kujidai mbele za watu
    C. kutishia maisha
    D. kuwa na gere
  7. Kisawe cha neneo ufisadi kinahusisha haya ytoe isipokuwa?
    A. Chirimiri
    B. Chauchau
    C. Utapeli
    D. Kuzuka mbuyu
  8. Raisi Nkurunziza aliondolewa mamlakani na nani?
    A. Wananchi wake
    B. viongozi ambao walimchukia
    C. wananjeshi wa nchi jirani
    D. wanajeshi wa nchi aliyoongoza
  9. Swala la viongozi pupinduliwa nchini Burundi
    A. halijawahi kutokea kamwe
    B. hutokea mara kwa mara
    C. lime wahi kutokea tena hapo awali
    D. huwa ni jambo la kawaida
  10. Habari hii inaelezea kuhusu
    A. Raisi wa Burundi
    B. Historia ya inchi ya Burundi
    C. Viongozi wa kiimla nchini Burundi
    D. Mapinduzi ya serikali ya Burundi

Soma habari hii kisha ujibu maswali 41-50

Pamoja na hadhi na umaarufu wa kiswahili, bado lugha hii inakumbana na matatizo makubwa ya dhana na matumizi sahihi. Bado kuna baadhi ya watu wanaonasibisha Kiswahili na dini ya Kiislamu na hili limekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwa watumiaji wake. Pia kuna upinzani mkubwa kutoka katika lugha ambazo zimekwisha kujitanua katika dunia kama vile Kiingerza, Kifaransa, Kihispania, Kijerumani, Kichina, Kireno na Kiarabu. Watumiaji au watu wenye asili ya lugha hizo wanakipiga vita Kiswahili wakihofia kuwa wasipofanya hivyo kitazimeza lugha zao.

Kudharauliwa kwa lugha ya Kiswahili na kupigiwa chapuo kwa lugha za kigeni kwamba ndizo pekee zinazofaa kutumiwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kuwa zina hadhi ni changamoto kubwa. Kuna kasumba mbaya na mtazamo hasi kuhusu Kiswahili ambao unawafanya Wakenya kukitukuza na kushabikia zaidi Kiingereza ni sawa na lugha nyingine tu. Huku tukichunguza nafasi ya Kiswahili katika mfumo wa elimu nchini Kenya, ni vyema tukumbuke kuwa mfumo wa elimu wa nchi yoyote inayotegemea lugha ya kigeni hasa lugha ya waliokuwa watawala wao wa kikoloni huendeleza maadili ya kigeni na utegemezi.

Ingawa kwa sababu ya utandawazi, lugha huathiriana duniani kote, lugha za kigeni katika mfumo wa elimu hunuia kuendeleza mila na desturi za kigeni ambazo nyingi yazo haziambatani wala kulingana na matarajio na mahitaji ya kimaendeleo ya nchi kama ya kenya. Kwa hivyo, ni muhimu kwa wataalamu, watafiti na wasomi wa lugha ya Kiswahili kujaribu kuipa nafasi inayostahiki lugha hii katika mfumo wetu wa elimu. Njia mojawapo ya kufanikisha malengo ya elimu katika nchi yoyote ile iwayo.

Kucheleweshwa kwa maamuzi ya sera ya kukipa hadhi Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia na lugha funzwa inayotahiniwa katika nyanja zote za elimu ni pigo kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya Kiswahili. hali ya Wakenya kuwa nyuma katika kufanya tafiti mbalimbali kuhusu vipengele muhimu vya fasihi na simu katika Kiswahili ili kuona ni jinsi gani tunaweza kufunguka kiakili na kufahamu umuhimu wa kuwa na lugha ya Kiswahili ni pingamizi nyingine. Uchumi mdogo wa nchi yetu.

  1. Kwa mujibu wa makala haya Kiswahili kinakumbwa na matatizo makubwa ya?
    A. lugha nyingi pinzani
    B. mawazo kuhusu matumizi sahili
    C. waja wanaotumia lugha kivolaya
    D. lugha za msimba
  2. Watu wengi husababisha lugha ya Kiswahili na?
    A. lugha ya kiarabu
    B. lugha za kibantu
    C. dini ya kiislamu
    D. wafuasi wa dini ya kiislamu
  3. Lugha duniani ambazo tayari zimekwishajitamua ni zote hizi isipokuwa?
    A. Kifaranja
    B. kihabeshi
    C. kijerumani                    
    D. kireno
  4. Wanaokipinga Kiswahili ni wale ambao?
    A. hawakielewi Kiswahili
    B. wanao lazimika kuzungumza lugha hii
    C. wasioelewa sheria na kanuni zake
    D. wenye kiherehere kuwa lugha zao zitamezwa
  5. Mtazamo hasi kuhusu Kiswahili ni?
    ule wenye dhana aali
    B. ule wenye dhana mbili
    C. usio na dhana mbaya
    D. husiano unaoleweka na wengi
  6. Lugha ya kigeni katika mfumo wa elimu
    husaidia wengine katika nchi ile
    B. huboresha elimu kwa wakazi
    C. huendeleza mila na desturi za ughaibuni
    D. huleta maendeleo ya kielimu
  7. Ni kina nani wanaoshauriwa na mwandishi kuhusika katika kukipa Kiswahili nafasi inayostahiki?
    A. wenyeji, wageni na wakoloni
    B. watafiti, wageni na wenyeji
    C. watalamu, watafiti na wasomi
    D. wasomi, wageni na wazalendo
  8. Kiswahili hutumika katika shughuli hizi zote isipokuwa?
    A. kuimba wimbo wa taifa
    B. bungeni
    C. mahakamani
    D. katika somo la kingenge
  9. Mwandishi analalamika kuwa wakenya hawafanyi nini kuhusiana na lugha?
    A. hawafanyi utafiti
    B. hawakizungumzi Kiswahili
    C. huchanganya lugha ya Kiswahili na za Kigeni
    D. hukiboronga Kiswahili
  10. Makala haya yameeleza kuhusu
    A. Lugha rasmi duniani
    B. Lugha za kigeni
    C. Uwezekano wa kiswahili kutwezwa
    D. Nafasi ya lugha ya Kiswahili nchini na ulimwenguni

INSHA

Andika insha itakayomalizia kwa maneno haya.

......kwa kweli huo ulikuwa moto wa kuotea mbali.

 



MAJIBU

kiswa set 3 ms

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - KCPE 2021 Prediction Set 3 (Questions and Answers).


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest