MAAGIZO
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Insha zote sharti ziandikwe katika kijitabu cha majibu ulichopewa.
- Lazima.
Wewe ni mhariri wa gazeti la ‘Pevuka’. Andika tahariri kuhusu kiini cha mauaji katika ndoa na hatua za kukabiliana na janga hili. - Janga la Korona limeathiri jamii kwa chanya na hasi. Jadili.
- Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
- Endeleza kisa hiki.
“Nisamehe baba.Nilipotoshwa.Sitarudia kitendo kama hiki cha kufedhehesha tena. Sitakaidi tena makanyo yako. Nilijikuta nimepiga magoti mbele ya babangu
MARKING SCHEME
-
- Kichwa :Jina la gazeti, tarehe na mada chini ya kichwa.
- Utangulizi :Ufafanuzi mfupi wa mada.
- Mwili :Maelezo kamili ya maudhui.
- Hitimisho :
- jina la kampuni inayomiliki gazeti.
- majina ya wahariri na vyeo vyao.
Maudhui:
Sababu za mauaji katika ndoa.- Tamaa ya mali.
- Mfadhaiko wa moyo/msongo wa kimawazo.
- Matumizi ya dawa za kulevya.
- Ukosefu wa ushauri nasaha.
- Ukosefu wa uaminifu katika ndoa.
- Wanandoa kutelekeza majukumu ya kinyumba.
- Ubadhirifu.
- Dini/ushirikina/Imani potovu za kidini.
- Kutotimiza/kutoshughulikia mahitaji ya kimsingi ya familia kama lishe, makazi, karo na kadhalika.
- Taasubi ya kiume/kike/utamaduni.
Suluhisho- Ushauri nasaha.
- Kuelimisha jamii kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto katika ndoa.
- Kuimarisha demokrasia katika kitendo cha familia.
- Kuimarisha hali ya kiuchumi kwa wanandoa.
- Hatua kali za kisheria kwa wanaotekeleza unyama huu.
- Kukabiliana na dawa za kulevya.
- Viongozi wa kidini kuwajibikia majukumu ya kuelekeza wanajamii.
- Hili ni swali la mjadala.
Mtahiniwa ataje hoja za kuunga na kupinga kuunga.
Hasara/Athari hasi- Shule zilifungwa ili kukabiliana na hali hii.
- Watu walifariki.
- Hoteli zilifungwa ili kukabiliana na ugonjwa huu.
- Usafiri uliathirika kwani baadhi ya maeneo yalipigwa marufuku.
- Watu walipoteza kazi kwani wengi wao ajira zao zilifungwa.
- Msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ulishuhudiwa.
- Mikutano ya hadhara ilipigwa marufuko.
- Uhuru wa kuabudu uliathirika kwani maabadi yalifungwa kwa muda.
- Amri ya kutotoka usiku ili kukabiliana na ugonjwa huu iliwekwa.
- Kalenda ya Elimu ilibadilika kwani wanafunzi walikaa sana nyumbani.
- Unyanyapaa ulishuhudiwa kwa kutengwa kwa wale waliokuwa na ugonjwa huo.
- Mwingiliano na uhusiano wa wanajamii uliathirika kwa amri ya kutosalimiana kwa mikono na kutokusanyika kila mara.
Faida/mazuri- Teknolijia iliweza kuimarika
- Watu walijifunza njia badala za kufanya kazi
- Wazazi na watoto walipata nafasi nzuri ya kutangamana na wengine
- Sekta ya Afya iliweza kuimarika kwani ilibidi hospitali zikarabatiwe na zingine kujengwa upya
- Juhudi za utafiti zilichacha ili kutafuta tiba/Chanjo
- Biashara kama vile kuuza barakoa zilichacha
- Usafi uliimarika hasa kwa ushauri wa kunawa mikono
- Mashirika ya kibinadamu yaliweza kuonyesha mchango wao kwa kuwasaidia wale walioathirika.
- Wanafunzi na walimu walipata nafasi ya kupumzika
- Talanta zilikuzwa kwani wengi walitumia muda wa kutofanya kazi kupalilia vipawa vyao.
Tanbihi
- Mtahini ahakika hoja za wanafunzi.
- Mtahiniwa lazima aonyeshe pande zote mbili.
- Atoe msimamo wake.
- Akishughulikia upande mmoja atunzwe. (x/10)
-
- Mtahiniwa alenge maana kuwa anayefanya jambo la kuumiza wengi huenda akaumiza mtu wao.
- Alenge kuonyesha si vyema kufanya jambo la kuumiza wengi.
- Aonyeshe pande mbili za methali.
- Akionyesha upande mmoja atunzwe. x/10.
- Akipotoka kimaudhui asitunzwe Zaidi ya 2/20.
-
- Kisa kionyeshe kuwa alikuwa amekanywa akakaidi.
- Aonyeshe kuwa alipotoshwa.
- Asipotumia mbinu rejeshi amepotoka na asituzwe Zaidi ya alama tatu.
- Asipoonyesha kuwa alikuwa amekanywa amepotoshwa na sababu za kutokwa na damu amepungukiwa na asipishe alama kumi.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Pavement Mock Exams 2021/2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students