- UFAHAMU (Alama 10)
Soma hadithi kisha ujibu maswali yanayofuata. (Alama 5)
Mbuni ni ndege wa porini. Anatupa mayai na nyama.Yai lake ni kubwa sana. Mbuni ni ndege mkubwa kuliko ndege wote.
Ni mrefu sana. Ana shingo ndefu na miguu mirefu. Mbuni ana mbio sana. Pia hawezi kuruka juu.- Mbuni anatupa ____ na _____ (alama 2)
- Mbuni ana ____ ndefu na _____ mirefu. (alama 2)
- Mbuni hawezi kufanya nini? _____ (alama 1)
Soma kisa kifuatacho kisha ujibu maswali. (Alama 5)
Simba na Swara waliishi pamoja. Walipenda usafi. Walikula chakula safi, walilala pahali safi na walivaa nguo safi. Pia waliosha miili yao kwa maji safi. Walihakikisha mazingira yao ni safi. Walifagia nyumba zao.Waliokota taka na kuzichoma. Magonjwa kwao yalikuwa ni hadithi tu!- Simba na Swara walipenda ______ (alama 1)
- Taja mambo mawili ambayo wanyama walifanya ili mazingira yao yawe safi. (alama 2)
- Wanyama waliosha ____ yao kwa maji safi. (alama 1)
- Usafi huleta _____ (ugonjwa, afya bora) (alama 1)
- SARUFI (Alama 15)
- Andika kwa herufi kubwa. (Alama 3)
- barabara _____
- gharama _____
- nyumbani _____
- Tenganisha silabi. (alama 2)
- Kipepeo ____
- Thelathini ____
- Chora na upake rangi taa za trafiki: (alama 3)
- Tumia 'huyo' au 'hao' kujaza nafasi: (alama 2)
- Mnyama _____ ni hatari sana.
- Wanafunzi ____ wameandika barua.
- Tafuta maneno yenye sauti/p/kwenye jedwali. (alama 3)
- Ambatanisha neno na maana yake. (alama 2)
Neno Maana
Nauli Mtu au watu wanaosafiri.
Abiria Pesa anazolipa mtu anayesafiri. - KUANDIKA (Alama 10)
Andika sentensi tano utakazosomewa na mwalimu.
- Andika kwa herufi kubwa. (Alama 3)
MPANGO WA KUASHIRIA
-
-
- mayai, nyama
- shingo, miguu
- hawezi kuruka juu
-
- usafi
-
- walifagia nyumba zao
- waliokota taka na kuzichoma
- miili
- afya bora
-
-
-
- BARABARA
- GHARAMA
- NYUMBANI
-
- KI-PE-PE-O
- TH-E-LA-TH-I-NI
- Kuelekezwa na mwalimu
-
- huyo
- hao
-
- punda
- pika
- pale
- pesa
- pata
- paka
- pita
- Nauli - Pesa anazolipa mtu anayesafiri
Abiria - Mtu au watu wanaosafiri - Kuelekezwa na mwalimu
-
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Download Shughuli za Kiswahili Ufahamu, Sarufi na Kuandika Questions and Answers - CBC Grade 2 End Term 2 Exams 2023 Set 1.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students