Kiswahili - Grade 7 Curriculum Designs

Rate this item
(17 votes)

WIZARA YA ELIMU
MTAALA WA DARAJA YA AWALI YA SHULE YA UPILI
GREDI YA 7
KISWAHILI

 

MGAO WA VIPINDI

  Somo Vipindi kwa wiki
(Dakika 40 kwa kipindi)
1 English 5
2 Kiswahili/KSL 4
3 Mathematics 5
4 Integrated Science 4
5 Health Education 2
6 Pre-Technical and Pre-Career Education 5
7 Social Studies 3
8 Religious Education (CRE/IRE/HRE) 2
9 Business Studies 3
10 Agriculture 3
11 Life Skills Education 1
12 Physical Education and Sports 2
13 Optional Subject 3
14 Optional Subject 3
  jumla 45

MALENGO YA KITAIFA YA ELIMU NCHINI KENYA
Elimu nchini Kenya inatakiwa: Kukuza na kustawisha utaifa, uzalendo na kuendeleza umoja wa kitaifa.
Nchini Kenya kuna jamii zenye mila, dini na tamaduni mbalimbali lakini tofauti hizi hazifai kuzitenganisha. Lazima waweze kuishi na kutangamana kama Wakenya. Elimu ina jukumu kuu la kuwezesha vijana kujenga hisia za uzalendo na utaifa kwa kuondoa mivutano na kukuza mielekeo chanya ya kuheshimiana itakayowezesha jamii kuishi pamoja kwa utangamano na kujenga uzalendo ili kuchangia uhai wa taifa.

  1.  Kukidhi mahitaji ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na viwanda yanayochangia maendeleo ya kitaifa.
    Elimu inafaa kuwaandaa vijana wa nchi kutekeleza wajibu wenye umuhimu katika maisha nchini.
    1. Mahitaji ya kijamii
      Elimu nchini Kenya lazima iwatayarishe vijana kwa mabadiliko ya mielekeo na mahusiano ambayo yanahitajika kwa maendeleo ya haraka ya uchumi wa kisasa. Kuna uwezekano
    2. wa kuwa na mapinduzi kimyakimya ya kijamii kutokana na maendeleo ya haraka ya usasa. Elimu inapaswa kuwasaidia vijana kujirekekebisha kutokana na mabadiliko haya.
    3. Mahitaji ya kiuchumi
      Elimu nchini Kenya inafaa kukuza raia walio na stadi, maarifa, ujuzi na sifa za kibinafsi zinazohitajika kuhimili maendeleo ya kiuchumi. Kenya inajenga uchumi huru na wa kisasa ambao unahitaji wafanyakazi wa kutosha, walio na maarifa yanayohitajika na wa humu nchini.
    4. Mahitaji ya kiteknolojia na ya kiviwanda
      Elimu nchini Kenya inafaa kuwapa vijana stadi na mielekeo inayohitajika kwa maendeleo ya kiviwanda.
      Kenya inatambua mabadiliko ya haraka ya kiviwanda na kiteknolojia yanayofanyika, hasa katika ulimwengu ulioendelea. Tunaweza kuwa sehemu ya maendeleo haya ikiwa mfumo wetu wa elimu utalenga kimakusudi maarifa, stadi na mielekeo itakayotayarisha vijana kwa mabadiliko ya yanayoendelea ulimwenguni.
  2. Kutoa nafasi ya kujiendeleza na kujitosheleza.
    Elimu inapaswa kumwezesha mtu kutambua, kukuza na kuimarisha kipawa chake ili aweze kujiendeleza na kujitosheleza. Inafaa kuwawezesha watoto kukuza uwezo wao. Kipengele muhimu cha maendeleo ya kibinafsi ni ujenzi wa tabia ifaayo.
  3. Kuwawezesha wananchi kuimarisha maadili na amali za kijamii na kidini.
    Elimu inakusudiwa kukuza maarifa, stadi na mielekeo itakayoimarisha upataji wa maadili na kuwasaidia watoto kukua wakiwa wenye nidhamu, wanaojitegemea na raia wakamilifu.
  4.  Kuimarisha usawa wa kijamii na uwajibikaji.
    Usawa wa kijamii kwa mfano, usawa wa kijinsia huimarika watu wa jamii na jinsia zote wanapopata elimu sawa.
    Elimu inafaa ikuze usawa wa kijamii na uwajibikaji wa kijamii kutokana na mfumo wa elimu unaowezesha fursa sawa ya elimu kwa wote. Inafaa kuwapa watoto wote fursa mbalimbali na zilizo na changamoto kwa mazoezi ya pamoja na ushirika katika huduma za kijamii bila kujali jinsia, uwezo au mazingira ya kijiografia.
  5. Kukuza uthamini wa tamaduni mbalimbali nchini Kenya.
    Elimu inafaa kutoa nafasi kwa wanaosoma kuelewa, kuthamini, kukuza na kudumisha tamaduni faafu na kudondoa zile potofu kulingana na jamii ya wakati uliopo ili kujenga jamii ya kisasa.
  6. Kuimarisha utambuzi wa uhusiano wa kimataifa na kukuza mwelekeo chanya kwa mataifa mengine.
    Kenya kama nchi mojawapo ya jamii ya kimataifa inakusudia elimu iwaelekeze Wakenya kutambua na kuthamini mahusiano ya kimataifa kwa kuzingatia mikataba, uwajibikaji, haki na manufaa yanayoambatana na ushirika huo.
  7. Kustawisha mwelekeo chanya kuhusu afya bora na uhifadhi wa mazingira.
    Elimu inakusudiwa kujenga mielekeo ifaayo miongoni mwa vijana kuhusu udumishaji wa afya bora na mazingira kwa kujiepusha na mienendo inayoweza kudhuru afya ya mwili na akili. Elimu inafaa pia kuimarisha mielekeo chanya kuhusu ukuzaji na uhifadhi wa mazingira. Inafaa kuwaelekeza vijana wa Kenya kukubali haja ya mazingira safi.

MATOKEO YA KIWANGO CHA KATI CHA ELIMU YA MSINGI
Kufikia mwisho wa kiwango cha kati cha elimu mwanafunzi aweze:

  1. Kutumia ujuzi wa kusoma na kuandika, ujuzi wa kuhesabu na kufikiri kimantiki ifaavyo katika kujieleza.
  2. Kuwasiliana kikamilifu katika miktadha mbalimbali.
  3. Kudhihirisha ujuzi wa kijamii, kiimani na kimaadili kwa ajili ya mahusiano mema.
  4. Kutalii, kubadilisha, kusimamia na kutunza mazingira ifaavyo kwa ajili ya ujifunzaji na maendeleo endelevu.
  5. Kufanya usafi, kufuata kanuni zifaazo za usafi na lishe ili kuimarisha afya.
  6. Kudhihirisha mienendo ya kimaadili na kuonyesha uraia mwema kama wajibu wa kiraia.
  7. Kuonyesha ridhaa kwa mirathi mingi na tofauti ya kitamaduni nchini ili kuleta mshikamano wa kimahusiano.
  8. Kudhibiti masuala mtambuko katika jamii ifaavyo.
  9. Kutumia ujuzi wa kidijitali ifaavyo kwa madhumuni ya mawasiliano na ujifunzaji.

KAULI KIINI
Somo la Kiswahili litampa mwanafunzi wa daraja la awali la Shule ya Upili umilisi katika shughuli za kila siku. Umilisi huu utajengea haiba na uwezo wake wa kuwasiliana na kuhusiana katika jamii, kitaifa na kimataifa. Aidha, litamwendeleza kielimu na kumwandaa kwa ulimwengu wa kazi. Somo hili litampa mwanafunzi hamasa ya kumudu na kufurahia lugha na fasihi kwa kuzihusisha na tajiriba na mazingira yake. Hali kadhalika, litampa mwanafunzi maarifa ya kijamii na kitamaduni. Mwanafunzi ataweza kujieleza na vilevile kupata fursa ya kutoa huduma kwa jamii.

MATOKEO YA KIJUMLA YANAYOTARAJIWA KATIKA DARAJA YA AWALI YA SHULE YA UPILI
Kufikia mwisho wa daraja ya awali katika Shule ya Upili, mwanafunzi aweze:

  1. kujieleza ipasavyo kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwa njia ya maandishi na mazungumzo
  2. kuwasiliana ipasavyo katika miktadha mbalimbali ya kijamii
  3. kujenga desturi ya kusoma na kufasiri maandishi kwa ufasaha
  4. kutumia lugha kiubunifu kusimulia na kuandika tungo mbalimbali
  5. kushiriki katika shughuli za kijamii zinazochangia ujifunzaji
  6. kutumia teknolojia ipasavyo katika ujifunzaji na mawasiliano ili kukuza ujuzi wa kidijitali
  7. kutumia maadili yanayohitajika maishani kupitia stadi za lugha ya Kiswahili
  8. kufurahia na kuthamini lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi, ya taifa na kimataifa.
MADA 1.0 USAFI WA KIBINAFSI
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
1.1 Kusikiliza na Kuzungumza 1.1.1 Kusikiliza na Kujibu
(Vipindi 2)

Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:

  1. kutambua vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji wa mazungumzo
  2. kutambua vipengele vya kuzingatia katika kujibu mazungumzo
  3. kutumia vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kujibu mazungumzo
  4. kuchangamkia kushiriki mazungumzo katika miktadha mbalimbali.

Mwanafunzi aelekezwe:

  • kutambua vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza (k.v. kusikiliza kwa makini, kumtazama mzungumzaji kwa makini ili kupata ishara za uso, kutikisa kichwa kuonyesha kusikia kauli, kutumia maneno au vihisishi vya kumhimiza kuendelea kuzungumza (k.v ehe), kuepuka vizuizi vya mawasiliano (k.v. kutazama nje), kumtazama mzungumzaji ana kwa ana, n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua vipengele vya kuzingatia katika kujibu mazungumzo (k.v. kutumia lugha ya adabu, kutomkata kalima mzungumzaji, ubadilishanaji zamu ufaao, kujibu kwa kujikita katika kiini cha swali/mazungumzo, n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
    kusikiliza mazungumzo kuhusu suala lengwa katika kifaa cha kidijitali (k.v. simu, redio au vinasa sauti) huku akizingatia vipengele vya kuboresha usikilizaji wa mazungumzo
  • kusikiliza na kujibu mazungumzo (k.v kutoka kwa mwalimu, wenzake au kutoka kwenye vifaa vya kidijitali) ipasavyo
  • kuigiza mazungumzo (k.v. ya simu) kuhusu suala lengwa akiwa katika kikundi kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya kusikiliza na kujibu mazungumzo
  • kushiriki mazungumzo na mzazi au mlezi kuhusu suala lengwa kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya kusikiliza na kujibu mazungumzo.
  1. Je, unaposikiliza mazungumzo unapaswa kuzingatia nini ili kupata ujumbe unaowasilishwa?
  2. Unazingatia nini unapomjibu mtu katika mazungumzo?

Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa

  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoeleza kwa uwazi alichokisikiliza kuhusu suala lengwa kwa kuzingatia vipengele vifaavyo vya kujibia mazungumzo.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika mazungumzo kwenye kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kama vile simu, redio na vinasa sauti kusikilizia mazungumzo mbalimbali na kutambua vipengele vya kusikiliza na kuzungumza vilivyozingatiwa.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapopendekeza vipengele vya kuzingatia ili kuhakikisha usikilizaji faafu.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposikiliza mazungumzo na kuyajibu ipasavyo bila woga. Pia anapochangia katika shughuli ya kikundi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki mazungumzo na wenzake, mzazi au mlezi na kujifunza njia bora za kusikiliza na kujibu mazungumzo.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika shughuli za kikundi; pia anapoheshimu zamu ya wenzake katika mazungumzo.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapotunza vifaa vya kidijitali anavyotumia katika mazungumzo.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Usafi wa kibinafsi – mwanafunzi anaposikiliza, kushiriki na kuigiza mazungumzo kuhusu suala lengwa. Pia anapotumia ipasavyo vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kujibu mazungumzo.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – dhana ya kusikiliza na kujibu ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.
  • Science and Technology, Health Education na Home Science – usafi wa kibinafsi ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji wa mazungumzo. Anatambua kwa wepesi vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji wa mazungumzo. Anatambua vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji wa mazungumzo. Anatambua baadhi ya vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji wa mazungumzo. Anatambua, kwa kusaidiwa, baadhi ya vipengele vya kuzingatia katika usikilizaji wa mazungumzo.
Kuweza kutambua vipengele vya kuzingatia katika kujibu mazungumzo. Anatambua kwa urahisi vipengele vya kuzingatia katika kujibu mazungumzo. Anatambua vipengele vya kuzingatia katika kujibu mazungumzo. Anatambua baadhi ya vipengele vya kuzingatia katika kujibu mazungumzo. Anatambua baadhi ya vipengele vya kuzingatia katika kujibu mazungumzo kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kujibu mazungumzo. Anatumia kwa wepesi vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kujibu mazungumzo. Anatumia vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kujibu mazungumzo. Anatumia baadhi ya vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kujibu mazungumzo. Anatumia, kwa kusaidiwa, baadhi ya vipengele vifaavyo katika kusikiliza na kujibu mazungumzo.





Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi
1.2 Kusoma 1.2.1 Ufahamu wa Kifungu cha Simulizi
(Vipindi 2)

Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:

  1. kudondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu
  2. kupanga matukio yanavyofuatana katika kifungu cha ufahamu
  3. kufanya utabiri na ufasiri kutokana na kifungu cha ufahamu
  4. kueleza msamiati katika kifungu cha ufahamu
  5. kuchangamkia kusoma vifungu vya ufahamu ili kukuza uelewa wa habari.

Mwanafunzi aelekezwe:

  • kusoma kifungu cha ufahamu cha simulizi kwenye kitabu au kifaa cha kidijitali (k.v. redio, simu, n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kudondoa habari mahususi (k.v. nani, nini, wapi, lini, n.k.) katika kifungu cha ufahamu cha simulizi
  • kupanga matukio yanavyofuatana katika
    kifungu cha ufahamu cha simulizi akiwa peke yake au katika kikundi
  • kufanya utabiri na ufasiri kutokana na
    kifungu cha ufahamu cha simulizi alichosoma akiwa peke yake au katika kikundi
  • kueleza msamiati (k.v. maneno na nahau)
    katika kifungu cha ufahamu cha simulizi na kuueleza kwa kutumia kamusi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusoma vifungu simulizi mtandaoni au kwenye vitabu kuhusu suala lengwa akiwa na mwenzake au katika kikundi kisha atambue na kueleza maana za msamiati wa usafi wa kibinafsi kulingana na muktadha wa matumizi
    kumsomea mzazi au mlezi sentensi kuhusu usafi wa kibinafsi kisha wajadiliane maana za msamiati wa suala husika kimuktadha.
  1. Kwa nini tunasoma ufahamu?
  2. Je, ni mambo gani yanayoweza kukusaidia kuelewa kifungu cha ufahamu?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kudondoa habari mahususi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na mwenzake katika shughuli za kikundi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapotumia msamiati wa suala lengwa kwa usahihi katika muktadha maalum.
  • Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anapobashiri na kufasiri kutokana na kifungu cha ufahamu.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anaposakura mtandaoni na kusoma vifungu kuhusu suala lengwa.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapomsomea mzazi au mlezi kifungu na kuutambua msamiati wa suala lengwa.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi. Pia anapotunza vifaa vya kidijitali anavyotumia.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Usafi wa kibinafsi – mwanafunzi anaposoma matini kuhusu suala lengwa na kuzingatia ujumbe.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – kusoma kwa ufahamu ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.
  • Science and Technology, Health Education na Home Science – usafi wa kibinafsi ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kudondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu kwa urahisi. Anadondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa baadhi ya habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa baadhi ya habari mahususi katika kifungu cha ufahamu kwa kusaidiwa.
Kuweza kupanga matukio yanavyofuatana katika kifungu cha ufahamu. Anapanga matukio yanavyofuatana katika kifungu cha ufahamu kwa urahisi. Anapanga matukio yanavyofuatana katika kifungu cha ufahamu. Anapanga baadhi ya matukio yanavyofuatana katika kifungu cha ufahamu. Anapanga baadhi ya matukio yanavyofuatana katika kifungu cha ufahamu kwa kuelekezwa.
Kuweza kufanya utabiri na ufasiri kutokana na kifungu cha ufahamu. Anafanya utabiri na ufasiri kutokana na kifungu cha ufahamu kwa urahisi. Anafanya utabiri na ufasiri kutokana na kifungu cha ufahamu. Anafanya kwa kiasi utabiri na ufasiri kutokana na kifungu cha ufahamu. Anafanya kwa kiasi utabiri na ufasiri kutokana na kifungu cha ufahamu kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza msamiati katika kifungu cha ufahamu. Anaeleza msamiati katika kifungu cha ufahamu kwa urahisi. Anaeleza msamiati katika kifungu cha ufahamu. Anaeleza baadhi ya msamiati katika kifungu cha ufahamu. Anaeleza baadhi ya msamiati katika kifungu cha ufahamu kwa kusaidiwa.




Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi
1.3 Kuandika 1.3.1 Viakifishi
(Vipindi 2)

Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:

  1.  kutambua matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika maneno, sentensi na vifungu
  2. kutumia herufi kubwa na kikomo ipasavyo katika maneno, sentensi na vifungu
  3. kuonea fahari matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika maneno, sentensi na vifungu ili kufanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua matumizi ya herufi kubwa na kikomo (k.v. kutumia herufi kubwa kuanzia majina ya watu, mwanzoni mwa kila neno kuu katika anwani ya kitabu; kikomo mwishoni mwa sentensi ya taarifa n.k.) katika maneno, sentensi na vifungu kwenye matini andishi au za kidijitali akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuandika maneno, sentensi au vifungu kuhusu suala lengwa kwa kutumia herufi kubwa na kikomo ipasavyo akiwa peke yake au katika kikundi
  • kuandika kifungu kifupi kwa kuzingatia herufi kubwa na kikomo ipasavyo kwenye kifaa cha kidijitali (k.v. tarakilishi) na kuwasambazia wenzake kwenye mtandao ili wakitolee maoni
  • kushirikiana na wenzake kusahihisha kifungu kuhusu suala lengwa ambacho hakijatumia herufi kubwa na kikomo ipasavyo
  • kuwasomea wenzake kifungu alichoandika na kuwataka waandike maneno na sentensi zinazostahili kuwa na herufi kubwa na kikomo
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kutafiti mtandaoni au kwenye vitabu vya ziada kuhusu matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika maneno, sentensi na vifungu.
Herufi kubwa na kikomo hutumika vipi katika maandishi?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  •  Mawasiliano – mwanafunzi anapowasomea wenzake kifungu kwa ufasaha na anaposhiriki katika mijadala na wanafunzi wenzake na wazazi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kusahihisha vifungu.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia kifaa cha kidijitali kuandika kifungu na kukisambaza mtandaoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika vifungu vyenye matumizi yafaayo ya herufi kubwa na kikomo.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi wake kutafiti mtandaoni kuhusu matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika maneno, sentensi na vifungu.
  • Uwazaji kina – mwanafunzi anapotumia herufi kubwa na kikomo katika kifungu alichokiandika.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Usafi wa kibinafsi – mwanafunzi anapoandika kifungu kuhusu suala lengwa kwa kutumia herufi kubwa na kikomo ipasavyo.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – matumizi ya herufi kubwa na kikomo ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.
  • Integrated Science, Health Education na Home Science – usafi wa kibinafsi ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika maneno, sentensi na vifungu. Anatambua matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika maneno, sentensi na vifungu kwa urahisi. Anatambua matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika maneno, sentensi na vifungu. Anatambua matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika baadhi ya maneno, sentensi na sehemu za vifungu. Anatambua matumizi ya herufi kubwa na kikomo katika baadhi ya maneno, sentensi na sehemu za vifungu kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia herufi kubwa na kikomo ipasavyo katika maneno, sentensi na vifungu. Anatumia herufi kubwa na kikomo ipasavyo katika maneno, sentensi na vifungu kwa urahisi. Anatumia herufi kubwa na kikomo ipasavyo katika maneno, sentensi na vifungu.kubwa na kikomo ipasavyo katika maneno, sentensi na vifungu. Anatumia herufi kubwa na kubwa na kikomo ipasavyo katika baadhi ya maneno, sentensi na sehemu za vifungu. Anatumia herufi kikomo ipasavyo katika baadhi ya maneno, sentensi na sehemu za vifungu kwa kuelekezwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi
1.4 Sarufi 1.4.1 Nomino za Pekee na za Kawaida
(Vipindi 2)

Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:

  1. kutambua nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu
  2. kutambua aina za nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu
  3. kutumia nomino za pekee na za kawaida ipasavyo katika sentensi na vifungu
  4.  kuchangamkia matumizi ya nomino za pekee na za kawaida katika sentensi na vifungu ili kufanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua nomino za pekee (k.v. Kenya, Jumatatu, Kiptoo, Kisiwa chenye Hazina, n.k.) na za kawaida (k.v. mwanafunzi, kalamu, nyumba, mkeka, n.k.) kwenye orodha, sentensi na vifungu akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutaja aina za nomino za pekee (k.v. majina ya watu, siku za wiki, miezi ya mwaka, mito, nchi, anwani za vitabu, za magazeti na za majarida, n.k.) akiwa peke yake au na wenzake katika kikundi
  • kutenga nomino za pekee na za kawaida katika orodha ya maneno, sentensi au vifungu kwenye vitabu, tarakilishi, chati n.k. akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga sentensi au vifungu kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za pekee na za kawaida akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kumtajia mzazi au mlezi wake nomino za pekee (k.v. Mjomba Selemani, Inspekta Lama, Ziwa Naivasha, Mto Tana, n.k) na za kawaida (k.v. sabuni, maji, dodoki, mgomba, bustani, miti, n.k.) katika mazingira ya nyumbani.
  1. Ni vitu gani katika mazingira yako ambavyo ni nomino za pekee?
  2. Ni vitu gani katika mazingira yako ambavyo ni nomino za kawaida?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi akitumia nomino za pekee na za kawaida.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia kazi za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kutambua nomino za pekee na za kawaida.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuhusu suala lengwa akitumia nomino za pekee na za kawaida.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kutambua nomino za pekee na za kawaida kisha kuzitungia sentensi sahihi na vifungu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapomtajia mzazi au mlezi wake nomino za pekee katika mazingira ya nyumbani.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika shughuli za kikundi.
  • Amani – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kwa utulivu.
Masuala Mtambuko
  • Usafi wa kibinafsi – mwanafunzi anapoandika sentensi au kifungu kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za pekee na za kawaida.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – dhana ya nomino za pekee na za kawaida ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.
  • Integrated Science, Health Education na Home Science – usafi wa kibinafsi ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu. Anatambua kwa wepesi nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu. Anatambua nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu. Anatambua baadhi ya nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu. Anatambua baadhi ya nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua aina za nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu. Anatambua kwa wepesi aina za nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu. Anatambua aina za nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu. Anatambua baadhi ya aina za nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu. Anatambua baadhi ya aina za nomino za pekee na za kawaida kwenye orodha ya maneno, sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia nomino za pekee na za kawaida ipasavyo katika sentensi na vifungu. Anatumia nomino za pekee na za kawaida ipasavyo katika sentensi na vifungu kwa urahisi. Anatumia nomino za pekee na za kawaida ipasavyo katika sentensi na vifungu. Anatumia nomino za pekee na za kawaida ipasavyo katika baadhi ya sentensi na vifungu. Anatumia nomino za pekee na za kawaida ipasavyo katika baadhi ya sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.



MADA 2.0 LISHE BORA
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
2.1 Kusikiliza na Kuzungumza 2.1.1 Kusikiliza kwa Kina
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua sauti /dh/ na /th/ katika silabi na maneno
  2. kutamka sauti /dh/ na /th/ ipasavyo katika silabi na maneno
  3. kutumia maneno yenye sauti /dh/ na /th/ katika sentensi ili kuyafautisha kimaana.
  4. kuonea fahari matamshi bora ya sauti /dh/ na /th/ katika mazungumzo.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua sauti /dh/ na /th/ katika maneno na silabi (k.v dhamani/thamani; adhiri/athiri; dhibiti/thibiti, n.k.)
  • kutambua maneno yenye sauti /dh/ na /th/ katika matini andishi au za kidijitali na kuyatamka ipasavyo akiwa na wenzake
  • kutumia maneno yenye sauti /dh/ na /th/ kwenye sentensi ili kuyatofautisha kimaana katika kifaa cha kidijitali au katika vitabu akiwa na wenzake katika kikundi
  • kuunda vitanzandimi vinavyotumia sauti /dh/ na /th/ kwenye kifaa cha kidijitali au katika vitabu akiwa na wenzake katika kikundi
  • kusoma vitanzandimi alivyounda akizingatia matamshi bora ya sauti /dh/ na /th/
  • kushirikisha mzazi au mlezi wake kusoma kifungu kuhusu suala lengwa akizingatia matamshi bora ya sauti /dh/ na / th/.
Ni maneno yepi unayoyajua yaliyo na sauti /dh/ na /th/?

Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa

  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotamka maneno yenye sauti /dh/ na/ th/ ipasavyo katika sentensi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika mazungumzo kwenye kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kuunda na kusikiliza vitanzandimi vyenye sauti /dh/ na /th/.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapounda vitanzandimi vyenye sauti /dh/ na /th/ na kuvitamka ipasavyo katika kikundi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapotamka ipasavyo sauti /dh/ na /th/ na anapochangia katika kazi ya kikundi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki na mzazi au mlezi wake kusoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora ya sauti /dh/ na /th/.
Maadili
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi na kutunza vifaa vya kidijitali anavyotumia.
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi kwa utulivu.
Masuala Mtambuko
  • Lishe bora – mwanafunzi anapotamka na kuzingatia maneno yenye sauti lengwa ipasavyo katika muktadha wa suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – dhana ya kutofautisha na kutamka sauti ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.
  • Integrated Science, Health Education na Home Science – lishe bora ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua sauti /dh/ na /th/ katika silabi na maneno. Anatambua kwa wepesi sauti /dh/ na /th/ katika silabi na maneno. Anatambua sauti /dh/ na /th/ katika silabi na maneno. Anatambua sauti /dh/ na /th/ katika baadhi ya silabi na maneno. Anatambua sauti /dh/ na /th/ katika baadhi ya silabi na maneno kwa kusaidiwa.
Kuweza kutamka sauti /dh/ na /th/ ipasavyo katika silabi na maneno. Anatamka sauti /dh/ na /th/ ipasavyo katika silabi na maneno kwa wepesi. Anatamka sauti /dh/ na /th/ ipasavyo katika silabi na maneno. Anatamka sauti /dh/ na /th/ ipasavyo katika baadhi ya silabi na maneno. Anatamka sauti /dh/ na /th/ ipasavyo katika baadhi ya silabi na maneno kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia maneno yenye sauti /dh/ na /th/ katika sentensi. Anatumia maneno yenye sauti /dh/ na /th/ katika sentensi kwa urahisi. Anatumia maneno yenye sauti /dh/ na /th/ katika sentensi. Anatumia baadhi ya maneno yenye sauti /dh/ na /th/ katika sentensi. Anatumia baadhi ya maneno yenye sauti /dh/ na /th/ katika sentensi kwa kusaidiwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
2.2 Kusoma 2.2.1 Kusoma kwa Mapana
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia
  2. kutumia ipasavyo msamiati uliotumiwa katika matini aliyosoma
  3. kueleza ujumbe wa matini aliyosoma
  4. kutoa muhtasari wa matini ya kujichagulia aliyosoma
  5. kuweka rekodi ya aliyosoma kwa kuyanakili katika kijitabu
  6. kujenga mazoea ya kusoma matini za miktadha mbalimbali kupanua mawanda wa fikra.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia (andishi au ya kidijitali) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutumia kamusi kutafuta maana za maneno asiyoyajua akiwa peke yake au katika kikundi
  • kujenga rekodi ya msamiati aliojifunza katika kitabu
  • kumtungia mwenzake sentensi akitumia msamiati katika matini aliyoisoma (ya kidijitali au maandishi)
  • kuwaeleza wenzake ujumbe wa matini aliyoisoma
  • kutoa muhtasari wa matini ya kujichagulia aliyosoma na kuwasilisha kwa wenzake ili waitolee maoni
  • kurekodi aliyoyasoma katika kijitabu chake kwa marejeleo ya baadaye
  • kusakura mtandaoni na kujichagulia matini ya ziada kisha aisome
  • kumshirikisha mzazi au mlezi kuchagua matini mtandaoni au maktabani yanayohusu lishe bora ili kuyatolea maoni.
  1. Unapenda kusoma matini za aina gani?
  2. Unazingatia nini unapochagua matini ya kujisomea?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoandika muhtasari na kuuwasilisha kwa wenzake.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapotangamana na wenzake na kuwawasilishia muhtasari wa matini ya kujichagulia aliyosoma.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapomtungia mwenzake sentensi kutokana na msamiati wa matini ya kujichagulia akizingatia ufasaha wa lugha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoeleza ujumbe wa matini aliyosoma.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapojichagulia matini ya kusoma na kutafuta maana za maneno asiyoyajua kwenye kamusi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anaposakura mtandaoni na kujichagulia matini ya kusoma.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake wanapowasilisha muhtasari wa matini ya kujichagulia waliyosoma.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kutafuta na kusoma matini aliyojichagulia. Pia anapozingatia nidhamu anaposakura mtandaoni.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kutunga sentensi akitumia msamiati aliojifunza.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko mbalimbali (k.v. lishe bora, utunzaji wa mazingira, masuala ya jinsia, n.k.) kulingana na matini zinazosomwa na mwanafunzi.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusoma kwa mapana.
  • Integrated Science, Health Education na Home Science – lishe bora ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua msamiati uliotumiwa katika matini aliyosoma. Anatambua kwa urahisi msamiati uliotumiwa katika matini aliyosoma. Anatambua msamiati uliotumiwa katika matini aliyosoma. Anatambua baadhi ya msamiati uliotumiwa katika matini aliyosoma. Anatambua baadhi ya msamiati uliotumiwa katika matini aliyosoma kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia ipasavyo msamiati aliosoma katika matini. Anatumia ipasavyo na kwa urahisi msamiati aliosoma katika matini. Anatumia ipasavyo msamiati aliosoma katika matini. Anatumia ipasavyo baadhi ya msamiati aliosoma katika matini. Anatumia ipasavyo baadhi ya msamiati aliosoma katika matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza ujumbe wa matini aliyosoma. Anaeleza ujumbe wa matini aliyosoma kwa urahisi. Anaeleza ujumbe wa matini aliyosoma. Anaeleza kwa kiasi ujumbe wa matini aliyosoma. Anaeleza kwa kiasi ujumbe wa matini aliyosoma kwa kusaidiwa.
Kuweza kutoa muhtasari wa matini aliyosoma. Anatoa muhtasari wa matini aliyosoma kwa urahisi. Anatoa muhtasari wa matini aliyosoma. Anatoa muhtasari wa sehemu ya matini aliyosoma. Anatoa muhtasari wa sehemu ya matini aliyosoma kwa kusaidiwa.
Kuweza kuweka rekodi ya aliyosoma kwa kuyanakili katika kijitabu. Anaweka rekodi ya aliyosoma kwa kuyanakili katika kijitabu kwa wepesi. Anaweka rekodi ya aliyosoma kwa kuyanakili katika kijitabu. Anaweka kwa kiasi rekodi ya aliyosoma kwa kuyanakili katika kijitabu. Anaweka kwa kiasi rekodi ya aliyosoma kwa kuyanakili katika kijitabu kwa kuelekezwa.

 

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
2.3 Kuandika 2.3.1 Barua ya Kirafiki ya Kutoa Mwaliko
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo mwanafunzi aweze:
  1. kueleza umuhimu wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu masuala mbalimbali katika jamii
  2. kutambua ujumbe katika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko
  3. kutambua vipengele vya kimuundo vya barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko
  4. kuandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa kuzingatia ujumbe, muundo na lugha ifaayo
  5. kufurahia uandishi wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko ili kufanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza umuhimu wa kuandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu maswala mbalimbali (k.v. kuleta jamii pamoja, kuimarisha utangamano, kuhamasisha jamii, n.k.) akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutambua ujumbe katika kielelezo cha barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kujadili katika kikundi vipengele vya kimuundo vya barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko (k.v. anwani ya mwandishi, tarehe, n.k.)
  • kushiriki katika kujadili na wenzake kuhusu lugha inayofaa katika uandishi wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko
  • kuandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu suala lengwa (k.v kushiriki katika upishi wa vyakula vya kiasili, kushiriki kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa vyakula vya kiasili, n.k.) na kuwasomea wenzake darasani ili waitathmini
  • kumwandikia rafiki, mzazi au mlezi barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwenye hafla fulani (k.v. sherehe ya siku ya kuzaliwa) kwa kutumia vifaa vya kidijitali na kuwasambazia wenzake pamoja na mwalimu mtandaoni, kwa kuzingatia maadili ya mtandaoni, ili kuitolea maoni.

 

  1.  Je, ni shughuli gani zinazoweza kukufanya uandike barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko?
  2. Je, ni mambo gani yanayotiliwa maanani katika kuandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko ya kutoa mwaliko na kuheshimu maoni ya wenzake.

Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa

  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoandika ipasavyo na kwa ufasaha barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa rafiki, mzazi au mlezi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kujadili ujumbe, lugha na muundo wa barua ya kirafiki
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kuandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko na kuisambaza mtandaoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika kwa mvuto barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapomwandikia rafiki au mzazi wake barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko ili kutoa maoni.
  • Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anapopendekeza shughuli ambazo zinaweza kumfanya aandike barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko. Pia anapoandika barua kuhusu masuala yanayoathiri jamii na kuwashirikisha wenzake katika kupendekeza suluhu.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi. Pia anapotumia vifaa vya kidijitali inavyostahili.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika shughuli za kikundi.
  • Amani – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi kwa utulivu, heshima na kusikilizana.

Masuala Mtambuko

  • Lishe bora – mwanafunzi anapoandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu suala lengwa.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha za kiuamilifu.
  • Integrated Science, Health Education na Home Science – lishe bora ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza umuhimu wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu masuala mbalimbali katika jamii. Anaeleza kwa wepesi umuhimu wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu masuala mbalimbali katika jamii. Anaeleza umuhimu wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu masuala mbalimbali katika jamii. Anaeleza baadhi ya umuhimu wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu masuala mbalimbali katika jamii. Anaeleza baadhi ya umuhimu wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kuhusu masuala mbalimbali katika jamii kwa kuelekezwa.
Kuweza kutambua ujumbe katika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko. Anatambua ujumbe katika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa urahisi. Anatambua ujumbe katika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko. Anatambua ujumbe katika baadhi ya sehemu za barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko. Anatambua ujumbe katika baadhi ya sehemu za barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua vipengele vya kimuundo vya barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko. Anatambua kwa wepesi vipengele vya kimuundo vya barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko. Anatambua vipengele vya kimuundo vya barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko. Anatambua baadhi ya vipengele vya kimuundo vya barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko. Anatambua baadhi ya vipengele vya kimuundo vya barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa kusaidiwa.
Kuweza kuandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa kuzingatia ujumbe,muundo na lugha ifaayo. Anaandika kwa ufasaha barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa kuzingatia ujumbe, muundo na lugha ifaayo. Anaandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko kwa kuzingatia ujumbe,muundo na lugha ifaayo. Anaandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko akizingatia kwa kiasi ujumbe,muundo na lugha ifaayo. Anaandika barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko akizingatia kwa kiasi ujumbe,muundo na lugha ifaayo kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
2.4 Sarufi 2.4.1 Nomino za Makundi na za Dhahania
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua nomino za makundi na za dhahania kwenye matini
  2. kutumia nomino za makundi na za dhahania ifaavyo katika sentensi na vifungu
  3. kuchangamkia kutumia nomino za makundi na za dhahania katika mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwa:
  • kutambua nomino za makundi (k.v. mkungu, mtungo, tita, bunda, shada, jamii, kikosi, genge, n.k) na za dhahania (k.v. ugonjwa, usingizi, furaha, shibe, elimu, maisha, n.k.) kwenye chati, kadi maneno, kapu maneno na matini nyingine akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutenga nomino za makundi na za dhahania katika orodha ya maneno, sentensi au vifungu kwa kuzipigia mstari au kuzikolezea wino katika matini za kimaandishi au za kidijitali akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushirikiana na wenzake katika kikundi kutambua nomino za makundi na za dhahania katika mazingira ya shuleni na nyumbani na kuzitungia sentensi
  • kutunga sentensi kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za makundi na za dhahania akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga aya kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za makundi na za dhahania akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushirikiana na mzazi au mlezi wake kutambua nomino za makundi na za dhahania kwenye mtandao au kwenye vitabu vya ziada na kuzitungia sentensi.
  1. Ni nomino gani za makundi zinazopatikana katika mazingira ya shuleni na ya nyumbani?
  2. Ni nomino gani za dhahania zinazopatikana katika mazingira ya shuleni na ya nyumbani?
  • Umilisi wa Kimsingi UnaokuzwaMawasiliano – mwanafunzi anapomtajia kwa ufasaha mwenzake nomino za makundi na za dhahania katika mazingira ya shuleni na nyumbani.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia kikamilifu katika kazi za kikundi kutambua na kutenga nomino za makundi na za dhahania.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kutambua nomino za makundi na za dhahania.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuhusu suala lengwa akitumia nomino za makundi na za dhahania.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kutambua nomino za makundi na za dhahania na kuzitungia sentensi na vifungu sahihi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapomtajia mwenzake nomino za makundi katika mazingira ya shuleni na nyumbani.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika shughuli za kikundi.

Masuala Mtambuko

  • Lishe bora – mwanafunzi anapotunga sentensi na vifungu kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – dhana ya nomino za makundi na za dhahania ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.
  • Science and Technology, Health Education na Home Science – lishe bora ni mojawapo ya masuala yanayoshughulikiwa katika masomo haya.


Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua nomino za makundi na za dhahania kwenye matini. Anatambua kwa wepesi nomino za makundi na za dhahania kwenye matini. Anatambua nomino za makundi na za dhahania kwenye matini. Anatambua baadhi ya nomino za makundi na za dhahania kwenye matini. Anatambua baadhi ya nomino za makundi na za dhahania kwenye matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia nomino za makundi na za dhahania ifaavyo katika sentensi na vifungu. Anatumia nomino za makundi na za dhahania ifaavyo na kwa urahisi katika sentensi na vifungu. Anatumia nomino za makundi na za dhahania ifaavyo katika sentensi na vifungu. Anatumia baadhi ya nomino za makundi na za dhahania ifaavyo katika sentensi na vifungu. Anatumia baadhi ya nomino za makundi na za dhahania ifaavyo katika sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.

 

MADA 3.0 UHURU WA WANYAMA
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
3.1 Kusikiliza na Kuzungumza 3.1.1 Tanzu za Fasihi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya fasihi ili kuipambanua
  2. kujadili sifa za tanzu za fasihi
  3. kutambua aina za tungo za fasihi simulizi na fasihi andishi katika matini
  4. kuwasilisha utungo wa fasihi anaoujua
  5. kufurahia kushiriki katika uwasilishaji wa fasihi simulizi na fasihi andishi ili kujenga ufasaha wa lugha na fasihi.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kushiriki na wenzake kueleza kikamilifu maana ya fasihi katika jamii
  • kutambua tanzu za fasihi (fasihi andishi na simulizi) akiwa peke yake au katika kikundi
  • kueleza maana ya fasihi simulizi na andishi akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutofautisha kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi akiwa katika kikundi
  • kujadili sifa za fasihi simulizi (k.v. kuwasilishwa kwa njia ya mdomo, kuwa mali ya jamii, n.k.) na fasihi andishi (k.v. kuandikwa, kuwa mali ya mtu binafsi, n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua tungo za fasihi simulizi (k.v. hadithi, semi, mazungumzo, ushairi simulizi na maigizo) na fasihi andishi (k.v. novela, riwaya, tamthilia, ushairi na hadithi fupi) kutoka simulizi za moja kwa moja au kwenye matini za kidijitali
  • kuwawasilishia wenzake utungo wa fasihi (k.v. hadithi za wanyama n.k.) ili waitolee maoni
  • kushiriki na mzazi au mlezi wake kutafiti kuhusu tanzu za fasihi simulizi na andishi katika jamii yake.
  1. Je, jamii yako ina tungo zipi za fasihi simulizi?
  2. Kuna tofauti gani kati ya fasihi simulizi na andishi?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoeleza kwa ufasaha maana na sifa za fasihi andishi na fasihi simulizi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika kazi ya kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kujifunza sifa za fasihi simulizi na andishi.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapojieleza kwa mitindo mbalimbali.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapojieleza katika kazi ya kikundi na kujenga ukakamavu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi kutambua tanzu za fasihi simulizi na andishi katika jamii yake.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kujieleza.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapotunza vifaa vya kidijitali anavyotumia kujifunzia sifa za fasihi simulizi na andishi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Uraia – mwanafunzi anapothamini tungo za fasihi simulizi katika jamii.
Masuala Mtambuko
  • Ushirikishi wa wazazi – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi kutambua tungo za fasihi simulizi na andishi katika jamii.
  • Uhuru wa wanyama – mwanafunzi anaposimulia tungo na kutilia maanani uhuru wa wanyama.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia dhana ya tungo za fasihi simulizi na andishi.
  • Social Studies na Agriculture – masomo haya pia yanashughulikia masuala ya utunzaji wa wanyama.

 

Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya fasihi ili kuipambanua. Anaeleza maana ya fasihi kwa urahisi ili kuipambanua. Anaeleza maana ya fasihi ili kuipambanua. Anaeleza kwa kiasi maana ya fasihi ili kuipambanua. Anaeleza kwa kiasi maana ya fasihi ili kuipambanua kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili sifa za tanzu za fasihi. Anajadili sifa za tanzu za fasihi kwa wepesi. Anajadili sifa za tanzu za fasihi. Anajadili baadhi ya sifa za tanzu za fasihi. Anajadili baadhi ya sifa za tanzu za fasihi kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua aina za tungo za fasihi simulizi na fasihi andishi. Anatambua aina za tungo za fasihi simulizi na fasihi andishi kwa urahisi. Anatambua aina za tungo za fasihi simulizi na fasihi andishi. Anatambua baadhi ya aina za tungo za fasihi simulizi na fasihi andishi. Anatambua baadhi ya aina za tungo za fasihi simulizi na fasihi andishi kwa kusaidiwa.
Kuweza kuwasilisha utungo wa fasihi anaoujua. Anawasilisha kwa ufasaha utungo wa fasihi anaoujua. Anawasilisha utungo wa fasihi anaoujua. Anawasilisha sehemu za utungo wa fasihi anaoujua. Anawasilisha sehemu ya utungo wa fasihi anaoujua kwa kusaidiwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
3.2 Kusoma 3.2.1 Kusoma kwa Kina
Novela
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya novela ili kuipambanua
  2. kujadili sifa za novela kama utanzu wa fasihi andishi
  3. kuchangamkia usomaji wa novela ili kukuza stadi ya kusoma.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya novela akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutafiti maktabani au mtandaoni kuhusu maana na sifa za novela (k.v. wahusika wachache, maudhui machache n.k.) akiwa peke yake au katika kikundi
  • kuwasambazia wenzake matokeo ya utafiti wake ili wasome na kutolea maon
  • kujadili sifa za novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusoma novela iliyoteuliwa na mwalimu na kutambua sifa zake akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma na kutambua sifa za novela.
Novela ni utungo wa aina gani?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapochangia katika shughuli za kikundi kwa kutumia lugha fasaha.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapotangamana na wenzake katika kikundi huku akitoa maoni yake na kuheshimu ya wengine.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anaposakura mtandaoni ili kutafiti kuhusu maana na sifa za novela.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapofanya utafiti maktabani au mtandaoni kuhusu maana na sifa za novela. Pia anaposoma tafiti za wenzake na kuzitolea maoni.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapowawasilishia wenzake sifa za novela katika kikundi.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kikundi wanapojadili sifa za novela.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali ipasavyo na kuzingatia maadili anapotafiti mtandaoni.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kuwasilisha maoni yao katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika kazi za kikundi.

Masuala Mtambuko

  • Masuala mtambuko anuwai – mwanafunzi anaposoma novela.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusoma kwa kina.
  • Social Studies na Agriculture – masomo haya pia yanashughulikia masuala ya utunzaji wa wanyama.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya novela ili kuipambanua. Anaeleza kwa urahisi maana ya novela ili kuipambanua. Anaeleza maana ya novela ili kuipambanua. Anaeleza kwa kiasi maana ya novela ili kuipambanua. Anaeleza kwa kiasi maana ya novela ili kuipambanua kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili sifa za novela kama utanzu wa fasihi andishi. Anajadili kwa urahisi sifa za novela kama utanzu wa fasihi andishi. Anajadili sifa za novela kama utanzu wa fasihi andishi. Anajadili baadhi ya sifa za novela kama utanzu wa fasihi andishi. Anajadili baadhi ya sifa za novela kama utanzu wa fasihi andishi kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
3.3 Kuandika 3.3.1 Insha za Kubuni
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kuteua mada na ujumbe wa kuandikia insha ya kubuni
  2. kujadili vidokezo kulingana na mada ya kuandikia insha ya kubuni
  3. kuandika vidokezo vyenye ujumbe unaolingana na mada ya insha ya kubuni
  4. kuandika insha ya kubuni inayozingatia vidokezo vilivyoandaliwa
  5. kufurahia kuandaa vidokezo vyenye ujumbe unaolingana na mada ya insha.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kuteua mada kulingana na ujumbe anaoandikia akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutafiti kuhusu mada anayoiandikia (k.v mtandaoni,vitabuni, magazetini, n.k.) kuhusu masuala yanayoathiri jamii akiwa peke yake au katika kikundi
  • kujadiliana na wenzake vidokezo vya mada aliyoteua
  • kuandika vidokezo vyenye ujumbe unaolingana na mada akiwa peke yake au kwa kushirikiana na wenzake
  • kuwasomea wenzake katika kikundi vidokezo alivyoandika au awasambazie kwenye kifaa cha kidijitali ili wavitolee maoni
  • kuandika insha ya kubuni inayozingatia vidokezo alivyoandaa
  • kuwasilisha insha yake darasani au mtandaoni ili wenzake wamtolee maoni
  • kushirikiana na mzazi au mlezi wake kuandaa vidokezo na kuandika insha ya kubuni kulingana na mada aliyoiteua.
Ni mambo gani unayozingatia unapoandaa vidokezo vya insha ya kubuni?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapojadiliana na wenzake kwa ufasaha vidokezo vya insha ya kubuni.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kujadili vidokezo vya insha ya kubuni.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kutafiti kuhusu mada anayoandikia.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoteua mada na vidokezo mwafaka vya kuandikia insha ya kubuni.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapotafiti kuhusu mada anayoandikia kwenye makala mbalimbali.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kuteua mada mwafaka na kuiandalia vidokezo.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi. Pia anapozingatia nidhamu anaposakura mtandaoni.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
• Masuala mtambuko anuwai – mwanafunzi anapotafiti na kuteua mada kuhusu masuala yanayoathiri jamii.
Uhusiano na Masomo Mengine
● English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha za kubuni.
● Social Studies na Agriculture – masomo haya pia yanashughulikia masuala ya utunzaji wa wanyama.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kuteua mada na ujumbe wa kuandikia insha ya kubuni. Anateua mada na ujumbe wa kuandikia insha ya kubuni kwa urahisi. Anateua mada na ujumbe wa kuandikia insha ya kubuni. Anachukua muda kuteua mada na ujumbe wa kuandikia insha ya kubuni. Anachukua muda kuteua mada na ujumbe wa kuandikia insha ya kubuni kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili vidokezo kulingana na mada ya kuandikia insha ya kubuni. Anajadili kwa urahisi vidokezo kulingana na mada ya kuandikia insha ya kubuni. Anajadili vidokezo kulingana na mada ya kuandikia insha ya kubuni. Anajadili baadhi ya vidokezo kulingana na mada ya kuandikia insha ya kubuni. Anajadili baadhi ya vidokezo kulingana na mada ya kuandikia insha ya kubuni kwa kusaidiwa.
Kuweza kuandika vidokezo vyenye ujumbe unaolingana na mada ya insha ya kubuni. Anaandika vidokezo vyenye ujumbe unaolingana na mada ya insha ya kubuni kwa urahisi. Anaandika vidokezo vyenye ujumbe unaolingana na mada ya insha ya kubuni. Anaandika baadhi ya vidokezo vyenye ujumbe unaolingana na mada ya insha ya kubuni. Anaandika baadhi ya vidokezo vyenye ujumbe unaolingana na mada ya insha ya kubuni kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandika insha ya kubuni inayozingatia vidokezo vilivyoandaliwa. Anaandika kwa mvuto insha ya kubuni inayozingatia vidokezo vilivyoandaliwa. Anaandika insha ya kubuni inayozingatia vidokezo vilivyoandaliwa. Anaandika kwa kiasi insha ya kubuni inayozingatia vidokezo vilivyoandaliwa. Anaandika kwa kiasi insha ya kubuni inayozingatia vidokezo vilivyoandaliwa kwa kusaidiwa.




Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
3.4 Sarufi 3.4.1 Nomino za Wingi na za Vitenzi-jina (Vipindi 2) Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua nomino za wingi na za vitenzi-jina katika matini
  2. kutumia nomino za wingi na za vitenzi-jina ipasavyo katika sentensi na vifungu
  3. kufurahia matumizi ya nomino za wingi na za vitenzi-jina katika mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua nomino za wingi (k.v. maji, changarawe, n.k) na za vitenzi-jina (k.v kusimama, kula, kuchunga, n.k.) kwenye chati, kadi maneno au kapu maneno akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutenga nomino za wingi na za vitenzi-jina katika orodha ya maneno, sentensi au vifungu kwa kuzipigia mstari au kuzikolezea wino katika matini za kidijitali akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kumtajia mwenzake nomino za wingi na za vitenzi-jina katika mazingira ya shuleni na ya nyumbani
  • kutunga sentensi kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za wingi na za vitenzi-jina akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga aya kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za wingi na za vitenzi-jina akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushirikiana na mzazi au mlezi wake kutafiti (k.v. mtandaoni, vitabuni, n.k.) kuhusu nomino za wingi na za vitenzi-jina na kuzitungia sentensi kisha awasomee wenzake darasani ili wamtolee maoni.
Je, ni nomino zipi za wingi na za vitenzi jina zinazopatikana katika mazingira yako?
Umilisi wa kimsingi unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapomtajia mwenzake kwa ufasaha nomino za wingi na za vitenzi-jina katika mazingira yake.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapochangia katika kazi za vikundi kutambua na kutenga nomino za wingi na za vitenzi-jina.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kutafiti kuhusu nomino za wingi na za vitenzi-jina.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuhusu suala lengwa akitumia nomino za wingi na za vitenzi-jina.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kutambua nomino za wingi na za vitenzi-jina na kuzitungia sentensi na vifungu sahihi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapotafiti mtandaoni kuhusu nomino za wingi na za vitenzi-jina kisha kuwasomea wenzake darasani ili wamtolee maoni.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Maslahi ya wanyama – mwanafunzi anapotunga sentensi na aya kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za wingi na za vitenzi-jina.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia aina za nomino.
  • Social Studies na Agriculture – masomo haya pia yanashughulikia masuala ya utunzaji wa wanyama.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua nomino za wingi na za vitenzi-jina katika matini. Anatambua kwa wepesi nomino za wingi na za vitenzi-jina katika matini. Anatambua nomino za wingi na za vitenzi-jina katika matini. Anatambua baadhi ya nomino za wingi na za vitenzi-jina katika matini. Anatambua baadhi ya nomino za wingi na za vitenzi-jina katika matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia nomino za wingi na za vitenzi-jina ipasavyo katika sentensi na vifungu. Anatumia nomino za wingi na za vitenzi-jina ipasavyo katika sentensi na vifungu kwa urahisi. Anatumia nomino za wingi na za vitenzi-jina ipasavyo katika sentensi na vifungu. Anatumia nomino za wingi na za vitenzi-jina ipasavyo katika baadhi ya sentensi na vifungu. Anatumia nomino za wingi na za vitenzi-jina ipasavyo katika baadhi ya sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.



MADA 4.0 AINA ZA MALIASILI
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
4.1 Kusikiliza na Kuzungumza 4.1.1 Nyimbo za
Watoto na
Bembelezi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya nyimbo za watoto na bembelezi
  2. kujadili sifa za nyimbo za watoto na bembelezi
  3. kujadili mitindo ya uwasilishaji wa nyimbo za watoto na bembelezi
  4. kuwasilisha nyimbo za watoto na bembelezi kwa kuzingatia uwasilishaji ufaao
  5. kuchangamkia uwasilishaji na ujumbe wa nyimbo za watoto na bembelezi ili kukuza ubunifu.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya nyimbo za watoto na bembelezi akiwa na wenzake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutafiti vitabuni au mtandaoni kuhusu sifa za nyimbo za watoto na bembelezi
  • kuwasilisha matokeo ya utafiti wake kwa wenzake ili waweze kujadili sifa hizo
  • kusikiliza vielelezo vya nyimbo za watoto na bembelezi kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au kifaa cha kidijitali (k.v. redio, rununu, kipakatalishi, runinga, n.k.)
  • kushirikiana na wenzake kujadili mitindo ya uwasilishaji wa nyimbo za watoto na bembelezi (k.v. urudiaji wa sauti, maneno na vifungu vya maneno, uchezeshaji wa viungo vya mwili, n.k.) katika nyimbo walizosikiliza
  • kuimba nyimbo za watoto na bembelezi kwa kuzingatia mitindo mbalimbali ya uwasilishaji akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga nyimbo nyepesi za watoto na bembelezi akiwa peke yake au katika kikundi na kuziwasilisha kwa kutumia mitindo ifaayo
  • Kuimba wimbo wa watoto na bembelezi akiwa na mzazi au mlezi wake na kujadili ujumbe katika nyimbo hizo.
 
  1. Je, ni nyimbo gani za watoto unazozijua katika jamii yako?
  2. Unapomwimbia mtoto bembelezi, unazingatia nini ili apate kulala?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – anapojadiliana na wenzake kuhusu uwasilishaji wa nyimbo za watoto na bembelezi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kuimba nyimbo kwenye kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusikiliza nyimbo mbalimbali za watoto na bembelezi.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga na kuwasilisha nyimbo za watoto na bembelezi
  • Kujiamini – mwanafunzi anapoimba na kuwasilisha nyimbo. Pia anapochangia ifaavyo katika shughuli za kikundi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi kuimba nyimbo za watoto na bembelezi.
  • Uraia – mwanafunzi anaposikiliza nyimbo mbalimbali za watoto na bembelezi kutoka jamii tofautitofauti.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika shughuli za kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Haki za watoto – mwanafunzi anapotunga na kuwasilisha nyimbo zinazohusu masuala ya watoto.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia dhana ya tungo za fasihi simulizi.
  • Performing Arts – somo hili pia linashughulikia uwasilishaji wa nyimbo na uimbaji.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya nyimbo za watoto na bembelezi. Anaeleza maana ya nyimbo za watoto na bembelezi kwa urahisi. Anaeleza maana ya nyimbo za watoto na bembelezi. Anaeleza kwa kiasi maana ya nyimbo za watoto na bembelezi. Anaeleza kwa kiasi maana ya nyimbo za watoto na bembelezi kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili ujumbe katika nyimbo za watoto na bembelezi. Anajadili ujumbe katika nyimbo za watoto na bembelezi kwa wepesi. Anajadili ujumbe katika nyimbo za watoto na bembelezi. Anajadili kwa kiasi ujumbe katika nyimbo za watoto na bembelezi. Anajadili kwa kiasi ujumbe katika nyimbo za watoto na bembelezi kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili mitindo ya uwasilishaji wa nyimbo za watoto na bembelezi. Anajadili mitindo ya uwasilishaji wa nyimbo za watoto na bembelezi kwa urahisi. Anajadili mitindo ya uwasilishaji wa nyimbo za watoto na bembelezi. Anajadili baadhi ya mitindo ya uwasilishaji wa nyimbo za watoto na bembelezi. Anajadili baadhi ya mitindo ya uwasilishaji wa nyimbo za watoto na bembelezi kwa kusaidiwa.
Kuweza kuwasilisha nyimbo za watoto na bembelezi kwa kuzingatia mitindo mbalimbali ya uwasilishaji. Anawasilisha nyimbo za watoto na bembelezi kwa kuzingatia mitindo mbalimbali ya uwasilishaji kwa urahisi. Anawasilisha nyimbo za watoto na bembelezi kwa kuzingatia mitindo mbalimbali ya uwasilishaji. Anawasilisha baadhi ya nyimbo za watoto na bembelezi kwa kuzingatia mitindo mbalimbali ya uwasilishaji. Anawasilisha baadhi ya nyimbo za watoto na bembelezi kwa kuzingatia baadhi ya mitindo ya uwasilishaji.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
4.2 Kusoma 4.2.1 Kusoma kwa Ufasaha
(Vipindi 2)

Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:

  1. kusoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora
  2. kusoma kifungu kwa kasi ifaayo
  3. kusoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo
  4. kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo
  5. kuridhia kusoma makala kwa kuzingatia vipengele vinavyofanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kujadiliana na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kusoma makala kwa ufasaha
  • kutazama vielelezo vya video za watu wanaosoma kwa ufasaha makala (k.v. hotuba, habari, n.k.) akiwa peke yake au na wenzake
  • kusoma kifungu kuhusu suala lengwa katika matini andishi au ya kidijitali akizingatia matamshi bora akiwa peke yake au katika kikundi
  • kusoma kifungu cha habari kwa kasi ifaayo kuhusu suala lengwa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusoma kifungu akizingatia sauti ifaayo (k.v. kiwango cha sauti na kiimbo) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikindi
  • kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo panapofaa (k.v. ishara za uso na mikono) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusoma mbele ya wenzake kazi yake ili wamtolee maoni
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma makala akizingatia vipengele vya usomaji bora.
Unazingatia nini ili kusoma makala kwa ufasaha?

Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa

  • Mawasiliano – mwanafunzi anapofanikiwa kusoma makala kwa ufasaha na anapojadiliana na wenzake katika kikundi kuhusu vipengele vya kimsingi vya kusoma kwa ufasaha.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kuhusu vipengle vya kusoma kwa ufasaha.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposoma kifungu kwa ufasaha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotumia ishara wakati wa kusoma kifungu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli ya kusoma anakuza hamu ya ujifunzaji.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi wanapojadili vipengele vya usomaji bora.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika mjadala wakati wa shughuli ya ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuwasomea wenzake kifungu.
  • Umoja – mwanafunzi anapotangamana na wenzake katika kikundi kujadili vipengele vya usomaji bora.

Masuala Mtambuko

  • Masuala ya elimu ya mazingira – mwanafunzi anaposoma ujumbe unaohusu maliasili.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia stadi ya kusoma.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia suala la maliasili.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kusoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora. Anasoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora kwa urahisi. Anasoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora. Anasoma sehemu za kifungu kwa kuzingatia matamshi bora. Anasoma sehemu za kifungu kwa kuzingatia matamshi bora kwa kusaidiwa.
Kuweza kusoma kifungu kwa kasi ifaayo. Anasoma kifungu kwa kasi ifaayo kwa urahisi. Anasoma kifungu kwa kasi ifaayo. Anasoma sehemu za kifungu kwa kasi ifaayo. Anasoma sehemu za kifungu kwa kasi ifaayo kwa kusaidiwa.
Kuweza kusoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo. Anasoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo kwa urahisi. Anasoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo. Anasoma sehemu za kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo. Anasoma sehemu za kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo kwa kusaidiwa.
Kuweza kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo. Anasoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo kwa urahisi. Anasoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo. Anasoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo katika baadhi ya sehemu. Anasoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo katika baadhi ya sehemu kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
4.3 Kuandika 4.3.1 Insha za Kubuni
Masimulizi
(Vipindi 2)

Kufikia mwisho wa mada ndogo mwanafunzi aweze:

  1. kutambua lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi
  2. kujadili umuhimu wa lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi
  3. kubainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi 
  4. kujadili umuhimu wa wahusika na mandhari katika insha za masimulizi 
  5. kuandika insha ya masimulizi akizingatia lugha, wahusika na mandhari ifaavyo 
  6. kufurahia kuandika insha ya masimulizi akizingatia lugha, wahusika na mandhari ifaavyo katika insha ya masimulizi ili kukuza ubunifu.

Mwanafunzi aelekezwe:

  • kutambua lugha ya kiubunifu katika vielelezo vya insha za masimulizi akiwa peke yake au katika kikundi
  • kushirikiana na wenzake kujadili umuhimu wa lugha ya kiubunifu katika vielelezo vya insha za masimulizi
  • kubainisha wahusika na mandhari katika vielelezo vya insha za masimulizi kutoka kwenye maandishi au vifaa vya kidijitali akiwa peke yake au katika kikundi
  • kushirikiana na wenzake kujadili umuhimu wa wahusika na mandhari katika insha za masimulizi
  • kuandika insha ya masimulizi akitumia lugha kiubunifu na kuwabainisha wahusika na mandhari akizingatia suala lengwa
  • kuwasomea wenzake insha aliyoandika ili waitathmini
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma kileelezo cha insha ya masimulizi kisha watambue matumizi ya lugha kiubunifu na ubainishaji wa wahusika na mandhari.
Je, ni mambo gani utahitaji kuzingatia ili kuandika insha nzuri ya masimulizi?

Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa

  •  Mawasiliano – mwanafunzi anapojadili kwa ufasaha umuhimu wa ubainishaji wa wahusika na mandhari katika insha za masimulizi. Pia anapowasomea wenzake insha aliyoandika ili waitathmini.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kutathmini insha. Anapojadiliana na wenzake kuhusu umuhimu wa kubainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusoma vielelezo vya insha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika insha kwa kutumia lugha kiubunifu na kubainisha wahusika na mandhari.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapowasomea wenzake insha aliyoandika na kuwataka waitathmini.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kuwasomea wenzake insha ya masimulizi.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi. Pia anapotathmini insha za wenzake.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia shughuli za kikundi.

Masuala Mtambuko

  • Masuala ya elimu ya mazingira – mwanafunzi anapoandika insha ya masimulizi kuhusu aina za maliasili kwa kuzingatia matumizi ya lugha kiubunifu, ubainishaji wa wahusika na mandhari.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yana mada zinazoshughulikia vipengele vya masimulizi.
  • Social Studies – somo hili pia lina mada inayoshughulikia masuala ya kiuchumi kama vile maliasili.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi. Anatambua lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi kwa urahisi. Anatambua lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi. Anatambua lugha ya kiubunifu katika baadhi ya sehemu za insha za masimulizi. Anatambua lugha ya kiubunifu katika baadhi ya sehemu za insha za masimulizi kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili umuhimu wa lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi. Anajadili kwa wepesi umuhimu wa lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi. Anajadili umuhimu wa lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi. Anajadili baadhi ya umuhimu wa lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi. Anajadili baadhi ya umuhimu wa lugha ya kiubunifu katika insha za masimulizi kwa kusaidiwa.
Kuweza kubainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi. Anabainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi kwa urahisi. Anabainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi. Anabainisha baadhi ya wahusika na mandhari katika insha za masimulizi. Anabainisha baadhi ya wahusika na mandhari katika insha za masimulizi kwa kusaidiwa.
Kujadili umuhimu wa kubainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi. Anajadili kwa wepesi umuhimu wa kubainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi. Anajadili umuhimu wa kubainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi. Anajadili baadhi ya umuhimu wa kubainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi. Anajadili baadhi ya umuhimu wa kubainisha wahusika na mandhari katika insha za masimulizi kwa kusaidiwa.
Kuweza kuandika insha ya masimulizi akizingatia lugha, wahusika na mandhari ifaavyo Anaandika kiubunifu insha ya masimulizi akizingatia lugha, wahusika na mandhari ifaavyo. Anaandika insha ya masimulizi akizingatia lugha, wahusika na mandhari ifaavyo. Anaandika insha ya masimulizi akizingatia kwa kiasi lugha, wahusika na mandhari. Anaandika insha ya masimulizi akizingatia kwa kiasi lugha, wahusika na mandhari kwa kusaidiwa.

 

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
4.4 Sarufi 4.4.1 Nyakati na Hali
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
a) kubainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo, uliopita na ujao katika sentensi na vifungu kwa usahihi
b) kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo katika sentensi na vifungu
c) kuchangamkia kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo ili kuboresha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kushirikiane na wenzake katika kikundi  kubainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo, uliopita na ujao kutoka kwenye chati, mti maneno, kapu maneno au kwa kupigia mstari kwenye sentensi na vifungu
  • kusoma kifungu na kutambua nyakati zilizotumiwa akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutunga sentensi kwa kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuandika sentensi kuhusu suala lengwa katika wakati uliopo, uliopita au ujao kwenye kifaa cha kidijitali na kuwasambazia wenzake mtandaoni ili wazibadilishe katika nyakati zinazozingatiwa
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kubadilisha nyakati katika kifungu kulingana na maagizo.
Kwa nini tunatumia nyakati mbalimbali katika mawasiliano?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapowatungia wenzake sentensi kwa kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika kazi za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia kifaa cha kidijitali kuandika sentensi katika wakati lengwa na kuwasambazia wenzake mtandaoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi na kuzibadilisha katika wakati uliopo, uliopita na ujao ipasavyo.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapochangia kutambua nyakati na kuzitungia sentensi ifaavyo.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi. Pia anapotunza vifaa vya kidijitali anavyotumia.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya elimu ya mazingira – kupitia utunzi wa sentensi na vifungu mbalimbali kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia nyakati na hali.
  • Social Studies – somo hili pia lina mada inayoshughulikia maliasili



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kubainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo, uliopita na ujao katika sentensi na vifungu kwa usahihi. Anabainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo, uliopita na ujao katika sentensi na vifungu kwa usahihi na wepesi. Anabainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo, uliopita na ujao katika sentensi na vifungu kwa usahihi. Anabainisha baadhi ya vitenzi vilivyo katika wakati uliopo, uliopita na ujao katika sentensi na vifungu. Anabainisha baadhi ya vitenzi vilivyo katika wakati uliopo, uliopita na ujao katika sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo katika sentensi na vifungu. Anatunga sentensi kwa kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo kwa wepesi. Anatunga sentensi kwa kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo. Anatunga baadhi ya sentensi kwa kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo. Anatunga baadhi ya sentensi kwa kutumia wakati uliopo, uliopita na ujao ifaavyo kwa kusaidiwa.




MADA 5.0: UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
5.1 Kusikiliza na Kuzungumza 5.1.1
Mazungumzo
Mahususi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku
  2. kutambua majibu ya maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku
  3. kutambua maamkuzi yanayotumiwa na makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na majibu ya maamkuzi hayo
  4. kutumia maamkuzi na maagano mwafaka katika miktadha mbalimbali
  5. kujenga mazoea ya kutumia maamkuzi na maagano mwafaka katika maisha ya kila siku ili kufanikisha mahusiano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua, katika mazungumzo, kapu maneno, kadi maneno au matini mbalimbali, maamkuzi pamoja na majibu ya maamkuzi hayo (k.v. habari za asubuhi – njema/nzuri, sabalkheri – aheri, n.k) na maagano pamoja na majibu ya maagano hayo (k.v. kwaheri – ya kuonana, alamsiki – binuru) yanayotumiwa miktadha anuwai, akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua maamkuzi mwafaka kwa kuzingatia mahusiano ya kijamii (k.v. mtoto kwa mzazi; shikamoo – marahaba, mwanafunzi kwa mwalimu; shikamoo – marahaba) na maagano mwafaka kulingana na nyakati za siku akiwa peke yake au katika kikundi
  • kusikiliza mazungumzo kuhusu suala lengwa katika kifaa cha kidijitali (k.v simu, redio, kinasa sauti n.k.) na kutaja maamkuzi na maagano yaliyotumiwa, akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuigiza mazungumzo (k.v. kati ya mwalimu na mwanafunzi, mwanafunzi na mwanafunzi, mtoto na mzazi au mlezi n.k) akiwa katika kikundi kwa kuzingatia maamkuzi na maagano mwafaka
  • kushirikiana na wenzake kujadili kuhusu maamkuzi na maagano yanayotumiwa na makundi mbalimbali katika jamii zao
  • kushiriki mazungumzo na mzazi au mlezi wake kwa kuzingatia maamkuzi na maagano mwafaka.
  1. Je, ni maamkuzi na maagano gani yanayotumiwa katika jamii yako?
  2. Kwa nini ni muhimu kujua maamkuzi na maagano mbalimbali?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoigiza mazungumzo na wenzake kwa kuzingatia maamkuzi na maagano yafaayo.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kutambua maamkuzi na maagano, pamoja na majibu, katika miktadha mbalimbali ya kijamii.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusikiliza maamkuzi na maagano mbalimbali.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoigiza maamkuzi na maagano mbalimbali.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposhiriki mazungumzo na kutumia maamkuzi na maagano kwa ukakamavu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki mazungumzo na mzazi au mlezi akizingatia maamkuzi na maagano mwafaka. Pia anapojadili na wenzake kuhusu maamkuzi na maagano katika jamii zao.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anaposhiriki katika uigizaji na anapotunza vifaa vya kidijitali vinavyotumiwa.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.

Masuala Mtambuko

  • Masuala ya kijamii – mwanafunzi anapotumia maamkuzi na maagano ifaayo akizingatia umri, cheo au rika.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yana masuala yanayoshughulikia maamkuzi na maagano.
  • Social Studies – somo hili pia lina mada inayoshughulikia masuala ya kijamii.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku. Anatambua maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku kwa wepesi. Anatambua maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku. Anatambua baadhi ya maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku. Anatambua baadhi ya maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua majibu ya maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku. Anatambua majibu ya maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku kwa urahisi. Anatambua majibu ya maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku. Anatambua baadhi ya majibu ya maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku. Anatambua baadhi ya majibu ya maamkuzi na maagano ya nyakati mbalimbali za siku kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua maamkuzi yanayotumiwa na makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na majibu ya maamkuzi hayo. Anatambua kwa wepesi maamkuzi yanayotumiwa na makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na majibu ya maamkuzi hayo. Anatambua maamkuzi yanayotumiwa na makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na majibu ya maamkuzi hayo. Anatambua baadhi ya maamkuzi yanayotumiwa na makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na baadhi ya majibu ya maamkuzi hayo. Anatambua, kwa kuelekezwa, baadhi ya maamkuzi yanayotumiwa na makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na majibu ya maamkuzi hayo.
Kuweza kutumia maamkuzi na maagano mwafaka katika miktadha mbalimbali. Anatumia maamkuzi na maagano mwafaka kwa urahisi katika miktadha mbalimbali. Anatumia maamkuzi na maagano mwafaka katika miktadha mbalimbali. Anatumia baadhi ya maamkuzi na maagano mwafaka katika miktadha mbalimbali. Anatumia, kwa kuelekezwa, baadhi ya maamkuzi na maagano mwafaka katika miktadha mbalimbali.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
5.2 Kusoma 5.2.1 Kusoma kwa Ufahamu
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kudondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu
  2. kueleza habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi
  3. kueleza maana ya msamiati kulingana na muktadha wa kifungu cha ufahamu
  4. kuchangamkia kusoma kwa ufahamu ili kukuza uelewa wa habari.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kudondoa habari mahususi (k.v. nani, nini, wapi, lini) katika kifungu cha ufahamu
  • kutambua msamiati mpya (k.v. maneno na nahau) katika kifungu cha ufahamu na kuueleza kwa kutumia kamusi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuandika habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi akiwa peke yake au kwa kushirikiana na wenzake
  • kuwawasilishia wenzake kazi yake ili wamtolee maoni
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma kifungu cha ufahamu na kujibu maswali.
Unazingatia nini unapodondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anaposoma kifungu kwa ufasaha.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kusoma kifungu.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kusoma na kudondoa habari katika kifungu.
  • Ubunifu – mwanafunzi anaposoma kwa ufasaha na kubainisha ujumbe katika kifungu na kukiandika kwa ufupi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposakura na kusoma makala mbalimbali ya suala lengwa ili kusoma vifungu.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya kijinsia – mwanafunzi anaposoma matini kuhusu suala lengwa.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya kijinsia – mwanafunzi anaposoma matini kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusoma kwa ufasaha.
  • Social Studies – somo hili pia lina mada inayoshughulikia masuala ya kijamii.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kudondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu kwa urahisi. Anadondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa baadhi ya habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa baadhi ya habari mahususi katika kifungu cha ufahamu kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaeleza habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi na kwa urahisi. Anaeleza habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaeleza sehemu ya habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaeleza sehemu ya habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza maana ya msamiati kulingana na muktadha wa kifungu cha ufahamu. Anaeleza maana ya msamiati kulingana na muktadha wa kifungu cha ufahamu kwa urahisi. Anaeleza maana ya msamiati kulingana na muktadha wa kifungu cha ufahamu. Anaeleza maana ya baadhi ya msamiati kulingana na muktadha wa kifungu cha ufahamu. Anaeleza maana ya baadhi ya msamiati kwa kuzingatia muktadha wa kifungu cha ufahamu kwa kuelekezwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
5.3
Kuandika
5.3.1
Insha ya Maelekezo
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya insha ya maelekezo
  2. kutambua aina za insha za maelekezo
  3. kujadili sifa za insha ya maelekezo
  4. kuandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo
  5. kuandika insha akizingatia vipengele muhimu vya insha ya maelekezo
  6. kufurahia kuandika insha ya maelekezo akizingatia vipengele vyake muhimu ili kufanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya insha ya maelekezo akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutambua anwani ya insha ya maelekezo ambayo amesoma kwenye matini akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikund
  • kutambua aina za insha za maelekezo kwenye maandishi au vifaa vya kidijitali akiwa peke yake au katika kikundi
  • kujadili sifa za insha ya maelekezo kwa kuzingatia vielelezo vya insha kwenye matini za kimaandishi au za kidijitali (k.v usahihi wa habari, mpangilio wa maelezo wenye mantiki, lugha sahili, maelezo yanayotoka upande mmoja, n.k.)
  • kushiriki katika kikundi kuandaa mpangilio ufaao wa hatua za insha ya maelekezo
  • kuandika insha ya maelekezo akizingatia vipengele vyake muhimu (k.v anwani na mpangilio mwafaka wa hatua) huku akitumia vipengele vya lugha vinavyotumiwa kuelekeza ili kumjengea msomaji taswira kamili ya anachoelekezwa kufanya
  • kuwasomea wenzake katika kikundi insha aliyoandika darasani au awasambazie kwenye vifaa vya kidijitali ili waitolee maoni
  • kuandika insha ya maelekezo akizingatia anwani na mpangilio mwafaka wa hatua huku akitumia vipengele vya lugha vinavyotumiwa kuelekeza ili kumjengea msomaji taswira kamili ya anachoelekezwa kufanya
  • kuwasomea wenzake katika kikundi insha aliyoandika darasani au kuwasambazia kwenye vifaa vya kidijitali ili waitolee maoni
  • kushirikiana na wenzake kusahihisha insha ya maelekezo aliyoandika kwa kuzingatia anwani na mpangilio ufaao wa hatua
  • kumsambazia mwalimu kifungu aluchoifupisha ili akitathmini
  1. Unataka kumwelekeza rafiki yako nyumbani kwenu. Utatumia mpangilio gani wa hatua ili asipotee njia?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoandika insha kwa ufasaha na anapoisoma vizuri.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika kujadili kuhusu insha ya maelekezo.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusambazia insha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoteua lugha mwafaka na kufaulu kutoa maelezo bayana ya anachoelekeza.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapowasomea wenzake insha aliyoandika ili waitolee maoni.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kuwasomea wenzake insha hadharani.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya kijamii – mwanafunzi anapoandika insha kuhusu suala la kijinsia.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya insha ya maelekezo. Anaeleza maana ya insha ya maelekezo kwa urahisi. Anaeleza maana ya insha ya maelekezo. Anaeleza kwa kiasi maana ya insha ya maelekezo. Anaeleza kwa kiasi maana ya insha ya maelekezo kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua aina za insha za maelekezo. Anatambua aina za insha za maelekezo kwa urahisi. Anatambua aina za insha za maelekezo. Anatambua baadhi ya aina za insha za maelekezo. Anatambua baadhi ya aina za insha za maelekezo kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili sifa za insha ya maelekezo. Anajadili sifa za insha ya maelekezo kwa urahisi. Anajadili sifa za insha ya maelekezo. Anajadili baadhi ya sifa za insha ya maelekezo. Anajadili baadhi ya sifa za insha ya maelekezo kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo. Anaandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo kwa wepesi. Anaandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo. Anaandaa kwa kiasi mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo. Anaandaa kwa kiasi mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandika insha akizingatia vipengele muhimu vya insha ya maelekezo. Anaandika kwa wepesi insha akizingatia vipengele muhimu vya insha ya maelekezo. Anaandika insha ya maelekezo akizingatia vipengele muhimu vya insha ya maelekezo. Anaandika insha ya maelekezo akizingatia baadhi ya vipengele muhimu vya insha ya maelekezo. Anaandika insha ya maelekezo akizingatia baadhi ya vipengele muhimu vya insha ya maelekezo kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
5.4 Sarufi 5.4.1 Nyakati na Hali
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kubainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea katika sentensi na vifungu
  2. kutumia wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea ifaavyo katika sentensi na vifungu
  3. kuchangamkia kutumia wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea ifaavyo ili kuboresha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kushirikiana na wenzake katika kikundi kubainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea kutoka kwenye chati, mti maneno, kapu maneno au kwa kuvipigia mstari kwenye sentensi na vifungu
  • kusoma kifungu kuhusu suala lengwa na kutambua nyakati na hali zilizotumiwa akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutunga sentensi kwa kutumia wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea ifaavyo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuandika sentensi kuhusu suala lengwa katika wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea kwenye kifaa cha kidijitali na kuwasambazia wenzake mtandaoni ili waziweke katika nyakati na hali zinazozingatiwa
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kubadilisha nyakati na hali katika kifungu kulingana na maagizo.
Kwa nini tunazingatia nyakati na hali mbalimbali katika mawasiliano?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapowatungia wenzake sentensi kwa kutumia nyakati na hali mbalimbali.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika kazi za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia kifaa cha kidijitali kuandika sentensi katika wakati na hali lengwa na kuwasambazia wenzake mtandaoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapobadilisha nyakati na hali mbalimbali na kutunga sentensi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapochangia kutambua nyakati na hali na kuzitungia sentensi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi wake kubadilisha nyakati na hali katika kifungu.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya kijamii – mwanafunzi anapotunga sentensi kuhusu suala la kijinsia.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia nyakati na hali.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kubainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea katika sentensi na vifungu. Anabainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea katika sentensi na vifungu kwa urahisi Anabainisha vitenzi vilivyo katika wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea katika sentensi na vifungu Anabainisha baadhi ya vitenzi vilivyo katika wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea katika sentensi na vifungu. Anabainisha baadhi ya vitenzi vilivyo katika wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea katika sentensi na vifungu kwa kuelekezwa
Kuweza kutumia wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea ifaavyo katika sentensi na vifungu. Anatunga sentensi kwa kutumia wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea ifaavyo kwa wepesi. Anatunga sentensi kwa kutumia wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea ifaavyo. Anatunga baadhi ya sentensi kwa kutumia wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea ifaavyo. Anatunga baadhi ya sentensi kwa kutumia wakati uliopo hali ya kuendelea, uliopita hali ya kuendelea na ujao hali ya kuendelea ifaavyo kwa kusaidiwa.





MADA 6.0: USALAMA SHULENI
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
6 .1 Kusikiliza na Kuzungumza 6.1.1 Kusikiliza kwa Kufasiri
Matini
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza kwa usahihi masuala yanayozungumziwa katika matini ya kusikiliza
  2. kufasiri habari katika matini ya kusikiliza
  3. kueleza maana ya msamiati kama ulivyotumika katika matini ya kusikiliza
  4. kutabiri kitakachotokea katika matini kwa kurejelea vidokezo katika matini ya kusikiliza
  5. kufurahia kufasiri matini za kusikiliza ili kukuza stadi ya kusikiliza.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza masuala yanayozungumziwa katika matini aliyosikiliza kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au katika vifaa vya kidijitali (k.v. simu, redio, kipakatalishi au runinga) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kufasiri habari katika matini aliyosikiliza akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kueleza maana ya msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumika katika habari aliyosikiliza akiwa peke yake,wawiliwawili au katika kikundi
  • kutabiri kitakachotokea katika matini kwa kurejelea vidokezo (k.v. picha, kichwa/anwani na toni ya mzungumzaji) vilivyopo katika matini akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusikiliza na kuchanganua habari katika matini za aina mbalimbali kuhusu suala lengwa.
Je, ni mambo gani utakayozingatia katika kuchanganua habari uliyosikiliza?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoeleza kwa ufasaha masuala yanayozungumziwa katika matini aliyosikiliza.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia ipasavyo vifaa vya kidijitali kama vile simu, redio, kipakatalishi au runinga kusikiliza matini.
  • Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anapotabiri kitakachotokea katika matini aliyosikiliza.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapowaelezea wenzake kuhusu masuala yanayozungumziwa katika matini aliyosikiliza.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapoeleza masuala yanayozungumziwa katika matini aliyosikiliza.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi na kutunza vifaa vya kidijitali anavyotumia.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wengine katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Suala la usalama – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika kikundi kuchanganua habari kwenye matini aliyosikiliza kuhusu usalama shuleni.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusikiliza na kufasiri matini.
  • Physical Education and Sports, Integrated Science na Home Science – masomo haya pia yanashughulikia masuala ya usalama.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza kwa usahihi masuala yanayozungumziwa katika matini ya kusikiliza. Anaeleza kwa usahihi na wepesi masuala yanayozungumziwa katika matini ya kusikiliza. Anaeleza kwa usahihi masuala yanayozungumziwa katika matini ya kusikiliza Anaeleza kwa usahihi baadhi ya masuala yanayozungumziwa katika matini ya kusikiliza. Anaeleza kwa usahihi baadhi ya masuala yanayozungumziwa katika matini ya kusikiliza.
Kuweza kufasiri habari katika matini ya kusikiliza. Anafasiri habari kwa wepesi katika matini ya kusikiliza. Anafasiri habari katika matini ya kusikiliza. Anafasiri baadhi ya habari katika matini ya kusikiliza. Anafasiri baadhi ya habari katika matini ya kusikiliza kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza maana ya msamiati kama ulivyotumika katika matini ya kusikiliza. Anaeleza maana ya msamiati kama ulivyotumika katika matini ya kusikiliza kwa urahisi. Anaeleza maana ya msamiati kama ulivyotumika katika matini ya kusikiliza. Anaeleza maana ya baadhi ya msamiati kama ulivyotumika katika matini ya kusikiliza. Anaeleza maana ya baadhi ya msamiati kama ulivyotumika katika matini ya kusikiliza kwa kusaidiwa.
Kuweza kutabiri kitakachotokea katika matini kwa kurejelea vidokezo vilivyopo. Anatabiri kwa wepesi kitakachotokea katika matini kwa kurejelea vidokezo vilivyopo. Anatabiri kitakachotokea katika matini kwa kurejelea vidokezo vilivyopo. Anatabiri kwa kiasi kitakachotokea katika matini kwa kurejelea vidokezo vilivyopo. Anatabiri kwa kiasi kitakachotokea katika matini kwa kurejelea vidokezo vilivyopo kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
6.2 Kusoma 6.2.1 Kusoma kwa Kina
Maudhui na Dhamira
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza dhana za maudhui na dhamira katika fasihi
  2. kujadili maudhui katika novela
  3. kujadili dhamira katika novela
  4. kutoa muhtasari wa dhamira na maudhui kuhusu novela
  5. kujenga mazoea ya usomaji wa kazi za fasihi katika maisha ya kila siku.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya maudhui katika fasihi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua maudhui mbalimbali katika novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake au katika kikundi
  • kujadili maudhui ya novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuwawasilishia wenzake darasani uchambuzi wake kuhusu maudhui ili waitolee maoni
  • kuandika maelezo mafupi kuhusu maudhui katika novela aliyosoma
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma chapisho la novela au kutoka mtandaoni na kutambua ujumbe wake
  • kueleza maana ya dhamira katika fasihi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua dhamira ya novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake au akiwa na wenzake
  • kuandika maelezo mafupi kuhusu dhamira ya novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake au katika kikundi
  • kuwawasilishia wenzake darasani uchambuzi wake kuhusu dhamira
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma novela iliyochapishwa au kutoka mtandaoni na kutambua dhamira yake.
Vitabu vya fasihi ulivyowahi kusoma vinazungumzia nini?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotambua na kujadili maudhui na dhamira kwenye novela akiwa na wenzake katika kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapotangamana na wenzake ili kuigiza matukio katika novela.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapoigiza novela katika kikundi na kuwawasilishia wenzake ufupisho wa maudhui na dhamira ili waujadili na kutoa maoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoigiza matukio katika novela akiwa na wenzake kwenye kikundi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapochambua maudhui na dhamira katika novela na kushirikiana na mzazi au mlezi katika uchambuzi.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake wanapotambua na kujadili maudhui na dhamira kwenye novela katika kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapotoa maoni kuhusu uwasilishaji wa wengine ili kuwarekebisha na kuwahimiza.
  • Umoja – mwanafunzi anapotagusana na wengine katika kikundi ili kutambua na kujadili maudhui na dhamira kwenye novela.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko anuwai – mwanafunzi anaposoma novela na kuchambua dhamira na maudhui yaliyomo.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusoma kwa kina.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza dhana za maudhui na dhamira katika fasihi. Anafafanua dhana za maudhui na dhamira katika fasihi kwa wepesi. Anafafanua dhana za maudhui na dhamira katika fasihi. Anafafanua kwa kiasi dhana za maudhui na dhamira katika fasihi. Anafafanua kwa kiasi dhana za maudhui na dhamira katika fasihi kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua na kujadili maudhui katika novela. Anatambua na kujadili maudhui katika novela kwa urahisi. Anatambua na kujadili maudhui katika novela. Anatambua bila kujadili maudhui katika novela. Anatambua bila kujadili maudhui katika novela kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua na kujadili dhamira katika novela. Anatambua na kujadili dhamira katika novela kwa urahisi. Anatambua na kujadili dhamira katika novela. Anatambua bila kujadili dhamira katika novela. Anatambua bila kujadili dhamira katika novela kwa kusaidiwa.
Kuweza kutoa muhtasari wa dhamira na maudhui kuhusu novela. Anatoa muhtasari wa dhamira na maudhui kuhusu novela kwa wepesi. Anatoa muhtasari wa dhamira na maudhui kuhusu novela. Anatoa kwa kiasi muhtasari wa dhamira na maudhui kuhusu novela. Anatoa muhtasari wa dhamira na maudhui kuhusu novela kwa kuelekezwa.

 

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
6.3 Kuandika 6.3.1 Insha za Masimulizi
Picha
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo mwanafunzi aweze:
  1. kubuni anwani inayooana na kisa atakachosimulia kutokana na picha kwenye matini
  2. kutoa maelezo dhahiri kuhusu matukio katika picha kwenye matini
  3. kuandika kisa chenye maelezo dhahiri kutokana na picha kwenye matini
  4. kufurahia kusimulia kisa kutokana na picha ili kukuza ubunifu.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kushirikiana na wenzake katika kikundi kusimuliana matukio kutokana na picha kwenye matini kuhusu suala lengwa
  • kubuni anwani inayooana na kisa atakachosimulia kutokana na picha kwenye matini akiwa peke yake au kwenye kikundi
  • kutoa maelezo dhahiri kuhusu matukio katika picha kwenye matini akiwa peke yake au katika kikundi
  • kuandika kisa chenye maelezo dhahiri kutokana na picha kwenye matini
  • kuwasomea wenzake kisa alichoandika ili wakitolee maoni
  • kushirikiana na mzazi au mlezi wake kutafiti mtandaoni au vitabuni kuhusu insha za picha kisha wasimuliane visa kutokana na picha.
Je, ni vigezo vipi utakavyozingatia wakati wa kuandika insha ya kubuni kutokana na picha?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotoa maelezo dhahiri kutokana na picha kwenye matini.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kujadiliana kuhusu matukio kwenye picha.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia kifaa cha kidijitali kutafiti kuhusu insha za kusimulia mtandaoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika kisa chenye maelezo dhahiri kutokana na picha.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapotafuta habari mtandaoni au vitabuni na mzazi au mlezi wake.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi. Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.

Masuala Mtambuko

  • Masuala ya usalama – mwanafunzi anapoandika insha kuhusu usalama shuleni.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kubuni anwani inayooana na kisa atakachosimulia kutokana na picha kwenye matini. Anabuni kwa urahisi anwani inayooana na kisa atakachosimulia kutokana na picha kwenye matini. Anabuni anwani inayooana na kisa atakachosimulia kutokana na picha kwenye matini. Anabuni anwani inayooana kwa kiasi na kisa atakachosimulia kutokana na picha kwenye matini. Anabuni anwani inayooana kwa kiasi na kisa atakachosimulia kutokana na picha kwenye matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutoa maelezo dhahiri kuhusu matukio katika picha kwenye matini. Anatoa maelezo dhahiri kuhusu matukio katika picha kwenye matini kwa wepesi. Anatoa maelezo dhahiri kuhusu matukio katika picha kwenye matini. Anatoa baadhi ya maelezo dhahiri kuhusu matukio katika picha kwenye matini. Anatoa baadhi ya maelezo dhahiri kuhusu matukio katika picha kwenye matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kuandika kisa chenye maelezo dhahiri kutokana na picha kwenye matini. Anaandika kwa wepesi kisa chenye maelezo dhahiri kutokana na picha kwenye matini. Anaandika kisa chenye maelezo dhahiri kutokana na picha kwenye matini. Anaandika kwa kiasi kisa chenye maelezo dhahiri kutokana na picha kwenye matini. Anaandika kwa kiasi kisa chenye maelezo dhahiri kutokana na picha kwenye matini kwa kusaidiwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
6.4 Sarufi 6.4.1 Vitenzi Vikuu na Vitenzi Visaidizi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua vitenzi vikuu na visaidizi katika sentensi
  2. kutumia vitenzi vikuu na visaidizi ipasavyo katika sentensi
  3. kuchangamkia kutumia vitenzi vikuu na visaidizi ipasavyo katika mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua vitenzi vikuu (k.v. cheka, tembea, shiba, pona, soma, n.k.) na visaidizi (k.v. kuwa, weza, kuja, -ngali, bidi, wahi, n.k.) kwenye chati, kadi maneno, kapu maneno au tarakilishi akiwa peke yake au katika kikundi
  • kubainisha vitenzi vikuu na visaidizi katika sentensi au vifungu kwenye vitabu, tarakilishi au chati kwa kuvikolezea wino au kuvipigia mstari akiwa na wenzake au katika kikundi
  • kutunga sentensi kuhusu masuala mtambuko anuwai kwa kutumia ipasavyo vitenzi vikuu na visaidizi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushirikiana na mzazi au mlezi wake kutunga sentensi zinazohusu shughuli katika mazingira ya nyumbani kwa kutumia vitenzi vikuu na visaidizi (k.v. Mtoto huyu huwa anajali usalama wake).
Kuna tofauti gani kati ya vitenzi vikuu na visaidizi?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotaja kwa uwazi vitenzi vikuu na visaidizi vinavyojitokeza katika sentensi na vifungu.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapochangia kazi za kikundi huku akiwapa wenzake nafasi ya kushiriki na kutoa maoni yao.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kutambua vitenzi vikuu na visaidizi.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi akitumia vitenzi vikuu na visaidizi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapochangia kutambua vitenzi vikuu na visaidizi na kuvitungia sentensi na vifungu sahihi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi wake kutunga sentensi zenye vitenzi vikuu na visaidizi vinavyohusu shughuli katika mazingira ya nyumbani.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wengine nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko anuwai – mwanafunzi anapotunga sentensi kwa kutumia vitenzi vikuu na visaidizi kwa kuzingatia masuala mtambuko.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia aina za vitenzi.
  • Home Science na Integrated Science – masomo haya pia yana mada zinazoshughulikia masuala ya usalama.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua vitenzi vikuu na visaidizi katika sentensi. Anatambua kwa wepesi vitenzi vikuu na visaidizi katika sentensi. Anatambua vitenzi vikuu na visaidizi katika sentensi. Anatambua baadhi ya vitenzi vikuu na visaidizi katika sentensi. Anatambua baadhi ya vitenzi vikuu na visaidizi katika sentensi kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia vitenzi vikuu na visaidizi ipasavyo katika sentensi. Anatumia vitenzi vikuu na visaidizi ipasavyo katika sentensi kwa urahisi. Anatumia vitenzi vikuu na visaidizi ipasavyo katika sentensi. Anatumia vitenzi vikuu na visaidizi ipasavyo katika baadhi ya sentensi. Anatumia vitenzi vikuu na visaidizi ipasavyo katika baadhi ya sentensi kwa kuelekezwa.

 

MADA 7.0: KUHUDUMIA JAMII SHULENI
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
7.1 Kusikiliza na Kuzungumza 7.1.1 Kusikiliza kwa Ufahamu
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua ujumbe katika ufahamu wa kusikiliza
  2. kueleza maana ya msamiati ulio katika ufahamu wa kusikiliza
  3. kufasiri ujumbe kutokana na ufahamu wa kusikiliza
  4. kuchangamkia kushiriki katika kusikiliza kwa ufahamu ili kukuza stadi ya kusikiliza kwa ufahamu.
Mwanafunzi aelekezwe:
  •  kutambua ujumbe wa suala lengwa uliotumiwa katika ufahamu wa kusikiliza kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au kwenye kifaa cha kidijitali, akiwa peke yake au katika kikundi
  • kueleza maana za msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumiwa katika kauli au sentensi zilizosemwa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusikiliza kauli au vifungu vya sentensi kuhusu suala lengwa kutoka kwa mwalimu au mgeni mwalikwa akiwa peke yake na katika kikundi na kufasiri ujumbe katika kauli au sentensi hizo
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusikiliza kwa ufahamu kuhusu suala lengwa kutoka kwa kifaa cha kidijitali na kutambua maana ya msamiati na ujumbe muhimu.
  1. Je, kusikiliza kwa ufahamu kuna faida zipi?
  2. Rafiki yako anakutolea maelezo mafupi kuhusu umuhimu wa kuihudumia jamii ya shule yako. Utafanya nini ili uelewe anachosema?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
● Mawasiliano – mwanafunzi anapozisema kwa usahihi kauli au sentensi zilizosemwa.
● Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki katika kujadili kuhusu vipengele vya kuzingatia katika kusikiliza kwa ufahamu.
● Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusikiliza kauli na sentensi na kujibu.
● Ubunifu – mwanafunzi anaposikiliza na kusema upya alichoambiwa. Pia anapofasiri wazo kuu.
● Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anapofasiri ujumbe kutokana na ufahamu wa kusikiliza.
● Kujiamini – mwanafunzi anaposikiliza kauli au sentensi na kujibu bila woga. Pia anapochangia katika shughuli ya vikundi.
● Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki shughuli ya kusikiliza kwa ufahamu na mzazi au mlezi wake na kujifunza njia bora za kusikiliza na kujibu katika shughuli ya kusikiliza kwa ufahamu.
Maadili
● Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika shughuli za vikundi; pia anapoheshimu zamu ya wenzake katika mazungumzo.
● Upendo – mwanafunzi anapowasikiliza wasemaji kwa makini. Pia anapowapa wanafunzi wenzake zamu ya kuzungumza.
● Uwajibikaji – mwanafunzi anapotunza vifaa vya kidijitali anavyotumia katika mazungumzo.
● Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za vikundi.
Masuala Mtambuko
● Masuala ya shughuli za huduma kwa jamii – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli ya ujifunzaji wa kusikiliza kwa ufahamu kuhusu kuhudumia jamii shuleni.
Uhusiano na Masomo Mengine
● English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia dhana ya kusikiliza kwa ufahamu.
● Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua ujumbe katika ufahamu wa kusikiliza. Anatambua kwa wepesi ujumbe katika ufahamu wa kusikiliza. Anatambua ujumbe katika ufahamu wa kusikiliza. Anatambua baadhi ya ujumbe katika ufahamu wa kusikiliza. Anatambua baadhi ya ujumbe katika ufahamu wa kusikiliza kwa kuelekezwa.
Kuweza kueleza maana ya msamiati ulio katika ufahamu wa kusikiliza. Anaeleza kwa wepesi maana ya msamiati ulio katika ufahamu wa kusikiliza. Anaeleza maana ya msamiati ulio katika ufahamu wa kusikiliza. Anaeleza maana ya baadhi ya msamiati ulio katika ufahamu wa kusikiliza. Anaeleza maana ya baadhi ya msamiati ulio katika ufahamu wa kusikiliza kwa kusaidiwa.
Kuweza kufasiri ujumbe kutokana na ufahamu wa kusikiliza. Anafasiri kwa ufasaha ujumbe kutokana na ufahamu wa kusikiliza. Anafasiri ujumbe kutokana na ufahamu wa kusikiliza. Anafasiri baadhi ya ujumbe kutokana na ufahamu wa kusikiliza. Anafasiri baadhi ya ujumbe kutokana na ufahamu wa kusikiliza kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
7.2 Kusoma 7.2.1 Ufupisho
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya ufupisho ili kuupambanua
  2. kutambua habari kuu za aya na kuzieleza kwa usahihi katika sentensi moja
  3. kufupisha kifungu akizingatia mpangilio ufaao wa habari kutokana na matini
  4. kufurahia kufupisha habari kwa usahihi katika mawasiliano ya kila siku.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya ufupisho akiwa peke yake au katika kikundi ili kuupambanua
  • kusoma kifungu kuhusu suala lengwa katika matini andishi au ya kidijitali akiwa peke yake au katika kikund
  • kutambua kwenye matini andishi au ya kidijitali habari kuu za aya na kuzieleza kwa usahihi kwa kuzingatia mtazamo wa matini katika matini ya kufupishwa akishirikiana na wenzake
  • kufupisha kifungu alichosoma kwa kuzingatia mpangilio ufaao wa habari sahihi kutokana na matini akishirikiana na wenzake katika kikundi
  • kuwawasilishia wenzake kazi yake ili waitolee maoni
  • kushirikiana na mzazi au mlezi wake kufupisha kifungu wakizingatia mpangilio ufaao wa habari sahihi kutokana na matini.
Unazingatia nini unapofupisha kifungu?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapojadiliana na wenzake katika kikundi habari kuu za aya kwenye kifungu alichosoma.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kudondoa habari kuu za aya muhimu katika kifungu.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapoandaa ufupisho na kuwawasilishia wenzake ili waitolee maoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika ufupisho kwa kuzingatia mpangilio ufaao.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anaposoma kifungu mtandaoni na kudondoa hoja muhimu.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi wanapojadili hoja na maneno muhimu.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi. Pia, anapojitolea kuiandaa kazi yake ili kuwawasilishia wenzake.
  • Umoja – mwanafunzi anapotangamana na wenzake katika kikundi kujadili maneno na hoja muhimu katika kifungu.
Masuala Mtambuko
  • Huduma kwa jamii – mwanafunzi apofupisha kifungu kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia ufupisho.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya ufupisho ili kuupambanua. Anaeleza kwa urahisi maana ya ufupisho ili kuupambanua. Anaeleza maana ya ufupisho ili kuupambanua. Anaeleza kwa kiasi maana ya ufupisho ili kuupambanua. Anaeleza kwa kiasi maana ya ufupisho ili kuupambanua kwa kuelekezwa.
Kuweza kutambua habari kuu za aya na kuzieleza kwa usahihi katika sentensi moja. Anatambua kwa urahisi habari kuu za aya na kuzieleza kwa usahihi katika sentensi moja kwa urahisi. Anatambua habari kuu za aya na kuzieleza kwa usahihi katika sentensi moja. Anatambua baadhi ya habari kuu za aya na kuzieleza kwa usahihi katika sentensi moja. Anatambua baadhi ya habari kuu za aya na kuzieleza kwa usahihi katika sentensi moja kwa kusaidiwa.
Kuweza kufupisha kifungu akizingatia mpangilio ufaao wa habari kutokana na matini. Anafupisha kifungu akizingatia mpangilio ufaao wa habari kutokana na matini kwa urahisi. Anafupisha kifungu akizingatia mpangilio ufaao wa habari kutokana na matini. Anafupisha sehemu ya kifungu akizingatia mpangilio ufaao wa habari kutokana na matini. Anafupisha sehemu ya kifungu akizingatia mpangilio ufaao wa habari kutokana na matini kwa kuelekezwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
7.3 Kuandika 7.3.1 Insha za Kubuni Maelezo
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya insha ya maelezo
  2. kutambua msamiati ufaao katika kutoa maelezo
  3. kutambua umuhimu wa msamiati ufaao katika insha ya maelezo
  4. kutumia msamiati ufaao kwa ufasaha katika kuandika insha ya maelezo
  5. kufurahia kuandika insha za maelezo ili kujenga stadi ya kuandika.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua msamiati ufaao katika kutoa maelezo (k.v vivumishi, vielezi, n.k) kutoka kwa vielelezo vya insha kwenye matini za kimaandishi au za kidijitali akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutumia kifaa cha kidijitali kupigia mstari maneno yaliyotumiwa kutoa maelezo katika kifungu akiwa peke yake, katika kikundi au na mzazi au mlezi wake
  • kutambua umuhimu wa kuteua maneno yafaayo katika insha kielelezo (k.v. kushawishi, kuburudisha, kupasha habari au kufunza)
  • kuandika insha ya maelezo kwa kuzingatia msamiati ufaao ili kujenga maelezo dhahiri yenye kuathiri hisia mbalimbali na kutekeleza majukumu ya kushawishi, kuburudisha, kupasha habari au kufunza
  • kuwasomea wenzake insha aliyoandika ili waitolee maoni.
Je, unatumia lugha ya aina gani unapotaka kumweleza mtu jambo fulani ili aweze kupata picha kamili?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoandika insha ya maelezo inayotumia maneno yanayojenga picha dhahiri.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kusahihisha insha.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kupigia mstari maneno yaliyotumiwa.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapofaulu kuandika insha inayosawiri picha halisi ya kitu anachoelezea.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapowasomea wenzake insha aliyoandika ili waikosoe pamoja.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposhiriki kuwasomea wenzake insha.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko mbalimbali - kutokana na maelezo yanayotolewa na mwanafunzi katika insha yake.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha ya maelezo.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya insha ya maelezo. Anaeleza maana ya insha ya maelezo kwa urahisi. Anaeleza maana ya insha ya maelezo. Anaeleza kwa kiasi maana ya insha ya maelezo. Anaeleza kwa kiasi maana ya insha ya maelezo kwa kuelekezwa.
Kuweza kutambua msamiati ufaao katika kutoa maelezo. Anatambua kwa urahisi msamiati ufaao katika kutoa maelezo. Anatambua msamiati ufaao katika kutoa maelezo. Anatambua baadhi ya msamiati ufaao katika kutoa maelezo. Anatambua baadhi ya msamiati ufaao katika kutoa maelezo kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua umuhimu wa msamiati ufaao katika insha ya maelezo. Anatambua kwa urahisi umuhimu wa msamiati ufaao katika insha ya maelezo. Anatambua umuhimu wa msamiati ufaao katika insha ya maelezo. Anatambua baadhi ya umuhimu wa msamiati ufaao katika insha ya maelezo. Anatambua baadhi ya umuhimu wa msamiati ufaao katika insha ya maelezo kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia msamiati ufaao kwa ufasaha katika kuandika insha ya maelezo. Anatumia msamiati ufaao kwa ufasaha katika kuandika insha ya maelezo kwa urahisi. Anatumia msamiati ufaao kwa ufasaha katika kuandika insha ya maelezo. Anatumia baadhi ya msamiati ufaao kwa ufasaha katika kuandika insha za maelezo. Anatumia baadhi ya msamiati ufaao kwa ufasaha katika kuandika insha za maelezo kwa kuelekezwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
7.4 Sarufi 7.4.1 Vitenzi vishirikishi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua vitenzi vishirikishi katika matini mbalimbali
  2. kutumia vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu
  3. kuonea fahari matumizi ya vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu.
Mwanafunzi aelekezwe:
  •  kujadili na mwenzake maana ya vitenzi vishirikishi
  • kuchopoa vitenzi vishirikishi (k.v. ni, si, yu, ndiye, ndio, ndipo) kwenye chati, kadi maneno, kapu maneno au tarakilishi
  • kutaja vitenzi vishirikishi vinavyojitokeza katika sentensi na vifungu akiwa na wenzake katika kikundi
  • kutenga vitenzi vishirikishi katika orodha ya maneno, sentensi au vifungu kwenye vitabu, tarakilishi kwa kuvikolezea wino au kuvipigia mstari
  • kutunga sentensi na vifungu kwa kutumia vitenzi vishirikishi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushirikiana na mzazi au mlezi wake kutunga sentensi zenye vitenzi vishirikishi zinazohusu shughuli katika mazingira ya nyumbani (k.v Mtoto alikuwa nje ya mlango, Yeye ndiye hupika, n.k.)
Je, unajua aina gani za vitenzi?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotaja kwa uwazi vitenzi vishirikishi vinavyojitokeza katika sentensi na vifungu. Pia anapojadiliana na mwenzake kuhusu maana ya kitenzi kishirikishi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia kazi za vikundi huku akiwapa wenzake nafasi ya kushiriki na kutoa maoni yao.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kutambua vitenzi vishirikishi.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuhusu suala lengwa akitumia vitenzi vishirikishi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposhiriki kutambua vitenzi vishirikishi na kuvitungia sentensi sahihi na vifungu kwa ukakamavu.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  •  Masuala ya huduma kwa jamii – mwanafunzi anapoandika sentensi na vifungu kuhusu suala lengwa kwa kutumia vitenzi vishirikishi.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia aina za vitenzi.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu. Anatambua kwa wepesi vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu. Anatambua vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu. Anatambua baadhi ya vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu. Anatambua baadhi ya vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu. Anatumia vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu kwa urahisi. Anatumia vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu. Anatumia baadhi ya vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu. Anatumia baadhi ya vitenzi vishirikishi katika sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.





MADA 8.0 ULANGUZI WA BINADAMU
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
8.1 Kusikiliza na Kuzungumza 8.1.1 Mazungumzo ya Kupasha Habari
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya mazungumzo ya kupasha habari ili kuyatofautisha na aina nyingine za mazungumzo
  2. kutambua aina za mazungumzo ya kupasha habari
  3. kujadili vipengele vya kuzingatia katika mazungumzo ya kupasha habari
  4. kupasha habari kwa kutumia vipengele vifaavyo vya mazungumzo ya kup-asha habari
  5. kuchangamkia kupasha habari mbalimbali ili kufanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya mazungumzo ya kupasha habari akiwa peke yake au katika kikundi
  • kushiriki katika vikundi kujadili aina za mazungumzo ya kupasha habari katika jamii yake (k.v mihadhara, mafunzo shuleni kuhusu suala fulani, maelezo kuhusu namna ya kutumia kifaa fulani, warsha, semina, n.k.)
  • kutambua mazungumzo ya kupasha habari kutoka kwenye aina za mazungumzo alizosikiliza kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa, wanafunzi wenzake au vifaa vya kidijitali (k.v. vinasasauti)
  • kusikiliza mazungumzo ya kupasha habari yakitolewa na mwalimu, mgeni mwalikwa au katika vifaa vya kidijitali na kutathmini kama yametumia vipengele vifaavyo vya mazungumzo ya kupasha habari
  • kujadili vipengele vya kuzingatia katika mazungumzo ya kupasha habari (k.v. kuteua mada, kuzingatia ukweli wa masuala kulingana na suala kuu unalozungumzia, kutumia lugha sahili kulingana na hadhira, n.k.) akiwa peke yake au katika kikundi
  • kushiriki katika mazungumzo ya kupasha habari kuhusu suala lengwa akiwa peke yake au katika kikundi akitumia vipengele vifaavyo vya mazungumzo ya kupasha habari
  • kushiriki katika mazungumzo na mzazi au mlezi wake kuhusu suala lengwa huku akitumia vipengele vifaavyo vya uwasilishaji wa mazungumzo ya kupasha habari.
  1. Je, mazungumzo ya kupasha habari hutol-ewa katika miktadha gani ya jamii yako?
  2. Je, utatumia mikakati gani ili kuwapasha wanajamii habari kuhusu mambo mbalimbali?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapowaelimisha wenzake kuhusu suala lengwa kwa kutumia lugha sahili. Pia anapowaeleza wenzake kwa lugha nyepesi kuhusu vipengele vya kuzingatia ili kufanikisha mawasiliano.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga mazungumzo ya kupasha habari kuhusu suala lengwa.
  • Uwazaji kina – mwanafunzi anapopasha habari kuhusu mambo mbalimbali yanayoathiri jamii.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposhiriki katika mazungumzo ili kupasha habari kuhusu suala lengwa.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki na mzazi au mlezi wake katika mazungumzo ya kupasha habari kuhusu suala lengwa.

Maadili

  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapoihusisha hadhira yake. Pia anapowapa wenzake zamu ya kushiriki katika mazungumzo kuhusu suala lengwa.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapotunza vifaa vya kidijitali anavyotumia katika kujifunza mazungumzo ya kupasha habari.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
  • Amani – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi kwa utulivu.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya usalama – mwanafunzi anaposhiriki katika kupasha habari kuhusu suala la ulanguzi wa binadamu.
  • Ukakamavu – mwanafunzi anapowapasha wenzake habari kuhusu ulanguzi wa binadamu.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia stadi ya kuzungumza.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii kama vile ulanguzi wa binadamu.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya mazungumzo ya kupasha habari kwa usahihi. Anaeleza kwa urahisi maana ya mazungumzo ya kupasha habari kwa usahihi. Anaeleza maana ya mazungumzo ya kupasha habari kwa usahihi. Anaeleza kwa kiasi maana ya mazungumzo ya kupasha habari. Anaeleza kwa kiasi maana ya mazungumzo ya kupasha habari kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua aina za mazungumzo ya kupasha habari. Anatambua kwa urahisi aina za mazungumzo ya kupasha habari. Anatambua aina za mazungumzo ya kupasha habari. Anatambua baadhi ya aina za mazungumzo za kupasha habari. Anatambua baadhi ya aina za mazungumzo ya kupasha habari kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili vipengele vya kuzingatia katika mazungumzo ya kupasha habari. Anajadili kwa wepesi vipengele vya kuzingatia katika mazungumzo ya kupasha habari. Anajadili vipengele vya kuzingatia katika mazungumzo ya kupasha habari. Anajadili baadhi ya vipengele vya kuzingatia katika mazungumzo ya kupasha habari. Anajadili baadhi ya vipengele vya kuzingatia katika mazungumzo ya kupasha habari kwa kusaidiwa.
Kuweza kupasha habari kwa kutumia vipengele vifaavyo vya mazungumzo ya kupasha habari. Anapasha habari kwa wepesi kwa kutumia vipengele vifaavyo vya mazungumzo ya kupasha habari. Anapasha habari kwa kutumia vipengele vifaavyo vya mazungumzo ya kupasha habari. Anapasha habari kwa kutumia baadhi ya vipengele vifaavyo vya mazungumzo ya kupasha habari. Anapasha habari kwa kutumia baadhi ya vipengele vifaavyo vya mazungumzo ya kupasha habari kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
8.2 Kusoma 8.2.1 Kusoma kwa Kina
Mandhari na Ploti
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya mandhari na ploti katika fasihi
  2. kutambua mandhari mbalimbali na ploti ya novela
  3. kueleza umuhimu wa mandhari na ploti ya novela
  4. kuandika maelezo mafupi kuhusu mandhari na ploti ya novela aliyosoma
  5. kuchangamkia nafasi ya mandhari na ploti katika kazi ya fasihi.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya mandhari katika fasihi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua mandhari mbalimbali katika novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake au katika kikundi
  • kujadili umuhimu wa mandhari ya novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake au katika kikundi
  • kuwawasilishia wenzake darasani uchambuzi wake kuhusu mandhari
  • kuandika maelezo mafupi kuhusu mandhari ya novela iliyoteuliwa na mwalimu
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma chapisho la novela au kutoka mtandaoni na kutambua mandhari yake
  • kueleza maana ya ploti katika fasihi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi kutambua ploti ya novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake au akiwa na wenzake
  • kujadili umuhimu wa ploti ya novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake au na wenzake
  • kuandika maelezo mafupi kuhusu ploti ya novela iliyoteuliwa na mwalimu
  • kuwawasilishia wenzake darasani uchambuzi wake kuhusu ploti
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma novela iliyochapishwa au kutoka mtandaoni na kutambua ploti yake.
  1. Ni mandhari gani unayokumbuka yaliyo katika kazi za fasihi ulizowahi kusoma?
  2. Ploti ya hadithi ina vipengele gani?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotambua na kujadili mandhari na ploti katika novela akiwa na wenzake katika kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapotangamana na wenzake kuchambua mandhari na ploti ya novela.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapowasilisha kazi yake darasani.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapochanganua habari katika novela ili kupata mandhari na ploti.
  • Uwazaji kina – mwanafunzi anapoeleza umuhimu wa mandhari na ploti katika novela.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapotafiti na kujiandaa ili awawasilishie wenzake muhtasari wa mandhari na ploti.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake wanapotambua na kujadili mandhari na ploti kwenye novela katika kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapotoa maoni kuhusu uwasilishaji wa wengine ili kuwarekebisha na kuwahimiza.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anaposoma na kuchanganua novela.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wengine katika kikundi ili kutambua na kujadili mandhari na ploti kwenye novela.
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anapochangia katika kikundi, anapofanya uchambuzi kuhusu mandhari na ploti katika novela na kuwasilisha akiwa na wenzake anajifunza ukakamavu, mbinu za mawasiliano na stahamala.
  • Masuala mtambuko anuwai – kutokana na ujumbe katika novela.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusoma kwa kina.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya mandhari na ploti katika fasihi. Anaeleza maana ya mandhari na ploti katika fasihi kwa urahisi. Anaeleza maana ya mandhari na ploti katika fasihi. Anatoa maelezo kiasi kuhusu maana ya mandhari na ploti katika fasihi. Anatoa maelezo kiasi kuhusu maana ya mandhari na ploti katika fasihi kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua mandhari mbalimbali na ploti katika novela. Anatambua mandhari mbalimbali na ploti katika novela kwa urahisi. Anatambua mandhari mbalimbali na ploti katika novela. Anatambua baadhi ya mandhari na baadhi ya vipengele vya ploti katika novela. Anatambua baadhi ya mandhari na baadhi ya vipengele vya ploti katika novela kwa kuelekezwa.
Kuweza kueleza umuhimu wa mandhari na ploti katika novela. Anaeleza umuhimu wa mandhari na ploti katika novela kwa urahisi. Anaeleza umuhimu wa mandhari na ploti katika novela. Anaeleza baadhi ya umuhimu wa mandhari na ploti katika novela. Anaeleza baadhi ya umuhimu wa mandhari na ploti katika novela kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandika maelezo mafupi kuhusu mandhari na ploti ya novela aliyosoma. Anaandika maelezo mafupi kuhusu mandhari na ploti ya novela aliyosoma kwa wepesi. Anaandika maelezo mafupi kuhusu mandhari na ploti ya novela aliyosoma. Anaandika kwa kiasi maelezo mafupi kuhusu mandhari na ploti ya novela aliyosoma. Anaandika kwa kiasi maelezo mafupi kuhusu mandhari na ploti ya novela aliyosoma.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
8.3 Kuandika 8.3.1 Kuandika
Viakifishi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua matumizi ya kiulizi na koma katika maneno, sentensi au vifungu
  2. kutumia kiulizi na koma ipasavyo katika maneno, sentensi au vifungu
  3. kufurahia matumizi bora ya kiulizi na koma katika maneno, sentensi au vifungu.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua matumizi ya kiulizi (k.v. mwishoni mwa sentensi ya swali) na koma (k.v kutenga orodha ya vitu vitatu au kuandika anwani, n.k.) katika maneno, sentensi au vifungu vya maneno kwenye matini andishi na za kidijitali akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutumia kifaa cha kidijitali kusoma matumizi ya kiulizi na koma akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuandika maneno, sentensi au vifungu vya maneno kuhusu suala lengwa kwa kutumia kiulizi na koma ipasavyo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuandika kwenye kifaa cha kidijitali (k.v. tarakilishi) kifungu kifupi kuhusu suala lengwa kwa kuzingatia kiulizi na koma ipasavyo na kuwasambazia wenzake kwenye mtandao ili wakitolee maoni
  • kushirikiana na wenzake kusahihisha kifungu kuhusu suala lengwa ambacho hakijatumia kiulizi na koma ipasavyo
  • kuwasomea wenzake kifungu alichoandika na kuwataka waandike maneno, sentensi au vifungu vinavyostahili kuwa na kiulizi na koma
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kutafiti mtandaoni au katika vitabu vya ziada kuhusu matumizi ya kiulizi na koma katika maneno, sentensi au vifungu.
  1. Je, kiulizi hutumiwa vipi katika maandishi?
  2. Je, koma hutumiwa wapi katika sentensi?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotumia koma na kiulizi ipasavyo katika maandishi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika kujadili matumizi ya kiulizi na koma.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia kifaa cha kidijitali kusoma matumizi ya kiulizi na koma.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika vifungu vyenye matumizi yafaayo ya kiulizi na koma ubunifu wake unajengeka.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi kutafiti mtandaoni au katika vitabu vya ziada kuhusu matumizi ya kiulizi na koma.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko anuwai (k.v. ulanguzi wa binadamu, haki za watoto, n.k.) kulingana na sentensi na vifungu vinavyotungwa na mwanafunzi.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uakifishaji.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua matumizi ya kiulizi na koma katika maneno, sentensi au vifungu. Anatambua matumizi ya kiulizi na koma katika maneno, sentensi au vifungu kwa urahisi. Anatambua matumizi ya kiulizi na koma katika maneno, sentensi au vifungu. Anatambua baadhi ya matumizi ya kiulizi na koma katika maneno, sentensi au vifungu. Anatambua baadhi ya matumizi ya kiulizi na koma katika maneno, sentensi au vifungu kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia kiulizi na koma ipasavyo katika maneno, sentensi au vifungu. Anatumia kiulizi na koma ipasavyo katika maneno, sentensi au vifungu kwa urahisi. Anatumia kiulizi na koma ipasavyo katika maneno, sentensi au vifungu. Anatumia kiulizi na koma ipasavyo katika baadhi ya maneno, sentensi au vifungu. Anatumia kiulizi na koma ipasavyo katika baadhi ya maneno, sentensi au vifungu kwa kuelekezwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
8.4 Sarufi 8.4.1 Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua nomino za ngeli ya A-WA na U-I katika matini mbalimbali
  2. kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya A-WA na U-I katika sentensi
  3. kutumia nomino za ngeli ya A-WA na U-I katika sentensi na vifungu kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi
  4. kuchangamkia kutumia nomino za ngeli ya A-WA na U-I katika sentensi na vifungu.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kuchopoa nomino za ngeli ya A-WA (k.v. mtoto, ndege, simba, msichana, n.k) na U-I (k.v. mti, mkono, n.k.) kwenye chati, kadi maneno, kapu maneno au tarakilishi akiwa peke, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutaja majina ya vitu katika mazingira ya shuleni yaliyo katika ngeli ya A-WA (k.v. mwalimu, mwanafunzi, mpishi n.k) na U-I (k.v mti, mlango, n.k.) akiwa na wenzake katika kikundi
  • kutenga nomino za ngeli ya A-WA na U-I katika orodha ya nomino, sentensi au vifungu kwenye vitabu, tarakilishi, chati kwa kuzikolezea wino au kuzipigia mstari akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya A-WA na U-I katika sentensi na mafungu ya maneno akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga sentensi au vifungu vyenye upatanisho ufaao wa kisarufi kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za ngeli ya A-WA na U-I akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kumtajia mzazi au mlezi wake majina yaliyo katika ngeli ya A-WA (k.v mama, kuku, ndege, n.k.) na U-I (k.v mti, mto, mkeka, msitu n.k.) katika mazingira ya nyumbani.
Ni vitu gani katika mazingira yako vilivyo na majina yanayopatikana katika ngeli ya A-WA na U-I?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotoa mchango katika kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kutambua nomino katika ngeli ya A-WA na U-I.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuhusu suala lengwa akitumia nomino za ngeli ya A-WA na U-I.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kutambua nomino za ngeli ya A-WA na U-I na kuzitungia sentensi na vifungu sahihi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapomtajia mzazi au mlezi wake nomino za ngeli ya A-WA na U-I katika mazingira ya nyumbani.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kutenga nomino za ngeli ya A-WA na U-I katika sentensi na vifungu.
  • Masuala ya ulanguzi wa binadamu – mwanafunzi anapoandika kifungu kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za ngeli ya A-WA na U-I.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia upatanisho wa kisarufi.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya ulanguzi wa binadamu.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua nomino katika ngeli ya A-WA na U-I katika matini. Anatambua kwa wepesi nomino katika ngeli ya A-WA na U-I katika matini. Anatambua nomino katika ngeli ya A-WA na U-I katika matini. Anatambua baadhi ya nomino katika ngeli ya A-WA na U-I katika matini. Anatambua baadhi ya nomino katika ngeli ya A-WA na U-I katika matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi katika ngeli ya A-WA na U-I katika sentensi. Anatambua kwa wepesi viambishi vya upatanisho wa kisarufi katika ngeli ya A-WA na U-I katika sentensi. Anatambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi katika ngeli ya A-WA na U-I katika sentensi. Anatambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi katika ngeli ya A-WA na U-I katika baadhi ya sentensi. Anatambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi katika ngeli ya A-WA na U-I katika baadhi ya sentensi kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia nomino katika ngeli ya A-WA na U-I kutunga sentensi zenye upatanisho ufaao wa kisarufi. Anatumia nomino katika ngeli za A-WA na U-I kutunga sentensi zenye upatanisho ufaao wa kisarufi kwa wepesi. Anatumia nomino katika ngeli ya A-WA na U-I kutunga sentensi zenye upatanisho ufaao wa kisarufi. Anatumia baadhi ya nomino katika ngeli ya A-WA na U-I kutunga sentensi zenye upatanisho ufaao wa kisarufi. Anatumia baadhi ya nomino katika ngeli ya A-WA na U-I kutunga sentensi zenye upatanisho ufaao wa kisarufi kwa kusaidiwa.



MADA 9.0 MATUMIZI YA VIFAA VYA KIDIJITALI KATIKA MAWASILIANO
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
9.1 Kusikiliza na Kuzungumza 9.1.1 Kusikiliza kwa Kina
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua sauti /d/ na /nd/ katika silabi na maneno
  2. kutamka sauti /d/ na /nd/ ipasavyo ili kuzitofautisha kimatamshi katika silabi na maneno
  3. kuchangamkia matamshi bora ya sauti /d/ na /nd /katika mazungumzo ya kawaida ili kufanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua sauti /d/ na /nd/ katika maneno na silabi (k.v. doa/ndoa; duni/nduni; dugu/ndugu, n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutafuta maneno yenye sauti /d/ na /nd/ katika matini andishi na za kidijitali na kuyatamka ipasavyo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga vitanzandimi vinavyotumia sauti /d/ na /nd/ na kujirekodi kwa kutumia kifaa cha kidijitali (k.v simu, tabuleti, redio na kanda za sauti)
  • kusikiliza akiwa na wenzake vitanzandimi alivyovirekodi ili kuvitathmini
  • kusikiliza vitanzandimi vinavyotumia sauti /d/ na /nd/ katika kifaa cha kidijitali (k.v simu, redio na kanda za sauti.) akiwa na wenzake katika kikundi
  • kushiriki mazungumzo na mzazi au mlezi wake kwa kuzingatia matamshi bora ya sauti /d/na /nd/.
Ni maneno yepi unayoyajua yaliyo na sauti /d/ na /nd/?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anaposhiriki katika mazungumzo na kutamka sauti /d/ na /nd/ ipasavyo.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapochangia katika shughuli za kutafuta maneno yenye sauti lengwa katika matini akiwa na wenzake.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kusikiliza vitanzandimi vyenye sauti lengwa.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotafuta maneno yenye sauti lengwa na kuyatamka ipasavyo.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapotamka ipasavyo sauti lengwa na anapochangia katika kazi ya kikundi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki mazungumzo na mzazi au mlezi kwa kuzingatia matamshi bora ya sauti lengwa.
Maadili
  • Upendo – mwanafunzi anapopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi na kutunza vifaa vya kidijitali anavyotumia.
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anapotamka na kutofautisha sauti lengwa na wenzake katika kikundi.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia dhana ya kutofautisha na kutamka sauti.
  • Computer Science – somo hili pia linashughulikia ujuzi wa kidijitali.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua sauti /d/na /nd/ katika silabi na maneno. Anatambua kwa urahisi sauti /d /na /nd/ katika silabi na maneno. Anatambua sauti /d/ na /nd/ katika silabi na maneno. Anatambua sauti /d/ na /nd/ katika baadhi ya silabi na maneno. Anatambua sauti /d/ na /nd/ katika baadhi ya silabi na maneno kwa kusaidiwa.
Kutamka sauti /d/na /nd/ ipasavyo katika silabi na maneno. Anatamka sauti /d/ na /nd/ ipasavyo katika silabi na maneno kwa ufasaha. Anatamka sauti /d/ na /nd/ ipasavyo katika silabi na maneno. Anatamka sauti /d/na /nd/ ipasavyo katika baadhi ya silabi na maneno. Anatamka sauti /d/ na /nd/ ipasavyo katika baadhi ya silabi na maneno kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
9.2 Kusoma 9.2.1 Ufahamu wa Kifungu cha Shawishi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kudondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu
  2. kueleza maana ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu
  3. kueleza habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi
  4. kuchangamkia usomaji wa ufahamu ili kukuza uelewa wa habari.
Mwanafunzi aelekezwe;
  • kudondoa habari mahususi (k.v. nani, nini, wapi, lini, n.k.) katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi
  • kueleza maana ya msamiati kuhusu suala lengwa (k.v. maneno na nahau) katika kifungu cha ufahamu cha kushawishi na kuueleza kwa kutumia kamusi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuandika habari za kifungu cha ufahamu cha ushawishi kwa ufupi akiwa peke yake au kwa kushirikiana na wenzake
  • kuwawasilishia wenzake kazi yake ili wamtolee maoni
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma kifungu cha ufahamu na kujibu maswali.
Kifungu cha ushawishi kina sifa gani?

Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa

  • Mawasiliano – mwanafunzi anapowasilisha kazi yake ya ufahamu kwa wenzake.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki kazi za kikundi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kukamilisha kikamilifu kazi yake ya ufahamu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za ujifunzaji.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko anuwai – yanayojitokeza katika kifungu cha ufahamu.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusoma kwa ufahamu.
  • Computer Science – somo hili pia linashughulikia suala la matumizi ya vifaa vya kidijitali.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kudondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu kwa wepesi. Anadondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa baadhi ya habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa baadhi ya habari mahususi katika kifungu cha ufahamu kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza maana ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu. Anaeleza maana ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu kwa urahisi. Anaeleza maana ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu. Anaeleza maana ya baadhi ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu. Anaeleza maana ya baadhi ya msamiati na vifungu vya maneno katika kifungu cha ufahamu kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaeleza habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi na kwa urahisi. Anaeleza habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaeleza sehemu ya habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaeleza sehemu ya habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi kwa kusaidiwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
9.3 Kuandika 9.3.1 Insha za Kubuni
Masimulizi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua vipengele vinavyozingatiwa kujenga wazo katika insha ya masimulizi
  2. kueleza vipengele vinavyojenga wazo kuhusu insha ya masimulizi
  3. kuandika insha ya masimulizi akikuza wazo katika aya ipasavyo
  4. kufurahia utunzi wa insha za masimulizi zenye mpangilio mzuri wa wazo.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua vipengele vinavyozingatiwa kujenga wazo (k.v. mada, utangulizi, kati, hitimisho, n.k.) katika insha ya masimulizi kwenye matini za kimaandishi na za kidijitali akiwa peke yake au katika kikundi
  • kushirikiana na wenzake kueleza vipengele vinavyojenga mawazo
  • kuandika insha ya masimulizi akizingatia sehemu ya mwanzo, kati na hitimisho
  • kuwasomea wenzake katika kikundi insha aliyoandika au awasambazie kwenye vifaa vya kidijitali ili waitolee maoni
  • kushirikiana na wenzake kusahihisha insha ya maelezo aliyoandika kuhusu suala lengwa kwa kuzingatia vipengele vya mwanzo, kati na hitimisho.
Ni sehemu gani kuu katika mpangilio wa matukio ya insha ya masimulizi?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoandika na kuwasomea wenzake insha aliyoiandika.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika kusahihisha insha.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusambazia insha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika insha ya masimulizi yenye kuzingatia vipengele vifaavyo vya kujenga wazo.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapowasomea wenzake insha aliyoandika ili waikosoe pamoja.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kuandika na kuwasomea wenzake insha.
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi, anaposahihisha insha na wenzake na kujifunza ukakamavu, stahamala na kujiamini.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha.



⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua vipengele vinavyozingatiwa kujenga wazo katika insha ya masimulizi. Anatambua kwa wepesi vipengele vinavyozingatiwa kujenga wazo katika insha ya masimulizi. Anatambua vipengele vinavyozingatiwa kujenga wazo katika insha ya masimulizi. Anatambua baadhi ya vipengele vinavyozingatiwa kujenga wazo katika insha ya masimulizi. Anatambua baadhi ya vipengele vinavyozingatiwa kujenga wazo katika insha ya masimulizi kwa kuelekezwa.
Kuweza kueleza vipengele vinavyojenga wazo kuhusu insha ya masimulizi. Anaeleza vipengele vinavyojenga wazo kuhusu insha ya masimulizi kwa urahisi. Anaeleza vipengele vinavyojenga wazo kuhusu insha ya masimulizi. Anaeleza baadhi ya vipengele vinavyojenga wazo kuhusu insha ya masimulizi. Anaeleza baadhi ya vipengele vinavyojenga wazo kuhusu insha ya masimulizi kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandika insha ya masimulizi akikuza wazo katika aya ipasavyo. Anaandika kwa wepesi insha ya masimulizi akikuza wazo katika aya ipasavyo. Anaandika insha ya masimulizi akikuza wazo katika aya ipasavyo. Anaandika insha ya masimulizi akikuza kwa kiasi wazo katika aya ipasavyo. Anaandika insha ya masimulizi akikuza kwa kiasi wazo katika aya kwa kuelekezwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
9.4 Sarufi 9.4.1 Ngeli na Upatanisho wa Kisarufi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA katika matini
  2. kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya KI-VI na LI-YA katika sentensi
  3. kutumia nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi
  4. kuchangamkia kutumia nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA ipasavyo ili kuimarisha umilisi wa lugha.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kuchopoa nomino katika ngeli ya KI-VI (k.v. kiwambo - viwambo, kipakatalishi - vipakatalishi, kitabu - vitabu, chama - vyama, kidole - vidole, n.k.) na LI-YA (k.v. gari - magari, jiwe - mawe, n.k.) kwenye chati, kadi maneno, kapu maneno au tarakilishi akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutaja vifaa vya shuleni vyenye majina ya ngeli ya KI-VI (k.v. kifutio - vifutio, kiti - viti n.k.) na LI-YA (k.v. tunda - matunda, jicho - macho, shamba - mashamba, jiko - meko, bega - mabega, n.k.) akiwa na wenzake katika kikundi
  • kutenga nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA katika orodha ya nomino, sentensi au vifungu kwenye vitabu, vifaa vya kidijitali, chati za maneno kwa kuzikolezea wino au kuzipigia mstari akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya KI-VI na LI-YA katika sentensi na mafungu akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga sentensi au vifungu vyenye upatanisho ufaao wa kisarufi kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kumtajia mzazi au mlezi majina ambayo yamo katika ngeli ya KI – VI (k.v. chandarua- vyandarua, kijiko-vijiko, chakula - vyakula,) na LI-YA (k.v. jiko - meko, shamba - mashamba, embe – maembe n.k.) katika mazingira ya nyumbani.
  1.  Ni vitu gani katika mazingira ya shuleni vilivyo katika ngeli ya KI-VI?
  2. Ni vitu gani katika mazingira ya shuleni vilivyo katika ngeli ya LI-YA?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotaja mifano ya vifaa vya shuleni vilivyo na majina ya ngeli ya KI-VI na LI-YA na kusikiliza mifano ya wenzake.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika kazi za kikundi na kuwaruhusu wenzake pia kuchangia.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali ipasavyo kutambua nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuhusu suala lengwa akitumia nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapotambua nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA na kuzitungia sentensi na vifungu vilivyo na upatanisho ufaao wa kisarufi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapomtajia mzazi au mlezi wake nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA katika mazingira ya nyumbani.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Kujiamini – mwanafunzi anapochangia na kushirikiana na wenzake katika kikundi.
  • Kujithamini – mwanafunzi anapoandika kifungu kuhusu suala lengwa kwa kutumia nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia upatanisho wa kisarufi.
  • Computer Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya matumizi ya vifaa vya kidijitali.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA katika matini. Anatambua kwa urahisi nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA katika matini. Anatambua nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA katika matini. Anatambua baadhi ya nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA katika matini. Anatambua baadhi ya nomino za ngeli ya KI-VI na LI-YA katika matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya KI-VI na LI-YA katika sentensi. Anatambua kwa wepesi viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya KI-VI na LI-YA katika sentensi. Anatambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya KI-VI na LI-YA katika sentensi. Anatambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya KI-VI na LI-YA katika baadhi ya sentensi. Anatambua viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli ya KI-VI na LI-YA katika baadhi ya sentensi kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi. Anatumia nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi kwa wepesi. Anatumia nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi. Anatumia baadhi ya nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi. Anatumia baadhi ya nomino katika ngeli ya KI-VI na LI-YA kwa kuzingatia upatanisho ufaao wa kisarufi kwa kusaidiwa.







MADA 10.0 KUJITHAMINI
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
10.1 Kusikiliza na Kuzungumza 10.1.1 Nyimbo za Kazi na za Dini
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya nyimbo za kazi na za dini ili kuzibainisha
  2. kutambua mazingira ambapo nyimbo za kazi na za dini huimbwa
  3. kueleza ujumbe katika nyimbo za kazi na za dini
  4. kuwasilisha nyimbo za kazi na za dini kwa kuzingatia hisia na ishara za mwili
  5. kuchangamkia nyimbo za kazi na za dini kama vipera vya fasihi simulizi.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kusikiliza kielelezo cha wimbo wa kazi na wa dini kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au kifaa cha kidijitali (k.v. redio, rununu, kipakatalishi na runinga) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kueleza maana ya nyimbo za kazi na za dini ili kuzibainisha akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutambua mazingira ambapo nyimbo za kazi na za dini huimbwa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kueleza ujumbe katika nyimbo za kazi na za dini akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuwasilisha nyimbo za kazi na za dini kuzingatia hisia na ishara akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kujirekodi akiimba nyimbo za kazi na za dini kwa kutumia vifaa vya kidijitali na kusikiliza akiwa na wenzake
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kujadili ujumbe katika nyimbo za kazi na za dini na kuziimba kuzingatia hisia na ishara za mwili.
  1. Je, unajua nyimbo zipi katika jamii yako
  2. Je, nyimbo za kazi na za dini zinatofautianaje?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anaposhiriki kutambua vipengele vya kimsingi vya nyimbo za kazi na dini kwenye kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kusikiliza nyimbo mbalimbali za kazi na za dini.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapowasilisha nyimbo za kazi na za dini akizingatia hisia na ishara za mwili zifaazo.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapowasilisha nyimbo kwa wepesi na ukakamavu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi kutunga na kuimba nyimbo kwa kuzingatia hisia na ishara za mwili.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika shughuli za kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za uimbaji.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapochukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi na pia kutunza vifaa vya kidijitali anavyotumia.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Kujithamini – mwanafunzi anapotunga na kuwasilisha nyimbo za kazi na za dini.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia dhana ya tungo za fasihi simulizi.
  • Performing Arts – somo hili pia linashughulikia nyimbo.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya nyimbo za kazi na za dini. Anaeleza maana ya nyimbo za kazi na za dini ipasavyo kwa urahisi. Anaeleza maana ya nyimbo za kazi na za dini. Anaeleza kwa kiasi maana ya nyimbo za kazi na za dini. Anaeleza kwa kiasi maana ya nyimbo za kazi na za dini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua mazingira ambapo nyimbo za kazi na za dini huimbwa. Anatambua mazingira ambapo nyimbo za kazi na za dini huimbwa kwa urahisi. Anatambua mazingira ambapo nyimbo za kazi na za dini huimbwa. Anatambua baadhi ya mazingira ambapo nyimbo za kazi na za dini huimbwa. Anatambua baadhi ya mazingira ambapo nyimbo za kazi na za dini huimbwa kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza ujumbe katika nyimbo za kazi na za dini. Anaeleza ujumbe katika nyimbo za kazi na za dini kwa wepesi. Anaeleza ujumbe katika nyimbo za kazi na za dini. Anaeleza baadhi ya ujumbe katika nyimbo za kazi na za dini. Anaeleza baadhi ya ujumbe katika nyimbo za kazi na za dini kwa kuelekezwa.
Kuweza kuwasilisha nyimbo za kazi na za dini kwa kuzingatia hisia na ishara za mwili. Anawasilisha kwa wepesi nyimbo za kazi na za dini kwa kuzingatia hisia na ishara za mwili. Anawasilisha nyimbo za kazi na za dini kwa kuzingatia hisia na ishara za mwili. Anawasilisha kwa kiasi nyimbo za kazi na za dini kwa kuzingatia hisia na ishara za mwili. Anawasilisha kwa kiasi nyimbo za kazi na za dini kwa kuzingatia hisia na ishara za mwili kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
10.2 Kusoma 10.2.1 Kusoma kwa Kina
Wahusika
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua wahusika katika novela
  2. kujadili sifa za wahusika katika novela
  3. kueleza uhusiano kati ya wahusika katika novela
  4. kuandika muhtasari wa sifa za wahusika katika novela
  5. kujadili mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika katika novela
  6. kujenga mazoea ya usomaji wa kazi za kifasihi katika maisha ya kila siku.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua wahusika katika novela iliyoteuliwa na mwalimu, akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kujadili sifa za wahusika katika novela iliyoteuliwa na mwalimu (k.v. usiri, uovu, ukali, udadisi, n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuigiza wahusika katika novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa na wenzake kwenye kikundi ili kukuza uelewa wa sifa zao
  • kueleza uhusiano kati ya wahusika katika novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutazama video kuhusu wahusika katika novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa na wenzake
  • kuandaa muhtasari kuhusu sifa za wahusika katika video aliyotazama
  • kujadili mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika akiwa peke yake au na wenzake kumsimulia mzazi au mlezi wake hadithi ya novela na kujadiliana kuhusu wahusika wawili.
Ni mambo yapi yanayokuweze- sha kuwaelewa wahusika katika novela?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano na ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapoigiza na wenzake wahusika katika novela.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotazama video kuhusu wahusika katika novela kwenye vifaa vya kidijitali.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoigiza wahusika katika novela.
  • Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anapochambua sifa za wahusika katika novela.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapomhadithia mzazi au mlezi hadithi ya novela na kujadiliana kuhusu wahusika.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika majadiliano ya kuwachambua wahusika katika kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko anuwai – mwanafunzi anaposoma novela.

Uhusiano na Masomo Mengine

  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusoma kwa kina.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua wahusika katika novela aliyosoma. Anatambua wahusika katika novela aliyosoma kwa urahisi. Anatambua wahusika katika novela aliyosoma. Anatambua baadhi ya wahusika katika novela aliyosoma. Anatambua baadhi ya wahusika katika novela aliyosoma kwa kuelekezwa.
Kuweza kujadili sifa za wahusika katika novela. Anaweza kujadili sifa za wahusika katika novela kwa urahisi. Anaweza kujadili sifa za wahusika katika novela. Anaweza kujadili baadhi ya sifa za wahusika katika novela. Anaweza kujadili baadhi ya sifa za wahusika katika novela kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza uhusiano kati ya wahusika katika novela. Anaweza kueleza uhusiano kati ya wahusika katika novela kwa urahisi. Anaweza kueleza uhusiano kati ya wahusika katika novela. Anaweza kueleza kwa kiasi uhusiano kati ya wahusika katika novela. Anaweza kueleza kwa kiasi uhusiano kati ya wahusika katika novela kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandika muhtasari wa sifa za wahusika katika novela. Anaandika muhtasari wa sifa za wahusika katika novela kwa wepesi. Anaandika muhtasari wa sifa za wahusika katika novela. Anaandika kwa kiasi muhtasari wa sifa za wahusika katika novela. Anaandika kwa kiasi muhtasari wa sifa za wahusika katika novela kwa kusaidiwa.
Kujadili mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika katika novela. Anajadili mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika katika novela kwa urahisi. Anajadili mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika katika novela. Anajadili baadhi ya mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika katika novela. Anajadili baadhi ya mafunzo yanayotokana na matendo ya wahusika katika novela kwa kuelekezwa.





Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
10.3 Kuandika 10.3.1 Barua ya Kuomba Msamaha
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
a) kueleza umuhimu wa barua rasmi ya kuomba msamaha
b) kutambua ujumbe katika barua rasmi ya kuomba msamaha
c) kutambua vipengele vya kimuundo vya barua rasmi ya kuomba msamaha
d) kuandika barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kuzingatia ujumbe, muundo na lugha ifaayo
e) kufurahia kujieleza kwa njia ifaayo kupitia kwa barua.
Mwanafunzi aelekezwe:
• kueleza umuhimu wa kuandika barua rasmi ya kuomba msamaha kuhusu matukio mbalimbali (k.v. kukosa kuhudhuria darasa, kuchelewa kufika shuleni, n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
• kutambua ujumbe unaoafiki barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kujadiliana na mwenzake
• kujadili katika kikundi vipengele vya kimuundo vya barua rasmi ya kuomba msamaha (k.v. anwani, suala linaloshughulikiwa, sahihi n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
• kujadili na wenzake kuhusu lugha inayofaa katika uandishi wa barua rasmi ya kuomba msamaha
• kuandika barua rasmi ya kuomba msamaha kuhusu matukio mbalimbali na kuwasomea wenzake darasani ili waitolee maoni
• kuandika barua ya kuomba msamaha katika kifaa cha kidijitali na kuwasambazia wenzake kupitia mtandao ili waitolee maoni.
1. Je, ni mambo gani
yanayoweza kukufanya uandike barua rasmi ya kuomba msamaha?
2. Je, utazingatia nini unapoandika barua ya kuomba msamaha?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotoa mchango katika kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika kujadili vipengele vya barua rasmi ya kuomba msamaha.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kuandika barua na kuisambazia wengine
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika barua rasmi ya kuomba msamaha.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapoandika barua rasmi ya kuomba msamaha.
  • Uwazaji kina – mwanafunzi anapowaza kuhusu matukio yanayomfanya mtu kuomba msamaha.
  • Uraia – mwanafunzi anapoomba msamaha anajenga mshikamano katika jamii au taifa.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa nafasi wenzake kuchangia katika shughuli za ujifunzaji.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi. • Amani – mwanafunzi anapoandika barua kuomba msamaha. 
Masuala Mtambuko
  • Kujali maslahi – mwanafunzi anapoandika barua ya kuomba msamaha.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha za kiuamilifu.
  • Masomo ya Dini – masomo haya pia yana masuala yanayohimiza msamaha.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza umuhimu wa barua rasmi ya kuomba msamaha. Anaeleza kwa urahisi umuhimu wa barua rasmi ya kuomba msamaha. Anaeleza umuhimu wa barua rasmi ya kuomba msamaha. Anaeleza kwa kiasi umuhimu wa barua rasmi ya kuomba msamaha. Anaeleza kwa kiasi umuhimu wa barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua ujumbe katika barua rasmi ya kuomba msamaha. Anatambua ujumbe katika barua rasmi ya kuomba msamaha kwa urahisi. Anatambua ujumbe katika barua rasmi ya kuomba msamaha . Anatambua ujumbe katika barua rasmi ya kuomba msamaha. Anatambua baadhi ya ujumbe katika barua rasmi ya kuomba msamaha. Anatambua baadhi ya ujumbe katika barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kuelekezwa.
Kuweza kutambua vipengele vya kimuundo vya barua rasmi ya kuomba msamaha. Anatambua kwa wepesi vipengele vya kimuundo vya barua rasmi ya kuomba msamaha. Anatambua vipengele vya kimuundo vya barua rasmi ya kuomba msamaha. Anatambua baadhi ya vipengele vya kimuundo vya barua rasmi ya kuomba msamaha. Anatambua baadhi ya vipengele vya kimuundo vya barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kusaidiwa.
Kuweza kuandika barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kuzingatia ujumbe, muundo na lugha ifaayo. Anaandika kwa urahisi barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kuzingatia ujumbe, muundo na lugha ifaayo. Anaandika barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kuzingatia ujumbe, muundo na lugha ifaayo. Anaandika barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kuzingatia baadhi ya vipengele vya ujumbe, muundo na lugha ifaayo. Anaandika barua rasmi ya kuomba msamaha kwa kuzingatia baadhi ya vipengele vya ujumbe, muundo na lugha ifaayo kwa kuelekezwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
10.4 Sarufi 10.4.1 Vinyume vya Maneno
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza dhana ya kinyume cha maneno
  2. kutambua vinyume vya nomino na vivumishi katika fungu la maneno
  3. kutumia vinyume vya nomino na vivumishi katika fungu la maneno
  4. kuchangamkia kutumia vinyume vya nomino na vivumishi katika mawasiliano.

Mwanafunzi aelekezwe:

  •  kujadili maana ya kinyume cha maneno akiwa na mwenzake au katika kikundi
  • kutambua vinyume vya nomino (k.v. mwalimu - mwanafunzi, mzee - kijana n.k.) na vivumishi (k.v. jasiri - mwoga) kwa kutumia kadi maneno, mti maneno, kapu maneno akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua vinyume vya nomino na vivumishi katika fungu la maneno (k.v orodha ya maneno, sentensi na vifungu vya maneno) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuchagua sentensi zinazoashiria matumizi ya vinyume vya nomino na vivumishi kutoka kwa sentensi mbalimbali kwenye vitabu,tarakilishi au chati akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga sentensi sahihi akitumia vinyume vya nomino na vivumishi akiwa peke yake au katika kikundi
  • kusakura mtandaoni au katika vitabu vya ziada akiwa na mzazi au mlezi ili kupata vinyume zaidi vya nomino na vivumishi.
Je, ni vinyume gani vya nomino na vivumishi unavyovijua?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotoa mchango katika kazi ya kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kutambua vinyume vya nomino na vivumishi.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuonyesha vinyume vya nomino na vivumishi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposhiriki katika kutambua vinyume vya nomino na vivumishi na kuvitungia sentensi sahihi.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kuchopoa vinyume vya nomino na vivumishi na kutunga sentensi sahihi
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia vinyume vya maneno.
  • Social Studies – somo hili pia huangazia dhana ya kujiamini.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza dhana ya kinyume cha maneno. Anaeleza dhana ya kinyume cha maneno kwa urahisi. Anaeleza dhana ya kinyume cha maneno. Anaeleza kwa kiasi dhana ya kinyume cha maneno. Anaeleza kwa kiasi dhana ya kinyume cha maneno kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua vinyume vya nomino na vivumishi katika fungu la maneno. Anatambua vinyume vya nomino na vivumishi katika fungu la maneno kwa wepesi. Anatambua vinyume vya nomino na vivumishi katika fungu la maneno. Anatambua baadhi ya vinyume vya nomino na vivumishi katika fungu la maneno. Anatambua baadhi ya vinyume vya nomino na vivumishi katika fungu la maneno kwa kuelekezwa.
Kuweza kutumia vinyume vya nomino na vivumishi katika sentensi na vifungu. Anatumia vinyume vya nomino na vivumishi katika sentensi na vifungu kwa wepesi. Anatumia vinyume vya nomino na vivumishi katika sentensi na vifungu. Anatumia baadhi ya vinyume vya nomino na vivumishi katika sentensi na vifungu. Anatumia baadhi ya vinyume vya nomino na vivumishi katika sentensi na vifungu kwa kusaidiwa.






MADA 11.0 MAJUKUMU YA WATOTO
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
11.1 Kusikiliza na Kuzungumza 11.1.1 Kuzungumza kwa Kuambatanisha na Vitendo
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo
  2. kutambua umuhimu wa kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo
  3. kujadili vitendo vya kuambatanisha na mazungumzo
  4. kutoa mazungumzo kwa kuyaambatanisha na vitendo vifaavyo
  5. kujenga mazoea ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo ili kufanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua umuhimu wa kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo (k.v. kumwelekeza mtu njia, kueleza jinsi ya kutayarisha chakula n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuigiza jinsi ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo akiwa peke yake,wawiliwawili au katika kikundi
  • kushiriki na wenzake katika kikundi kusikiliza au kutazama mazungumzo yanayoambatanisha vitendo kutoka kwa mwalimu, mgeni mwalikwa au kwenye vifaa vya kidijitali
  • kujadili vitendo vya kuambatanisha na mazungumzo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusikiliza au kutazama mazungumzo yanayoambatana na vitendo kuhusu suala lengwa na kubainisha vipengele vya kuzungumza kwa aina hii vilivyozingatiwa akiwa katika kikundi
  • kuwasilisha mazungumzo yanayoambatana na vitendo kuhusu suala lengwa kwa kuzingatia vitendo vifaavyo akiwa peke yake au katika kikundi
  • kushiriki na mzazi au mlezi wake katika kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo kuhusu suala lengwa.
  1. Ni vitendo gani tunatumia tunapozungumza?
  2. Kuna umuhimu gani wa kutumia vitendo tunapozungumza?

Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa

  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotumia lugha nyepesi kuwaelimisha wenzake kuhusu majukumu ya watoto huku akiambatanisha na vitendo.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika kikundi.
  • Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anaposhiriki katika kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo na kufafanua namna ya kutekeleza jambo fulani.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapowasilisha mazungumzo kuhusu suala lengwa kwa kutumia mbinu zifaazo za kufanikisha mazungumzo.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapojadili na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kuzungumza na kuambatanisha na vitendo katika kikundi.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake zamu ya kushiriki katika mazungumzo bila kuwakata kauli.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapovitunza vifaa vya kidijitali anavyovitumia kuwaelezea wenzake kuhusu suala fulani.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki na wengine na kuchangia katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Uraia – mwanafunzi anapomshirikisha mzazi au mlezi wake katika kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo kuhusu majukumu ya watoto.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia stadi ya mazungumzo.
  • Social Studies na Religious Education – masomo haya pia yanashughulikia majukumu ya watoto.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo.  Anaeleza maana ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo kwa usahihi.  Anaeleza maana ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo.  Anaeleza kwa kiasi maana ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo.  Anaeleza kwa kiasi maana ya kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo kwa kusaidiwa.
 Kuweza kutambua umuhimu wa kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo.  Anatambua kwa wepesi umuhimu wa kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo.  Anatambua umuhimu wa kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo.  Anatambua baadhi ya umuhimu wa kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo.  Anatambua baadhi ya umuhimu wa kuzungumza kwa kuambatanisha na vitendo kwa kusaidiwa.
 Kuweza kujadili vitendo vya kuambatanisha na mazungumzo.  Anajadili kwa urahisi vitendo vya kuambatanisha na mazungumzo.  Anajadili vitendo vya kuambatanisha na mazungumzo. Anajadili baadhi ya vitendo vya kuambatanisha na mazungumzo.   Anajadili baadhi ya vitendo vya kuambatanisha na mazungumzo kwa kuelekezwa.
 Kuweza kutoa mazungumzo kwa kuyaambatanisha na vitendo vifaavyo.  Anatoa mazungumzo kwa kuyaambatanisha na vitendo vifaavyo kwa urahisi.  Anatoa mazungumzo kwa kuyaambatanisha na vitendo vifaavyo.  Anatoa mazungumzo kwa kuyaambatanisha na baadhi ya vitendo vifaavyo.  Anatoa mazungumzo kwa kuyaambatanisha na baadhi ya vitendo vifaavyo kwa kusaidiwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
11.2 Kusoma 11.2.1
Kusoma kwa Mapana
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza ujumbe wa matini ya kujichagulia
  2. kutambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia
  3. kutumia ipasavyo msamiati aliosoma katika matini ya kujichagulia
  4. kutoa muhtasari wa matini ya kujichagulia aliyosoma
  5. kujenga mazoea ya kusoma matini mbalimbali katika maisha ya kila siku.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza ujumbe wa matini ya kujichagulia aliyosoma akiwa na wenzake
  • kutambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia (andishi au ya kidijitali; ya kisayansi, kisiasa. kihistoria, kifasihi, michezo, n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutumia kamusi kutafuta maana za maneno asiyoyajua akiwa peke yake au katika kikundi
  • kujenga rekodi ya msamiati aliojifunza katika kitabu
  • kumtungia mwenzake sentensi akitumia msamiati katika matini aliyoisoma
  • kutoa muhtasari wa matini ya kujichagulia aliyosoma na kuwasilisha kwa wenzake ili waitolee maoni
  • kusakura mtandaoni na kujichagulia matini ya ziada kisha aisome.
  1. Unapenda kusoma matini za aina gani?
  2. Unazingatia nini unapochagua matini ya kujisomea?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoandika muhtasari na kuuwasilisha kwa wenzake.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapotangamana na wenzake na kuwawasilishia muhtasari wa matini ya kujichagulia aliyosoma
  • Kujiamini – mwanafunzi anapomtungia mwenzake sentensi kutokana na msamiati wa matini ya kujichagulia akizingatia ufasaha wa lugha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapomtungia mwenzake sentensi akitumia msamiati katika matini aliyoisoma.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapojichagulia matini ya kusoma na kutafuta maana za maneno asiyoyajua kwenye kamusi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anaposakura mtandaoni na kujichagulia matini ya kusoma.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake wanapowasilisha muhtasari wa matini ya kujichagulia waliyosoma.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kutafuta na kusoma matini aliyojichagulia. Pia anapozingatia nidhamu anaposakura mtandaoni
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kutunga sentensi akitumia msamiati aliojifunza.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya watoto – mwanafunzi anaposoma kifungu kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusoma kwa mapana.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza ujumbe wa matini ya kujichagulia. Anaeleza ujumbe wa matini ya kujichagulia kwa urahisi. Anaeleza ujumbe wa matini ya kujichagulia. Anaeleza baadhi ya ujumbe wa matini ya kujichagulia. Anaeleza baadhi ya ujumbe wa matini ya kujichagulia kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia. Anatambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia kwa urahisi. Anatambua msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia. Anatambua baadhi ya msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia. Anatambua baadhi ya msamiati uliotumiwa katika matini ya kujichagulia kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia ipasavyo msamiati aliosoma katika matini ya kujichagulia. Anatumia ipasavyo msamiati aliosoma katika matini ya kujichagulia. Anatumia ipasavyo msamiati aliosoma katika matini ya kujichagulia. Anatumia ipasavyo baadhi ya msamiati aliosoma katika matini ya kujichagulia. Anatumia ipasavyo baadhi ya msamiati aliosoma katika matini ya kujichagulia kwa kusaidiwa.
Kuweza kutoa muhtasari wa matini ya kujichagulia Anatoa muhtasari wa aliyosoma. matini ya kujichagulia aliyosoma kwa urahisi. Anatoa muhtasari wa matini ya kujichagulia aliyosoma. Anatoa muhtasari wa sehemu ya matini ya kujichagulia aliyosoma. Anatoa muhtasari wa sehemu ya matini ya kujichagulia aliyosoma kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
11.3 Kuandika 11.3.1 Insha za Maelezo
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua vipengele vya mpangilio wa insha ya maelezo
  2. kueleza mpangilio wa insha ya maelez
  3. kuandika insha ya maelezo inayozingatia mpangilio ufaao wa maelezo
  4. kufurahia kuandika insha za maelezo katika maisha ya kila siku akizingatia mpangilio ufaao wa maelezo.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua mpangilio wa insha ya maelezo katika matini za kimaandishi au za kidijitali (k.v. mpangilio unaozingatia mahali, hasa kama maelezo yanahusu mahali na mpangilio unaozingatia mfuatano wa matukio kiwakati n.k) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushirikiana na wenzake kueleza jinsi maelezo yalivyopangwa katika insha ya maelezo (k.v. mfuatano ufaao wa matukio kuanzia la kwanza hadi la mwisho na matumizi ya viungio kuendeleza wazo)
  • kuandika vidokezo vya insha vinavyozingatia jinsi maelezo yalivyopangwa katika insha ya maelezo kuhusu suala lengwa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikund
  • kuandika insha ya maelezo akizingatia mpangilio ufaao wa maelezo
  • kuwasomea wenzake katika kikundi insha aliyoandika au awasambazie kwenye vifaa vya kidijitali ili waitolee maoni
  • kushirikiana na wenzake kusahihisha insha ya maelezo aliyoandika akizingatia mpangilio ufaao wa maelezo.
Je, unawezaje kupanga matukio katika insha ya maelezo?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoandika insha na kuwasomea wenzake darasani.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika kusahihisha insha.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kuwasambazia wenzake insha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika insha yenye mpangilio mzuri wa maelezo.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapowasomea wenzake kwa ufasaha insha aliyoandika ili waikosoe pamoja.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapoandika insha na kuwasomea wenzake.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi na pia anaposahihisha insha na wenzake.
  • Haki za watoto – mwanafunzi anapoandika insha ya maelezo kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua vipengele vya mpangilio wa insha za maelezo. Anatambua vipengele vya mpangilio wa insha za maelezo kwa urahisi. Anatambua vipengele vya mpangilio wa insha za maelezo. Anatambua baadhi ya vipengele vya mpangilio wa insha za maelezo. Anatambua baadhi ya vipengele vya mpangilio wa insha za maelezo kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza mpangilio wa insha ya maelezo. Anaeleza mpangilio wa insha ya maelezo kwa urahisi. Anaeleza mpangilio wa insha ya maelezo. Anaeleza baadhi ya sehemu za mpangilio wa insha ya maelezo. Anaeleza baadhi ya sehemu za mpangilio wa insha ya maelezo kwa kusaidiwa.
Kuweza kuandika insha ya maelezo inayozingatia mpangilio ufaao wa maelezo. Anaandika insha ya maelezo inayozingatia mpangilio ufaao wa maelezo kwa weledi. Anaandika insha ya maelezo inayozingatia mpangilio ufaao wa maelezo. Anaandika insha ya maelezo inayozingatia kwa kiasi mpangilio ufaao wa maelezo. Anaandika insha ya maelezo inayozingatia kwa kiasi mpangilio ufaao wa maelezo kwa kuelekezwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
11.4 Sarufi 11.4.1 Mnyambuliko wa Vitenzi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1.  kutambua kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa katika vitenzi
  2. kutumia vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa ipasavy
  3. kuchangamkia kutumia ipasavyo vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa ili kujenga ufasaha wa lugha.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa (k.v. som-a, som-e-a, som-w-a) mtawalia akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuteua vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa (k.v. soma, somea, somwa) mtawalia, kwenye chati, kadi maneno, kapu maneno au tarakilishi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kugeuza vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa akiwa na wenzake katika kikundi
  • kutenga vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa katika sentensi na vifungu kwenye vitabu, tarakilishi, chati kwa kuvikolezea wino au kuvipigia mstari akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutunga sentensi au vifungu kuhusu
Ni kauli gani za vitenzi unazozijua?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotoa mchango wake katika kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kutambua vitenzi katika kauli mbalimbali.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuhusu suala lengwa akitumia vitenzi katika kauli mbalimbali.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapotambua viambishi vya kauli mbalimbali.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kuteua vitenzi katika kauli mbalimbali.
  • Majukukumu ya watoto – mwanafunzi anapoandika kifungu kuhusu suala lengwa kwa kutumia vitenzi katika kauli mbalimbali.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia mnyambuliko wa vitenzi.
  • Integrated Science na Home Science – masomo haya pia yanashughulikia masuala ya watoto.



Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa katika vitenzi. Anatambua kwa wepesi kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa katika vitenzi. Anatambua kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa katika vitenzi. Anatambua baadhi ya kauli za kutenda, kutendea na kutendwa katika baadhi ya vitenzi. Anatambua baadhi ya kauli za kutenda, kutendea na kutendwa katika baadhi ya vitenzi kwa kuelekezwa.
Kuweza kutumia vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa ipasavyo. Anatumia kwa urahisi vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa ipasavyo. Anatumia vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa ipasavyo. Anatumia baadhi ya vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa ipasavyo. Anatumia baadhi ya vitenzi katika kauli ya kutenda, kutendea na kutendwa ipasavyo kwa kusaidiwa.

 

MADA 12.0 MAGONJWA YANAYOAMBUKIZWA
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
12.1 Kusikiliza na Kuzungumza 12.1.1 Kusikiliza kwa Makini
(Vipindi 2)

Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:

  1. kutambua hoja muhimu katika habari aliyosikiliza
  2.  kuwasilisha hoja muhimu katika habari
  3.  kujenga mazoea ya kutambua hoja katika habari anayosikiliza ili kuimarisha usikilizaji wa makini.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua hoja muhimu katika habari aliyosikiliza kuhusu suala lengwa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusikiliza habari kuhusu suala lengwa na kutaja hoja muhimu kwa maneno machache
  • kutafiti mtandaoni kuhusu suala lengwa na kuwawasilishia wenzake hoja muhimu kuhusu suala hilo kwa maneno machache
  • kumsomea mzazi au mlezi habari kuhusu suala lengwa na kushirikiana kutambua hoja.
Kwa nini ni muhimu kutambua hoja katika habari uliyosikiliza?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapowatolea wenzake hoja muhimu katika habari aliyosikiliza inayochangia uelewa wa suala hilo
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika kazi ya kikundi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kusikiliza na kuwatajia wenzake hoja muhimu kuhusu suala lengwa kwa ufupi.
  • Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anaposikiliza habari, kuichanganua na kutambua hoja muhimu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapotafiti kwenye mtandao kuhusu suala lengwa na kuwasilisha hoja kuu kwa ufupi. Pia anaposhiriki mazungumzo na mzazi au mlezi wake kuhusu suala lengwa na kuiwasilisha habari hiyo upya kwa hoja fupi.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoiwasilisha upya habari aliyosikiliza kupitia hoja kuu.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wengine fursa ya kutambua na kusema hoja muhimu bila kuwakatiza.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapotunza vifaa vya kidijitali anavyotumia kujifunzia.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya afya – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika mazungumzo kuhusu suala lengwa na kutambua ujumbe au hoja muhimu; anapata maarifa kuhusu magonjwa ya kuambukiza.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya afya – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika mazungumzo kuhusu suala lengwa na kutambua ujumbe au hoja muhimu; anapata maarifa kuhusu magonjwa ya kuambukiza.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia stadi ya kusikiliza.
  • Integrated Science, Homescience na Health Education – masomo haya pia yanashughulikia magonjwa yanayoambukizwa.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua hoja muhimu katika habari aliyosikiliza. Anatambua kwa wepesi hoja muhimu katika habari aliyosikiliza. Anatambua hoja muhimu katika habari aliyosikiliza. Anatambua baadhi ya hoja muhimu katika habari aliyosikiliza. Anatambua baadhi ya hoja muhimu katika habari aliyosikiliza kwa kuelekezwa.
Kuweza kuwasilisha hoja muhimu katika habari aliyosikiliza. Anawasilisha hoja muhimu katika habari aliyosikiliza kwa urahisi. Anawasilisha hoja muhimu katika habari aliyosikiliza. Anawasilisha baadhi ya hoja muhimu katika habari aliyosikiliza. Anawasilisha, kwa kusaidiwa, baadhi ya hoja muhimu katika habari aliyosikiliza.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
12.2 Kusoma 12.2.1 Kusoma kwa Ufasaha
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kusoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora
  2. kusoma kifungu kwa kasi ifaayo
  3. kusoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo
  4. kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo
  5. kuridhia kusoma makala kwa kuzingatia vipengele vinavyofanikisha mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kujadiliana na wenzake vipengele vya kuzingatia katika kusoma makala kwa ufasaha
  • kutazama vielelezo vya video za watu wanaosoma kwa ufasaha makala (k.v hotuba, habari, n.k.) akiwa peke yake au na wenzak
  • kusoma kifungu kuhusu suala lengwa katika matini andishi au ya kidijitali akizingatia matamshi bora akiwa peke yake au katika kikundi
  • kusoma kifungu cha habari kwa kasi ifaayo kuhusu suala lengwa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusoma kifungu akizingatia sauti ifaayo (k.v kiwango cha sauti na kiimbo) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo panapofaa (k.v ishara za uso na mikono) akiwa peke yake,wawiliwawili au katika kikundi
  • kusoma mbele ya wenzake kazi yake ili wamtolee maoni
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma makala akingatia vipengele vya usomaji bora.
Unazingatia nini ili kusoma makala kwa ufasaha?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapofanikiwa kusoma makala kwa ufasaha na anapojadiliana na wenzake katika kikundi kuhusu vipengele vya kimsingi vya kusoma kwa ufasaha.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kuhusu vipengle vya kusoma kwa ufasaha.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposoma kifungu kwa ufasaha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotumia ishara wakati wa kusoma kifungu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli ya kusoma anakuza hamu ya ujifunzaji.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi wanapojadili vipengele vya usomaji bora.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika mjadala wakati wa shughuli ya ujifunzaji katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuwasomea wenzake kifungu.
  • Umoja – mwanafunzi anapotangamana na wenzake katika kikundi kujadili vipengele vya usomaji bora.
Masuala Mtambuko
  • Masuala ya afya – mwanafunzi anapofupisha ujumbe unaohusu magonjwa yanayoambukizwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia stadi ya kusoma.
  • Homescience, Health Education na Integrated Science – masomo haya pia yanashughulikia magonjwa yanayoambukizwa.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kusoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora. Anasoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora kwa urahisi. Anasoma kifungu kwa kuzingatia matamshi bora. Anasoma sehemu za kifungu kwa kuzingatia matamshi bora. Anasoma sehemu za kifungu kwa kuzingatia matamshi bora kwa kusaidiwa.
Kusoma kifungu kwa kasi ifaayo. Anasoma kifungu kwa kasi ifaayo kwa urahisi. Anasoma kifungu kwa kasi ifaayo. Anasoma sehemu za kifungu kwa kasi ifaayo. Anasoma sehemu za kifungu kwa kasi ifaayo kwa kusaidiwa.
Kusoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo. Anasoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo kwa urahisi. Anasoma kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo. Anasoma sehemu za kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo. Anasoma sehemu za kifungu kwa kutumia sauti ipasavyo kwa kusaidiwa.
Kusoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo. Anasoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo kwa urahisi. Anasoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo. Anasoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo katika baadhi ya sehemu. Anasoma kifungu kwa kuambatanisha ishara zifaazo katika baadhi ya sehemu kwa kusaidiwa.



Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
12.3 Kuandika 12.3.1 Hotuba ya Kupasha Habari
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya hotuba ya kupasha habari
  2. kutambua hotuba ya kupasha habari katika matini
  3. kueleza ujumbe, lugha na muundo wa hotuba ya kupasha habari
  4. kuandika hotuba ya kupasha habari kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao
  5. kuchangamkia nafasi ya hotuba ya kupasha habari katika mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya hotuba ya kupasha habari akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kujadiliana na wenzake kuhusu ujumbe (unaolenga kuelimisha kundi lengwa), lugha (nyepesi inayoeleweka) na muundo ufaao wa hotuba ya kupasha habar
  • kujadili na wenzake miktadha inayochochea hotuba ya kupasha habari
  • kujadili na wenzake vidokezo vinavyoweza kutumiwa katika kuandika hotuba ya kupasha habari
  • kuandika hotuba ya kupasha habari kuhusu suala lengwa akizingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao kisha awasambazie wenzake mtandaoni au kuwasomea darasani ili waitolee maoni
  • kushirikiana na mzazi au mlezi wake kuandika hotuba ya kupasha habari kuhusu suala linaloathiri jamii yao.
Ni mambo yepi ambayo yanaweza kuelezwa kupitia kwa hotuba?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotoa mchango katika kikundi kuhusu hotuba ya kupasha habari.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kujadili ujumbe, lugha na muundo wa hotuba ya kupasha habari.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia tarakilishi kuandika hotuba ya kupasha habari na kuisambaza kwa mtandao.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika hotuba ya kupasha habari.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi kuandika hotuba ya kupasha habari kuhusu suala linaloathiri jamii yao.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
  • Amani – mwanafunzi anapoweza kuwapasha wenzake habari kwa utulivu.
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kujadili ujumbe, lugha na muundo wa hotuba ya kupasha habari hukuza ukakamavu, stahamala na kujiamini.
  • Uraia – mwanafunzi anapoandika hotuba ya kupasha habari kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa kiuamilifu.
  • Homescience, Health Education na Integrated Science – masomo haya pia yanashughulikia magonjwa yanayoambukizwa.


Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kueleza maana ya hotuba ya kupasha habari. Anaeleza maana ya hotuba ya kupasha habari kwa urahisi. Anaeleza maana ya hotuba ya kupasha habari. Anaeleza kwa kiasi maana ya hotuba ya kupasha habari. Anaeleza kwa kiasi maana ya hotuba ya kupasha habari kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua hotuba ya kupasha habari katika matini. Anatambua kwa wepesi hotuba ya kupasha habari katika matini. Anatambua hotuba ya kupasha habari katika matini. Anatambua hotuba ya kupasha habari katika baadhi ya matini. Anatambua hotuba ya kupasha habari katika matini mbalimbali kwa kuelekezwa.
Kuweza kueleza ujumbe, lugha na muundo wa hotuba ya kupasha habari. Anaeleza kwa urahisi ujumbe, lugha na muundo wa hotuba ya kupasha habari. Anaeleza ujumbe, lugha na muundo wa hotuba ya kupasha habari. Anaeleza baadhi ya masuala ya ujumbe, lugha na muundo wa hotuba ya kupasha habari. Anaeleza baadhi ya masuala ya ujumbe, lugha na muundo wa hotuba ya kupasha habari kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandika hotuba ya kupasha habari kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao. Anaandika kwa urahisi hotuba ya kupasha habari kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao. Anaandika hotuba ya kupasha habari kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao. Anaandika hotuba ya kupasha habari kwa kuzingatia baadhi ya vipengele vya ujumbe, lugha na muundo ufaao. Anaandika hotuba ya kupasha habari kwa kuzingatia baadhi ya vipengele vya ujumbe, lugha na muundo ufaao kwa kusaidiwa.

 

Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
12.4 Sarufi 12.4.1 Aina za Sentensi
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1.  kueleza maana ya sentensi sahili na ambatano
  2. kutambua sentensi sahili na ambatano katika matini
  3. kutunga sentensi sahili na ambatano ipasavyo
  4. kuchangamkia matumizi ya sentensi sahili na ambatano katika mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya sentensi sahili na ambatano akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutenga sentensi sahili na ambatano katika orodha ya sentensi kwenye vitabu, chati au tarakilishi kwa kuzipigia mstari au kuzikolezea wino akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutaja sentensi sahili na ambatano zinazojitokeza katika vifungu akiwa na wenzake katika kikundi
  • kutunga sentensi sahili na ambatano ipasavyo kuhusu suala lengwa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuunganisha sentensi sahili mbili au zaidi kuunda sentensi ambatano akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuunda sentensi sahili kutokana na sentensi ambatano akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kumtungia mzazi au mlezi sentensi sahili na ambatano zinazohusu shughuli katika mazingira ya nyumbani.
  1. Ni aina gani ya sentensi unazozijua?
  2. Je, sentensi sahili na ambatano hutofautianaje?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotaja sentensi sahili na ambatano zinazojitokeza katika vifungu akiwa na wenzake.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na kuchangia katika kazi za kikundi na kuwapa wenzake nafasi ya kuchangia.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kutambua sentensi sahili na ambatano.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuhusu suala lengwa akitumia sentensi sahili na ambatano.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kutambua sentensi sahili na ambatano katika kifungu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapomtungia mzazi au mlezi wake sentensi sahili na ambatano zinazohusu shughuli katika mazingira ya nyumbani.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kutunga sentensi sahili na ambatano.
  • Magonjwa yanayoambukizwa – mwanafunzi anapotunga sentensi sahili na ambatano kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia aina za sentensi.
  • Homescience, Health Education na Integrated Science – masomo haya pia yanashughulikia magonjwa yanayoambukizwa.\



⇒Viwango
⇓Vigezo 
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya sentensi sahili na ambatano. Anaeleza kwa urahisi maana ya sentensi sahili na ambatano. Anaeleza maana ya sentensi sahili na ambatano. Anaeleza kwa kiasi maana ya sentensi sahili na ambatano. Anaeleza kwa kiasi maana ya sentensi sahili na ambatano kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua sentensi sahili na ambatano katika matini. Anatambua kwa urahisi sentensi sahili na ambatano katika matini. Anatambua sentensi sahili na ambatano katika matini. Anatambua baadhi ya sentensi sahili na ambatano katika matini. Anatambua baadhi ya sentensi sahili na ambatano katika matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutunga sentensi sahili na ambatano ipasavyo. Anatunga sentensi sahili na ambatano ipasavyo kwa urahisi. Anatunga sentensi sahili na ambatano ipasavyo. Anatunga baadhi ya sentensi sahili na ambatano ipasavyo. Anatunga baadhi ya sentensi sahili na ambatano kwa kuelekezwa.



MADA 13.0 UTATUZI WA MIZOZO
Mada Mada Ndogo Matokeo Maalum Yanayotarajiwa    Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji      Maswali Dadisi     
13 .1 Kusikiliza na Kuzungumza 13.1.1 Wahusika katika Nyimbo
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua wahusika katika wimbo
  2. kuchambua wahusika katika wimbo
  3. kueleza mafunzo kutokana na wahusika katika wimbo
  4. kufurahia kushiriki katika uchanganuzi wa wahusika katika nyimbo.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua wahusika katika wimbo anaosikiliza au kuimba na wenzake katika kikundi (k.v mwimbaji, hadhira na wahusika wengine kwenye wimbo)

● kuchambua akiwa na wenzake wahusika katika wimbo anaosikiliza au kuimba
● kuimba au kusikiliza wimbo katika vifaa vya kidijitali (k.v simu, redio, kipakatalishi na runinga) kuhusu suala lengwa akiwa na wenzake huku akichukua nafasi mbalimbali (k.v mwimbaji, hadhira n.k.)
● kueleza mafunzo kutokana na wahusika katika wimbo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kutunga wimbo kuhusu mada lengwa na kuwawasilishia wenzake ili kuchanganua wahusika
● kushirikiana na mzazi au mlezi kuchanganua wahusika katika nyimbo mbalimbali kutoka kwa jamii yake.
Je, ni wahusika gani katika wimbo unaowajua?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapochambua wahusika kwa njia wazi akiwa na wenzake.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapochangia hoja katika kazi za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusikilizia nyimbo.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga wimbo kuhusu suala lengwa na kuwawasilishia wenzake.
  • Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anapochanganua wahusika na nafasi zao katika wimbo.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapowawasilishia wenzake wimbo alioutunga.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapochanganua wimbo kuhusu mada lengwa na mzazi au mlezi wake.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi na kutunza vifaa vya kidijitali anavyotumia.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anapoimba nyimbo.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia tungo za fasihi simulizi.
  • Life Skills na Social Studies – masomo haya pia yanashughulikia utatuzi wa mizozo.
  • Performing arts – somo hili pia linashughulikia uwasilisaji wa nyimbo

Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua wahusika katika wimbo. Anatambua wahusika katika wimbo kwa wepesi. Anatambua wahusika katika wimbo. Anatambua baadhi ya wahusika katika wimbo. Anatambua baadhi ya wahusika katika wimbo kwa kuelekezwa.
Kuweza kuchambua wahusika katika wimbo. Anachambua kwa wepesi wahusika katika wimbo. Anachambua wahusika katika wimbo. Anachambua baadhi ya wahusika katika wimbo. Anachambua baadhi ya wahusika katika wimbo kwa kuelekezwa.
Kuweza kueleza mafunzo kutokana na wahusika katika wimbo. Anaeleza kwa urahisi mafunzo kutokana na wahusika katika wimbo. Anaeleza mafunzo kutokana na wahusika katika wimbo. Anaeleza baadhi ya mafunzo kutokana na wahusika katika wimbo. Anaeleza baadhi ya mafunzo kutokana na wahusika katika wimbo kwa kuelekezwa.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Swali Dadisi 
13.2 Kusoma  13.2.1 Kusoma kwa Kina
Mbinu za Lugha
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya mbinu za lugha katika fasihi
  2. kutambua mbinu za lugha katika novela
  3. kueleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika novela
  4. kufurahia kuchanganua matumizi ya mbinu za lugha katika fasihi.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza maana ya mbinu za lugha katika fasihi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutambua mbinu za lugha (k.v. tashbihi, sitiari, nahau, methali, tasfida, tanakali za sauti n.k.) katika novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kueleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika novela iliyoteuliwa na mwalimu akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kuhakiki uwasilishaji wa wenzake na kutoa maoni
  • kufanya utafiti maktabani au mtandaoni kuhusu matumizi ya mbinu za lugha katika novela
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kujadili kuhusu matumizi ya mbinu za lugha katika novela.
Mbinu za lugha zina umuhimu gani zinapotumiwa katika kifungu?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anaposhiriki katika kutambua mbinu za lugha kwenye novela aliyosoma akiwa na wenzake katika kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anapotangamana na wenzake katika kikundi kujadili matumizi ya mbinu za lugha katika novela.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapowawasilishia wenzake muhtasari wa matumizi ya mbinu za lugha katika novela kwa kutetea hoja zake.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapofanya utafiti maktabani na mtandaoni kuhusu matumizi ya mbinu za lugha katika novela.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapotangamana na wenzake katika kikundi kujadili mbinu za lugha katika novela huku akiheshimu maoni yao.
  • Upendo – mwanafunzi anapohakiki uwasilishaji wa wenzake kuhusu mbinu za lugha katika novela huku akiwakosoa kwa upendo na kuwahimiza.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojiandaa ipasavyo ili kuwawasilishia wenzake kazi yake kuhusu mbinu za lugha katika novela. Pia anapochukua hatua ya kutafiti kuhusu matumizi ya mbinu za lugha maktabani au mtandaoni.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi ili kujadili matumizi ya mbinu za lugha katika novela.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko anuwai – kulingana na ujumbe katika novela.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English – somo hili pia linashughulikia kusoma kwa kina.
  • Life Skills na Social Studies – masomo haya pia yanashughulikia utatuzi wa mizozo.

Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kueleza maana ya mbinu za lugha katika fasihi. Anaeleza maana ya mbinu za lugha katika fasihi kwa urahisi. Anaeleza maana ya mbinu za lugha katika fasihi. Anatoa maelezo kiasi kuhusu maana ya mbinu za lugha katika fasihi. Anatoa maelezo kiasi kuhusu maana ya mbinu za lugha katika fasihi kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua mbinu za lugha katika novela. Anatambua mbinu za lugha katika novela kwa urahisi. Anatambua mbinu za lugha katika novela. Anatambua baadhi ya mbinu za lugha katika novela. Anatambua baadhi ya mbinu za lugha katika novela kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika novela. Anaeleza kwa urahisi umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika novela. Anaeleza umuhimu wa mbinu za lugha zilizotumiwa katika novela. Anaeleza umuhimu wa baadhi ya mbinu za lugha zilizotumiwa katika novela. Anaeleza umuhimu wa baadhi ya mbinu za lugha zilizotumiwa katika novela kwa kuelekezwa.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
 13.3 Kuandika  13.3.1 Insha za Kubuni
Maelezo
(Vipindi 2)

Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:

  1. kutambua mambo ya kimsingi katika uandishi wa insha ya maelezo
  2. kuandika insha ya maelezo inayodhihirisha sifa za mtu
  3. kuchangamkia kutoa maelezo kamilifu kuhusu kitu au jambo.
Mwanafunzi aelekezwe:
• kutambua dhana ya insha ya maelezo akiwa peke yake au katika kikundi
• kutambua mambo ya kimsingi katika uandishi wa insha ya maelezo akiwa na wenzake katika kikundi
• kujadiliana na wenzake kuhusu mada ya insha ya maelezo
• kuandaa vidokezo vya insha ya maelezo kuhusu sura na matendo ya mtu anayelengwa katika insha ya maelezo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
• kuandika insha ya maelezo inayotoa sifa za mtu akizingatia muundo ufaao na inayohusisha suala lengwa kisha awasomee wenzake darasani
• kubuni insha ya maelezo inayotoa sifa za mtu kisha awasambazie wenzake mtandaoni ili waitolee maoni
• kutolea insha za wenzake maoni kwa upendo
1. Je, insha ya maelezo inahusu nini?
2. Je, ni vigezo vipi vinatumika katika kuandika insha ya maelezo?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotoa mchango wake katika kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kujadiliana kuhusu insha ya maelezo.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kuandika insha ya maelezo na kuisambaza mtandaoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika insha ya maelezo kwa muundo ufaao.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapobuni na kusambaza insha kwa wenzake.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapotolea insha za wenzake maoni.
Masuala Mtambuko
  • Utatuzi wa mizozo – mwanafunzi anapoandika insha kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha za maelezo.
  • Life Skills na Social Studies – masomo haya pia yanashughulikia utatuzi wa mizozo.

Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua mambo ya kimsingi katika uandishi wa insha ya maelezo. Anatambua kwa urahisi mambo ya kimsingi katika uandishi wa insha ya maelezo. Anatambua mambo ya kimsingi katika uandishi wa insha ya maelezo. Anatambua baadhi ya mambo ya kimsingi katika uandishi wa insha ya maelezo. Anatambua baadhi ya mambo ya kimsingi katika uandishi wa insha ya maelezo kwa kusaidiwa.
Kuweza kuandika insha ya maelezo inayodhihirisha sifa za mtu. Anaandika kwa wepesi insha ya maelezo inayodhihirisha sifa za mtu. Anaandika insha ya maelezo inayodhihirisha sifa za mtu. Anaandika insha ya maelezo inayodhihirisha baadhi ya sifa za mtu. Anaandika insha ya maelezo inayodhihirisha baadhi ya sifa za mtu kwa kuelekezwa.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
13.4 Sarufi 13.4.1 Ukanushaji kwa Kuzingatia Nyakati
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana ya ukanushaji
  2. kutambua nyakati katika matini
  3. kutambua ukanushaji kwa kuzingatia wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao katika matini
  4. kutunga sentensi kwa kuzingatia ukanushaji katika wakati uliopita, uliopo na ujao
  5. kuchangamkia kukanusha sentensi katika wakati uliopita, uliopo na ujao ili kukuza mawasiliano.
Mwanafunzi aelekezwe:
● kueleza maana ya ukanushaji akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kutambua nyakati tatu tofauti (uliopita, uliopo, ujao) kutoka kwenye chati, mti maneno, vitabu au vifaa vya kidijitali akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kutambua ukanushaji wa sentensi katika wakati uliopita, uliopo na ujao akiwa na wenzake katika kikundi
● kutunga sentensi kwa kutumia nyakati hizo na kujadiliana na wenzake wakiwa wawili wawili au katika kikundi
● kutunga sentensi zinazoonyesha ukanushaji katika wakati uliopita, uliopo na ujao kuhusu suala lengwa kisha awatumie wenzake kupitia vifaa vya kidijitali
● kushirikiana na mzazi au mlezi kutunga sentensi zinazoonyesha ukanushaji wa wakati uliopo, uliopita na ujao.
unakanusha sentensi kwa kuzingatia nyakati gani?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anaposhiriki kikamilifu katika kazi za kikundi na mawasiliano mtandaoni.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kutambua ukanushaji kwa kuzingatia nyakati.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahihi kuonyesha ukanushaji wa nyakati.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kutambua ukanushaji wa nyakati na kuutungia sentensi sahihi.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Utatuzi wa mizozo – mwanafunzi anapotunga sentensi kuhusu suala lengwa.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia ukanushaji.
  • Life Skills na Social Studies – masomo haya pia yanashughulikia utatuzi wa mizozo.

 Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana ya ukanushaji. Anaeleza maana ya ukanushaji kwa urahisi. Anaeleza maana ya ukanushaji. Anaeleza kwa kiasi maana ya ukanushaji. Anaeleza kwa kiasi maana ya ukanushaji kwa kuelekezwa.
Kuweza kutambua nyakati katika matini. Anatambua kwa wepesi nyakati katika matini. Anatambua nyakati katika matini. Anatambua baadhi ya nyakati katika matini. Anatambua baadhi ya nyakati katika matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua ukanushaji kwa kuzingatia wakati uliopita, uliopo na ujao katika matini. Anatambua kwa wepesi ukanushaji kwa kuzingatia wakati uliopita, uliopo na ujao katika matini. Anatambua ukanushaji kwa kuzingatia wakati uliopita, uliopo na ujao katika matini. Anatambua baadhi ya ukanushaji kwa kuzingatia wakati uliopita, uliopo na ujao katika matini.  Anatambua baadhi ya ukanushaji kwa kuzingatia wakati uliopita, uliopo na ujao katika matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kutunga sentensi kwa kuzingatia ukanushaji wa wakati uliopita, uliopo na ujao. Anatunga sentensi kwa kuzingatia ukanushaji wa wakati uliopita, uliopo na ujao kwa wepesi. Anatunga sentensi kwa kuzingatia ukanushaji wa wakati uliopita, uliopo na ujao. Anatunga baadhi ya sentensi kwa kuzingatia ukanushaji wa wakati uliopita, uliopo na ujao. Anatunga baadhi ya sentensi kwa kuzingatia ukanushaji wa wakati uliopita, uliopo na ujao kwa kuelekezwa.

 

                                                             14.0 MATUMIZI YA PESA    
 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
 14.1 Kusikiliza na Kuzungumza 14.1.1 Lugha katika Nyimbo
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo
  2. kujadili umuhimu wa vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo teule
  3. kuonea fahari uchanganuzi wa lugha katika nyimbo kama utungo wa fasihi simulizi.
Mwanafunzi aelekezwe:
● kutambua vipengele vya lugha (k.v urudiaji, nahau, methali, maneno yasiyokuwa na maana n.k.) kwa kusikiliza nyimbo kuhusu suala lengwa kutoka kwa mwalimu, kwenye maandishi (k.v vitabu, chati n.k) au vifaa vya kidijitali, akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kujadili umuhimu wa vipengele vya lugha vilivyotumika katika nyimbo walizosikiliza akiwa na wenzake
● kutunga wimbo unaohusiana na suala lengwa akizingatia vipengele vya lugha katika nyimbo akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kushirikiana na mzazi au mlezi wake kusikiliza na kutambua vipengele vya lugha katika nyimbo.
1. Nyimbo hutumia vipengele gani vya lugha?
2. Kutumia vipengele mbalimbali vya lugha katika wimbo kuna umuhimu gani?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotambua vipengele vya lugha katika nyimbo.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali katika kusikiliza nyimbo.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga wimbo na kuzingatia vipengele vya lugha.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapojadili na wenzake katika kikundi vipengele vya lugha katika nyimbo kwa njia wazi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhirikiana na mzazi au mlezi wake kusikiliza nyimbo na kutambua vipengele vya lugha vilivyotumika.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Matumizi ya pesa – mwanafunzi anapotunga nyimbo kuhusu suala lengwa
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia tungo za fasihi simulizi.
  • Business Studies – somo hili pia linashughulikia ujuzi wa matumizi ya pesa.
  • Performing Arts – somo hili pia linashughulikia nyimbo.
 

Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo. Anatambua vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo kwa urahisi. Anatambua vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo. Anatambua baadhi ya vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo. Anatambua baadhi ya vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo kwa kuelekezwa.
Kuweza kujadili vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo teule. Anajadili vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo teule. Anajadili vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo teule. Anajadili baadhi ya vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo teule. Anajadili baadhi ya vipengele vya lugha vinavyotumika katika nyimbo teule kwa kusaidiwa.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
14.2 Kusoma 14.2.1 Ufahamu wa Kifungu cha Mjadala
(Vipindi 2)
Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kudondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu
  2. kutambua msamiati mpya katika kifungu cha ufahamu
  3. kuandika habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi
  4. kuchambua mitazamo katika kifungu cha mjadala
  5. kuridhia kusoma kwa ufahamu ili kukuza uelewa wa habari.
Mwanafunzi aelekezwe:
● kudondoa habari mahususi (k.v. nani, nini, wapi, lini) katika kifungu cha mjadala cha ufahamu
● kutambua msamiati mpya (k.v. maneno na nahau) kuhusu suala lengwa katika kifungu cha ufahamu na kuueleza kwa kutumia kamusi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kuandika habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi akiwa peke yake au kwa kushirikiana na wenzake
● kuchambua mitazamo iliyo katika kifungu cha ufahamu cha mjadala (k.v. tofauti na mifanano iliyopo) akiwa peke yake au na wenzake
● kuwawasilishia wenzake kazi yake ili wamtolee maoni
● kutathmini kazi ya wenzake kwa upendo
● kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma kifungu cha ufahamu na kujibu maswali.
1. Kwa nini tunasoma ufahamu?
2. Je, ni mambo gani yanayoweza kukusaidia kuelewa kifungu cha ufahamu?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapowasilisha kazi yake ya ufahamu kwa wenzake.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki kazi za kikundi.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kukamilisha kikamilifu kazi yake ya ufahamu.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za ujifunzaji.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapotathmini kazi ya wenzake kwa upendo.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko anuwai – yanayojitokeza katika kifungu cha ufahamu.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia hushughulikia stadi ya kusoma.
  • Business Studies – somo hili pia linashughulikia ujuzi wa matumizi ya pesa.
 

 Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kudondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu. Anadondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu kwa urahisi.   Anadondoa habari mahususi katika kifungu cha ufahamu.  Anadondoa baadhi ya habari mahususi katika kifungu cha ufahamu.  Anadondoa baadhi ya habari mahususi katika kifungu cha ufahamu kwa kusaidiwa.
 Kuweza kutambua msamiati katika kifungu cha ufahamu. Anatambua msamiati katika kifungu cha ufahamu kwa urahisi.  Anatambua msamiati katika kifungu cha ufahamu.  Anatambua msamiati baadhi ya nyakati katika kifungu cha ufahamu. Anatambua msamiati baadhi ya nyakati katika kifungu cha ufahamu kwa kusaidiwa.
Kuweza kuandika habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaandika habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi kwa urahisi. Anaandika habari za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaandika habari za sehemu za kifungu cha ufahamu kwa ufupi. Anaandika habari za sehemu za kifungu cha ufahamu kwa ufupi kwa kusaidiwa
Kuweza kuchambua mitazamo katika katika kifungu cha mjadala. Anachambua mitazamo katika katika kifungu cha mjadala kwa urahisi. Anachambua mitazamo katika katika kifungu cha mjadala. Anachambua baadhi ya mitazamo katika kifungu cha mjadala. Anachambua baadhi ya mitazamo katika kifungu cha mjadala kwa kusaidiwa.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
14.3 Kuandika 14.3.1
Insha ya Maelekezo
(Vipindi 2)
 Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua aina za insha za maelekezo
  2. kujadili sifa za insha ya maelekezo
  3. kuandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo
  4. kuandika insha ya maelekezo akizingatia vipengele muhimu vya insha ya maelekezo
  5. kufurahia kutoa maelekezo ifaavyo katika maisha ya kila siku akizingatia anwani na mpangilio ufaao wa hatua.
 Mwanafunzi aelekezwe:
● kubainisha sifa za insha ya maelekezo kwa kuzingatia vielelezo vya insha kwenye matini za kimaandishi au za kidijitali (k.v usahihi wa habari, mpangilio wa maelezo wenye mantiki, lugha sahili, maelezo yanayotoka upande mmoja, n.k)
● kujadili na wenzake aina za insha za maelekezo
● kushiriki katika kikundi kujadili mpangilio ufaao wa hatua za kuelekeza
● kuandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo
● kuandika insha ya maelekezo akizingatia anwani na mpangilio mwafaka wa hatua huku akitumia vipengele vya lugha vinavyotumiwa kuelekeza ili kumjengea msomaji taswira kamili ya anachoelekezwa kufanya
● kuwasomea wenzake katika kikundi insha aliyoandika darasani au awasambazie kwenye vifaa vya kidijitali ili waitolee maoni
kushirikiana na wenzake kusahihisha insha ya maelekezo aliyoandika kwa kuzingatia anwani na mpangilio ufaao wa hatua.
 Unataka kumwelekeza rafiki yako nyumbani kwenu. Utatumia mpangilio gani wa hatua ili asipotee njia?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapoandika insha kwa ufasaha na anapoisoma vizuri.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki na wenzake katika kujadili kuhusu anwani na hatua katika kielelezo cha insha ya maelekezo waliyosoma.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusambaza insha.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoteua lugha mwafaka na kufaulu kutoa maelezo bayana ya anachoelekeza.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapowasomea wenzake insha aliyoandika ili waitolee maoni.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofaulu kuwasomea wenzake insha hadharani.
    
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
    
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi na kusahihisha insha na wenzake na kujifunza ukakamavu, stahamala na kujiamini.
    
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa insha za maelekezo.
    

 Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua aina za insha za maelekezo. Anatambua aina za insha za maelekezo kwa urahisi. Anatambua aina za insha za maelekezo. Anatambua baadhi ya aina za insha za maelekezo. Anatambua baadhi ya aina za insha za maelekezo kwa kusaidiwa.
Kuweza kujadili sifa za insha ya maelekezo. Anajadili sifa za insha ya maelekezo kwa urahisi. Anajadili sifa za insha ya maelekezo.  Anajadili baadhi ya sifa za insha ya maelekezo. Anajadili baadhi ya sifa za insha ya maelekezo kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo. Anaandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo kwa wepesi. Anaandaa mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo. Anaandaa kwa kiasi mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo. Anaandaa kwa kiasi mpangilio wa hatua za insha ya maelekezo kwa kuelekezwa.
Kuweza kuandika insha ya maelekezo akizingatia vipengele muhimu vya insha ya maelekezo. Anaandika kwa wepesi insha ya maelekezo akizingatia vipengele muhimu vya insha ya maelekezo. Anaandika insha ya maelekezo akizingatia vipengele muhimu vya insha ya maelekezo. Anaandika insha ya maelekezo akizingatia baadhi ya vipengele muhimu vya insha ya maelekezo. Anaandika insha ya maelekezo akizingatia baadhi ya vipengele muhimu vya insha ya maelekezo kwa kusaidiwa.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
14.4 Sarufi 14.4.1 Ukubwa wa Nomino

(Vipindi 2)
 Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua nomino katika hali ya ukubwa kwenye matini
  2. kutambua viambishi vya ukubwa katika nomino
  3. kutumia nomino katika hali ya ukubwa ipasavyo
  4. kuchangamkia kutumia nomino katika hali ya ukubwa katika sentensi.
 Mwanafunzi aelekezwe:
● kutambua nomino katika hali ya ukubwa (k.v. jitu, joka, jiji, kapu, goma, jisu, jishamba, n.k.) kwenye orodha ya nomino, chati, kadi maneno, kapu maneno, sentensi, vifungu vya maneno au tarakilishi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kutambua viambishi vya ukubwa katika maneno akiwa peke yake au katika kikundi
● kuandika majina ya vifaa vya darasani katika ukubwa (k.v. jidawati, jitabu, n.k) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kuambatanisha nomino za hali ya wastani na za hali ya ukubwa kwa usahihi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kubadilisha nomino za hali ya wastani ziwe katika katika hali ya ukubwa akiwa peke yake au katika kikundi
● kutunga sentensi akitumia nomino katika hali ya ukubwa kuhusu suala lengwa na kuwasilisha darasani ili wenzake wazitathmini
● kushirikiana na mzazi au mlezi kutambua majina ya vifaa vya nyumbani katika ukubwa (k.v. jimeza, jijiko, jisahani, n.k.) na kutunga sentensi.
 Unazingatia nini unapoandika nomino katika ukubwa?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
    
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapowapa wenzake nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika shughuli za kikundi.
    
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi anajifunza ukakamavu, stahamala na kujiamini.
  • Masuala ya kifedha – mwanafunzi anapotunga sentensi mbalimbali kuhusu suala lengwa.
    
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia nomino.
    

Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
 Kuweza kutambua nomino katika hali ya ukubwa katika matini.  Anatambua kwa wepesi nomino katika hali ya ukubwa katika matini.  Anatambua nomino katika hali ya ukubwa katika matini.  Anatambua baadhi ya nomino katika hali ya ukubwa katika matini.  Anatambua baadhi ya nomino katika hali ya ukubwa katika matini kwa kusaidiwa.
 Kuweza kutambua viambishi vya ukubwa katika nomino.  Anatambua kwa urahisi viambishi vya ukubwa katika nomino.  Anatambua viambishi vya ukubwa katika nomino.  Anatambua baadhi ya viambishi vya ukubwa katika nomino.  Anatambua viambishi vya ukubwa katika nomino kwa kusaidiwa.
 Kuweza kutumia nomino katika hali ya ukubwa ipasavyo.  Anatumia kwa urahisi nomino katika hali ya ukubwa ipasavyo.  Anatumia nomino katika hali ya ukubwa ipasavyo.  Anatumia baadhi ya nomino katika hali ya ukubwa ipasavyo.  Anatumia baadhi ya nomino katika hali ya ukubwa ipasavyo kwa kuelekezwa.

 

                                                     MADA 15.0 MAADILI YA MTU BINAFSI
 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
15.1 Kusikiliza na Kuzungumza 15.1.1Kusikiliza Habari na Kujibu
(Vipindi 2)
 Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua masuala katika matini aliyosikiliza
  2. kutambua msamiati wa suala lengwa katika matini aliyosikiliza
  3. kutabiri yatakayotokea katika matini kutokana na vidokezo alivyosikia katika habari
  4. kueleza maana za msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumiwa katika matini aliyosikiliza
  5. kuchangamkia kushiriki katika kusikiliza kwa ufahamu ili kukuza stadi ya kusikiliza.
 Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua masuala yanayoshughulikiwa katika matini kuhusu suala lengwa aliyosikiliza akiwa peke yake au katika kikundi
  • kutambua msamiati wa suala lengwa uliotumiwa katika matini alizosikiliza kutoka kwenye kifaa cha kidijitali, kutoka kwa mwalimu au mgeni mwalikwa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kutabiri kitakachotokea au atakachofanya mhusika kutoka kwenye matini aliyosikiliza kwa kuzingatia vidokezo (k.v. anwani, picha n.k.) anavyopatana navyo katika usikilizaji akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kueleza maana za msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumiwa katika matini aliyosikiliza akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kusikiliza matini kuhusu suala lengwa kutoka kwa mwalimu au mgeni mwalikwa akiwa na wenzake katika kikundi na kufasiri wazo kuu katika habari hiyo
  • kusikiliza habari kwenye vifaa vya kidijitali (k.v. kinasasauti) kuhusu suala lengwa akiwa katika kikundi na kutaja masuala yanayoshughulikiwa
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kutafiti kwenye tovuti salama kuhusu maadili ya mtu binafsi na kutambua suala kuu au masuala makuu katika matini.
 Je, ni mambo gani yanayokuelekeza kufasiri suala muhimu katika habari unayosikiliza?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – Mwanafunzi anapoeleza kwa uwazi suala kuu au masuala makuu katika matini.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki katika kikundi na kuchangia kutambua na kueleza maana za msamiati wa suala lengwa katika matini aliyosikiliza.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusikilizia habari na kujibu kulingana na maagizo.
  • Kujiamini – mwanafunzi anaposikiliza matini ipasavyo na anapochangia katika shughuli za kikundi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposhiriki shughuli ya kusikiliza kwa ufahamu na mzazi au mlezi wake na kujifunza maaarifa ya kuwasilisha habari kuhusu maadili ya mtu binafsi.
    
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika shughuli za kikundi; pia anapoheshimu zamu ya wenzake katika mazungumzo.
  • Upendo – mwanafunzi anapowasikiliza wasemaji kwa makini. Pia anapowapa wanafunzi wenzake zamu za kuzungumza.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapotunza vifaa vya kidijitali anavyotumia katika mazungumzo
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
    
Masuala Mtambuko
  • Maadili ya mtu binafsi – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kusikiliza na kujibu mazungumzo kuhusu suala lengwa.
    
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia kusikiliza kwa ufahamu.
  • Social Studies – somo hili pia linashughulikia masuala ya kijamii.
    

Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
 Kuweza kutambua masuala katika matini aliyosikiliza.  Anatambua kwa wepesi masuala katika matini aliyosikiliza. Anatambua masuala katika matini aliyosikiliza.   Anatambua baadhi ya masuala katika matini aliyosikiliza.  Anatambua baadhi ya masuala katika matini aliyosikiliza kwa kuelekezwa.
 Kuweza kutambua msamiati wa suala lengwa katika matini aliyosikiliza.  Anatambua kwa urahisi msamiati wa suala lengwa katika matini aliyosikiliza.  Anatambua msamiati wa suala lengwa katika matini aliyosikiliza.  Anatambua baadhi ya msamiati wa suala lengwa katika matini aliyosikiliza.  Anatambua, kwa kuelekezwa baadhi ya msamiati wa suala lengwa katika matini aliyosikiliza.
 Kuweza kutabiri yatakayotokea katika matini kutokana na vidokezo alivyosikia katika habari.  Anatabiri kwa urahisi yatakayotokea katika matini kutokana na vidokezo alivyopata katika matini.  Anatabiri yatakayotokea katika matini kutokana na vidokezo alivyopata katika matini.  Anatabiri kwa kiasi yatakayotokea katika matini kutokana na vidokezo alivyopata katika matini.  Anatabiri kwa kiasi yatakayotokea katika matini kutokana na vidokezo alivyopata katika matini kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza maana za msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumiwa katika matini aliyosikiliza. Anaeleza kwa wepesi maana za msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumiwa katika matini aliyosikiliza. Anaeleza maana za msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumiwa katika matini aliyosikiliza. Anaeleza maana za baadhi ya msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumiwa katika matini aliyosikiliza. Anaeleza kwa kusaidiwa, maana za baadhi ya msamiati wa suala lengwa kama ulivyotumiwa katika matini aliyosikiliza.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
15.2 Kusoma 15.2.1 Ufupisho
(Vipindi 2)
 Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza kwa usahihi ujumbe wa aya za matini kwa sentensi mojamoja
  2. kueleza kwa usahihi ujumbe wa aya zote za matini kwa aya moja
  3. kuandika ufupisho unaozingatia mtazamo wa matini ya kufupishwa
  4. kufurahia kufupisha ujumbe kwa usahihi katika miktadha mbalimbali.
 Mwanafunzi aelekezwe:
  • kueleza kwa usahihi ujumbe katika kila aya kwa kutumia sentensi mojamoja akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kueleza kwa usahihi ujumbe wa aya zote za matini kwa aya moja akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kujadili katika kikundi kuhusu jinsi ya kuandika ufupisho wa matini
  • kushirikiana na mzazi au mlezi kusoma kifungu na kuandika ufupisho kutoka mtandaoni na kutambua.
 Ni mambo gani yanayokusaidia kuandika ufupisho?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapojadiliana na wenzake kuhusu ufupisho wa matini.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki katika kazi za kikundi.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kusoma kifungu.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapofanya ufupisho wa matini katika kikundi.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anaposoma kifungu kutoka mtandaoni na kukifupisha.
    
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Upendo – mwanafunzi anapopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujifunzaji darasani na katika kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
    
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kutambua na kufupisha kifungu.
  • Maadili ya mtu binafsi – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kusoma na kufupisha kifungu kuhusu suala lengwa.
    
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English – somo hili pia hushughulikia dhana ya ufupisho.
    

Vigezo na Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
 Kuweza kueleza kwa usahihi ujumbe wa aya za matini kwa sentensi mojamoja.  Anaeleza kwa usahihi na wepesi ujumbe wa aya za matini kwa sentensi mojamoja.  Anaeleza kwa usahihi ujumbe wa aya za matini kwa sentensi mojamoja.  Anaeleza kwa usahihi ujumbe wa baadhi ya aya za matini kwa sentensi mojamoja.  Anaeleza kwa usahihi sehemu ya ujumbe wa baadhi ya aya za matini kwa sentensi mojamoja kwa kusaidiwa.
 Kuweza kueleza kwa usahihi ujumbe wa aya zote za matini kwa aya moja.  Anaeleza kwa usahihi ujumbe wa aya zote za matini kwa aya moja kwa urahisi.  Anaeleza kwa usahihi ujumbe wa aya zote za matini kwa aya moja.  Anaeleza kwa usahihi sehemu ya ujumbe wa baadhi ya aya za matini kwa aya moja.  Anaeleza kwa usahihi ujumbe wa baadhi ya aya za matini kwa aya moja kwa kuelekezwa.
 Kuweza kuandika ufupisho unaozingatia mtazamo wa matini ya kufupishwa.  Anaandika ufupisho unaozingatia mtazamo wa matini ya kufupishwa kwa wepesi.  Anaandika ufupisho unaozingatia mtazamo wa matini ya kufupishwa.  Anaandika ufupisho bila kuzingatia mtazamo wa matini ya kufupishwa.  Anaandika ufupisho bila kuzingatia mtazamo wa matini ya kufupishwa kwa kusaidiwa.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
 15.3 Kuandika 

15.3.1 Kuandika Kidijitali

Baruapepe

(Vipindi 2)

 Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua ujumbe unaoafiki baruapepe kwa rafiki
  2. kutambua vipengele vya kimuundo vya baruapepe kwa rafiki
  3. kutumia lugha inayofaa katika uandishi wa baruapepe kwa rafiki
  4. kuandika baruapepe kwa rafiki kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao
  5. kujenga mazoea ya kuwasiliana kuandika kwa baruapepe kwa rafiki.
 Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua ujumbe unaoafiki baruapepe kwa rafiki kwa kujadiliana na mwenzake
  • kujadili vipengele vya kimuundo vya baruapepe kwa rafiki akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
  • kushiriki katika kujadili na wenzake kuhusu lugha inayofaa katika uandishi wa baruapepe kwa rafiki
  • kuandika baruapepe kwa rafiki kwenye tarakilishi na kumsambazia mwenzake kupitia mtandao ili aitolee maoni
  • kumwandikia mwalimu wake baruapepe kwa rafiki ili aitathmini.
  1. Je, ni mambo gani yanayoweza kukufanya uandike baruapepe kwa rafiki?
  2. Je, utazingatia nini unapoandika barua pepe kwa rafiki yako?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano – mwanafunzi anapotoa mchango katika kazi ya kikundi.
  • Ushirikiano – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kujadili ujumbe, lugha na muundo wa baruapepe kwa rafiki.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia tarakilishi kuandika baruapepe kwa rafiki na kuisambaza mtandaoni.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapoandika baruapepe kwa rafiki.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapoandika baruapepe kwa rafiki kwenye tarakilishi na kumsambazia mwalimu.
    
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
    
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kikundi kujadili ujumbe, lugha na muundo wa baruapepe kwa rafiki.
    
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English, Indigenous Languages na Foreign Languages – masomo haya pia yanashughulikia uandishi wa kiuamilifu.
    

Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kutambua ujumbe unaoafiki baruapepe kwa rafiki. Anatambua ujumbe unaoafiki baruapepe kwa rafiki kwa urahisi. Anatambua ujumbe unaoafiki baruapepe kwa rafiki. Anatambua baadhi ya ujumbe unaoafiki baruapepe kwa rafiki. Anatambua baadhi ya ujumbe unaoafiki baruapepe kwa rafiki kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua vipengele vya kimuundo vya baruapepe kwa rafiki. Anatambua kwa wepesi vipengele vya kimuundo vya baruapepe kwa rafiki. Anatambua vipengele vya kimuundo vya baruapepe kwa rafiki. Anatambua baadhi ya vipengele vya kimuundo vya baruapepe kwa rafiki. Anatambua baadhi ya vipengele vya kimuundo vya baruapepe kwa rafiki kwa kusaidiwa.
Kuweza kutumia lugha inayofaa katika uandishi wa baruapepe kwa rafiki. Anatumia lugha inayofaa katika uandishi wa baruapepe kwa rafiki kwa urahisi. Anatumia lugha inayofaa katika uandishi wa baruapepe kwa rafiki. Anatumia kwa kiasi lugha inayofaa katika uandishi wa baruapepe kwa rafiki. Anatumia kwa kiasi lugha inayofaa katika uandishi wa baruapepe kwa rafiki.
Kuweza kuandika baruapepe kwa rafiki kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao. Anaandika kwa urahisi baruapepe kwa rafiki kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufao Anaandika baruapepe kwa rafiki kwa kuzingatia ujumbe, lugha na muundo ufaao. Anaandika baruapepe kwa rafiki kwa kuzingatia ujumbe na baadhi ya vipengele vya lugha na muundo ufaao. Anaandika baruapepe kwa rafiki kwa kuzingatia ujumbe na baadhi ya vipengele vya lugha na muundo ufaao kwa kuelekezwa.

 

 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shughuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
 15.4 Kuandika  15.4.1 Usemi Halisi na Usemi wa Taarifa

(Vipindi 2)
 Kufikia mwisho wa mada ndogo, mwanafunzi aweze:
  1. kueleza maana za usemi halisi na usemi wa taarifa
  2. kutambua kanuni za kubadilisha usemi halisi kuwa usemi wa taarifa
  3. kutumia usemi halisi na usemi wa taarifa ifaavyo
  4. kuchangamkia matumizi ya usemi halisi na usemi wa taarifa katika mawasiliano.
 Mwanafunzi aelekezwe:
● kueleza maana za usemi halisi na usemi wa taarifa akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kutambua kanuni za kimsingi za kubadilisha usemi halisi kuwa usemi wa taarifa (k.v leo kuwa siku hiyo, kwetu kuwa kwao, hapa kuwa hapo, kiambishi ‘ta’ cha wakati kuwa ‘nge’ n.k.) akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kutungia wenzake katika kikundi sentensi sahili za usemi halisi na usemi wa taarifa akizingatia suala lengwa
● kumsomea mwenzake sentensi sahili alizotunga za usemi halisi na usemi wa taarifa
● kubadilisha sentensi sahili kutoka usemi halisi hadi usemi wa taarifa na usemi wa taarifa hadi usemi halisi akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi
● kushirikiana na wenzake kutunga na kutathmini sentensi sahili za usemi halisi na usemi wa taarifa.
 Ni kwa usemi gani tunaweza kuwasilisha ujumbe?
Je, ni mambo gani unayazingatia wakati wa kubadilisha usemi halisi kuwa usemi wa taarifa?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Mawasiliano na ushirikiano – mwanafunzi anaposhiriki katika kazi za kikundi na kujadili usemi halisi na wa taarifa.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotambua sentensi sahili za usemi halisi na usemi wa taarifa kwenye matini ya kidijitali.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapomsomea mwenzake sentensi sahili alizotunga za usemi halisi na usemi wa taarifa.
  • Ubunifu – mwanafunzi anapotunga sentensi sahili za usemi halisi na usemi wa taarifa.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapotunga na kutathmini sentensi sahili za usemi halisi na usemi wa taarifa na wenzake.
    
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu maoni ya wenzake katika kazi ya kikundi.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapojitolea kuchukua nafasi mbalimbali katika shughuli za kikundi.
  • Umoja – mwanafunzi anaposhiriki katika shughuli za kikundi.
    
Masuala Mtambuko
  • Ukakamavu – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake katika kutambua sentensi sahili za usemi halisi na usemi wa taarifa anakuza ukakamavu, stahamala na kujiamini.
  • Maadili ya mtu binafsi – mwanafunzi anaposhirikiana na wenzake kutumia usemi halisi na wa taarifa katika sentensi kuhusu suala lengwa.
    
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English – somo hili pia hushughulikia dhana ya usemi halisi na usemi wa taarifa.
    

Viwango vya Kuzingatia Katika Kutathmini

⇒Viwango
⇓Vigezo
Kuzidisha Matarajio  Kufikia Matarajio Kukaribia Matarajio Mbali na Matarajio
Kuweza kueleza maana za usemi halisi na usemi wa taarifa. Anaeleza maana za usemi halisi na usemi wa taarifa kwa ufasaha. Anaeleza maana za usemi halisi na usemi wa taarifa. Anaeleza kwa kiasi maana za usemi halisi na usemi wa taarifa. Anaeleza kwa kiasi maana za usemi halisi na usemi wa taarifa kwa kusaidiwa.
Kuweza kutambua kanuni za kubadilisha usemi halisi kuwa usemi wa taarifa. Anatambua kanuni za kubadilisha usemi halisi kuwa usemi wa taarifa kwa urahisi. Anatambua kanuni za kubadilisha usemi halisi kuwa usemi wa taarifa. Anatambua baadhi ya kanuni za kubadilisha usemi halisi kuwa usemi wa taarifa. Anatambua baadhi ya kanuni za kubadilisha usemi halisi kuwa usemi wa taarifa kwa kuelekezwa.
Kuweza kutumia usemi halisi na usemi wa taarifa ifaavyo. Anatumia usemi halisi na usemi wa taarifa ifaavyo kwa urahisi. Anatumia usemi halisi na usemi wa taarifa ifaavyo. Anatumia baadhi ya usemi halisi na usemi wa taarifa ifaavyo. Anatumia baadhi ya usemi halisi na usemi wa taarifa ifaavyo kwa kusaidiwa.


SHUGHULI ZA HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOCHANGIA UJIFUNZAJI

Mradi wa shughuli ya huduma za kijamii umejikita katika mada ndogo ya fasihi simulizi. Mradi huu utamwezesha mwanafunzi kuelewa dhana ya fasihi simulizi aliyojifunza darasani. Mradi huu utahusisha ukusanyaji wa nyimbo za watoto. Kazi hii itatumika shuleni kama nyenzo ya kufundisha fasihi simulizi.

Mradi huu utahitaji mwanafunzi kutambua aina mbalimbali za nyimbo za watoto katika fasihi simulizi na njia mwafaka ya kukusanya nyimbo hizo. Ili kutekeleza mradi huu mwanafunzi ashirikishwe katika kikundi.

Mradi huu utatekelezwa kwa:

  1. Kutambua nyimbo za mbalimbali za fasihi simulizi
  2. kutambua mbinu mwafaka ya kukusanya nyimbo za watoto katika fasihi simulizi
  3. kutambua mahali watakapozuru ili kupata nyimbo mbalimbali za watoto
  4. kuomba idhini ya kufanya utafiti kutoka kwa wasimamizi wa shule
  5. kuenda nyanjani kufanya utafiti
  6. kurekodi au kunasa nyimbo za watoto kwa kutumia vifaa vya kidijitali
  7. kuwasilisha nyimbo walizokusanya
  8. kueleza mafanikio na changamoto ya kazi mradi.
 Mada   Mada Ndogo   Matokeo Maalum Yanayotarajiwa   Mapendekezo ya Shighuli za Ujifunzaji   Maswali Dadisi 
Kusikiliza na kuzungumza Nyimbo za Watoto Kusikiliza na Kuzungumza
Nyimbo za Watoto
Kufikia mwisho wa kazi mradi, mwanafunzi aweze:
  1. kutambua mbinu mwafaka za kukusanya nyimbo za watoto
  2. kukusanya aina mbalimbali za nyimbo za watoto katika jamii
  3. kujadili ujumbe unaojitokeza katika nyimbo mbalimbali za watoto alizozikusanya
  4. kueleza mafunzo yanayojitokeza katika aina mbalimbali za nyimbo za watoto alizozikusanya
  5. kuchangamkia nafasi ya fasihi simulizi katika ukuzaji wa lugha.
Mwanafunzi aelekezwe:
  • kutambua mbinu mwafaka za kukusanya nyimbo za watoto katika jamii yake akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi kujadiliana na wenzake kuhusu mbinu alizozitambua
  • kukusanya aina mbalimbali za nyimbo za watoto (k.v. za kuvuka barabara, za kuaga mwalimu, n.k.) katika jamii yake
  • kurekodi (inapowezekana) nyimbo za watoto kwa kutumia kifaa cha kidijitali ili kumsaidia katika kuzichambua
  • kujadili sifa za nyimbo za watoto alizozikusanya (k.m. unaimbwa lini, na akina nani, kwa nini n.k) akishirikiana na wenzake katika kikundi
  • kutathmini ujumbe unaojitokeza katika kila wimbo alioukusanya akiwa na wenzake katika kikundi
  • kujadili mafunzo yanayojitokeza katika nyimbo za watoto alizozikusanya
  • kuwasilishia kazi yake kwa wenzake na mwalimu ili waitathmini
  • kutathmini kazi za wenzake kwa upendo.
  1. Je, ni nyimbo gani za watoto unazozijua?
  2. Je, ni ujumbe gani unaopata katika nyimbo za watoto unazozijua?
Umilisi wa Kimsingi Unaokuzwa
  • Uwazaji kina na utatuzi wa matatizo – mwanafunzi anapofikiri kuhusu ujumbe na mafunzo yanayojitokeza katika nyimbo za watoto.
  • Mawasiliano na ushirikiano – mwanafunzi anapowasiliana na watu anapokusanya nyimbo za watoto.
  • Ujuzi wa kidijitali – mwanafunzi anapotumia vifaa vya kidijitali kurekodi nyimbo za watoto.
  • Kujiamini – mwanafunzi anapowasilisha nyimbo za watoto alizozikusanya.
  • Hamu ya ujifunzaji – mwanafunzi anapoenda nyanjani kukusanya na kujifunza nyimbo mbalimbali za watoto.
Maadili
  • Heshima – mwanafunzi anapoheshimu wanajamii anaotangamana nao wakati wa kukusanya nyimbo za watoto.
  • Uwajibikaji – mwanafunzi anapokusanya aina mbalimbali za nyimbo za watoto.
  • Amani – mwanafunzi anapokusanya aina mbalimbali za nyimbo za watoto kwa utulivu.
Masuala Mtambuko
  • Masuala mtambuko anuwai – kutegemea aina mbalimbali za nyimbo za watoto.
Uhusiano na Masomo Mengine
  • English na Indigenous Languages – masomo haya pia yanashughulikia tungo za fasihi simulizi.

Vigezo na Viwango vya Kuzingatia katika Kutathmini

⇒Viwango
 ⇓Vigezo
 Kuzidisha Matarajio   Kufikia Matarajio   Kukaribia Matarajio   Mbali na Matarajio 
Kuweza kutambua mbinu mwafaka za kukusanya nyimbo za watoto. Anatambua mbinu mwafaka za kukusanya nyimbo za watoto kwa urahisi. Anatambua mbinu mwafaka za kukusanya nyimbo za watoto. Anatambua baadhi ya mbinu mwafaka za kukusanya nyimbo za watoto. Anatambua baadhi ya mbinu mwafaka za kukusanya nyimbo za watoto kwa kusaidiwa.
Kuweza kukusanya aina mbalimbali za nyimbo za watoto katika jamii. Anakusanya kwa umahiri aina mbalimbali za nyimbo za watoto katika jamii. Anakusanya aina mbalimbali za nyimbo za watoto katika jamii. Anakusanya nyimbo chache za watoto katika jamii. Anakusanya nyimbo chache za watoto katika jamii kwa kuelekezwa.
Kuweza kujadili ujumbe unaojitokeza katika nyimbo mbalimbali za watoto alizozikusanya. Anajadili kwa urahisi ujumbe unaojitokeza katika nyimbo mbalimbali za watoto alizozikusanya. Anajadili ujumbe unaojitokeza katika nyimbo mbalimbali za watoto alizozikusanya. Anajadili baadhi ya ujumbe unaojitokeza katika nyimbo mbalimbali za watoto alizozikusanya. Anajadili baadhi ya ujumbe unaojitokeza katika nyimbo mbalimbali za watoto alizozikusanya kwa kusaidiwa.
Kuweza kueleza mafunzo yanayojitokeza katika aina mbalimbali za nyimbo za watoto alizozikusanya. Anaeleza kwa ufasaha mafunzo yanayojitokeza katika aina mbalimbali za nyimbo za watoto alizozikusanya. Anaeleza mafunzo yanayojitokeza katika aina mbalimbali za nyimbo za watoto alizozikusanya. Anaeleza baadhi ya mafunzo yanayojitokeza katika aina mbalimbali za nyimbo za watoto alizozikusanya. Anaeleza baadhi ya mafunzo yanayojitokeza katika aina mbalimbali za nyimbo za watoto alizozikusanya kwa kuelekezwa.

MUHTASARI WA MBINU ZA KUTATHMINI, NYENZO ZA KUFUNDISHIA NA MAPENDEKEZO YA SHUGHULI NYINGINE ZILIZORATIBIWA ZA UJIFUNZAJI

MADA  MAPENDEKEZO YA MBINU ZA KUTATHMINI  MAPENDEKEZO YA NYENZO ZA KUFUNDISHIA  MAPENDEKEZO YA SHUGHULI NYINGINE ZILIZORATIBIWA ZA UJIFUNZAJI 
KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
  1. Kumakinikia jinsi mwanafunzi anavyotumia lugha katika mawasiliano
  2. Kujibu maswali
  3. Maigizo
  4. Kutambua k.m. kwenye orodha
  5. Kuambatanisha maneno na majibu
  6. Mijadala
  7. Mazungumzo
  8. Matumizi ya ishara za mwili k.v ishara za uso, za mikono na mabega kuimarisha masimulizi yake
  9. Wanafunzi kufanyiana tathmini
  • Chati
  • Michoro na picha
  • Mgeni mwalikwa
  • Vifaa vya kidijitali (k.v tarakilishi/vipakatalishi, kinasasauti, rununu, projekta, video)
  • Mti maneno
  • Kapu maneno
  • Vitabu mbalimbali
  1. Kazi ya vikundi
  2. Vyama vya ushirika shuleni
  3. Mijadala inayohusu masuala mtambuko mbalimbali
  4. Ziara za nyanjani
  5. Kutagusana na vyombo vya habari na vifaa vingine vya kidijitali
KUSOMA
  1. Kutunga sentensi k.m. kwa kutumia msamiati lengwa
  2. Kujibu maswali k.m. katika ufahamu
  3. Kutoa muhtasari wa ufahamu au matini yaliyosomwa
  4. Kusoma kwa sauti
  5. Wanafunzi kufanyiana tathmini
  6. Potfolio
  7. Shajara
  • Tarakilishi/vipakatalishi
  • Kinasasauti
  • Rununu
  • projekta
  • Kamusi mbalimbali
  1. Kazi ya vikundi
  2. Vyama vya ushirika shuleni
  3. Mijadala inayohusu masuala mtambuko mbalimbali
  4. Ziara za nyanjani
  5. Kutagusana na vyombo vya habari na vifaa vingine vya kidijitali
KUANDIKA
  1.  Kuandika tungo mbalimbali
  2. Wanafunzi kufanyiana tathmini
  3. Potfolio
  4. Shajara
  5. Mijadala kuhusu vidokezo vya insha
  • Kielelezo cha insha ya masimulizi
  • Kielelezo cha insha ya maelezo
  • Kielelezo cha insha ya maelekezo
  • Nakala ya barua ya kirafiki
  • Nakala ya barua rasmi
  • Barua pepe
  1. Kazi ya vikundi
  2. Vyama vya ushirika shuleni
  3. Mijadala inayohusu masuala mtambuko mbalimbali
  4. Ziara za nyanjani
  5. Kutagusana na vyombo vya habari na vifaa vingine vya kidijitali
SARUFI
  1. Kutambua k.m. kwenye orodha
  2. Kuambatanisha maneno lengwa
  3. Kujaza mapengo
  4. Kutunga sentensi
  5. Kazi mradi
  • Tarakilishi/vipakatalishi
  • Kinasasauti
  • Rununu
  • projekta
  • Kapu maneno
  • Mti maneno
  • Kadi maneno
  • Picha za vitu mbalimbali
  • Michoro
  • Chati
  • Mabango
  • Sanamu
  • Nyenzo halisi
  1. Kazi ya vikundi
  2. Vyama vya ushirika shuleni
  3. Ziara za nyanjani
  4. Kutagusana na vyombo vya habari na vifaa vingine vya kidijitali

 

Read 4535 times Last modified on Wednesday, 04 January 2023 09:00

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.