WIKI |
KIPINDI |
MADA |
MADA NDOGO |
MATOKEO MAALUM YANAYOTOKEA |
MASWALI DADISI |
MAPENDEKEZO YA SHUGLI ZA UFUNZAJI |
PENDEKEZO LA TATHMINI |
NYEZO |
MAONI |
1 |
1 |
Shambani. |
Sauti. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi bora kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha usomaji |
Ni sauti zipi Unazoweza kutamka? |
Mwanafunzi atambue sauti bw, fy na kw katika maneno. Mwanafunzi asikilize silabi za sauti lengwa ikitamkwa na mwalimu kisha atamke pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa peke yake, wawili wawili na kama darasa. Mifano ya silabi hizi ni: bwa, bwe; fya, fye; kwa, kwe, kwi n.k. |
Mwalimu asikilize baadhi ya sauti ambazo wanafunzi wanaweza kutamka kwa pamoja. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 2-3 |
|
|
2 |
Kusikiliza na kuzungumza |
sauti |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi bora kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha usomaji kuandika maneno kutokana na silabi zilizofunzwa ili kuimarisha uandishi bora |
Unajua kusoma sauti zipi mbili zinazotamkwa? Unajua kuandika maneno gani yanayoundwa kutokana na sauti mbili zinazotamkwa pamoja |
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia (papaya) kusikiliza sauti lengwa ikitamkwa. Mwanafunzi aweza kusikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa. Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi k.v. silabi bwana, bweka, fyata, fyeka, kwao, kwea na kwekwe. Mwanafunzi aandike herufi za sauti alizosoma hewani na vitabuni pamoja na maneno yanayojumuisha sauti hizo. |
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wameweza Kuandika baadhi ya sauti mbili zinazofanana. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 4-5 |
|
|
3 |
Msamiati. |
Kusikiliza na kuzungu mza |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua msamiati unaohusiana na shughuli za shambani ili kuimarisha mawasiliano kusoma maneno na sentensi kuhusu shambani ili kuimarisha usomaji kutunga sentensi akitumia msamiati wa shambani ili kuimarisha mawasilian |
Je, wajua vifaa vipi vinavyotumik a shambani? |
Mwanafunzi asome msamiati wa shambani kama vile jembe, shoka, upanga, kifyekeo, plau, trekta, lima, fyeka, panda na kwekwe katika kadi na chati. Mwanafunzi ataje majina ya vifaa halisi, picha au michoro anavyoonyeshwa. Mwanafunzi atazame vifaa vya shambani hivyo kwenye tarakilishi au tabuleti vikifanya kazi. Mwanafunzi achore maumbo ya vifaa vinavyotumika shambani. |
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanatambua vifaa vinavyotumika shambani. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 6 |
|
2 |
1 |
Msamiati. |
Kusikiliza na kuzungu mza |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kuandika maneno na sentensi zinazojumuisha msamiati wa shambani katika kujenga uandishi bora kuthamini matumizi ya msamiati wa shambani katika mawasiliano |
Ni kifaa kipi cha shamba unachoweza kuchora? |
Wanafunzi waambatanishe kadi za maneno na vifaa halisi wakiwa katika vikundi. Wanafunzi waweza kushiriki katika nyimbo na mashairi kuhusu shambani. Mwanafunzi aandike majina ya vifaa vinavyotumika shambani. Mwanafunzi atunge na kusoma sentensi akitumia msamiati wa shambani. |
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wameweza kuchora baadhi ya vifaa vya shamba vinavyochorwa. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 8-9 |
|
|
2 |
Kusikiliza nakuzungum za. |
Masimulizi |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kusikiliza kwa makini masimulizi kuhusu shambani katika kujenga usikivu kutaja majina ya vifa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza |
Je, ni vifaa vipi hutumika shambani? |
Mwanafunzi kusimulia kuhusu shambani. Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu vifaa vinavyotumika shambani kama vile; jembe, shoka, upanga, kifyekeo, plau, trekta, lima, fyeka na panda akionyeshwa vifaa halisi, picha au michoro. Mwanafunzi aelezee umuhimu wa vifaa vinavyotumika shambani. |
Mwalimu ahakikishe kwamba wanafunzi wamesikiliza kwa makini ili kuimarisha umasikivu. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 10 |
|
|
3 |
Kusikiliza nakuzungumza |
Masimulizi |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kuelezea vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza kuelezea shughuli zinazofanyika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza kutambua matumizi ya vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha stadi ya kuzungumza kuthamini umuhimu wa vifaa vinavyotumika shambani |
|
Mwanafunzi aweza kushirikishwa katika nyimbo au mashairi kuhusu vifaa vinavyotumika shambani. Mwanafunzi aweza kushirikishwa katika kuigiza vitendo vinavyofanywa shambani |
Mwalimu ahakikishe kuwa mwanafunzi anaeza kuelezea baadhi ya vifaa vinavyotumika shambani. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 11 |
|
3 |
1 |
Kusoma. |
Hadithi. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua picha za vifaa vinavyotumika shambani ili kuimarisha ufahamu wa hadithi kusoma hadithi za picha zinazohusu shamba ili kujenga usomaji bora |
Unaona nini katika picha? Ni nini kitakachotend eka katika hadithi? |
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi. Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi. Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi. Mwanafunzi asome na wengine darasani, wakiwa wawili na baadaye asome peke yake |
Mwalimu awawezeshe wanafunzi kusoma hadithi kwa makini huku wakiielewa. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 12 |
|
|
2 |
Kusoma. |
Hadithi. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kusikiliza hadithi zikisomwa na mwalimu kuhusu vifaa vinavyotumika shambani ili kujenga usikivu kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu shambani ili kupata ujumbe kuchangamkia kusoma hadithi za vifaa vinavyotumika shambani ili kuendeleza stadi ya usomaji |
Ni vifaa vipi vimetajwa katika hadithi? |
Wanafunzi waweza kusomeana hadithi wakiwa wawili wawili au katika vikundi. Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia vifaa vya kiteknolojia k.m. tarakilishi na projekta. Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kwa kutumia jitabu mbele ya darasa. Mwanafunzi athibitishe utabiri wao baada ya kusoma hadithi. |
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanaweza kusomeana hadithi wakiwa wiwili wawili. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 13 |
|
|
3 |
Kusikiliza na kuzungumza. |
Kuandika. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi ya uandishi |
Je, ni mambo yapi yanayofaa kuzingatiwa unapoandika kisa? |
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka mwingine. Mwanafunzi aelezee yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k. Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwanafunzi. |
Mwalimu ahakikishe wanafunzi wanafahamu mambo ya kuzingatia unapoelezea kisa chochote. |
Mwanafunzi Tarakilishi 1Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk,2-3 |
|
4 |
1 |
Kusikiliza na kuzungumza |
Kuandika |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi. |
Je, ni kisa gani unachoweza kuandika juu ya shamba? |
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili. Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo, uhariri na uchapishaji. |
Mwalimu awasikiliza wanafunzi wakipeana kisa chochote kile kuhusu shamba. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 14 |
|
|
2 |
Sarufi |
Nafsi ya tatu wakati ujaoumoja na wingi |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua maneno na viambishi vinavyotumika kuonyesha nafsi ya tatu na wakati ujao katika umoja na wingi ili kuimarisha mawasiliano kutumia nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika sentensi kwa usahihi ili kuimarisha mawasiliano |
Je, unatumia neno gani kuonyeshea mwenzako akiwa mbali |
Mwanafunzi atumie nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika mazungumzo. Mwanafunzi atumie nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi katika sentensi. Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia nafsi ya tatu wakati ujao hali ya umoja na wingi. Wanafunzi wanaweza kupewa sentensi zinazojumuisha nafsi na nyakati mbalimbali wazitambue katika vikundi |
Mwalimu asikilize wanafunzi wakitumia baadhi ya maneno yanayoonyesha nafsi ya tatu na wakati ujao katika umoja. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 15 |
|
|
3 |
Sarufi |
Nafsi ya tatu wakati ujaoumoja na wingi |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kusoma vifungu vilivyo na nafsi ya tatu, wakati ujao kwa umoja na wingi ili kujenga usomaji kuandika vifungu vilivyo na nafsi ya tatu, wakati ujao kwa umoja na wingi ili kujenga uandishi bora |
Ikiwa nanuia kusafiri kesho, nitasemaje? |
Mwanafunzi aweza kupewa zoezi katika tarakilishi ili atumie mbinu ya kuburura na kutia kapuni. Mwanafunzi aigize vitendo vya kuashiria nafsi ya kwanza, ya pili na ya tatu huku akitunga sentensi. Mwanafunzi aweza kupata ufafanuzi wa nafsi kwa kutumia vibonzo katika tarakilishi. |
Mwalimu awasikilize wanafunzi wakisoma vifungu kwa makini. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk,16-17 |
|
5 |
1 |
Uzalendo. |
Sauti mbili tofauti zinazotam kwa pamoja |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi bora kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha usomaji |
Ni sauti zipi unazojua kutamka? Unajua kusoma silabi zipi katika maneno? |
Mwafunzi atambue sauti mw, nd na pw katika maneno. Mwanafunzi asikilize mwalimu akizitamka silabi zinazotokana na sauti lengwa kisha atamke pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa pekee, wawili na darasa zima k.m mwa, mwe, mwi na mwo |
Mwalimu asikilize wanafunzi wakitamka silabi mbili pamoja ili kuimarisha matamshi bora. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 18-19 |
|
|
2 |
|
Sauti mbili tofauti zinazotam kwa pamoja |
kuandika silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha uandishi bora kusoma maneno kwa kutumia silabi zinazotokana na sauti lengwa ili kuimarisha usomaji |
Unajua kusoma silabi zipi katika maneno? |
Mwanafunzi aweza kutumia teknolojia kama vile papaya, tarakilishi, projekta na kipaza sauti kumsaidia kuimarisha matamshi yake. Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akitamka sauti lengwa. Mwanafunzi atambue sauti alizosoma katika maneno kwa mfano k. m mwana, mwananchi, ndoo, ndizi, uzalendo, pwani, pweza na pweke |
Mwalimu awaangalie wanafunzi wakiandika silabi mbili zinazotokanan na silabi lengwa. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 20-21 |
|
|
3 |
|
Sauti mbili tofauti zinazotam kwa pamoja |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kusoma hadithi zilizo na maneno yaliyo na sauti lengwa ili kumsaidia mwanafunzi kutamka sauti husika ili kuimarisha matamshi na usomaji Kuchangamkia kutamka sauti lengwa ili kuimarisha mawasiliano. |
Ni herufi na maneno yapi yanayoundwa kutokana na sauti mbili zinazotamkwa pamoja? |
Mwanafunzi asome maneno kwa kutumia silabi na kugawa yaliyo marefu zaidi katika sehemu ndogo ndogo. Wanafunzi wasome hadithi zilizo na maneno yaliyobeba sauti lengwa darasani au wawili wawili. Mwanafunzi anakili herufi na maneno yanayotokana na sauti alizofunzwa. Wanafunzi aandike maneno yanayojumuisha sauti lengwa. |
Mwalimu awasikilize wanafunzi wakisema baadhi ya maneno ambayo yanaundwa kutokana na sauti mbili zinazotamkwa pamoja. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 21-22 |
|
6 |
1 |
Msamiati. |
Msamiati. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua msamiati ambao unahusiana na uzalendo ili kuimarisha mawasiliano kusoma msamiati unaohusiana na uzalendo ili kujenga usomaji |
Je, uzalendo ni nini? |
Mwanafunzi asome maneno yanayohusiana na uzalendo kama vile; umoja, amani, upendo, bendera, taifa, nchi, raia, gwaride, rangi za bendera kwa kutumia kadi za maneno. Mwanafunzi aeleze maana ya msamiati wa uzalendo. Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu maana za maneno yanayohusiana na uzalendo |
Mwalimu awasikile wanafunzi wakifafanua baadhi ya msamiati unaotokana na uzalendo. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 23 |
|
|
2 |
Kusikiliza na Kuzungumza : |
Masimulizi |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua maneno yanayoonyesha uzalendo ili kuyatumia katika mawasiliano kusimulia visa vinavyojumuisha mambo yanayoweza kuimarisha uzalendo ili kujenga stadi ya kuzungumza |
Je, ni nini maana ya uzalendo? Uzalendo una umuhimu gani? |
Mwanafunzi aeleze baadhi ya mambo yanayoweza kuimarisha uzalendo katika nchi yake kwa kutumia mgeni mwalikwa. Mwanafunzi asimulie visa vinavyojumuisha mambo yanayoweza kuimarisha uzalendo kama vile amani, umoja, upendo na bendera ya Kenya. Mwanafunzi asikilize kwa makini hadithi anazosimuliwa. |
Mwalimu kuwasikiliza wanafunzi wakielezea maana ya uzalendo baada ya kipindi. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 26 |
|
|
3 |
Kusikiliza na Kuzungumza : |
Masimulizi |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kusikiliza masimulizi kuhusu uzalendo ili kuimarisha usikivu Kuthamini umuhimu wa uzalendo katika maisha ya kila siku. |
Je, ni kwa njia zipi unaweza kuonyesha uzalendo? Bendera ina umuhimu gani? |
Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha vitendo vya kizalendo. Wanafunzi wajadiliane kuhusu uzalendo katika makundi. Wanafunzi waimbe wimbo wa taifa na kujadili maana ya baadhi ya maneno ya kizalendo katika wimbo huo. Mwanafunzi atunge sentensi kuhusu baadhi ya mambo yanayohusu uzalendo. |
Mwalimu awasikilize wanafunzi huku wakisema umuhimu wa bendera. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 27 |
|
7 |
1 |
Kusoma: |
Hadithi. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua rangi za bendera ili kuimarisha uzalendo kutambua maneno yanayohusiana na uzalendo ili kuimarisha mawasiliano |
Je, unajua nini kuhusu uzalendo? Ni vipi unavyoweza kuonyesha upendo kwa nchi yako? |
Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi. Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi. Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma hadithi |
|
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 28 |
|
|
2 |
Kuandika |
Kuandika |
kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi ya uandishi |
Je, ni mambo yapi yanayofaa kuzingatiwa unapoandika kisa? |
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka. Mwanafunzi aelezee yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k. Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa na mwanafunzi |
Mwalimu awaangalie wanafunzi wakiandika kisa kwa hati nadhifu. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 30 |
|
|
3 |
|
Kuandika |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi. |
Je, ni tukio gani unaloweza kukumbuka na kuandikia kisa? |
Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili. Mwanafunzi aandike kisa kifupi kinachohusiana na mada. Kisa hiki kifuate hatua tano za uandishi: maandalizi, nakala ya kwanza, marejeleo, uhariri na uchapishaji |
Mwalimu awasikilize wanafunzi wakijadili tukio wanaloweza kukumbuka ili Kuandika kisa. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 31 |
|
8 |
1 |
Sarufi |
Matumizi ya: -ake na -ao) |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua matumizi ya; -ake na –ao ili kuimarisha mawasiliano kusoma vifungu vya maneno vinavyojumuisha -ake na -ao ili kujenga usomaji kutunga sentensi akitumia -ake na ao ili kuimarisha ubunifu |
Je, utatumia neno gani kuonyesha kwamba unachozungu mzia ni chako? Je, ni nini wingi wa – ake? |
Mwanafunzi aonyeshe vitu vyake na vya wengine darasani na kuvirejelea akitumia ake na –ao. Mwanafunzi asome vifungu vyenye matumizi -ake na –ao. Mwananafunzi akamilishe vifungu kwa kutumia -ake na – ao km Kalamu ______ (kalamu yake)- Kalamu ______ (Kalamu zao); kitabu ______ (Kitabu chako) – Kitabu ______(Vitabu vyao). Mwanafunzi atunge sentensi kwa kutumia –ake na – ao |
Mwalimu awasikilize wanafunzi wakiongea kuhusu vitu vyao wenyewe. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 32-33 |
|
|
2 |
Miezi ya Mwaka. |
Sauti mbili tofauti zinazotam kwa pamoja. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua sauti mbili zinazotamkwa pamoja ili kuimarisha matamshi bora kutamka sauti lengwa ili kuimarisha matamshi bora kusoma silabi za sauti lengwa ili kuimarisha usomaji |
Ni sauti zipi unazojua kutamka? Unajua kusoma herufi zipi? |
Mwanafunzi atambue sauti mb, nj na ng katika maneno. Mwanafunzi amsikilize mwalimu akitamka silabi zinazotokana na sauti lengwa kisha atamke. Pamoja na mwalimu na baadaye atamke akiwa pekee, wawili na darasa zima. Mifano ya silabi hizi ni: mba, mbe, mbi, nja, nje, nji, nga, nge na ngi. Mwanafunzi aweza kutumia vifaa vya ki teknolojia kama vile papaya, tarakilishi, projekta na kipazasauti |
Mwalimu asikie mifano kutoka kwa wanafunzi kuhusu sauti mbili zinazotamkwa pamoja. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 34-35 |
|
|
3 |
Msamiati |
Majina ya miezi |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua miezi ya mwaka ili kuimarisha stadi ya kuzungumza kusoma majina ya miezi ya mwaka ili kuimarisha usomaji bora |
Je, unajua majina yapi ya miezi? |
Mwanafunzi asome majina ya miezi ya mwaka ipasavyo kwa kutumia kadi za maneno. Wanafunzi waweza kukariri mashairi yanayohusu miezi ya mwaka. Mwanafunzi aweza kuimba nyimbo zinazohusu miezi ya mwaka. Mwanafunzi aandike majina ya miezi ya mwaka. |
Mwalimu awasikilize wanafunzi wakitaja baadhi ya majina ya miezi wanayoijua. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 39 |
|
9 |
1 |
Msamiati. |
Majina ya miezi. |
Kuandika majina ya miezi ya mwaka kwa mfuatano ili kujenga uandishi bora. Kutumia majina ya miezi katika sentensi ili kujenga ubunifu. Kuchangamkia majina ya miezi katika mawasiliano ya kila siku. |
Je, ulizaliwa mwezi gani?
|
Mwanafunzi aandike majina ya miezi ya mwaka. Wanafunzi waweza kushirikishwa katika kupanga upya majina miezi ya mwaka yaliyoparaganywa. Mwanafunzi atunge sentensi akitumia majina ya miezi ya mwaka. Mwanafunzi aweza kuonyeshwa vibonzo vikitaja miezi ya mwaka na kuelezea matukio tofauti ya mwaka. |
Mwalimu awaangalie wanafunzi wakiandika majina ya miezi katika daftari zao. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 40 |
|
|
2 |
Msamiati. |
Tarakimu 51-100. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze; Kutambua nambari 51-100 kwa maneno ili kuimarisha stadi ya kuzungumza. Kusoma nambari 51100 kwa maneno ili kuimarisha usomaji bora. |
Unaweza kuandika nambari zipi? |
Mwanafunzi asome majina ya nambari 51100 Wanafunzi waweza kupatiwa kadi za nambari 51-100 na majina yake ili kuziambatanisha katika makundi. Mwanafunzi aandike nambari 51-100. Wanafunzi waweza kushirikishwa kupanga upya majina yaliparaganywa ya nambari 51-100. |
Mwalimu awasikilize wanafunzi wakitaja nambari hamsini hadi mia moja. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 41 |
|
|
3 |
Kusikiliza na Kuzungumza . |
Masimuli zi. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua majina ya miezi ya mwaka kwa Kiswahili ili kuimarisha mawasiliano kutaja miezi ya mwaka kwa Kiswahili ili kuimarisha stadi ya kuzungumza |
Unajua miezi gani ya mwaka? Je, ulizaliwa mwezi gani? |
Mwanafunzi ataje miezi ya mwaka. Mwanafunzi aweza kuelezea mambo yanayofanyika miezi fulani kv kufungua shule mwezi wa Januari, kufunga shule mwezi wa Aprili. Mwanafunzi asimulie kuhusu matukio katika miezi mbalimbali k.v. kuzaliwa, shehere za kidini na kitaifa. Mwanafunzi aweza kuimba nyimbo na kukariri mashairi kuhusu miezi ya mwaka. |
Mwalimu awasikilize wanafunzi wakimueleza kuhusu mwezi waliozaliwa. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 44 |
|
10 |
1 |
Kusoma: |
Hadithi. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kufahamu hadithi aliyoisoma na aliyosomewa kuhusu miezi ya mwaka ili kupata ujumbe kuchangamkia kusoma hadithi katika maisha ya kila siku |
Je, waweza kukumbuka nini ulichosoma au kusomewa? |
Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi aliyosoma. Mwanafunzi atoe muhtasari wa hadithi aliyosoma au kusomewa. |
Mwalimu asikilize wanafunzi wakieleza hadithi aliyowasomea. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 47 |
|
|
2 |
Kuandika |
Kusikiliza na kuzungu mza. |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kuandika kisa kifupi kwa hati nadhifu kulingana na mada ili kujenga stadi ya uandishi Kufurahia uandishi wa visa tofauti ili kuimarisha mawasiliano andishi. |
Je, ni mambo yapi yanayofaa kuzingatiwa unapoandika kisa? Je, unaweza kuandika kisa kipi kuhusu jambo ulilofanya katika mwezi fulani wa mwaka? |
Mwanafunzi apewe hadithi yenye mapengo ajaze kwa maneno mwafaka Mwanafunzi aeleze yaliyo muhimu katika uandishi k.v. mwandiko nadhifu, maudhui, mtiririko n.k. Mwanafunzi asome kielelezo cha kisa kilichoandikwa. Wanafunzi waweza kuandika kisa kifupi wakiwa wawili wawili |
Mwalimu awaangalie wanafunzi wakiandika kisa kifupi kwa hati nadhifu. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 49 |
|
|
3 |
Sarufi. |
Matumizi ya Kikomo |
Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze; Kutambua matumizi ya kikomo (.) katika kuimarisha mawasiliano kuakifisha sentensi kwa kutumia kikomo (.) katika kuimarisha uandishi bora kuzingatia kikomo (.) anaposoma kifungu na sentensi ili kuimarisha usomaji bora kuthamini matumizi ya kikomo (.) katika mawasiliano. |
Unajua alama zipi za kuakifisha? Je, kikomo (.) huwekwa wapi katika sentensi? |
Mwanafunzi asome sentensi zenye kikomo (.) katika vikundi Mwanafunzi aakifishe sentensi fupi kwa kutumia kikomo (.). Mwanafunzi aandike sentensi ukitumia kikomo (.). |
Mwalimu awasikilize wanafunzi wakieleza jinsi wanavyotumia kikomo. |
Mwanafunzi Tarakilishi Kiswahili Dadisi Gredi ya tatu uk, 50-51 |
|
Kiswahili Schemes - Grade 3 Schemes of Work Term 1 2023
Published in
Grade 3 Schemes of Work Term 1 2023
Tagged under
Leave a comment
Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.