Kiswahili Schemes - Grade 2 Schemes of Work Term 3 2023

Rate this item
(2 votes)

WIKI

KIPINDI

MADA

MADA NDOGO

MATOKEO MAALUM YANAYOTOKEA

MASWALI DADISI

MAPENDEKEZO YA SHUGLI ZA UFUNZAJI

KAZI YA ZIADA

NYEZO

MAONI

1

1

Kuandika

Sauti na majina ya Kiswahili sh, th

kutambua sauti za herufi mbili katika kuimarisha matamshi bora kutamka sauti za Kiswahili za herufi mbili katika kuimarisha matamshi bora kusoma silabi za sauti zinazoundwa kutokana na sauti mbili ili kuimarisha usomaji

Je, ni maneno kama gani ambayo yana sauti /sh /na /th /?

Mwanafunzi atambue sauti /sh/na /th/ katika maneno

Mwanafunzi asikilize sauti lengwa ikitamkwa na mwalimu kisha atamke pamoja na mwalimu na mwishowe atamke akiwa peke yake, wawili na kama darasa nzima.

Mwanafunzi aweza kutumia vifaa vya kiteknolojia kama vile papaya, tarakilishi na projekta kusikiliza sauti lengwa ikitamkwa.

Mwalimu asikilize wanafunzi wakitaja maneno ambayo yana sauti sh.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk147

 

 

2

Sarufi

Nafsi ya pili wakati uliopita

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua maneno na viambishi vinavyowakilisha nafsi ya pili wakati uliopita ili kuimarisha mawasiliano kusoma vifungu vya maneno yanayoashiria nafsi ya pili wakati uliopita ili kuimarisha usomaji

Je, unatumia neno gani kumzungumzia mwenzako aliye karibu?

Mwanafunzi atumie nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi katika mazungumzo. Mwanafunzi atumie nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi katika sentensi.

Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia maneno na viambishi vinavyowakilisha nafsi ya pili wakati uliopita kama vile, wewe, u, li, nyinyi na m hali ya umoja na wingi

Mwalimu asikilize wanafunzi wakitaja maneno yaliyo katika nafsi ya pili wakati uliopita.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk148

 

 

3

kusoma

Alfabeti ya kiswahili

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua alfabeti ya Kiswahili ili kuimarisha usomaji kusoma alfabeti ya Kiswahili kwa mfuatano ufaao katika kuimarisha matumizi ya kamusi baadaye

Je, lugha ya Kiswahili ina herufi ngapi?

Je, ni herufi gani  unazoweza kusoma?

Mwanafunzi asome alfabeti ya Kiswahili kwa mfuatano: a, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, l, m, n, ng’, ny, o, p, r, s, sh, t, th, u, v, w, y, z.

Mwanafunzi aweza kusoma alfabeti kwenye chati.

Mwanafunzi aweza kuimba wimbo wa alfabeti.

Mwalimu asikilize wanafunzi wakitaja alfabeti za Kiswahili.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk151

 

2

1

msamiati

Kusikiliza na kuzungumza

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua msamiati ambao hutumiwa katikahali ya anga ili kuelezea hali ya anga ifaavyo kutambua hali ya anga ya siku husika ili kuimarisha mawasiliano

Je, ni vipi unavyoweza kuelezea upepo?

Mwanafunzi atoe maana ya msamiati unaohusu hali ya anga.

Mwanafunzi atunge sentensi sahihi akitumia msamiati unaohusu hali ya anga kama vile upepo, jua, mvua na mawingu.

Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha hali mbalimbali za anga.

Mwalimu asikilize msamiati wa hali ya anga kutoka kwa wanafunzi.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk152-153

 

 

2

sarufi

Matumizi ya nafsi ya pili wakati uliopita.

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua maneno na viambishi vinavyowakilisha nafsi ya pili wakati uliopita ili kuimarisha mawasiliano kusoma vifungu vya maneno yanayoashiria nafsi ya pili wakati uliopita ili kuimarisha usomaji

Je, unatumia neno gani kumzungumzia mwenzako aliye karibu?

Mwanafunzi atumie nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi katika mazungumzo.

Mwanafunzi atumie nafsi ya pili wakati uliopita hali ya umoja na wingi katika sentensi.

Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia maneno na viambishi vinavyowakilisha nafsi ya pili wakati uliopita kama vile, wewe, u, li, nyinyi na m hali ya umoja na wingi.

Mwalimu awape wanafunzi zoezi.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk155-156

 

 

3

kusoma

Safari ya jangwani

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua picha za kuonyesha hali ya anga ili kuimarisha ufahamu kutambua maneno yanayohusiana na hali ya anga ili kuimarisha usomaji

Je, ni hadithi zipi ambazo umewahi kusoma?

Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye hadithi.

Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.

Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.

Mwalimu awasikilize wanafunzi wakisoma.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk157-158.

 

3

1

Msamiati

Hali ya anga

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua msamiati ambao hutumiwa katika hali ya anga ili kuelezea hali ya anga ifaavyo kutambua hali ya anga ya siku husika ili kuimarisha mawasiliano

Je, ni vipi unavyoweza kuelezea upepo?

Mwanafunzi atoe maana ya msamiati unaohusu hali ya anga.

Mwanafunzi atunge sentensi sahihi akitumia msamiati unaohusu hali ya anga kama vile upepo, jua, mvua na mawingu.

Mwanafunzi aweza kutazama video inayoonyesha hali mbalimbali za anga.

Mwalimu asikilize misamiati kuhusu hali ya anga kutoka kwa wanafiunzi.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk159-160

 

 

2

sarufi

Matumizi ya hili na haya

kuandika sentensi zinazojumuisha hili na haya katika kuimarisha uandishi Kuchangamkia matumizi ya huyo na hayakatika maawasiliano.

Unatumia neno gani kuuliza swali kuhusu mwenzako?

Mwanafunzi aandike sentensi zinadhihirisha matumizi ya hili na haya

Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwa kutumia huyo na hili

Mwanafunzi aigize vitendo vya kuwaashiria watu mbalimbali kwa kutumia hili na haya

Mwalimu awape wanafunzi zoezi .

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk161

 

 

3

shairi

Giza mchana

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua picha za kuonyesha hali ya anga ili kuimarisha ufahamu kutambua maneno yanayohusiana na hali ya anga ili kuimarisha usomaji

Unakumbuka nani katika hadithi hiyo?

Mwanafunzi ajadili picha zilizojumuishwa kwenye shairi.

Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.

Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.

Mwalimu asikilize mwanafunzi akisoma shairi.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk162-163

 

4

1

Kuandika

Alphabeti ya kiswahili

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kubainisha irabu za Kiswahili ili kuelewa jinsi silabi huundwa kubainisha konsonanti za Kiswahili ili kuelewa jinsi silabi huundwa

Alfabeti ni nini?

Lugha ya Kiswahili ina konsonanti ngapi?

Mwanafunzi aweza kusoma alfabeti kwenye chati.

Mwanafunzi aweza kuimba wimbo wa alfabeti.

Mwanafunzi aweza kusikiliza alfabeti ya Kiswahili ikikaririwa kwenye vifaa vya kiteknolojia kama vile kinasasauti.

Mwalimu atazame wanafunzi akiandika alfabeti.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk164-165

 

 

2

masimulizi

Kusikiliza na

kuzungumza

kusimulia kuhusu hali mbalimbali za anga ili kuimarisha stadi ya kuzungumza kusikiliza masimulizi kuhusu hali ya anga ili kujenga umakinifu

Unaona nini katika chati ya hali ya anga?

Mwanafunzi aweza kutazama video inayohusu hali ya anga.

Wanafunzi waweza kupewa nafasi kwenda nje ya darasa na kujadiliana kuhusu hali ya anga wakati huo.

Mwanafunzi ashiriki katika majadiliano kuhusu hali za anga.

Mwalimu asikilize masimulizi ya wanafunzi kuhusu hali ya anga.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk166

 

 

3

Kusoma

Siku ya mvua

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kusikiliza hadithi za mwalimu kuhusu hali ya anga ili kujenga stadi ya kusoma na kusikiliza kufahamu hadithi aliyoisoma kuhusu hali ya anga ili kupata ujumbe

Unakumbuka nani katika hadithi hiyo?

Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kwa kutumia tarakilishi na projekta.

Mwanafunzi asome hadithi kutoka kwa jitabu mbele ya darasa.

Mwanafunzi aweza kusoma hadithi kutoka kwa kitabu cha hadithi.

Mwalimu awasikilize wanafunzi wakisoma hadithi.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk167

 

5

1

Lishe bora

Kusoma

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua vyakula vinavyofaa mwili ili kuimarisha stadi ya kuzungumza

kuzungumzia juu ya chakula anachokipenda ili kuimarisha mazungumzo

Unapenda kula chakula gani?

Chakula unachokila husaidiaje mwili

Mwanafunzi ataje baadhi ya vyakula kwa kuonyeshwa michoro na vyakula halisi.

Wanafunzi wajadiliane

kuhusu umuhimu wa vyakula mbalimbali k.m. vinavyompa mtu nguvu,

Mwalimu asikilize umuhimu wa lishe bora kutoka kwa wanafunzi.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk169-170

 

 

2

Sarufi

Matumizi ya

hiki na hivi

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua matumizi ya hiki na hivi katika kuimarisha mawasiliano kutumia hiki na hivi katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano

kusoma vifungu vinavyojumuisha hiki na hivi katika kuimarisha stadi ya kusoma

Ni nini wingi wa hiki?

Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwenye vifungu au sentensi zinazojumuisha hiki na hivi

Mwanafunzi aonyeshe vitu mbalimbali kama vile vyakula ili kuvitungia sentensi katika vikundi k.m. Chakula hiki – vyakula hivi.

Mwalimu asikilize matumizi ya hiki

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk170-171

 

 

3

Msamiati

Vitamin na proteni

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua vyakula vinavyofaa mwili ili kuimarisha stadi ya kuzungumza

kuzungumzia juu ya chakula anachokipenda ili kuimarisha mazungumzo

Chakula unachokila husaidiaje mwili?

Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu chakula kinachodhuru afya k.m. vibanzi, biskuti

Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akisimulia kuhusu lishe bora na madhara ya vyakula vinavyodhuru afya

Mwalimu awape wanafunzi kazi ya ziada.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk183

 

6

1

kusoma

Mashidano ya riadha

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kusoma hadithi kwa mtiririko ufao ili kuimarisha stadi ya kusoma

kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa ili kuelewa ujumbe katika hadithi

kuchangamkia kusoma hadithi ili kuendelea kujenga stadi ya kusoma.

Ni hadithi ipi iliyokufurahisha zaidi?

Mwanafunzi atabiri kitakachotokea kwenye hadithi.

Mwanafunzi afahamu matumizi ya msamiati uliotumika kwenye hadithi.

Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi, asome pamoja na mwalimu kisha asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi.

Mwalimu awasikilize wanafunzi wkisoma.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk188-18

 

 

2

Msamiati

Matumizi ya hiki na hivi

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua matumizi ya hiki na kuimarisha mawasiliano kutumia hiki na hivi katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano

kusoma vifungu vinavyojumuisha hiki na hivi katika kuimarisha stadi ya kusoma hivi katika

Ni nini wingi wa hiki?

Mwanafunzi aonyeshe vitu mbalimbali kama vile vyakula ili kuvitungia sentensi katika vikundi k.m. chakula hiki – vyakula hivi.

Mwanafunzi aweza kupewa vifungu vyenye mapengo wakamilishe kwa kutumia hiki na hivi wakiwa wawili wawili k.m. chakula (hiki), vyakula (hivi).

Mwalimu awape wanafunzi zoezi

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk185

 

 

3

Kusoma

Faida ya chakula bora

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kuzungumzia juu ya chakula kinachodhuru afya ili kuelewa madhara ya vyakula hivyo

kusikiliza masimulizi kuhusu lishe bora ili kujenga stadi ya kusikiliza

Chakula unachokila husaidiaje mwili?

Mwanafunzi ashiriki katika mjadala kuhusu chakula kinachodhuru afya k.m. vibanzi, biskuti

Mwanafunzi aweza kumsikiliza mgeni mwalikwa akisimulia kuhusu lishe bora na madhara ya vyakula vinavyodhuru afya

Mwalimu awape wanafunzi faida ya chakula bora.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk186

 

7

1

Sarufi

Matumizi ya hiki na hivi

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua matumizi ya hiki na hivi katika kuimarisha mawasiliano kutumia hiki na hivi katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano

kusoma vifungu vinavyojumuisha hiki na hivi katika kuimarisha stadi ya kusoma

Unatumia neon gano kuomnyesheaukaribu wa kitabu, kifutio, kiatu na kijiti?

Mwanafunzi aweza kujaza mapengo kwenye vifungu au sentensi zinazojumuisha hiki na hivi

Mwanafunzi aonyeshe vitu mbalimbali kama vile vyakula ili kuvitungia sentensi katika vikundi k.m. Chakula hiki – vyakula hivi.

Mwalimu awape wanafunzi zoezi katika vikundi.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk190

 

 

2

msamiati

Vyakula vinavyodhuru afya

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutumia msamiati ulisomwa katika kutunga sentensi ili kuimarisha mawasiliano

kuthamini kula chakula kinachofaidi mwili ili kujikinga kutokana na madhara ya ukosefu wa lishe bora

Ni chakula kipi kinachofaidi mwili zaidi?

Ni chakula kipi kinachodhuru afya?

Mwanafunzi atazame kwenye vyombo vya kiteknolojia na kuvijadili picha za vyakula vinavyoashiria msamiati unaorejelewa.

Mwanafunzi asome majina mbalimbali ya vyakula kwenye kadi za maneno.

Mwanafunzi anakili kwenye daftari msamiati unaofunzwa.

Mwalimu awaelezee wanafunzi kuhusu chakula kinachodhuru afya.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk190-191

 

 

3

kusoma

Paka wangu

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze:

kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa ili kuelewa ujumbe

Kupenda kusoma hadithi kuhusu wanyama wa nyumbani ili kuendeleza usomaji.

Unakumbuka nini katika hadithi hiyo?

Mwanafunzi asikilize mwalimu anaposoma hadithi, asome pamoja na mwalimu kisha asome peke yake, wakiwa wawili wawili au katika vikundi.

Mwanafunzi aweza kusikiliza hadithi ikisomwa kupitia kinasa sauti.

Mwanafunzi athibitishe utabiri wake baada ya kusoma na kusomewa hadithi.

Mwalimu awaulize wanafunzi kuhusu mnyama wanaopenda.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk193-194

 

8

1

msamiati

Wanyama wa nyumbani

Kufikia mwisho  wa mada, mwanafunzi aweze: kutumia majina ya wanyama

katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano 

kutumia msamiati unaohusu utunzaji wanyama katika sentensi ili kujenga mapenzi ya kuwatunza wanyama wa nyumbani

Kwa nini unampenda mnyama huyo?

Mwanafunzi achore baadhi ya wanyama na kuandika majina yao.

Mwanafunzi aweza kuonyeshwa video ya utunzaji wa wanyama.

Mwanafunzi aweza kutazama michoro na picha za wanyama wa nyumbani na wanyama wakitunzwa.

Mwalimu awapatie wanafunzi kazi ya vikundi.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk197-198

 

 

2

Kusoma

Punda mweupe

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: Kusoma hadithi kwa mtiririko ufao ili kuimarisha usomaji kufahamu hadithi aliyosoma na kusomewa ili kuelewa ujumbe

Kupenda kusoma hadithi kuhusu wanyama wa nyumbani ili kuendeleza usomaji.

Unakumbuka nini katika hadithi hiyo?

Mwanafunzi aweza kutazama video ya mtu au mtoto akisoma hadithi husika kwa ufasaha kisha aige usomi ule.

Mwanafunzi ajibu na kuuliza maswali kuhusu hadithi aliyosoma na kusomewa.

Mwanafunzi aweza kusimulia hadithi kutokana na picha alizopewa kuhusu wanyama wa nyumbani

Mwalimu awasikilize wanafunzi wakisoma ufahamu.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk206-210

 

 

3

sarufi

Matumizi ya hili na haya

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutambua matumizi ya hili na haya ili kuimarisha mawasiliano kutumia hili na haya katika sentensi sahihi ili kuimarisha mawasiliano kusoma vifungu vinavyojumuisha matumizi ya hili na haya ili kujenga usomaji kuandika vifungu

Unatumia neno gani kuonyeshea tunda lililo karibu nawe?

Unatumia neno gani kuonyeshea dawati lako?

Mwanafunzi asome vifungu vyenye matumizi ya hili na haya kama vile embe hili – maembe haya; dawati hili – madawati haya; jani hili – majani haya.

Wanafunzi waweza kujaza mapengo kwa kutumia hili na haya.

Mwanafunzi aonyeshwe vitu mbalimbali kama vile tunda kwa kurejelea hili na haya kwa mfano: tunda hili – matunda haya; embe hili –

Mwalimu awape wanafunzi zoezi la kufanya.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk219-222

 

 

 

Msamiati na masimulizi

Kusikiliza na kuzungumza

Kufikia mwisho wa mada, mwanafunzi aweze: kutumia majina ya wanyama katika sentensi ili kuimarisha mawasiliano kutumia msamiati unaohusu utunzaji wanyama katika sentensi ili kujenga mapenzi ya kuwatunza wanyama wa nyumbani 

Kuthamini umuhimu wa kuwatunza wanyama wa nyumbani.

Umuhimu wa wanyama n upi?

Mwanafunzi achore baadhi ya wanyama na kuandika majina yao.

Mwanafunzi aweza kuonyeshwa video ya utunzaji wa wanyama.

Mwanafunzi aweza kutazama michoro na picha za wanyama wa nyumbani na wanyama wakitunzwa.

Mwanafunzi asimulie kuhusu mnyama anayapenda.

Tarakilishi

Mwalimu

Mwanafunzi

Nyota ya Kiswahili uk215-221

 

9

TATHMINI

Read 408 times Last modified on Wednesday, 15 February 2023 11:50

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.