Friday, 19 May 2023 13:49

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Opener Exams Term 2 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Kuna aina nyingi za simu. Simu ambayo hutumika sana ni simul ya mkononi. Simu ya mkononi huitwa rununu, rukono, simutamba au selula. Watu wengi sana hutumia simu siku hizi. Hii ni tofauti na kitambo ambapo watu waliotumia simu walikuwa wachache. Kazi kubwa ya simu ya mkononi ni mawasiliano. Mawasiliano ni kupitisha. ujumbe kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine. Faida ya mawasiliano ya kuzungumza kwa simu ni kuwa hata watu wasiojua kusoma na kuandika huweza kuwasiliana.
Simu pia huweza kutumika kuandika arafa. Arafa ni ujumbe mfupi unaoandikwa na kutumwa kutumia simu. Vilevile, simu hutumika kucheza muziki. Nyimbo mbalimbali huchezwa kwa kutumia simu. Hata hivyo, ni vyema. kuwa mwangalifu unaposikiliza nyimbo kwa kutumia simu. Unapotumia vidude viwekwavyo masikioni wakati wa kusikiliza muziki, hakikisha kuwa sauti ni ya kiwango cha chini. Kusikiliza muziki wa sauti ya juu kwa muda mrefu ukitumia vidude vya masikioni huweza kuyaharibu masikio. Ni muhimu mno kuchagua nyimbo zenye mafunzo mazuri. Baadhi ya nyimbo huwa na maneno machafu yasiyofaa. Nyimbo kama hizo hazifai kusikilizwa hata kidogo.
Kunao watu ambao husikiliza redio kupitia simu. Watu hao husikiliza taarifa za habari na mambo mengine kupitia redio iliyo kwenye simu. Simu pia hutumika kupiga hesabu kwa kutumia kikokotoo, kupiga picha na kucheza video. Hakika, simu ina umuhimu mkubwa katika maisha. Hata hivyo, simul pia ina madhara yake. Kutumia simu kila wakati kunaleta shida mbalimbali. Kwa mwanafunzi, kutumia simu kila wakati humpotezea mwanafunzi huyo nafasi ya kufanya mambo muhimu. Mambo muhimu. kwa mwanafunzi ni kusoma na kufanya kazi za ziada.

  1. Gani si jina la simu ya mkononi kulingana na kifungu?
    1. runinga
    2. simutamba
    3. selula
    4. rukono
  2. Kwa nini watu wengi hununua simu za mkononi kulingana na kifungu?
    1. Ili wasikilize muziki
    2. Ili watazame video
    3. Ili wasikilize redio
    4. Ili wawasiliane na wenzao
  3. Kulingana na aya ya kwanza, ni kweli kuwa;
    1. Watu walio na simu si wengi mno
    2. Hata watu wasiojua kusoma na kuandika huwasiliana kwa kutumia simu
    3. Kitambo, watu wengi mno walikuwa na simu kuliko siku hizi
    4. Kazi pekee ya simu ya mkononi ni mawasiliano 
  4. Ukitaka kutumia simu kuwasiliana na mtu aliye na shida ya kusikia utafanya nini?
    1. Utamwandikia arafa
    2. Utampigia simu
    3. Utamwandikia barua
    4. Utatuma mtu aongee naye
  5. Kutumia vidude vya masikioni kusikiliza muziki wa sauti ya juu kwa muda mrefu. huweza kumfanya mtu akawa;
    1. kipofu
    2. kiziwi
    3. bubu
    4. kiwete
  6. Kulingana na ufahamu, ni kweli kuwa;
    1. Simu haina manufaa yoyote
    2. Simu haina madhara yoyote
    3. Simu ina faida na madhara
    4. Simu ina madhara pekee
  7. Simu hutumika kufanya mambo yafuatayo. isipokuwa;
    1. kuwasiliana
    2. kusafiri
    3. kupiga picha
    4. kusikiliza muziki
  8. Aya ya mwisho inaeleza kuwa jambo muhimu kwa mwanafunzi ni kufanya nini?
    1. kucheza na wenzake
    2. kutumia rununu
    3. kusoma na kufanya kazi ya ziada
    4. kuwasaidia wazazi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Simba ndiye aliyekuwa mfalme wa mwituni. Wanyama wote walifurahia kuongozwa na simba. Siku moja Simba alitangaza kwamba alikuwa mgonjwa mahututi na kwamba alikaribia kuaga dunia. Hivyo aliwaalika wanyama wote waende nyumbani kwake kumwona na kusikia maneno yake ya mwisho. Hali hiyo iliwafanya wanyama wote wawe na woga kama kunguru.Wanyama wengi waliingiwa na wasiwasi kwa sababu walimpenda sana mfalme wao na hawakutaka afe.
Hivyo mbuzi alienda kwenye pango alimoishi Mfalme Simba ili kumjulia hali. Alisimama kwenye sehemu ya kuingilia pangoni na kusikiliza kwa muda mrefu. Kisha kondoo alikuja na akaingia pangoni moja kwa moja. Kabla hajatoka mwanafarasi naye alikuja kupokea ushauri wa mwisho wa mtalme, akaingia pangoni. Mbuzi alipoona kuwa wenzake hawakutoka nje, aliondoka. Baada ya muda mfupi simba alijitokeza nje akionekana kupata nafuu ya haraka, akaja kwenye lango lake la kuingilia pangoni ili apunge upepo wa nje. Alipopiga macho kushoto na kulia alimwona mbweha, akiwa amejiinamia akisubiri nje ya pango kwa muda mrefu.
"Kwa ini ewe mbweha hujaja ndani ya pango kutoa heshima zako za mwisho kwangu? Mbona unakaa tu apa nje ukicheza?" Simba alimwuliza.
"Nisamehe Bwana Mkubwa," Mbweha alijitetea, "ila katika kuja kwangu hapa nimegundua alama za nyayo za wanyama wengi ambao wamekwisha kukutembelea pangoni mwako; na nikichunguza kwa makini zaidi naona alama nyingi za kwato zikiingia ndani, na sioni zitokazo nje. Hadi hapo nitakapowaona wanyama waliokwishaingia pangoni mwako wakitoka nje, sitaingia. Ninaona ni heri nibaki huku huku nje kwenye uwazi na hewa safi.
Ujumbe ulipowafikia wanyama wengine, walimpeleka Simba mahakamani na kumshtaki. Simba alihukumiwa kifungo cha mwongo mmoja. Vilevile, alinyang'anywa mamlaka ya kuwa mfalme. Mbweha alichaguliwa kuwa kiongozi kwa kuwa alisema ukweli na kukomesha uovu uliokuwa ukiendelea.

  1. Simba alimaanisha nini aliposema kuwa
    'alikaribia kuaga dunia"?
    1. afya yake ilikuwa sawa
    2. halikuwa akihisi njaa
    3. alikuwa karibu kufa
    4. alikuwa karibu na dunia
  2. Ufahamu huu unaonyesha kuwa simba alikuwa mnyama mwenye;
    1. busara
    2. tamaa
    3. uchoyo
    4. ujanja
  3. Maneno 'woga kama kunguru' ni mfano wa; Tuulinde wetu mwili, kuwe maisha mazuri.
    1. nahaù
    2. kitendawili
    3. methali
    4. tashbihi
  4. Kwa nini mbweha hakuona nyayo za wanyama ambao walitoka nje?
    1. pengine alikuwa na shida ya macho.
    2. wanyama hao waliliwa na simba
    3. wanyama hao hawakujua njia ya kutoka nje
    4. wanyama walitoka mbweha akiwa ameangalia chini
  5. Mnyama gani aliyeelewa kuwa 'polepole ndiyo mwendo'?
    1. mbuzi
    2. chui
    3. mwanafarasi
    4. kondoo

Soma ubeti ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.
Kuwa nayo nzuri siha, ni jambo muhimu sana,
Hufanya tuwe na raha, tufanye mengi mapana,
Huondolea jeraha, leo vilevile jana,
Tuulinde wetu mwili, kuwe maisha mazuri

  1. Ubeti huo una mizani mingapi?
    1. 4
    2. 64
    3. 32
    4. 8
  2. Kina cha mwisho cha ubeti huu ni kipi?
    1. ha
    2. li
    3. ri
    4. na

Jaza nafasi zilizoachwa kwa jibu linalofaa zaidi.
Mwanafunzi ................16................... , awe mvulana au msichana ................17................... kuhakikisha kuwa anatia bidii katika masomo yake. Mwanafunzi ambaye ................18................... masomoni hufaulu wakati  ................19................... mtihani wake. Bidii si jambo la wakati  ................20...................  tu, la hasha! Ni jambo la kila wakati.

  1.                                  
    1. yoyote
    2. wowote
    3. yeyote
    4. lolote
  2.            
    1. hafai
    2. anafaa
    3. anafai
    4. wanafaa
  3.                                  
    1. anazembea
    2. anajilegeza
    3. anajitolea
    4. anafifia
  4.                            
    1. anapoufanya
    2. anapoifanya
    3. anapoyafanya
    4. anapomfanya
  5.                        
    1. umoja
    2. wamoja
    3. moja
    4. mmoja

Jibu maswali yanayofuata kulingana na maagizo.

  1. Tambua aina za vivumishi vilivyopigiwa mistari.
    Wanafunzi wale wamenunua madaftari mawili.
    1. kimilikishi, cha idadi
    2. kiashiria, cha idadi
    3. cha sifa, kimilikishi
    4. kiashiria, kimilikishi 
  2. Onyesha ukubwa wa;
    Ngamia wa mtoto amelala chini ya mti.
    1. Jigamia la jitoto limelala chini ya jiti.
    2. Kigamia cha kitoto kimelala chini ya kijiti.
    3. Gamia wa toto amelala chini ya jiti.
    4. Gamia la toto limelala chini ya jiti.
  3. Panga maneno yafuatayo jinsi yanavyofuatana kwenye kamusi.
    1. muhebi
    2. muhtasari
    3. muhula
    4. muhogo
      1. i, iv, iii, ii
      2. i, iv, ii, iii
      3. i, ii, iv, iii
      4. iii, ii, i, iv
  4. Chagua maneno mawili yenye maana sawa na 'figo'.
    1. nso, buki
    2. mtima, moyo
    3. kifua, kidari
    4. paji, panda
  5. Maelezo gani yaliyo sahihi kuhusu matumizi ya koloni?
    1. Hutumika kutanguliza orodha.
    2. Hutumika kuonyesha sauti zenye ving’ong’o.
    3. Hutumika mwanzoni mwa sentensi.
    4. Hutumika kuonyesha visawe.
  6. Onyesha wingi wa;
    Ukuta wenye ufa umeangukia ubua.
    1. Nyuta zenye nyufa zimeangukia mabua.
    2. Kuta zenye nyufa zimeangukia mabua.
    3. Kuta zenye nyufa zimeangukia bua.
    4. Nyuta zenye nyufa zimeangukia bua. 
  7. Tambua ishara itumikayo kwenye tarakilishi kuonyesha 'chapa koza'.
    1. U
    2. I
    3. B
    4. C
  8. Sentensi ifuatayo itaandikwaje katika kauli ya kutendewa?
    Mama amepika chakula cha mtoto.
    1. Chakula cha mtoto kimepikwa na mama.
    2. Mama amempikia mtoto chakula.
    3. Mtoto amepikiwa chakula na mama.
    4. Mama amepikiwa chakula na mtoto.
  9. Mpole ni kwa 'njiwa' kama vile mwaminifu ni kwa ...............................
    1. kunguru
    2. malaika
    3. chiriku
    4. mchana
  10. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
    Yule anatembea polepole.
    1. kivumishi, kielezi
    2. kiwakilishi, kielezi
    3. kivumishi, kiwakilishi
    4. kiwakilishi, kivumishi

INSHA

Andika insha ya masimulizi kuhusu mada ifuatayo.
SIKU YA MICHEZO SHULENI

MARKING SCHEME

swa adad

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Opener Exams Term 2 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students