COMPETENCY BASED CURICULUM
GREDI YA 5, MWISHO WA MUHULA WA 1
SHUGHULI ZA KISWAHILI
JINA....................................................SHULE............................................
ZOEZI 1: KUSOMA KWA UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha uyjibu swali la 1 hadi la 7
Mipango yote ya sherehe ya kuzaliwa kwa baba yangu ilikuwa imepangwa ikapangika.Ilikuwa siku ya tatu ya juma. Baba alikuwa akikamilisha miaka thelathini na tisa. Yeye hakuwa amekula chumvi nyingi kama alivyokuwa babaye Meishisana.
Mapochopocho ya vyakula mbalimbali yalikuwa yakinukia mezani na hata mekoni. Vyakula kama vile pilau, biriani , maandazi na vibanzi vilivutia sana machoni pa wageni watano waalikwa. Nilishangaa nilipomwona Bwana Kauleni akidondokwa na mate kwa sababu ya kuitamani keki yenyewe. Watu wengine ambao sikuwatambua kwa majina yao, walikuwa wameketi kitako sebuleni huku wamejipamba kweli kweli. Bila shaka wote walijawa na tabasamu nyusoni pao. Keki yenyewe ilikuwa tamu kama halua. Mimi mwenyewe nilihusika kwa kuwakaribisha marafiki zangu kwenye viti baada ya kuvipanga.
Maswali
- Je, kisa hiki kinahusu sherehe ya nani?
________________________________ - Sherehe yenyewe ilikuwa siku gani ya juma?
________________________________ - Mwandishi alitumia maneno, "hakuwa amekula chumvi nyingi." Je, hii inamaanisha nini ?
________________________________________________________________ - Wageni walikuwa wameketi kitako. Pigia mstari kielezi katika sentensi hii.
________________________________ - Je, sherehe hii ilihudhuriwa na wageni wangapi waalikwa?
________________________________ - Taja jina la babuye mwandishi.
________________________________ - Kifungu ulichokisoma kinahusu nini?
________________________________
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 8 hadi la 14.
Mwaka huu ulipoanza, sote tulifurahi kurudi katika shule yetu. Shule hiyo inajulikana kama Mematele. Ina wanafunzi elfu moja na mia mbili na mabasi sita. Mabasi yote ya shule hiyo yamepakwa rangi ya manjano.
Tulipowasili shuleni, tuliingia madarasani na kuketi kwenye viti vyetu. Mwalimu mmoja ambaye tulimpenda sana alingia darasani na kutuamkua, " Hamjambo wanafunzi " Nasi tukajibu, "Hatujambo
mwalimu Matunda. Shikamoo"
Kengele ilipopigwa tulielekea gwarideni Tulisimama wima tulipokuwa tukiimba wimbo wa taifa. Baadaye mwalimu alitukagua endapo kucha zetu zilikuwa safi. Mwalimu wetu alitushauri tuwe tukinywa maji mengi kila siku ili tuwe na afya njema.
MASWALI - Malizia sentensi hii
Mwaka huu ulipoanza sote tulifurahi
________________________________ - Mwandishi husomea katika skuli gani?
________________________________ - Shule ya mwandishi ina wanafunzi wangapi?
________________________________ - Mabasi ya shule katika nchi hii ya msimulizi yamepakwa rangl gani?
________________________________________________________________ - Salamu hamjambo hujibiwa hatujambo je, masalheri hujibiwa aje?
________________________________ - Ni nani aliwashauri wanagenzi kunywa maji mengi?
________________________________ - Kwa nini wanafunzi walishauriwa kunywa maji mengi?
________________________________
ZOEZI II:SARUFI
- Teua salamu ambayo haijaambatanishwa ipasavyo.
Habari ya jioni.... njema
Kwa heri..... ya kuonana
Alamsiki.... aleikum salaam
Makiwa .... unayo - Je, kati ya maneno haya katika kamusi, ni neno gani litakuwa la pili?
Muhubiri, Muhutasari, Muhula, Mtihani, Mshtakiwa ________________________________ - Mstatili huu una maneno matano ya nomino za vitenzi-jina. Je, ni neno lipi halifai kuwa hapa?
[Kulala, Kukimbia, Kalia, Kusoma, kutibiwa]
________________________________
Andika kwa wingi. - Mtoto aliacha dawati lake shuleni.
________________________________ - Mwalimu wangu huja mapema shuleni
________________________________
Chagua neno lifaalo kujaza nafasi. - Matata ___________nyanya samaki. (alibeba, alimbebea, alimbeba)
- Tulienda sokoni ___________tununue matunda. (ili, kwa sababu).
- Kamilisha methali hii. Asiyekujua ___________{akuthanini, hakuthamini, hakudhamini}
- Ni sentensi gani haijakanushwa vyema?
Tunaenda sokoni Hatuendi sokoni Mama yangu amechelewa Mama yangu hachelewi Walionana mwaka jana Hawakuonana mwaka jana. Juma ni mwanafunzi hodari Juma si mwanafunzi hodari - Nomino,"jua, lepe, jasho, joto na giza," hupatikana katika ngeli ya ___________
- Andika sentensi hii katika hali ya ukubwa
Mtoto wake anasoma _________________________________ - Je, sentensi hii iko katika wakati gani?______________________
Mlinzi mwenyewe analilinda rinda la mama. - ______________________(Karamu ,Ghulamu, Kalamu) ya arusi ilikuwa ya kupendeza sana.
- Siku hiyo ___________(pipi,vivi, bibi) arusi alivaa gauni jeupe pe pe pe.
Jaza mianya iliyoachwa kwa maneno yafaayo kutoka kwenye mabano (Shule, mwiko, vitunguuu,, sabuni) - Mama alipokuwa akisonga ugali alitumia______________________
- Idadi ya wanafunzi katika ___________yetu ni elfu mbili.
INSHA
Andika insha kuhusu: MWALIMU NIMPENDAYE
MAAKIZO
- Sherehe ya kuzaliwa ya baba( ya mwandishi)
- siku ya tatu
- Hakuwa mzee sana
- kitako
- watano
- Meishisana
- sherehe ya siku ya kuzaliwa
- kurudi katika shule yetu
- Mematele
- elfu moja mia mbili
- manjano
- aheri
- mwalimu
- wawe na afya njema
- alamsiki
- mtihani
- kalia
- watoto waliacha madawati yao shuleni
- walimu wetu huja mapema shuleni
- alimbebea
- ili
- hakudhamini
- mama yangu amechelewa
- LI-YA
- jitoto lake linasoma
- wakati uliopo
- karamu
- bibi
- mwiko
- shule
Download Kiswahili Activities - Grade 5 End Term 1 Exam 2021 SET 2.
Tap Here to Download for 30/-
Get on WhatsApp for 30/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students