Fasihi Andishi - Kiswahili Fasihi Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

  • Fasihi Andishi ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno yaliyoandikwa kupitisha ujumbe. Ni sanaa inayopitishwa kwa njia ya maandishi


Tanzu za Fasihi Andishi

  • Kuna tanzu nne kuu za Fasihi Simulizi:
    1. Hadithi Fupi - kazi andishi ya fasihi isiyokuwa ndefu sana
    2. Riwaya - kazi andishi ya fasihi ambayo huwa ndefu kuliko hadithi fupi
    3. Tamthilia- kazi andishi ya fasihi inayowasilisha mchezo wa kuigiza
    4. Mashairi - mashairi yaliyochapishwa huwa chini ya fasihi andishi.

Riwaya

  • Riwaya ni kazi ya fasihi andishi ambayo huwa ndefu na aghalabu riwaya moja hujaza kitabu kizima.
  • Riwaya huwa na wahusika wengi na huangazia mawazo kadhaa. Aidha, riwaya hufanyika katika mazingira mbalimbali na aghalabu huchukua muda mrefu ikilinganishwa na hadithi fupi.

Aina za Riwaya

  • Kunazo aina kadhaa za Riwaya katika Fasihi Andishi:
    • Riwaya sahili - visa vyake husimuliwa moja kwa moja na huwa rahisi kueleweka
    • Riwaya changamano - hii ni riwaya ambayo huhitaji kusomwa kwa makini ili kueleweka.
      - Aghalabu huwa na maudhui mengi na wahusika wengi ambao wanachangia katika tatizo kuu katika riwaya hiyo. Hujengwa kwa taharuki ili kuwavutia hadhira kutazamia jinsi tatizo kuu litakavyotatuliwa. Hutumia mbinu za taharuki na visengere nyuma/mbele.
    • Riwaya ya kibarua - hutumia muundo wa barua kuwasilisha ujumbe wake.
    • Riwaya kiambo - huhusisha maswala ya kawaida katika jamii

Mifano ya Riwaya

  • Kidagaa kimemwozea
  • Siku Njema
  • Utengano
  • Mwisho wa Kosa
  • Chozi la Heri

 

Tamthilia

  • Tamthilia au tamthiliya ni sanaa ambayo huwasilisha mchezo wa kuigiza kwa njia ya maandishi.
  • Majina ya wahusika huandikwa katika upande wa kushoto, kisha koloni, halafu hufuatiwa na maneno halisi yaliyotamkwa na mhusika huyo.

Aina za Tamthilia

  • Kunazo aina kadhaa za tamthilia katika fasihi andishi:
    1. Tamthilia Cheshi/Komedia - ni mchezo wa kuchekesha. Maudhui yake huundwa kwa lengo la kutumbuiza hadhira.
    2. Tamthilia Simanzi/Trejedia - ni mchezo uliojaa huzuni, mikasa, mikosi, visa vya kutisha na aghalabu baadhi ya wahusika wakuu hufa.
    3. Tamthilia Simanzi-Cheshi/Trejikomedia - ni mchezo wenye visa vya kuhuzunisha lakini pia unawasilisha kwa njia ya kuchekesha. Aghalabu wahusika hutumia kejeli kuchekesha hadhira ijapokuwa kuna shida fulani inayowakabili. Baadhi ya wahusika wakuu hukumbwa na mikasa. Mfano: Kifo Kisimani (na Kithaka Wa Mberia)
    4. Tamthilia Tatizo - ni mchezo wa kuigiza ambapo wahusika huwa na tatizo/shida kuu wanalotaka kulitatua. Tamthilia hii aghalabu hutumia mbinu ya taharuki ili kuwafanya hadhira wawe makini ili kuona jinsi tatizo hilo litakavyoishia.
    5. Tamthilia ya Domestiki Drama - ni mchezo unaoangazia maisha ya kawaida ya watu kama vile familia, urafiki, ndoa n.k
    6. Tamthilia ya Melodrama - ni mchezo ambao husisitiza sifa za wahusika kwa kuunda wahusika kuunda wahusika wenye sifa zilizopigiwa chuku na zisizobadilika. Tamthilia hizi huundwa kwa namna inayowafanya hadhira wawapende wahusika fulani na wawachukie wahusika wengine.
      Kwa mfano:
      • Shujaa ambaye hushinda kila mara
      • Wahusika wabaya ambao hubakia wabaya kutoka mwanzo hadi mwishi
      • Wahusika wazuri ambao hufanya vitendo vizuri kutoka mwanzo hadi mwisho
      • Wapenzi ambao hata wakitenganishwa bado watapendana
      • Aghalabu huishia kwa raha mustarehe

Mifano ya Tamthilia

  1. Kifo Kisimani
  2. Shamba la Wanyama
  3. Mstahiki Meya
  4. Kigogo


Sifa za Fasihi Andishi

  1. Hupitishwa kwa njia ya maandishi
  2. Ni mali ya mtu binafsi
  3. Haiwezi kubadilishwa
  4. Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa


Umuhimu wa Fasihi Andishi

  1. Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi
  2. Kukuza lugha
  3. Kuburudisha
  4. Kuelimisha
  5. Kukashifu tabia zisizoandamana na maadili ya jamii
  6. Kuonya, kuelekeza, kunasihi


Uchambuzi wa Fasihi Andishi

- Unapochambua kazi ya fasihi andishi zingatia:

  1. Aina ya Kazi Andishi
    • Tambua aina au kipera cha kazi andishi ikiwa ni riwaya, hadithi fupi au tamthilia
  2. Wahusika
    • Tambua wahusika katika kazi hiyo ya fasihi
    • Fafanua sifa za kila mhusika kwa kutumia vivumishi au virai vivumishi vinavyolingana na hulka za mhusika huyo.
    • Aidha, unapaswa kuyakinisha sifa hizo kwa kutolea mifano kutoka kwenye hadithi
    • Taja aina ya wahusika
  3. Maudhui na Dhamira
    • Maudhui - ni nini kinachofanyika?
    • Dhamira - lengo/kusudi la kazi hiyo ni nini?
  4. Mandhari
    • Hadithi inafanyika katika mazingira gani?
    • Mazingira hayo yanachangia vipi katika kisa hicho au sifa za wahusika?
    • Msanii ameunda hali gani? (hisia, n.k)
  5. Mbinu za Lugha
    • Taja kwa kutolea mifano, fani za lugha zilizotumika ili kuifanya lugha iwe ya kuvutia zaidi
    • Fafanua mbinu za sanaa zilizotumika na utaje mifano mwafaka


Wahusika Katika Fasihi Andishi

  • Fasihi Andishi hutumia wahusika wanadamu, kinyume na Fasihi Simulizi ambayo hutumia wahusika changamano (watu, wanyama, mazimwi n.k). Kunazo aina kadhaa za wahusika katika kazi ya fasihi andishi kama vile: tamthilia, riwaya na hadithi fupi.

Aina za Wahusika

  1. Wahusika Wakuu hawa ni wahusika ambao wanahusishwa na takribani visa vyote katika riwaya/tamthilia. Wahusika huhusishwa kutoka mwanzo hadi mwisho. Aghalabu mhusika mkuu hafi isipokuwa katika trejedia/simanzi au hufa kifo cha ushujaa.
  2. Wahusika Wasaidizi hawa ni wahusika wanaosaidia kujenga mhusika mkuu. Hutokeza mara nyingi katika hadithi. Wahusika wasaidizi wanaweza kuwa na visa vyao. Kwa mfano marafiki na aila za wahusika wakuu.
  3. Wahusika Wadogo ni wahusika ambao wanafanya kazi ndogo sana katika fasihi kama vile kujenga maudhui au mandhari. Wahusika hawa wakitolewa, riwaya/tamthilia inaweza kuendela bila kubadilika sana. Kwa mfano mwenye duka ambalo mhusika alinunua kitu fulani.
  4. Wahusika Bapa hawa ni wahusika wasiobadilika kutoka mwanzo hadi mwisho. Kwa mfano, mhusika mbaya anabakia kuwa mbaya kutoka mwanzo hadi mwisho. Sifa za wahusika bapa huweza kutambulika mwanzoni mwa hadithi/riwaya. Wahusika bapa hawawakilishi sifa halisia za binadamu. Nia yao ni kujenga tabia moja tu.
    - Kuna aina mbili za wahusika bapa:
    • Wahusika bapa-sugu - huoenyesha msimamo wao kulingana na masimulizi ya msanii.
    • Wahusika bapa-vielelezo - msimamo wao hutambulika kulingana na majina yao. Msanii hutumia mbinu ya majazi au lakabu kuwapatia wahusika majina yanayolingana na sifa zao. Kwa mfano: Mhusika Rehema ni mwenye huruma na neema kutoka mwanzo hadi mwisho.
  5. Wahusika Duara mhusika duara hubadilika kitabia katika fasihi. Hawana msimamo thabiti.
    - Hubadilika kulingana na maudhui na mazingira. Kwa mfano, msichana aliyeanza kama mpole na mwadilifu anapobadilika na kuwa mtovu wa nidhamu, kahaba na asiyeshirikiana na mtu yeyote.
  6. Wahusika Wafoili huwa katikati ya wahusika bapa na wahusika duara. Wanaweza kuchukua msimamo fulani katika maswala fulani lakini pia wanaweza kubadilisha msimamo huo wakati mwingine kulingana na hali. Wahusika hawa hutegemea wahusika duara na wahusika bapa ili kutoa sifa zao. Kwa mfano, wakiishi na mhusika bapa, wanaweza kuchukua msimamo wa mhusika huyo lakini wakikaa sana na mhusika mwengine, wanabadilika. Wahusika hawa aghalabu huwakilisha uhalisi wa binadamu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Fasihi Andishi - Kiswahili Fasihi Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest