Fasihi Simulizi - Kiswahili Fasihi Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

  • Fasihi Simulizi ni utanzu wa fasihi ambao unawakilisha sanaa ya lugha inayopitishwa kutoka kwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya maneno/masimulizi ya mdomo.


Tanzu za Fasihi Simulizi

Tanzu ni aina za tungo zenye muundo uliokaribia kufanana

  • Hadithi/Ngano
  • Ushairi Simulizi
  • Maigizo
  • Semi
  • Mazungumzo

Vipera vya Tanzu za Fasihi Simulizi

  • Kipera ni utungo wa fasihi simulizi unaowasilishwa mbele ya watu.

HADITHI/NGANO

  • Khurafa
  • Hekaya
  • Mighani/Visakale
  • Usuli/Visaviini
  • Visasili
  • Hadithi za Mtanziko
  • Hadithi za Mazimwi

USHAIRI SIMULIZI

  • Nyimbo
  • Maghani
  • Ngonjera
  • Mashairi Mepesi

 

SEMI

  • Methali
  • Vitendawili
  • Mafumbo
  • Vitanza Ndimi na Vichezea Maneno
  • Misemo na Nahau
  • Lakabu
  • Misimu

MAIGIZO

  • Michezo ya Kuigiza
  • Michezo ya Watoto/Chekechea
  • Ngomezi
  • Miviga
  • Vichekesho
  • Majigambo/Vivugo
  • Maonyesho

MAZUNGUMZO

  • Malumbano ya Utani
  • Mazungumzo/Soga
  • Ulumbi


Sifa za Fasihi Simulizi

  1. Hupitishwa kwa njia ya mdomo
  2. Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au wahusika
  3. Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali
  4. Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.
  5. Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.
  6. Aghalabu huwa na funzo fulani


Umuhimu wa Fasihi Simulizi

  1. Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira
  2. Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii
  3. Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira yao
  4. Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokana na sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo
  5. Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii
  6. Kuunganisha watu - huleta watu pamoja
  7. Kukuza lugha - fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia mbinu mbalimbali za lugha.
  8. Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.
  9. Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda


Wahusika Katika Fasihi Simulizi

  • Wahusika ni viumbe wa sanaa ambao hutumiwa katika kazi ya fasihi kuwasilisha maswala mbalimbali.
    • Fanani-anayetunga na kuwasilisha fasihi simulizi.
    • Hadhira-kusikiliza, kutazama, kushiriki wa kuimba, kuuliza maswali, kutegua vitendawili, kupiga makofi, n.k. kuna aina mbili za hadhira: (i) hadhira tendi/hai na (ii) hadhira tuli.
    • Wanyama-wanaofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja, ulaghai, tamaa na ujinga na wanaobakia wanyama tu.
    • Binadamu
    • Mazimwi na majitu-viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile jicho moja, vichwa viwili au zaidi, nusu mtu na nusu myama, wenye tamaa iliyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu, kuhifadhi na kutunza binadamu ananyoyapendeza.
    • Wahusika vitu (visivyo na uhai) mawe, miti, vijaluba, vibuyu-hutumiwa kuibua imani za kidini.
    • Mizimu-roho za waliokufa-hutembea, hula na huathiri binadamu.
    • Miungu-viumbe vyenye uwezo mkubwa dhidi ya binadamu k.m. katika mighani na visasili.


Njia za Kukusanya Fasihi Simulizi

Kuchunza/utazamaji

  • Kutazama kwa makini yanayotokea na kuandika.

Umuhimu/ubora/uzuri

  1. Kupata habari za kutegemewa na kuaminika.
  2. Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
  3. Ni njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika
  4. Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
  5. Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji

Udhaifu

  1. Shida ya mawasiliano.
  2. Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kumshuku na kusitisha uwasilishaji
  3. Ghali kwa kumbidi mtafiti kusafiri
  4. huhitaji muda mrefu

Kusikiliza wasanii wakiwasilisha tungo zao.

Umuhimu

  1. Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
  2. Kupata habari za kutegemewa na kuaminika.
  3. Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
  4. Kikwazo cha mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  5. Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji.

Udhaifu

  • Shida ya mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  • Huhitaji muda mrefu-kusafiri na kusikiliza.
  • Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kutowasilisha ipasavyo.
  •  Ghali kwa gharama ya usafiri.

 

Mahojiano

  • Kuhoji wanaofahamu mengi kuhusu fasihi simulizi.

Umuhimu

  1. Kuweza kung’amua wakati mhojiwa anatoa habari zisizo za kweli.
  2. Kuweza kufafanulia mhojiwa maswali ili kuweza kupata habari sahihi zaidi.
  3. Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
  4. Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
  5. Kupata habari za kutegewa na kuaminika

Udhaifu

  1. Huhitaji muda mrefu.
  2. Mhojiwa kutotoa habari kwa kutomwamini mtafiti kwa ugeni wake.
  3. Kikwazo cha mawasiliano-si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  4. Ghali kwa gharama ya usafiri.

Kurekodi katika kanda za sauti/tepurekoda

Umuhimu

  1. Kuweza kudumu na kufikia vizazi vingi.
  2. Sifa za uwasilishaji/uhai kama vile toni na kiimbo kuhifadhiwa.
  3. Mkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa.
  4. Kupata habari za kutegewa na kuaminika
  5. Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji

Udhaifu

  1. Chaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.
  2. Hakiwezi kunasa uigizaji.
  3. Fanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwa.
  4. Ghali kwa kuhitaji kununua kifaa na kumbidi mtafiti kusafiri.

Kurekodi kwa filamu na video

  • Hunasa picha zenye miondoko na sauti.

Umuhimu

  1. Video huhifadhi uigizaji, ishara na kiimbo/toni.
  2. Kuonyesha uhalisi wa mandhari
  3. Mkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa
  4. Kazi iliyokusanywa hivi hudumu kwa muda mrefu.
  5. Njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika
  6. Kupata habari za kutegewa na kuaminika

Udhaifu

  1. Chombo chaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.
  2. Fanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwa.
  3. Njia ghali.
  4. Fanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwa.
  5. Ghali kwa gharama ya ya usafiri na kununua filamu na kamera ya video.
  6. Data yaweza kufisidiwa na hivyo kutowafikia walengwa.

Kupiga picha kwa kamera

  • Hunasa picha zisizo na miondoko na sauti

Umuhimu

  1. Huonyesha uhalisi wa mandhari.
  2. Huweza kuhifadhi ishara.
  3. Mkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa.
  4. Kupata habari za kuaminiwa na kutegemeka.

Udhaifu

  1. Ghali kwa gharama ya ya usafiri na kununua kamera.
  2. Sifa za uhai kama vile kiimbo haziwezi kuhifadhiwa.
  3. Yaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.
  4. Data yaweza kufisidiwa na hivyo kutowafikia walengwa

Kushiriki katika kazi ya fasihi simulizi k.v. ngoma, soga, n.k.

Umuhimu

  1. Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji.
  2. Kupata habari za kutegewa na kuaminika.
  3. Njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  4. Kukuza utangamano wa mtafiti na wanajamii.
  5. Kuweza kunasa na kuhifadhi sifa za kiimbo, toni na ishara.

Udhaifu

  1. Kuchukua muda mrefu.
  2. Ugeni wa msanii kusababisha washiriki kuwa na wasiwasi na kutotenda kama kawaida.
  3. Njia ghali kwa kuhitaji mtafiti kusafiri mbali.
  4. Mtafiti aweza kusahau kwa kuhifadhi akilini.

Kutumia hojaji

  • Fomu yenye maswali funge au wazi.

Umuhimu

  1. Gharama ya chini.
  2. Yaweza kutumika katika mahojiano.
  3. Huokoa muda kwani mtafiti aweza kuituma na kuachia mhojiwa kujaza.
  4. Hupatia habari za kuaminika na kutegemeka.

Udhaifu

  1. Utata wa maswali kusababisha majibu yasiyo sahihi.
  2. Si nzuri kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  3. Kutopata sifa za uwasilishaji kama vile kiimbo, toni na ishara.
  4. Wahojiwa kukataa kuijaza kutokana na mwelekeo hasi dhidhi ya hojaji na hivyo kukwamiza utafiti.

Vifaa vya Kukusanya Fasihi Simulizi na Udhaifu Wake

  1. Vinasa sauti/tepu rekoda
  2. Kamera
  3. Filamu na video
  4. Diski za kompyuta
  5. Kalamu na karatasi

Umuhimu

  1. Kuweza kudumu na kufikia vizazi vingi.
  2. Si rahisi kusahaulika-hubakia vile vile.
  3. Si njia ghali kama vile video

Udhaifu

  1. Sifa za uwasilishaji kama vile toni, kiimbo/toni na ishara haziwezi kuhifadhika hivyo kupotea.
  2. Hupunguza hadhira kwa kulenga tu wanaojua kusoma na kuandika na hivyo kuathiri usambazaji wake.


Mbinu za Kuhifadhi Fasihi Simulizi

  1. Huhifadhiwa na binadamu akilini k.m. ngano hupokewa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
  2. Katika maumbile au mazingira k.m. fisi daima huchechemea , kinyonga naye hutembea pole pole.
  3. Katika vifaa meme k.m. nyimbo, hadithi, maigizo n.k. huweza kuhifadhiwa katika kanda za sauti, video, sidi na diski za kompyuta.
  4. Katika michoro k.m. picha huhifadhi matukio maalum k.v. za kabila fulani likiwinda au likisherehekea.


Umuhimu wa Kukusanya/Kuhifadhi Fasihi Simulizi

  1. Ili isipotee k.m. kwa kusahaulika.
  2. Kuirekodi ili kuiendeleza kwa kuirithisha kwa vizazi vijavyo.
  3. Ili kulinganisha fasihi simulizi za jamii mbalimbali na kuonyesha tofauti zake.
  4. Ili kuhakikisha mtiririko katika uwasilishaji.
  5. Kutunza historia ya jamii ili vizazi vijavyo viijue.
  6. Ili kuziba mapengo ya utafiti yaliyomo kwa vile kuna tungo ambazo hazijatafitiwa kwa kina.
  7. Kuendeleza elimu ya jadi ya jamii.
  8. Kuingiliana na jamii iliyo chanzo cha fasihi humwezesha kuelewa na utamaduni na fasihi yake kwa ujumla
  9. Humwezesha mwanafunzi kuona vipengele hai vya fasihi k.v. uigizaji, toni na kiimbo ambavyo husaidia kuielewa kwa kina.
  10. Husaidia kuhifadhi tamaduni za jamii kwa nia ya kuzipitisha kwa vizazi vijavyo.
  11. Husaidia kuelewa utamaduni wa jamii nyingine.
  12. Humwezesha mwanafunzi kupata maarifa ya kufanya utafiti katika taaluma nyingine k.v. sosholojia.
  13. Kujua fasihi simulizi za jamii nyingine humfanya mtafiti kuzielewa na kuzikubali jamii hizo na hivyo kuendeleza amani katika nchi.
  14. Ili kusahihisha mawazo mapotovu kuhusu baadhi ya tanzu na vipera vya fasihi simulizi.

 

 



Matatizo Yanayomkabili Mkusanyaji wa Fasihi Simulizi

  1. Gharama ya utafiti kuwa kubwa kiasi cha mtafiti kutoimudu k.v. kusafiria, kununulia vifaa.
  2. Kutojaziwa hojaji kutokana na mtazamo hasi wa jamii dhidi ya ujazaji wake.
  3. Wanajamii kukataa kutoa habari wakishuku mtafiti anawapeleleza au kwa kuona haya.
  4. Wanajamii wengine kudai walipwe kabla ya kutoa habari na hivyo kukwamiza utafiti.
  5. Mbinu nyingine k.v. hojaji huhitaji watu wanaojua kusoma na kuandika na ikiwa mhojiwa hajui utafiti utakwamizwa.
  6. Uchache wa wazee na wataalamu wa fasihi simulizi kusababisha kukosekana au kupatikana kwa data isiyo ya kutegemewa.
  7. Utawala kukataa kutoa idhini ya kufanya utafiti.
  8. Kukosa ufadhili na utafiti kutofanywa kwa kutomudu gharama.
  9. Muda wa utafiti kutotosha na hivyo kutopata habari za kutosha kuhusiana na mada yake.
  10. Kikwazo cha mawasiliano ikiwa mtafiti na mhojiwa hawatumii lugha moja na mhojiwa hajui lugha nyingine na kumbidi mtafiti kukodi mkalimani na gharama kuongezeka.
  11. Ukosefu wa vyombo vya usafiri kunakochelewesha utafiti na kutomalizika katika muda uliopangwa.
  12. Ukosefu wa usalama k.v. kuvamiwa kwa kushukiwa anapeleleza na kuibiwa vifaa.


Changamoto Zinazokabili Ukusanyaji wa Fasihi Simulizi

  • Ukosefu wa utafiti wa kutosha kwani kuna vipera ambavyo bado havijaandikwa.
  • Uchache wa wataalamu wa kutafitia na kuendeleza utafiti.
  • Watu kuhamia mijini na kuingiliana na wa jamii nyingine na kufanya uhifadhi na urithishaji wa fasihi kutowezekana.
  • Mtaala wa elimu kupuuza lugha ya kiasili inayotumiwa kuhifadhia na kurithisha fasihi simulizi na hivyo kukatiza ukuaji wake.
  • Fasihi simulizi kuhusishwa na ukale na hivyo kutoona haja ya kuirithisha na kuihifadhi.
  • Kuhifadhiwa kwa fasihi simulizi akilini kusababisha kusahaulika, kubadilika hata kufa kwake.


Jinsi Jamii ya Sasa Inavyojaribu Kuhifadhi Fasihi Simulizi

  • Tamasha za muziziki kunakokaririwa na kuimbwa mashairi.
  • Sherehe za arusi, jando, mazishi mawaida.
  • Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia redio na runinga.
  • Sarakasi za wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho.
  • Ngoma za kienyeji kama isukuti katika hafla za kisiasa na harusi.
  • Utambaji wa hadithi hasa katika sehemu za mashambani.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Fasihi Simulizi - Kiswahili Fasihi Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest