Barua Rasmi - Kiswahili Insha Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

 • Barua ambazo huandikwa na kutumwa ofisini kwa kutaka kuomba kazi, kuomba msaada, malalamiko, kutoa maoni gazetini, n.k.


Muundo

 • Anwani ya mwandishi (wima au mshazari. Usiweke jina)
  • Anwani hii huandikwa katika sehemu ya juu upande wa kulia wa karatasi.
  • Anwani hii hujumuisha: Makao ya mwandishi k.m shule, kijiji n.k. Sanduku la posta (S.L.P.) Mji na tarehe aandikapo barua husika.
 • Marejeleo k.m. REJ: SUD/MSS/054/009 (nambari ya kumbukumbu, faili au nambari ya barua)
 • Anwani ya mwandikiwa k.m. Mkurugenzi,
  - Anwani hii hujumulisha, cheo au dhima ya mwandikiwa, sanduku la posta na mji.
  - Huandikwa upande wa kushoto laini moja baada ya tarehe.

  Kiwanda cha majani chai cha Kangaita,
  S.L.P, 12000, Kerugoya au


  KWA ANAYEHUSIKA

 • Kupitia kwa: MWALIMU MKUU, anwani
 • Mtajo k.m. Kwa Bwana/Bibi/Profesa/Daktari/Mhubiri
 • MINT/KUH/YAH - Kichwa cha barua/lengo la kuandika barua. Huandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari k.m.
  MINT: OMBI LA KAZI YA UALIMU/MAPENDEKEZO KUHUSU JUMA MRISHO/ MWALIKO WA KUHUDHURIA KONGAMANO LA KISWAHILI
 • Utangulizi (Mintaarafu ya tangazo mlilochapisha…naandika kuomba…jinsia…ahadi kufanya kazi kwa bidii)
  - Aya hii huwa fupi mno na hutumiwa na mwandishi kujitambua na vilevile kusema matakwa yake kwa ufupi.
 • Mwili (matatizo, madhara, mapendekezo (naomba, paswa, stahili, naonelea ni bora)
   -Sehemu hii vilevile huwa fupi na kwa muhtasari. Mwandishi huitumia kuelezea (Iwapo anaomba nafasi ya kazi.): -sifa zake, -umri, -ujuzi wa kazi, -tajriba ya kazi n.k.
 • Hitimisho (Natumai, Nitashukuru…
  - Hii huwa ni aya ya mwisho ambapo mwandishi hujaribu “kumguza moyo” msomaji wa barua yake. Aghalabu katika aya hii mwandishi huomba matakwa yake yatiliwe maanani.
 • Wasalaam
  - Hii ndiyo sehemu ya mwisho ambayo huonyesha jina la mwandishi. Sanasana huwa hivi:
  Wako mwaminifu/mtiifu,
  sahihi,
  jina
  /cheo, 


Mfano wa Barua Rasmi

Shule ya Muthithi,
S.L.P 49,
MARAGUA.
10-03-2006.


Meneja, Kampuni ya MLO,
S.L.P 17,
SABASABA.

Kwa Meneja,

MINT: MAOMBI YA NAFASI YA KAZI

Kwa unyenyekevu mkuu, ninaomba nafasi ya kazi ya ubawabu katika kampuni yako. Mimi ni mwanaume wa umri wa miaka ishirini na minane. Nimehitimu elimu ya upili na kufanya kazi za ubawabu katika kampuni mbalimbali. Katika makampuni hayo yote, nimeonyesha bidii, uajibikaji na nidhamu ya hali ya juu.

Ukinipa nafasi hii, nitafanya kazi kwa kujitolea wala sitakuvunja moyo.

Pamoja na barua hii, nimeandamanisha ushuhuda wa mengi kunihusu. Nitakushukuru ukinipa nafasi ya kunihoji.

Wako mwaminifu,

Sahihi

Soja Mkali ja Chui.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Barua Rasmi - Kiswahili Insha Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest