Insha ya Ratiba - Kiswahili Insha Notes

Share via Whatsapp
 • Ratiba ni orodha ya mpangilio wa namna mambo yatakavyofuatana katika shughuli fulani.
 • Lengo lake ni kuhakikisha wakati unatumiwa vizuri ili mambo fulani yasije yakakosa kutendwa kutokana na upungufu wa wakati.
 • Ratiba hutumika katika sherehe, mikutano, mazishi, hafla, tamasha, n.k


Sehemu za Ratiba

 1. Kichwa
  • Kichwa cha ratiba hutaja mambo yafuatayo:
   • Shughuli yenyewe - Taja jina la tukio ambalo unaandalia ratiba. Kwa mfano Harusi ya Bwana na Bi Arusi, Siku ya Zawadi
   • Tarehe ya shughuli - je shughuli hiyo itafanyika lini?
   • Mahali- Taja mahali ambapo shughuli hiyo itafanyikia. kwa mfano katika uwanja wa michezo wa Kasarani, kanisa la St. Mtakatifu
  • Mfano wa kichwa cha ratiba:
   • Ratiba ya Hafla ya Ukimwi katika Bustani la Uhuru tarehe tano Januari.
   • Ratiba ya Mazishi ya Dkt. Marehemu tarehe 20/12/1923 Kijijini Vikwazoni
 2. Mwili
  • Mwili wa ratiba hujumuisha mambo mbalimbali yatakayofanyika katika mpangilio maalum, saa mbalimbali. Ni vizuri kuzingatia vipengele vifuatavyo:
   • Saa - Onyesha saa ambazo tukio limepangiwa kuanza hadi linapotakiwa kumalizika
   • Mahali - Ikiwa shughuli tofauti zinafanyika katika mahali mbalimbali kama vile vyumba tofauti, inapaswa hutaje mahali ambapo kila jambo litafanyikia.
   • Wahusika - Taja mtu au watu waliopewa wajibu wa kutekeleza jambo fulani. Hii huwasaidia kujitayarisha ipasavyo.


Mfano wa Ratiba

RATIBA YA MAZISHI YA MZEE MAUTI TAREHE 20/12/1923 KIJIJINI MIZUKANI

SAA SHUGHULI
07: 00 Marafiki wa Mauti watoa mwili kutoka SlowDeath Hospital
10: 30 Maombi katika kanisa la G.I.Z.A yakiongozwa na Pst. Muna Fiki
11: 15 Mwili kuwasilishwa nyumbani, familia ya Mauti
12: 00 Kupakuliwa kwa chakula na Bi Kamafisi, Bi Mwachafu na wapishi walioteuliwa
1: 10 Kukusanyika kwa umati
2: 00 Maombi ya kuanzisha shughuli za mazishi
2: 30 Shuhuda zikiongozwa na Mzee Siachwinyuma
3: 00 Ushuhuda wa serikali na Chifu Mtesi
3: 40 Kuteremshwa kwa mwili kaburini na vijana walioteuliwa
4: 00 Shukrani za Mwisho, na Mwenyekiti wa Chama cha Kufa Tukusaidie
6: 00 Kugawana mali ya marehemu, na wazee wa kijiji
Join our whatsapp group for latest updates

Download Insha ya Ratiba - Kiswahili Insha Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest