Maagizo
- Andika insha mbili. lnsha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Lazima
Wewe ni katibu wa jopokazi ambalo limeteuliwa kuchunguza sababu za wanafunzi wa shule za upili kupuuza masomo ya kiufundi. Andika ripoti ya uchunguzi huo huku ukitoa mapendekezo. - Maktaba ya shule yenu haina magazeti. Andika makala kuonyesha umuhimu wa maktaba hiyo kuwa na magazeti.
- Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
Mpanda ovyo hula ovyo. - Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo:
Msongamano wa wanunuzi, wapitanjia na wasukuma mkokoteni katikati mwa wachuuzi wa kila aina ulinitanabahisha kuwa nimefika mji wa Tafaruku.
Mwongozo wa Kusahihishia
- Hii ni ripoti.
Yafuatayo yazingatiwe:- Muundo
Sura ya ripoti idhihirike.- Kichwa – kionyeshe kiini cha uchunguzi.
- Utangulizi
- Mtahiniwa ataje jopokazi: wanachama walioteuliwa, aliyeteua jopokazi
- Hadidu za rejea (Masharti na mipaka ya utekelezaji wa kazi
iliyopangiwa jopokazi.) - Sampuli lengwa - habari zilikokusanywa.
- Njia za ukusanyaji – hojaji, mahojiano, majadiliano kwenye vikundi.
- Mwili – hoja zijadiliwe humu; vichwa vidogo vitumiwe.
- sababu/mapuuza/matokeo
- Mapendekezo
- Hitimisho
- sahihi, jina, tarehe (kimalizio)
- Maudhui
Baadhi ya hoja ni:- Msisitizo mkubwa kwenye masomo ya kiakademia.
- Kutokuwa na vielelezo tosha vya watu waliofanikiwa kwa kufuatia masomo ya aina hii.
- Masomo haya kutohimizwa katika shule nyingi kwa sababu ya ukosefu wa vifaa.
- Ukosefu wa walimu waliohitimu katika taaluma hizi.
- Shinikizo kutoka kwa wazazi - wanafunzi wajishughulishe na masomo
mengine. - Mtazamo hasi kuwa baadhi ya masomo kama vile ufundi wa mabomba ni duni.
- Hapajawa na mfumo bayana unaoonyesha hatua ambazo mwanafunzi/mwanagenzi atapitia hadi pengine Chuo Kikuu.
- Mafunzo mengine ya kiufundi ni ghali.
- Vyuo vichache vya kiufundi katika sehemu za mashambani.
- Vyuo vingine vya kiufundi vimegeuzwa kuwa vyuo vikuu, hivyo wanafunzi kutoona umuhimu wa vyuo vya kiufundi.
- Baadhi huenda wasimudu masomo ya kisayansi, hivyo kukata tamaa.
- Masomo haya yanahitaji mtaji ndipo anayesomea apate ajira.
- Mtazamo potovu kuwa masomo haya ni ya mapato ya chini.
- Walimu kuwavunja wanafunzi moyo.
- Masomo haya hayana mvuto kwa wanafunzi.
- Masomo haya huwafunga wanafunzi kuhusika wenyewe.
- Mtazamo hasi wa kijinsia, utamaduni,itikadi n.k.
N/B Hoja zingine ziko wazi.
Apewe mkwaju wa hoja.
Mtahiniwa atoe angaa pendekezo moja.Akitoa mawili au zaidi, ni bora zaidi.Asiye na pendekezo atakuwa amepungukiwa kimaudhui hivyo asipite kiwango cha C (alama 10).- Mtaala usisitize masomo ya kiufundi kuanzia ngazi za chini.
- Vyuo vya Ualimu vihușishe ufundishaji wa masomo ya kiufundi.
- Serikali iongeze ufadhili kwa masomo ya kiufundi.
- Kuwe na mfumo bayana unaoonyesha taaluma ambayo mwanafunzi atasomea akifuatia masomo ya kiufundi.
Kipengele kimoja kisimkwaze mwanafunzi akakosa 45
N/B -Akiandika ripoti ya kawaida atakuwa amepotoka kimtindo, hivyo akadiriwe vilivyo,
- Muundo
- Makala yaonyeshe umuhimu wa magazeti.
Sura ya Makala idhihirike.
Baadhi ya hoja ni:- Kujuza kuhusu yanayojiri nchini/ulimwenguni.
- Kupalilia usomaji wa mapana.
- Hukuza ubunifu - mwanafunzi atajifunza mitindo mbalimbali ya uandishi.
- Kufunzia/kujifunzia sajili za magazeti.
- Baadhi huwa na safu ya kufunzia vipengele vya lugha.
- Hukuza stadi za kuhariri.
- Hupalilia uwazaji wa kina, kwa mfano kupitia kujaza mraba.
- Kupalilia mazoea ya kusoma.
- Kufanikisha somo la maktaba.
- Kupalilia mbinu za kitafiti/mazoea ya kudadisi.
- Kuburudisha
- Kuimarisha masomo kupitia kwa maswali na majibu
*Aadhibiwe 45 iwapo atakosa sura ya insha.
*Atakayepinga pekee amepotoka kimaudhui.
*Atakayepinga na kuonyesha umuhimu, apate mkwaju kwa umuhimu -atakuwa amepungukiwa kimtindo
- Hii ni insha ya Methali.
Kisa kidhihirishe maana ifuatayo:
Mtu asipotia bidii katika jambo matokeo yake huwa hafifu...
AU
Kiasi cha kufanikiwa katika jambo hutegemea matayarisho/mikakati ambayo inawekwa.
Baadhi ya hali ambazo zinaweza kujitokeza ni:- Mwanafunzi kutojitayarisha ipasavyo kwa ajili ya mtihani na hatimaye kupata alama
zisizoridhisha. - Wakulima wakose kujiandaa ipasavyo, mwishowe wapate mavuno haba
- Shirika likose kuweka mikakati ifaayo kuimarisha pato lake; lisipate faida, mwishowe
lifilisike. - Mlezi kutowaelekeza watoto ipasavyo, watoto kuinukia kuwa wasiotegemewa.
- Mwajiri kutojaribu kuimarisha uhusiano wake na waajiriwa wake, migogoro izidi, uzalishaji mali uathirike vibaya
Tanbihi- Vipengele vitatu vya kimuundo vijitokeze; Utangulizi, mwili, hitimisho.
- Kichwa cha makala kidhihirike.
- Sharti insha idhihirishe juhudi hafifu/mikakati hafifu/ukosefu wa kujiandaa na baadaye hali/matokeo yasiyoridhisha
- Atakayejihusisha au akahusisha mtu mwingine atakuwa amejibu swali
- Ashughulikie pande zote mbili za methali. Atakayeshughulikia upande mmoja asipite alama 10 (c+)
- Mwanafunzi kutojitayarisha ipasavyo kwa ajili ya mtihani na hatimaye kupata alama
- Hii ni insha ya kibunilizi.
Mtahiniwa atunge kisa ambacho kinaoana na mwanzo huu.
Usimulizi unaweza kubainisha hali zifuatazo:- Msimulizi asimulie yaliyotokea baada ya kuwasili, labda hata anaibiwa.
- Msimulizi aonyeshe alikoenda baada ya kuwasili, labda anapokelewa na mwenyeji wake; kisha asimulie maisha yake huko kwa mwenyeji wake.
- Anaweza kuwa anapitia hapa tu; pengine anatoka garini kupumzika kabla ya
kuendelea na safari yake. Baadaye anaendeleza usimulizi wake hadi panapoishia
safari. - Msimulizi anaweza kuanza kwa kauli hizi, kisha akaturudisha nyuma kusimulia kisa
ambacho kinamleta hapa. (mbinu rejeshi) - Anaweza pia kusimulia maisha ya watu wa mji huu.
- Akikosa kunakili dondoo, lakini amelenga kisa aadhibiwe kimtindo.
- Akiandika kisa ndotoni, atakuwa amejibu swali, bora ioane na mahitaji ya swali.
- Si lazima ataje mji wa Tafaruku.
- Kisa kiwe na kichwa.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2020 Past Papers.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students