MAAGIZO
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
- Kisha chagua insha moja nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- lazima
Siku za hivi karibuni umesoma riwaya mpya iliyoandikwa na Msanifu Kombo inayoitwa : Afrika imelaaniwa. Andika tahakiki ya riwaya hii. - Hatua ya serikali kuu kumpa kila mwanafunzi wa darasa la kwanza tarakilishi ni manufaa sana. Jadili
- Andika kisa kitakachodihirisha ukweli wa methali ifuatayo: Ukiona cha mwenzako kikinyolewa na chako tia maji
- Andika insha itakayomalizikia kwa kauli hii: Ama kweli sikufikiria wala kutegemea kuwa aushi yangu ingebadilika jinsi hiyo.
MARKING SCHEME
- Hii ni insha ya tahakiki. Insha hii ni lazima ionyeshe sehemu zifuatazo: kichwa, utangulizi, mwili , na hitimisho.
- Kichwa/ anwani
Anwani itaje jina halisi la kitabu au inaweza kuhusu jambo muhimu ambalo linatawala kitabu
Anwani iandikwe kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari. - Utangulizi
Hii ni sehemu ya kwanza ambayo ni lazima iwe na sehemu hizi:- Mada ya kitabu : Afrika Imelaaniwa
- Jina la mwandishi
- Wachapishaji
- Mwaka wa kuchapishwa
- Mhakiki
- Kurasa
- Bei
- Yaliyomo
- Mtindo- mwanafunzi aeleze jinsi mwandishi alivyotumia lugha ili kunata hadhira yake na kuwasilisha maudhui yake.
- Katika aya ya kwanza, mtahiniwa aeleze kwa kifupi dhamira ya yaliyomo kwenye riwaya
- Mtahiniwa aeleze maudhui machache na jinsi yameifanya Afrika kulaaniwa.
- Wahusika –awataje na tabia zao na pengine umuhimu wao
- Maoni yake-hapa mtahiniwa anaweza kuonyesha kufaulu au kutofaulu kwake kimtindo, maudhui au uundaji wa wahusika wake.
- Tamati- atoe maoni yake ya jumla kuhusu kitabu
utunzaji - Atakayekosa sehemu zote za kichwa na utangulizi atakuwa amekosa sura na aondolewe alama 4 baada ya kutunzwa.
- Sura- idhihirishe sura ya tahakiki
- Mtahini akadirie utangulizi na vipengele vya kichwa na yaliyomo
- Hoja za mtahiniwa zitakuwa bora ikiwa zitafungamanishwa na kichwa.
- Atakayekosa kufanya haya ana upungufu wa maudhui na asipate alama c 8/20
- Mtahini atie mikwaju pembezoni kuonyesha mtahiniwa amezingatia utangulizi, maudhui, wahusika, mtindo , udhaifu na tamati
- Insha inayozingatia vipengele vyote imekamilika. Akikosa baadhi ya vipengele akadirie vilivyo.
Urefu - Lazima insha itimize urefu kamili wa maneno 400
- Insha yenye urefu wa robo asipite kiwango cha D+ 05
- Insha yenye urefu wa nusu isipite kiwango cha C+ 10 wakati wa utunzaji hata kama amezingatia vipengele vyote.
- Insha yenye urefu wa robo tatu asipate kiwango cha B+ 15 wakati wa utunzaji hata kama amezingatia vipengele vyote.
- Atakayekosa kurejelea mwandishi Msanifu Kombo, au anwani Afrika Imelaaniwa, achukuliwe kuwa na upungufu wa kimtindo
- Kichwa/ anwani
- manufaa
-tarakilishi zitarahisisha ufunzaji wa masomo mbalimbali kwa upande wa mwalimu
-zitakuza na kuimarisha ubunifu miongoni mwa wanafunzi
-hatua hii itamtanguliza mapema mwanafunzi katika ulimwengu wa tarakilishi na teknohama
-hurahisisha kuelewa haraka kwa masomo kwa kurahisisha mada ngumu katika silabasi kwa mwanafunzi
-itaboresha matokeo ya mtihani kwa wanafunzi husika
-itaimarisha uchumi wa watengenezaji wa tarakilishi na program
-zitatumika katika utafiti
-zitapunguza mzigo kwa wanafunzi wa kubeba vitabu vingi.
Hasara
-ni ghali kutekeleza-inahitaji fadha nyingi
-bila kuwepo kwa walimu walio na umilisi wa kutosha wa kompyuta, hatua hiyo haitakuwa na manufaa
-kutakuwa na tatizo la usalama wa wanafunzi na tarakilishi zenyewe
-baadhi ya shule hazina miundo-msingi ya kutekeleza masomo ya tarakikilishi kama vile kawi na madarasa.
-zisipodhibitiwa, tarakilishi zitaweza kusababisha utovu wa maadili kwa wanafunzi kupitia mitandao - hili ni swali la methali
-mtahiniwa sharti atunge kisa kinachoafikiana na methali yenyewe
-mtahiniwa ashughulikie pande zote mbili za methali husika
-ukiona cha mwenzako kikinyolewa-huu ni upande wa kwanza
-na chako tia maji- huu ni upande wa pili
-mtahiniwa awe na hoja toshelezi katika pande zote mbili
-amalize kwa kutoa funzo kutokana na methali - andika insha itakayomalizikia kwa kauli hii;ama kweli sikufikiria wala kutegemea kuwa aushi yangu ingebadilika jinsi hiyo.
Maneno kiini katika kauli hii ni; sikufikiria, aushi yangu na ingebadilika, .hali inayodhihirika katika mdokezo huu ni mabadiliko yanayotokea katika maisha ya mhusika. Kisa kidhihirishe:- Mabadiliko yanayotokea katika maisha ya mhusika
- Mhusika anaweza kuwa aliishi kimaskini kisha akabahatika kumpata mfadhili
- Mhusika ambaye alitelekezwa na familia yake amepata mhisani
- Mhusika ambaye alizoea kuishi maisha ya juu anaipoteza kazi yake na maisha yanakuwa magumu
- Mhusika ambaye anawapoteza wazazi wake akiwa na umri mdogo analazimika kujitegemea
- Mhusika anagunduliwa kuugua ugonjwa hatari usio na tiba
- Mhusika ambaye anaachana na mumewe au mkewe kwa hiari au sharuti kisha maisha yanamharibikia.
Tanbihi - mtahiniwa atakuwa amepotoka kimaudhui pale tu hakumaliza kwa kauli aliyopewa, hivyo kuandika yasiyohusiana na swali
- mtahiniwa akikosa kumaliza kwa kauli aliyopewa lakini kisa chake kioane na kauli ya swali, atakuwa hajapotoka kimaudhui bali atakuwa amepungukiwa kimtindo tu
- akikosa kumaliza kwa kauli hii na kisa kisioane na kauli ya swali, atakuwa amejitungia swali
- mtahiniwa asimulie kisa kinachodhihirisha hali yoyote: chanya au hasi.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download KISWAHILI PAPER 1 - 2019 KCSE CEKENA MOCK EXAMINATION (QUESTIONS AND ANSWERS).
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students