SEHEMU A
LAZIMA -RIWAYA
- CHOZI LA HERI- A. MATEI
“Riwaya ya Chozi la Heri inaakisi uozo uliomo katika Jamii nyingi barani Afrika”
Thibitisha kauli hii kwa kurenjerea Riwaya (al 20)
SEHEMU B
TAMTHILIA KIGOGO (P. KEA)
- “Do ! Do ! Simameni ! Simameni! leo kutanyesha mawe ! “
- Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)
- Fafanua mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo hili (al 4)
- Huku ukitoa mifano jadili hoja sita zinazodhihirisha jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika Tamthilia ya kigogo (al 12)
AU
- Kwa kuirejerea Tamthilia ya Kigogo eleza jinsi mwandishi alivyotumia mbinu ya Majazi(al 20)
SEHEMU C
HADITHI FUPI
TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
(A.Chokoko na D.Kayanda)
- “Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
- Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)
- Tambua tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili (al 2)
- Fafanua sifa nne za msemaji (al 4)
- Jadili maudhui ya utabaka ukirejerea hadithi husika (al 10)
AU
- Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi;
- Mapenzi ya kifaraurongo (al 10)
- Mame Bakari (al 10)
SEHEMU YA D
USHAIRI
- Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.
Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani
Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani
Hiani pamwe ukora wenye kuhini.
Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu
Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili
Muwili hata kidari, kidari kuwa thakili
Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli.
Misuli kuwa hafifu, hafifu kama muwele
Muwele wa hitilafu, hitilafi ya nduwele
Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale.
Vishale vinitomele, vitomele vikwato
Vikwato pia maole, maole kufanya mito
Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto.
Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
Kutamka wazi vino, vino subira kutaka
Kutaka imani mno, mno n'sipate wahaka
Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.
Mashaka haya ya leo, leo yawe yarnepita
Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota
Nyota njema ingarao, ing'arao kunikita
Kunikita salamani, salamani nikadata.- Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani ? (alama 2)
- Shairi hili ni la Bahari gani kwa kuzingatia : (alama 4)
- Mpangilio wa maneno
- Mpangilio wa vina
- Kwa kutokea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (alama 4)
- Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
- Kwa kutolea mifano, eleza jinzi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (alama 6)
AU
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. (alama 20)
Barabara.
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nitulize akili
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi
Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghafla nakumbuka ilivyosema
Ile sauti zamani kidogo
Kuwa tayari kupanda na kushuka.‖
Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima niifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka.
Jambo moja nakumbuka: Mungu
Je, nimwombe tena? Hadi lini?
Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena
Kitu kimoja nakiamini
Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitafika mwisho wake
Ikiwa wangu mwisho haitauwahi kabla.
(Timothy Arege)
Maswali.- Taja na ueleze aina ya shairi hili. (alama 2)
- Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
- Fafanua dhamira ya shairi hili. (alama 2)
- Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili. (alama 3)
- Tanakali za sauti
- Mbinu rejeshi
- Taswira
- Eleza umhimu wa maswali balagha katika shairi. (alama 2)
- Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari. (alama 4)
- Eleza matumizi ya mistari mishata katika shairi hili. (alama 2)
- Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi. (alama 3)
- Kuruba
- Siha
- Machweo
SEHEMU E FASIHI SIMULIZI
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yaliyoulizwa.
Hapo zamani za kale, Mungu alituma wajumbe wawili waende duniani. Wajumbe hawa ni Kinyonga na Mjusi. Kwanza alimtuma Kinyonga na kumwagiza akaseme “wanadamu hamtakufa.” Kinyonga alienda kwa mwendo wa kuduwaa, akasimama hapa na pale akila matunda ya miti. Kwa sababu ya hali hii alichelewa sana kufikisha ujumbe kwa binadamu.
Baada ya muda kupita, Mungu alimtuma Mjusi na ujumbe akaseme, “Mwanadamu sharti kufa.” Mjusi aliunyanyua mkia akafyatuka pu! Mbio akawahi duniani kabla ya kinyonga kuwasili. Kwa haraka alitangaza agizo kuu, “Wanadamu sharti kufa!” Akarejelea haraka kwa Mungu. Baada ya muda kinyonga naye akafika duniana na kutangaza, “Wanadamu hamtakufa!” Wanadamu wakapinga mara na kusema, “La! Tumeshapata ujumbe wa Mjusi, wanadamu sharti kufa! Hatuwezi kupokea tena neno lako! Basi kulingana na neno la mjusi, wanadamu hufa.- Tambua aina hii ya hadithi (al 2)
- Toa sababu za jibu lako katika (a) i. (al 1)
- Eleza sifa tatu zinazohusishwa na ngano za fasihi simulizi katika hadithi hii. (al 3)
- Fafanua hulka mbili za Kinyonga kwa mujibu wa makala haya (al 2)
- Hadithi hii ina umuhimu gani? (al 4)
- Taja njia zozote nne za kukusanya kazi za fasihi simulizi (al 4)
- Fafanua jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi (al 4)
MARKING SCHEME
MAJIBU SEHEMU A
RIWAYA
- SWALI 1
- Mauaji- K.m Tery na wanawe walikumbana na janga la kifo baada ya kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba yao.
- Dawa za kulevya- Dick alipotekwa nyara alilazimika kuuza dawa za kulevya kwa muda wa miaka kumi.
- Ukabila – Ukabila unajitokeza wakati vita vinapozuka baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya. Majirani pia wanawageuka wenzao ambao walikuwawametoka katika kabila au ukoo tofauti na wao.
- Ulevi – Kuna matumizi ya pombe haramu k.m vijana wa vyuovikuu wanabugia pombe yenye sumu inayowafanya wengine kuaga dunia.
- Ukeketaji – Wasichana wa shule ya msingi wanapashwa tohara. Wengine wanayapoteza maisha yao huku wengine wakiponea chupuchupu.
- Ndoa za mapema- Wasichana wachanga wanalazimishwa kuolewa na vizee na kuacha masomo yao
- Usherati – Kimai alipoondoka kwenda shambani Bw. Tenge angeamua kumleta mwanamke mmoja baada ya mwingine.
- Mahusiano ya kimapenzi kati ya walimu na wanafunzi k.m Fumba na mwanafunzi wake Rehema.
- Ufisadi- Watoto kutoka familia zinazojiweza kiuchumi kupewa mikopo/ Ruzuku nao wana wa maskini kulazimika kufanya vibarua wakati wa likizo ili kujilipia karo.
- Utekaji nyara- Dick anatekwa nyara na kulazimishwa kuuza dawa za kulevya.
- Uavyaji mimba- Sauna anapopachikwa mimba na babake, mamake alimsaidia kuavya na kumwonya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu unyama wa babake.
- Mahusiano ya kimapenzi bainai ya watoto na wazazi wao- Sauna anashirikiana na babake mlezi kimapenzi na kuishia kupachikwa mimba.
- Ajira kwa watoto- Watoto wa darasa la tano kuhuzishwa katika kazi ya kuchuna majani chai kwa malipo kidogo m.f Chandachema
- Wizi/uporaji wa mali- Wakati vita vinapozukabaadhi ya watu wanaonekana wakipora maduka ya Kihindi, Kiarabu na hata ya Waafrika wenzao
- Ubakaji – Genge la mabarobaro watano linawabaka Lime na Mwanaheri hadharani.
- Ulanguzi wa watoto- Kangara na Sauna walifanya biashara haramu ya kuwauza watoto wa vijana.
- Kutupwa kwa watoto- Neema anakiokota kitoto kichanga kikiwa kwenye karatasi ya Sandarusi kwenye mchafukoge wa taka.
(Zozote 10 x 2= 20)
SEHEMU B
TAMTHILIA KIGOGO
-
-
- Ni maneno ya Ngurumo
- Anawaambia walevi wenzake
- Wako Mangweni kwa Mamapima/Asiya
- Anayasema maneno haya anapowaona Tunu na Sudi kwa mamapima jambo ambalo halikuwa la kawaida. (al 4)
-
- Nidaa - Do! Do ! Do!
- Takriri- Simameni! Simameni! Simameni!
- Jazanda - Kutanyesha mawe (al 4)
-
- Mtetezi wa haki- Tunu na Asha wanatetea haki za Wanasagamoyo
- Jasiri- Tunu anamkabili Majoka bila uoga
- Msomi- Tunu anasomea uanasheria
Ashua amesomea ualimu - Chombo cha burundani/ Kustareheka- Majoka anapomwona Ashua akiingia ofisini mwake anaona kuwa amerudi kwake kuonja asali.
- Mbeya- Ashua anamkejeli Husda kuwa ana sifa ya umbeya iwe hadharani ama faraghani.
- Mzalendo- Tunu analipenda jimbo anapopigania mabadiliko yatakayowafaa Wanasagamoyo .
- Mwasherati/ Asherati- Asiya ana uhusiano wa kimapenzi na Ngurumo ilhali yeye ni mke wa Boza.
- Pia anahusishwa na Keki za Uroda. - Mpenda anasa na starehe- Husda hupenda kwenda kwenye hoteli ya kifahari kujivinjari.
- Mpyoro/mwenye matusi- Husda anamtusi Ashua kwa kumwita hawara, kidudumtu na mbeya.
- Mwenye msimamo dabiti (zozote 6x2=12)
-
- SWALI LA 3
TAMTHILIA- Majoka – Nyoka mkubwa mwenye sumu.
Majoka ni mkali na anatekeleza maovu mengi dhidi ya Wanasagamoyo mfano mauaji. - Tunu- Zawadi
Anawafaa Wanasagamoyo kwa kupigania haki zao k.v kufunguliwa kwa sokola Chapakazi. - Husda- Mtu mwenye chuki/ Mtu mwenye kijicho.
Husda anamwonea Ashua kijicho kwa kuwa amesoma hadi chuo kikuu. - Mamapima- Anapima pombe na kuwauzia walevi Mangweni
- Sudi- Bahati njema
– Anabahatika kumwoa Ashua mwanamke mwenye bidii na msomi.
Pia amebahatika kuwa na kipawa cha uchongangi vinyago. - Sagamoyo- Kuponda moyo.
Wanasaga wanapitia mateso na maumivu makali ya moyo - Chapakazi- Mahali pa kufanyia kazi kwa bidii.
Wanasagamoyo wanatia bidii ili kuweza kujikimu. - Boza- Mtu mjinga/ mpumbavu.
Boza anaiunga mkono serikali kipofu.
Mke wake anazini na Ngurumo lakini yey hajui. - Kenga- Kulaghai/ kuhadaa
-Kufanya mtu aamini jambo lisilokuwa la kweli
-Ushauri potovu wa Kenga unachangia kuporomosha utawala wa majoka
-Pia alimdanganya majoka kuwa mabo yako shwari na mwishowe anamgeuka na kujiunga na Tunu. - Kombe- Aina ya mmea unaotambaa wenye sumu kali
-Kombe alikuwa sumu kwa akina Sudi kwa kuwa alikuwa akihusiana na m rengo wa Majoka na hakutaka kuonyesha msimamo wake wazi. - Ngurumo- Ni sauti kubwa k.v ya Simba au inayosikika angani wakati wa mvua.
Ngurumo alikuwa na hulka kama za ngurumo za radi. Anatumiwa kuuana na kuwapiga wapinzani wa Majoka. - Chopi- Kitendo cha kukosa kuwa imara
-Chopi ana tabia za mtu aliyelewa na hakuzingatia maagizo anayopewa na Majoka. - Siti- Jina la heshima kwa mwanamke ambalo hutanguliziwa kabla ya jiana lake.
-Siti alikuwa mfanyikazi wa Majoka na Majoka academy na inasemekana wafanyikazi wa hapo waliheshimiwa. (Zozote 10 x 2= 20)
- Majoka – Nyoka mkubwa mwenye sumu.
SEHEMU C
- HADITHI FUPI
- Msemaji ni Dennis
Anayeambiwa ni Penina
Wamo chumbani mwa Dennis chuoni.
Penina alikuwa anamwelezea Dennis kuwa angetaka awe mpenzi wake ndipo Dennis anapinga kwani wanatoka matabaka tofauti. (al 4)
- Msemaji ni Dennis
- Methali- Mzoea vya sahani vya vigae hawezi
Msemo – Kupigania mikono ielekee vinywani. (al 2) -
- Msemaji ni Dennis
- Msomi
- Mwenye bidii
- Mwadilifu
- Mwenye matumaini
- Mwepesi wa kushawishika/kudanganyika
- Mwenye wasiwasi/mwoga (al 4)
-
- Matajiri wanaendesha magari ya kifahari
- Wazazi wa Dennis wanafanya kazi ya vibarua
- Dennis alikosa chakula akakunywa uji
- Penina alitumiwa shilingi 5,000 kila wiki za matumizi
- Wazazi wa wanafunzi wengine walimiliki mabasi na matatu ishara ya utajiri
- Wengine walimiliki nyumba za ghorofa
- Baadhi ya wanafunzi walimiliki simu za dhamani.
- Watoto wa maskini hawakufanya vyema katika mitihani yao.
- Dennis alikuwa bila mpenzi kwani vijana maskini hawakupendwa.
- Wengine walivalia mavazi ya vitambaa vya dhamani na vilivyovutia.
- Shakila alitoka kwenye familia tajiri ambapo wazaziwe walimiliki shirika la uchapishaji.
- Watoto wa maskini hawakufanya vyema katika mitihani yao. (Zozote 10x 1=10)
- SWALI LA 5 :
- MAPENZI YA KIFARAURONGO
- Daktari mabonga anawasiliti wanafunzi kwa kukosa kuyajibu maswali yao.
- Penina anamsaliti Dennis anapomwambia hawezi kuolewa na mume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa. Anavunja uchumba wao.
- Serikali inawasaliti vijana wanapokosa ajira baada ya kuhitmu masomo yao ya chuoni.
- Penina anamsaliti Dennis anapomfukunza kutoka kwenye nyuma waliokuwa wakiishi.
- Penina anawasiliti wazazi wake kwa kutowatii wanapomtahadharisha dhidi ya kuchumbiwa na Dennis.
- Wanafunzi chuoni wanausaliti wajibu wao wa kusoma wanapoanza kuchumbiana.
- Penina anamsaliti Dennis anapommalizia chakula akidai kwamba hakuwa amemwachia pesa za kununua chakula. Dennis hakuwa na ajira na anatoka familia maskini.
- Wanajamii wanaisaliti familia ya kina Dennis wanapowakejeli kwa sababu ya kuwa maskini.(Zozote 5x2=10)
- MAME BAKARI
- Janadume linamsaliti Sara kwa kumvamia na kumbaka akitoka masomoni.
- Beluwa anamsaliti Sara kwa kufichua siri ya mimba yake kwao
- Jamii inamsaliti mwanamke kwa kumwona kuwa mkosaji tukio la ubakaji linapotokea
- Baba yake Sara anamsaliti mkewe kwa kutompa nafasi ya kujitetea.
- Wazazi wa kiume wanawasaliti mabinti zao wanapokuwa wajawazito kwa kuwafukuza kutoka nyumbani
- Dhana ya usaliti inajitokeza wakati Sara anakisia kwamba wanajamii wangemsusia na kumtenga kama mgonjwa wa ukoma iwapo wangeujua ujauzito wake uliokuwa wa kubakwa. (Zozote 5x2=10)
SEHEMU YA D
USHAIRI
- MAPENZI YA KIFARAURONGO
- SWALI LA 6
-
- Ili asiwe na wasiwasi wa kutukanwa na kuhiniwa
- Ili aepuke kufanyiwa mabaya (alama 2)
-
- Pindu/ Mkufu/ Nyoka
- Ukaraguni (alama 4)
-
- Tashbihi- Hafifu kama muwele (alama 2)
- Uradidi/Takriri – subira
- bora,kobora,ukora
-kiburi, kudhuri n.k (alama 2)
- Misuli kuwa dhaifu sana kama ya mgonjwa, hasa mgonjwa mwenye tatizo la uwele ambao unasumbua sana daima usiopona kwa tiba. (Zote 4x1=4)
-
- Inkisari- Kuleta urari wa mizani . Mfano Kilo- Kilicho
- Tabdila – Kuleta urari wa vina
Kudhuri- kudhuru
Maole – maozi - Mazida- Kuleta urari wa vina na mizani.
Vinitomele- vinitome
Muwili- mwili
-
- SWALI LA 7
- Shairi huru
-Halina mpangilio wa vina
- Halina mpangilio wa mishororo
-Halina mpangilio wa vipande (alama 2) - Uchungu
Masikitiko (alama 2) - Linazungumzia hali ya kukata tama katika maisha
Msimulizi anatamani maisha yamwendee vizuri (alama 2) -
- Nimechoka tiki
- Ghafla nakumbuka ilivyosema
- –Ya mtu aliyechoka
- ya mtu aliyekata tama
- Mtu anayepanda na kushuka mabonde (alama 3x1=3)
- -KUsisitiza hali aliyoko mshairi
-Kuonyesha utamaushi wa maisha kwa mshairi(alama 2) - Anaamini kuwa lazima aendelee kujikaza ili kukabiliana na kila hatua mpya ya maisha huku akijiburura kuifuata barabara yenye giza na unyuvu. Hata nikishikwa na kujitoa kwa mitego hiyo kwa kweli nitafika mwisho wake iwapo hatima yangu haitafikia mbele. (alama 4 x1=4)
- -Ghafla nakumbuka ilivyosema
- Natamani kuketi
-Ingawa nimechoka
Mwanafunzi atoe mifano mishata katika shairi
Mwalimu akadirie mifano ya mishata (Zozote 2x1=2) -
- Mahali njia inapinda
- Afya
- Jioni/magharibi (alama 3 x1=3)
- Shairi huru
- SWALI LA 8
SEHEMU E FASIHI SIMULIZI-
- Kisasili (al 2)
- Inaeleza jinsi kifo kilivyoingia duniani/ Asili ya kifo (al 1)
–Mwanzo maalum- Hapo zamani za kale
-Wahusika wanyama
-Wanyama kuwasilisha tabia za binadamu
-Tanakali za sauti. (Zozote 3x1=3)
- –Mvivu/ Mnyonge
-Mtiifu (Zozote 2x1=2) - –Huburudisha
-Huhifadhi historia ya jamii
-Huendeleza utamandunu wa jamii
-Huipa jamii mwelekeo
-Huonya/ Huadhibu
-Hukuza usirikiano
-Hukuza stadi za lugha (Zozote 4x1=4) - –Kutazama
- Kushiriki
-Kurekodi
-Kutumia Hojaji
-Mahojiano (al 4) - -Tamasha za muziki
-Sherehe za arusi, jando,mazishi na matambiko
-Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia vyombo vya habari
-Michezo ya kuigiza katika vyombo vya habari
-Tamasha za drama
-Sarakasi zifanywazo na wasanii
-Ngoma za kienyeji k.v Isikuti
-Watafiti wanaokusanya na kuhifadhi vipera vya fasihi simulizi (Zozote 4x1=4)
-
Download KISWAHILI PAPER 3 - 2019 KCSE CEKENA MOCK EXAMINATION (QUESTIONS AND ANSWERS).
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students