- Andika jina lako na nambari yako ya mtihani.
- Tia sahihi yako kasha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
- Andika insha mbili
- Swali la kwanza ni la lazima
- Kasha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizoakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
SWALI |
UPEO |
ALAMA |
1 |
20 |
|
20 |
||
JUMLA |
40 |
MASWALI
- LAZIMA
Wewe ni mhariri wa gazeti la Angaza. Andika tahariri kuhusu umuhimu wa wanafunzi kushiriki katika michezo na masomo mengine yasiyokuwa ya kiakademia. - Maovu ya kijamii yamekithiri sana miongoni mwa vijana. Eleza chanzo na upendekeze hatua zinazofaa kuchukuliwa ili kusitisha maovu haya.
- Tunga kisa kitakachodhihirisha matumizi methali ifuatayo:
Jifya moja haliinjiki chungu - Andika kisa kinachoanza kwa maneno haya.
“Umeletwa hapa na wasamaria wema.” Sauti ikanieleza. Nikavuta kumbukizi
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
KIDATO CHA NNE
Mwongozo - insha 102/1
- Hii ni insha ya tahariri
Sura ya tahariri idhihirike
GAZETI LA ANGAZA
ALHAMISI, OKTOBA 10, 2022
TAHARIRI KUHUSU UMUHIMU WA MICHEZO NA MASOMO YASIYO YA KIAKADEMIA
Maudhui
Baadhi ya maudhui/hoja- Huimarisha afya ya wanafunzi
- Huwasaidia kutumia muda wao vizuri
- Huwawezesha kukuza vipawa vyao
- Huwachangamsha baada ya siku nzima ya masomo hasa darasani
- Huwakutanisha na wanafunzi wa shule nyingine
- Huimarisha uhusiano kati ya wanafunzi na walimu wao.
- Huwafungulia milango ya ajira
- Hukuza uwajibikaji na uongozi miongoni mwa wanafunzi
- Huwasaidia kuwasilisha jumbe hasa kupitia mashindano ya muziki na drama
- Huwasaidia kuimarika kimasomo hasa kupitia mashindano ya sayansi na teknolojia.
Mtahini aeleze angalau hoja nane.
- Maovu ya kijamii yamekithiri sana miongoni mwa vijana. Eleza chanzo na upendekeze hatua zinazofaa kuchukuliwa ili kusitisha maovu haya
- Maovu ya kijamii.
- ndoa za jinsia moja
- Kuavya mimba
- Wizi wa mabavu
- Ubakaji
- Uasherati/usinzi
- Ndoa za mapema
- Wanafunzi kuchoma shule
- Chanzo cha maovu ya kijamii
- Uhaba wa kazi
- Ukosefu wa maelekezi
- Shinikizo la hirimu
- Umaskini /ukata
- Changamoto katika ndoa
- Ukengeushi
- Matumizi ya dawa za kulevya
- Ukosefu wa mbinu za kufidia muda mwingi walionao vijana
- Uigaji wa kiholela , tabia hasi
- Ushawishi potovu kutoka/kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
- Mapendekezo
- Ushauri nasaha utolewe kwa vijana kupitia asas mabalimbali za kijamii.
- Kuchukuliwe hatua kali za kisheria kama vile vifungo virefu , kutozwa faini.
- Kubuniwe jipo maalum la kupambana na matumizi ya dawa za kulevya.
- Mtaala wa elimu uhusishe mafundisho maalum kuhusu tamaduni zenye umuhimu.
- Wazazi na asasi nyingine kuwaonya vijana dhidi ya kushiriki mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa.
- Kubuniwe sera za kudhibiti matumizi ya mitandao hasa miongoni mwa vijana.
- Viongozi wa kidini waadilishe jamii kupitia mafundisho maabadani.
- Vyombo vya habari vidhibitiwe na kuchuja yale ambayo vinawasilisha.
- Maovu ya kijamii.
- Jifya moja haliinjiki chungu.
Hii ni insha ya methali
Mtahiniwa abuni kisa kitakachodhihirisha maana ifuatayo: hamna mtu anayefanya mamabo pekee akafaulu.
Hivyo anaweza kutunga kisa kinachosimulia:- Mtu aliyekataa kushirikiana na wengine kufanya mambo fulani na mwishowe akashindwa kufaulu.
- Ushirikiano katika jamii k.v shuleni, kijijini, nyumbani n.k ulioleta faida.
- Kisa kilenge kuokolewa kwa mkasa k.v ajali, ndoa za mapema, tohara n.k
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mincks Group of Schools Mock Examinations 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students