Maagizo
- Andika insha MBILI. Insha ya KWANZA ni ya LAZIMA.
- Chagua insha moja nyingine kutoka tatu zilizobaki.
- Kila Insha isipungue maneno 400.
- Kila Insha ina alama 20.
- Lazima :
Wewe ni mwenyekiti wa jopo lililoteuliwa kuchunguza chanzo cha utovu wa usalama kijijini Sokoto. Andika ripoti maalum /rasmi kuhusu jambo hili. - Magonjwa mengi yanasababishwa na mitindo ya kisasa ya maisha.
Jadili. - Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mchagua nazi hupata koroma.
- Andika insha itakayoanza kwa maneno haya:
Milipuko mikubwa ilisikika pu! Pu! Puu! Kisha niliwaona watu wakikimbia kuelekea pande zote…
MARKING SCHEME
- Atambue kuwa ni swali la ripoti rasmi. Lazima insha hii iwe na anwani iliyo wazi, yaani iwe na neno ripoti, ya nani, kuhusu nini na wapi ?
Sharti sura ya ripoti maalum au rasmi izingatiwe:Kichwa, utangulizi, taratibu/yaliyoshughulikiwa, mwili/matokeo ya uchunguzi,hitimisho,mapendekezo na sahihi.
Baadhi ya hoja:
Insha iwe na maudhui yasiyopungua matano. Baadhi ya hoja ni kama vile:- Ulevi
- Ukosefu wa kazi
- Wanyama wa pori kama vile ndovu
- Watoto kutopelekwa shule
- Utepetevu wa vyombo vyombo vya usalama
- Adhabu nyepesi zinazotolewa na mahakama
- Wazazi kutotekeleza wajibu wao kwa watoto
- Tamaduni zilizopitwa na wakati kama tohara, wizi wa mifugo n.k
Sharti mtahiniwa atoe mapendekezo ya kutatua tatitizo hili k.v- Kupiga marufuku utengenazaji na unywaji wa pombe haramu
- Kuanza miradi ya kuajiri vijana
- Watoto wote kupelekwa shule
- Vyombo vya usalama kuwa macho na kupigana na uhalifu
- Adhabu kali kutolewa kwa wahalifu
- Wazazi kutekeleza wajibu wao wa kutunza watoto
- Kukabiliana vikali na makundi haramu
- Kutupilia mbali tamaduni zilizopitwa na wakati
Asiyezingatia sura ya ripoti aadhibiwe kwa kuondolewa 4s
Makosa ya sarufi na hijai yaadhibiwe yanapotokea
- Mtahiniwa aandike insha ya hoja
- Sharti ataje hoja, kuifafanua na kuitolea mifano
- Lazima aunge mkono hoja aliyopewa
- Pia aonyeshe upande wa pili wa hoja aliyopewa.
- Aeleze mitindo ya maisha ya kisasa.
- Hoja zake ziwe tano au zaidi
Hoja za kuunga mkono:- Baadhi ya vyakula hasa vyenye mafuta, madini,sukari na chumvi husababisha magonjwa kama vile msukumo wa damu na kisukari
- Kukosa mazoezi ya mwili hasa kwa sababu ya matumizi ya magari ya usafiri na ya kibinafsi na watu hawatembei kwa miguu.
- Matumizi ya pombe huleta madhara mengi kwa mwili yanayosababisha magonjwa ya akili.
- Mienendo mibaya hasa kushiriki mapenzi ovyo ovyo husababisha magonjwa ya ukimwi, kisonono na magonjwa mengine ya zinaa.
- Uchafuzi wa mazingira husababisha magonjwa kama vile ya pumu,malaria ,kipindupindu n.k
Hoja za kupinga:- Atetee kwamba magonjwa hayasababishwi tu na mitindo ya maisha ya kisasa.
- Baadhi ya magonjwa hurithishwa katika familia.
- Kuna magonjwa yanayoletwa na wadudu kama vile mbu, konokono n.k
- Magonjwa kama vile mafua husababishwa na hali ya anga na si hali ya maisha.
- Hali za kimaumbile kama vile mafuriko husababisha magonjwa kama vile kipindupindu.
- Sharti aelewa kuwa ni methali.
- Atunge kisa ambacho kinaoana vizuri na maana ya matumizi ya methali hii.
- Kisa chake kiwe cha kuvutia.
- Sharti aonyeshe pande mbili za methali.Aonyeshe mhusika anayechagua kitu au jambo zuri lakini analikosa na kupata lingine la kiwango cha chini.
- Anatakiwa kuonyesha kuwa tusiwe watu wa kuchagua vitu bali tufanye bidii kupata tunachokihitaji.
- Makosa ya hijai na sarufi yaadhibiwe yanapotokea
-
- Ni sharti mtahiniwa aanze kwa maneno aliyopewa.
- Anatakiwa kuanza kwa maneno yale bila ya kubadilisha wala kuyapunguza.
- Kisa chake kiwa cha kuvutia na aonyeshe ni matukio yapi yaliyosababisha milipuko ile, kulikuwa na majeruhi na watu walitoroka kwenda wapi? Ni nini kilichotokea baada ya hapo?
- Asipoanza kwa maneno aliyopewa atuzwe alama ya bakshishi
USAHIHISHAJI KWA JUMLA
- Sharti mtahiniwa ajibu maswali mawili pekee.
- Kazi ya mtahiniwa iwe nadhifu na ipangwe vizuri kiaya.
- Makosa ya hijai na sarufi yaadhibiwe yanapotokea.
- Baada ya kusahihisha kazi ya mtahiniwa, awekwe kwenye viwango ya A-D vilivyowekwa na baraza la kitaifa la mitihani K.N.E.C
- Mtahini atakayepotoka, atakayejitungia swali au atakayetumia lugha isiyo Kiswahili atuzwe alama ya BK01.
- Urefu wa insha sharti uzingatiwe (maneno 400) ¼Urefu ukadiriwe hivi:
Maneno 100 200 300 400 Kiwango ¼insha ½insha ¾insha Kamili
Tanbihi:
- Hizi ndizo alama za juu iwapo mtahiniwa ameandika kiwango hicho cha maneno . Kisha aadhibiwe makosa mengine.
- Mtindo wa zamani wa kuondoa alama 2U ulitupiliwa mbali.
Alama zifuatazo zitumiwe katika usahihishaji.
✓Msamiati unaofaa
×Msamiati usiofaa
−Kosa la hijai
═Kosa la sarufi
^Alama ya achwa – neno linapoachwa katika sentensi
Download Kiswahili Paper 1 Kenya High Post Mock Exams 2020 - Questions and Answers.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students