MAAGIZO
- Jibu maswali manne pekee.
- Swali la kwanza ni lazima.
- Maswali hayo mengine matatu yachaguliww kutoka sehemu nne zilizobaki
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
SEHEMU A: Riwaya
- LAZIMA
Assumpta K. Matei: Chozi la heri
“Hili lilimtia …………. uchungu, akajiona kama aliyedhalilishwa na mwanamke.”- Yaweke maneno haya katika muktadha wake (alama 4)
- Taja suala linalodokezwa katika dondoo hili (alama 1)
- Kwa kutumia hoja kumi na tano, eleza namna suala ulilolitaja hapo juu 1 (b) linalijitokeza
(ala. 15)
SEHEMU B: Tamthilia
Kigogo (Pauline Kea)
Jibu swali la pili au la tatu
- “Kubali pendekezo letu la kufungwa kwa soko……… huoni hii ni fursa nzuri ya kulipiza kisasi?”
- Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
- Kufungwa kwa soko ni ukatili. Mbali na ukatili huu, toa mifano mingine ya ukatili kwenye tamthilia. (alama 9)
- Msemaji wa maneno haya ni mshauri mbaya. Thibitisha kutoka kwenye dondoo na kwingineko tamthiliani. (alama 7)
-
- Fafanua mbinu kumi anazotumia Majoka katika kuuendeleza uongozi wake(alama 10)
- Eleza namna mbinu ya ishara ilivyotumiwa katika tamthilia ya Kigogo (alama 10)
SEHEMU C: Hadithi Fupi
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (Alifa Chokocho na Dumu Kayanda)
Jibu swali la 4 au la 5
- “…………… Ningeondoka ….. mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.”
- Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
- Onyesha vile Kinaya kinavyojitokeza katika dondoo hili (alama 2)
- “Kinaya kimetumika kwingine katika hadithi husika. Thibitisha kwa kutumia hoja tisa (alama 9)
- Eleza umuhimu wa msemaji katika hadithi hii (alama 5)
-
- Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa (alama 13)
- Kwa kurejelea hadithi ya Shibe inatumaliza, eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza (alama 7)
SEHEMU D: Fasihi Simulizi
- Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali
Heri ujue mapema
Nasaba yetu haina woga
Woga haumei kwetu, humea kwa kina mamako.
Tulichinja jogoo na fahali ili uwe mwanaume.
Ah! Kisu cha ngariba ni kikali ajabu.
Iwapo utatikisa kichwacho.
Uhamie kwa wasiotahiri,
Ama tukwite njeku.
Mpwangu kumbuka hili,
Wanaume wa mlango wetu
Si waoga wa kisu
Wao hukatwa mchana hadi usiku
Wala hawalalamiki.
Siku nilipokatwa
Nilisimama tisti
Nikacheka ngariba kwa tashtiti
Halikunitoka chozi.
Iwapo utapepesa kope
Wasichana wa kwetu na wa mbali
Wote watakucheka
Ubaki ukinuna.
Sembe umepokea
Na supu ya makongoro ukabugia
Sema unachotaka
Usije kunitia aibu
Maswali;- Taja na uthibitishe shughuli zozote za kiuchumi za jamii ya wimbo huu (alama 4)
- Ni nani mwimbaji wa wimbo huu na anawaimbia nani? (alama 2)
- Huu ni wimbo wa aina gani? Thibitisha (alama 2)
- Mwimbaji wa wimbo huu ana taasubi ya kiume. Thibitisha kauli hii. (alama 2)
- Eleza wajibu wa nyimbo katika jamii (alama 6)
- Ijapokuwa nyimbo ni nzuri, zina ubaya wake. Thibitisha kauli hii (alama 4)
SEHEMU E: Ushairi (alama 20)
Jibu swali la 7 au la 8
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Kama dau baharini, duniya inavyoyumba,
Limeshamiri tufani, kila mmoja lakumba,
Viumbe tu hali gani!
Duniya yatishika, utahisi kama kwamba,
Vilima vyaporomoka, na kuvurugika myamba,
Viumbe tu hali gani!
Tufani hilo la kusi, languruma na kutamba,
Linapuliza kwa kasi, hapana kisichoyumba,
Viumbe tu hali gani!
Mujiwe ni kubwa sana, mfanowe kama nyumba,
Yazuka na kugongana, wala hatuna la kwamba,
Viumbe tu hali gani!
Mibuyu hata mivule, kama usufi na pamba,
Inarusha vilevile, seuze hiyi migomba
Viumbe tu hali gani!
Ni kipi kilotuliya, tuwazeni na kudumba,
Mandovu kiangaliya, yagongana na masimba,
Fisi wako hali gani!
Hata papa baharini, tufani limewakumba,
Walioko mikondoni, kila mmoja asamba,
Dagaa wa hali gani!
Mashehe wa mdaduwa, kwa ubani na uvumba,
Tufani hilo kwa kuwa, kusoze kwake kutamba,
Itokee afueni!
(Shairi la ‘Tufani’ la Haji Gora Haji, katika Tamthilia ya Maisha, uk 62)
Maswali;- Taja na ueleze mikondo ya shairi hili (alama 4)
- Eleza dhamira ya shairi hili (alama 2)
- Taja tamathali za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 2)
- Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
- Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano. (alama 3)
- Onyesha matumizi ya idhini ya kishairi . (alama 3)
- Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mjibu wa shairi hili (alama 2)
- Mdaduwa :
- Kutamba :
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo Kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.
Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi ya maua zikimtetea
Nao umande kumbusu miguuni;
Na miti yote hujipinda migogo
Kumpapasa, kumtoa matongo;
Na yeye kundelea kwa furaha
Kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha …….
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani?
Katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho.
Kuna jambo gani linalomridhisha?
Kama si kujua ni kutojua
Laiti angalijua, laiti angalijua!
Maswali:- Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili. (alama 2)
- Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili (ala. 4)
- Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili (alama 3)
- Maswali ya balagha katika shairi hili yanasisitiza maudhui yapi? (alama 2)
- Kwa kutoa mifano, bainisha vipengele vitatu vya Kimtindo katika shairi hili (alama 3)
- Eleza toni ya shairi hili (alama 2)
- Bainisha nafsineni katika shairi hili (alama 1)
- Eleza muundo wa shairi hili (alama 3)
MARKING SCHEME
-
- maelezo ya mwandishi
- Anamrejelea Bwana Kimbaumbau
- Ni baada ya Sauna kukataa kushiriki mapenzi naye
- Wote wawili walikuwa Kazini
- Ubabedume/ Taasubi ya kiume
-
- Jamaa za Kangata kupinga elimu ya mabinti zake
- Kimbaumbau kumdhulumu Naomi anapokataa kujihusisha kimapenzi naye.
- Mwimo Msubili kutotaka kukutana na mwanamke asubuhi kwa madai kuwa ni Mkosi.
- Lime na Mwanaheri kunajisiwa na vijana wahuni.
- Bwana Maya anamdhulumu mamake Sauna kwa mapigo na matusi aulizapo swali lolote lile.
- Kuuzwa kwa Pete kwa Fungo ili wazazi wake wapate pesa za kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.
- Pete anabakwa na mlevi anapolewa chakari
- Mamake Zohari kuridhia kila asemalo mumewe na kushidwa kumtetea anapopata himila.
- Mamake Mwangeke aliwahi kumwonya kulia kama msichana. Hii ni ishara kuwa jamii yamwona mwanamke kama mnyonge.
- Mwanzi anakataa kukubali matokeo ya uchaguzi madhali anashindwa na mwanamke, Mwekevu.
- Wahafidhina kuamini kwamba mtoto wa kiume ndiye pekee anayestahili kuwa mrithi wa mali ya babake.
- Ushindi wa Mwekevu unaonekana kama kutoheshimiwa kwa mwanaume.
- Mwekevu kusingiziwa wizi wa kura anapomshida Mwanzi.
- Kutishwa, kutusiwa na hata kutengwa kwa Mwekevu anapojitosa katika siasa zilizoaminiwa kuwa ni za wanaume
- Fungo anamharibia Pete maisha anapomwoa kisha kumfukuza anapojifungua mtoto.
- Mwanamke kuonekana kama mnyonge anayestahili kulia akabiliwapo na vizingiti au changamoto maishani. Mwanaume hafai kulia
- maelezo ya mwandishi
-
- maneno haya ni ya sauti ya mzee Kenga mawazoni mwa Majoka. Haya yanatendeka katika Ofisi ya Mzee Majoka wakati Husda na Ashua wanapigana. Majoka anakumbuka ushauri wa Kenga wa jinsi ya kumnasa Ashua kwa kusababisha fujo baina yake na Husda
-
- Kumwaga kemikali na taka sokoni licha ya kuwa wananchi wanakaa na kufanyia biashara zao katika soko.
- Kuwatumia wahuni kunyamazisha wapinzani. Mzee Kenga anakutana na Wahuni chini ya mbuyu ambao baadaye wanamwumiza Tunu.
- Kuruhusu dawa za kulevya na wanafunzi ambao wanakuwa makabeji
- Kuwaua wapinzani, kama vile vijana watano walioandamana
- Kuwatumia polisi kuwaua na kurushia waandamanaji risasi na vitoa machozi.
- Kuwanyima wafanyakazi haki, kama vile walimu na wauguzi wanaongezewa asilimia ndogo ya mshahara kasha kupandisha kodi.
- Utawala kuruhusu uuzaji wa pombe haramu kinyume na katiba, ambao umesababisha vifo na kufanya watu kuwa vipofu.
- Kufungulia biashara ya ukataji miti ilhai watu wanategemea miti hiyo kuboresha mazingira.
- Kufunga kituo cha runinga ya Mzalendo kwa kuonyesha mkutano wa Tunu na wapinzani wengine wa utawala.
- Utawala kutumia vyombo vya dola kuwafukuza watu wanaoenda sokoni na kuweka ulinzi mkali licha ya kuwa ulikuwa uwanja wa umma.
- Kuwarushia wakazi vijikaratasi vyenye ujumbe hasimu wakitakikana wapahame mahali ambapo wamekuwa wakiishi kwa muda wote wa uhai wao.
-
- Kenga anamshauri Majoka amwalike Ashua na Husda ili patashika itokee, naye Majoka apate jinsi atakavyolipiza kisasi kwa Sudi kwa kukataa kuchonga kinyago.
- Anamshauri Majoka atangaze kuwa maandamano ni haramu kisha anawamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi dhidi ya umma unaondoa maandamano.
- Majoka anakataa Suala la polisi kutumia nguvu zaidi lakini Kenga anamwambia “Acha moyo wa huruma….. Siasa na hisia haziivi kwenye chungu kimoja ndugu yangu.
- Anakubali pendekezo la Majoka la kufunga Runinga ya Mzalendo kwa kupeperusha matangazo ya mkutano moja kwa moja.
- Kenga alihusika katika kupanga mauaji ya Jabali kwani Majoka anamsifu kwa kupanga hilo na hata wanapigishana Konzi
- Anaibua pendekezo la kumuua Chopi kwa kutofuata maagizo ya kumuua Tunu akisema, “Nafikiri Chopi lazima aende safari.”
- Anamwambia Majoka kuwa si kweli kwamba watu watampigia Tunu kura na kusema, “Tunu hawezi kupigiwa hata!”
- Anapendekea kukusanya kodi ya juu na kukataa kuitumia vyema na kwa njia halali k.v. kutoa taka.
-
- Fafanua mbinu kumi anazotumia Majoka katika uongozi wake.
- Uvumi kwa mfano – Sudi na Ashua wanaiwinda roho ya Tunu
- Ahadi za uwongo – kutoa chakula kwa wasiojiweza
- Zawadi - keki za uhuru
- Vitisho - Akiwa chopi watamwaga unga
- Mapendeleo - Tunu na Ashua walipewa kazi wakakataa. Ashua angekuwa mwalimu mkuu katika shule mojawapo za Majoka kama angekubali.
- Sela - Wanaompinga wanafungwa jela k.v. Sudi anasema amefungwa mara nyingi katika jela alikofungwa Ashua.
- polisi - polisi wanatawanya waandamanaji
- Mabavu - Madai ya kuwafukuza wafadhili wa wapinzani ili wavunje kambi zao Sagamoyo, Nguvu zaidi kutawanya waandamanji
- Kudhibiti vyombo vya dola - Majoka kutaka kufunga vituo vyote kibaki Sauti ya Mashujaa
- Ulaghai - mf. Kuongeza mishahara ya walimu na wauguzi kisha kupandisha kodi.
- mavamizi - mf. Tunu kuvamiwa na kuvunjwa muundi
- Ulinzi - Majoka ana walinzi wengi. (10 x 1 = 10)
- Ishara
- Kinyago cha kike kinachochongwa na Sudi na kukiita shujaa halisi wa Sagamoyo kinaashiria shujaa wa kike atakayelikomboa Jimbo la Sagamoyo dhidi ya uongozi dhalimu
- Fimbo ya Kenga yenye kichwa cha Nyoka ni ishara ya jinsi alivyokuwa katili kwa raia. Kwa mfano, anamuua Jabali
- Uchafu wa soko ya chapakazi ambao unamsababisha hata Mzee Kenga kuziba pua yake anapoenda huko ni ishara ya maovu yaliyokithiri jimboni Sagamoyo.
- Kitendo cha Majoka kuzungumza na babu yake anapozirai ni ishara kuwa wafu walikuwa wakimwita madhali naye aliokuwa amewaua
- Majoka kuvaa mkufu shingoni wenye kidani cha umbo la swila ni ishara ya namna Majoka alivyokuwa hatari kwa maisha ya raia wa jimbo la Sagamoyo.
- Kujaa kwa maziara jimboni Sagamoyo hadi hakuna nafasi ya kuwazika wafu wengine ni ishara ya mauaji yaliyokuwa yametekelezwa na Majoka.
- Kilio na machozi mengi ndani ya ziwa lililofunika damu ni ishara ya raia waliouliwa na Majoka wanalilia haki yao.
- Kutojaa kwa raia jinsi ilivyo kawaida katika mkutano wa kuadhinisha sherehe za uhuru pamoja na siku ya kuzaliwa kwa Majoka ni ishara ya raia kuasi Majoka kutokana na uongozi wake dhalimu.
- Hali ya Majoka kujiona ndani ya ziwa lililofurika damu ni ishara ya mauaji mengi ya raia aliyokuwa akitekeleza katika uongozi wake.
- Damu ya Jabali anayoiona Majoka ikitiririka mikononi mwake akiwa amezirai ni ishara kuwa yeye ndiye aliyemuua Jabali
- Fafanua mbinu kumi anazotumia Majoka katika uongozi wake.
-
- Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
Haya ni maneno ya Jairo. Anahutubu katika sherehe ya kumuaga mwalimu Mosi ambaye alikuwa anastaafu kutoka kazi ya ualimu. Sherehe hii ilifanyika shuleni. Jairo anamkosoa mwalimu Mosi kumpatia matumaini ya uongo masomoni ilhali alijua hawakuwa na uwezo wa kimasomo badala ya kumruhusu aende ajaribu mbinu nyingine ya kujikimu kimaisha ili awe mtu wa maana katika jamii. - Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza (alama 2)
Jairo anamkosoa mwalimu kwa kumfunza na kumpa matumaini maishani badala ya kumwachilia mapema aende akaibe na kuua. Jairo analodokeza hapa ni kuwa ili mtu awe wa maana ni lazima aibe na aue. - “Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu” Thibitisha (ala. 9)
- Ni kinaya kwa Jairo kudai ili mtu awe wa maana, athaminiwe na kuitwa mhesimiwa na kuwa bingwa lazima aibe, apore au aue
- Ni kinaya kwa Jairo kuuona uelekezi na ushauri wa mwalimu wake kama upotoshi na upotezaji wa muda. Jairo anadai alipotezewa muda kwa kupatiwa matumaini ya uongo.
- Ni kinaya pia kwa mwalimu Mosi kutaka ahutubie mtu ambaye atamkosa badala ya kumsifu.
- Ni kinaya kwa Jairo kuona elimu haina manufaa yeyote ilhali wenzake walifaidi kutoka kwa elimu ya mwalimu wao.
- Ni kinaya kwa Jairo kumtoa bintiye na mkewe kama zawadi kwa mwalimu wake kama shukrani ya zawadi anazompa. Ni kinaya kwa mtu kubadili mkewe kama zawadi.
- Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa pombe ni kiliwazo cha kimawazo kinachomsahaulisha masibu ya maisha na kumkosoa mwalimu wake kwa kumwonya dhidi ya matumizi ya pombe.
- Ni kinaya kwa mkewe jairo kukubali kitendo cha mumewe Jairo kumtoa kama zawadi kwa familia nyingine. Anakubali kubadilishwa na mali.
- Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa ufuska ndio raha ya maisha na kuwa uaadilifu haufai. Anadai kuwa maisha ni bora bila nasaha za mwalimu.
- Ni kinaya kwa mkewe mwalimu Mosi, Sera kukubali na kumkaribisha mwanamke mwingine na watoto wake kwenye familia yake.
- Umuhimu wa msemaji katika hadithi (alama 5)
- Ni kielelezo cha utovu wa nidhamu miongoni wa wanafunzi. Anakunywa pombe na hata kujihusisha katika ufuska.
- Kupitia kwake uwajibikaji wa mwalimu Mosi unajitokeza. Kama mwalimu alimkanya kunywa pombe na hata ufuska.
- Anaendeleza maudhui ya umaskini katika hadithi.
- Anakuza sifa za wahusika wengine kama vile Mwalimu Mosi.
- Ametumiwa kudhihirisha ukweli wa methali “asante ya punda ni mateke.”
- Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
-
- Masharti ya Kisasa
- Mwanaume humposa mwanamke. Dadi alienda nyumbani kwa Kidawa kumposa
- Mwanamke ndiye huamua wakati wa kuolewa na nani wa kumwoa. Kidawa alimchagua Dadi baada ya muda mrefu.
- Ndoa huandamana na masharti. Dadi alipewa masharti na Kidawa ili akubali kuolewa naye.
- Wanandoa hufanya kazi pamoja ili kukithi mahitaji ya nyumbani. Dadi anachunza samaki na Kidawa ni metroni
- Wanaume hawafurahi wake wao wanapotangamana na wanaume wengine. Kidawa anaposimama kuongea na wanaume, Dadi anadhika sana.
- Wanandoa husaidiana kazi za nyumbani, Dadi anasaidia kidawa kazi za nyumbani kama vile kuosha vyombo na kufagia.
- Wanandoa wanapanga uzazi, Dadi na Kidawa wanapanga kuwa na mtoto mmoja pekee.
- Mwanamke anaajiriwa. Kidawa aliajiriwa shuleni kama metroni.
- Mwanamke anajinunulia nguo na fashoni nyingine. Kidawa ananunua viatu na kanzu anayovalia kwenda kazini.
- Ndoa imekosa uaminifu. Dadi anashuku kuwa Kidawa ana mapenzi na mwalimu mkuu.
- Kiwango cha elimu si kikwazo katika ndoa. Kidawa anaolewa na Dadi licha ya kuwa ana kisomo cha juu kuliko Dadi.
- Mwanamke amekengeuka. Kidawa anapenda fashoni.
- Wote wawili. Mwanamke na mwanaume wanachangizana nyumbani.
- Kuna makubaliano ya kufanya mambo kwa pamoja. (13 x 1 = 13)
- Shibe inatumaliza
- Mzee Mambo hafanyi kazi wizarani ilhali analipwa mshahara mkubwa kuliko Sasa na Mbura wanaofanya kazi wizarani
- Mambo anatumia runinga ya taifa inayofaa kuufahamisha umma masuala ya taifa lao kwa maslahi yake. Anaitumia kupeperusha sherehe inauofahamika nyumbani kwake.
- Mambo anaifilisi serikali kwa kutumia pesa za serikali kugharamia sherehe zake binafsi. DJ na wenzake wanalipwa mabilioni ya pesa za serikali kwa kusimamia sherehe hii.
- DJ anaipunja serikali kwa kutumia mtaji wa bohari kuu ya dawa za serikali kufungua duka lake la dawa.
- DJ anaifilisi serikali kwa kupokea huduma za maji, umeme na matibabu bure ilhali wananchi maskini wanazilipia.
- Wafanyakazi wa umma wanaibia serikali saa za kazi. Sasa na Mbura wanahudhuria sherehe zilizofanyika kwa Mambo siku nzima ilhali walipaswa kuwa kazini.
- Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kwa maslahi yake binafsi. Kwa mfano, anayatumia kusomba maji, chakula, kuwaleta jamaa wa Mambo shereheni na mapambo.
(7 x 1 = 7)
- Masharti ya Kisasa
-
- Shughuli za kiuchumi
- Ufugaji / wafugaji – Anayeimbiwa wimbo alipozaliwa fahali alichinjwa.
- Ukulima / kilimo - Anaahidiwa shamba la migomba na maparachichi
- Nani mwimbaji wa wimbo na anamwimbia nani? (alama 2)
- Mwimbaji – mjomba
- Mwimbiwa – mpwa (mtoto wa dadake mwimbaji)
- Huu ni wimbo wa aina gani? Thibitisha (alama 2)
- Wimbo wa tohara / nyisho – mpwake anatayarishiwa kukabiliana na kisu cha ngariba
Mwanafunzi lazima athibitishe
- Wimbo wa tohara / nyisho – mpwake anatayarishiwa kukabiliana na kisu cha ngariba
- Mwimbaji wa wimbo huu ana taasubi ya kiume – Thibitisha kauli hii (alama 2)
- Anaona kuwa waoga ni akina mama
- Anasifu wanume wa mbari yao kuwa si waoga
- Akilia atachekwa na wasichana
- Anaambiwa kuwa ni “Ndume / mme” akabiliane na kisu
- Nyimbo zina wajibu gani katika jamii (alama 6)
- Huwatayarisha wanapoenda kupashwa tohara
- Hukashifu woga na kuhimiza ujasiri
- Husawiri falsafa ya jamii. Wanaume hawaogopi.
- Huonyesha majukumu mapya ya wanaotiwa jandoni
- Huleta jamii pamoja
- Hukuza na kuendeleza tamaduni na desturi za jamii
- Hutumbuiza / huburudisha
- Hukosoa / kusahihisha maovu
- Ijapokuwa nyimbo ni nzuri zina ubaya wake. Thibitisha kauli hii (alama 4)
(ubaya wa nyimbo)- Huweza kuibua hisia za ukabila na utabaka
- Hutumika kueneza propaganda. Hueneza uchochezi
- Kuna ukosefu wa maadili katika baadhi ya nyimbo. Baadhi huwa na matusi, vitendo vya ngono n.k.
- Nyimbo zinalevya/ pumbaza watu
- Husababisha uzembe
- Baadhi huwa ghali/huhitaji kiasi kingi cha pesa kununua au kutoa na kuzirekodi
- Shughuli za kiuchumi
-
- Taja na ueleze mikondo ya shairi hili (alama 4)
- Tathlitha
- Mathnani
- Msuko
- Ukara
- Sabilia
- Eleza dhamira ya shairi hili (alama 2)
- Kuzindua /kuonyesha watu jinsi maisha ya ulimwengu yalivyo na misukosuko/ matatizo
- Taja tamathali za usemi zilizotumiwa katika shairi hili (alama 2)
- Sitiari - papa, ndovu, samba, fisi dagaa – kusimamia watu
- Tashbihi - kama dau baharini, mibuyu na mivute inatikiswa kama usufi na pamba
- Eleza muundo wa shairi hili (alama 4)
- Beti 8
- Kila ubeti una mishororo mitatu
- Kila mshororo una migao 2 ila kibwagizo (cha mmoja)
- Vina vya mwisho vinatiririka lakini vya kati haritiririki
- Shairi halina kibwagizo
- Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa 5 (alama 3)
- Mibuyu na mivute inasukwa kama pamba au usufi seuze migomba hii, viumbe tu hali gani
- Onyesha matumizi ya idhini ya kishairi (alama 3)
- Tabdila - duniya, mgamba, hiyi, kiangaliya
- Inkisari - la kwamba (kuamba – kusema)
- Kuboronga sarufi
- na kuvurugika myamba
- Limeshamiri tofani
- Kila mmoja lakumba
- Mibuyu… kama usufi na pamba inarushwa
- Eleza maana ya maneno haya (alama 2
- Mdaduwa - mwenye kufanya sawa (kusawazisha)
- Kutamba - Kusambaa
- Taja na ueleze mikondo ya shairi hili (alama 4)
-
- Hali ya mzungumziwa
- Mcheshi
- Mwenye bidii
- Maskini
-
- Inkisari; babuze – babu zetu
- Kuboronga sarufi;
Aliye na kubwa hamu
Aliye na hamu kubwa
-
- Taswira sikivu, anasikiliza videge vya anga vinavyotumbuiza
- Taswira mnuso; Rihi ya maua zikimletea
- Taswira mguso; umande kumbusu miguuni
- Maswali ya balagha hukuza maudhui ya unyanyasaji
Pia kunyimwa haki kwa binadamu maskini -
- Tashihisi - umande kumbusu miguuni
- Kinaya - kuwa mrejelewa anafuraha ilhali anafanya kazi za sulubu (kulima)
- Tashibihi - Tabasamu kama mtu aliye na kubwa hamu
- Huruma - mateso mrejelewa anayoyapitia
- Mchunguzi / mpita njia wa karibu na mrejelewa
-
- Beti tatu
- Mistari mishata
- Mishororo haina mizani sawa
- Hakuna urari wa vina
- Hali ya mzungumziwa
Download Kiswahili Paper 3 Kenya High Post Mock Exams 2020 - Questions and Answers.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students