Kiswahili Paper 3 Questions - Kapsabet Boys Post Mock 2023 Exams

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; Riwaya, Ushairi, Hadithi fupi na Fasihi Simulizi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.


MASWALI

SEHEMU YA A: TAMTHILIA
T.M Arege: Bembea ya Maisha

  1. LAZIMA
    1.  Tumbo lenyewe limeshafanya mazoea. Ardhi hiyo ya kulimwa na kuzalisha chakula iko wapi? Hata ingekuwepo mvua yenyewe imefanya ugeni. Imeadimika afadhali wali wa daku. Sasa ni wakati wa kujifunga masombo…
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      2. Fafanua sifa za msemaji wa maneno haya. (alama 2)
      3. Eleza vipengele vinne vya kimtindo vinavyobainika katika dondoo hili. (alama 4)
    2. Eleza jinsi maudhui ya uwajibikaji yanavyojitokeza katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. (alama 10)

SEHEMU B: RIWAYA A. Matei: Chozi la Heri
Jibu swali la 2 au la 3

  1. “Anayeusikiliza wimbo huu anauona mrefu kuliko zile ambazo mja huyu huimba kila siku.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Eleza aina ya “wimbo huu”. (alama 2)
    3. Eleza aina mbili za taswira zinazojitokeza kwenye “wimbo huu”. (alama 4)
    4. Eleza maudhui mbalimbali yanayojitokeza kwenye “wimbo huu”. (alama 10)
  2.  “Nakumbuka asubuhi ya pili baada ya mtafaruku kuanza. Nilikuwa sebuleni na mwanangu tukitizama runinga”.
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 6)
    3. Tambua mbinu kuu ya kimtindo iliyotumika katika dondoo. (alama 2)
    4. Kwa kutolea mifano mwafaka eleza jinsi mbinu uliyotaja hapo juu ilivyotumika kukuza
      maudhui riwayani. (alama 8)

SEHEMU YA C: USHAIRI
Jibu swali la 4 au la 5

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Mtu ni afiya yake, ndio uzima wa mtu,
    Mtu ni kuwa na chake, hakuwi ela kwa kitu,
    Mtu ni bahati yake, kupendekeza kwa watu,
    Mtu si fakhari kwake, kuitwa nyama ya mwitu.

    Mtu ni ulimi wake, kunena vyema na watu,
    Mtu ni kijungu chake, kuweka mawe matatu,
    Mtu ni mwenda kwa lake, mtoshwa na kila kitu, Mtu si uzuri kwake, kuitwa nyama ya mwitu.

    Mtu ni mwenye nadhari, apimaye kila kitu,
    Mtu ni moyo hariri, mwenye imani na watu,
    Mtu ni alo na ari, shika sana mwana kwetu,
    Mtu si yake fakhari, kuitwa nyama ya mwitu.

    Mtu ni mkono wazi, mtasada kuna watu,
    Mtu ni mwenye maozi, ku oneya kila kitu,
    Mtu ni alo tulizi, asopenda utukutu,
    Mtu si jambo pendezi, kuitwa nyama ya mwitu.

    Mtu ni mwenye ahadi, ndio u’ngwana na utu,
    Mtu ni alo baridi, mbe mbelezi wa watu,
    Mtu ni moyo asadi, aso onewa na mtu,
    Mtu si yake ifadi, kuitwa nyama ya mwitu.
    Mtu niliyo yanena, pima sana ewe mtu,
    Mtu si kujatukana, kukirihi nyoyo watu, Mtu nakupa maana, wende nyendo za kiutu, Mtu si uzuri sana, kuitwa nyama ya mwitu.

    Maswali
    1. Jadili ujumbe wa mshairi. (alama 2)
    2. Ainisha shairi kutegema: (alama 2)
      1. Mpangilio wa maneno.
      2. Vina.
      3. Idadi ya mishororo.
      4.  Idadi ya vipande.
    3. Eleza mbinu nne za kimtindo ambazo zimetumiwa. (alama 4)
    4. Thibitisha matumizi ya uhuru wa kishairi. (alama 3)
    5. Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi. (alama 4)
    6. Fafanua nafsi-neni na nafsi-nenewa katika shairi hili. (alama 2)
    7. Kwa kutolea mifano, eleza aina tatu za urudiaji zinazojitokeza kwenye shairi hili. (alama 3)
  2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Nikiwa na njaa na matambara mwilini,
    Nimehudumika kama hayawani,
    Kupigwa na kutukanwa,
    Kimya kama kupita kwa shetani,
    Nafasi ya kupumzika hakuna,
    Ya kulala hakuna,
    Ya kuwaza hakuna,
    Basi kwani hili kufanyika,
    Ni kosa gani lilotendeka,
    Liloniletea adhabu hii isomalilizika?

    Ewe mwewe urukaye juu angani,
    Wajua lililomo mwangu moyoni,
    Niambie pale mipunga inapopepea,
    Ikatema miale ya jua,
    Mamangu bado angali amesimama akisubiri?
    Je nadhari hujitokeza usoni, Ikielekea huku kizuizini?

    Mpenzi mama, nitarudi nyumbani,
    Nitarudi hata kama ni kifoni,
    Hata kama maiti yangu imekatikakatika,
    Vipande elfu, elfu kumi, Nitarudi nyumbani,
    Nikipenya kwenye ukuta huu, Nikipitia mwingine kama shetani,
    Nitarudi mpenzi mama…Hata kama kifoni!

    Maswali
    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
    2.  Tambua nafsi-neni katika shairi hili. (alama 2)
    3. Eleza toni mbili zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 2)
    4.  Eleza mambo manne ambayo mshairi analalamikia. (alama 4)
    5. Fafanua dhamira katika shairi hili. (alama 2)
    6. Thibitisha kuwa hili ni shairi huru. (alama 2)
    7. Taja na ufafanue sifa mbili za nafsi neni. (alama 2)
    8.  Fafanua mbinu tatu za kimtindo zilizotumika katika ubeti wa tatu. (alama 3)
    9. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili. (alama 2)
      1. Hayawani
      2. Nadhari

SEHEMU D: HADITHI FUPI
D.W Lutomia na P. Muthama(wah): Mapambazuko ya Machweo na Hadithi nyingine
Jibu swali la 6 au la 7
D.W Lutomia: Msiba wa kujitakia

  1. “Wetu ni wetu, hata akiwa mbaya…ni wetu.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Eleza sifa za huyu anayeshikilia msimamo wa “mtu wetu”. (alama 2)
    3. Eleza mbinu mbili za kimtindo zinazojitokeza kwenye dondoo hili. (alama 4)
    4. Kwa kurejelea hadithi “Msiba wa Kujitakia”, eleza misimamo mbalimbali ya mwandishi. (alama 10)
      R.Wangari: Fadhila za Punda
  2.  
    1. Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho. (alama 10)
      Alasiri ile, baada ya ibada mbili, mhubiri akawa hoi kwa mavune. Akatamani kufika nyumbani apumzike, kazi ya kuwalisha kondoo wa Mungu si kazi rahisi. Wamefika nusu safari, bintiye katulia kama maji mtungini. Akimtazama kipembe, anamkumbusha marehemu mkewe.Miaka mitatu sasa na dhiki ya kuondokewa haijamwisha. Alihisi ukiwa, akatamani mwenziye.Sasa kazi kukilea kitoto chao, kibinti hiki kilicho mlanda mamake kama shilingi kwa ya pili. Nyumba ilijaa kicheko alipokuwa hai mamake Lilia. Kama si bintiye ambaye ulimi wake hautulii, kihoro kingemvamia labda hata kumvuta kuelekea kaburini. Lakini Lilia, malaika wake, hampi utulivu wa kuwaza sana kuhusu upweke wake. Ilimshangaza sasa kuwa kanyamaza vile. Kumbe kwa muda tu!
    2. Kwa kutolea mifano mwafaka eleza jinsi hadithi “Kila Mchezea Wembe” ilivyotumia kinaya
      kufanikisha ujumbe wake. (alama 10)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
      Ikiwa kweli wewe ni mkaza mwanangu,
      Nami ndimi nilompa uhai mwana unoringia,
      Anokufanya upite ukinitemea mate,
      Chakula kuninyima, wajukuu kunikataza ushirika,
      Mungu na waone chozi langu, wasikie kilio changu,
      Mizimu nawaone uchungu wangu, radhi zao wasiwahi kukupa,
      Laana wakumiminie, uje kulizwa mara mia na wanao,
      Usiwahi kufurahia hata siku moja pato lao,
      Watalokupa likuletee simanzi badala ya furaha,
      Wakaza wanao wasikuuguze katika utu uzima wako!
      1. Tambua aina ya mazungumzo haya na utoe sababu. (alama 2)
      2. Eleza sifa mbili za nafsi nenewa. (alama 2)
      3. Taja na ueleze sifa nne za kipera hiki cha fasihi simulizi. (alama 4)
      4.  Unanuia kutumia mbinu ya maandishi kuhifadhi kipera hiki cha fasihi simulizi. Eleza
        faida na hasara za kutumia mbinu hii. (alama 6)
    2. Eleza faida tatu na hasara tatu za miviga . (alama 6)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions - Kapsabet Boys Post Mock 2023 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?