MAAGIZO KWA MTAHINIWA:
- Karatasi hii ina maswali manne.
- Jibu maswali mawili pekee.Kila swali lina alama 20.
- Swali la kwanza ni la lazima. kisha chagua swali la pili kutoka miongoni mwa matatu yaliyosalia.
- Majibu yote yaandikwe katika lugha ya Kiswahili.
- Visa vingi vya udaganyifu katika mtihani wa kitaifa wa kuhitimu cheti cha sekondari vimekuwa vikiripotiwa nchini mwako kila uchao. Andika barua kwa mhariri kuhusu suala hili
- Serikali za magatuzi zitainua kiwango cha maendeleo nchini. Jadili.
- Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mchagua nazi hupata koroma.
- Andika insha itakayoanza kwa maneno haya:
Milipuko mikubwa ilisikika pu! Pu! Puu! Kisha niliwaona watu wakikimbia kuelekea pande zote…
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
- Hii ni insha ya kiuamilifu na kwa hivyo ina sura maalum. Hii insha iwe na kichwa mfano ifuate mtindo wa barua rasmi
Sababu za udanganyifu kutokea, mfano- Shinikizo kuwa wavyele wanataka wanao kupasi
- Ushindani baina ya shule mbalimbali
- Shinikizo la marafiki
- Walimu kutaka masomo yao kuongoza
- Shule kutaka hadhi ya shule kudumu
- Kutaka kupata nafasi ya digrii bora/kozi bora katika chuo kikuu
Njia zinazowezesha udaganyifu- Matumizi ya rununu / simu
- Wasimamizi wa mitihani kutomakinika
- Ulegevu wa baraza la mitihani kwamba hapana mikakati madhubuti ya kukabiliana na udaganyifu
- Kuwepo kwa mtandao na vitandazi vya kijamii kuwasiliana
Mapendekezo - Baraza la mitihani kuwajibika
- Adhabu kali kutolewa kwa wahusika
- Kuwajibika kwa wasimamizi wa mitihani
- Watahiniwa kufuzwa umuhimu wa kukwepa udaganyifu katika mitihani
- Serikali za magatuzi zitainua kiwango cha maendeleo nchini. Jadili.
Zingatia baadhi ya hoja- Serikali zilizojikita mashinani
- Huduma anuai zitapatikana karibu na wananchi
- Mali ya asili itazalishwa pakubwa
- Faida itatumika kuongeza / kuleta ushuru wa kaunti / gatuzi
- Miundo msingi itaimarishwa sana
- Ufisadi utapungua
- Kila gatuzi litapania kuwa bora kimaendeleo
- Umaskini utapunguka kwa kiasi kikubwa
- Uzalendo utaimarika
- Mchagua nazi hupata koroma. Sharti aelewa kuwa ni methali.
- Atunge kisa ambacho kinaoana vizuri na maana ya matumizi ya methali hii.
- Kisa chake kiwe cha kuvutia.
- Sharti aonyeshe pande mbili za methali.Aonyeshe mhusika anayechagua kitu au jambo zuri lakini analikosa na kupata lingine la kiwango cha chini.
- Anatakiwa kuonyesha kuwa tusiwe watu wa kuchagua vitu bali tufanye bidii kupata tunachokihitaji.
- Andika insha itakayoanza kwa maneno haya:
Milipuko mikubwa ilisikika pu! Pu! Puu! Kisha niliwaona watu wakikimbia kuelekea pande zote…- Ni sharti mtahiniwa aanze kwa maneno aliyopewa.
- Anatakiwa kuanza kwa maneno yale bila ya kubadilisha wala kuyapunguza.
- Kisa chake kiwa cha kuvutia na aonyeshe ni matukio yapi yaliyosababisha milipuko ile, kulikuwa na majeruhi na watu walitoroka kwenda wapi? Ni nini kilichotokea baada ya hapo?
- Asipoanza kwa maneno aliyopewa atuzwe alama ya bakshishi
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 3 Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students