Viambishi - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

 • Kiambishi ni silabi inayofungamanishwa na mzizi wa neno ili kuleta maana iliyokusudiwa. Viambishi havina maana kamilifu peke yake: huhitaji kufungamanishwa na mzizi wa neno. Kwa hivyo, kiambishi ni mofimu tegemezi inayoongeza maana fulani katika neno kama vile ngeli, wakati, hali, mnyambuliko wa kitendo n.k


Aina za Viambishi

 • Kuna aina mbili kuu za viambishi:
  1. Viambishi Awali
  2. Viambishi Tamati

Viambishi Awali

 • Viambishi hivi hutokea kabla ya mzizi ya neno/shina la kitenzi. Kuna aina kadhaa za viambishi hivi kama vile viambishi viwakilishi vya nafsi, ngeli, mahali, wakati, hali n.k

Viambishi Viwakilishi vya Ngeli

 • Hizi ni silabi zinazowakilisha ngeli katika neno. Mfumo wa ngeli unaokubalika hutumia viambishi hivi kubainisha ngeli mbali mbali.
  k.m:

  a-me-avy-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya A-WA(umoja)
  zi-ta-pasuk-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli I-ZI wingi
  ki-li-pote-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI(umoja)
  ya-na-angaz-iw-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya LI-YA(wingi)

Viambishi Viwakilishi vya Nafsi

 • Hivi ni viambishi ambavyo huonyesha nafsi katika neno. Kuna aina mbili za viambishi viwakilishi vya nafsi:
  1. Viambishi Viwakilishi vya Nafsi ya Mtendaji/Mtenda
   - Hutumika kuonyesha aliyefanya kitendo katika neno.
   - Kama viambishi vya Ngeli ya Mtendaji, v
   iambishi hivi ndivyo vinavyotangulia viambishi vingine katika kitenzi.
   NAFSI UMOJA  WINGI  MFANO
   YA KWANZA  NI TU ni-na-andik-a, tu-li-shind-a
   YA PILI U M u-me-kasir-ik-a, m-na-pig-w-a
   YA TATU A WA a-li-simam-a, wa-ta-p-ew-a

  2. Viambishi Viwakilishi vya Nafsi ya Mtendewa/Mtendwa
   - Hutumika kuonyesha nafsi ya aliyeathirika na kitendo katika neno. Kama viambishi viwakilishi vya ngeli ya mtendewa, mara nyingi viambishi hivi huwekwa punde kabla ya shina la kitenzi.
   - Viambishi viwakilishi vya mtendewa ni sawa na viambishi viwakilishi vya mtendaji isipokuwa:
   NAFSI YA MTENDEWA  KIAMBISHI  MFANO
   YA PILI UMOJA KU zi-me-ku-fik-i-a
   YA PILI WINGI M, MU, WA  ni-na-wa-tum-a
   YA TATU UMOJA M ni-ta-m-tambu-a

Viambishi Viwakilishi vya Wakati/ Hali

 • Hivi ni viambishi ambavyo vinapowekwa kabla ya shina la kitenzi, vinatufahamisha wakati kitendo hicho kilipofanyika.
 • Viambishi hivi ni:
  KIAMBISHI  HUWAKILISHA: MFANO
  LI wakati uliopita ki-li-chom-ek-a
  ME wakati timilifu (uliopita muda mfupi)  zi-me-anguk-a
  NA wakati uliopo tu-na-ku-subir-i
  TA wakati ujao wa-ta-ni-ju-lish-a
  HU wakati wa mazoea hu-som-e-a
  A wakati usiodhihirika a-tu-pend-a
  KA wakati usiodhihirika zi-ka-teket-e-a
  PO PO ya wakati a-li-po-wasil-i
  KI KI ya masharti ni-ki-zi-angali-a

Viambishi Viwakilishi vya Kukanusha Wakati

 • Viambishi hivi hutumika kukanusha kitenzi katika sentensi kulingana na wakati au hali
  KIAMBISHI HUKANUSHA MFANO
  KU wakati uliopita ha-ku-ingi-a
  JA wakati timilifu (uliopita muda mfupi)  si-ja-ku-uliz-i-a
  -I* wakati uliopo na wa mazoea ha-som-i
  TA wakati ujao ha-ki-ta-maliz-ik-a
 • Tanbihi: * Tunapokanusha wakati uliopo, wakati wa mazoea na wakati usiodhihirika, tunatumia kiambishi kiishio(I) badala ya kutumia kiambishi tamati.
  k.m:si-ku-ju-i, ha-pat-ik-an-i

Viambishi Viwakilishi vya Kukanusha Nafsi

 • Tunapokanusha kitenzi, kiambishi cha kwanzwa hubadilika kulingana na nafsi.
  KIAMBISHI  MATUMIZI MFANO
  SI nafsi ya kwanza  si-ku-wa-on-a
  HU nafsi ya pili hu-ni-faham-u
  HA nafsi ya tatu ha-ta-chuku-a


Viambishi Virejeshi vya Ngeli

 • Hurejelea ngeli ya mtendewa au mtendwa na hutumika hasa katika vishazi tegemezi (vyenye o - rejeshi) k.m:
  • wa-li-cho-ni-tum-i-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya KI-VI
  • ni-ta-ka-ye-m-salim-i-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya A-WA
  • u-li-ko-ji-fich-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya mahali KU
  • tu-li-po-pa-safish-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya mahali PO

Viambishi vya ngeli

 • Ni viambishi vile ambavyo husimamia ngeli katika kitenzi ili kuonyesha mtenda au mtendwa.
  k.m: (vitabu) vilivyonunuliwa
  (vi-li-vyo-nunul-il-w-a)  => vi- na -vyo- ni viambishi vya ngeli.

Viambishi Tamati

 • Viambishi tama hutokea baada ya shina la kitenzi na hutumika kutuarifu kauli au myambuliko wa kitenzi hicho.

Viishio

 • Katika kauli ya kutenda, vitenzi vyenye asili ya Kibantu huishia kwa sauti "-a". Kwa mfano: a-na-omb-a, tu-li-zo-andik-a

  Tanbihi: Tunapokanusha vitenzi hivi vyenye asili ya Kibantu katika wakati uliopo na wakati wa mazoea, kiishio "-a" hubadilika na kuwa "-i" Kwa mfano: Ha-pat-ik-an-i, Si-ku-ju-i
 • Vitenzi vyenye asili ya kigeni huchukua viishio tofauti kama vile e, i na u katika kauli ya kutenda. Kwa mfano: ha-wa-ja-tu-jib-u, a-na-tu-subir-i, ni-me-ku-sameh-e
 • Hata hivyo katika kauli nyinginezo (isipokuwa kauli ya kutenda) vitenzi hivi vya kigeni huchukua kiishio "a". k.m harib-ik-a, tu-me-jib-iw-a

Viambishi Viwakilishi vya Kauli ya Kitenzi

 • Hubadilika kulingana na mnyambuliko wa kitenzi.
  KAULI KIAMBISHI MFANO
  KUTENDEA e, i omb-e-a, pig-i-a,
  KUTENDEANA  ean, ian omb-ean-a, pig-ian-a,
  KUTENDWA w som-w-a
  KUTENDEWA ew, iw omb-ew-a, pig-iw-a
  KUTENDEKA ek pend-ek-a
  KUTENDESHA  esh, ez, ish, iz  kom-esh-a, ing-iz-a
  KUTENDANA an finy-an-a


Uainishaji wa Neno

 • Kuainisha ni kugawa neno katika viambishi vyake mbalimbali. Tunapoainisha neno, tunaonyesha mzizi wa neno pamoja na viambishi vyote vilivyofungamanishwa kuunda neno hilo.

 

Mifano:

Ainisha maneno yafuatayo:

 1. nitasoma → ni-ta-som-a

  ni → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja
  ta → kiambishi kiwakilishi cha waka= ujao
  som → shina la kitenzi cha kusoma
  a → kiishio

 2. walipozipata → wa-li-po-zi-pat-a

  wa → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili wingi
  li → kiambishi kiwakilishi cha waka= uliopita
  po → kiambishi kiwakilishi cha po ya wakati au cha ngeli ya mahali PO
  zi → kiambishi kiwakilishi cha kitendwa, ngeli ya I-ZI wingi
  pat → shina la kitenzi cha kupata
  a → kiishio

 3. vimeshikamana → vi-me-shik-aman-a

  vi → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI wingi
  me → kiambishi kiwakilishi cha waka= uliopita muda mfupi
  shik → shina la kitenzi cha kupata
  aman→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendamana
  a → kiishio

 4. mnayemkimbilia → m-na-ye-m-kimbi-li-a

  m → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili wingi
  na → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo
  ye → kiambishi kirejeshi cha nafsi ya tatu
  m→ kiambishi kiwakilishi cha mtendewa, nafsi ya tatu umoja
  kimbi → mzizi wa kitenzi cha kukimbia
  li → kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendea
  a → kiishio

 5. yakimwagika → ya-ki-mwag-ik-a

  ya → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya YA-YA
  ki → kiambishi kiwakilishi cha KI-ya masharti au au cha KI-ya kuendelea
  mwag → mzizi wa neno mwaga
  ik→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendeka
  a → kiishio
 6. hawakukushibisha → ha-wa-ku-ku-shib-ish-a

  ha → kiambishi kiwakilishi cha kukanusha
  wa → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya tatu wingi
  ku → kiambishi kiwakilishi cha kukanusha waka= uliopita
  ku → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili mtendewa
  shib → mzizi wa kitenzi cha kushiba
  ish→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendesha
  a → kiishio

 7. lililolililia → li-li-lo-li-li-li-a

  li → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya LI-YA umoja
  li → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopita
  lo → kiambishi kirejeshi cha ngeli ya LI-YA umoja
  li→ kiambishi kiwakilishi cha mtendewa, ngeli ya LI-YA
  li → shina la kitenzi cha kulia
  li → kiambishi kiishio cha kauli ya kutendea
  a → kiishio
Join our whatsapp group for latest updates

Download Viambishi - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest