Ukubwa na Udogo; Umoja na Wingi - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Ukubwa na Udogo

 • Maneno huwekwa katika ukubwa au udogo yanapozidi kiasi cha wastani kinachotarajiwa. Hali ya ukubwa na udogo hutumika hasa unaposifia au kudharau kitu

Ukubwa

 • Nomino zote katika hali ya ukubwa huwa katika ngeli ya LI-YA. Tunaweka maneno katika ukubwa kwa kuongeza kiungo JI na/au kutoa kiwakilishi cha ngeli

Udogo

 • Maneno huwekwa katika udogo ili kusifia udogo wao au kudharau kiasi chake. Nomino zote katika hali ya udogo huwa katika ngeli ya KI-VI. Maneno huwekwa katika udogo kwa kuongeza kiungo ki- au kiji-.
 • Katika baadhi ya maneno, kiambishi kiwakilishi cha ngeli huachwa nje tunapoweka maneno katika udogo.

Wastani

 • Hii ni hali ya kawaida/katikati ya nomino. Si kubwa si ndogo.
  WASTANI UDOGO UKUBWA
1. mtu kijitu jitu
2. mto kijito jito
3. kitu kijikitu jikitu
4. mtoto kitoto/kijitoto toto/jitoto
5. mlango kijilango lango
6. mwiko kijimwiko/kijiko jimwiko
7. chungu kijichungu jungu
8. nyumba chumba/kijumba jumba
9. kikapu kijikapu kapu/jikapu
10. miji kijiji jiji


Umoja na Wingi

 • Sentensi za Kiswahili zinaweza kubadilishwa kutoka kwa umoja hadi wingi, kulingana na ngeli yake.
 • Baadhi ya ngeli hubaki sawia katika umoja na wingi.

 

 

 

 

Mifano ifuatayo itakuonyesha umoja na wingi wa sentensi katika ngeli mbalimbali.

Ngeli ya A-WA
1. Mtoto huyu ni mvivu sana. Watoto hawa ni wavuvi sana.
2. Mwizi aliyeiba ng'ombe wa mzee mkongwe amekamatwa na mwananchi. Wezi walioiba ng'ombe wa wazee wakongwe wamekamatwa na wananchi
Ngeli ya KI-VI
1. Kitabu chako kiko juu ya kitanda Vitabu vyenu viko juu ya vitanda
2. Chumba kile kidogo kimeangukia chungu Vyumba vile vidogo vimeangukia vyungu.
Ngeli ya LI-YA
1. Jani lile linaficha tunda kubwa ambalo limeiva Majani yale yanaficha matunda makubwa ambayo
yameiva.
2. Jiko lolote lenye kaa moto litolewe nje Meko yoyote yenye makaa moto yatolewe nje.
Ngeli ya U-I
1. Mtaa huo hauna mti wowote Mitaa hiyo haina miti yoyote.
2. Huu ndio mto uletao maji katika mji wetu Hii ndiyo mito iletayo maji katika mito yetu.
Ngeli ya U-ZI
1. Ukuta mwingine umepigwa kwa upembe Kuta nyingine zimevunjwa kwa pembe.
2. Ubao mrefu uliokuwa kwenye ua wetu ulikatwa kwa upanga mweusi Ndefu ndefu zilizokuwa kwenye nyua zetu zilikatwa kwa panga nyeusi.
Ngeli ya I-ZI
1. Nyumba iliyo karibu na barabara ile imefungwa Nyumba zilizo karibu na barabara zile zimefungwa.
2. Ndoo yenye maji imewekwa juu ya mbao kubwa Ndoo zenye maji zimewekwa juu ya mbao kubwa.
Ngeli ya U-YA
1. Uyoga uliokuwa hapa umeoza. Mayoga yaliyokuwa hapa yameoza.
2. Mhindi wa kuchoma umeibiwa. Mahindi ya kuchoma yameibiwa.
Ngeli ya YA-YA
1. Mafuta na maji hayawezi kuchanganyika Mafuta na maji hayawezi kuchanganyika.
2. Marashi haya yananukia vizuri Marashi haya yananaukia vizuri
Ngeli ya I-I
1. Sukari imemwagika kwenye changarawe hii. Sukari imemwagika kwenye changarawe hii.
2. Damu ni nzito kuliko maji Damu ni nzito kuliko maji.
Ngeli ya U-U
1. Uji uliopikwa kwa unga wa wimbi ni mtamu kuliko ule wa mtama. Uji uliopikwa kwa unga wa wimbi ni mtamu kuliko
ule wa mtama.
2 Ugali ni tamu lakini mboga haina chumvi. Ugali ni tamu lakini mboga haina chumvi.
Ngeli ya PA
1. Mahali ambapo palipandwa maua panapendeza sana Mahali ambapo palipandwa maua panapendeza sana.
Ngeli ya KU
1. Huku niliko hakuvutii kama kwangu Huku tuliko hakuvutii kama kwetu
2. Kukimbia huku kunachosha. Kukimbia huku kunachosha.
Ngeli ya MU
1 Nyumbani humu mna giza totoro Nyumbani humu mna giza totoro

Join our whatsapp group for latest updates

Download Ukubwa na Udogo; Umoja na Wingi - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest