Mwingiliano wa Maneno - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

 • Hali ya maneno kuwa na matumizi tofauti mifano:


Kiwakilishi kuwa Kivumishi

 1. Huyu analia.
 2. Mtoto huyu analia.


Kivumishi kuwa Kiwakilishi

 1. Vikombe vizuri vitavunjika.
 2. Vizuri vitaliwa.


Kivumishi kuwa Nomino

 1. Mti mrefu haupandiki.
 2. Mrefu alikufa jana jioni.


Kivumishi kuwa Kielezi

 1. Viatu vibaya vitachomwa.
 2. Uliifanya kazi vibaya.
 3. Mtu mjinga ni huyu.
 4. Anakaa mjinga.


Nomino kuwa Kivumishi

 1. Tajiri alimdharau Razaro.
 2. Mtu tajiri huheshimiwa.


Nomino kuwa Kielezi

 1. Nairobi ni mji mkuu.
 2. Amewasili Nairobi.
 3. Kitoto kinalia.
 4. Unaongea kitoto.
 5. Haraka haina baraka.
 6. Fanya haraka tuondoke hapa.
 7. Sindano ya babu imepotea
 8. Alidungwa sindano/kwa sindano na daktari.


Kielezi kuwa Nomino

 1. Niliwasili jana.
 2. Jana yangu haikuwa nzuri.


Kitenzi kuwa Nomino

 1. Nataka kulala sasa.
 2. Kulala kwake kunaudhi.


Nomino kuwa Kiunganishi

 1. Ila yake imemwathiri sana.
 2. Watu wote ila yeye walikwenda.
 3. Kichwa changu kina walakini.
 4. Nimekula walakini sijashiba.


Kielezi kuwa Kihisishi

 1. Mwenda pole hajikwai.
 2. Pole! Usijali utapona.
 3. Amepaka rangi sawasawa.
 4. Sawasawa! Siku moja tutakutana.


Kihusishi kuwa Kielezi

 1. Paka amepanda juu ya mti.
 2. Ameingia katika choo.


Kitenzi kuwa Kielezi

 1. Mtoto akilia atatapika.
 2. Aliingia akilia.


Nomino kuwa Kihisishi

 1. Gege anacheza ala yake ya muziki.
 2. Ala! Waniwekea uchafu katika chakula?
Join our whatsapp group for latest updates

Download Mwingiliano wa Maneno - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest