KISWAHILI PAPER 1 - 2019 KCSE KASSU JOINT MOCK EXAMS (QUESTIONS AND ANSWERS)

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili, insha ya kwanza ni lazima
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo zilizobakia tatu.
  • Kila insha isipungue maneno 400
  • Kila insha ina alama 20
  • Kila insha LAZIMA iandikwe kwa lugha ya Kiswahili

LAZIMA

  1. Suala la kuzorota kwa usalama nchini kenya limekuwa donda ndugu. Andika mahojiano kati ya waziri wa usalama wa kitaifa na mwandishi wa habari kuhusu chanzo na mbinu za kukabiliana na janga hili
  1. Ufisadi ndicho kikwazo kikuu cha maendeleo hapa nchini.eleza
  1. Andika kisa kinachodhibitisha ukweli wa methali.
    Jifya moja haliijiki chungu
  1. Andika insha itakayomalizikia kwa maneno; …nilitamani ardhi ipasuke nitumbukie huko nisionekane.


MARKING SCHEME

  1. Hii ni insha ya mahojiano. Mwanafunzi azingatie sura ya insha ya mahojiano asipofuata sura aondolewe alama nne. Utangulizi huwa na maelezo mafupi yanayoandikwa katika mabano. Mwanafunzi anaweza kutaja mahali pa mahojiano iwapo hakutaja katika kichwa. Mwanafunzi abuni majina/vyeo vya wahusika. Mtindo wa kitamthilia utumiwe
  2. Hisia na ishara mbalimbali huonyeshwa kwenye mabano kwa mfano vicheko, huzuni.
    Hoja[chanzo]
    • Makundi haramu
    • Uvamizi wa kigaidi
    • Mizozo ya kidini
    • Wizi wa mifugo
    • Mafunzo ya itikadi kali
    • Mtazamo hasi wa wananchi kwa walinda usalama
    • Siasa duni
    • Ukabila
    • Unasaba
    • Dawa za kulevya

      Kukabiliana
    • Hatua kali kwa wanaovuruga Amani
    • Walinda usalama kuwa imara
    • Serikali iwahami walinda usalama na vifaa vya kisasa
    • Vijana kutahadhari wasitumiwe vibaya na viongozi
    • Dini ihubiri Amani zibuniwe na nyinginezo
    • Tume za umoja na maudhiano zibuniwe kuhamasisha wananchi kuhusiana na uslama.
  1. Ufisadi kama kikwazo
    • Kazini – mapendeleo/ukabila/unasaba
    • Biashara haramu
    • Kandarasi/zabuni – kupewa wasiostahili
    • Elimu – Udanganyifu katika mitihani/kupewa alama/kufanyiwa mitihani
    • Kukwepa ushuru hasa viongozi
    • Miundo msingi kuwa mbovu kutokana na uporaji
    • Afya – hakuna madawa
    • Usalama – ugaidi
    • Mfumko wa bei/gharama ya maisha kupanda
    • Barabarani – ajali nyingi.

      TANBIHI – mtahiniwa aeleza tu/aunge mkono pekee wala asipinge kauli hii. baadhi ya watahiniwa wataelezea ujia za kupingana na ufisadi watakuwa wamepotoka.
  2. Mtahiniwa atunge kisa kitakachoonyesha au kushauri watu washirikiane katika shughuli zozote wazifanyazo. Hamna mtu anayeweza kufanya mambo yoyote yakafana bila ya kuwategemea watu wengine.
    TANBIHI. Uandishi huu waweza fanana na umoja ni nguvu utengano ni udhaifu/kidole kimoja hakivuji chawa. Mtahiniwa aeleza maana ya undani wa methali wala si jifya halisia sababu atapotoka utungo wa mtahiniwa uwe na pande mbili.
    • Uchache/ukosefu wa washiriki katika kufanikisha jambo fulani.
    • Kutofaulu/kutofana kwa jambo fulani
  3. Mtahiniwa atoe kisa kinachoona na maneno aliyopewa
    Kisa kiwe cha kusisimua
    Mtahiniwa ajipate katika hali ya kujutia/kushangaa/hofu/huzunisha ambavyo inamfanye ajione afadhari ajiue.
    Hali ngumu ambayo msimulizi alipitia akapoteza matumaini kuishi tena mfano;
    • msichana kubakwa na kuambukizwa magojwa na kuonelea heri afe
    • Msomi kuhitimu shahada nyingi na kukosa ajira nakupoteza matumaini
    • Mtu kupoteza familia yake yote alafu kukosa ,matumaini
    • Mme au mke kumpata mwezake akiwa si mwaminifu katika ndoa.
      Kadiri hoja/kazi zingine za mwanafunzi

INSHA
MWONGOZO
Utangulizi

     Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahini wa kuwasiliana na msomoji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi, akizingatia mada aliyopewa.Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa .Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo na mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kuikadiria kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivopendekezwa.

VIWANGO MBALIMBALI
D – ( D YA CHINI ) MAKI 01 - 02

  • Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile.
  • Kujitungia swali tofauti na kulijibu.
  • Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya Ndimi.
  • Kunakili swali au maswali na kuyakariri.
  • Kunakili swali au kichwa tu.

D – WASTANI MAKI 04 – 05

  • Mtiririko wa mawazo haupo.
  • Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.
  • Matumizi ya lugha ni hafifu mno.
  • Kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (D YA JUU) MAKI 04 - 05

  • Insha huwa na makosa mengi ya kila aina, Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.
  • Hoja hazikuelezwa kikamilifu / mada haikukazwa vilivyo.
  • Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.
  • Mtahiniwa hujirudiarudia.
  • Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.
  • Insha ya urefu wa robo yaani, isiyozidi maneno 174 isipite kiwango hiki.

C- (C YA CHINI) MAKI 06- 07

  • Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
  • Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
  • Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi , ya hijai na ya msamiati na insha haieleweki kwa urahisi.

C WASTANI MAKI 08

  • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
  • Dhana tofauti hazijitokezi wazi.
  • Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.
  • Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.
  • Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa.
  • Ana shida ya uakifishaji.
  • Anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ua msamiati lakini bado insha inaeleweka.

C+ (C YA JUU) MAKI 09- 10

  • Anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini bado insha inaeleweka.
  • Dhana tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu.
  • Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
  • Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
  • Anashida ya uakifishaji.
  • Kuna makosa ya sarufi ya msamiati na hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.
  • Insha ya kiwango cha nusu, yaani maneno 175- 274 isizidi kiwango hiki.

B – (B YA CHINI) MAKI 11- 12

  • Anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofauti akizingatia mada.
  • Ana mtiririko mzuri wa mawazo.
  • Anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia
  • Makosa yanadhihirika / ni kiasi

B (B YA CHINI) MAKI 13

  • Anathihirisha hali ya kuimudu lugha.
  • Mawazo yake yanathihirika akizigatia mada.
  • Anateua na kutumia mifano michache ya misamiati mwafaka.
  • Sanja yake ni mzuri.
  • Makosa ni machache.

B+ (B YA JUU) MAKI 14 - 15

  • Mawazo yake yanadhihirika na anajieleza waziwazi.
  • Anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
  • Ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.
  • Sarufi yake ni nzuri.
  • Uakifishaji wake wa sentensi ni mzuri.
  • Makosa ni machache ya hapa na pale.
  • Insha ya urefiu wa robo tatu, yaani maneno 274 – 374, isipite kiwango hiki.

A- (A YA CHINI) MAKI 16- 17

  • Anadhihirisha ukomavu wa lugha.
  • Mawazo yake yanadhihirika na anaishughulikia mada.
  • Ana mtiririiko mzuri wa mawazo.
  • Msamiati wake ni mzuri na unavutia.
  • Sarufi yake ni nzuri.
  • Makosa ni machache yasiyokusudiwa.

A WASTANI MAKI – 18

  • Anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada.
  • Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato.
  • Anatoa hoja zilizokomaa.
  • Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi.
  • Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.
  • Makosa ni nadra kupatikana.

A+ (A YA JUU) 19 – 20

  • Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughulikiwa vilivyo.
  • Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato.
  • Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.
  • Msamiati wake ni wa hali ya juu na unavutia zaidi.
  • Sarufi yake ni nzuri zaidi.
  • Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi, kiufundi.
  • Makosa yote kwa jumla hayazidi matano.

    Kila ukurasa uwe na alama ya chini katikati ili kuthibitisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo.
    Baada ya kutoa tuzo, lazima mtahini aandike udhaifu wa mtahiniwa.
    Mfano wa kutuza:
    Robo Tatu
    C 08/20

    Udhaifu
  • Urefu
  • Maudhui
  • Hijai
  • Sarufi
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 1 - 2019 KCSE KASSU JOINT MOCK EXAMS (QUESTIONS AND ANSWERS).


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest