MAAGIZO
- Jibu maswali yote.
- Andika majibu yako katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
- Majibu yako yaandikwe kwa lugha ya kiswahili
- SEHEMU YA A: UFAHAMU (alama 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali
“Swala la idadi kubwa ya watoto wadogo wanaoendelea kumiminika mijini na kuonekana wakiranaranda mijini ovyo,halijapewa umuhimu wowote wa haja na serikali za nchi nyingi,licha ya mijadala katika warsha anuwai,zilizofanyika kujadili swala hili nyeti.
Kwa kutokuwa na sheria ama sera iliyo wazi kuhusu haki na usalama wa watoto,sarikali zetu hazina budi kukubali kubeba uzito wote wa lawama. Hii ni kwa sababu, serikali zetu zimelipuuza na kuvalia miwani swala hili kwa kuchukulia kuwa litapotea lenyewe katika hewa yabisi. Yafaa ifahamike kuwa usalama wetu katika siku zijazo utategemea jinsi tutakavyolikabili ana kwa ana tatizo hili wakati huu. Wakati wa kutenda ni sasa. Aidha, watoto hawa wanaokulia mitaani bila malezi,maelekezo wala mwongozo mwafaka wa kimaisha, wanakua bila mapenzi hivyo hawajui maana ya kupenda. Wanachokijua ni chuki na haja ya kulipiza kisasi dhidhi ya jamii iliyowachonga jinsi walivyo. Hawajali lolote hata kifo. Wako tayari kujikabidhi kwa haini yeyote mwenye nia mbaya,bila kujali matokeo, muradi tu, wapate riziki.
Tunapendekeza kwa serikali, washirika dau kama vile mashirika ya kujitolea, viongozi wa dini, shule, vyuo na wananchi kwa jumla wachange bia katika kutafuta mikakati ya kulitatua tatizo hili kabla halijageuka kuwa janga la kijamii ambalo tutashindwa kulimudu. Mpango wa vijana hawa kujiunga na huduma ya taifa ni jambo linalofaa kutiliwa maanani.
Tunapendekeza makao Zaidi ya watoto wanaozurura mijini yajengwe ambapo watapata mafunzo ya kiufundi yatakayowawezesha kujitegemea maishani. Badala ya kulitegea mgongo swala hili, serikali zinawajibika kuwasajili hawa watoto ili waweze kuunganishwa na familia na koo zao. Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Elimu jamii umebainisha kuwa ni asilimia kumi tu ya watoto hawa wa mitaani wasiokuwa na mahali wawezapo kupaita nyumbani. Asilimia tisini iliyobaki, angalau wana mahali wanapoweza kupaita nyumbani ilhali wanaendelea kuwa mitaani. Wazazi tumesahau wajibu wetu. Wengi wetu tumelikimbia jukumu la ulezi tulilopewa na muumba. Hawa waliojipaka masizi mwilin mzima, wanaozurura ovyo mitaani, si matokeo ya maumbile;hawakuja duniani kwa sadfa, hawakuulizwa wala kushauriwa. Makosa ni yetu wazazi. Tuliwaleta hapa duniani, kisha tukawakimbia.Hatutasamehewa duniani na akhera.
Mwenye njaa hana miiko. Ili kijiruzuku, hawa watoto daima wanachumia jaani.Kwa kudura ya jalia, huenda siku moja watalia kivulini. Asiyekuwa na wake ana mungu.Aghalabu, watoto wanaozurura mitaani hupewa pesa na wafadhili. Wakati mwingine wanaiba. Maisha haya ya kuomba au kuiba wanaona yanaridhisha Zaidi kuliko kumenyeka na kazi ya kibarua kutwa kucha. Kwa bahati mbaya, watoto hawa wamatumia pesa wanazopata kutoka kwa wafadhili kujichimbia kaburi. Aidha pesa wanazopatiwa watoto hawa wanazitumia kununulia gundi badala ya chakula.
Wafadhili wanashauriwa wawape chakula hawa watoto badala ya pesa taslimu. Kusema kweli, unapompa mtoto wa mitaani pesa,utakuwa unainua biashara ya mwenye kiwanda cha gundi,jambo ambalo litakuwa sawa na kuweka sahihi mkataba wa kifo cha mtoto mwenyewe.
Wataalamu wa afya wanaonya kuwa gundi ikivutwa kwa muda mrefu inaweza kusababisha upofu au kifo.Wataalamu hawa wanazidi kutuarifu kuwa matumizi ya muda mrefu ya gundi huathiri ubongo,figo na maini. Mtumiaji pia anaweza kupoteza uwezo wa kutembea na hata kupooza kabisa.
Sababu wanazotoa hawa watoto ni kwamba, uvutaji gundi,huwaondolea njaa,baridi ya usiku na kuwatuliza mawazo. Ni jambo la kusikitisha kwamba tunaendelea kushuhudia bila kujali hawa watoto ambao ni kiungo cha jamii yetu,wakijiangamiza. Wananchi kwa ujumla hawaha budi kuhamasishwa dhidhi ya athari ya matumizi ya gundi.Wafanya biashara wanaowauzia watoto hawa gundi yafaa wakome,la sivyo wachukuliwe hatua.Kutolitatua tatizo hili la watoto wa mitaani hivi sasa,kutapeleka kuwako kwa kizazi cha mitaani ambacho kitazaliwa mitaani,kulelewa mitaani,kuoa mitaani na kufia mitaani.Kadiri mataifa yanavyoendelea kujitia hamnazo kuhusiana na swala hili,ndivyo tunavyokubalia jinai itawale,sasa na wakati ujao.
Hawa watoto watakapokua,watageuka kuwa wapigaji watu kabari,majambazi,wezi wa kutumia nguvu ama watatumiwa na mahaini kutimiza uhaini wao.Hawa watoto wenye njaa,watalazimika hatimaye,kuwatoa wenywe shibe tonge mdomoni.Matokeo ya hali hii ni kwamba katika siku zijazo,hawa ndio watu watakaotunyima starehe ya kulala unono.Watatuchafya mitaani,majumbani,vijijini na kutuvizia mabarabarani.Tuna sababu nzuri ya kutiwa hofu na tatizo hili,kwani jinsi kizazi kinavyozidi kupanuka,inaonekana tumelitega bomu ambalo litakuja kutulipukia usoni mwetu.”
Maswali- Taja jambo moja linalochangia kuweko kwa watoto wanaorandaranda mitaani. (alama 1)
- Maisha ya mitaani huathirije watoto? ( alama 3)
- Tatizo la watoto wanaorandaranda mitaani laweza kutatuliwaje? (alama 3)
- Eleza maana ya: (alama 2)
- Hawa watoto wanachumia jaani
- Jinsi kizazi cha mitaani kinavyozidi kupanuka,inaonekana tumelitega bomu ambalo litakuja kutulipukia usoni mwetu. (alama 2)
- Mwenye njaa hana miiko. (alama 2)
- Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kwenye taaria: (alama 2)
- Aidha:
- Gundi:
- UFUPISHO
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Kadiri jamii mbalimbali zinavyotagusana, ndivyo lugha zinazozungumzwa na jamii hizi nazo zinavyoingiliana na kuathiriana. Mojawapo ya athari hizi ni ukopaji wa msamiati. Jamii zinazopakana au kutagusana hukopa msamiati kutoka kwa lugha jirani na kuutumia kuelezea dhana mpya zinazoingia katika utamaduni wao kupitia kwa mitagusano ya kijamii.
Lugha ya Kiingereza, kwa mfano, imekopa kutoka lugha nyingine kama vile Kifaransa na Kilatini. Mathalani, istilahi nyingi za kisheria zimekopwa kutoka lugha ya Kifaransa. Aidha, Kiingereza kimekopa kutoka lugha ya Kiswahili. Maneno ya Kiswahili kama vile mwalimu, jiko, mandazi, panga, buibui, ngoma na hata wananchi, sasa yameingia katika kamusi za Kiingereza, kumaanisha kuwa yamekubaliwa kama msamiati rasmi wa lugha ya Kiingereza.
Kiswahili nacho kimeathiriwa na lugha nyingine. Kimekopa msamiati wa Kiingereza na hata Kiarabu. Katika tungo nyingi za kishairi, kwa mfano, Utenzi wa Mwanakupona utapata msamiati wa Kiarabu uliotoholewa. Lugha nyingine ambazo zimeathiri Kiswahili ni pamoja na Kijerumani ambako msamiati kama vile ‘shule’ ulikopwa na kutoholewa kwa neno schule. Msamiati kama vile ‘leso’, ‘karata’ na ‘mvinyo’ yamekopwa kutoka lugha ya Kireno, huku majina ‘balozi’ na ‘bahasha’ yakikopwa kutoka Kituruki.
Pamoja na ukopaji wa vipengele vya lugha, mtagusano wa lugha una athari nyingine. Lugha zinapokuja pamoja, mazingira ya wingi-lugha huzuka. Baadhi ya watu hujifunza zaidi ya lugha moja. Mtu anayeweza kuzungumza zaidi ya lugha moja anaweza kujieleza kwa urahisi kwa kuchanganya msamiati wa lugha tofauti. Aidha, anaweza kubadilisha msimbo kulingana na matilaha yake. Ikiwa anataka kukubalika na jamii-lugha anayotagusana nayo, atatumia lugha ya jamii hiyo ili kujinasibisha na kujitambulisha nayo. Wazungumzaji hupata visawe vya maneno kuelezea dhana zile zile, hivyo kuboresha mitindo yao ya mawasiliano.
Kadhalika, kutagusana kwa lugha kunaweza kusababisha kubuniwa kwa lugha ngeni ambayo inarahisisha mawasiliano. Wakati mwingine, watu wanaozungumza lugha tofauti wanapokutana, hubuni mfumo sahili wa lugha ili kufanikisha mawasiliano. Pijini ni mfano wa lugha iliyobuniwa kwa njia hii. Pijini huchota msamiati kutoka lugha zilizotagusana. Sheng ni mfano mwingine wa lugha ambayo ilibuniwa kutokana na kutagusana kwa lugha ya Kiswahili, lugha za kiasili na Kiingereza.
Japokuwa kuna faida nyingi za wingi-lugha, hasara pia zipo. Mazingira ya wingi-lugha huwapa wazungumzaji fursa ya kuchagua lugha wanayotaka kuwasiliana kwayo. Katika hali hii, lugha yenye ushawishi mkubwa kijamii, kiuchumi na kisiasa ndiyo inayopendelewa zaidi. Wingi-lugha unaweza kusababisha kukwezwa kwa lugha moja na kudunishwa kwa lugha nyingine. Mathalani, kuwepo kwa lugha nyingi nchini kulizua haja ya kukwezwa kwa lugha ya Kiswahili huku zingine za kiasili zikipuuzwa.
Lugha hukua kwa kutumiwa. Lugha isipozungumzwa kwa muda mrefu, watu hupoteza umilisi ambao huifanya kuwa vigumu kuirithisha kwa vizazi. Lugha inaweza pia kukosa wazungumzaji ikiwa wale wanaoizungumza ni wachache, au ikaathiriwa na mtagusano na lugha nyingine iliyo na wazungumzaji wengi. Katika hali kama hii, lugha hiyo hukabiliwa na tisho la kudidimia au hata kufa. Ikiwa jamii itakosa kudhibiti sera za matumizi ya lugha yake, baadhi ya lugha zitafifia au zitakufa na kusahaulika kabisa.- Bila kupoteza maana, fupisha aya za kwanza tatu. (Maneno 50-60)(Alama 10, 1 ya mtiririko)
- Kwa mujibu wa taarifa hii, mtagusano wa lugha una athari gani?maneno 20-30(Alama 5, 1 ya mtiririko)
- SEHEMU YA C: MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
- Taja sifa tatu za kuainisha irabu (alama2)
- Ainisha viambishi katika neno lifuatalo: (alama2)
Alifiwa - Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
Zainabu aliandikiwa barua na Zubeda - Onyesha miundo mitatu ya kundi nomino (alama 3)
- Andika maana mbili tofauti ya sentensi ifuatayo (alama 2)
Walipiganishwa na kakake - Tunga sentensi tatu tofauti kuonyesha matumizi matatus ya ngeli ya mahali (alama 3)
- Ainisha vielezi namna katika sentensi ifuatayo; [alama 2]
Mlevi alianguka mchangani tifu kwa kutembea ovyo. - Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizopewa (alama 2)
- LA [TENDESHA]
- soma[tendeana]
- Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya visanduku (alama 4)
Yule mzee ajengaye barabara ametuzwa. - Andika katika usemi wa taarifa. (alama 4)
“Karibu Bakari,tafadhali kaa,” Juma akasema. “Asante je,habari za nyumbani?” - Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi ifutayo. (alama 1)
Ukuta uliobomolewa ulisababisha hasara kubwa. - Unda nomino mbili kutokana na neno dhuru (alama 2)
- Andika kinyume cha: (alama1)
Walizama walipokuwa wakikusanya mchanga. - Tunga sentensi moja kutofautisha baina ya bure na pure (alama 2)
- Bainisha matumizi ya ku katika sentensi hii (alama 3)
Mkurugenzi hakukusaidia ulipoenda kula Mombasa anakofanya kazi. - Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu ( alama 2)
- Bumba ni kwa nyuki…………………………..ni kwa samaki na…………………….ni kwa siafu. (alama 2)
- Eleza maana ya ngeli (alama 1)
- SEHEMU YA D: ISIMU JAMII (alama 10)
Kwa kutumia sifa tano, linganua sajili ya mahakamani na sajili ya sokoni (alama 10)
MARKING SCHEME
- UFAHAMU: ALAMA 15
-
- Wazazi kukwepa jukumu la ulezi.
- Kutokuwa na sheria/sera iliyo wazi kuhusu usalama wa watoto
Hoja yoyote 1x1=1
-
- Hukosa mapenzi.
- Hukosa malezi,maelekezo na mwongozo mwafaka maishani
Huiga tabia bofu K.M kuvuta gundi na kuiba.
Njaa
Zozote 3x1=3
-
- Kutiliwa maanani kwa mpango wa vijana wa kujiunga na huduma ya taifa
- Kuongeza makao ya watoto na kuwapa mafunzo ya kiufundi
- kuwasajili watoto ili waweze kuunganishwa na familia zao
- Wafadhili wawape chakula badala ya pesa taslimu
- Wanaowauzia gundi wahamasishwe dhidi ya matumizi yake
Zozote 3x1=3
-
- Tegemeo lao ni makombo na takataka iliyo mapipani (alama 2)
- Kutolitatua tatizo la watoto wanaorandaranda mitaani kutatuletea matatizo
- Mhitaji hachagui chochote (alama 2)
-
- Aidha-pia
- Gundi- Kitu kiolevu na kinachonata kunachonuswa na watoto kama kileo 1x2=2
-
- UFUPISHO
- HOJA ZA KUZINGATIA (Alama 9, 1 za mtiririko)
- Mitagusano ya kijamii hufanya lugha kuingiliana.
- Pia lugha huadhiriana
- Ukopaji wa vipengele vya lugha ni moja ya athari hizo/msamiati
- Istilahi nyingi za kisheria zimekopwa kutoka lugha ya kifaransa.
- Msamiati hukopwa ili kueleza dhana ngeni.
- Lugha zote hukopa.
- Kiingereza kimekopa kutoka.
- Kilatini, Kifaransa na Kiswahili.
- Kiswahili nacho kimekopa kutoka.
- Kiingereza, Kiarabu, Kireno, Kituruki na Kijerumani.
MFANO WAJIBU HALISI - Mitagusano ya kijamii huleta maingiliano yana yosababisha jamii kuathiriana kilugha. Baadhi ya athari hizo za ukopaji wa vipengele vya lugha.
- Msamiati hukopwa ili kuelezea dhana mpya, lugha zote hukopa msamiati kwa mfano Kiingereza, Kiarabu, Kituruki, Kireno na Kijerumani (maneno 48).
- HOJA ZA KUZINGATIA (Alama 6, 1 za mtiririko)
- Kuzuka kwa hali ya uwingi – lugha.
- Ukuaji wa lugha.
- Kuzuka kwa lugha mpya.
- Kudunishwa kwa lugha.
- Kufa kwa lugha.
MFANO WA JIBU HALISI - Mtagusano wa lugha una faida na hasara. Kwanza, husababisha kuzuka kwa hali ya wingi – lugha, aidha, lugha hukua kwa kukopa msamiati kutoka lugha nyingine.
- Mtagusano pia husababisha kuzuka kwa lugha mpya, kwa upande mwingine, uwingi – lugha hukwezwa na kudunishwa baadhi ya lugha, lugha inayodunishwa huingia katika ya kufa (maneno 47).
- HOJA ZA KUZINGATIA (Alama 9, 1 za mtiririko)
- MATUMIZI YA LUGHA :Alama 40.
- semuya kutamkia mahali pa kutamkia mkao wa midomo
(alama 1x1=2) - A-li-f-iw-a
(alama 1/2x2=1) - Kitondo/tendewa- Zainabu Kipozi/tendwa- Barua (1x2=2)
- N-moja pekee
N+U+N
N+KISHAZI TEGEMEZIW PEKEE
N/W+V - Kakake aliwafanya watu wengine wapigane.
Yeye na kakake waliwafanya kupigana
Waligonganishwa
Yeye na kakake walikosana
(2x1=2) - pa/po
ku/ko
mu/mo - Tifu, onyo.(alama 2)
-
- lisha
someana - KN[V+N+S]+KT[T]
KN
KT
V
N
J
T
Yule
Mzee
Ajengaye barabara
ametuzwa
- lisha
- Juma alimkaribisha Bakari akamsihi akae.Bakari alimshukuru Juma na akataka kujua habari za nyumbani.
(1x4=4) - Ukuta uliobomoka- Kishazi tegemezi
Ulisababisha hasara kubwa- Kishazi huru (1x2=2) - kudhuru
madhara - Walielea/waliibuka wakitawanya mchanga. (1/2x2=2
pure-mchanganyiko wa mahindi na maharagwe
bure-bila kabisa - nafsi
- kikanushi wakati uliopita
- ngeli ya mahali
- mama alikuwa amepika alama 2
- kishazi/mtungo
msafara - Ngeli ni mkusanyiko au makundi ya nomino/
- semuya kutamkia mahali pa kutamkia mkao wa midomo
- SEHEMU YA NNE ISIMU JAMII (ALAMA 10)
1.Sentensi ndefu ndefu
1.sentensi fupifupi
2.lugha rasmi
2.lugha ya kawaida
3.Hunukuu vifungu vya kisheria /msamiati maalum
3.Hutumia msamiati wa kawaida
4.Hukopa kutoka lugha za kigeni-kilatini
4.Hutumia lugha rahisi na inayoeleweka na wote
5.Huwa kuna mkarimani
5.hakuhitaji mkarimani/muuzaji na mnunuzi huelewana
6.kuna mpangilio maalum wakati kesi inapoendeshwa
6.kuna kukatiza kauli
(1x2x5=10)
Download KISWAHILI PAPER 2 - 2019 KCSE KASSU JOINT MOCK EXAMS (QUESTIONS AND ANSWERS).
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students