Maagizo
- Jibu maswali manne pekee.
- Swali la kwanza ni la lazima.
- Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani
Sehemu ya B, sehemu ya Sehemu ya D na Sehemu ya E. - Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
- Kila swali lina alama ishirini (20)
- Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Karatasi hii ina kurasa zilizopigwa chapa.
- Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
KWA MATUMIZI YA MTAJINI PEKEE
SWALI | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 | 8 | JUMLA |
MASWALI
1. SEHEMU YA A: SWALI LA LAZIMA-SHAIRI
1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Mungu naomba subira, subira nayo imani
Imani iliyo bora, bora hapa duniani
Duniani mwakombora, kombora nayo hiani
Hiani pamwe ukora wenye kuhini.
Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhuli
Ufidhuli wakudhuri, kudhuri wangu muwili
Muwili hata kidari, kidari kuwa thakili
Thakili kisinawiri,kisinawiri misuli.
Misuli kuwa hafifu, hafifu kama muwele
Muwele wa hitilafu, hitilafu ya nduwele
Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
Milele kutoniafu,kutoniafu na vishale.
Vishale vinitomele, vitomele vikwato
Vikwato pia maole, maole kufanya mito
Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
Kitoto kilo vipele,vipele vyenye fiakuto.
Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
Kutamka wazi vino, vinosubira kutaka
Kutaka Imani mno, mno n'sipate wahaka
Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.
Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita
Yamepita na vilio, vilio vipishe nyota
Nyota nje naing'arao, ing'arao kunikita
Kunikita salamani salamani ni kadata.
(T. Arege)
- Kwa nini nafsineni anaomba subira na amani?(alama 2)
- Ainisha shairi hili kwa kuzingatia: (alama 4)
- Mpangilio wa maneno
- Mpangilio wa vina
- Idadi ya vipande
- Idadi ya mishororo
- Kwa kutoa mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (alama 4)
- Bainisha toni ya shairi hili. (alama 2)
- Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari.(alama 4)
- Huku ukitoa mifano,eleza jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (alama 4)
SEHEMU B: HADITHI FUPI
(A. Chokocho na D. Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine.)
Jibu swali la 2 au la 3
2. Mapenzi ya Kifaurongo - Kena Wasike
- "Ameghairi nia na kubadilika kama msimu."
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alamat)
- Tambua mbinu mbili za lugha zinazoyojitokeza katika dondoo. (alama2)
- Eleza sifa zozote tatu za mzungumziwa.(alama3)
- Ni maudhui yepi yanaendelezwa na mzungumziwa? Jadili yoyote matatu. (alama3)
- Kwa kutoa ithibati kwenye hadithi,onyesha ni vipi mrejelewa ameghairi nia na kubadilika kama msimu (alama 8)
Au
3. Mwalimu Mstaaafu
- "Mwalimu Mstaafu Mosi ni mfano wa kufuata kielelezo kisichomithilika." Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi. (alama 10)
- Mwandishi wa hadithi "Mwalimu Mstaafu' ametumia mbinu ya kinaya kwa ufanisi mkubwa. Thibitisha. (alama. 10)
SEHEMU C: RIWAYA : CHOZI LA KHERI- Assumpta K. Matei
Jibu swali la 4 au la 5
4. "...bila kuwa na mwelekezi ningerudia uwele wangu, yakawa yale ya mwenye
kovu sidhani kapona."
- Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
- Bainisha tamathali mbili zinazojitokeza katika dondoo hili.(alama 2)
- Eleza umuhimu wa msemewa katika ujenzi wa riwaya ya Chozi la Heri. (alama 4)
- "Ufisadi umetia doa maisha ya wahusika wengi katika riwaya." Hakiki. (alama 10)
Au
5. Tathmini jinsi mwandishi amefaulu katika matumizi ya majazi ukirejelea wahusika katika riwaya nzima.(alama 20)
SEHEMU D:TAMTHILI-KIGOGO Pauline Kea
Jibu swali la 6 au la 7
6. "Hana miguu kwa sasa pengine atambae kwa tumbo kama nyoka!"
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
- Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo (alama 2)
- Eleza sifa zozote nne za msemaji (alama 4)
- Eleza umuhimu wa mrejelewa katika kuendeleza tamthilia. (alama 10)
Au.
7. "Wanawake wamekandamizwa barani Afrika."Kwa kurejelea tamthilia ya Kigogo, Thibitisha ukweli wa kauli hii.
(alama 20)
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI.
Jibu swali la nane
8.
- Huku ukitoa hoja sita linganisha aina mbili kuu za fasihi.(alama 6)
- Jadili vipengele sita vya kuzingatia katika uchanganuzi wa hadithi.(alama 6)
- Jadili sifa mbili za vitanza ndimi kwa kurejelea sauti.(alama 2)
- Tambua istilahi zinzotokana na maelezo haya:
- Msimulizi wa fasihi simulizi anaitwaje kwa jumla?(alama 1)
- Shujaa katika mighani pia anaweza kuitwa nani?(alama 1)
- Sherehe za kitamaduni ambazo hufungwa na jamii katika kipindi fulani maalum huitwaje?(alama 1)
- Mavazi au vifaa vinavyotumiwa na wasanii kuakisi hali halisi ya mambo wakati wa kuwasilisha fasihi huitwaje?(alama 1
- Mtambaji wa hadithi hutumia ujuzi gani anapoibadilisha hadithi yake moja kwa moja mbele ya hadhira bila kuathiri usimulizi wake?(alama 1)
- Wanaosimuliwa ili kuonyesha kazi ya fasihi simulizi hupewa jina hili. (alama 1)
Download Kiswahili Paper 3 Questions - Alliance Girl's High School Mock December 2020.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students