Maagizo
- Andika jina lako na namba yako ya usajili (ADM) katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
- Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafast ulizoachiwa hapo juu.
- Jibu maswali yote.
- Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali
- Majibu yote ni lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Usitoe ukurasa wowote kutoka kwenye kijitabu hiki.
- Karatasi hii ina kurasa 10 zilizopigwa chapa.
- Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
Kwa matumizi ya mtahini pekee
SWALI | UPEO | ALAMA |
1. UFAHAMU | 15 | |
2. MUHTASARI | 15 | |
3. SARUFI | 40 | |
4. ISIMUJAMII | 10 | |
JUMLA | 80 |
MASWALI
1. UFAHAMU: (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha y'ibu maswali.
Nchi nyingi duniani zimetia sahihi mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto. Haki hizi ni pamoja na uhai, lishe bora inayotosha na makazi bora yaliyo salama. Hali kadhalika, kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Elimu inastahili kutolewa bure, iwe inayofaa na inayopatikana kwa urahisi. Isitoshe, mtoto hastahili kupigwa, kudunishwa, wala kubaguliwa kwa namna yoyote ile iwe kitabaka, kirangi, kijinsia au vinginevyo. Mtoto hapaswi kufanya kazi za kitumwa, nzito na za kushurutishwa. Vile vile, mtoto ana haki ya kutunzwa na kulindwa dhidi ya hali yoyote inayoweza kumhatarisha. Fauka ya haya, mtoto anastahili kushirikishwa katika kufanya maamuzi yanayoweza kumwathiri maishani. Pia mtoto ana haki ya kupata huduma za afya, mahitaji maalum na habari kuhusu masuala mbalimbali. Pamoja na hayo, mtoto anastahili kupendwa na kuheshimiwa kimawazo na kihisia.
Haki za watoto zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, serikali na wazazi wakiwa katika mstari wa nyie. Hii ndiyo sababu serikali za mataifa mengi zimeshirikisha haki hizi katika katiba na sheria za nchi husika. Yeyote anayezikiuka anapasa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Walakini haki hizi bado zinakiukwa. Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao. Kuna watoto ambao hawajawahi hata kupata kibanda cha kuweka ubavu. Wengi wa hawa wamejipata wakiselelea kwenye mitaa na hata majaa ya miji na vijji ambako hulazimika kupitisha usiku hata katika majira ya kipupwe na masikal Wengine hawapati chakula; licha ya kuwa wanatakiwa kupata chakula chenye lishe bora. Kwao kutarajia mlo awamu tatu kwa siku ni njozi; kwani hata awamu moja ni adimu kupata! La kusikitisha ni kwamba wale wanaotarajiwa kuwa vigogo wa kuzilinda haki hizi ndio wanaoongoza katika kupalilia ukiukaji wazo. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kushinikizwa kufanya kazi za sulubu kipunda, kunyanyaswa kijinsia, kuishi katika mazingira hatari na hata kuuawa. Baadhi ya wanaohusika na vitendo hivi hasi huwa wazazi au jamaa wa karibu kama vile wajomba, shangazi au wahudumu wa nyumbani.
Madhila yanayowapata watoto hayatokei tu katika mazingira ya nyumbani. Mateso huvuka mipaka na kufikia ngazi ya kimataifa. Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwa vitani Linalokata maini ni kwamba baadhi ya viongozi katika mataifa haya hawafanyi lolote kuwanusuru. Lao huwa kuwatazama watoto wanaotakiwa kuwalinda wakigeuzwa kuwa mababe wa kuua na kuuana. Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Pia hulazimika kuvaa mabuti ya kijeshi ambayo huwa nanga kwao kubeba, licha ya bunduki zinazokaribia kuwazidi uzani.
Mojawapo ya mambo ambayo viongozi nchini humu walilenga shabaha kuyafikia baada ya kujinyakulia uhuru ni elimu kwa wote. Hata hivyo, hii imekuwa kama ndoto isiyotabirika katika baadhi ya janibu. Ni kweli kwamba sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi nchini
humu inaendelea kutekelezwa. Hata hivyo, asilimia ya watoto na hata watu wazima wasiojua kusoma na kuandika ingali kubwa. Jukwaa la vijiji nchini humu na hata katika mataifa mengine ya ulimwengu wa tatu limesheheni idadi kubwa ya watoto wasioenda shuleni. Kichocheo kikuu cha hali hii ni kwam ba wazazi na walezi wamejipata katika lindi la ufukara uliokithiri. Hata wanapojitahidi kujinyanyua na kujikuna wajipatapo kuyakidhi mahitaji ya kielimu ya wanao, wao hujipata wakitapatapa katika kinamasi hicho hicho cha ulitima. Matokeo ni kwamba watoto wa matajiri wanaendelea kuelimika huku wa maskini wakibakia kwenye kiza cha ujinga. Wanaong'ang'ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana.
Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe tufanye hima tuungane mikono na kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu utekelezaji wa haki za watoto. Twapaswa kuhimiza serikali zetu kufanya kila ziwezavyo kuhakikisha kuwa watoto wote wako shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto na kukomesha dhuluma, mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada bungeni kuhusu haki za watoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda kwa dhati
MASWALI
- Huku ukitoa mifano minne, eleza hali ya kinyume inayojitokeza katika aya ya pili. (alama 4)
- Eleza namna hali ya usalama inavyoathiri utekelezaji wa haki za watoto kwa mujibu wa kifungu. (alama 3)
- Kwa kurejelea aya ya nne, onyesha mchango wa serikali katika kuwajibikia haki za watoto. Kwa kurejelea aya ya nn (alama 3)
- "Wanaong'ang'ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana." Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu (alama 2)
Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa (alama 3)- Vigogo ......
- huwa nanga kwao ....
- kujikuna wajipatapo..........
2. UFUPISHO (alama 15)
Zamani za kale mafunzo yenye maadili yalikuwa kipengele muhimu cha maisha ya binadamu. Elimu ya kiasili ilisisitiza sana suala la maadili. Unewakuta maajuza wameketi kando ya moto na wajukuu wao wakiwafunza maadili mbalimbali na kuwatahadharisha juu ya miiko ya jamii zao. Ngano za aina mbali mbali zilitumiwa kupitisha mafunzo na mashauri mbalimbali. Visa vilivohusiana na ujanja wa wanyama wadogo kama sungur vilitumiwa kuwaonya walaghai, hadithi za kupasuka msamba kwa fisi mlafi zilitumiwa kuwatahadharisha wenye tamaa. Almuradi elimu ya kiasili iliyitosheleza.
Mafunzo ya jandoni na unyagoni yalikuwa muhimu mno. Wavulana walifunzwa jinsi ya kuzikimu familia zao na kuwajibika katika ndoa. Hawa walihimizwa kutafuta mali kwanza kabla ya kujitwika zigo la ndoa.
Walisisitiziwa kuwa mke alihitaji kupaliliwa kama mgomba; mke ni nguo ati. Nao wasichana walifunzwa kuwatii waume zao na kuwa walezi wema. Walikumbushwa kuwa mwanamke asiyejua kupikia aila yake alikuwa mzigo na aibu kibwa sana kwa sababu lilikuwa jukumu la amii mzima wala si kwa mzazi pekee.
Majilio ya elimu ya kizungu yalivurunga mengi ya kiasili. Yale mafunzo ya maadili sasa yemeanza kupotea wengine wanayosoma vitabuni tu. Kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, mama na baba wamo mbioni kuwachumia watoto wao. Hawana muda mwingi wa kuwaadilisha wana wao. Hata wapatapo muda baadhi yao
wanaona haya kuwazungumzia haya, yaani akina nyanya, nao wamo katika kumbo hili la usasa. Wao pia ni wachumi na hawana muda wa kuzungumza na wajukuu wao. Si ajabu kupata kuwa wasichana wengine wanaolewa hata kabla ya kujua mambo ya kimsingi kuhusiana na maisha ya ndoa kama vile umuhimu wa kuwa na uhusiano bora na wakwe. Wengine hata hawajui kupika wala kufua vyema. Wamezoea kufanyiwa haya na vijakazi.
Heshima nayo imekuwa msamiati uliosahaulika kabisa. Si ibura kupata kwamba mkaza mwana unajibizana na mama mkwe nusura watiane madole machoni. Ati wao pia wana haki; hawapaswi kuamrishwa na wakwe. Vijana hawazingatia maadili ya jamii. Unapata kijana akipitana na mzee bila hata kumsalimu. Hili ni jambo ambalo halikukubaliwa katika tamaduni za kale. Mavazi ya vijana nayo yanakatisha tamaa. Utampata msichana kavaa nguo iliyombana kiasi cha kutoweza kutembea na viatu ambavyo vinamfanya kuelea angani. Maadili ni yale matendo ya haki na utu ambayo yanakubalika na jamii fulani. Zamani wana wote walishughulikiwa na jamii. Hata hivyo siku hizi si ajabu kuona kuwa mwana wa mkata anakosa kwenda shule kwa sababu baba hamudu karo ya shule. Kila mtu anavutia ngozi upande wake. Hili ni jambo la kutia majonzi mno. Wengine nao wamejitahidi kuwadhulumu hata mayatima ili kujifaidi. Baadhi ya watu wamepania kujitayarisha kwa njia zisizo hatali. Wengine nao hawaheshimu mali yaw engine. Visa vya wizi vimezidi nchini na kuhofisha wengi wapenda haki. Kuna wale wanaoiba kimasomaso kwa kutumia nguvu, wakavamia nyumba za watu na kuondoka na mali. Pia kuna wale wanaoiba kwa kutumia maarifa ya kalamu.
MASWALI
- Eleza mambo yaliyodumisha maadili katika jamii kabla ya ujio wa elimu ya kizungu. (maneno 50-60)
(alama 6; 1 ya utiririko)
Matayarisho
............................................................
Nakala safi
............................................................ - Elimu ya kizungu ilichangiaje kuzorota kwa maadili katika jamii. (maneno 70) (alama 9; 2 za utiririko)
Matayarisho
............................................................
Nakala safi
............................................................
3. MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
a) Huku ukizingatia jinsi hewa inavyozuiliwa, ainisha sauti zifuatazo:
- /y/........
- /sh...........
- /h.............................. ......................................
- /nyl..... ...................
b) Andika neno lenye muundo ufuatao.
- irabu, irabu, irabu ....
- irabu, konsonanti, konsonanti, konsonanti, irabu (alama 2)
c) Ainisha mofimu katika maneno yafuatayo: (alama 2)
- mwanao
............................................................ - azingatiaye
...........................
d) Onyesha aina za vielezi katika sentensi zifuatazo: (alama 2)
- Barabara ndefu zaidi ilisakafiwa barabara.
- Kiplagat alianza kula alipoambiwa asishike chakula hivi hivi.
e) Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa. (alama 2) Mwanamke huyu alibeba ndoo hizi hadi sokoni.
f) Tunga sentensi yenye muundo ufuatao.(alama 2) KN(RH+RH) + KT(t + V)
g) Tunga sentensi ukitumia neno alikuwa kama:
- kitenzi kishirikishi kikamilifu (alama 1)
- kitenzi kisaidizi (alama 1)
h) Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa:(alama 3)
Mwanasiasa alisema, "Mkinipigia kura nitawajengea zahanati kabla mwisho wa mwaka huu."
i) Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani?(alama 1)
- ufizi
- firigisi ...............
j) Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu. .. Waziri anasoma hotuba yake. (alama 1)
k) Andika sentensi ifuatayo katika hali kanushi: (alama 1)
Nzige wengi walikuwa wanavamia maeneo hayo kabla ya serikali kuchukua hatua.
1) Bainisha kiima na yambwa katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Mama alimpikia mgeni wetu nyama ya kuku.
m) Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo..(alama 2)
Mwalimu aliyetuzwa jana alifundisha shairi lililotungwa na Kezilahabi.
n) Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya daka na taka,(alama 2)
0) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi ka.(alama 2)
P) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari. (alama 4)
Genge la wezi lilituvamia.
q) Bainisha virai katika sentensi ifuatayo.(alama 3)
Pikipiki iliyonunuliwa jana iliharibika karibu na mto.
r) Eleza majukumu ya sentensi ifuatayo:(alama 1)
Nipe kalamu yangu mara moja!
s) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari katika kauli zilizo mabanoni (alama 2)
Kazi hii imekuwa (tendea) ngumu sana lakini siwezi kufa (tendeshwa) moyo.
t) Taja methali inayoafiki maelezo yafuatayo:(alama I)
Mtu anayetegemewa katika jamii akiondoka wanaomtegemea huwa mashakani.
5. ISIMU JAMII (Alama 10)
"Mwenye sikio amesikia. Usiwe kama mimi. Wapurukushe wote wakupotoshao. Fuata ruwaza ya wanaokujali. Kwangu nimejishika sikio baada ya laiti nyingi: Macho yamefumbuka. Usiseme nitazeeker huku. Lengo langu ni kuwahi uzamili na hata uzamifu. Kwani kuitwa profesa ni kosa? Niwafae wengine kimasomaso na kihali"
- Taja na kuthibitisha sajili ya mazungumzo haya.(alama 2)
- Tambua mazingira ambamo mazungumzo haya yanatokea.(alama 1)
- Eleza sifa zozote saba za lugha zilizotumika kwenye mazungumzo haya(alama 7)
Download Kiswahili Paper 2 Questions - Alliance Girl's High School Mock December 2020.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students