MAAGIZO:
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
MASWALI
- Lazima
Andika dayolojia kati ya katibu wa usalama wa ndani na waandishi wa habari kuhusu jinsi ya kuzuia uhalifu nchini. (alama20) - Utelekezaji wa mtoto wa kiume katika nchini ni janga kuu. Jadili. (alama20)
- Mpiga mbizi nchi kavu huchunua usowe. (alama20
- Tunga kisa kitakachomalizikia kwa maneno yafuatayo: (alama20)
...mwishowe nilikuja kung’amua kwamba jitihada za wenzangu ndizo zilizonisaidia kuvuka daraja hiyo.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
1. Swali la Lazima
Hii ni insha ya dayolojia. (Mazungumzo yanahusiana watu wawili au zaidi)
Muundo
- Kichwa - Kitaje wahusika, wapi na mada.
- Utangulizi - Kudokeza mazingira ya dayolojia kwa kifupi na maelezo yawe katika mabano
- Mwendelezo - Mtindo wa kitamthilia utumiwe
- Mwisho - Uamuzi kuhusu mada ujitokeze pamoja na hitimisho rasmi ya dayolojia.
- Majina ya wahusika yawepo na yaandikwe upande wa mkono wa kushoto
- Majina hayo yafuatwe na nukta pacha.
- Ufafanuzi wa matendo ya wahusika uwe kwenye mabano
- Msemaji mmoja asitawale dayolojia
Hoja
- Kuhamasisha wanachi kuwajibikia usalama wao.
- Kuimarisha taasisi za mahakama na jela.
- Polisi kuimarisha doria
- Kuhimiza kukubali mpango wa usalama wa nyumba kumi
- Kupiga vita ufisadi katika kikosi cha askari na washikadau katika nyanja ya usalama.
- Kuimarisha uchumi na nafasi za kazi
- Kutumia teknolojia ya kisasa kupambana na uhalifu.
- Kuongeza idadi ya walinda usalama.
- Kuwapa walinda usalama mafunzo zaidi
Mwalimu akadirie hoja nyingine. - Utelekezaji wa mtoto wa Kiume
Jinsi ametelekezwa
- Kukosa waelekezi
- Kuwachwa kujikidhi pekee.
- Kutopigiwa debe kama msichana.
- Kutwikwa majukumu angali mchanga.
- Kutojaliwa na mashirika ya ufadhili.
- Vyama vya ku;igania mvulana kutowajibika.
- Kunyimwa nafasi ya masomo.
- Kukosa mashirika ya utafiti kuhusu wavulana.
Janga
- Anaacha masomo
- Anaingilia dawa za kulevya na anasa.
- Anaungana na vikundi vya ugaidi.
- Wanakosa hadhi ya mwanamume.
- Kuchangia kuporomoka kwa misingi ya kifamilia.
- Kukosa viongozi wa kesho.
TANBIHI
- Lazima aonyeshe pande mbili, asipo atuzwe nusu ya alama.
- Kuwe na kichwa au mada.
- AtImize maneno kati 300 – 400
- Kadiria hoja nyinginezo.
- Mtahiniwa atunge kisa kinachodhihirisha jinsi yeye / mtu mwengine alivyojiingiza katika janga na alivyopata madhara / matatizo.
- Mtahiniwa abuni kisa kitakachooana na sentensi yenyewe.
- Asipotumia robo tatu ya maneno katika sentensi aadhibiwe.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Achievers Joint Mock Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students