MAAGIZO:
- Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
MASWALI
SEHEMU YA A: UFAHAMU (ALAMA15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Katiba ni utaratibu wa sheria unaoweka mpango wa jamii kuendesha mambo.Ni muhimu kila raia ajue katiba ya nchi yake.
Katiba yaweza kuwa imeandikwa au haikuandikwa. Katika jamii za jadi, katiba ilihifadhiwa na kupokezwa kwa mdomo. Mtindo wa kuandika katiba ulianza nchini Marekani mwaka 1787. Ingawa katiba hii imefanyiwa mabadiliko hapa na pale,bado ni ileile. Kenya ilipowekwa chini ya himaya ya Uingereza mwaka 1895, ilianza kutumia katiba ya Uingereza. Baada ya masetla wa kikoloni kujikita, Kenya kuwa koloni. Hii ililazimu pawe na katiba nyingine mwaka 1920. Waafrika waliupinga mfumo huu kwa sababu haukuwahusisha kikamilifu kwenye masuala ya uongozi. Utetezi wa wanasiasa uliilazimisha serikali ya Uingereza kuitisha makongamano mbalimbali kama vile lile la Devonshire na mengine ili kurekebisha katiba. Waafrika hawakuridhika. Wakaendelea kudai katiba mwafaka. Harakati hizi zilileta kuitishwa kwa kongamano la katiba la Lancaster. Lengo lilikuwa kuandika katiba itakayotumiwa nchini hadi leo. Kati ya wajumbe walioenda Uingereza kuandika katiba mwaka 1962 ni pamoja na Tom Mboya, Jean Marie Seroney, Julius Kiano, Jomo Kenyatta, Masinde Muliro, Oginga Odinga, Ronald Ngala, Daniel Arap Moi na James Gichuru. Wengine ni Martin Shikuku, Dennis Akumu, Taita Towett, Abdilahi Nassir, Jeremiah Nyaga na John Keen.
Katiba ni kitovu cha taifa. Baina ya mambo inayotekeleza ni kuweka utaratibu na kanuni za utawala, kwa mfano, utawala wa kimikoa na serikali za wilaya. Pamoja na haya, katiba hufafanua vyombo vikuu vya serikali ,mamlaka yavyo na mipaka yavyo ya kutenda. Vyombo hivi ni bunge, mahakama, urais, jeshi n.k. Hali kadhalika, katiba hupambanua haki za raia.
Hii hudumisha demokrasia na huwawezesha wananchi kupata uhuru na haki za kimsingi. Katiba hukinga haki za kila raia, hasa kutokana na udhalimu wa wengi au wenye uwezo mkubwa. Zaidi ya yote, katiba huimarisha asasi za umma ili kudumisha uwajibikaji.
Katiba huhalalishwa na watawaliwa. Hii hutokea wanaposhirikishwa katika uandishi wake. Kuanzia miaka ya themanini, raia walianza kudai katiba igeuzwe. Mwamko wa kutaka mageuzi ulianza kwa harakati za kubadilisha mfumo wa kisiasa kutoka ule wa chama kimoja hadi ule wa demokrasia ya vyama vingi. Haja ya mfumo mpya wa kisiasa ulilenga kuwashirikisha wananchi katika utawala na kuondoa uimla.
Harakati zilitia fora miaka ya tisini. Mambo yaliyochochea hali hii ni mengi. Kwanza, katiba iliyokuwa imeandikwa na watu wachache ilikuwa imefanyiwa marekebisho mengi. Marekebisho haya yalimpa rais mamlaka mengi juu ya serikali kuu na vyombo tofauti vya serikali. Pili, viongozi na watu wenye uwezo na utajiri walipuuza katiba. Raia walihisi wanadhulumiwa. Walipinga hali ya wachache waliomzunguka rais kunufaika huku umma ukitengwa. Tatu, kutokana na uongozi uliokuweko wakati huo, wanawake, watoto na walemavu walidhulumiwa na kukosa uwakilishi
ufaao.Hatimaye, pakawa na ongezeko la uharibifu wa mazingira, ufisadi na unyakuzi wa mali ya umma kama vile ardhi.
Waliopigania katiba mpya walikuwa na haja ya katiba ambayo uandikaji wake ungewahusisha Wakenya wote. Mwanzoni, serikali ilipinga wito wa mabadiliko. Lakini mnamo mwaka 2001 iliunda Tume ya Marekebisho ya Katiba ili kutekeleza mahitaji ya wananchi. Tume hii iliwahamasisha na kuwashawishi raia kutoa maoni. Tume iliandaa vikao katika maeneo ya ubunge 210 ambapo wananchi walitoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya katiba waliyotaka.
Katika mapendekezo hayo raia walisisitiza mambo kadhaa. Jambo la kwanza ni utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi na maafisa wa umma .Jambo lingine ni kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na walemavu. Raia walidai kanuni za usawa na ulinganifu. Aidha walitilia mkazo mahitaji ya msingi kama chakula, afya nzuri, makao, elimu, usalama, uchumi, na kadhalika.
Msingi wa mapendekezo hayo yote ni kuwepo na amani ya kitaifa, umoja na uadilifu ili kulinda maslahi ya wananchi wote na taifa.
Maswali :
- Eleza kilichosababisha kongamano la katiba la Lancaster (alama3)
- Tambua mambo matatu yaliyotiliwa mkazo na raia katika maoni yao kuhusu katiba. (alama3)
- Eleza umuhimu wa katiba kwa mujibu wa taarifa. (alama3)
- Taja sababu zilizochangia ubadilishaji wa katiba. (alama3)
- Ni nini kinachomaanishwa na maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa. (alama3)
- Kitovu
Harakati
Hamasisha
- Kitovu
SEHEMU YA B: UFUPISHO: (ALAMA 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata:
Katika safu yangu hii sina lengo la kuzishambulia dini zetu na namuomba
Mungu sana asiniandikie dhambi kutokana na ninayotaka kuyandika. Lakini nashawishika kuikumbusha jamii yangu ambayo inatufanya watu tuzione dini zetu zinamkandamiza mwanamke. Dini zetu kubwa kama Uislamu na Ukristo zinatuelekeza mwanamke kumheshimu mumewe na kumsikiliza anachosema, lakini kwa yeye kufuata maadili ya dini na si kukuambia uue ukakubali.
Wakati dini inasema utekeleze amri ya mumeo na wao wameelezwa mambo ya kuwafanyia wanawake, ikiwa ni pamoja na kuwaheshima na kuwaridhisha kadri ya uwezo wao.
Kutokana na hilo la amri, wanaume wengi ndio wamechukua kama tiketi ya kunyanyasa mwanamke na hata kumnyima fursa ya kujiendeleza kielimu na hata kufanya shughuli za kuongeza kipato. Unakuta familia ni ya kimaskini, baba hana fedha za kutosha kuihudumia familia yake, lakini baba huyo anataka kujishughulisha na shughuli yoyote ya kumuingizia kipato kinachoweza kuwasaidia wote na matokeo yake kuendelea kuwepo, kwenye dimbwi la umasikini. Wengine kwa hofu ya kupata changamoto kutoka kwa wake zao wanawakatalia wanawake walio wao kujiendeleza kielimu au kutafuta mwanamke asiyeelimika ili asiweze kuhoji mambo kadhaa ndani ya nyumba.
Hili limebainishwa hivi karibuni na shirika moja lisilo la kiserikali huko kigoma ambapo katika utafiti wao asilimia 90% ya wanawake wa vijijini wanashindwa kutoa hoja kutokana na uelewa wao duni na kutoa sababu ya kuwa hiyo ni kutokana na ukosefu wa elimu, masuala ya kidini yanayomwelekeza mwanamke kufuata amri za mumewe, mila na desturi kadhaa.
Dini zote zinaeleza wazi umuhimu wa mtu kupata elimu bila kubagua kama ya kiislamu inavyosema; mtu anapata thawabu anapotafuta elimu na anatakiwa aitafute popote bila kujali umbali na hata ikiwezekana kufika China ambapo inaaminika ni mbali.
Sijawahi kuona wala kusikia dini ikisema mwanamke asipate elimu lakini baba zangu na kaka zangu wanaume wanalipotosha hili kutaka kuendelea kumkandamiza mwanamke bila kufikiri kuwa mwanamke ni msaada mkubwa kwao na kwa maendeleo ya taifa lote; ikiwa leo tupo katika harakati za kupata maendeleo na nchi hii hivi kweli tutafanikiwa?
Mapambano ya kuleta maendeleo yaanze katika ngazi ya familia kwa kuondoka kwa ujinga wa kumkandamiza mwanamke ili naye aelimike, aweze kujenga hoja, aweze kujitafutia kipato na mwisho kusaidia katika maendeleo ya familia ambayo kwa njia nyingine ndiyo maendeleo yenyewe ya taifa hili.
Maswali
- Fupisha aya tano za kwanza. (Maneno 70). (Alama8)
MATAYARISHO
NAKALA SAFI - Mwanamke anaweza kuendelezwa vipi. Rejelea aya mbili za mwisho. (Maneno 50).(Alama 7)
MATAYARISHO
NAKALA SAFI
SEHEMU YA C: SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
- Toa sifa bainifu za sauti /h/ (alama 2)
- Taja aina mbili kuu za ala za sauti kisha utoe mfano mmoja mmoja. (alama 2)
- Andika maneno mawili yenye muundo ufuatao wa silabi. (alama 1)
KKKI - Onyesha vikwamizo viwili ambavyo ni konsonanti hafifu (alama 1)
- Andika katika wakati ujao hali timilifu (alama 2)
Wanafunzi walifanya mtihani wa mwigo - Andika kwa msemo wa taarifa: (alama 2)
Askari: Ulikuwa unaelekea wapi uliposhambuliwa?
Jirani: Nilikuwa nikienda sokoni jana. - Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
Ajapo tutamlaki kwa shangwe. - Sahihisha sentensi ifuatayo.
Mtu ambaye aliyechukua kitabu chenye kilikuwa hapa arudishe. (alama 1) - Tumia mzizi –w- katika sentensi kama: (alama 2)
- Kitenzi kisaidizi.
- Kitenzi Kishirikishi.
- Tunga sentensi kubainisha matumizi ya ‘na’ kama. (alama 2)
- Kihusishi cha ‘na’ ya mtenda.
- Kiunganishi cha kuongeza
- Weka kirejeshi ‘O’ tamati kwenye kitenzi chunga kisha ukitungie sentensi. (alama1)
- Tunga sentensi sahihi ukitumia kihisishi cha kukataa. (alama 2)
- Tunga sentensi ya neno moja yenye sehemu zifuatazo : (alama 2)
Kikanushi
Hali timilifu
Mtendewa
Kitenzi cha silabi moja
Kauli ya kutendesha
Kiishio - Ainisha shamirisho katika sentensi hii
Ali alimnunulia Asha viatu kwa pesa zake. (alama 2) - Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya I-ZI kutungia sentensi iliyoko katika hali ya ukubwa - wingi. (alama 2)
- Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mstari. (alama 2)
Mwalimu anakuita ofisini umweleze ulikoweka kijitabu chake. - Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii. (alama 3)
Kwa nini umeishi kwao kwa miaka mingi? - Eleza maana tatu zinazopatikana katika sentensi hii. (alama 3)
- Alikuwa amenijuza kuwa angefika kwao.
- Changanua sentensi kwa njia ya matawi (alama 4)
Yeye na mama yule si watu wazuri sana - Andika sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo. (alama 2)
Nimewaleta askari kituoni ili wawalinde wananchi wote wanaosumbuliwa na majambazi.
(Anza: Wananchi ...)
SEHEMU YA D: ISIMU JAMII
Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
................napinga hoja iliyotolewa na waziri wa Finance ya kuongeza ushuru wa asilimia tatu kwa Wakenya. Baada ya kumsikiza kwa makini, napenda kumkosoa kwa kudhihirisha kuwa..................Housing levy kulingana na kifungu nambari ...................
Maswali
- Bainisha sajili ya mazungumzo haya. (alama 2)
- Huku ukidhibitisha , eleza ni vipi ambavyo mnenaji angefanikisha ujumbe wake (alama 8)
MWONGOZO
SEHEMU YA A: UFAHAMU MWONGOZO.
- Eleza kilichosababisha kongamano la katiba la Lancaster (alama 3)
- Waafrika hawakua wamehusushwa katika katiba ya mwaka wa 1920.
- Waafrika walitaka kuhusika katika masuala ya uongozi.
- Utetezi wa wanasiasa ulilazimu serikali ya uingereza kuitisha kongamano.
- Taja mambo matatu yaliyotiliwa-mkazo na raia katika maoni yao kuhusu katiba. (alama 3)
- Utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi.
- Kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na walemavu.
- Kanuni za usawa na ulinganifu.
- Eleza umuhimu wa katiba kwa mujibu wataarifa. (alama 3)
- kuweka utaratibu na kanuni za utawala mf utawala wa kimikoa.
- Hufafanua vyombo vikuu vya serikali, mamlaka yavyo na mipaka yavyo ya kutenda.
- Hupambanua haki za raia.
- Taja sababu zilizochangia ubadilishaji wa katiba. (alama 3)
- Katiba iliyokuwa imeandikwa na watu wachache ilikuwa imefanyiwa marekebisho mengi.
- Viongozi na watu wenye uwezo na utajiri walipuuza katiba.
- Kutokana na uongozi uliokuweko wakati huo, watoto na watoto na walemavu walidhulumiwa na kukosa uwakilishi ufaao.
- Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika taarifa. (alama 3)
- Kitovu : Chenye maana na umuhimu.
- Harakati : Shughuli za kufanya jambo fulani.
- Hamasisha : Kufanya jambo lieleweke na kukubalika.
SEHEMU B: UFUPISHO
-
- Sina lengo la kuzishambulia dini zetu na namuomba mungu asiniandikie dhambi.
- Dini za uislamu na ukristo zinatuelekeza mwanamke kumheshimu mumewe na kumsikiliza anachosema.
- Dini imewapa wanawake jukumu la kufuata amri ya mumeo.
- Wanaume wengi wamechukua amri hii kunyanyasa na kuwanyima fursa ya elimu na hofu ya kupata kipato.
- 90% ya wanawake hawatoi hoja kwa sababu wao wameiamini kuwa dini.
- Wanaume huwa na hofu ya kupata changamoto kutoka kwa wake waliojiendeleza kielimu.
- Dini zinaeleza umuhimu wa mtu kupata elimu bila kubagua.
(Hoja – 7, Mtiririko 1, Jumla alama 8)
-
- Kwa kupata elimu.
- Asikandamizwe kwa vyovyote.
- Tutambue umuhimu wa mwanamke katika ujenzi wa taifa.
- Atafute kipato cha familia.
- Aweze kutoa maoni ya ujenzi wa nchi.
- Imani potovu za kidini zitupiliwe mbali.
( Hoja – 6,Mtiririko – 1,Jumla 7)
SEHEMU YA C: SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
- sifa bainifu za sauti |h|-
Kikwamizo
Sauti ya koromeo - Ala tuli – meno, kaakaa gumu, ufizi, koromeo n.k.
- Ala sogezi – midomo, ulimi. (4 x ½ = 2)
- KKKI – Mbwembwe, nywa
- (2x 1 = 2)
- Vikwamizo viwili ambavyo ni konsonanti hafifu - (2x1 = 2)
|f|,|s|,|sh|,|th| - Wakati ujao hali timilifu (1x2=2)
Wanafunzi watakuwa wamefanya mtihani wa mwigo. - Askari alimuuliza jirani alikuwa akielekea wapi aliposhambuliwa naye jirani
akamjibu kuwa alikuwa akienda sokoni siku hiyo jioni (4 x ½ = 2) - Ajapo – Kishazi tegemezi, tutamlaki kwa shangwe – Kishazi huru. (2 x 1)
- Mtu aliyechukua kitabu kilichokuwa hapa arudishe au mtu ambaye alichukua kitabu kilichokuwa hapa arudishe. (1 x 1)
- Kitenzi kisaidizi – Amekuwa akicheza mpria.
- Kitenzi kishirikishi – Ali amekuwa mwizi. (2 x 1=2)
- Shamba la Bw. Komu lililimwa (2x1=2)
- Kihusishi cha ‘na’ ya mtenda – na Hassan
- Kiunganishi cha kuongeza – Ali na Hamisi
- Achungaye, wachungwao, kichungwacho n.k (1 x 1)
(Sentensi iwe sahihi kisarufi) - Kihisishi cha kukataa
- Hata !
- Kamwe! Kamwe! usinihusishe, mimi simo.
- Ng’o! najua watamani maziwa yangu lakini sikupi ng’o! (yeyote 1x2=alama 2)
-
- Mfano: sijakulisha (1x1=1)
- Viatu – Kipozi
- Pesa – ala (2 x 1 = 2)
- Madege hayo yalitua hapa jana. (1 x 2 = 2)
- ku- Kiambishi cha nafsi ya pili.
- ni - Ndani ya
ko - Mahali.
Ki - Udogo wa nomino. 4 x 1/2 = al 2\
- ni - Ndani ya
- Kwa – Kiulizi
Kwao – Umiliki wa mahali
Kwa – Muda/Kipindi (3x1=3) - Yeye mwenyewe alikuwa amenifahamisha kuwa angefika kwa watu wengine.
- Yeye mwenyewe alikuwa amenijuza angefika kwao yaani nyumbani anamotoka yeye.
- Mtu mwingine angefika kwa aliyenijuza. (3x1=3)
- Kuchanganua kwa matawi
- Wananchi wote wanaosumbuliwa na majambazi watalindwa na askari niliowaleta kituoni.
ISIMU JAMII
- Sajili ya bungeni
- ili kufanikisha ujumbe:
_ achanganye msimbo/ndimi – waziri wa Finance.- Atumie Msamiati maalum – hoja, kifungu nambari.
- Atumie lugha ya adabu – napenda kumkosoa
- Sentesi ndefu ili kufafanua hoja
- Atumie lugha yenye sifa za kisheria ili aonane na muktdha husika
- Atumie lugha sanifu ili kufikisha ujumbe kikamilifu
- Atumie viziada lugha ili kusisitiza ujumbe
- Urudiaji wa baadhi ya maneno ili kusisitiza ujumbe wake
- Lugha yenye sifa ya kutaja nyadhifa za watu.mfano bw.spika,
- Apandishe na kushusha kiimbo ili avutie wasilikizaji wa hoja yake.
- Atumie ishara na miondoko ili kuondoa ukinaifu.
- Atumie lugha ya mnato ili kushawishi wabunge wenzake
Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Achievers Joint Mock Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students