Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Achievers Joint Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo.

  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.


MASWALI

SEHEMU YA A: SWALI LA LAZIMA

RIWAYA YA CHOZI LA HERI. (ASUMPTA MATEI)

  1. Nimechoka.Nimechoka kukilovya kifua changu...Nimechoka kuitwa mwizi......Nimechoka kupigania mwenzi...na mwenzi mwenyewe haoni.
    1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Taja na ueleze mbinu ya lugha iliyotumika. (alama 2)
    3. Fafanua sifa za mnenaji katika dondoo. (alama 4)
    4. Jamii ya riwaya hii imekumbwa na migogoro chungu nzima. Dhibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea riwaya nzima. (alama 10)

SEHEMU YA B: TAMTHILIA YA BEMBEA YA MAISHA (TIMOTHY M. AREGE)

  1. ''Mwache mtoto apumzike.Hivi atayashika mangapi?''
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Fafanua toni ya dondoo hili. (alama 3)
    3. Eleza sifa za mnenewa. (alama7)
    4. Mnenaji ana umuhimu upikatika tamthilia? (alama 6
  1. Tamthilia ya Bembea ya maisha inaashiria mabadiliko mengi maishani.Jadili jinsi mabadiliko haya yanavyojitokeza. (alama20)

SEHEMU YA C: HADITHI FUPI.

MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE.

  1. Nilisikia kama maruweruwe,''Mamangu eeh!Mama eeh!''....
    1. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
    2. Pambanua mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo. (alama 4)
    3. Fafanua matukio yaliyomfanya mnenaji kuyanena maneno yale. (alama 6)
    4. Jadili sifa za mnenaji wa maneno haya. (alama 6)

5.Eleza matatizo yanayomkumba mtoto msichana kwa mujibu wa hadithi zifuatazo:

  1. Sabina
  2. pupa
  3. kifo cha suluhu
  4. Ahadi ni deni

SEHEMU YA D: USHAIRI

6. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata:

Jukwani naingia, huku hapa pasokota,
Kwa uchungu ninalia, hii tumbo nitaikata,
Msiba mejiletea, nimekila kiso takata,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wazee hata vijana,wote umewasubua,
Huruma nao hauna, heshima kawakosea,
Ukambani na Sagana, hata mbwa wararua,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wahasibu ofisini,kibwebwe mejifunga,
Miaka mingi vitabuni, ili wasikose unga,
Nadhari wanadhamini, hesabu wanazirenga,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wapenzi wa kiholela, pia wanakuogopa,
Baada yao kulala, wana wao wanatupa,
Wakihitaji chakula, wanachokora mapipa,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wafugaji hata nao, kama dawa wakwamini,
Hawajali jiranio, wamesusia amani,
Wanaiba ng'ombe wao, na kuzua kisirani,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Nayo mizozo ya maji, kaonekana kwa mara,
Hiyo nayo ni dibaji, sababu sio harara,
Njaa wahepe wenyeji, huo ndio mkarara,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Ningeweza kukuuza, ingekuwa siku njema,
Tena kwa bei ya meza, sokoni nimesimama,
Wala tena singewaza, kuhusu wali na sima,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Hatima umefikika, naenda zangu nikale,
Mate yanidondoka, kwa mnukio wa wale,
Naomba kwenda kukaa, wala sio nikalale,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Maswali

  1. Lipe anwani mwafaka shairi hili. (alama 2)
  2. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (alama 2)
  3. Huku ukitolea mifano mwafaka, taja arudhi zilizotumiwa katika ubeti wa tatu. (alama 4)
  4. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
  5. Thibitisha kuwepo kwa idhini ya ushairi. (alama 2)
  6. Taja madhila anayoelezea mtunzi wa shairi hili yaletwayo na tumbo. (alama 4)
  7. Elezea maana ya maneno yafuatayo. (alama 2)
    1. Dibaji
    2. Harara

7. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Nimechoka
Nilivyofikisha hapa, na juu kupandishwa
Na kwa hila gani, au, zilipofungwa
Ncha za waya hii ngumu ya maisha, sijui.

Wanadamu wameinama.Wanasali kwa haraka sasa.
Utafikiri wanahesabu mchanga utakaojaza kaburi langu.
Vichwa vyeupe vinacheka.Kingine kinasema tena:
“Mnaliona Hilo! Joga !” Vichwa vinachela.Wanasali.
“Nyinyi nyote hamna akili!Mnaniudhi!
Hamwoni hali yangu!” Napiga kelele.Lakini vichwa
Havitishi,na wanadamu hawatingishiki.

Sauti ya baba inasema kwa msisitizo
“Najua utafika wakati itakulazimu kudondoka.
“Lakini unazo nguvu bado,na usikate tamaa,
Ila usitegemee kusifiwa au kusaidiwa;
Vichwa vyote hivi vilidondoka kutoka umbali huo,
Nawe kudondoka,utadondoka!

Ninaendelea kuning’inia.Nimechoka.Mikono
Inaniuma;hatari ya vitimbo.Vinacheka.Wanasali
Sasa wanaimba.Sitaki nyimbo zao;maana
Mimi bado nimeniong’inia na vitimbo having’oki.
Lakini pole pole ninaanza kutabasamu.
Sijafikia hatua ya kucheka;maana nimechoka,
Kichomi kimenipata na sijadondoka

Lakini najiona nimening’inia kama ndege
Aliyenaswa na mtego wa mtoto mdogo
Mimi,Lakini ni mwanadamu na akili zangu
Timamu.Ninaweza kudondoka, kama nikipenda.

Lakini ninaogopa chini yangu naona miti
Iliyochongwa ikifuata usawa wa waya hii,
Ikingoja kwa hamu,kama mshikaki kunichoma,
Kunitoboa na kufurahia kimya kimya,
Uzuri wa kupita katika mwili mwororo wa binadamu.
Lazima nishike kwa nguvu nisianguke kama kifurushi
Cha pamba cha mtoto mdogo kilichokwisha pimwa.

Mikono inaniuma, na waya imekwishanikata vidole.
Damu imetiririka hadi kwapani;kujipangusa siwezi.
Nimechoka.Kadiri niendeleavyo kunig’inia, ndivyo
Sura yangu ionyeshavyo vizuri alama za uchovu.
Ninatazama huku na huko kuwatafuta wenye huruma.
Lakini wanadamu wote wazima wanainamisha vichwa
Chini kama kwamba hawanijui;hata jamaa zangu!

Ninaendelea kuning’inia kama picha iliyotundikwa
Katika shamba la mawele, na mwenye shamba
Huvuta waya kutoka nyumbani,itingishike kuwatisha
ndege.
Machozi yananitoka,kuyapangua siwezi.
Ninajitahidi kutoa sauti kwa nguvu;
“Jamani e! Nisaidie! Ng’oeni hivyo vitimbo!”
Lakini wanadamu wameinama.Wanaanza sasa kusali.

Kati ya vitimbo, vichwa vinazuka ardhini
Ukweli wa maisha unakuwa kama ndoto ya uwongo.
Kichwa kimoja kinasema kwa sauti “Mnaliona Hilo!”
Halafu vichjwa vyote vyeupe vinacheka.Ninashangaa.
Ninashangaa zaidi kusikia sauti ya baba
Ikicheka miongoni mwa vichwa hivyo vyeupe.
Siyaamini macho,siyaamini masikio, sikiamini kichwa.

Maswali:

  1. Shairi hili ni la “udhanaishi” Fafanua kauli hii. (alama 4)
  2. onyesha kwa kutoa mifano miwili, jinsi msanii alivyotumia tamathali zifuatazo (alama 6)
    1. Jazanda
    2. Uhuishi
  3. Andika ubeti wa saba kwa lugha tutumbi. (alama 4)
  4. Eleza maana ya mishororo “vichwa vyote hivi vilidondoka kutoka umbali huo, nawe kudondoka utadondoka”. (alama 2)
  5. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1. Maghani ni nini? (alama 2)
    2. Eleza sifa za maghani. (alama 6)
    3. Fafanua aina zozote tatu za maghani. (alama 6)
    4. Eleza matatizo yoyote sita yanayomkumba mtafiti anapotafiti maghani. (alama 6)


MWONGOZO 

RIWAYA YA CHOZI LA HERI.

(ASUMPTA MATEI)

  1. Nimechoka.Nimechoka kukilovya kifua changu...Nimechoka kuitwa mwizi......Nimechoka kupigania penzi la mwenzi...na mwenzi mwenyewe haoni…ka
    1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      Maneno ya Subira katika barua kwa mwanawe Mwanaheri.
      Ni baada ya subira kukata tamaa na kuwatelekeza wanawe kwa machungu ya kuonewa na jamaa ya mumewe.
      4x1=4
    2. Taja na ueleze mbinu ya lugha iliyotumika. (alama 2)
      Mbinu ya lugha - Takriri
      Kurudia rudia neno - nimechoka
      2x1=2
    3. Fafanua sifa za mnenaji katika dondoo. (alama 4.)
      Sifa za Subira -
      mvumilivu
      mwenye mapenzi ya dhati
      mshauri mwema
      mwenye kukata tamaa
      mwenye utu
      Ataje na aeleze
      zozote 4x1=4
    4. Jamii ya riwaya hii imekumbwa na migogoro chungu nzima. Dhibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea riwaya nzima. (alama 10)
      Mgogoro wa kifamilia - familia ya kina Pete
      Mgogoro wa Kisiasa - Mwekevu na mpinzani wake
      Mgogoro wa Kikabila - Subira anafukuzwa na wakwe zake.
      Mgogoro wa kikoloni - Mkoloni anapuuza sera za mwafrika.
      Mgogoro wa Kiimani - Lily anakinzana na uamuzi wa Mwangeka kuwa askari.
      Mgogoro wa Kisaikolojia - Umu anawazia mengi akiwa darasani
      Mgogoro wa kitamaduni - Tuama anapashwa tohara na mwishowe kubadili nia.
      Mgogoro wa ardhi - serikali inaamua kuwaondoa watu msitu wa mamba.
      Aeleze zozote 5x2=10

SEHEMU YA B: TAMTHILIA YA BEMBEA YA MAISHA.
TIMOTHY M. AREGE
JIBU SWALI LA 2 AU 3

  1. ''Mwache mtoto apumzike.Hivi atayashika mangapi?''
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4.)
      Maneno ya Sara akimwambia Yona mumewe wakiwa nyumbani kwao.
      Walikuwa wakizungumzia kuhusu hali ya afya ya Sara na kuhusika kwa Neema katika matibabu.
      4x1=4
    2. Fafanua toni ya dondoo hili. (alama 3)
      Toni ya huruma
      Toni ya chini na ya unyenyekevu
      Toni ya mapenzi
      3x1=3
    3. Eleza sifa za mnenewa. (alama7)
      Mwenye bidii
      Mwenye rabsha/katili
      Mwenye majuto
      Mwenye huruma
      mlevi
      Msomi
      Mbabedume
      Mwajibikaji
      Mtamaduni
      zozote7x1=7
      Ataje na aeleze
    4. Mnenaji ana umuhimu upi katika tamthilia? (alama 6)
      1. Kielelezo cha wanawake wema
        wavumilivu katika ndoa zenye misukosuko
        Wawajibikaji kwa kuwalea na kuwasomesha watoto wao.
        Watiifu na wasiokata tamaa maishani.
        Washauri wema kwa wanao.
        Wenye heshima kwa bwana zao.
      2. Anaendeleza maudhui yafuatayo;
        Ndoa, malezi, wosia.
        6x1=6
  2. Tamthilia ya Bembea ya maisha inaashiria mabadiliko mengi maishani.Jadili jinsi mabadiliko haya yanavyojitokeza.
    Mabadiliko ya utamaduni - suala la ndoa.
    Wasichana waliozwa punde tu baada ya kubaleghe
    Yona hangeingia jikoni kupika
    kuhusu mtoto wa kike kama asiyekamilika.
    Anaweza kuridhi mali
    Sarah anabadilika sana baada ya kuugua yale maradhi yanayomdhoofisha.
    Mabadiliko ya mitazamo.
    Neema anabadilisha mtazamo kuhusu babake
    BUNJU anabadilisha mtazamo wake kuhusuNeema
    Yona alikuwa mzuri mwanzoni kisha akadharauliwa kwa kukosa mtoto wa kiume.
    Anabadilika na kuachana na ulevi.
    Anaanza kuwa na huruma kwa mkewe mgonjwa.
    Jamii inabadilika na kuiona familia ya Yona tofauti.

SEHEMU YA C: HADITHI FUPI

MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE.
Jibu swali la 4 au 5

  1. Nilisikia kama maruweruwe,''Mamangu eeh!Mama eeh!''....
    1. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
      Maneno ya msimulizi wa hadithi Tembo katika barua aliyoiandikia mkewe Emmi akirejelea unyende alioupiga Emmi baada ya kupata alama nyekundu za midomo nguoni mwake.
      Alikuwa amerejea nyumbani baada ya shughuli za ulevi . na kuhadaiwa na Bi.kizee aliyempeleka kwake.
    2. Eleza mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo. (alama 4)
      Tashbihi – kama maruweruwe
      Nidaa – Eeh!
      2x2=4
    3. Fafanua matukio yaliyomfanya mnenaji kuyanena maneno yale. (alama 6)
      Tembo anajipata hospitalini amepofuka baada ya kubugia pombe sumu.
      Baada ya kinywaji anaenda kusakata densi.
      Binti Fulani aliyejiremba sana anamuandama.
      Anajipata asubuhi kwa yule mwanamke.
      Amegeuka Bi. kizee wa kutisha na kiwete pia.
      Pombe ilimhadaa kuwa ni msichana mrembo.
      Amepoteza pesa zote.
      Anamlipa kwa akiba yake kwenye soksi.
      Nyumbani Emmi hamuulizi chochote hadi anapopata zile alama za rangi nyekundu na kupiga unyende huu.
      6x1=6
    4. Jadili sifa za mnenaji wa maneno haya. (alama 6)
      Mzinzi –
      Mwenye shukrani
      Mwoga
      Mwenye tamaa
      Mpyaro
      Mwenye mapuuza
      Mnyenyekevu
      Asiyewajibika
      Ataje na aeleze
      6x1=6
  2. Eleza matatizo yanayomkumba mtoto msichana kwa mujibu wa hadithi zifuatazo;
    Sabina
    pupa
    kifo cha suluhu
    Ahadi ni deni
    SABINA
    • Kulazimika kuamka mapema kabisa-sabina aliamka kukama ngombe,kutoa kisonzo na kupeleka maziwa sokoni.
    • Ukosefu wa sare nzuri
    • Kukomazwa mapema kutokana na majukumu magumu na mengi aliyopewa Sabina.
    • Kuchukuliwa kama kijakazi
    • Kuozwa mapema na mjombake Ombati.
      Kujihusisha kimapenzi wangali shuleni.mfano Nyaboke.
      5x1=5

PUPA

  • Ulanguzi wa wasichana wadogo kwenye madanguro.
  • Kukosa mavazi mazuri.
  • Kukosa lishe bora
  • Ukosefu wa fedha za elimu ya juu
  • KUkiukwa kwa haki yao ya kuwa huru na kupata masomo.
  • Kulazimishwa kufanya mapenzi na wanaume wenye tamaa pale kwenye madanguro.
    5x1=5

KIFO CHA SULUHU.

  • Kukosa karo – Abigael anakosa karo ya chuo kikuu
  • Ukahaba ili wakidhi mahitaji yao
  • Kulazimishwa kuavya mimba
  • Kuambukizwa magonjwa
  • Kulazimika kuchukua muda mrefu chuoni kwa sababu ya matatizo.

AHADI NI DENI

  • Ndoa za mapema- Fadhumo aliolewa akiwa kidato cha pili.
  • Kuacha shule kwa kukosa karo
  • Vifo vya wazazi- babake Fadhumo
  • Ubaguzi wa kijinsia katika elimu.
  • Kuchukuliwa kama chombo cha kukidhi mahitaji ya wanaume – jamaa ya babake.

SEHEMU YA D: USHAIRI

    1. Tumbo lisilotosheka/matatizo ya tumbo (1 x 2)
    2. Tarbia – mishororo mine
      1 – Kutaja (2)
      1 – Kueleza
    3. Arudhi.
      Mishororo mine kila ubeti
      Vina vya kati ni, nga
      Vipande viwili – ukwapi na utao
      Kibwagizo
      Mizani – ukwapi (8) utao (8) (4 x 1)
    4. Lugha nathari
      Wapendanao mapenzi yasiyo na dhati wanakuogopa. Wapatao mimba, watoto wao hawajali.
      Watoto watakapo chakula huwa wanatafuta mapipani. Tumbo nikupe nini ili utosheke? (4 x 1)
    5. Idhini ya mshairi.
      Inkisari mf. We – wewe nitakupani
      Kuboronga sarufi mf. Wafugaji hata nao – Hata nao wafugaji.
      Tabdila mf. Umewasubua – umewasumbua.
      Mazida mf. Mnukio – mnuko (2 x 1)
    6. Kukcsa heshima – hata mbwa wararua.
      Ufisadi – hesabu wanazirenga.
      Kutowajibikia wana – wanachokora mapipa.
      Wizi – wa ng’ombe.
      Mizozo/kutoelewana – mradi waliepe njaa. (4 x 1)
    7.  
      1. Dibaji – Thibitisha/shalali.
      2. Harara – hasira/hamaki
        (2x1=2)
  1.  
    1. Ugumu wa maisha unaofananishwa na kufungwa kwa waya
      • Hakuna mtu wa kumsaidia ila tu watazamaji wanamcheka
      • Ukweli wa maisha umekuwa kama ndoto ya uwongo –alitarajia mema lakini umegeuka vitendawil
      • Machozi na damu zinamtiririka bila wa kumhurumia na kumpanguza
      • Babake ni mmoja wa wanaomcheka kisha anamsisitizia kwa atadondoka tu
      • Vitumbo vimechongwa chini yake tayari kumtoboa
      • Vichwa vimezuka ardhini –ishara ya wengi waliopitia njia hii gumu ya maisha (Alama 4)
    2. Eleza kwa kutoa mifano miwili miwili jinsi msanii alivyotumia tamathali zifuatazo: (al.6)
      1. Jazanda
        1. Vitimbo – Vikwazo katika maisha vinavyolemeza
        2. Waya – mhusika (binadamu )
        3. Kichomi –maisha magumu ya kukatisha tama
        4. Vichwa – Jazanda ya watangulizi wake waliopitia hali hii gumu.
      2. Tashihisi
        • Kichwa kinasema kwa sauti
        • Vitumbo vikingoja kumtoboa
        • Vichwa vinacheka
        • Kichomi kinampata
    3. Andika ubeti wa saba kwa lugha tutumbi (al 4)
      Mzunguzaji anasema kwamba sauti ya baba inamwarifu kwa kusisitiza kuwa hilo ndilo njia na ana
      nguvu lakini wakati utafika na atadondoka.Anaelezwa asitarajie msaada na sifa.Anaelezwa kuwa watangulizi wake walipita mkondo huo wa maisha.
    4. Eleza maana ya mshororo “vichwa vyote hivi vilidondoka katika umbali uo, nawe kudondoka utadondoka” Wengi wamepita matatizo / ugumu huo na huu mkondo wa maisha na ni lazima hayakumbali na kujizatiti.Mwisho ukifika ataondoka. (al 2)
    5. Eleza umbo la shairi hili (al 4)
      • Lina beti nane
      • Beti zote zina mishororo saba isipokuwa ubeti wa saba
      • Mishororo inatofuatiana, mingine mirefu na mingine mifupi.
        mfano ubeti 8 mshororo wa mwisho “ kichomi kimenipata na sijaondoka”
      • Halina mpangilio maalum wa vipandi
      • Halina mtiririko wa vina.
  2. FASIHI SIMULIZI.
    1. Maana ya maghani
      • Mashairi ya kukaririwa tu hayaimbwi.
      • Hutolewa kwa kalima badala ya kuimbwa. (alama 2)
    2. Sifa za maghani.
      • Ni tungo la kishairi. Yaani yana muundo wa ushairi.
      • Husimulia matukio kwa kirefu hasa yanayotambwa.
      • Hutungwa papo hapo na kusemwa mbele ya hadhira.
      • Hutungwa kwa ufundi ukubwa.
      • Huweza kutolewa na mtu mmoja au kundi ki watu.
      • Anayeghani hujisifu / kusifu kitu / jambo fulani.
      • Huwa na majigambo mengi.
        Huambatana na ala mbalimbali za muziki. (alama zozote 6x1 = 6)
    3. Aina tatu za maghani.
      • Tondozi – Tungo zinazoghanwa na huwasifu watu, wanyama na vitu.
      • Tendi - Huitwa pia ushairi wa ushujaa. Hujumuisha sifa zinazoonyehsa mafanikio ya mashujaa na mbolezi zinazoonyesha anguko la shujaa / mtawala.
      • Rara – hadithi fupi na nyepesi za kishairi zinazopitishwa kwa mdomo.
      • Huzungumzia tajriba ya maisha.
      • Pembezi – Ni aina ya tondozi inayotolewa kusifu watu fulani pekee mf. viongozi, waganga mashuhuri, waelezi wazuri, wapenzi waliopigania pendo lao n.k.
      • Sifo – Ni mashairi ya sifa ambayo hughanwa kumsifu mtu fulani kutokana na matendo yake ya kishujaa (zozote 3x2 = 6)
    4. Umuhimu wa maghani.
      • Kushukiwa kuwa mpelelezi
      • Wahojiwa kutoa habari za uongo
      • Kutokuwepo wa watu wenye ujuzi wa maghani
      • Mila na desturi nyingi kuwa zimeadhiriwa na usasa
      • Ukosefu wa fedha za kufanya utafiti
      • Maghani kuchukukuliwa kuwa ukale uliopitwa na wakati
        (zozote 6x1 = alama 6) Tanbihi: Mtahiniwa asipoelezea umuhimu Aadhibiwe
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Achievers Joint Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?