MAAGIZO
- Andika insha mbili
- Swali la kwanza ni la LAZIMA
- Kila insha isipungue maneno 400
- Chagua insha nyingine moja kutoka kwa hizo tatu zilizosalia
- Kila insha iandikwe kwa lugha ya Kiswahili
- Karatasi hii ina kurasa 12,mtahiniwa ahakikishe kuwa maswali yote yamo na yamepigwa chapa
MASWALI
- LAZIMA
Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa kuchunguza vyanzo vya ongezeko la umaskini nchini. Andika ripoti ya uchunguzi huo huku ukitoa mapedekezo (alama20) - Unywaji wa pombe haramu umekithiri miongoni mwa vijana shuleni. Wewe kama kiranja wa ushauri nasaha, waandikie ilani kuhusu madhara ya pombe haramu (alama20)
- Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali; Achanikaye kwenye mpini hafi njaa (alama20)
- Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno yafuatayo;
Majeruhi walifikishwa hospitalini mmoja baada ya mwingine wakiwa katika hali mahututi. Sauti nzito ya daktari mkuu ilihanikiza hewani baada ya ………………… (alama20)
MWONGOZO
- Hii ni ripoti
Yafuatayo yazingatiwe:- Muundo
Sura ya ripoti idhihirike.- Kichwa - kionyeshe kiini cha uchunguzi
- Utangulizi
- Mtahiniwa ataje jopokazi: Wanachama walioteuliwa, aliyeteua jopokazi.
- Hadidu za rejea (Masharti na mipaka ya utekelezaji wa kazi iliyopangiwa jopokazi)
- Sampuli lengwa - Habari zilizokusanywa.
- Njia za ukusanyaji - Hojaji, Mahojiano, Majadiliano kwenye vikundi
- Mwili - Hoja zijadiliwe humu, vichwa vidogo vitumiwe
- Vyanzo/visababishi
- Mapendekezo
- Hitimisho
- Kimalizo(sahihi, jina, tarehe)
- MAUDHUI
Baadhi ya hoja ni:- Majanga - Kama magonjwa, Mafuriko n.k ambayo huharibu mali na kusababisha umaskini
- Bei duni ya bidhaa katika masoko - wakulima wanakosa motisha
- Uzembe na utegemezi wa wananchi - Wanakosa kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali.
- Mabadiliko ya hali ya hewa yasiyoweza kubashiliwa - Kuwa na vipindi virefu vya jua/ukame
- Mtazamo hasi wa vijana kuhusu kazi - wanataka kazi za ofisi na hivyo kudharau baadhi ya kazi
- Kuongezeka kwa idadi ya watu nchini.
- Ufisadi katika nchi za kiafrika - rasilimali ambazo zingewafaidi watu huporwa na kunufaisha vigogo wachache
- Utawala mbaya unaosababisha vita na chuki
- Kuporomoka kwa uchumi wa nchi, hivyo mapato ya kitaifa yanadidimia.
- Kusambaa kwa magonjwa yasiyo na tiba mfano; Ukimwi na Saratani hivyo kuathiri jamii kwa kiwango kikubwa.
- Ukosefu wa elimu mwafaka ambayo haiwawezeshi wanafunzi kumiliki stadi za kuweza kujitegemea na kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali.
- Madeni mengi kutoka mataifa ya kigeni
- Ukosefu wa nyenzo muhimu k.v mtaji za kuzalisha mali.
- Vijana kukataa masomo
Mtahiniwa atoe angaa mapendekezo mawili - Kuimarisha na kupanua kilimo kwa kuyalima mashamba zaidi
- Kuongeza nafasi za elimu ya juu ili watu wapate ujuzi utakaowafaa kuzimbua riziki.
- Kupunguza mikopo kutoka ughaibuni
- Kuhamasisha wanacnhi kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa kujitegemea
- Kuwaelimisha wanajamii kuhusu namna na umuhimu wa kupanga kazi
- Serikali kukomesha ufisadi nchini
- Kuimarisha bei ya bidhaa za mashambani katika masoko nchini
- Kuweka mtaala wa elimu unaooana na mahitaji /gharama ya maisha
- Kuhamasisha vijana kutotegemea kazi za kiofisi pekee bali waanzishe miradi midogo midogo ya kibiashara.
Tan:- Sharti muundo wa ripoti ujitokeze
- Mtahiniwa atakayepotoka kisura kabisa aadhibiwe alama nne(4s)
- Atakayepungukiwa na sehemu mojawapo ya ripoti, achukuliwe kwamba amepungukiwa kimtindo.
- Sharti mtahiniwa ajadili vyanzo vya ongezeko la umaskini nchini.
- Muundo
- Hii ni ilani
Yafuatayo yazingatiwe:- Muundo
- Kichwa
Kibainishe yafuatayo:- Jina la idara ya ushauri nasaha /anayetoa ilani
- Inatoka wapi na walengwa ni kina nani
- Mada - Sharti itaje ilani na inahusu nini
- Utangulizi
Maelezo mafupi kuhusu kinachozungumziwa - Mwili
Hoja/maudhui yajadiliwe hapa - Hitimisho
Mtahiniwa aonyeshe hatari ya kukaidi tahadhari iliyotolewa
Sahihi
Jina
Cheo
- Kichwa
- Maudhui
Baadhi ya maudhui ni;- Kudhoofisha afya ya watumiaji kwa watumiaji k.v figo na maini
- Husababisha mafarakano miongoni na wanafunzi na walimu
- Huathiri uwezo wa ubongo wa kuweza kuamua kwa urahisi
- Kutumwa nyumbani kwa wanaotumia pombe hii na hivyo kukatiza elimu
- Kusababisha ufujaji wa pesa miongoni mwa wanafunzi
- Kusababisha vifo miongoni mwa wanafunzi
- ukosefu wa maadili miongoni mwa vijana mfano wizi ili kupata pesa za kununua pombe
- Kusababisha utengano wa mahusiano baina ya wazazi na wanafunzi, walimu na wanafunzi.
- Husababisha ajali barabarani (Shule za kutwa)
- Hufanya mtumiaji awe mlegevu kimasomo
Tan:- Sharti muundo wa ilani ujitokeze
- Atakayepungukiwa na sehemu mojawapo ya ilani achukuliwe kwamba amepungukiwa kimuundo.
- Sharti mtahiniwa ajadili madhara yanayotokana na unywaji wa pombe haramu miongoni mwa vijana shuleni
- Muundo
- Hii ni insha ya methali
Kisa kidhihirishe maana ya ifuatayo:
Mtu anayetaabika kwa kazi sana mwishowe hufanikiwa katika shughuli ile
Baadhi ya hali ambazo zinaweza kujitokeza ni:- Mtahiniwa anaweza kutumia mpini kufanya kazi ngumu ya ukulima, mwishowe afanikiwe kwa kupata mazao mengi
- Mhusika awe katika hali ngumu ya maisha, ateseke katika mazingira hayo na mwishowe afanikiwe
mfano: hali ngumu ya;- kimapenzi/ndoa
- kibiashara
- kielimu
- kikazi
- kidini n.k
Tanbihi:- Pande zote za methali sharti zionekane
- Atakayeshughulikia kijisehemu kimoja asipite kiwango cha C+ (alama 10)
- Mtahiniwa anaweza akatumia nafsi ya kwanza au mbinu rejeshi
- Lazima mtahiniwa aonyeshe hali ngumu iliyomkabili mhusika, jinsi alivyoteseka na alivyofanikiwa baadaye
- Hii ni insha ya kibinulizi
Mtahiniwa aandike insha inayoanza kwa maneno aliyopewa
Kisa kinaweza kudhihirisha hali zifuatazo:- Mmoja wa majeruhi aweza kuwa jamaa wa karibu wa daktari mkuu
- Hali mbaya ya majeruhi ilimfanya daktari mkuu atoe sauti mzito
- Idadi kubwa ya majeruhi waliofikishwa hospitalini ilimshtua daktari aliyetaka kuondoka hospitalini
Tan:- Mtahiniwa ajikite katika mazingira ya hospitalini
- Sharti mtahiniwa asimulie kiini cha sauti nzito ya daktari mkuu kusikika na kuhanikiza hewani
- Mtahiniwa anaweza kutumia nafsi ya kwanza pale ambapo yeye ni miongoni mwa waathiriwa au mtazamaji
- Mbinu rejeshi inaweza pia kutumika
USAHIHISHAJI NA UTUNZAJI
Mtahini aisome insha ya mwanafunzi kwa kuzingatia;
- Maudhui
- Msamiati
- Sarufi
- Hijai/tahajia
- Muundo
- sura
- Mpangilio wa aya
- Mtindo – upekee wa matumizi ya lugha
- Urefu
Maneno chini ya 174 – 05 +
Maneno chini ya 174 – 274 (Nusu) – 10 C+
Maneno chini ya 275 – 374 (Robo tatu) – 15 B+
Maneno chini ya 375 – 400 (Kamili) – 20 A
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Cekana Mock Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students